Main content blocks
Section outline
-
Mada Ndogo: Midahalo na mijadala kuhusu shughuli
za maendeleo na uzalishajimali dhidi ya
umaskini nchiniSOMO LA 10: Mdahalo10.1 Mdahalo kuhusu ‘Elimu ni muhimu kwa maendeleo ya
wananchi kuliko biashara’Katika makundi ya wanafunzi watatu watatu, chunguzeni mchoro ufuatao kisha
mjadili kuhusu kinachoendelea katika mchoro wenyewe. Baada ya kujadiliana,
someni kifungu cha mdahalo kinachofuata kisha mjibu maswali yanayofuata.




Maswali ya ufahamu1. Mada ya mdahalo iliyokuwa ikizungumziwa ilikuwa ipi?
2. Eleza tofauti kati ya watetezi na wapinzani.
3. Bigirimana alitoa hoja zipi?
4. Mukamwiza alitoa hoja zipi?
5. Mukandayisenga alitoa hoja gani?
6. Eleza hoja ambazo Msikilizaji mshiriki 1 alitoa.
7. Msikilizaji mshiriki 2 alitoa hoja zipi?
8. Taja jina jingine la ‘mdahalo’.
9. Mwenyekiti hufanya kazi gani katika shughuli za mdahalo?10.2 Msamiati kuhusu mdahaloKatika makundi ya wanafunzi watatu watatu, tafuteni msamiati mpya kutoka
katika kifungu cha mazungumzo yaliyotangulia na kuueleza. Zingatieni
matumizi ya msamiati huo katika kifungu hicho na mtumie kamusi pale
inapohitajika.Zoezi la 10.1Katika makundi ya wanafunzi watatu watatu, elezeni maana ya msamiati
uliopigiwa mistari katika sentensi zifuatazo kisha mtunge sentensi sahihi kwa
kutumia msamiati huo.
1. Alitupatia fursa ya kueleza shughuli za maendeleo ya kijiji chetu.
2. Mukeshimana alitoa hoja nzuri katika mazungumzo yetu.
3. Sisi tulitetea mawazo yake kwa sababu alisema ukweli.
4. Mimi ninapinga mawazo ya watu wanaotaka kuendelea kuishi kwa
kutegemea misaada tu.
5. Nyirahabineza alichaguliwa kuwa mwenyekiti wa Chama cha
Wanafunzi wa Kiswahili nchini Rwanda (CHAWAKIRWA).
6. Wageni hawa walikuja kuwekeza nchini mwetu na wanaendelea
kupata faida nyingi.
7. Mafunzo ya rafiki yangu yalichukua gharama kubwa.
8. Matokeo ya mtihani wetu ni mazuri kwa sababu tumefaulu.
9. Tujiepushe na ulevi kwa sababu ni kikwazo kwa maisha mazuri ya
watu.
10. Tulianzisha biashara ya kufuga kondoo na pato letu linaongezeka kila
mwaka.Zoezi la 10.2Katika makundi ya wanafunzi watatu watatu, kamilisheni sentensi zifuatazo
kwa kutumia maneno yafuatayo: walipiga makofi, maarifa, mshiriki,
kutambua, itatunufaisha, anafananisha.Kwa mfano: Baada ya ____________ kuwa Bwiza hakufaulu katika
somo la Kiswahili niliamua kumsaidia.
Jibu: Baada ya kutambua kuwa Bwiza hakufaulu katika somo la
Kiswahili niliamua kumsaidia.
1. Watu hawa wana ___________ mbalimbali ya kutekeleza miradi.
2. Washiriki wote wa mkutano ____________ baada ya kusikia hoja
nzuri za Kayisabe na wenzake.
3. Mwenyekiti wa mkutano wetu anasema kuwa kila _____________
anapaswa kutoa hoja zake.
4. Mtu huyu _______________ elimu na utajiri.
5. Kazi hii ___________ wote kwa kutuwezesha kupata pesa za kujisaidia.Zoezi la 10.3Katika makundi ya wanafunzi wawili wawili, husisheni maneno yaliyoandikwa
katika sehemu A na maelezo yake katika sehemu B.
Kwa mfano: 1
C
Sehemu A Sehemu B
1. mwenyekiti A. mazungumzo kati ya watu wenye mitazamo
tofauti
2. mdahalo B. jambo muhimu
3. msingi CH. mtu aliyechaguliwa kuongoza mdahalo
4. wanatatua D. ufupisho
5. muhtasari E. wanaondoa tatizo10.3 Matumizi ya lugha: MajadilianoKatika makundi ya wanafunzi watatu watatu, jadilini maswali yafuatayo na
mwelezane kuhusu:
1. Mdahalo ni nini?
2. Toa mifano ya mada mbili zinazoweza kuzungumziwa katika mdahalo.
3. Ni watu gani ambao hushirikishwa katika mdahalo?
4. Watu hao huwa na mawazo au misimamo tofauti. Eleza misimamo hiyo.
5. Taja tabia za kujiepusha katika mdahalo.Zoezi la 10.4Katika makundi ya wanafunzi wawili wawili, jazeni herufi zilizoachwa ili
kuunda neno kamili.Kwa mfano:
• Mazungumzo au majadiliano kati ya watu wengi ambaoMaelezo muhimu!
huzungumzia jambo moja maalumu na huwa na mitazamo tofauti
huitwa mdahalo.
• Mtazamo wa kwanza hutoa hoja zinazotetea au kuunga mkono
wazo kuu.
• Mtazamo wa pili hutoa hoja za kupinga au kukataa wazo kuu.
• Washiriki wa mdahalo ni:
1. Mwenyekiti:
• Huongoza mazungumzo au majadiliano.
•Hupanga muda utakaotumiwa na kila msemaji kutoa hoja.
• Huchagua wasemaji katika mdahalo.
• Hupigisha kura baada ya mazungumzo ili kutaka kujua upande
ulioshinda kati ya upande wa watetezi na ule wa wapinzani.2. Katibu:
•Huandika na kusoma hoja za wasemaji wote.
• Hutangaza matokeo ya kura zilizopigwa baada ya mazungumzo.
3. Watetezi:
• Hawa ni wasemaji wanaotetea mada au wazo kuu linalozungumziwa.
4. Wapinzani:
•Hawa ni wasemaji wanaopinga mawazo yanayotetea wazo kuu la
mada.
5. Wasikilizaji washiriki:
• Hawa wanashiriki kwa kusikiliza hoja za pande mbili: upande wa
utetezi na upande wa upinzani.
Baadhi ya tabia za kuepuka katika mdahalo ni: matumizi ya lugha
yenye matusi na uchochezi, kutohifadhi wakati uliotengewa, kupandwa na
hasira upande wako unaposhindwa, n.k.10.4 Kusikiliza na kuzungumza: Kuandaa mdahalo
Katika makundi ya wanafunzi wanane wanane chagueni moja kati ya mada
zifuatazo kisha mwandae mdahalo wenu.
1. Elimu ndio msingi wa maisha mazuri.
2. Wazazi wana nafasi kubwa katika malezi ya watoto wao kuliko walimu.
3. Ni lazima viongozi wa kidini washirikiane na wanasiasa katika mipango
ya maendeleo ya wananchi.
4. Vitabu ndivyo vifaa muhimu katika elimu.
Katika maandalizi yenu, zingatieni mambo yafuatayo:• Jadilini maana ya msamiati uliotumiwa katika mada mlizopewa ili muweze
kuelewa mada hizo.
• Hakikisheni kuwa mnaelewa jambo muhimu linalozungumziwa katika
kila mada.
• Hakikisheni kuwa mmechagua mwenyekiti, katibu, wasikilizaji washiriki,
watetezi na wapinzani.
• Kila mzungumzaji aandae na kupanga hoja zake vizuri.
• Kila mzungumzaji anapaswa kuwa na nidhamu kwa kuheshimu maelekezo
ya mwenyekiti.
10.5 Sarufi: Wakati uliotimilika, tungo yakinishi
Katika makundi ya wanafunzi watatu watatu, chunguzeni sentensi zinazofuata
katika umoja na wingi kisha mwelezane ugunduzi wenu na baadaye mjibu zoezi
linalofuata.
Je, mmegundua nini?
Zoezi la 10.5
Katika makundi ya wanafunzi watatu watatu, tungeni sentensi moja moja kwa
kutumia kitenzi zungumza kwa kutumia kiambishi ‘me’ kama kilivyotumiwa
katika tungo zenye kitenzi toa zilizo hapo juu. Tumia nafsi: mimi, wewe, yeye,sisi, nyinyi na wao.
Kwa mfano:
Mimi nimezungumza na mwalimu wangu.Sisi tumezungumza na walimu wetu.
Maelezo muhimu!
• Kiambishi ‘me’ kinarudiwarudiwa katika vitenzi vyote baada
ya viambishi nafsi ni, u, a, tu, m na wa. Kiambishi ‘me’ ni
kiambishi cha wakati uliotimilika, tungo yakinishi.
• Wakati uliotimilika huonyesha kuwa tendo tayari limefanyika na
kumalizika.
Kwa mfano:
• Mimi nimefanya zoezi langu. (zoezi tayari limeshafanywa)
• Kageruka ameondoka leo. (tendo la kuondoka tayarilimeshamalizika)
Matumizi ya wakati uliotimilika katika sentensi
Katika makundi ya wanafunzi watatu watatu, chunguzeni sentensi zifuatazo kwakuziambatisha pamoja na michoro iliyopo. Elezaneni mlichogundua.


Zoezi la 10.6
Katika makundi ya wanafunzi wawili wawili, jazeni nafasi zilizoachwa wazi
kwa kutumia kitenzi kinachofaa katika wakati uliotimilika, tungo yakinishi.
Kwa mfano: Mwalimu ______ (kueleza) vizuri mambo yote muhimu.
Jibu: Mwalimu ameeleza vizuri mambo yote muhimu.
1. Sisi na viongozi wetu _________(kujadiliana) kuhusu umuhimu wa
Kiswahili.
2. Wewe ________ (kutazama) mchezo wa kandanda kwenye runinga.
3. Mama yangu ________ (kuagiza) bidhaa nyingi kutoka Uchina.
4. Mtetezi huyu na wasikilizaji washiriki wote_________(kuzungumzia)
mambo muhimu.
5. Mlango wa nyumba hii ________ (kufunguliwa) ili wageni wote
waingie.
6. Kisu changu _________ (kupotea).
7. Nyumba zile _______ (kupakwa) rangi na mafundi wawili.
8. Vitabu vingi vya Kiswahili ________ (kuchapishwa).
9. Midahalo miwili _________ (kushirikisha) wasemaji wenye hoja nzuri.
10. Mimi _________ (kuimba) wimbo wa kumsifu Mungu katika ibada
yetu.
10.5.1 Wakati uliotimilika, tungo kanushiKatika makundi ya wanafunzi wawili wawili, chunguzeni sentensi zinazofuata
katika umoja na wingi kisha mtunge sentensi zinazofanana nazo katika nafsizote.
Zoezi la 10.7
a) Katika makundi ya wanafunzi wawili wawili, tungeni sentensi moja
moja kwa kutumia kitenzi imba katika wakati uliotimilika, hali
yakinishi. Tumia nafsi: mimi, wewe, yeye, sisi, nyinyi na wao.b) Andikeni sentensi zenu katika hali kanushi.
Maelezo muhimu!• Kiambishi ‘me’ kimetumika kuonyesha wakati uliotimilika
katika tungo yakinishi.
• Katika wakati uliotimilika, kiambishi ‘ja’ kinatumiwa katikatungo kanushi badala ya kiambishi ‘me’ cha tungo yakinishi.
Zoezi la 10.8
Katika makundi ya wanafunzi wawili wawili, andikeni sentensi hizi katika
tungo kanushi.
Kwa mfano: Wewe umeimba wimbo mzuri sana.
Jibu: Wewe hujaimba wimbo mzuri sana.
1. Yeye ameagiza bidhaa nyingi kutoka Kigali.
2. Mimi nimezunguka mjini kwa gari.
3. Mtoto wangu amefaulu mitihani yake.
4. Nyumba yangu imesafishwa.5. Mgomba umechomwa.
Zoezi la 10.9
Baada ya kukanusha tungo katika zoezi la 10.8, ziandike katika wingi.
Kwa mfano: Wewe hujaimba wimbo mzuri sana. (umoja, tungo kanushi)
Jibu: Nyinyi hamjaimba nyimbo nzuri sana. (wingi, tungo kanushi)
SOMO LA 11: Mjadala
11.1 Mjadala kuhusu ‘Nafasi ya ukulima katikauzalishajimali dhidi ya umaskini’
Katika makundi ya wanafunzi watatu watatu, jadilini kuhusu kinachoendelea
katika michoro ifuatayo kisha msome kifungu cha mjadala kinachofuata kuhusu
nafasi ya kilimo katika shughuli za uzalishajimali dhidi ya umaskini na hapo
baadaye mjibu maswali yanayofuata.

Maswali ya ufahamu
1. Mada ya mjadala ilikuwa ipi?
2. Eleza tofauti kati ya ukulima na ufugaji.
3. Tatizo linaloathiri kilimo kulingana na Kawera ni lipi?
4. Serikali inashauriwa kufanya nini ili kusuluhisha matatizo ya kilimo?
5. Bagirishya alitoa hoja gani?
6. Mukandayisenga alitoa hoja gani?7. Eleza hitimisho ambalo Mwenyekiti alitoa.
11.2 Msamiati kuhusu ukulima
Jipangeni katika makundi ya wanafunzi watatu watatu, kisha mtafute maana ya
msamiati mpya katika kifungu cha mjadala kilichotangulia. Tafuteni maana ya
msamiati huo kulingana na matumizi yake katika kifungu hicho. Tumieni kamusipale inapohitajika.
Zoezi la 11.1
Katika makundi ya wanafunzi watatu watatu, chunguzeni sentensi zifuatazo
kisha mtunge sentensi zenu kwa kutumia maneno yaliyopigiwa mistari.
1. Taasisi ya kilimo imewaletea wakulima mbegu nzuri za mahindi.
2. Nyanya na vitunguu vinanunuliwa kwa bei nafuu mjini Kigali.
3. Ni lazima kila mkulima aache uvivu na kufanya kazi kwa bidii.
4. Mtaalamu mmoja wa kilimo ameonyesha namna nzuri ya kupanda
migomba.
5. Mkulima huyu ana bidii sana katika shughuli zake.
6. Watu hawa wanatimiza wajibu wao wa kufundisha wakulima.
7. Wadau wote wa kilimo wamekutania mjini Kigali.
8. Serikali ya Rwanda inatenga faranga nyingi za kuendesha sekta zakilimo na ufugaji.
Zoezi la 11.2

11.3 Matumizi ya lugha: Zoezi la jedwali
Katika makundi ya wanafunzi watatu watatu, jazeni nafasi hizi kwa kuzingatiamajibu ya maelezo yaliyo hapo chini:
Kwenda kulia
1 Mazungumzo kati ya watu wenye mitazamo tofauti kuhusu mada maalumu
6 Uchaguzi wa kupata mshindi
8 Maombi yanayoelekezwa kwa Mungu
9 Neno lionyeshalo kuwa hakuna kingine
10 Maelezo ya kupinga au kuunga mkono
11 Kitu kilichotengenezwa kwa ajili ya kukalia
12 Kinachotokana na mmea
14 Anakataa kuunga mkono16 Mazungumzo ya kujenga hoja yanayofanywa kwa ajili ya kufafanua jambo
Kwenda chini2 Jambo linalozungumzwa au kujadiliwa
3 Anaunga mkono
4 Chombo cha mawasiliano
5 Mtu anayeandika mawazo ya wasemaji na washiriki wengine katika
mdahalo
7 Kuwa kwa wingi
13 Kitu anachopata mtu baada ya kazi15 Isipokuwa
Maelezo muhimu!
• Mjadala ni mazungumzo kuhusu jambo maalum.
• Watu wanaoshiriki katika mazungumzo haya hutoa hoja zao
kuhusu jambo hilo.
• Jambo ambalo linazungumziwa huhitaji kufafanuliwa na kutolewa
maelezo.
• Katika mjadala kila mtu aliye na hoja huonyesha kuwa anataka
kusema na hupewa muda wake ili atoe hoja zake.
• Msemaji anaweza kutetea au kupinga mawazo ya wengine.
• Katika mjadala kuna kiongozi anayeongoza mazungumzo.
• Kiongozi huchagua anayezungumza na kuongoza mazungumzo na
kuhifadhi nidhamu.
• Washiriki nao hutoa hoja zao kuhusu mada iliyotolewa mpaka
wafikie uamuzi wao wa mwisho.• Hakuna kura zinazopigwa kama ilivyo katika mdahalo.
11.4 Kusikiliza na kuzungumza: Kuandaa mjadala
Katika makundi ya wanafunzi watano watano, chagueni moja kati ya mada
zifuatazo na kuandaa mdahalo wenu.
1. Umuhimu wa biashara katika uzalishajimali nchini Rwanda.
2. Umuhimu wa uongozi bora katika uzalishajimali dhidi ya umaskini.
3. Vikwazo vya kufanikisha kazi miongoni mwa vijana.
4. Nafasi ya shule za ufundi katika maendeleo na uzalishajimali nchini
Rwanda.11.5 Sarufi: Kauli asili na kauli taarifa
Katika makundi ya wanafunzi wawili wawili, chunguzeni sentensi zifuatazo kishamjibu maswali yaliyo hapo chini.


Je, mmegundua nini?
Zoezi la makundi
1. Linganisheni sentensi katika sehemu A na sentensi katika sehemu B kwa
kuonyesha sifa zake.
2. Tungeni sentensi mbili zenye sifa kama za sentensi za sehemu A nakuziandika kwa kuzingatia sifa za sentensi katika sehemu B.
Maelezo muhimu!
• Sentensi katika kundi A zinarudia maneno yaliyotamkwa na mtu bila
kubadilisha chochote katika kauli yake.
• Kauli hiyo imeandikwa kwa kutumia alama za usemi (“ ” ) na kuanza
kwa herufi kubwa.
Kwa mfano: Mwalimu alisema, “Mimi nitafundisha somo la Kiswahili.”
• Sentensi katika kundi B zinalenga kutuambia maneno ambayo
yalizungumzwa na mtu mwingine bila kuyarudia kama yalivyokuwa
katika kauli yake ya kwanza.
Kwa mfano: Mwalimu alisema kwamba yeye atafundisha somo la
Kiswahili.
• Sentensi katika kundi A zinaonyesha kauli ya mtu katika hali yake ya
kwanza na kauli hiyo inaitwa kauli asili.
• Sentensi katika kundi B zinatoa taarifa au habari ya kauli au maneno
yaliyosemwa na mtu mwingine bila kuongeza wala kupunguza maana
ya jambo aliloeleza. Kauli hiyo inaitwa kauli taarifa.
• Katika kauli ya taarifa mambo haya huzingatiwa:
• Nafsi hubadilika
• Mimi hubadilika na kuwa yeye• Sisi hubadilika na kuwa wao
Zoezi la 11.3
Katika makundi ya wanafunzi wawili wawili, badilisheni sentensi hizi za kauli
asili ziwe katika kauli taarifa.
Kwa mfano: Mkulima mmoja anasema, “Mimi nitapata mavuno mengi
sana.”
Jibu: Mkulima mmoja anasema kwamba yeye atapata mavuno
mengi sana.
1. Wazungumzaji hawa wanasema, “Sisi tunapenda kutoa maoni yetu.”
2. “Kabera atajijengea nyumba nzuri.” Mwanafunzi mmoja anasema.
3. “Mimi nitaingia darasani saa nane kamili.” Ndayisaba anasema.
4. Wakulima wanasema, “Mvua itanyesha na mimea yetu itastawi.”
5. Baba yangu anasema, “Ni lazima watoto wote wasome kwa bidii.”
6. “Sisi tutasaidia wakulima wetu kupata mbegu nzuri.” Mkuu wa wilaya
anasema.
7. “Mimi ninahitaji dereva mwenye ujuzi.”Mkuu wa kiwanda hiki anasema.
8. Mama yangu anasema, “Kisu changu kimepotea.”
9. “Kitanda changu ni kizuri.” Mgeni mmoja anasema.
10. “Mimi sikubaliani na mawazo ya mtetezi wa pili.” Mpinzani huyuanasema.
Zoezi la 11.4
Katika makundi ya wanafunzi wawili wawili, badilisheni sentensi hizi kutoka
kauli taarifa na kuziweka katika kauli asili.
Kwa mfano: Mama alisema kuwa alitaka kwenda sokoni.
Jibu: “Ninataka kwenda sokoni.” Mama alisema.
1. Baba aliniambia kuwa nikifika Kigali ninunue sare mpya.
2. Kaka alisema kuwa hakutaka kwenda shambani.
3. Mwalimu alisema aende hapo.
4. Kalisa alisema kuwa yeye aliandika barua hiyo.
5. Birasa alishangaa kuwa yeye hawezi kubeba mzigo huo.6. Mwalimu mkuu aliuliza sababu yake ya kulia.
SOMO LA 12: Mjadala
12.1 Mjadala kuhusu ‘Ufugaji kama njia ya kupigana naumaskini nchini’
Katika makundi ya wanafunzi watatu watatu, tazameni na mjadili kuhusu
kinachoendelea katika michoro hii kisha msome kifungu kilicho hapo chini nabaadaye mjibu maswali ya ufahamu yanayofuata.





Maswali ya ufahamu
1. Mjadala uliosoma ulihusu nini?
2. Bwana Niyibizi alitoa maoni gani kuhusiana na mada husika?
3. Nyiraneza alichangia mjadala kwa hoja zipi?
4. Muhirwa alitoa hoja zipi kuhusiana na umuhimu wa ufugaji?
5. Eleza hoja alizotoa Bwana Rwambibi.6. Mwenyekiti alihitimisha vipi mjadala huu?
12.2 Msamiati wa mjadala kuhusu ufugajiKatika makundi ya wanafunzi watatu watatu, tafuteni msamiati mpya katika
kifungu cha mazungumzo hapo juu na kuueleza. Zingatieni matumizi ya msamiatihuo katika kifungu hicho na mtumie kamusi pale inapohitajika.
Zoezi la 12.1
Katika makundi ya wanafunzi wawili wawili, chunguzeni sentensi zifuatazo
kisha mtunge sentensi zenu kwa kutumia maneno yaliyopigiwa mistari.
1. Watoto wanapenda kunywa maziwa ya ng’ombe.
2. Ni lazima sisi tupambane na umaskini kwa kufanya kazi kwa bidii.
3. Mtoto huyu ana shida ya kukosa karo ya shule.
4. Mfugaji huyu ametenga mnyama huyu mgonjwa ili asiambukize
wanyama wengine.
5. Kiwanda hiki kitafanya kazi kubwa ya kutengeneza nguo nyingi.
6. Si vizuri kupuuza ushauri wa viongozi wetu.
7. Mzungumzaji huyu amegusia umuhimu wa mifugo nchini Rwanda.
8. Eneo hili lina mazao mazuri kwa sababu lina rutuba nyingi.
9. Viwanda vyetu vinahitaji malighafi nyingi kutokana na kilimo.10. Mazungumzo yetu yamefikia kikomo kwa sasa.
Zoezi la 12.2
Chagueni neno kati ya yafuatayo ili kukamilisha sentensi hizi kwa usahihi:
mjadala, hoja, umoja, umaskini, mifugo, mbolea, maziwa
Kwa mfano: Ng’ombe wanatupatia ______________ ya kuweka katika
mimea yetu.
Jibu: Ng’ombe wanatupatia mbolea ya kuweka katika mimea
yetu.
1. Wizi wa ___________ unaweza kuleta hasara kubwa kwa wafugaji na
kuwarudisha katika hali ya ___________.
2. Watu wengi wanapenda kunywa ________ ili kupambana na magonjwa
mbalimbali.
3. Wafugaji hawa wamejiunga katika shirika kubwa kwa sababu wanajua
kwamba _________ ni nguvu.
4. __________ wetu umetufurahisha sana kwa sababu washiriki wotewalitoa ________ nzuri.
12.3 Matumizi ya lugha: Kuunda maneno kamiliKatika makundi ya mawafunzi wawili wawili, jaribuni kupanga sehemu za
maneno zifuatazo ili kuunda maneno kamili.
Kwa mfano: zi-te-m-te
Jibu: mtetezi
1. da-m-lo-ha
2. ki-mwe-ti-nye
3. zu-m-ngu-ji-za-m
4. pi-u-ni-nza
5. ja-la-da-m
6. li-u-sha-ji-za li-ma
7. fu-ji-u-ga
8. ku-m-li-ma
9. o-ma-ni10. li-ki-mo
Zoezi la 12.3
Katika makundi ya wanafunzi wawili wawili, jaribuni kupanga maneno
yafuatayo ili kuunda sentensi kamili na sahihi.
1. kazi lazima zinakwamisha za uvivu na ulevi tabia kwa sababu ni na
kujiepusha mbaya.
2. ya na kazi ufugaji za kilimo zinaweza raia kupigana wengi kuwasaidia
umaskini dhidi.
3. waweze bidii kazi mazuri kwa wafanya ni lazima watu ili kuwa maisha
na wote.
4. hushiriki katika na wengi kwa mjadala zao kutoa mdahalo watu hoja.
5. namna kuhusu sisi maendeleo kazi umuhimu na miradi wa tunajadilianaya kuanzisha ya.
12.4 Kusikiliza na kuzungumza: Kuandaa mjadala
Jigaweni katika makundi ya wanafunzi watano watano kisha mwandae mjadala
kuhusu mojawapo ya mada zifuatazo:
1. Kazi muhimu za kuleta maendeleo kwa wananchi2. Tabia za kujiepusha ili kufanikisha kazi.
12.5 Sarufi: Mabadiliko ya kauli asili na kauli taarifa
Katika makundi ya wanafunzi wawili wawili, chunguzeni kwa makini sentensizifuatazo ili muweze kujibu maswali yaliyo hapo chini:

Zoezi la 12.4
Katika makundi ya wanafunzi wawili wawili, jibuni maswali yafuatayo:
1. Linganisha sentensi katika A na sentensi katika B kwa kuonyesha sifa
zake.
2. Tunga sentensi sita kwa kuzingatia sentensi katika A na kuziandikatena kwa kuzingatia sifa za sentensi katika B.
Maelezo muhimu!
• Sentensi katika A ni za kauli asili na sentensi katika B zimeandikwa
katika kauli taarifa.
• Kutokana na kitenzi sema au uliza katika wakati uliopita, sentensi za
kauli asili zimetanguliwa na kitenzi ‘alisema’ au ‘aliuliza’.
Kwa mfano:
• Wafanyakazi walisema, “Leo tunafurahia matunda ya kazi yetu.”
• Dereva aliuliza, “Nani anataka kufika mjini Kigali?”
• Mwanafunzi mmoja aliuliza, “Mdahalo utafanyiwa wapi?”
• Alama ya kuuliza (?) na alama za kufunga na kufungua (“ ”) huwa
hazitumiwi katika kauli taarifa.
Kwa mfano: Dereva aliuliza mtu ambaye alitaka kufika mjini Kigali.
• Mambo yafuatayo hubadilika wakati wa kugeuza sentensi za kauli asili
na kuziandika katika kauli taarifa:
Zoezi la 12.5
Katika makundi ya wanafunzi wawili wawili, badilisheni sentensi zifuatazo
ziwe katika kauli taarifa.
Kwa mfano: Wanafunzi wote walisema, “Sisi tunatakiwa kufaulu katika
mitihani yote ya muhula huu.”
Jibu: Wanafunzi wote walisema kwamba wao walitakiwa kufaulu
katika mitihani yote ya muhula huo.
1. Seremala mmoja alisema, “Mimi ninaunda vitanda vikubwa.”
2. Mfugaji alisema, “Wanyama wetu wanakosa maji.”
3. Mwalimu alisema, “Wanafunzi hawa wanaenda kucheza.”
4. Mtoto wake alisema, “Mimi nitaenda kuchota maji pamoja na ndugu
yangu.”5. Bwana yule aliuliza, “Unataka nini hapa?”
Tathmini ya mada ya 3
Zoezi la 1
1. Katika makundi ya wanafunzi watano watano, andaeni mdahalo kuhusu:
‘Shule za umma ni bora kuliko shule za kibinafsi’.
2. Katika makundi yenu, jadilini kuhusu majukumu ya wahusika hawa wa
mdahalo:
a) Mwenyekiti b) Katibu ch) Wapinzani d) Watetezi
Zoezi la 2
Katika makundi ya wanafunzi watano watano, andaeni mjadala kuhusu:‘Athari za mavazi ya kisasa kwa wanajamii’.
Zoezi la 3
Katika makundi ya wanafunzi wawili wawili, andikeni sentensi hizi katika
tungo kanushi.
Kwa mfano: Wewe umeimba wimbo mzuri sana
Jibu: Wewe hujaimba wimbo mzuri sana
1. Yeye ameagiza bidhaa nyingi kutoka Kigali.
2. Mimi nimezunguka mjini kwa gari.
3. Mtoto wangu amefaulu mitihani yake
4. Nyumba yangu imesafishwa.
5. Mgomba umechomwa.
6. Kazi hii imefanywa vizuri.
7. Kitabu chako kimeharibika.
8. Utambi umekauka.
9. Udevu mrefu umenyolewa.10. Barua imetumwa.
Zoezi la 4
Baada ya kukanusha sentensi zilizo katika zoezi la 3 lililo hapo juu, ziandike
tena katika wingi.
Kwa mfano: Wewe hujaimba wimbo mzuri sana (umoja, tungo kanushi)
Jibu: Nyinyi hamjaimba (wingi, tungo kanushi)
Zoezi la 5
Katika makundi ya wanafunzi wawili wawili, andikeni sentensi hizi katika
wingi.
Kwa mfano: Kisu kimeibiwa
Jibu: Visu vimeibiwa.
1. Kiti kimevunjika
2. Mtu huyu ametuimbia vizuri.
3. Mzee huyu amelewa.
4. Mwanafunzi huyu ameelewa somo la Kiswahili.
5. Ng’ombe wangu amezaa leo.
6. Mto huu umefurika.
7. Kiongozi amewasili mapema.
8. Mbwa amekula chakula.
9. Uso wake umeharibika.
10. Mguu wangu umetibiwa vizuri.Zoezi la 6
Baada ya kuandika wingi wa sentensi katika zoezi la 3 lililo hapo juu, ziandike
upya katika tungo kanushi.
Kwa mfano: Visu vimeibiwa. (wingi, tungo yakinishi)
Jibu: Visu havijaibiwa. (wingi, tungo kanushi)
Zoezi la 7
Katika makundi ya wanafunzi wawili wawili, kamilisheni sentensi zifuatazo
kwa kutumia maneno yafuatayo:
walipiga kura, wanatushawishi, uchumi, dhahiri, kuinua
1. Kila mwananchi anapaswa kufanya kazi kwa bidii ili _______ kiwango
cha maisha yake.
2. _______________ wa nchi yetu utastawi baada ya kuanzisha miradi
mingi mizuri.
3. Viongozi hawa __________ kutumia mbinu za kisasa katika shughuli
zetu za kilimo na ufugaji.
4. Ni ________ kwamba raia wa Rwanda walipata maisha mazuri baada
ya kuanzishwa kwa shughuli za ‘Gira inka Munyarwanda’.
5. Juzi wanafunzi wote __________ kwa sababu Mkuu wa shule alitaka
orodha ya viongozi wa madarasa yote.
Zoezi la 9
Katika makundi yenu, badilisheni sentensi hizi ziwe katika kauli taarifa.
1. Rais alisema, “Kila mwananchi anaweza kujitajirisha kwa kufanya kazi
kwa bidii.”
2. Mkuu wa shule alisema, “Wanafunzi wawili hawajui kusoma vizuri.”
3. Wafanyakazi walisema, “Hatutaki kufanya kazi na watu wavivu.”
4. Wazazi waliuliza, “Nani anaenda kununua mavazi ya watoto wetu?”5. Mkulima alisema, “Mvua hainyeshi sana siku hizi.”
Zoezi la 10
Katika makundi yenu, badilisheni sentensi hizi ziwe katika kauli asili.
1. Kalisa alimwambia shangazi yake kuwa kesho yake angeenda Kigali.
2. Bagirishya alisema huku akitetemeka kuwa chumbani mwake
mlikuwa na nyoka.
3. Kasisi alituambia kuwa ikiwa tungependa kuendelea vyema
maishani, ingebidi tuwe na heshima.
4. Daktari alituambia kuwa UKIMWI ni ugonjwa hatari sana.5. Baba aliniuliza idadi ya mabao tuliyofungwa mchezoni.

