Topic outline

  • SURA YA KWANZA : MADA KUU 1: LUGHA NA MAZINGIRA

    MADA KUU 1: LUGHA NA MAZINGIRA

    MADA NDOGO: Utalii nchini Rwanda

    1.1 Mazungumzo kati ya Mpokeaji na Mtalii

    Katika makundi ya wanafunzi watatu watatu, tungeni sentensi sahihi kwa

    kueleza kinachoendelea au mnachokiona katika mchoro huu.



    Maswali ya ufahamu

    Katika makundi ya wanafunzi watatu watatu, someni tena kifungu cha mazungumzo
    kilicho hapo juu kati ya Mtalii na Mpokeaji, kisha mjibu maswali haya.

    1. Mtalii anatoka katika nchi gani? Yeye anataka nini?
    2. Taja vivutio vya utalii vilivyopo nchini Rwanda.
    3. Mtalii atatembelea vivutio gani?
    4. Mtalii atachukua muda gani nchini Rwanda?
    5. Umuhimu wa mwelekezaji wa watalii ni upi?
    6. Watu huruhusiwa kuingia katika mbuga za wanyama kuanzia saa ngapi
    na hutoka saa ngapi?
    7. Mtalii atatumia nambari za simu alizopewa kufanya nini?
    8. Mtalii ataanza shughuli yake ya kuzuru maeneo mbalimbali lini?
    9. Mtalii atatumia nini kusafiri hadi kwenye mbuga za wanyama?

    10. Huduma za hoteli kwa Mtalii ni zipi? 

    1.2 Msamiati kuhusu utalii

    Katika makundi ya wanafunzi watatu watatu, tafuteni msamiati mpya katika
    kifungu cha mazungumzo mlichosoma hapo juu kisha muutolee maelezo.
    Zingatieni matumizi ya msamiati huo katika kifungu hicho na mtumie kamusi

    pale panapohitajika. 

    Kwa mfano:

    mbuga – sehemu maalum ya kuwahifadhia wanyamapori

    Zoezi la 1.1

    A. Katika makundi ya wanafunzi watatu watatu, elezeni maana ya msamiati
    uliopigiwa mistari katika sentensi hizi kisha mtunge sentensi zenu sahihi
    kwa kutumia msamiati huo.

    1. Mtalii huyu kutoka nchi ya Ujerumani anataka kujua maeneo
    mazuri ya kuzuru nchini.
    2. Maeneo mengi ya nchi yetu yanavutia watalii wengi.
    3. Mtalii huyu anataka kuzuru wilaya ya Korongi ili aweze kutazama
    ziwa Kivu.
    4. Simba wengi waliletwa katika mbuga ya wanyama ya Akagera.
    5. Mbuga ya Wanyama ya Akagera ni kivutio muhimu cha utalii

    nchini Rwanda. 

    6. Mtalii huyu aliamua kufanya ziara ya kitalii ya siku tano nchini
    mwetu.
    7. Nchi yetu inatarajia kupokea watalii elfu themanini na watano
    mwaka huu.
    8. Mimi ninaona heri niondoke katika sehemu hii; sitaki wanyama
    wakali wanipate hapa.
    9. Unaweza kufanya ziara yako ya kitalii mjini Kigali kwa bei nafuu.

    10. Watalii hufurahia mazingira ya Akagera.

    B. Katika makundi ya wanafunzi watatu watatu, tungeni sentensi sahihi kwa

    kutumia maneno yaliyopigiwa mistari katika Zoezi la 1A

    1.3 Matumizi ya lugha: Aina mbalimbali za pesa

    Katika makundi ya wanafunzi watatu watatu, tazameni pesa zifuatazo kisha

    mziambatanishe kwa usahihi na nchi zinakotumika.




    Zoezi la 1.2

    Katika makundi ya wanafunzi wawili wawili, ambatanisheni aina za pesa

    zilizo katika sehemu A na nchi zinakotumika katika sehemu B kwa usahihi.

    Kwa mfano: Faranga - Rwanda


    Zoezi la 1.3

    Katika makundi ya wanafunzi wawili wawili, onyesheni aina za pesa ambazo

    hutumiwa katika nchi zifuatazo kwa kutunga sentensi sahihi. 

    Kwa mfano: Tanzania


    Zoezi la utafiti

    Katika makundi ya wanafunzi wawili wawili, badilisheni pesa za kigeni zifuatazo
    ziwe katika faranga za Rwanda kama ilivyo sasa hivi.

    Kwa mfano:
    Shilingi elfu moja za Kenya = Faranga elfu saba na mia tano za Rwanda
    1. Dola hamsini za Marekani
    2. Shilingi mia mbili za Uganda
    3. Shilingi hamsini za Tanzania
    4. Yuro tano za Ulaya
    5. Naira mia moja za Naijeria
    1.4 Kusikiliza na kuzungumza: Maigizo
    Katika makundi ya wanafunzi wawili wawili, igizeni mazungumzo mliyosoma
    hapo awali kati ya Mtalii na Mpokeaji. 

    1.5 Sarufi: Viulizi ‘nani’ na ‘nini’

    Katika makundi ya wanafunzi wawili wawili, someni sentensi zifuatazo kisha

    mfanye mazoezi yanayofuata.


    1. Nani atamaliza wiki mbili nchini Rwanda?
     Jibu: Mtalii.
    2. Nini kinavutia katika mbuga ya Akagera?
    Jibu: Wanyamapori kwa mfano: simba.
    3. Nani alimpa mtalii maelezo kuhusu hoteli ya kuishi?
    Jibu: Mpokeaji wa watalii.
    4. Nani atarudi mwaka ujao kwa shughuli za utalii?
    Jibu: Mtalii.
    5. Ni nini mtalii atalipa ili kuzuru mbuga ya wanyama?
    Jibu: Pesa za kiingilio

    Zoezi la 1.4

    Katika makundi ya wanafunzi wawili wawili, ulizeni maswali mliyosoma hapo
    juu kwa kuanza na kiulizi ‘je’.

    Kwa mfano: 
    Je, ni nani atamaliza wiki mbili nchini Rwanda? 

    Zoezi la 1.5

    Katika makundi ya wanafunzi wawili wawili, jazeni nafasi zilizoachwa wazi
    katika sentensi hizi kwa jibu sahihi kutoka kwenye mabano. 



    Maelezo muhimu!
    Maneno yaliyopigiwa mistari huitwa viulizi. Haya ni maneno
    ambayo hutumiwa kuulizia maswali. 
    Kwa mfano:

    i) Nani alikulipia karo ya muhula uliopita?
    Neno ‘nani’ linauliza kuhusu mtu aliyetenda kitendo cha kulipa
    karo. 
    ii) Nini kimekuhuzunisha?

    Neno ‘nini’ linauliza kuhusu kitu au jambo ambalo limemhuzunisha
    anayehusika.
    • Maneno ‘nani’ na ‘nini’ hayaongezewi viambishi ngeli vyovyote. 

    Zoezi la 1.6

    Tunga sentensi tano sahihi kwa kutumia kiulizi ‘nani’ na sentensi nyingine

    tano sahihi kwa kutumia kiulizi ‘nini’.

    Somo la 2 :  Mbuga za wanyama

    2.1 Kifungu kuhusu mbuga za wanyama nchini Rwanda

    Katika makundi ya wanafunzi wawili wawili, jadilini kuhusu mnachokiona
    katika picha hizi kisha, mjitokeze mbele ya wanafunzi wenzenu ili muwaeleze.
    Baadaye, msome kifungu kinachofuata cha habari kuhusu mbuga za wanyama
    zinazopatikana nchini Rwanda.


       

    Maswali ya ufahamu

    Katika makundi ya wanafunzi wawili wawili, someni tena kifungu cha habari
    kuhusu mbuga za wanyama kisha mjibu maswali yafuatayo.
    1. Nchi ya Rwanda inapatikana wapi?
    2. Je, ni vivutio gani vya utalii vinavyopatikana nchini Rwanda?
    3. Mbuga ya wanyama ya Akagera inahifadhi wanyama gani?
    4. Eleza sifa za mbuga ya Akagera.
    5. Mbuga ya wanyama ya milima mirefu inapatikana katika sehemu gani?
    Taja milima mirefu minne inayopatikana hapo.
    6. Mbuga hii inasifiwa kwa sababu ya kuwa na wanyama gani? Kwa nini
    wanyama hao wanapendwa sana na watalii?
    7. Je, ni sherehe gani inayofanywa kila mwaka kuhusiana na wanyama hao?
    8. Mbuga ya wanyama ya msitu wa Nyungwe inajulikana kwa sifa gani?
    9. Je, ni faida gani tunazopata kutokana na shughuli ya utalii?
    10. Ni mambo gani yanayostahili kukomeshwa ili utalii uweze kuendelea na
    kustawi? 

    2.2 Msamiati kuhusu mbuga za wanyama

    Katika makundi ya wanafunzi wawili wawili, tafuteni msamiati mpya katika
    kifungu cha habari mlichosoma kisha mueleze maana ya msamiati huo.
    Zingatieni matumizi ya msamiati huo katika kifungu hicho na mtumie kamusi
    pale panapohitajika. 

    Kwa mfano:

    msitu – eneo kubwa lisilokuwa na watu lenye mimea mingi

    Zoezi la 2.1

    Katika makundi ya wanafunzi wawili wawili, husisheni kwa usahihi maneno
    yaliyoandikwa katika sehemu A na maelezo yake katika sehemu B. Zingatieni
    mfano uliotolewa.


    Zoezi la 2.2

    Katika makundi ya wanafunzi wawili wawili, husisheni kwa usahihi sentensi
    zilizo hapo chini na picha zifuatazo.



    1. Mlima huu ni mrefu kuliko milima mingine nchini Rwanda.
    2. Mnyama huyu ana pembe ndefu.
    3. Ziwa hili lina kisiwa kimoja kilicho na vibanda vingi.
    4. Pundamilia na nyati huishi katika msitu huu.
    5. Ziwa hili lina samaki wengi.

    2.3 Matumizi ya lugha: Majadiliano

    Katika makundi ya wanafunzi watatu watatu, jaribuni kujadiliana kuhusu
    sifa za vivutio vya utalii mlivyojadili katika kifungu cha habari mlichosoma
    hapo awali. Tajeni vivutio ambavyo mngependa kutembelea huku mkitoa
    sababu za chaguo lenu. 

    2.3.1 Kuandika ufupisho/ Muhtasari

    Katika makundi ya wanafunzi watatu watatu, elezeni mambo muhimu
    yaliyozungumziwa katika kifungu cha habari mlichosoma. Msinakili sentensi
    zilizotumiwa katika kifungu hicho, jaribuni kutumia maneno yenu na kuunda
    sentensi zenu zilizofupishwa. Tumieni maneno yasiyozidi mia moja (100). 

    Maelezo muhimu

    Kabla ya kuandika ufupisho wenu ni vyema: 

    1. Kusoma kwa makini kifungu kilichopo na kuandika mawazo muhimu.
    Soma mara tatu ili kuelewa vizuri.
    2. Kujibu maswali haya:
    • Kifungu cha habari kinahusu nini? (Andika sentensi moja)
    • Kifungu hiki kina aya ngapi? (Tambua aya zinazojenga kifungu hiki).
    • Andikeni wazo moja kutoka kwa kila aya.
    3. Kuunganisha mawazo mliyoorodhesha na kuandika habari kamili. Ili
    mwandike vizuri ni vyema:
    • Kutumia maneno yenu wenyewe (msitumie maneno pamoja na sentensi
    zilizotumiwa katika kifungu cha habari mlichokisoma)
    • Kutoa maelezo bila kupotosha ujumbe asilia.
    • Kuhakikisha kuwa mmerejelea mawazo yote muhimu yanayopatikana
    katika kifungu cha habari mlichokisoma.
    • Kuhakikisha kuwa hakuna makosa ya kisarufi.
    • Kuhakikisha kwamba mmezingatia urefu unaofaa.
    • Kuzingatia matumizi ya alama za uandishi.
    Habari hiyo mliyoandika kwa kuzingatia maelekezo hayo hapo juu ni
    muhtasari au ufupisho wa habari asilia mliyosoma. Neno ‘ufupisho’
    linatokana na kitenzi ‘fupisha’ lenye maana ya ‘kufanya maelezo kuwa
    mafupi au kupunguza urefu wake’. 

    Mfano wa ufupisho wa kifungu kuhusu mbuga za
    wanyama


    Rwanda ni nchi iliyo na vivutio vingi vya kitalii kama vile: mito
    mbalimbali, mbuga za wanyama, misitu ya kiasili, hoteli nzuri, maziwa,
    milima mirefu pamoja na nyumba za kuhifadhia vifaa vya utamaduni wetu.
    Mbuga ya wanyama ya Akagera inapendwa na watu wengi. Mbuga hii ina
    wanyama kama vile: pundamilia, swara, paa, twiga, vifaru, tembo, simba
    pamoja na wanyama wengine. Pia, mbuga hii ina savana ya kupendeza.
    Mbuga ya wanyama ya milima mirefu ya Virunga huvutia kwa milima yake
    mirefu kama vile: Kalisimbi, Muhabura, Bisoke, Sabyinyo, Nyamuragira na
    Nyiragongo. Mbuga hii pia inajulikana kwa wanyama wanaoitwa ‘sokwe
    watu’.

    Mbuga ya msitu wa Nyungwe inafahamika kwa miti yake mirefu sana
    pamoja na ndege wa aina nyingi wasiopatikana kwingi ulimwenguni. Vivutio
    hivi vina manufaa mengi ya kiuchumi kwa Wanyarwanda. Ni lengo la kila
    Mnyarwanda kuhakikisha kuwa anatunza vivutio hivi ili utalii uendelee
    kutufaidi. (Maneno 140 )

    2.4 Kusikiliza na kuzungumza: Majadiliano

    Katika makundi ya wanafunzi wawili wawili, jadilini kuhusu mbuga za wanyama
    zinazopatikana nchini Rwanda na kuyaandika maelezo yenu kwa ufupi halafu
    mjitokeze mbele ya wanafunzi wenzenu na kuwasomea kuhusu mbuga hizo

    pamoja na sifa zao.

    2.5 Sarufi: Kiulizi ‘lini’

    Jigaweni katika makundi ya wanafunzi wawili wawili ili mchunguze sentensi
    zifuatazo katika umoja na wingi kisha mfanye zoezi linalofuata.



    Zoezi la 2.3

    Katika makundi ya wanafunzi wawili wawili:

    1. Jadilini aina ya neno lililopigiwa mstari katika sentensi mlizopewa.
    2. Jadilini mabadiliko ya sentensi hizo yanayojitokeza katika umoja na wingi.
    3. Tungeni sentensi tano sahihi kwa kutumia neno lililopigiwa mstari.

    Zoezi la 2.4

    Katika makundi yenu ya wanafunzi wawili wawili, jazeni nafasi zilizo wazi

    katika sentensi hizi kwa jibu sahihi kutoka kwenye mabano.

    Maelezo muhimu!

    Neno ‘lini’ ni kiulizi cha wakati. Hutumika katika sentensi kuulizia

    wakati wa kutendeka kwa kitendo fulani. 

    Kwa mfano: Utasafisha chumba cha mgonjwa lini?
    Jibu:      Kesho jioni.
    Jibu linalotolewa kwa sentensi iliyo na neno ‘lini’ linaonyesha majira
    mbalimbali ya wakati kama vile: majira ya siku (asubuhi, usiku, alasiri,
    mchana, jioni), saa, siku, wiki, mwezi, mwaka miongoni mwa nyakati

    nyingine.

    Zoezi la 2.5

    Katika makundi ya wanafunzi watatu watatu, andikeni sentensi hizi upya

    katika hali ya kuuliza kwa kufuata maagizo yaliyo kwenye mabano.

    Kwa mfano: Mgeni ataondoka kesho jioni. (Tumia: lini)
    Jibu: Mgeni ataondoka lini?
    1. Mtalii alizuru mbuga ya wanyama. (Tumia: Nani)
    2. Chakula hiki kitaliwa kesho. (Tumia: Nini)
    3. Watalii kutoka Marekani watafika kesho asubuhi. (Tumia: lini)
    4. Mwelekezaji atawapeleka watalii mjini Kigali. (Tumia: Nani)
    5. Kisu kitanunuliwa sokoni. (Tumia: Nini)

    Zoezi la 2.6

    A. Tunga sentensi tano sahihi kwa kutumia kiulizi ‘lini’.

    B. Andika sentensi ulizotunga katika sehemu A katika umoja au wingi.

    SOMO LA 3: Mwelekezaji na MtaliiSOMO LA 3: Mwelekezaji na Mtalii

    3.1 Mazungumzo kati ya Mwelekezaji na Mtalii
    Tazameni mchoro huu katika makundi ya wanafunzi watatu watatu kisha
    mwelezane mnachokiona.





    

    

    Maswali ya ufahamu

    Katika makundi ya wanafunzi watatu watatu, someni tena kifungu cha
    mazungumzo kati ya Mwelekezaji na Mtalii, kisha mjibu maswali haya.

    1. Kwa nini wanyama hufurahia kuishi katika mazingira ya mbuga ya
    Akagera?
    2. Taja vitu vilivyomfurahisha mgeni wa kitalii.
    3. Mgeni huyu alifika lini nchini Rwanda?
    4. Mgeni huyu wa kitalii atarudi nchini kwao lini?
    5. Ni wanyama gani wanaopatikana katika mbuga ya wanyama ya Akagera?
    6. Ndovu mwenye umri mrefu kuliko wengine ana sifa gani?
    7. Sungura hupenda nini?
    8. Ili sungura wasitoroke mwelekezaji alifanya nini?
    9. Ni wakati gani wanyama hujificha?

    10. Waharibifu wa mazingira hufanya nini?

    3.2 Msamiati kuhusu ziara ya kitalii

    Katika makundi ya wanafunzi watatu watatu, tafuteni msamiati mpya kutoka
    katika kifungu cha mazungumzo mlichosoma hapo juu na kuueleza. Zingatieni
    matumizi ya msamiati huo katika kifungu hicho na mtumie kamusi pale

    inapohitajika. 

    Zoezi la 3.1

    Katika makundi ya wanafunzi wawili wawili, husisheni kwa usahihi msamiati

    katika sehemu A na maelezo yake katika sehemu B. Zingatieni mfano uliopo.

    Zoezi la 3.2

    Katika makundi ya wanafunzi wawili wawili, husisheni kwa usahihi michoro

    na picha hizi na sentensi zinazofuata. 


    1. Watalii wanawatazama wanyama katika mbuga ya Akagera.
    2. Mtoto wa simba anaitwa shibli.
    3. Msitu wa Virunga una miti mingi na sokwe wengi.
    4. Walinzi wa mbuga za wanyama wamewashika wasasi waliokuwa
    wakiwinda ndovu kwa ajili ya pembe zao.

    5. Wanafunzi walienda kuzuru mbuga ya Wanyama.

    3.3 Matumizi ya lugha: Majadiliano

    Katika makundi ya wanafunzi wawili wawili, jadilini kuhusu wanyamapori
    ambao mmewahi kuwaona kwa kuelezana:
    1. Majina ya wanyamapori hao.
    2. Sifa za wanyamapori hao.
    3. Chakula cha wanyamapori hao.
    4. Maumbile ya wanyamapori hao.
    5. Uliwaona wanyama hao wapi?

    6. Wanyamapori hao wanapenda kuishi katika mazingira ya aina gani?

    A. Chunguza picha za wanyama hawa na kuzihusisha na majina yao sahihi


    B. Katika makundi ya wanafunzi wawili wawili, onyesheni wanyama ambao
    hufugwa na wanyamapori (wanyama wasiofugwa) kati ya wanyama walio

    hapo juu.

    3.4 Kusikiliza na kuzungumza: Maigizo

    Katika makundi ya wanafunzi wawili wawili, igizeni mazungumzo mliyosoma

    kati ya Mwelekezaji na Mtalii wa kigeni. 

    3.5 Sarufi

    Viulizi ‘wapi’ na ‘vipi’
    Katika makundi ya wanafunzi wawili wawili, chunguzeni sentensi zifuatazo kisha
    mjibu maswali haya.

    Sentensi 1: Kila siku tunapokea watalii wengi kutoka Marekani.
    Swali: Kila siku tunapokea watalii wengi kutoka wapi?
    Sentensi 2: Mgeni alihudumiwa vizuri.
    Swali: Mgeni alihudumiwa vipi?
    Sentensi 3: Mgeni alifurahishwa na huduma ya hoteli.
    Swali: Mgeni alifurahishwa na huduma ya wapi?
    Sentensi 4: Ndovu alionekana mpole.
    Swali: Ndovu alionekana vipi?

    Je, mmegundua nini?

    Zoezi la 3.4

    Katika makundi ya wanafunzi wawili wawili, tungeni sentensi tano kama hizo
    zilizoandikwa hapo juu. Kutokana na sentensi utakazotunga, tunga maswali

    yake kwa kutumia neno ‘wapi’

    Maelezo muhimu!


    Zoezi la 3.5

    Tunga maswali kuhusu maneno yaliyopigiwa mstari katika sentensi hizi kwa

    kutumia viulizi sahihi.

    Kwa mfano:
                                       1. Mwanafunzi huyu anasomea Uchina

    Jibu:                        Mwanafunzi huyu anasomea wapi?

    2.Mwanafunzi   huyu anaandika vizuri

    Jibu:                         Mwanafunzi huyu anaandika vipi?

    1. Dereva huyu anatoka Afrika Kusini.
    2. Sembare anaingia chumbani mwake haraka.
    3. Gari la mtalii limesimama nje ya nyumba yetu.
    4. Simba anajificha vichakani.

    5. Ndugu yangu anatembea polepole

    Zoezi la 3.6

    Katika makundi ya wanafunzi wawili wawili, tungeni sentensi tano katika

    umoja na wingi kwa kutumia viulizi ‘wapi’ na ‘vipi

    Zoezi la 3.7

    Jaza nafasi zilizoachwa wazi kwa kutumia jibu sahihi kutoka kwa yaliyo
    kwenye mabano.
    1. Kijana mmoja alienda _________ ? (nani, nini, wapi)
    2. Waziri ataondoka _________ ? (nani, vipi, nini)
    3. Mtumishi amepoteza ufagio wake ___________? (lini, nani, wapi)
    4. Fundi hodari amejenga nyumba __________? (nani, vipi, nini)

    5. Mwalimu wetu ameenda __________? (nani, nini, wapi) 

    3.5.1 Kiulizi ‘kwa nini’

    Katika makundi ya wanafunzi wawili wawili, chunguzeni sentensi zifuatazo.
    Sentensi 1: Mtalii atatembelea mbuga ya wanyama ili kuwaona
     wanyamapori.
    SwaliKwa nini mtalii atatembelea mbuga ya wanyama?
    Sentensi 2: Mgeni alifurahi kwa sababu alipewa huduma nzuri.
    Swali: Kwa nini mgeni alifurahi? 

    Zoezi la 3.8

    1. Katika makundi ya wanafunzi wawili, tungeni sentensi mbili mbili kama
    hizo zilizoandikwa hapo juu. (Sentensi 1 na 2)
    2. Tunga maswali kwa sentensi mlizotunga katika swali la 1 hapo juu.
    (Hakikisha kuwa mmetumia kwa nini katika maswali yenu).
    
    Maelezo muhimu!
     Maneno ‘kwa nini’ yanatumiwa kuulizia sababu ya kufanyika
     kwa jambo fulani
    .
    Kwa mfano:
    Sentensi 1: Mwanafunzi huyu alipewa zawadi kwa sababu
                             anathamini mazingira yake.
    • Swali: Kwa nini mwanafunzi huyu alipewa zawadi?
    (Maneno ‘kwa nini’ yametumiwa kuulizia sababu ya kupewa zawadi

    kwa mwanafunzi huyu).

    • Sentensi 2: Waelekezaji walipewa mafundisho ili wajue namna
     ya kuwapokea wageni.
    • Swali: Kwa nini waelekezaji walipewa mafundisho?
    (Maneno ‘kwa nini’ yametumiwa kuulizia sababu ya waelekezaji
    kupewa mafundisho). Maneno ya kuulizia maswali huitwa viulizi.

    Zoezi la 3.9
    Katika makundi ya wanafunzi wawili wawili, ulizeni maswali kuhusu maneno
    na vifungu vya maneno vilivyopigiwa mstari katika sentensi hizi.

    Kwa mfano: Mtalii huyu hupenda kuja Rwanda kwa sababu Rwanda

    ni nchi nzuri.

    Jibu: Kwa nini mtalii huyu hupenda kuja Rwanda

    1. Mtoto huyu analia kwa sababu anataka chakula.
    2. Mkulima huyu alichinja mbuzi mmoja kwa sababu ana wageni.
    3. Mukandori anakaa katika nyumba hii kwa sababu alihamishwa kikazi.
    4. Mtu huyu amepelekwa jela kwa sababu alihukumiwa kifungo cha miaka
    miwili.
    5. Mama na baba wamekaa sebuleni kwa sababu wanazungumza na
    wageni wetu. 
    
    SOMO LA 4: Utamaduni na utalii
    
    4.1 Kifungu kuhusu utamaduni na utalii

    Katika makundi ya wanafunzi wawili wawili, chunguzeni picha hizi kisha mjadili

    kuhusu mnachokiona na kuwaelezea wenzenu.


    Soma kifungu cha habari kinachofuata kuhusu utamaduni na utalii kisha mjibu
    maswali yanayofuata. Kifungu hiki kinaeleza jinsi utamaduni unavyoweza

    kutumiwa katika utalii na kuleta manufaa kwa nchi.

    Maswali ya ufahamu

    I. Katika makundi ya wanafunzi wawili wawili, someni tena kifungu cha
    ufahamu kilichotangulia kisha mjibu maswali yafuatayo.
    1. Kwa nini watu wengi hawaelewi umuhimu wa utamaduni?
    2. Utamaduni unahusu nini?
    3. Ni mambo gani yanayofanywa ili kuhifadhi utamaduni wetu?
    4. Taja maeneo ambapo tunaweza kupata nyumba za kuhifadhia
    utamaduni wetu?
    5. Taja vitu tunavyoweza kupata katika nyumba ya kuhifadhi utamaduni
    wetu iliyoko wilayani Huye.
    6. Nyumba iliyoko wilayani Nyanza ilikuwa makazi ya nani?
    7. Ni vitu gani vya kuvutia ambavyo tunaweza kukuta katika nyumba
    hiyo?

    8. Kwa nini tunafaa kujivunia utamaduni wetu?

    II. Katika makundi ya wanafunzi watatu watatu, andikeni kwa ufupi kifungu

    cha habari mlichosoma hapo juu. Tumieni maneno sabini (70). 

    4.2 Msamiati kuhusu utamaduni

    Katika makundi ya wanafunzi wawili wawili, tafuteni msamiati mpya kutoka
    katika kifungu cha habari mlichosoma kilichotangulia na kuueleza. Zingatieni
    matumizi ya msamiati huo katika kifungu hicho na mtumie kamusi pale

    panapohitajika. 

    Zoezi la 4.1

    Katika makundi ya wanafunzi wawili wawili, husisheni maneno yaliyoandikwa

    katika sehemu A na maelezo yake katika sehemu B. Zingatieni mfano uliopo.

    Zoezi la 4.2

    Katika makundi ya wanafunzi wawili wawili,
    husisheni mchoro na picha hizi na sentensi zifuatazo kwa usahihi.

    1. Wageni hupokelewa katika sebule hii nzuri kwa mazungumzo.
    2. Mama yangu huvaa taji la kitamaduni katika sherehe za harusi.
    3. Babu anawasimulia wajukuu wake hadithi ya kusisimua.
    4. Huu ni mtindo tofauti wa kukata nywele unaoitwa ‘Amasunzu’.

    5. Haya ni makazi yetu. Tuna nyumba nzuri ya kisasa.

    4.3 Matumizi ya lugha: Zoezi la msamiati

    Katika makundi ya wanafunzi wawili wawili, jazeni herufi zilizoachwa wazi

    katika visanduku vifuatavyo ili kuunda neno kamili. 

    4.4 Kusikiliza na kuzungumza: Majadiliano

    Katika makundi ya wanafunzi watatu watatu, jadilini kuhusu utamaduni na
    utalii halafu mjitokezee mbele ya wanafunzi wenzenu kuwaeleza kuhusu yale
    mliyoafikiana. Jaribuni kuhakikisha kwamba mmejibu maswali haya katika
    majadiliano yenu:
    1. Utamaduni unahusu nini?
    2. Utamaduni wa Wanyarwanda unatambulishwa na nini?
    3. Utamaduni unaweza kuvutia watalii?
    4. Ni faida gani tunaweza kupata kutokana na utamaduni?
    5. Tunaweza kufanya nini ili kuhifadhi utamaduni wetu?

    6. Ni hasara gani tunaweza kupata iwapo hatutathamini utamaduni wetu?

    4.5 Sarufi: Wakati wa mazoea, tungo yakinishi

    Katika makundi ya wanafunzi wawili wawili, someni sentensi zinazofuata katika

    umoja na wingi kisha mfanye zoezi lililo hapo chini.

    Zoezi la 4.3

    1. Katika makundi ya wanafunzi wawili wawili, tungeni sentensi moja moja
    kwa kutumia neno kila siku na kitenzi pika katika nafsi zifuatazo: mimi,
    wewe, yeye, sisinyinyi na wao.
    2. Linganisheni sentensi zenu na zile ulizotolewa hapo juu kuhusu kitenzi

    enda, chota na cheza.

    Maelezo muhimu!

    • Sehemu za kitenzi endachota na cheza zinaandikwa baada ya
    kutumia hu.
    • ‘hu’ inarudiwarudiwa katika vitenzi vyote baada ya nafsi mimi,
    wewe, yeye sisi, nyinyi na wao.
    • ‘hu’ inatumiwa kuonyesha kitendo kinachofanywa mara kwa mara,
    kila wakati.
    Kwa mfano: Mimi huchota maji kila asubuhi. (Kitendo cha kuchota
    maji kinafanywa kila asubuhi)
    • Kitenzi chota kimetumiwa katika wakati wa mazoea ili
    kuonyesha kuwa kitendo hicho kinafanywa kila asubuhi.

    Zoezi la 4.4

    Katika makundi ya wanafunzi wawili wawili, andikeni sentensi zifuatazo kwa
    kutumia wakati wa mazoea.
    Kwa mfano: Wachezaji hawa wanapenda kucheza kila jioni.
    Jibu: Wachezaji hawa hupenda kucheza kila jioni.
    1. Wagonjwa hawa wanapelekwa hospitalini kwa magari haya.
    2. Waimbaji hawa wanapata fedha nyingi kila wiki.
    3. Wageni wetu watafika kwenye uwanja wa ndege kabla ya saa kumi.
    4. Mimi nitatembea kwa miguu hadi kanisani.
    5. Mwalimu wetu ataondoka saa kumi na moja.

    Zoezi la 4.5
    Katika makundi ya wanafunzi wawili wawili, andikeni majibu ya sentensi
    za Zoezi la 4.4 (lililo hapo juu) katika umoja au wingi.
    Kwa mfano: Wachezaji hawa hupenda kucheza kila jioni.
    Jibu: Mchezaji huyu hupenda kucheza kila jioni.

    
    SOMO LA 5: Milima yetu
    

    5.1 Kifungu kuhusu ‘Milima yetu’

    Katika makundi ya wanafunzi wawili wawili, tazameni picha zifuatazo kisha
    mjadili kuhusu kile kinachoendelea au mnachokiona katika picha hizi kwa

    kujitokeza mbele ya wanafunzi wenzenu na kuwaelezea.


    Katika makundi ya wanafunzi wawili wawili, someni kifungu cha habari
    kinachofuata kuhusu ‘Milima yetu’ kisha mjibu maswali yanayofuata. Kifungu
    hiki kinaelezea milima mbalimbali inayopatikana nchini Rwanda na mazingira

    yake mazuri yanayovutia sana. 

    Maswali ya ufahamu

    I. Katika makundi ya wanafunzi wawili wawili, someni tena kifungu cha habari
    kilichotangulia, kisha mjibu maswali haya.
    1. Kwa nini watu wengi huita Rwanda ‘nchi yenye milima elfu moja’?
    2. Ni faida gani tunazopata kutokana na misitu yetu?
    3. Taja misitu mikubwa iliyozungumziwa katika kifungu hiki cha habari.
    4. Taja milima minne mirefu iliyozungumziwa katika habari hii.
    5. Milima hiyo hupatikana katika sehemu gani ya nchi yetu?
    6. Taja wilaya mbili na mlima mmoja mmoja unaopatikana katika kila
    wilaya.
    7. Ni kwa nini Mlima Kageyo unajulikana?
    8. Mwamba wa Ndaba una sifa gani?
    9. Serikali ya Rwanda huomba Wanyarwanda kufanya nini?
    10. Ni funzo gani tunalopata kutoka kwa viongozi wetu?
    II. Katika makundi ya wanafunzi watatu watatu, andikeni habari hii kwa ufupi.
    Tumieni idadi ya maneno mia moja. 

    5.2 Msamiati kuhusu ‘Milima yetu’

    Katika makundi ya wanafunzi wawili wawili, tafuteni msamiati mpya kutoka
    katika kifungu cha habari kilicho hapo juu na kuueleza. Zingatieni matumizi ya

    msamiati huo katika kifungu hicho na mtumie kamusi pale panapohitajika.

    Zoezi la 5.1

    Katika makundi ya wanafunzi wawili wawili, chunguzeni sentensi zifuatazo
    kisha mtunge sentensi zenu kwa kutumia maneno yaliyopigiwa mistari.
    1. Miongoni mwa viumbe wote, binadamu ndiye mwenye akili.
    2. Mjini Kigali kuna magari mengi mno.
    3. Hapa kuna mteremko mrefu, jihadhari usianguke.
    4. Watu wengi wananunua rangi hii kwa sababu inavutia sana.
    5. Mvua haijanyesha kwa muda mrefu; kuna ukame na wanyama wetu
    wamekosa maji na chakula.
    6. Mtu huyu alishikwa na polisi kwa sababu anaharibu mazingira kwa
    kuchoma misitu.
    7. Huwezi kulima hapa kwa sababu kuna mwamba mkubwa.

    8. Ni lazima kila mwananchi afanye kazi ili kupambana na umaskini.

    Zoezi la 5.2

    Katika makundi ya wanafunzi wawili wawili, husisheni mchoro na picha

    pamoja na sentensi ulizopewa hapo chini kwa usahihi.

    1. Mlima huu ni mrefu sana kuliko milima mingine.
    2. Watu hawa wanapanda miti.
    3. Msitu huu una ndovu wengi.

    4. Mteremko wa maji katika eneo hili unavutia sana.

    5.3 Matumizi ya lugha: Zoezi la jedwali

    Katika makundi ya wanafunzi wawili wawili, jazeni nafasi zilizoachwa wazi kwa

    kuzingatia maelezo yaliyo chini ya jedwali.

    Kwenda kulia

    1. Mtu anayetembelea mahali pa kuvutia kwa kujifurahisha
    4. Aina ya silaha inayotumiwa kukata mti
    5. Muda wa saa ishirini na nne
    8. Kujinyosha kitandani ili kupata usingizi
    10. Ndege jike anayefugwa
    12. Kupata kiumbe kichanga baada ya kukomaa kwa mimba
    14. Mimea mikubwa iliyopandwa shambani au kuota mwituni

    15. Sarafu ya Marekani

    Kwenda chini

    1. Mtu anayefanya kazi ya kulinda
    2. Azuru mbuga za wanyama
    3. Sehemu yenye pori, vichaka na nyasi au mwitu
    6. Kuangalia upande kilipo kitu fulani au kuenda mahali fulani
    7. Sehemu ya ardhi inayoinuka juu sana
    9. Safari ya kuzuru mahali kwa sababu maalumu
    11. Ukosefu wa maji
    13. Mnyama wa porini anayefanana na mbuzi

    5.4 Kusikiliza na kuzungumza: Majadiliano

    Katika makundi ya wanafunzi watatu watatu, jadilini kuhusu faida za utalii kwa
    wananchi halafu mjitokeze mbele ya darasa ili muwaeleze wanafunzi wenzenu
    kuhusu hoja mlizozipata. Katika majadiliano yenu, hakikisheni mmejibu maswali

    haya:

    1. Utalii ni nini?
    2. Ni sehemu zipi za utalii zilizo nchini mwetu?
    3. Ni watu gani wanaokuja kutalii nchini mwetu?
    4. Nchi yetu ina faida gani kwa kupokea watalii wengi?

    5. Wananchi wanapata faida gani kutokana na utalii?

    5.5 Sarufi: Wakati wa mazoea, tungo kanushi

    Katika makundi ya wanafunzi wawili wawili, someni sentensi zinazofuata katika

    umoja na wingi kisha mfanye zoezi lililo hapo chini.

    Zoezi la 5.3

    Katika makundi ya wanafunzi wawili wawili, tungeni sentensi moja moja kwa
    kutumia wakati wa mazoea (tungo yakinishi na tungo kanushi). Tumia nafsi

    zifuatazo: mimi, wewe, yeye, sisi, nyinyi na wao.

    Maelezo muhimu!

    Kiambishi hu’ kinarudiwarudiwa katika nafsi zote za tungo yakinishi.
    Kikanushi ‘ha’ hutumiwa katika vitenzi vinavyoisha kwa irabu ‘i’
    badala ya irabu ‘a’ katika tungo kanushi.
    Kwa mfano: Sisi hupandmiti. (tungo yakinishi)
     Sisi hatupandi miti. (tungo kanushi)
    Viambishi vya nafsi hutumiwa baada ya kikanushi ‘ha’ na hubadilika

    kulingana na nafsi au ngeli inayohusika.

    Kwa mfano: 


    Zoezi la 5.4

    Katika makundi ya wanafunzi wawili wawili, andikeni vitenzi vilivyo kwenye

    mabano kwa kutumia wakati wa mazoea, tungo yakinishi.

    Kwa mfano: Mtoto huyu _____ (kuchelewa) kufika shuleni kila asubuhi.

    Jibu: Mtoto huyu huchelewa kufika shuleni kila asubuhi.

    1. Wewe ______________ (kuandika) barua ndefu.

    2. Sisi ______________ (kusaidia) walemavu katika kijiji hiki.

    3. Watalii hawa ____________ (kufurahia) mazingira ya milima mirefu.

    4. Mkulima huyu ____________ (kupanda) miti katika mashamba yake.

    5. Mti huu ______________ (kuzaa) matunda mengi kila mwaka. 

    Zoezi la 5.5

    Katika makundi ya wanafunzi wawili wawili, andikeni sentensi za zoezi la 5.4

    lililotangulia katika tungo kanushi

    Kwa mfano:
    Sentensi: Mtoto huyu huchelewa kufika shuleni kila asubuhi.

    Jibu: Mtoto huyu hachelewi kufika shuleni kila asubuhi.

    Zoezi la 5.6

    Katika makundi ya wanafunzi wawili wawili, kanusheni tungo hizi kwa

    kuziandika katika umoja na wingi. 

    Kwa mfano: Kitabu changu hupendwa na watu wengi.
    Jibu: Umoja: Kitabu changu hakipendwi na watu wengi.
     Wingi: Vitabu vyetu havipendwi na watu wengi.
    1. Mwanafunzi yule hujibu vizuri maswali ya mwalimu.
    2. Mtalii hutembelea mbuga zetu za wanyama kila siku.
    3. Ukucha huu hupakwa rangi nyeupe baada ya mwezi mmoja.
    4. Ndege yule hulala kwenye mti huu.

    5. Kitanda chako hutumiwa na wageni wetu.

    SOMO LA 6: Maji yetu

    6.1 Kifungu kuhusu ‘Maji yetu’


    Katika makundi ya wanafunzi wawili wawili, someni kifungu cha habari

    kinachofuata ambacho kinahusu ‘Maji yetu’ kisha mjibu maswali yanayofuata. 



    Maswali ya ufahamu

    I. Katika makundi ya wanafunzi wawili wawili, someni tena kifungu cha habari
    kilichotangulia kisha mjibu maswali haya.

    1. Maji yana umuhimu gani kwa afya yetu?
    2. Maji huweza kutumiwa katika shughuli gani?
    3. Ni mambo gani yanayoweza kutokea iwapo tutakosa maji?
    4. Kwa nini nchi ya Rwanda ina maji ya kutosha?
    5. Taja maziwa matatu yapatikanayo nchini Rwanda na ueleze sehemu
    yanakopatikana.
    6. Taja mito iliyozungumziwa katika kifungu hiki.
    7. Ni vituo gani vilivyojengwa ili kutuletea nguvu za umeme?
    8. Rwanda inahesabiwa katika ukanda upi?
    9. Ukanda huo unazihusisha nchi gani?

    10. Taja mambo mawili ambayo watalii huyafurahia.

    II. Katika makundi ya wanafunzi wawili wawili, fupisheni kifungu cha habari
    mlichosoma hapo awali. Tumieni idadi ya maneno mia moja pekee.
    6.2 Msamiati kuhusu ‘Maji yetu’
    Zoezi la 6.1
    katika kifungu cha habari kilicho hapo juu na kuueleza. Zingatieni matumizi ya

    msamiati huo katika kifungu hicho na mtumie kamusi pale panapohitajika.

    1. Mwalimu wetu anatimiza kazi yake kwa kutufundisha vizuri.
    2. Mimi hufua nguo zangu kila Jumamosi kwa kutumia maji safi na
    sabuni.
    3. Ukosefu 
    wa mboga katika chakula unaweza kusababisha magonjwa
    mengi katika mwili wa binadamu.
    4. Rwanda inataka kuongeza vituo vya kutengeneza nguvu za umeme
    kwa kutumia mito yake.

    5. Rwanda hupata gesi nyingi kutoka Ziwa Kivu. 

    Zoezi la 6.2

    Katika makundi ya wanafunzi wawili wawili, chagueni neno linalofaa kati ya
    maneno yafuatayo kisha mjaze nafasi zilizo wazi katika sentensi hizi.
    Mtalii, Mto, Mbuga ya wanyama, ziwa, mbinu, Kisiwa

    Kwa mfano: Mwalimu anatumia ________ nzuri kufundisha somo la
     Kiswahili.
    Jibu: Mwalimu anatumia mbinu nzuri kufundisha somo la Kiswahili.
    1. _______ cha Ijwi kinapatikana ziwani Kivu.
    2. _______ huyu alilipa pesa nyingi ili aweze kuingia katika nyumba hii
    ya kitalii.
    3. __________ ya Akagera inatembelewa na wageni wengi kutoka nchi
    mbalimbali.
    4. Walimu wetu wanatarajia kwenda Karongi ili kufurahia mazingira ya
    ______ la Muhazi.

    5. Watalii wawili walienda kwa gari zuri kutazama _______ Mukungwa.

    6.3 Matumizi ya lughaMajadiliano

    Zoezi la 6.3

    Je, umewahi kutembelea ziwa lolote nchini Rwanda? Umewahi kufika kwenye
    kisiwa chochote nchini Rwanda? Jadilini kuhusu ziara zenu katika makundi ya

    wanafunzi wanne wanne huku mkielezeana:

     (a) Mliwaona wanyama gani wa majini?                                                                    (b) Mliona mito gani?

     (ch) Mlipanda vyombo vipi vya majini?                                                                        (d) Mlivua samaki? 

    Zoezi la 6.4

    Mkiwa wawili wawili, husisheni kwa usahihi maneno yaliyoandikwa katika

    sehemu A na maelezo yake katika sehemu B.

    \

    Zoezi la 6.5

    Katika makundi ya wanafunzi wawili wawili, husisheni picha hizi na sentensi

    zinazofuata kwa usahihi.


    1. Hiki ni kituo cha kutengeneza nguvu za umeme katika Mto Nyabarongo.
    2. Ziwani kuna chombo cha kusafiria.
    3. Watalii wanatembea kwenye mchanga karibu na bahari hii.

    4. Mamba amelala kwenye ufuo wa mto huu.

    6.4 Kusikiliza na kuzungumza: Majadiliano

    Zoezi la 6.6

    Katika makundi ya wanafunzi wawili wawili, jadilini kuhusu faida za kiutalii
    tunazopata kutokana na maji halafu mjitokeze mbele ya darasa ili kuwaelezea
    wenzenu. Hakikisheni kuwa mnajibu maswali haya katika majadiliano yenu:
    1. Ni vivutio vipi vya utalii vyenye mazingira ya maji?
    2. Ni mambo gani ya kuvutia tunayopata katika vivutio hivyo?

    3. Vivutio hivyo vinatumiwa vipi kuleta faida kwa nchi yetu? 

    6.4.1 Zoezi la imla

    Funga kitabu chako kisha katika daftari lako, andika kwa usahihi kifungu

    ambacho mwalimu wako atakusomea

    6.5 Sarufi: Kiulizi ‘-pi’

    Katika makundi ya wanafunzi wawili wawili, chunguzeni maswali yafuatayo

    katika umoja na wingi kisha mwelezeane ugunduzi wenu.


    Zoezi la 6.7

    Katika makundi ya wanafunzi wawili wawili, tungeni sentensi tano katika

    umoja na wingi kwa kutumia kiulizi “-pi” katika ngeli mbalimbali za Kiswahili.

    Zoezi la 6.8

    Katika makundi ya wanafunzi wawili wawili, kamilisheni sentensi zifuatazo

    kwa kutumia kiulizi ‘-pi’ kwa usahihi.

    Kwa mfano: Kiti ______ kitakaliwa na mtalii?
     Jibu: Kiti kipi kitakaliwa na mtalii?
    1. Mtoto ______ anaweza kupika uji?
    2. Viatu _______ vilinunuliwa na wageni hawa?
    3. Ng’ombe ________ walichinjwa sokoni jana?
    4. Kikombe _______ kilijazwa chai?

    5. Ubao _______ ulitengenezwa wiki iliyopita?

    Zoezi la 6.9

    Andika sentensi za zoezi la 8 (la hapo awali) katika umoja au wingi.

    Kwa mfano:
    Sentensi: (Umoja) Kiti kipi kitakaliwa na mtalii?

    Jibu: (Wingi) Viti vipi vitakaliwa na watalii?

    Maelezo muhimu!

    Kiulizi ‘-pi’ hutumika kuulizia swali kwa kumtaka mtu achague kitu
    kimoja au vitu fulani miongoni mwa vitu vingine vilivyopo.

    Kwa mfano: 

    Swali: Mwanafunzi yupi ni mwerevu?
    Jibu: Mwanafunzi mwerevu ni Kamaliza.
    Wanafunzi ni wengi lakini mzungumzaji anauliza swali ili ajue
    mwanafunzi mwerevu miongoni mwa wanafunzi wengi.
    Swali: Wanafunzi wapi/ wepi ni werevu?
    Jibu: Wanafunzi werevu ni Kamaliza na Iradukunda.
    Wanafunzi ni wengi lakini mzungumzaji anauliza swali ili ajue
    wanafunzi werevu tu miongoni mwa wanafunzi wote waliopo.

    Kiulizi ‘-pi’ kinatumika kulingana na ngeli inayohusika.

    Kwa mfano:
    Umoja                                                              Wingi                                           Ngeli

    Mtoto yupi analia?                      Watoto wapi/wepi wanalia?             A-WA
    Kitabu kipi kinasomwa?           Vitabu vipi vinasomwa?                     KI-VI
    Mlima upi umepandwa?           Milima ipi imepandwa?                      U-I
    Nyumba ipi itajengwa?              Nyumba zipi zitajengwa?                  I-ZI
    Ukuta upi umebomoka?           Kuta zipi zimebomoka?                     U-ZI

    Tathmini ya mada ya 1
    Zoezi la 1

    Jibu maswali yafuatayo kwa usahihi.

    1. Taja vivutio vya utalii vilivyopo nchini Rwanda.
    2. Taja baadhi ya wanyama ambao hupatikana katika mbuga ya wanyama
    ya Akagera.
    3. Mbuga ya wanyama ya milima ya Virunga inajulikana kwa wanyama
    gani?
    4. Kwa nini sisi kama Wanyarwanda tunafaa kujivunia utamaduni wetu?

    Zoezi la 2

    Andika sentensi hizi kwa kutumia wakati wa mazoea.
    1. Wewe utaandika ubaoni wakati wa somo letu.
    2. Mimi na ndugu yangu tutapika chakula baada ya somo letu.
    3. Wewe na mtalii huyu mtafurahia kutazama mnyama yule.
    4. Mkulima huyu na Semana watalima shamba lao katika mwezi wa
    Februari.
    5. Wanafunzi hawa wanaimba nyimbo za kufurahisha. 

    Zoezi la 3
    Taja aina za pesa ambazo hutumiwa katika nchi zifuatazo.
    1. Naijeria
    2. Japani
    3. Malawi
    4. Rwanda

    5. Kanada

    Zoezi la 4

    Kamilisha sentensi zifuatazo kwa kutumia kiulizi ‘-pi’ kwa usahihi.
    1. Kioo ______ kilivunjika?
    2. Mlima ______ una wanyamapori wengi?
    3. Ufagio ______ uliharibika?
    4. Ndizi ______ ni ya mtoto huyu?

    5. Mzigo ______ ni wa mgeni huyu?

    Zoezi la 5

    Jaza nafasi zilizo wazi kwa jibu sahihi kutoka kwenye mabano.
    1. __________ alizuru mbuga ya Akagera? (Nini, Nani)
    2. __________ kitaliwa na wageni? (Nani, Nini)
    3. __________ hajawahi kumwona simba? (Nini, Nani)
    4. __________ kitaletwa na mhudumu wa hoteli? (Nani, Nini)

    5. __________ kilitumika kuwapiga picha wanyamapori? (Nani, Nini)

    Zoezi la 6

    Tunga sentensi tano sahihi kwa kutumia kiulizi ‘kwa nini’.

    Mfano: Kwa nini unamwogopa simba?




  • SURA YA PILI : MADA KUU 2: LUGHA NA MATUKIO YA KIJAMII NA KITAIFA

    MADA NDOGO: Sikukuu, sherehe na matukio ya kitaifa nchini Rwanda 
    SOMO LA 7: Sikukuu, sherehe na matukio ya kitaifa katika kalenda

    7.1 Kifungu kuhusu sikukuu sherehe na matukio ya kitaifa nchini Rwanda

    Katika makundi ya wanafunzi wanne wanne, tazameni kalenda hii ya mwaka wa
    2016 kisha mjadiliane kuhusu tarehe maalum za sikukuu na matukio rasmi ya

    Kitaifa:


    Katika makundi ya wanafunzi wanne wanne, tazameni picha hizi kisha msome
    kifungu cha habari kinachofuata kuhusu sikukuu, sherehe na matukio ya
    kitaifa nchini Rwanda. Baada ya kusoma kifungu, mjibu maswali ya ufahamu

    yanayofuata.



    Maswali ya ufahamu

    1. Taja sherehe ambayo husherehekewa mwanzoni mwa mwaka.
    2. Taja sherehe ambayo husherehekewa mwishoni mwa mwaka.
    3. Ni tukio gani ambalo huadhimishwa tarehe saba mwezi wa Aprili
    nchini Rwanda?
    4. Ni sherehe gani ambayo hukumbukwa tarehe moja mwezi wa Februari
    nchini Rwanda?
    5. Ni sherehe gani ambayo huadhimishwa tarehe moja mwezi wa Julai
    nchini Rwanda?
    6. Taja sherehe mbili ambazo huadhimishwa na Wakristo.
    7. Taja sherehe mbili ambazo huadhimishwa na Waislamu.
    8. Sherehe ya Umuganura huadhimishwa mwezi gani?

    9. Sherehe ya Krismasi ni sikukuu ya dini gani?

    7.2 Msamiati kuhusu sikukuu nchini Rwanda

    Kutokana na kifungu cha habari mlichosoma hapo awali, katika makundi ya
    wanafunzi watatu watatu, jadilini kuhusu maana ya msamiati mpya uliojitokeza
    unaohusiana na sherehe na sikukuu nchini Rwanda. Kamusi ya Kiswahili inaweza

    kutumika inapohitajika.

    Kwa mfano:

    serikali: mfumo au chombo chenye mamlaka ya kutawala nchi au eneo

     fulani.

    Zoezi la 7.1

    A. Katika makundi ya wanafunzi watatu watatu, chunguzeni maana
    ya msamiati uliopigiwa mistari katika sentensi hizi. Tumieni kamusi
    panapohitajika.
    1.Wanyarwanda walipigana dhidi ya wakoloni.
    2.Wananchi hawafai kutumia mabavu wanapotafuta mali.
    3.Nchi yetu ilipata ukombozi miaka mingi iliyopita.
    4.Serikali yetu ina viongozi wazuri.
    5.Utawala wa rais wetu ni wa kuigwa na viongozi wengi duniani.
    B. Katika makundi yenu, tungeni sentensi sahihi kwa kutumia maneno

    yaliyopigiwa mistari katika sentensi za zoezi la 1A.

    Zoezi la 7.2

    Katika makundi ya wanafunzi watatu watatu, jazeni nafasi zilizo wazi katika

    sentensi hizi kwa jibu sahihi kutoka katika mabano. 

    1. Sherehe za mwaka mpya ________________ mwanzoni mwa kila
    mwaka. (huathimishwa, huadhimishwa)
    2. Rwanda ni ____________________ inayopendwa na watu wengi
    ulimwenguni. (inchi, nchi)
    3. ____________ ya Krismasi hufanyika tarehe 25 mwezi wa Disemba.
    (Shehere, Sherehe)
    4. Siku ya ______________ husherehekewa tarehe 1 mwezi wa Februari.
    (washujaa, mashujaa)
    5. ______________ husherehekewa wiki ya kwanza mwezi wa Agosti.

    (Umagunura, Umuganura)

    7.3 Matumizi ya lugha: Majadiliano

    Jigaweni katika makundi ya wanafunzi watano watano kisha mjadili kuhusu
    sherehe na sikukuu nchini Rwanda. Waeleze wenzako:
    1. Shughuli zote zinazofanyika katika sherehe za mwaka mpya.
    2. Nguo unazopenda kuvaa unapoenda katika sherehe za harusi.
    3. Sikukuu unayopenda kuadhimisha katika kalenda. Toa sababu.
    4. Umuhimu wa sikukuu na sherehe mbalimbali kwa Wanyarwanda.

    5. Umuhimu wa kuwa na Kalenda rasmi nyumbani.

    7.4 Kusikiliza na kuzungumza: Maigizo

    Katika makundi ya wanafunzi wawili wawili, tungeni na muigize mchezo mfupi
    kuhusu sikukuu nchini Rwanda. Mwanafunzi mmoja amuulize mwenzake maswali

    mbele ya darasa, naye ajibu vizuri.

    Mfano wa mazungumzo:

    Kamana: Habari dada Mukamana.
    Mukamana: Salama kaka.
    Kamana: Sikukuu ya Uhuru huadhimishwa lini?
    Mukamana: Sikukuu ya Uhuru huadhimishwa tarehe mosi mwezi wa Julai
     kila mwaka.

    Kamana: Ooh! Nimekumbuka. Asante sana dada

    Zoezi la imla

    Funga kitabu chako kisha ufungue daftari lako na uandike kwa usahihi

    maneno au vifungu vya maneno ambayo mwalimu wako atakusomea.

    7.5 Sarufi: Matumizi ya wakati uliopita 

    Katika makundi ya wanafunzi watatu watatu, tazameni michoro hii ya masimulizi
    mafupi yafuatayo kisha kila mmoja awasimulie wenzake alivyosherehekea mwaka

    mpya uliopita. 

      

    Katika sherehe za mwaka mpya uliopita, niliamka mapema, nikaoga,
    nikapiga mswaki, nikavaa nguo mpya na kunywa kiamshakinywa. Baadaye
    niliondoka na kuelekea kijijini kumtembelea kaka yangu. Nilipofika huko
    kijijini, niliwaona watoto wengi wakicheza kandanda katika uwanja mdogo.
    Nilijiunga nao. Baada ya dakika chache, mwamuzi wa mchezo huo alipuliza
    kipenga cha kuashiria mwisho wa mchezo huo. Timu ya Mashujaa ilipata

    ushindi wa mabao matatu kwa moja dhidi ya timu ya Simba.

    Swali: Eleza wakati uliotumika katika masimulizi mliyosoma hapo juu pamoja

    na masimulizi yenu kwa kutoa mifano ya vitenzi vilivyotumika.

    Zoezi la 7.3

    A. Orodhesha vitenzi vyote vilivyotumika katika masimulizi mliyoyasoma
    hapo awali.

    B. Tambua nyakati zilizotumika katika vitenzi mlivyoorodhesha

    Maelezo muhimu!

    Funga kitabu chako kisha ufungue daftari lako na uandike kwa usahihi

    maneno au vifungu vya maneno ambayo mwalimu wako atakusomea.

    7.5 Sarufi: Matumizi ya wakati uliopita

    Katika makundi ya wanafunzi watatu watatu, tazameni michoro hii ya masimulizi
    mafupi yafuatayo kisha kila mmoja awasimulie wenzake alivyosherehekea mwaka

    mpya uliopita. 


    Swali: Eleza wakati uliotumika katika masimulizi mliyosoma hapo juu pamoja

    na masimulizi yenu kwa kutoa mifano ya vitenzi vilivyotumika.

    Zoezi la 7.3

    A. Orodhesha vitenzi vyote vilivyotumika katika masimulizi mliyoyasoma
    hapo awali.

    B. Tambua nyakati zilizotumika katika vitenzi mlivyoorodhesha.

    Maelezo muhimu!

    Wakati uliopita huonyesha matukio ambayo huwa tayari yameshatendeka.
    Wakati uliopita hutumia kiambishi cha wakati -li-. Kiambishi hiki hutumika
    katika nafsi zote za Kiswahili.
    Kiambishi -ka- hutumika katika sentensi iliyo na matukio yanayofuatana

    katika wakati uliopita.

    Mifano:
    1. Nilitembea pamoja na kakangu.
    2. Aliamka akavaa nguo za michezo.
    3. Mimi nilipika chakula, nikala na kulala.
    4. Dereva aliwasha gari, akaliendesha haraka na kushikwa na polisi.
    5. Sisi tulivuna mahindi wiki iliyopita.
    Katika masimulizi ya wakati uliopita, maneno kama vile: halafu, kisha na

    baadaye hutumika.

    Zoezi la 7.4

    Katika makundi ya wanafunzi watatu watatu, jazeni nafasi zilizo wazi katika

    sentensi zinazofuata kwa kutumia wakati uliopita. 

    Kwa mfano: Mama __________ (fua) nguo, __________ (pika) na
     ________ (fagia) nyumba.
    Jibu: Mama alifua nguo, akapika na kufagia nyumba.
    1. Kaka __________ (oga), __________ (piga) nguo pasi na _________
    (enda) shuleni.
    2. Mtoto __________ (kunywa) maziwa, __________ (bembelezwa) na
    __________ (lala).
    3. Mwanafunzi ____________ (enda) shuleni, ____________ (soma) na
    __________ (fanya) mtihani.
    4. Ng’ombe ____________ (kula) nyasi, ____________ (kunywa) maji
    na __________ (rudi) zizini.
    5. Mmea _____________ (pandwa), ____________ (wekewa) mbolea

    na __________ (nyunyiziwa) maji.

    Zoezi la 7.5

    Katika makundi ya wanafunzi watatu watatu, badilisheni sentensi hizi ziwe
    katika wakati uliopita.

    1. Mama anapika wali.

    2. Mimi nitaenda shule.
    3. Kwa nini unalia?
    4. Siku ya sherehe ya Krismasi imefika.

    5. Wanyarwanda wanaadhimisha siku ya Mashujaa.

    Zoezi la 7.6

    Jigaweni katika makundi ya wanafunzi watatu watatu kisha mtunge sentensi

    tano sahihi kwa kutumia wakati uliopita ukitanguliza msamiati ufuatao

    Kwa mfano: Tarehe

    Tarehe moja mwezi wa Februari tuliadhimisha sikukuu ya Mashujaa.
    1. Uhuru
    2. Ukombozi
    3. Ukoloni
    4. Utawala

    5. Siasa

    7.6 Sarufi: Matumizi ya wakati ujao

    Katika makundi ya wanafunzi wawili wawili, tazameni mchoro wa kifungu
    kifuatacho kisha kila mmoja asimulie anavyopanga kusherehekea mwaka mpya

    ujao baada ya kusoma kifungu mlichopewa kwenye ukurasa unaofuata. 



    Swali: Eleza wakati uliotumika katika masimulizi mliyosoma hapo juu pamoja

    na masimulizi yenu kwa kutoa mifano ya vitenzi vilivyotumika.

    Zoezi la 7.7

    A. Orodhesha vitenzi vyote vilivyotumika katika masimulizi mliyoyasoma
    hapo awali.

    B. Tambua nyakati zilizotumika katika vitenzi mlivyoorodhesha.

    Zoezi la 7.8

    Katika makundi ya wanafunzi wawili wawili, jazeni nafasi zilizo wazi kwa

    vitenzi vilivyo kwenye mabano katika wakati ujao.

    Katika sherehe za Pasaka za mwaka ujao, Kamana ____________ (enda)

    kanisani kwa ajili ya ibada. Baadaye, __________ (tembelea) marafiki

    zake na kusherehekea pamoja nao. Kisha jioni ________________ (rudi)

    nyumbani. Ndugu yake Yusufu ______________ (pokea) kwenye kituo

    cha basi. Halafu ____________ (enda) nyumbani pamoja.

    Zoezi la 7.9

    Katika makundi ya wanafunzi wawili wawili, tungeni aya moja sahihi yenye

    kuhusisha matukio ya wakati ujao.

    Zoezi la 7.10

    Katika makundi ya wanafunzi watatu watatu, badilisheni sentensi zinazofuata

    ziwe katika wakati ujao.

    Kwa mfano: Mwalimu anaandika ubaoni.
    Jibu: Mwalimu ataandika ubaoni.
    1. Mwanafunzi huyu anasoma kitabu cha hadithi.
    2. Mbuga hii ilifunguliwa na rais wetu.
    3. Darasa letu limesafishwa na wanafunzi hawa.
    4. Kwa nini mnanunua vitabu vingine?

    5. Wanyamapori hawa wanakula nyasi.

    Maelezo muhimu!

    Wakati ujao hutumiwa kuonyesha matukio ambayo huwa yanatarajiwa
    kutendeka. Wakati huu hutumia kiambishi -ta-. Kiambishi hiki hutumika

    katika nafsi zote za Kiswahili.

    Mifano:
    1. Nitaomba walinzi wa mbuga waniongoze na baadaye nitapiga picha.
    2. Nitavaa kanzu nzuri halafu nitaenda msikitini kusali.
    3. Mwalimu atatufundisha kesho kisha atatupa mtihani.
    4. Sherehe ya Idi ul Fitri itaadhimishwa mwezi ujao.
    5. Wanafunzi watafanya mtihani wiki ijayo.
    Katika masimulizi ya matukio ya wakati ujao, maneno kama vile: kisha,

    halafu, mwishowe na baadaye hutumika.

    SOMO LA 8: Maadhimisho mbalimbali nchini Rwanda

    8.1 Shairi kuhusu maadhimisho mbalimbali nchini Rwanda

    Jigaweni katika makundi ya wanafunzi watatu watatu kisha mtazame picha hizi

    na hapo baadaye msome na kukariri shairi lifuatalo na kulijadili:



    Maswali ya tathmini

    Katika makundi ya wanafunzi watatu watatu, jadilini na mjibu maswali haya ya
    tathmini kuhusiana na shairi mlilosoma hapo awali.

    1. Taja sherehe ambayo huadhimishwa mwanzoni mwa kila mwaka.
    2. Sikukuuu ya Mashujaa husherehekewa lini?
    3. Pasaka huadhimishwa na watu gani? Wao hukumbuka nini katika siku hii?
    4. Taja sikukuu za Waislamu kutokana na shairi ulilosoma?
    5. Sikukuu ya Uhuru nchini Rwanda husherehekewa lini?
    6. Kumbukumbu za mauaji ya kimbari dhidi ya Watutsi hufanyika lini?
    7. Shairi hili lina mishororo mingapi?
    8. Taja kibwagizo cha shairi hili.
    9. Sherehe za Krismasi huadhimishwa lini?

    10. Sikukuu ya Umuganura hufanyika lini?

    8.2 Msamiati kuhusu maadhimisho mbalimbali

    Kutokana na shairi mlilosoma hapo awali, katika makundi ya wanafunzi
    watatu watatu, jadilini maana ya msamiati mpya uliojitokeza unaohusiana na
    maadhimisho mbalimbali nchini Rwanda. Kamusi ya Kiswahili inaweza kutumika

    inapohitajika.

    Kwa mfano:

    Ukombozi: matendo au vita vya kuokoa watu kutoka kwenye hali mbaya

     yenye mateso au hali ya unyonge.

    Zoezi la 8.1

    Jigaweni katika makundi ya wanafunzi watano watano kisha mtunge sentensi
    sahihi kwa kutumia msamiati uliopigiwa mistari katika sentensi zinazofuata.
    1. Leo tunaadhimisha sikukuu ya Mashujaa.
    2. Hii ni kalenda ya mwaka wa 2017.
    3. Mwezi wa kwanza katika kalenda ya mwaka ni Januari.
    4. Wakristo husherehekea sikukuu ya Pasaka kila mwaka.
    5. Waislamu husali mara tano kwa siku.
    6. Waislamu huadhimisha sherehe ya Idi-ul-Fitr kila mwaka.
    7. Msimu wa sherehe za Krismasi umefika.
    8. Wanyarwanda huadhimisha sikukuu ya Uhuru wa Taifa kila mwaka.
    9. Leo ni tarehe kumi mwezi Disemba mwaka 2016.

    10. Sherehe ya Umuganura itaadhimishwa kesho

    8.3 Matumizi ya lugha: Majadiliano

    Jigaweni katika makundi ya wanafunzi watano watano kisha mjadiliane na
    kuelezana kuhusu:
    1. Shughuli zinazofanyika nyumbani kwenu wakati wa sherehe za mwaka
    mpya.
    2.  Namna mnavyoadhimisha sikukuu iliyo katika mwezi Julai.
    3. Shughuli zinazotekelezwa kwenu wakati wa sherehe za Umuganura.
    4. Shughuli zinazotekelezwa wakati wa kuadhimisha sikukuu ya Ukombozi
    wa Taifa.
    5. Shughuli zinazofanyika wakati wa kuadhimisha sikukuu ya Uhuru wa

    Taifa.

    8.4 Kusikiliza na kuzungumza: Zoezi la mazungumzo

    Katika makundi ya wanafunzi wawili wawili, someni mazungumzo mafupi

    yafuatayo na majibu yatolewe palipo na maswali mbele ya wanafunzi wenzenu.

    Mazungumzo kati ya Kamana na Teta:

    Kamana: Sikukuu ya Uhuru huadhimishwa tarehe gani?
    Teta: Sikukuu ya Uhuru huadhimishwa tarehe moja mwezi wa Julai kila
    mwaka.
    Kamana: Sikukuu ya sherehe za mwaka mpya huadhimishwa tarehe gani?
    Teta: Sherehe za mwaka mpya huadhimishwa tarehe moja mwezi wa
    Januari kila mwaka.

    Endelezeni mazungumzo haya kwa maneno yenu wenyewe. 

    8.5 Sarufi: Vitenzi vya silabi moja

    Jigaweni katika makundi ya wanafunzi wawili wawili kisha mbainishe vitenzi

    vilivyo katika sentensi hizi zenye michoro.




    Zoezi la 8.2

    Katika makundi ya wanafunzi wawili wawili, tungeni sentensi tano sahihi kwa
    kutumia vitenzi vifuatavyo.
    Kwa mfano: kuja
    Jibu: Mwalimu alikuja kututembelea nyumbani kwetu.
    1. kufa
    2. kunywa
    3. kula
    4. kuwa

    5. kuja

    Maelezo muhimu!

    Katika lugha ya Kiswahili kuna vitenzi vyenye silabi moja. Vitenzi hivi
    huambatanishwa na ‘ku-’ katika matumizi.

    Kwa mfano:

    kufa:              –f 
    kuwa:            -w
    kunywa:      -nyw
    kula:              -l
    kuja:              -j

    Matumizi katika sentensi

    1. Mtoto alikunywa dawa.
    2. Ng’ombe alikula nyasi.

    3. Nyanya alikuja dukani.

    Zoezi la 8.3

    A. Katika makundi ya wanafunzi wawili wawili, rekebisheni sentensi hizi:
    1. Mwalimu alija darasani.
    2. Mbuzi wetu alifa jana.
    3. Kalisa alinywa maji.
    4. Dada alila wali.
    5. Mama aliwa mgonjwa.

    B. Kanusha sentensi mlizosahihisha katika A hapo juu.

    8.5.1 Vitenzi vya silabi moja, tungo yakinishi na kanushi

    Katika makundi ya wanafunzi wawili wawili, chunguzeni sentensi hizi kisha
    mjadili ugunduzi wenu.

    1. Mtoto alikunywa dawa.                           - Mtoto hakunywa dawa.
    2. Paka wao alikufa jana.                             - Paka wao hakufa jana.

    3. Mgeni alikuja haraka.                               - Mgeni hakuja haraka.

    Maelezo muhimu!

    Vitenzi vya silabi moja huambatanishwa na ‘ku-’ katika hali yakinishi.
    Katika hali kanushi, vitenzi hivi huambatanishwa na kikanushi ‘ha-’ na

    nafsi husika. 

    Kwa mfano:
    1. Wagonjwa walikula chakula. - Wagonjwa hawakula chakula.
    2. Walimu walikunywa chai. - Walimu hawakunywa chai.

    3. Paka wa jirani walikufa jana. - Paka wa jirani hawakufa jana.

    Zoezi la makundi

    Katika makundi ya wanafunzi wawili wawili, chunguzeni mifano ya sentensi

    katika jedwali hili.


    Zoezi la 8.4

    Katika makundi ya wanafunzi watatu watatu, tumieni vitenzi vyenye silabi
    moja vifuatavyo katika wakati uliopita hali yakinishi katika umoja na wingi.

    Tumieni nafsi zote za Kiswahili.

    Mfano: kunywa: -nyw

    Jibu: Mtoto alikunywa maziwa. - Watoto wali kunywa  maziwa.

    1. kuwa

    2. kuja
    3. kufa

    4. kula

    Zoezi la 8.5

    Katika makundi ya wanafunzi watatu watatu, tumieni vitenzi vyenye silabi
    moja vifuatavyo katika wakati uliopita hali kanushi. Tumieni nafsi zote za
    Kiswahili.

    Mfano: kunywa: -nyw
    Jibu: Mtoto hakunywa maziwa yote.

    1. kuwa
    2. kuja
    3. kufa

    4. kula

    Zoezi la 8.6

    Katika makundi ya wanafunzi watatu watatu, andikeni sentensi zifuatazo
    katika umoja au wingi.
    Kwa mfano:
    Umoja: Mwalimu alikuwa darasani.
    Wingi: Walimu walikuwa madarasani.
    1. Mtu huyu alikuja jana jioni.
    2. Wanafunzi hawa wanakunywa maziwa.
    3. Mtoto anakula mkate.
    4. Panya alikufa mtegoni.

    5. Viongozi walikuwa mjini Kigali.

    SOMO LA 9: Matumizi ya kalenda ya mwaka

    9.1 Mazungumzo kuhusu matumizi ya kalenda ya mwaka

    Katika makundi ya wanafunzi wawili wawili, tazameni kalenda hii ya mwaka wa
    2017 kisha msome mazungumzo yaliyo hapo chini na hatimaye mjibu maswali

    yanayofuata.

      


    Maswali ya ufahamu

    1. Mwezi wa Januari una Jumapili ngapi?
    2. Tarehe 5 mwezi wa Mei ni siku gani?
    3. Mwaka wa 2017 una siku ngapi?
    4. Mwezi wa Septemba una Jumatano ngapi?
    5. Sikukuu ya Mashujaa wa Taifa iliadhimishwa siku gani katika kalenda
    iliyo hapo juu?
    6. Krismasi itaadhimishwa siku gani katika kalenda iliyo hapo juu?
    7. Sikukuu ya mwaka mpya 2017 iliadhimishwa siku na tarehe gani?
    8. Mwezi wa Agosti una siku ngapi?
    9. Mwezi wa Disemba una Alhamisi ngapi?
    10. Ni miezi mingapi isiyokuwa na sikukuu katika kalenda iliyo hapo juu?

    Itaje.

    9.2 Msamiati kuhusu kalenda ya mwaka

    Zoezi la 9.1

    (i) Kutokana na mazungumzo kuhusu matumizi ya kalenda ya mwaka
    mliyoyasoma hapo awali, katika makundi ya wanafunzi watatu watatu,
    jadilini kuhusu maana ya msamiati uliopigiwa mistari katika sentensi
    zinazofuata. Kamusi ya Kiswahili inaweza kutumika inapohitajika.

    1. Jumamosi ni siku inayotangulia Jumapili.
    2. Huu ni mwezi wa Ramadhani.
    3. Siku hii imekuwa ya mikutano mingi.
    4. Mwezi wa kwanza katika kalenda ya mwaka ni Januari.
    5. Mwaka ujao tutazuru nchi ya Kenya.
    6. Sherehe za Krismasi hufanyika mwezi wa Disemba.
    7. Tarehe mbili mwezi ujao tutasafiri kuelekea kijijini kwetu.
    8. Tutafungua shule mwezi Mei.
    (ii) Katika makundi ya wanafunzi watatu watatu, tungeni sentensi sahihi kwa

    kutumia msamiati uliopigiwa mistari katika Zoezi la 1 (i) hapo juu.

    9.3 Matumizi ya lugha: Majadiliano

    Jigaweni katika makundi ya wanafunzi watatu watatu kisha mtazame mchoro

    ufuatao wa kalenda ya mwaka wa 2017 na kuijadili. 


    Katika makundi yenu, jadilini kuhusu namna ya kuisoma kalenda hiyo ya mwaka
    wa 2017 na kuielewa kimatumizi. Waelezee wenzako:
    1. Miezi yote iliyo na siku thelathini.
    2. Miezi yote iliyo na siku thelathini na moja.
    3. Mwezi ulio na siku chache kuliko miezi mingine.
    4. Miezi iliyo na Jumapili nyingi kuliko mingine.
    5. Miezi iliyo na sikukuu au matukio rasmi ya kitaifa ya kusherehekewa.
    6. Mwezi wa Disemba una Jumapili ngapi?
    7. Tarehe ya kwanza katika mwezi wa Septemba ni siku gani?

    8. Tarehe kumi mwezi wa Agosti ni siku gani?

    Maelezo muhimu!

    Kalenda ni kifaa kinachoonyesha siku, tarehe na miezi katika mwaka.
    • Mwaka una miezi kumi na miwili ambayo ni: Januari, Februari,
    Machi, Aprili, Mei, Juni, Julai, Agosti, Septemba, Oktoba,
    Novemba na Disemba.
    • Siku katika kila mwezi huanzia Jumapili hadi Jumamosi.
    • Mwaka mmoja una wiki hamsini na mbili.
    • Wiki moja ina siku saba ambazo ni: Jumapili, Jumatatu, Jumanne,
    Jumatano, Alhamisi, Ijumaa na Jumamosi.
    • Katika kalenda, siku za Jumapili huandikwa kwa kutumia wino wa
    rangi tofauti.
    • Siku za matukio makuu ya sherehe za kitaifa na kijamii huandikwa

    kwa kutumia wino wa rangi tofauti.

    9.4 Kusikiliza na kuzungumza: Maigizo

    Jigaweni katika makundi ya wanafunzi wawili wawili kisha mwigize mazungumzo
    mliyoyasoma hapo awali kati ya Birasa na Kalisa kuhusu matumizi ya kalenda ya

    mwaka.

    9.5 Sarufi

    Matumizi ya herufi kubwa na alama za uandishi

    Katika makundi ya wanafunzi wawili wawili, someni kifungu kifuatacho kisha
    mbainishe maneno yote yaliyotumia herufi kubwa pamoja na alama mbalimbali

    za uandishi na hapo baadaye mjibu maswali ya tathmini yanayofuata. 


    Maswali ya tathmini
    1. Eleza matumizi mbalimbali ya herufi kubwa kutokana na kifungu kifupi
    mlichosoma hapo awali kumhusu Biruta.
    Kwa mfano: Biruta anaishi Gikondo.
    Matumizi: Herufi kubwa imetumika mwanzoni mwa jina la mtu
     (Biruta) na jina la mahali (Gikondo).
    2. Eleza matumizi mbalimbali ya alama nyingine za uandishi kutokana na
    kifungu mlichosoma hapo juu kisha mwonyeshe matumizi katika sentensi.
    Kwa mfano: Nukta (.)
    Matumizi: Nukta imetumika mwishoni mwa sentensi kamili.
    Mfano wa sentensi: Biruta ni mwalimu mkuu katika shule ya

     sekondari ya Kamashashi iliyo mjini Kigali.

    Zoezi la 9.2

    Katika makundi ya wanafunzi watatu watatu, rekebisheni sentensi zifuatazo
    kwa kutumia alama za uandishi kwa usahihi.
    Kwa mfano: neza ataenda shule jumatatu
    Jibu: Neza ataenda shule Jumatatu.
    1. kwa nini ulichelewa shuleni
    2. lo umebeba mzigo huo pekee yako
    3. mama alienda sokoni kununua ndizi machungwa viazi na nanasi
    4. paka amekunywa maziwa

    5. ngabo atakuja lini

    Zoezi la 9.3

    Katika makundi ya wanafunzi watatu watatu, rekebisheni kifungu hiki kwa
    kutumia alama za uandishi pamoja na herufi kubwa kwa usahihi.

    siku moja nilienda sokoni kununua ndizi sukari samaki mboga na
    machungwa. njiani nilikutana na rafiki yangu birasa. alishangaa kuniona
    na kusema ah kumbe wewe pia huja sokoni nikamjibu kuwa mimi hupenda
    kumsaidia mama kununua bidhaa mbalimbali. nilimuuliza umekuja

    kununua nini. akanijibu kuwa alikuja kununua mboga na samaki

    Tathmini ya mada ya 2

    Zoezi la 1

    Jigaweni katika makundi ya wanafunzi watano watano kisha mjadili maswali
    yafuatayo. Waelezee wenzako kuhusu:
    1. Shughuli zinazofanyika wakati wa sikukuu ya Pasaka kwa Wakristo.
    2. Shughuli zinazofanyika wakati wa sikukuu ya Idi ul Fitri kwa Waislamu.
    3. Shughuli na burudani zinazofanyika katika sherehe ya harusi.
    4. Sherehe ya Kiislamu ya Idi ul Adha huadhimishwa lini? Jadili shughuli
    zinazofanyika wakati wa sherehe hiyo.
    5. Sherehe ya Kikristo ya Krismasi huadhimishwa lini? Jadili shughuli

    zinazofanyika wakati wa sherehe hiyo.

    Zoezi la 2

    Katika makundi ya wanafunzi wawili wawili, rekebisheni sentensi zifuatazo
    kwa kutumia alama za uandishi kwa usahihi
    kwa kutumia alama za uandishi kwa usahihi
    Kwa mfano: pasaka iliadhimishwa tarehe gani
    Jibu: Pasaka iliadhimishwa tarehe gani?
    1. baadhi ya sherehe katika kalenda yetu ni pasaka krismasi na umuganura
    2. siku ya kwanza ya wiki ni jumapili katika kalenda ya mwaka
    3. kamana anaishi wapi
    4. lo simu yangu imeanguka majini

    5. kilo moja ya chumvi huuzwa faranga mia mbili 200

    Zoezi la 3

    Katika makundi ya wanafunzi wawili wawili, andikeni sentensi zifuatazo
    katika wakati ujao.
    Kwa mfano: Baba alinunua maji, soda na mkate.
    Jibu: Baba atanunua maji, soda na mkate.
    1. Mwalimu alitufundisha Hisabati.
    2. Ng’ombe alikunywa maji mengi.
    3. Babu alitusimulia hadithi nzuri.
    4. Sikukuu ya Krismasi iliadhimishwa kwa sherehe kubwa.

    5. Manzi alinunua vitabu na kalamu.

    Zoezi la 4

    Katika makundi ya wanafunzi watatu watatu, tungeni sentensi kwa kutumia
    vitenzi vya silabi moja vifuatavyo katika wakati uliopita hali kanushi.
    Kwa mfano: kuja
    Jibu: Mwalimu hakuja shuleni jana.
    1. kunywa
    2. kula
    3. kuwa
    4. kuja

    5. kufa

    Zoezi la 5

    Katika makundi ya wanafunzi watatu watatu, tajeni majina ya alama za

    uandishi zifuatazo kisha mtunge sentensi moja kwa kila alama. 

    Kwa mfano: .
    Jibu: Nukta
    Sentensi: Tutaadhimisha sikukuu ya Ukombozi mwezi Julai.
    1. ?
    2. !
    3. ,
    4. :
    5. egg

    6.

    Zoezi la 6

    Katika makundi ya wanafunzi watano watano, wasimulie wenzako kuhusu

    sikukuu yoyote mliyoadhimisha kwa kuzingatia wakati uliopita.

    Zoezi la 7

    Katika makundi ya wanafunzi watatu watatu, tungeni sentensi sahihi kwa
    kutumia vitenzi vifuatavyo katika hali yakinishi na hali kanushi kwa kuzingatia

    wakati ujao. 

    Kwa mfano:                                                     andika
    Jibu:                                                                    (Yakinishi): Mwanafunzi ataandika ubaoni.
                                                                                    (Kanushi): Mwanafunzi hataandika ubaoni.
    1. sherehekea
    2. kula
    3. adhimisha
    4. kunywa

    5. soma

    Zoezi la 8

    Katika makundi ya wanafunzi watatu watatu, rekebisheni kifungu hiki kwa
    kutumia alama za uandishi pamoja na herufi kubwa kwa usahihi.

    sikukuu ya mwaka mpya huadhimishwa tarehe moja januari siku ya
    mashujaa huadhimishwa tarehe moja mwezi februari je wewe uliadhimisha
    sikukuu ya mwaka mpya kwa njia gani waislamu wana sherehe mbili kuu
    ambazo ni idi ul fitri pamoja na idi ul adha Wakristo vilevile wana sherehe
    mbili kuu ambazo ni krismasi pamoja na pasaka je wewe husherehekea

    sikukuu gani ya kidini.

    Zoezi la 9

    Katika makundi ya wanafunzi watatu watatu,
     rekebisheni sentensi hizi kwa kutumia alama

     za uandishi pamoja na herufi kubwa kwa usahihi.

    1. rais aliongoza sherehe ya siku ya uhuru katika uwanja wa gikondo
    2. je wewe ulihudhuria sherehe ya umuganura mwaka jana

    3. lo sikujua unaweza kuimba vizuri hivyo kwenye sherehe hiyo

  • SURA YA TATU: MADA KUU 3: UKUZAJI WA MATUMIZI YA LUGHA KIMAZUNGUMZO

    Mada Ndogo: Midahalo na mijadala kuhusu shughuli
    za maendeleo na uzalishajimali dhidi ya
    umaskini nchini 
    SOMO LA 10: Mdahalo
    10.1 Mdahalo kuhusu ‘Elimu ni muhimu kwa maendeleo ya
     wananchi kuliko biashara’
    Katika makundi ya wanafunzi watatu watatu, chunguzeni mchoro ufuatao kisha
    mjadili kuhusu kinachoendelea katika mchoro wenyewe. Baada ya kujadiliana,
    someni kifungu cha mdahalo kinachofuata kisha mjibu maswali yanayofuata.


     

    Maswali ya ufahamu
    1. Mada ya mdahalo iliyokuwa ikizungumziwa ilikuwa ipi?
    2. Eleza tofauti kati ya watetezi na wapinzani.
    3. Bigirimana alitoa hoja zipi?
    4. Mukamwiza alitoa hoja zipi?
    5. Mukandayisenga alitoa hoja gani?
    6. Eleza hoja ambazo Msikilizaji mshiriki 1 alitoa.
    7. Msikilizaji mshiriki 2 alitoa hoja zipi?
    8. Taja jina jingine la ‘mdahalo’.
    9. Mwenyekiti hufanya kazi gani katika shughuli za mdahalo?
    10.2 Msamiati kuhusu mdahalo
    Katika makundi ya wanafunzi watatu watatu, tafuteni msamiati mpya kutoka
    katika kifungu cha mazungumzo yaliyotangulia na kuueleza. Zingatieni
    matumizi ya msamiati huo katika kifungu hicho na mtumie kamusi pale
    inapohitajika. 
    Zoezi la 10.1
    Katika makundi ya wanafunzi watatu watatu, elezeni maana ya msamiati
    uliopigiwa mistari katika sentensi zifuatazo kisha mtunge sentensi sahihi kwa
    kutumia msamiati huo.
    1. Alitupatia fursa ya kueleza shughuli za maendeleo ya kijiji chetu.
    2. Mukeshimana alitoa hoja nzuri katika mazungumzo yetu.
    3. Sisi tulitetea mawazo yake kwa sababu alisema ukweli.
    4. Mimi ninapinga mawazo ya watu wanaotaka kuendelea kuishi kwa
    kutegemea misaada tu.
    5. Nyirahabineza alichaguliwa kuwa mwenyekiti wa Chama cha
    Wanafunzi wa Kiswahili nchini Rwanda (CHAWAKIRWA).
    6. Wageni hawa walikuja kuwekeza nchini mwetu na wanaendelea
    kupata faida nyingi.
    7. Mafunzo ya rafiki yangu yalichukua gharama kubwa.
    8. Matokeo ya mtihani wetu ni mazuri kwa sababu tumefaulu.
    9. Tujiepushe na ulevi kwa sababu ni kikwazo kwa maisha mazuri ya
    watu.
    10. Tulianzisha biashara ya kufuga kondoo na pato letu linaongezeka kila
    mwaka.
    Zoezi la 10.2
    Katika makundi ya wanafunzi watatu watatu, kamilisheni sentensi zifuatazo
    kwa kutumia maneno yafuatayo: walipiga makofi, maarifa, mshiriki,
    kutambua, itatunufaisha, anafananisha.
    Kwa mfano: Baada ya ____________ kuwa Bwiza hakufaulu katika
     somo la Kiswahili niliamua kumsaidia.
    Jibu: Baada ya kutambua kuwa Bwiza hakufaulu katika somo la
     Kiswahili niliamua kumsaidia.
    1. Watu hawa wana ___________ mbalimbali ya kutekeleza miradi.
    2. Washiriki wote wa mkutano ____________ baada ya kusikia hoja
    nzuri za Kayisabe na wenzake.
    3. Mwenyekiti wa mkutano wetu anasema kuwa kila _____________
    anapaswa kutoa hoja zake.
    4. Mtu huyu _______________ elimu na utajiri.
    5. Kazi hii ___________ wote kwa kutuwezesha kupata pesa za kujisaidia.
    Zoezi la 10.3
    Katika makundi ya wanafunzi wawili wawili, husisheni maneno yaliyoandikwa
    katika sehemu A na maelezo yake katika sehemu B.
    Kwa mfano: 1           C
     Sehemu A                                   Sehemu B
    1. mwenyekiti                                       A. mazungumzo kati ya watu wenye mitazamo
                                                                            tofauti
    2. mdahalo                                            B. jambo muhimu
    3. msingi                                                 CH. mtu aliyechaguliwa kuongoza mdahalo
    4. wanatatua                                        D. ufupisho
    5. muhtasari                                         E. wanaondoa tatizo
    10.3 Matumizi ya lugha: Majadiliano
    Katika makundi ya wanafunzi watatu watatu, jadilini maswali yafuatayo na
    mwelezane kuhusu:
    1. Mdahalo ni nini?
    2. Toa mifano ya mada mbili zinazoweza kuzungumziwa katika mdahalo.
    3. Ni watu gani ambao hushirikishwa katika mdahalo?
    4. Watu hao huwa na mawazo au misimamo tofauti. Eleza misimamo hiyo.
    5. Taja tabia za kujiepusha katika mdahalo.
    Zoezi la 10.4
    Katika makundi ya wanafunzi wawili wawili, jazeni herufi zilizoachwa ili
    kuunda neno kamili.
    Kwa mfano:

    Maelezo muhimu!
    Mazungumzo au majadiliano kati ya watu wengi ambao
    huzungumzia jambo moja maalumu na huwa na mitazamo tofauti
    huitwa mdahalo.
    • Mtazamo wa kwanza hutoa hoja zinazotetea au kuunga mkono
    wazo kuu.
    • Mtazamo wa pili hutoa hoja za kupinga au kukataa wazo kuu.
    Washiriki wa mdahalo ni:
    1. Mwenyekiti:
     Huongoza mazungumzo au majadiliano.
    Hupanga muda utakaotumiwa na kila msemaji kutoa hoja.
     Huchagua wasemaji katika mdahalo.
     Hupigisha kura baada ya mazungumzo ili kutaka kujua upande
    ulioshinda kati ya upande wa watetezi na ule wa wapinzani.
    2. Katibu:
    Huandika na kusoma hoja za wasemaji wote.
     Hutangaza matokeo ya kura zilizopigwa baada ya mazungumzo.
    3. Watetezi:
     Hawa ni wasemaji wanaotetea mada au wazo kuu linalozungumziwa.
    4. Wapinzani:
    Hawa ni wasemaji wanaopinga mawazo yanayotetea wazo kuu la
    mada.
    5. Wasikilizaji washiriki:
     Hawa wanashiriki kwa kusikiliza hoja za pande mbili: upande wa
    utetezi na upande wa upinzani.
    Baadhi ya tabia za kuepuka katika mdahalo ni: matumizi ya lugha
    yenye matusi na uchochezi, kutohifadhi wakati uliotengewa, kupandwa na
    hasira upande wako unaposhindwa, n.k.
    10.4 Kusikiliza na kuzungumza: Kuandaa mdahalo
    Katika makundi ya wanafunzi wanane wanane chagueni moja kati ya mada
    zifuatazo kisha mwandae mdahalo wenu.
    1. Elimu ndio msingi wa maisha mazuri.
    2. Wazazi wana nafasi kubwa katika malezi ya watoto wao kuliko walimu.
    3. Ni lazima viongozi wa kidini washirikiane na wanasiasa katika mipango
    ya maendeleo ya wananchi.
    4. Vitabu ndivyo vifaa muhimu katika elimu. 
    Katika maandalizi yenu, zingatieni mambo yafuatayo:
    • Jadilini maana ya msamiati uliotumiwa katika mada mlizopewa ili muweze
    kuelewa mada hizo.
    • Hakikisheni kuwa mnaelewa jambo muhimu linalozungumziwa katika
    kila mada.
    • Hakikisheni kuwa mmechagua mwenyekiti, katibu, wasikilizaji washiriki,
    watetezi na wapinzani.
    • Kila mzungumzaji aandae na kupanga hoja zake vizuri.
    • Kila mzungumzaji anapaswa kuwa na nidhamu kwa kuheshimu maelekezo
    ya mwenyekiti.

    10.5 Sarufi: Wakati uliotimilika, tungo yakinishi
    Katika makundi ya wanafunzi watatu watatu, chunguzeni sentensi zinazofuata
    katika umoja na wingi kisha mwelezane ugunduzi wenu na baadaye mjibu zoezi
    linalofuata.

    Je, mmegundua nini?

    Zoezi la 10.5

    Katika makundi ya wanafunzi watatu watatu, tungeni sentensi moja moja kwa
    kutumia kitenzi zungumza kwa kutumia kiambishi ‘me’ kama kilivyotumiwa
    katika tungo zenye kitenzi toa zilizo hapo juu. Tumia nafsi: mimi, wewe, yeye,

    sisi, nyinyi na wao.

    Kwa mfano:

    Mimi nimezungumza na mwalimu wangu.

    Sisi tumezungumza na walimu wetu.

    Maelezo muhimu!

    Kiambishi ‘me’ kinarudiwarudiwa katika vitenzi vyote baada
    ya viambishi nafsi ni, u, a, tu, m na wa. Kiambishi ‘me’ ni
    kiambishi cha wakati uliotimilika, tungo yakinishi.
    • Wakati uliotimilika huonyesha kuwa tendo tayari limefanyika na
    kumalizika.
    Kwa mfano:
    • Mimi nimefanya zoezi langu. (zoezi tayari limeshafanywa)
    • Kageruka ameondoka leo. (tendo la kuondoka tayari

    limeshamalizika)

    Matumizi ya wakati uliotimilika katika sentensi

    Katika makundi ya wanafunzi watatu watatu, chunguzeni sentensi zifuatazo kwa

    kuziambatisha pamoja na michoro iliyopo. Elezaneni mlichogundua. 




    Zoezi la 10.6

    Katika makundi ya wanafunzi wawili wawili, jazeni nafasi zilizoachwa wazi
    kwa kutumia kitenzi kinachofaa katika wakati uliotimilika, tungo yakinishi.
    Kwa mfano: Mwalimu ______ (kueleza) vizuri mambo yote muhimu.
    Jibu:                              Mwalimu ameeleza vizuri mambo yote muhimu.
    1. Sisi na viongozi wetu _________(kujadiliana) kuhusu umuhimu wa
    Kiswahili.
    2. Wewe ________ (kutazama) mchezo wa kandanda kwenye runinga.
    3. Mama yangu ________ (kuagiza) bidhaa nyingi kutoka Uchina.
    4. Mtetezi huyu na wasikilizaji washiriki wote_________(kuzungumzia)
    mambo muhimu.
    5. Mlango wa nyumba hii ________ (kufunguliwa) ili wageni wote
    waingie.
    6. Kisu changu _________ (kupotea).
    7. Nyumba zile _______ (kupakwa) rangi na mafundi wawili.
    8. Vitabu vingi vya Kiswahili ________ (kuchapishwa).
    9. Midahalo miwili _________ (kushirikisha) wasemaji wenye hoja nzuri.
    10. Mimi _________ (kuimba) wimbo wa kumsifu Mungu katika ibada
    yetu. 
    10.5.1 Wakati uliotimilika, tungo kanushi
    Katika makundi ya wanafunzi wawili wawili, chunguzeni sentensi zinazofuata
    katika umoja na wingi kisha mtunge sentensi zinazofanana nazo katika nafsi

    zote.

    

    Zoezi la 10.7

    a) Katika makundi ya wanafunzi wawili wawili, tungeni sentensi moja
    moja kwa kutumia kitenzi imba katika wakati uliotimilika, hali
    yakinishi. Tumia nafsi: mimi, wewe, yeye, sisi, nyinyi na wao.

    b) Andikeni sentensi zenu katika hali kanushi. 

    Maelezo muhimu!
    • Kiambishi ‘me’ kimetumika kuonyesha wakati uliotimilika
    katika tungo yakinishi.
    • Katika wakati uliotimilika, kiambishi ‘ja’ kinatumiwa katika

    tungo kanushi badala ya kiambishi ‘me’ cha tungo yakinishi. 

    Zoezi la 10.8

    Katika makundi ya wanafunzi wawili wawili, andikeni sentensi hizi katika
    tungo kanushi.
    Kwa mfano: Wewe umeimba wimbo mzuri sana.
    Jibu:                                      Wewe hujaimba wimbo mzuri sana.
    1. Yeye ameagiza bidhaa nyingi kutoka Kigali.
    2. Mimi nimezunguka mjini kwa gari.
    3. Mtoto wangu amefaulu mitihani yake.
    4. Nyumba yangu imesafishwa.

    5. Mgomba umechomwa.

    Zoezi la 10.9

    Baada ya kukanusha tungo katika zoezi la 10.8, ziandike katika wingi.
    Kwa mfano: Wewe hujaimba wimbo mzuri sana. (umoja, tungo kanushi)
    Jibu:              Nyinyi hamjaimba nyimbo nzuri sana. (wingi, tungo kanushi)
     

    SOMO LA 11: Mjadala

    11.1 Mjadala kuhusu ‘Nafasi ya ukulima katika

     uzalishajimali dhidi ya umaskini’

    Katika makundi ya wanafunzi watatu watatu, jadilini kuhusu kinachoendelea
    katika michoro ifuatayo kisha msome kifungu cha mjadala kinachofuata kuhusu
    nafasi ya kilimo katika shughuli za uzalishajimali dhidi ya umaskini na hapo
    baadaye mjibu maswali yanayofuata. 
     
                    

      


    Maswali ya ufahamu

    1. Mada ya mjadala ilikuwa ipi?
    2. Eleza tofauti kati ya ukulima na ufugaji.
    3. Tatizo linaloathiri kilimo kulingana na Kawera ni lipi?
    4. Serikali inashauriwa kufanya nini ili kusuluhisha matatizo ya kilimo?
    5. Bagirishya alitoa hoja gani?
    6. Mukandayisenga alitoa hoja gani?

    7. Eleza hitimisho ambalo Mwenyekiti alitoa.

    11.2 Msamiati kuhusu ukulima
    Jipangeni katika makundi ya wanafunzi watatu watatu, kisha mtafute maana ya
    msamiati mpya katika kifungu cha mjadala kilichotangulia. Tafuteni maana ya
    msamiati huo kulingana na matumizi yake katika kifungu hicho. Tumieni kamusi

    pale inapohitajika. 

    Zoezi la 11.1

    Katika makundi ya wanafunzi watatu watatu, chunguzeni sentensi zifuatazo
    kisha mtunge sentensi zenu kwa kutumia maneno yaliyopigiwa mistari.

    1. Taasisi ya kilimo imewaletea wakulima mbegu nzuri za mahindi.
    2. Nyanya na vitunguu vinanunuliwa kwa bei nafuu mjini Kigali.
    3. Ni lazima kila mkulima aache uvivu na kufanya kazi kwa bidii.
    4. Mtaalamu mmoja wa kilimo ameonyesha namna nzuri ya kupanda
    migomba.
    5. Mkulima huyu ana bidii sana katika shughuli zake.
    6. Watu hawa wanatimiza wajibu wao wa kufundisha wakulima.
    7. Wadau wote wa kilimo wamekutania mjini Kigali.
    8. Serikali ya Rwanda inatenga faranga nyingi za kuendesha sekta za

    kilimo na ufugaji.

    Zoezi la 11.2


    11.3 Matumizi ya lugha: Zoezi la jedwali

    Katika makundi ya wanafunzi watatu watatu, jazeni nafasi hizi kwa kuzingatia

    majibu ya maelezo yaliyo hapo chini:


    Kwenda kulia
    1 Mazungumzo kati ya watu wenye mitazamo tofauti kuhusu mada maalumu
    6 Uchaguzi wa kupata mshindi
    8 Maombi yanayoelekezwa kwa Mungu
    9 Neno lionyeshalo kuwa hakuna kingine
    10 Maelezo ya kupinga au kuunga mkono
    11 Kitu kilichotengenezwa kwa ajili ya kukalia
    12 Kinachotokana na mmea
    14 Anakataa kuunga mkono

    16 Mazungumzo ya kujenga hoja yanayofanywa kwa ajili ya kufafanua jambo

    Kwenda chini
    2 Jambo linalozungumzwa au kujadiliwa
    3 Anaunga mkono
    4 Chombo cha mawasiliano
    5 Mtu anayeandika mawazo ya wasemaji na washiriki wengine katika
    mdahalo
    7 Kuwa kwa wingi
    13 Kitu anachopata mtu baada ya kazi

    15 Isipokuwa

    Maelezo muhimu!

    Mjadala ni mazungumzo kuhusu jambo maalum.
    • Watu wanaoshiriki katika mazungumzo haya hutoa hoja zao
    kuhusu jambo hilo.
    • Jambo ambalo linazungumziwa huhitaji kufafanuliwa na kutolewa
    maelezo.
    • Katika mjadala kila mtu aliye na hoja huonyesha kuwa anataka
    kusema na hupewa muda wake ili atoe hoja zake.
    • Msemaji anaweza kutetea au kupinga mawazo ya wengine.
    • Katika mjadala kuna kiongozi anayeongoza mazungumzo.
    • Kiongozi huchagua anayezungumza na kuongoza mazungumzo na
    kuhifadhi nidhamu.
    • Washiriki nao hutoa hoja zao kuhusu mada iliyotolewa mpaka
    wafikie uamuzi wao wa mwisho.

    • Hakuna kura zinazopigwa kama ilivyo katika mdahalo.

    11.4 Kusikiliza na kuzungumza: Kuandaa mjadala
    Katika makundi ya wanafunzi watano watano, chagueni moja kati ya mada
    zifuatazo na kuandaa mdahalo wenu.
    1. Umuhimu wa biashara katika uzalishajimali nchini Rwanda.
    2. Umuhimu wa uongozi bora katika uzalishajimali dhidi ya umaskini.
    3. Vikwazo vya kufanikisha kazi miongoni mwa vijana.
    4. Nafasi ya shule za ufundi katika maendeleo na uzalishajimali nchini
    Rwanda.

    11.5 Sarufi: Kauli asili na kauli taarifa

    Katika makundi ya wanafunzi wawili wawili, chunguzeni sentensi zifuatazo kisha

    mjibu maswali yaliyo hapo chini. 



        Je, mmegundua nini?

    Zoezi la makundi

    1. Linganisheni sentensi katika sehemu A na sentensi katika sehemu B kwa
    kuonyesha sifa zake.
    2. Tungeni sentensi mbili zenye sifa kama za sentensi za sehemu A na

    kuziandika kwa kuzingatia sifa za sentensi katika sehemu B. 

    Maelezo muhimu!

    Sentensi katika kundi A zinarudia maneno yaliyotamkwa na mtu bila
    kubadilisha chochote katika kauli yake.
    • Kauli hiyo imeandikwa kwa kutumia alama za usemi (“ ” ) na kuanza
    kwa herufi kubwa.
    Kwa mfano: Mwalimu alisema, “Mimi nitafundisha somo la Kiswahili.”
    • Sentensi katika kundi B zinalenga kutuambia maneno ambayo
    yalizungumzwa na mtu mwingine bila kuyarudia kama yalivyokuwa
    katika kauli yake ya kwanza.
    Kwa mfano: Mwalimu alisema kwamba yeye atafundisha somo la
     Kiswahili.
    • Sentensi katika kundi A zinaonyesha kauli ya mtu katika hali yake ya
    kwanza na kauli hiyo inaitwa kauli asili.
    • Sentensi katika kundi B zinatoa taarifa au habari ya kauli au maneno
    yaliyosemwa na mtu mwingine bila kuongeza wala kupunguza maana
    ya jambo aliloeleza. Kauli hiyo inaitwa kauli taarifa.
    • Katika kauli ya taarifa mambo haya huzingatiwa:
    Nafsi hubadilika
    Mimi hubadilika na kuwa yeye

    Sisi hubadilika na kuwa wao

    Zoezi la 11.3

    Katika makundi ya wanafunzi wawili wawili, badilisheni sentensi hizi za kauli
    asili ziwe katika kauli taarifa.
    Kwa mfano: Mkulima mmoja anasema, “Mimi nitapata mavuno mengi
     sana.”
    Jibu:                           Mkulima mmoja anasema kwamba yeye atapata mavuno
     mengi sana.
    1. Wazungumzaji hawa wanasema, “Sisi tunapenda kutoa maoni yetu.”
    2. “Kabera atajijengea nyumba nzuri.” Mwanafunzi mmoja anasema.
    3. “Mimi nitaingia darasani saa nane kamili.” Ndayisaba anasema.
    4. Wakulima wanasema, “Mvua itanyesha na mimea yetu itastawi.”
    5. Baba yangu anasema, “Ni lazima watoto wote wasome kwa bidii.”
    6. “Sisi tutasaidia wakulima wetu kupata mbegu nzuri.” Mkuu wa wilaya
     anasema.
    7. “Mimi ninahitaji dereva mwenye ujuzi.”Mkuu wa kiwanda hiki anasema.
    8. Mama yangu anasema, “Kisu changu kimepotea.”
    9. “Kitanda changu ni kizuri.” Mgeni mmoja anasema.
    10. “Mimi sikubaliani na mawazo ya mtetezi wa pili.” Mpinzani huyu

     anasema.

    Zoezi la 11.4

    Katika makundi ya wanafunzi wawili wawili, badilisheni sentensi hizi kutoka
    kauli taarifa na kuziweka katika kauli asili.
    Kwa mfano: Mama alisema kuwa alitaka kwenda sokoni.
    Jibu: “Ninataka kwenda sokoni.” Mama alisema.
    1. Baba aliniambia kuwa nikifika Kigali ninunue sare mpya.
    2. Kaka alisema kuwa hakutaka kwenda shambani.
    3. Mwalimu alisema aende hapo.
    4. Kalisa alisema kuwa yeye aliandika barua hiyo.
    5. Birasa alishangaa kuwa yeye hawezi kubeba mzigo huo.

    6. Mwalimu mkuu aliuliza sababu yake ya kulia.

    SOMO LA 12: Mjadala

    12.1 Mjadala kuhusu ‘Ufugaji kama njia ya kupigana na

     umaskini nchini’

    Katika makundi ya wanafunzi watatu watatu, tazameni na mjadili kuhusu
    kinachoendelea katika michoro hii kisha msome kifungu kilicho hapo chini na

    baadaye mjibu maswali ya ufahamu yanayofuata.




    Maswali ya ufahamu

    1. Mjadala uliosoma ulihusu nini?
    2. Bwana Niyibizi alitoa maoni gani kuhusiana na mada husika?
    3. Nyiraneza alichangia mjadala kwa hoja zipi?
    4. Muhirwa alitoa hoja zipi kuhusiana na umuhimu wa ufugaji?
    5. Eleza hoja alizotoa Bwana Rwambibi.

    6. Mwenyekiti alihitimisha vipi mjadala huu?

    12.2 Msamiati wa mjadala kuhusu ufugaji
    Katika makundi ya wanafunzi watatu watatu, tafuteni msamiati mpya katika
    kifungu cha mazungumzo hapo juu na kuueleza. Zingatieni matumizi ya msamiati

    huo katika kifungu hicho na mtumie kamusi pale inapohitajika. 

    Zoezi la 12.1

    Katika makundi ya wanafunzi wawili wawili, chunguzeni sentensi zifuatazo
    kisha mtunge sentensi zenu kwa kutumia maneno yaliyopigiwa mistari.

    1. Watoto wanapenda kunywa maziwa ya ng’ombe.
    2. Ni lazima sisi tupambane na umaskini kwa kufanya kazi kwa bidii.
    3. Mtoto huyu ana shida ya kukosa karo ya shule.
    4. Mfugaji huyu ametenga mnyama huyu mgonjwa ili asiambukize
    wanyama wengine.
    5. Kiwanda hiki kitafanya kazi kubwa ya kutengeneza nguo nyingi.
    6. Si vizuri kupuuza ushauri wa viongozi wetu.
    7. Mzungumzaji huyu amegusia umuhimu wa mifugo nchini Rwanda.
    8. Eneo hili lina mazao mazuri kwa sababu lina rutuba nyingi.
    9. Viwanda vyetu vinahitaji malighafi nyingi kutokana na kilimo.

    10. Mazungumzo yetu yamefikia kikomo kwa sasa.

    Zoezi la 12.2

    Chagueni neno kati ya yafuatayo ili kukamilisha sentensi hizi kwa usahihi:
    mjadala, hoja, umoja, umaskini, mifugo, mbolea, maziwa
    Kwa mfano: Ng’ombe wanatupatia ______________ ya kuweka katika
     mimea yetu.
    Jibu: Ng’ombe wanatupatia mbolea ya kuweka katika mimea
     yetu.
    1. Wizi wa ___________ unaweza kuleta hasara kubwa kwa wafugaji na
    kuwarudisha katika hali ya ___________.
    2. Watu wengi wanapenda kunywa ________ ili kupambana na magonjwa
    mbalimbali.
    3. Wafugaji hawa wamejiunga katika shirika kubwa kwa sababu wanajua
    kwamba _________ ni nguvu.
    4. __________ wetu umetufurahisha sana kwa sababu washiriki wote

    walitoa ________ nzuri. 

    12.3 Matumizi ya lugha: Kuunda maneno kamili
    Katika makundi ya mawafunzi wawili wawili, jaribuni kupanga sehemu za
    maneno zifuatazo ili kuunda maneno kamili.
    Kwa mfano: zi-te-m-te
    Jibu: mtetezi
    1. da-m-lo-ha
    2. ki-mwe-ti-nye
    3. zu-m-ngu-ji-za-m
    4. pi-u-ni-nza
    5. ja-la-da-m
    6. li-u-sha-ji-za li-ma
    7. fu-ji-u-ga
    8. ku-m-li-ma
    9. o-ma-ni

    10. li-ki-mo

    Zoezi la 12.3

    Katika makundi ya wanafunzi wawili wawili, jaribuni kupanga maneno
    yafuatayo ili kuunda sentensi kamili na sahihi.
    1. kazi lazima zinakwamisha za uvivu na ulevi tabia kwa sababu ni na
    kujiepusha mbaya.
    2. ya na kazi ufugaji za kilimo zinaweza raia kupigana wengi kuwasaidia
    umaskini dhidi.
    3. waweze bidii kazi mazuri kwa wafanya ni lazima watu ili kuwa maisha
    na wote.
    4. hushiriki katika na wengi kwa mjadala zao kutoa mdahalo watu hoja.
    5. namna kuhusu sisi maendeleo kazi umuhimu na miradi wa tunajadiliana

    ya kuanzisha ya

    12.4 Kusikiliza na kuzungumza: Kuandaa mjadala

    Jigaweni katika makundi ya wanafunzi watano watano kisha mwandae mjadala
    kuhusu mojawapo ya mada zifuatazo:
    1. Kazi muhimu za kuleta maendeleo kwa wananchi

    2. Tabia za kujiepusha ili kufanikisha kazi. 

    12.5 Sarufi: Mabadiliko ya kauli asili na kauli taarifa

    Katika makundi ya wanafunzi wawili wawili, chunguzeni kwa makini sentensi

    zifuatazo ili muweze kujibu maswali yaliyo hapo chini: 


    Zoezi la 12.4

    Katika makundi ya wanafunzi wawili wawili, jibuni maswali yafuatayo:
    1. Linganisha sentensi katika A na sentensi katika B kwa kuonyesha sifa
    zake.
    2. Tunga sentensi sita kwa kuzingatia sentensi katika A na kuziandika

    tena kwa kuzingatia sifa za sentensi katika B.

    Maelezo muhimu!

    Sentensi katika A ni za kauli asili na sentensi katika B zimeandikwa
    katika kauli taarifa.
    • Kutokana na kitenzi sema au uliza katika wakati uliopita, sentensi za
    kauli asili zimetanguliwa na kitenzi ‘alisema’ au ‘aliuliza’.
    Kwa mfano:
    • Wafanyakazi walisema, “Leo tunafurahia matunda ya kazi yetu.”
    • Dereva aliuliza, “Nani anataka kufika mjini Kigali?”
    • Mwanafunzi mmoja aliuliza, “Mdahalo utafanyiwa wapi?”
    • Alama ya kuuliza (?) na alama za kufunga na kufungua (“ ”) huwa
    hazitumiwi katika kauli taarifa.
    Kwa mfano: Dereva aliuliza mtu ambaye alitaka kufika mjini Kigali.
    • Mambo yafuatayo hubadilika wakati wa kugeuza sentensi za kauli asili
    na kuziandika katika kauli taarifa: 


    Zoezi la 12.5

    Katika makundi ya wanafunzi wawili wawili, badilisheni sentensi zifuatazo
    ziwe katika kauli taarifa.
    Kwa mfano: Wanafunzi wote walisema, “Sisi tunatakiwa kufaulu katika
     mitihani yote ya muhula huu.”
    Jibu:                          Wanafunzi wote walisema kwamba wao walitakiwa kufaulu
     katika mitihani yote ya muhula huo.
    1. Seremala mmoja alisema, “Mimi ninaunda vitanda vikubwa.”
    2. Mfugaji alisema, “Wanyama wetu wanakosa maji.”
    3. Mwalimu alisema, “Wanafunzi hawa wanaenda kucheza.”
    4. Mtoto wake alisema, “Mimi nitaenda kuchota maji pamoja na ndugu
    yangu.”

    5. Bwana yule aliuliza, “Unataka nini hapa?” 

    Tathmini ya mada ya 3

     Zoezi la 1

    1. Katika makundi ya wanafunzi watano watano, andaeni mdahalo kuhusu:
     ‘Shule za umma ni bora kuliko shule za kibinafsi’.
    2. Katika makundi yenu, jadilini kuhusu majukumu ya wahusika hawa wa
     mdahalo:
    a) Mwenyekiti                            b) Katibu                                       ch) Wapinzani                    d) Watetezi
    Zoezi la 2
    Katika makundi ya wanafunzi watano watano, andaeni mjadala kuhusu:

     ‘Athari za mavazi ya kisasa kwa wanajamii’.

    Zoezi la 3

    Katika makundi ya wanafunzi wawili wawili, andikeni sentensi hizi katika
    tungo kanushi.
    Kwa mfano: Wewe umeimba wimbo mzuri sana
    Jibu:                             Wewe hujaimba wimbo mzuri sana
    1. Yeye ameagiza bidhaa nyingi kutoka Kigali.
    2. Mimi nimezunguka mjini kwa gari.
    3. Mtoto wangu amefaulu mitihani yake
    4. Nyumba yangu imesafishwa.
    5. Mgomba umechomwa.
    6. Kazi hii imefanywa vizuri.
    7. Kitabu chako kimeharibika.
    8. Utambi umekauka.
    9. Udevu mrefu umenyolewa.

    10. Barua imetumwa.

    Zoezi la 4

    Baada ya kukanusha sentensi zilizo katika zoezi la 3 lililo hapo juu, ziandike
    tena katika wingi.
    Kwa mfano:                                    Wewe hujaimba wimbo mzuri sana (umoja, tungo kanushi)
    Jibu: Nyinyi hamjaimba (wingi, tungo kanushi)

    Zoezi la 5

    Katika makundi ya wanafunzi wawili wawili, andikeni sentensi hizi katika
    wingi.
    Kwa mfano: Kisu kimeibiwa
    Jibu:                     Visu vimeibiwa.
    1. Kiti kimevunjika
    2. Mtu huyu ametuimbia vizuri.
    3. Mzee huyu amelewa.
    4. Mwanafunzi huyu ameelewa somo la Kiswahili.
    5. Ng’ombe wangu amezaa leo.
    6. Mto huu umefurika.
    7. Kiongozi amewasili mapema.
    8. Mbwa amekula chakula.
    9. Uso wake umeharibika.
    10. Mguu wangu umetibiwa vizuri.

    Zoezi la 6

    Baada ya kuandika wingi wa sentensi katika zoezi la 3 lililo hapo juu, ziandike
    upya katika tungo kanushi.
    Kwa mfano: Visu vimeibiwa. (wingi, tungo yakinishi)
    Jibu:                 Visu havijaibiwa. (wingi, tungo kanushi)

    Zoezi la 7
    Katika makundi ya wanafunzi wawili wawili, kamilisheni sentensi zifuatazo
    kwa kutumia maneno yafuatayo:
    walipiga kura, wanatushawishi, uchumi, dhahiri, kuinua
    1. Kila mwananchi anapaswa kufanya kazi kwa bidii ili _______ kiwango
    cha maisha yake.
    2. _______________ wa nchi yetu utastawi baada ya kuanzisha miradi
    mingi mizuri.
    3. Viongozi hawa __________ kutumia mbinu za kisasa katika shughuli
    zetu za kilimo na ufugaji.
    4. Ni ________ kwamba raia wa Rwanda walipata maisha mazuri baada
    ya kuanzishwa kwa shughuli za ‘Gira inka Munyarwanda’.
    5. Juzi wanafunzi wote __________ kwa sababu Mkuu wa shule alitaka
    orodha ya viongozi wa madarasa yote. 
    

    Zoezi la 9

    Katika makundi yenu, badilisheni sentensi hizi ziwe katika kauli taarifa.
    1. Rais alisema, “Kila mwananchi anaweza kujitajirisha kwa kufanya kazi
    kwa bidii.”
    2. Mkuu wa shule alisema, “Wanafunzi wawili hawajui kusoma vizuri.”
    3. Wafanyakazi walisema, “Hatutaki kufanya kazi na watu wavivu.”
    4. Wazazi waliuliza, “Nani anaenda kununua mavazi ya watoto wetu?”

    5. Mkulima alisema, “Mvua hainyeshi sana siku hizi.”

    Zoezi la 10

    Katika makundi yenu, badilisheni sentensi hizi ziwe katika kauli asili.
    1. Kalisa alimwambia shangazi yake kuwa kesho yake angeenda Kigali.
    2. Bagirishya alisema huku akitetemeka kuwa chumbani mwake
    mlikuwa na nyoka.
    3. Kasisi alituambia kuwa ikiwa tungependa kuendelea vyema
    maishani, ingebidi tuwe na heshima.
    4. Daktari alituambia kuwa UKIMWI ni ugonjwa hatari sana.

    5. Baba aliniuliza idadi ya mabao tuliyofungwa mchezoni.





  • SURA NINE: MADA KUU 4: UIMARISHAJI WA STADI YA UANDISHI NA MASIMULIZI KUPITIA LUGHA YA KISWAHILI

    MADA KUU 4: UIMARISHAJI WA STADI YA
     UANDISHI NA MASIMULIZI
     KUPITIA LUGHA YA KISWAHILI
    Mada Ndogo:                Utungaji wa insha
    SOMO LA 13: Sehemu kuu za insha
    13.1 Kifungu kuhusu somo la Kiswahili
    Katika makundi ya wanafunzi wanne wanne, tazameni michoro hii kisha msome
    kifungu cha habari kilicho hapo chini na kujibu maswali ya ufahamu yanayofuata.


    
    Maswali ya ufahamu
    Katika makundi ya wanafunzi wanne wanne, someni tena kifungu kilicho hapo
    juu kisha mjibu maswali yafuatayo.

    1. Wanafunzi wa shule ya Mtume Paulo walimpenda mwalimu yupi?
    2. Taja tabia za Bwana Gasimba.
    3. Mtu ambaye ni mcheshi ni mtu mwenye tabia ya aina gani?
    4. Kwa nini somo la insha liliwafurahisha wanafunzi?
    5. Katika insha, mada na utangulizi huhusu nini?
    6. Katika insha mwili wa insha huhusu nini?
    7. Mwanafunzi anahitajika kuandika nini katika hitimisho la insha?
    8. Je, umejifunza nini kutokana na kifungu hiki?

    13.2 Msamiati kuhusu sehemu za insha

    Kutokana na kifungu cha habari ulichosoma hapo juu, katika makundi ya
    wanafunzi watatu watatu, jadilini kuhusu maana ya msamiati mpya uliojitokeza
    unaohusiana na sehemu za insha. Kamusi ya Kiswahili inaweza kutumika
    panapohitajika.
    Kwa mfano:
    mada – neno au sentensi ambayo inatambulisha jambo linalozungumziwa
    katika insha iliyoandikwa. Aghalabu mada ya insha huwa haizidi maneno

    manane.

    Zoezi la 13.1

    A. Katika makundi ya wanafunzi watatu watatu, elezeni maana ya
    msamiati uliopigiwa mistari katika sentensi zinazofuata kulingana na jinsi
    ulivyotumika katika kifungu cha habari mlichosoma hapo awali.
    1. Somo la Kiswahili litaanza kesho saa mbili asubuhi.
    2. Mutoni aliandika insha bora kuliko wanafunzi wenzake.
    3. Utangulizi wa insha yako unavutia.
    4. Mwili wa insha hubeba ujumbe wa insha nzima.
    5. Sharti kila insha iwe na hitimisho.
    6. Masimulizi ya mwalimu wetu yalitufurahisha darasani.
    B. Katika makundi ya wanafunzi watatu watatu, tungeni sentensi sahihi kwa

    kutumia maneno yaliyopigiwa mistari katika Zoezi 1A lililo hapo juu.

    Maelezo muhimu!

    Sehemu kuu za insha ni:
    1. Mada au kichwa cha insha
    Mada ya insha hutambulisha jambo linalozungumziwa katika insha.
    Mada ya insha haifai kuzidi maneno manane. Mara nyingi mada ya
    insha huandikwa kwa herufi kubwa na kupigiwa mstari. Lazima mada
    iwe na mvuto kwa msomaji.
    2. Utangulizi au mwanzo wa insha
    Utangulizi wa insha mara nyingi huwa ni aya moja tu. Unafaa kuvutia
    kwa kiwango cha juu ili kumpa msomaji hamu ya kutaka kusoma insha
    nzima.
    3. Mwili wa insha
    Hii ndiyo sehemu muhimu sana kwa sababu inabeba ujumbe kamili wa
    insha nzima. Aya nyingi huandikwa hapa na ni bora aya hizi ziandikwe
    kwa namna ya kutiririsha matukio kuanzia mwanzo hadi mwisho wa
    insha.

    4. Hitimisho au mwisho wa insha

    Sehemu hii huwa na sentensi chache tu katika aya moja. Hitimisho
    hufupisha yaliyoandikwa katika mwili wa insha kwa namna ya kuvutia

    msomaji. 

    13.3 Matumizi ya lugha: Majadiliano

    Jigaweni katika makundi ya wanafunzi wanne wanne kisha mjadili kuhusu
    sehemu kuu za insha mnazozifahamu. Hakikisheni kuwa mmejibu maswali haya.
    1. Mada ya insha huhusu nini?
    2. Utangulizi wa insha huandikwa kwa kuzingatia mambo gani?
    3. Mwili wa insha huhusu nini?
    4. Hitimisho huandikwa vipi?

    5. Lugha inayotumika kuandika insha huwa ya aina gani?

    13.4 Kusikiliza na kuzungumza: Somo la imla
    Zoezi la Imla

    Sikiliza kwa makini sentensi utakazosomewa na mwalimu wako kisha

    uzinakili katika daftari lako kwa kuzingatia alama sahihi za uandishi.

    13.5 Sarufi
    Ngeli ya U-ZI
    Jigaweni katika makundi ya wanafunzi wawili wawili kisha msome aya ifuatayo

    na mworodheshe majina yaliyo katika ngeli ya U-ZI. 

    Katika makundi ya wanafunzi wawili wawili, tungeni sentensi katika umoja na
    wingi kwa kutumia maneno mliyoorodhesha hapo juu.

    Maelezo muhimu!

    Majina katika ngeli ya U-ZI katika sentensi hutumia kiambishi nafsi ‘u-‘
    katika umoja na kiambishi nafsi ‘zi-‘ katika wingi.
    Kwa mfano:
    1. Ukuta wa nyumba yangu umepakwa rangi.
    Kuta za nyumba zetu zimepakwa rangi.
    2. Wimbo mzuri umeimbwa na mtoto.
    Nyimbo nzuri zimeimbwa na watoto.

    Mifano ya majina na michoro yake katika ngeli ya U-ZI

    A. Katika makundi ya wanafunzi wawili wawili, kanusheni sentensi zifuatazo.
    Kwa mfano: Ufunguo mpya umepotea.
    Jibu:         Ufunguo mpya haujapotea.
    1. Ulimi wake umepona.
    2. Upanga huu utatumika kukatia muwa.
    3. Uzi wangu umekatika.
    4. Ukucha wako umeumia.
    5. Wimbo mrefu utaimbwa na wanafunzi.
    B. Katika makundi ya wanafunzi wawili wawili, andikeni sentensi mlizokanusha

    hapo juu katika wingi. 

    Zoezi la 13.2

    Katika makundi ya wanafunzi watatu watatu, tungeni sentensi sahihi katika
    umoja na wingi kwa kutumia majina yafuatayo katika hali yakinishi.
    Kwa mfano: Fito
    Jibu:                  Ufito mrefu utatumiwa kujengea nyumba.
                                 Fito ndefu zitatumiwa kujengea nyumba.
    1. kurasa
    2. ndevu
    3. wakati
    4. nyembe
    5. upanga

    6. ulimi

    Zoezi la 13.3

    Katika makundi ya wanafunzi watatu watatu, kanusheni sentensi mlizotunga
    katika zoezi la 13.2 lililo hapo juu.
    13.5.1 Ngeli ya U-ZI pamoja na vivumishi vya sifa
    Katika makundi ya wanafunzi watatu watatu, jadilini sentensi zinazofuata (zenye

    michoro na picha) kisha mwelezane maneno yaliyopigiwa mistari ni ya aina gani.

    Maelezo muhimu!

    Maneno ambayo hutumiwa kutoa maelezo zaidi kuhusu nomino huitwa
    vivumishi. Vivumishi vinavyoeleza namna nomino inavyoonekana na
    tabia ya nomino huitwa vivumishi vya sifa.
    Mifano:
    1. Ukuta mrefu umejengwa.
    2. Uso safi umepakwa mafuta.
    3. Ukucha mchafu utakatwa.

    4. Ufagio mpya utanunuliwa.

    Zoezi la 13.4

    Katika makundi ya wanafunzi watatu watatu, tambueni vivumishi vya sifa
    katika sentensi zinazofuata.
    Kwa mfano:                            Ufito mrefu umekatwa.
    Jibu: ‘mrefu’ ni kivumishi cha sifa
    a) Wimbo mzuri umeimbwa na wanafunzi hawa.
    b) Ukurasa mweupe umechafuliwa na mtoto yule.
    ch) Fagio mpya zitauzwa sokoni na mama yangu.
    d) Uzi mweusi utatumiwa kushonea nguo yake.

    e) Ndevu ndefu zitanyolewa kesho.

    Zoezi la 13.5
    Katika makundi ya wanafunzi wawili wawili, tungeni sentensi sahihi kwa
    kutumia majina ya ngeli ya U-ZI pamoja na vivumishi hivi.
    Kwa mfano:              -refu
    Jibu: Waraka mrefu umeandikwa na Kabera.
    1. -chafu
    2. safi
    3. -eusi
    4. -kubwa

    5. -dogo

    SOMO LA 14: Mambo ya kuzingatia katika uandishi wa insha
    14.1 Kifungu kuhusu malezi bora
    Katika makundi ya wanafunzi watatu watatu, tazameni michoro ifuatayo kisha
    mjadili na mwelezane mnachokiona na hapo baadaye msome kifungu cha habari

    kilicho hapo chini na kujibu maswali yanayofuata.

                     

                 

    Maswali ya ufahamu
    1. Eleza tabia za wazazi wa Mutesi.
    2. Mutesi ameiga tabia zipi kutoka kwa wazazi wake?
    3. Taja mambo muhimu ya kuzingatia katika kuandika insha.
    4. Malezi bora ni nini?
    5. Umejifunza nini kutokana na kifungu ulichosoma hapo juu?
    Maswali ya uhakiki
    1. Kifungu ulichosoma kina aya ngapi?
    2. Taja majina ya watu waliozungumziwa katika kifungu ulichosoma.
    3. Eleza tabia za watu uliowataja kutokana na kifungu ulichosoma.
    4. Eleza mawazo makuu yanayozungumziwa katika kila aya.

    5. Onyesha aya zinazojenga kila sehemu kuu ya insha uliyosoma.

    Maelezo muhimu!
    Mkusanyiko wa sentensi ambazo zinazungumzia wazo moja kuu
    huitwa aya.
    • Ili aya ieleweke, sharti mwandishi atumie kwa usahihi alama za
    uandishi kama vile: nukta, koma, mkato, herufi kubwa, n.k.

    14.2 Msamiati kuhusu uandishi wa insha

    Kutokana na kifungu cha mazungumzo ulichosoma hapo awali, katika makundi
    ya wanafunzi watatu watatu, jadilini kuhusu maana ya msamiati mpya
    uliojitokeza na kuhusiana, kisha utunge insha. Kamusi ya Kiswahili inaweza
    kutumika inapohitajika.
    Kwa mfano:
    insha – mtungo unaoandikwa kuhusu kitu, mtu au jambo kwa kufululiza
     maneno katika sentensi hadi katika aya kwa njia ya kusimulia au
     kuhadithia jambo fulani hatua kwa hatua. 
    Zoezi la 14.1

    A. Katika makundi ya wanafunzi watatu watatu, elezeni maana ya
    msamiati uliopigiwa mistari katika sentensi zinazofuata kulingana na jinsi
    ulivyotumika katika kifungu mlichosoma hapo awali.

    1. Mwalimu ameandika aya mbili za insha kwenye ubao.
    2. Mada ya insha aliyotupa mwalimu wetu ni rahisi.
    3. Sharti ubuni kisa akilini kabla ya kuandika insha.
    4. Insha nzuri inafaa kutiririka kutoka mwanzo hadi mwisho.
    5. Kila mwanafunzi anashauriwa kuwa na mwandiko safi.
    6. Mwalimu wetu hukosoa makosa yote ya kisarufi.
    7. Ni jukumu la kila mzazi kumpa mwanawe malezi mema.
    8. Mutesi aliziiga tabia nzuri za wazazi wake.
    B. Katika makundi ya wanafunzi watatu watatu, tungeni sentensi kwa kutumia
    msamiati uliopigiwa mistari katika sentensi za zoezi la 1A lililo hapo juu.

    Maelezo muhimu!
    Insha ni mtungo unaoandikwa kuhusu kitu, mtu au jambo kwa
    kufululiza maneno katika sentensi hadi katika aya kwa njia ya kusimulia
    au kuhadithia jambo fulani hatua kwa hatua. Insha inaweza kuandikwa

    katika mpango wa mazungumzo. 

    Mambo ya kuzingatia katika uandishi wa insha
    1. Mwandiko uwe safi: Maandishi yaonekane vizuri na yasomeke ili
    kurahisisha usomaji.
    2. Urefu: Insha iwe na urefu wa wastani (insha isiwe fupi sana na
    isiwe ndefu sana).
    3. Lugha ya insha: Sharti lugha sahihi, sanifu na rahisi kueleweka

    itumike ili kumvutia msomaji.

    4.3 Matumizi ya lugha: Majadiliano

    Jigaweni katika makundi ya wanafunzi wawili wawili kisha mjadili kuhusu
    mambo ambayo nyinyi huzingatia katika kuandika insha mbalimbali. Wanafunzi
    waelezane:
    1. Mada mbalimbali za insha mbalimbali.
    2. Mambo wanayozingatia wanapoandika insha.
    3. Namna ya kuboresha mwandiko usiofaa.
    4. Kiasi cha urefu wa kuandika insha mbalimbali.

    5. Mapambo mbalimbali yanayoweza kutumika katika kuandika insha.

    14.4 Kusikiliza na kuzungumza: Majadiliano

    Katika makundi ya wanafunzi wawili wawili, jadilini kuhusu namna ya kuandika

    insha bora kwa kuzingatia kifungu mlichosoma hapo awali.

    14.5 Sarufi

    Ngeli ya U-ZI pamoja na vivumishi viashiria

    Katika makundi ya wanafunzi wanne wanne, tazameni michoro ifuatayo kisha

    muilinganishe na sentensi zilizo chini yake.

    Zoezi la 14.2

    Katika makundi ya wanafunzi watatu watatu, andikeni wingi wa sentensi
    zinazofuata.
    1. Ukuta huu umekamilika kujengwa.
    2. Uso huo una kidonda.
    3. Ufagio ule umetumika kwa muda mrefu.
    4. Uzi huu unahitajika na mama.
    5. Wimbo huo unavutia.
    6. Wembe ule ulimkata mtoto.

    Je, mmegundua nini?

    Maelezo muhimu!

    Maneno ambayo hutumiwa kuonyesha umbali wa nomino huitwa
    vivumishi viashiria. Yaani ni maneno yanayoashiria iliko nomino.
    Kuna umbali wa aina tatu:
    a) Karibu na mzungumzaji
    Kwa mfano: Ukuta huu, uso huu, uzi huu n.k.
    b) Mbali kidogo na mzungumzaji
    Kwa mfano: Ukuta huo. uso huo. uzi huo n.k.
    ch) Mbali sana na mzungumzaji

    Kwa mfano: Ukuta ule, uso ule, uzi ule n.k

    Vivumishi viashiria katika wingi hutegemea umbali wa nomino
    inayorejelewa:
    a) Katika ngeli ya U-ZI, nomino ikiwa karibu na mzungumzaji, katika
    umoja kivumishi kiashiria kitakuwa ‘huu’ na katika wingi kitakuwa
    ‘hizi’.
    b) Katika ngeli ya U-ZI, nomino ikiwa mbali kidogo na mzungumzaji,
    katika umoja kivumishi kiashiria kitakuwa ‘huo’ na katika wingi
    kitakuwa ‘hizo’.
    ch) Katika ngeli ya U-ZI, nomino ikiwa mbali sana na mzungumzaji,
    katika umoja kivumishi kiashiria kitakuwa ‘ule’ na katika wingi

    kitakuwa ‘zile’.

    Zoezi la 14.3

    Katika makundi ya wanafunzi wawili wawili, andikeni umoja wa sentensi hizi.
    1. Kurasa hizi zimelowa maji.
    2. Kucha hizi zitakatwa.
    3. Funguo hizo ni za nyumba za walimu wetu.
    4. Panga hizi zitatumika shambani.

    5. Nyimbo hizo zinaimbwa vizuri sana.

    Zoezi la 14.4

    Katika makundi ya wanafunzi wawili wawili, jazeni nafasi zilizo wazi kwa
    kuchagua vivumishi viashiria sahihi kutoka kwenye mabano.
    1. Ukuta __________ umebomolewa. (zile, ule)
    2. Fito __________ zimevunjika. (hizo, hiyo)
    3. Nyuzi ___________ za manjano zimeuzwa. (ile, zile)
    4. Uso ___________ umevimba. (huu, hii)

    5. Nyembe __________ zitawakata watoto wale. (ile, zile)

    Zoezi la 14.5

    Katika makundi ya wanafunzi wawili wawili, tungeni sentensi sahihi kisarufi
    kwa kutumia majina yafuatayo ya ngeli ya U-ZI.

    1. Wimbo
    2. Waraka
    3. Ukuta
    4. Udevu

    5. Unywele

    SOMO LA 15: Aina mbalimbali za insha
    15.1 Kifungu kuhusu umuhimu wa adabu

    Katika makundi ya wanafunzi watatu watatu, tazameni michoro hii kisha
    mwelezane mnachokiona. Tangulizeni sentensi zenu kwa: Mimi ninaona…Hapo
    baadaye msome kifungu cha habari kilicho hapo chini na kujibu maswali ya

    ufahamu yanayofuata.



    Maswali ya ufahamu

    1. Eleza sifa za Mutoni.
    2. Eleza hali ya familia ya Mutoni.
    3. Kwa nini mwalimu wa somo la Kiswahili aliamua kumfadhili Mutoni?
    4. Kwa nini wanafunzi walimpenda Mutoni?

    5. Kozi ambayo Mutoni aliifanya chuoni ilikuwa na manufaa gani?

    Maswali ya uhakiki
    1. Eleza namna mada inavyohusiana na insha uliyosoma.
    2. Eleza mawazo makuu matatu yaliyojitokeza katika insha uliyosoma.
    3. Andika mawazo hayo kwa maneno yako mwenyewe. Usizidi maneno

    sabini (70).

    15.2 Msamiati kuhusiana na umuhimu wa adabu

    Kutokana na kifungu mlichosoma hapo awali, katika makundi ya wanafunzi
    wanne wanne, jadilini kuhusu maana ya msamiati mpya. Kamusi ya Kiswahili
    inaweza kutumika panapohitajika.
    Kwa mfano:

    wema - mambo mazuri anayoyafanya mtu

    Zoezi la 15.1

    A. Katika makundi ya wanafunzi wawili wawili, elezeni maana ya msamiati
    uliopigiwa mistari katika sentensi zinazofuata kulingana na jinsi
    ulivyotumika katika kifungu mlichosoma hapo awali.

    1. Mutoni anasoma katika kidato cha tatu.
    2. Baba yangu amelipa karo yote ya muhula huu.
    3. Mimi sina mahitaji mengi nyumbani.
    4. Wao wanaishi katika kijiji duni.
    5. Mama yangu ni mpole na mwenye bidii.
    6. Mutoni ndiye kiranja mkuu katika shule yao.
    7. Sare za wanafunzi hawa ni mpya.
    8. Ufadhili aliopata kaka yangu uliwafurahisha wazazi wetu.
    9. Kamana anasomea kozi ya udaktari chuoni.

    B. Katika makundi ya wanafunzi wawili wawili, tungeni sentensi sahihi kwa

    kutumia maneno yaliyopigiwa mistari katika sentensi za Zoezi la 1A.

    15.3 Matumizi ya lugha: Mifano ya insha
    15.3.1 Insha ya wasifu
    Katika makundi ya wanafunzi wawili wawili, tazameni michoro hii kisha msome

    mfano wa insha ifuatayo na mjadili maswali yanayofuata:



    Maswali ya uhakiki
    Katika makundi ya wanafunzi wawili wawili, jadilini maswali yanayofuata
    kutokana na mfano wa insha ya wasifu uliotolewa hapo juu.
    1. Eleza insha mliyosoma ni ya aina gani.
    2. Eleza mambo ya kuzingatia katika kuandika insha ya aina hii.
    3. Pendekeza kichwa cha insha hii.
    4. Eleza sifa ambazo ni za kimaumbile za baba anayezungumziwa katika
    insha mliyosoma.
    5. Taja tabia za baba anayezungumziwa katika insha mliyosoma hapo juu.
    6. Kwa nini watu wengi wanampenda baba huyu?

    7. Ni nini kinachoonyesha kuwa baba huyu ana bidii katika kazi yake?

    Maelezo muhimu!

    Insha zinazoeleza sifa nzuri au mbaya kuhusu maumbile ya mtu au kitu

    fulani huitwa insha za wasifu.

    Zoezi la kuandika
    Katika makundi ya wanafunzi wawili wawili, tungeni insha ya wasifu wako

    binafsi.

    15.3.2 Insha ya mazungumzo
    Katika makundi ya wanafunzi watatu watatu, tazameni mchoro huu kisha msome

    mfano wa insha ifuatayo na mjadili maswali yanayofuata: 

    Maswali ya uhakiki
    Katika makundi ya wanafunzi watatu watatu, jadilini maswali haya kutokana
    na mfano wa insha mliyoisoma hapo juu.
    1. Eleza insha mliyosoma ni ya aina gani.
    2. Eleza mambo ya kuzingatia katika kuandika insha ya aina hii.
    3. Pendekeza kichwa cha insha hii.
    4. Wazungumzaji katika mazungumzo haya ni kina nani?
    5. Eleza kazi ya daktari katika jamii.
    6. Daktari anamsaidia vipi Kayitesi?

    7. Kayitesi anaugua wapi?

    Maelezo muhimu!

    Insha zinazohusu mazungumzo kati ya watu wawili au zaidi huitwa

    insha za mazungumzo. Insha hizi huandikwa kwa mtindo wa tamthilia. 

    Zoezi la maigizo
    Katika makundi ya wanafunzi wawili wawili, igizeni mazungumzo kati ya Daktari

    na Mgonjwa (Kayitesi) mliyosoma hapo awali.

    Zoezi la kuandika
    Katika makundi ya wanafunzi wawili wawili, bunini mazungumzo kati ya

    mwalimu na mwanafunzi kisha myaigize. 

    15.4 Kusikiliza na kuzungumza
    Somo la imla


    Sikiliza kwa makini sentensi ambazo mwalimu wako atakusomea kisha uziandike

    kwa usahihi katika daftari lako.

    15.5 Sarufi

    Ngeli ya U-ZI pamoja na vivumishi vimilikishi
    Katika makundi ya wanafunzi watatu watatu, tazameni picha na michoro

    ifuatayo kisha muiambatanishe na sentensi zilizo chini yake.



    Mifano katika sentensi
    Umoja Wingi

    1. Wimbo wangu unavutia.                                                Nyimbo zetu zinavutia.
    2. Ukuta wangu umepakwa rangi.                                 Kuta zetu zimepakwa rangi.
    3. Unywele wako utanyolewa kesho.                           Nywele zenu zitanyolewa kesho.
    4. Uso wako umevimba.                                                       Nyuso zenu zimevimba.
    5. Uzi wake umepotea.                                                          Nyuzi zao zimepotea.

    6. Ukurasa wake umeandikwa.                                         Kurasa zao zimeandikwa.

    Zoezi la 15.2

    Katika makundi ya wanafunzi watatu watatu, tungeni sentensi sahihi kwa kutumia

    majina yafuatayo pamoja na vivumishi vimilikishi vilivyo kwenye mabano.
    Kwa mfano: Wimbo (wake)
    Jibu:                       Wimbo wake ulipendwa na wasikilizaji wote.
    1. Kurasa (zetu)
    2. Ufa (wako)
    3. Nyuzi (zenu)
    4. Ufito (wangu)

    5. Nyembe (zao)

    Zoezi la 15.3

    Katika makundi ya wanafunzi watatu watatu, andikeni sentensi zifuatazo katika
    wingi.

    Kwa mfano: Waraka wangu umetumwa.
    Jibu:                     Nyaraka zetu zimetumwa.
    1. Ubao wake umepakwa rangi nyekundu.
    2. Ukuta wako umeangukia nyumba yangu.
    3. Ukucha wangu umeumia vibaya.
    4. Wakati wako umekwisha.

    5. Wimbo wake ulirekodiwa jana mjini Kigali.

    Zoezi la 15.4
    Katika makundi ya wanafunzi watatu watatu, andikeni sentensi zifuatazo katika
    umoja.
    Kwa mfano:                Nyembe kali zitatumika kukata kucha.
    Jibu: Wembe mkali utatumika kukata ukucha.
    1. Ndevu za wavulana wale zimekuwa ndefu sana.
    2. Nywele za mabinti hawa ni nyeusi tititi.
    3. Nyayo za watoto hao zina matope.
    4. Nyakati za kusoma kwa wanafunzi zimekwisha.

    5. Nyuso za wazee wale zimepakwa mafuta.

    Zoezi la 15.5

    Andika wingi wa majina haya ya ngeli ya U-ZI.
    1. Wayo
    2. Wakati
    3. Wimbo
    4. Ufito

    5. Upinde

    SOMO LA 16: Aina za insha

    16.1 Kifungu kuhusu madhara ya uvivu

    Katika makundi ya wanafunzi watatu watatu, chunguzeni mchoro ufuatao
    kisha mjadili kuhusu kinachoendelea katika mchoro wenyewe. Hapo baadaye,
    msome kifungu kilicho hapo chini kuhusu madhara ya uvivu na mjibu maswali

    yanayofuata. 


    Maswali ya ufahamu

    1. Eleza maana ya uvivu.
    2. Eleza madhara ya uvivu.
    3. Uvivu huathiri mwanafunzi kwa namna gani?
    4. Nchi huathirika vipi kutokana na uvivu?
    5. Afya za watu wavivu huweza kuathirika kwa njia gani?
    6. Umejifunza nini kutokana na kifungu ulichokisoma?

    7. Eleza namna ya kuepukana na uvivu.

    16.2 Msamiati kuhusu madhara ya uvivu

    Katika makundi ya wanafunzi watatu watatu, tafuteni msamiati mpya kutoka
    katika kifungu mlichokisoma hapo juu na kuueleza. Zingatieni matumizi ya

    msamiati huo katika kifungu hicho na mtumie kamusi pale inapohitajika. 

    Zoezi la 16.1

    Katika makundi ya wanafunzi watatu watatu, chunguzeni sentensi zifuatazo
    kisha mtunge sentensi sahihi kwa kutumia maneno yaliyopigiwa mstari.
    1. Uvivu ni adui wa maendeleo kwa binadamu.
    2. Dawa za kulevya huathiri afya ya mtu anayezitumia.
    3. Umaskini na ujinga husababishwa na uvivu.
    4. Mwanafunzi yule alifanya bidii katika masomo yake na akafaulu.
    5. Usipojitahidi katika shughuli zako utaishia kuwa ombaomba.
    6. Mtu mvivu huweza kujiingiza katika uhalifu.

    7. Kamana alijitahidi katika mtihani wake wa kitaifa.

    Zoezi la 16.2

    Katika makundi ya wanafunzi wawili wawili, kamilisheni sentensi zifuatazo
    kwa kutumia maneno yafuatayo:
    wasumbufu, dawa za kulevya, masomo, bidii, maendeleo,

    ombaomba.

    Kwa mfano: Watu walio wavivu huishia kuwa _____________ sana
     katika jamii.
    Jibu: Watu walio wavivu huishia kuwa wasumbufu sana katika jamii.
    1. ______________ wamejaa mjini.
    2. Uvivu huathiri ______________ ya nchi.
    3. Mwanafunzi mvivu hawezi kufanikiwa katika ______________ yake.
    4. Ubakaji, ukorofi pamoja na matumizi ya ___________ yakomeshwe.
    5. Mtu akifanya ___________ katika shughuli zake atafanikiwa.

    

    16.3 Matumizi ya lugha: Aina za insha
    16.3.1 Insha ya maelezo


    Katika makundi ya wanafunzi watatu watatu, tazameni michoro hii kisha msome

    mfano wa insha ifuatayo na mjadili maswali yanayofuata: 

     

    Maswali ya uhakiki
    1. Waeleze wenzako insha uliyosoma ni ya aina gani?
    2. Mambo gani huzingatiwa katika kuandika insha ya aina hii?
    3. Eleza umuhimu wa maji kwa binadamu.
    4. Eleza umuhimu wa maji kwa mimea.
    5. Wanyama hufaidika vipi kutokana na maji?

    6. Miti hutusaidia kwa njia ipi kupata maji?

    Maelezo muhimu!
    Insha ambazo hutoa taarifa kuhusu mtu, kitu, mahali, hali au jambo fulani
    huitwa insha za maelezo. Insha hizi huhitaji maelezo ya kweli wala siyo

    maelezo ya kubuni.

    Zoezi la kuandika
    Andika insha ya maelezo kuhusu vivutio vya utalii katika nchi ya Rwanda.

    16.3.2 Insha ya barua rasmi

    Katika makundi ya wanafunzi wawili wawili, someni mfano wa insha ifuatayo

    kisha mjadili maswali yanayofuata. 

    Maswali ya uhakiki
    Katika makundi ya wanafunzi watatu watatu, jadilini maswali haya kwa
    kurejelea mfano wa insha mliyosoma hapo juu.
    1. Eleza insha mliyosoma ni ya aina gani.
    2. Eleza mambo ya kuzingatia katika kuandika insha ya aina hii.
    3. Pendekeza kichwa cha insha hii.
    4. Anwani ngapi zimetumika katika barua hii? Ni za kina nani?

    5. Lengo la kuandika barua hii ni lipi?

    Zoezi la kuandika/Utafiti

    1. Tunga mfano wa barua ya kirafiki.
    2. Eleza namna ya kuandika barua ya mwaliko. Buni mfano mmoja wa
    barua ya mwaliko.
    3. Ni mambo gani huzingatiwa katika kuandika:
    i) Barua rasmi
    ii) Barua ya kirafiki

    iii) Barua ya mwaliko

    16.4 Kusikiliza na kuzungumza
    Somo la imla

    i) Sikiliza kwa makini insha ambayo mwalimu wako atakusomea kisha
    uiandike katika daftari lako.
    ii) Kwa kufuata mfano wa insha uliyosomewa na mwalimu wako, buni insha

    yako mwenyewe inayofanana na hiyo.

    16.5 Sarufi
    Ngeli ya U-ZI pamoja na vivumishi vya idadi
    Katika makundi ya wanafunzi wanne wanne, tazameni michoro ifuatayo kisha

    muiambatanishe na sentensi zilizo chini yake

    Je, mmegundua nini?
    Katika makundi ya wanafunzi watatu watatu, jadilini kuhusu maneno yaliyopigiwa
    mistari katika sentensi zilizo hapo juu. Maneno hayo ni ya aina gani? Maneno
    hayo yanarejelea nini?
    Zoezi la 16.3
    Katika makundi ya wanafunzi watatu watatu, tungeni sentensi sahihi kwa
    kutumia majina yafuatayo pamoja na vivumishi vya idadi.
    Kwa mfano: nyembe nane
    Jibu:                                 Mwalimu alinunua nyembe nane kutoka dukani.

    1. Kuta (mbili)                                      2. Fagio (tatu)                     3. Teo (nne)

    4. Uzi (mmoja)                                     5. Nyuso (tano)                  6. Nyaraka (kumi)

    Maelezo muhimu!

    Maneno ambayo hutumiwa kutaja hesabu, idadi au kiasi cha vitu au
    viumbe fulani huitwa vivumishi vya idadi.
    Vivumishi vya idadi hugawika katika aina mbili:
    i) Vivumishi vya idadi kamili, kwa mfano: ukuta mmoja,
    kuta nne, uso mmoja, nyuso tano, upanga mmoja, panga
    nane, n.k.

    Mifano katika sentensi:
    a) Uzi mmoja umepotea.
    b) Nyuzi tano zimepotea.
    ch) Ukuta mmoja umejengwa.
    d) Kuta nne zimejengwa.
    ii) Vivumishi vya idadi isiyo kamili, kwa mfano: kuta chache,

    kurasa nyingi, nyimbo kadhaa, nyaraka tele, n.k.

    Mifano katika sentensi:
    a) Nyimbo nyingi ziliimbwa jana.

    b) Nyaraka kadhaa zimepotea.

    Zoezi la 16.4

    Katika makundi ya wanafunzi watatu watatu, tungeni sentensi sahihi kwa
    kutumia majina yafuatayo pamoja na vivumishi vya idadi.

    1. Wimbo (mmoja)
    2. Kurasa (nyingi)
    3. Nyufa (mbili)
    4. Uzi (mmoja)
    5. Fito (kadhaa)

    6. Nyembe (chache)

    Zoezi la 16.5
    Katika makundi ya wanafunzi watatu watatu, jazeni nafasi zilizo wazi katika
    sentensi zinazofuata kwa kutumia vivumishi vya idadi sahihi kutoka kwenye
    mabano.
    Kwa mfano: Nyaraka ____________ zimesomwa. (wanne, nne, zinne)
    Jibu:                  Nyaraka nne zimesomwa.
    1. Ulimi ____________ umeumia. (moja, mmoja, umoja)
    2. Fito ____________ zitatumika kujengea. (nyingi, vingi, wingi)
    3. Nyimbo __________ zimetungwa na baba yake. (chache, uchache,
    wachache)
    4. Nyuso ____________ zimepakwa mafuta. (tano, watano, vitano)

    5. Ufagio ____________ uliuzwa jana. (moja, mmoja, umoja)

    Tathmini ya mada ya 4

    Zoezi la 1

    Katika makundi ya wanafunzi watatu watatu, tungeni sentensi kwa
    kutumia majina yafuatayo ya ngeli ya U-ZI pamoja na vivumishi vimilikishi
    mlivyopewa kwenye mabano.
    1. Wimbo (wao)
    2. Kurasa (zake)
    3. Nyufa (zetu)
    4. Uzi (wangu)
    5. Fito (zenu)
    6. Nyembe (zako)

    Zoezi la 2

    Katika makundi ya wanafunzi watatu watatu, kanusheni sentensi hizi.
    1. Utepe wangu ulipotea.
    2. Kucha zenu zinapendeza.
    3. Upanga wake ulivunjika.
    4. Wimbo wa taifa unaimbwa sasa.

    5. Wakati wa mapumziko umewadia.

    Zoezi la 3

    Katika makundi ya wanafunzi watatu watatu, andikeni sentensi za zoezi la
    2 lililo hapo juu katika umoja au wingi hali yakinishi.

    Zoezi la 4

    Katika makundi ya wanafunzi watatu watatu, tambueni vivumishi vya sifa
    katika sentensi zifuatazo.
    1. Udevu mfupi hautakatwa.
    2. Ukuta mpana utapakwa rangi.
    3. Funguo nyepesi zimeanguka.
    4. Wembe mzee ulinikata.
    5. Ubao mweusi utatumika

    Zoezi la 5

    Katika makundi ya wanafunzi wanne wanne, tungeni:
    1. Wasifu kuhusu shule yako.
    2. Mazungumzo kati ya mzazi na mtoto wake.
    Zoezi la 6

    Katika makundi ya wanafunzi wanne wanne, jadilini kuhusu madhara ya uvivu
    katika jamii hasa kwa mwanafunzi.

    

    

  • Topic 5

    MADA KUU 5: LUGHA NA TEKNOLOJIA
    Mada Ndogo: Kiswahili katika teknolojia ya habari na

                                  mawasiliano.

    SOMO LA 17: Simu ya mkononi

    17.1 Mazungumzo kuhusu matumizi ya simu ya mkononi
    Katika makundi ya wanafunzi watatu watatu, tazameni picha zifuatazo
    kisha mwelezane vifaa mnavyoona pamoja na matumizi na umuhimu wake.
    Baadaye, msome kifungu cha mazungumzo kilicho hapo chini na mjibu maswali

    yanayofuata. 


                 

    Maswali ya ufahamu
    Katika makundi ya wanafunzi watatu watatu, someni tena kifungu cha
    mazungumzo yaliyo hapo juu kisha mjibu maswali yanayofuata.

    1. Taja wazungumzaji katika kifungu cha mazungumzo ulichosoma hapo
    juu.
    2. Bila shaka mazungumzo yanahusiana na teknolojia. Kwa nini? Eleza.
    3. Taja chombo cha mawasiliano kilichozungumziwa.
    4. Orodhesha matumizi yoyote mawili ya simu ya mkononi waliyotaja
    wazungumzaji.
    5. Mama ana matatizo gani kuhusiana na simu yake mpya?
    6. Kulingana na baba, ni mambo gani ambayo huathiri matumizi ya simu ya
    mkononi kijijini kwao?
    7. Teknolojia ni nini? Eleza kwa maneno yako mwenyewe.
    8. Taja msamiati wa adabu ambao umetumika katika kifungu cha

    mazungumzo mliyoyasoma.

    17.2 Msamiati kuhusu simu ya mkononi

    Katika makundi ya wanafunzi watatu watatu, tafuteni msamiati mpya kutoka
    katika kifungu cha mazungumzo mlichosoma na kuueleza. Zingatieni matumizi
    ya msamiati huo katika kifungu hicho na mtumie kamusi pale inapohitajika.

    Zoezi la 17.1
    Katika makundi ya wanafunzi watatu watatu, chunguzeni sentensi zifuatazo
    kisha mtunge sentensi sahihi kwa kutumia maneno yaliyopigiwa mstari.

    1. Simu ya mkononi ambayo mama alinunuliwa inamsaidia sana.
    2. Teknolojia katika nchi yetu imekua kwa kiwango kikubwa.
    3. Simu ya babu yangu ni ya kubofya vidude.
    4. Dada yangu aliye ng’ambo alinitumia arafa kwenye simu yangu.
    5. Baba atampigia mwalimu wetu simu ili kuniombea ruhusa.
    6. Simu mpya aliyonayo ni ya kugusa kwenye kiwambo chake.
    7. Simu yangu ina kamera nzuri sana.

    8. Intaneti ni muhimu sana katika matumizi ya simu.

    Zoezi la 17.2

    Katika makundi ya wanafunzi wawili wawili, kamilisheni sentensi zifuatazo
    kwa kutumia maneno yafuatayo:
    arafa, watisapu, kunasia mawimbi, fesibuku, simu, chaji
    Kwa mfano: Baba alinunua ____________ mpya baada ya ile ya
     kwanza kuibwa.
    Jibu:           Baba alinunua simu mpya baada ya ile ya kwanza kuibwa.
    1. Sharti simu iwe na ______________ ili iweze kutumika.
    2. Watu wengi siku hizi wanatumia _____________ na ______________
    kuwasiliana.
    3. Mitambo ya ____________ katika kijiji chetu imeharibika.
    4. Kaka alinitumia __________________ kunijulisha kuhusu gari jipya 
    alilonunua.

    17.3 Matumizi ya lugha: Majadiliano
    Katika makundi ya wanafunzi watatu watatu, tazameni mchoro na picha
    zifuatazo kisha mwelezane kinachoendelea kwa kurejelea:
    i) Vifaa vya mawasiliano unavyoviona;
    ii) Matumizi ya kila kifaa cha mawasiliano unachokiona;
    iii) Umuhimu wa kila kifaa cha mawasiliano unachokiona;
    iv) Kasoro au udhaifu wa kila kifaa cha mawasiliano unachokiona.
    

    Maelezo muhimu!
    Kifaa cha kutuma taarifa kwa njia ya kielektroniki kwa kutumia simu
    huitwa faksi. Taarifa inayotumwa pia huitwa faksi. Huhusisha matumizi
    ya umeme. Faksi ni aina ya barua au ujumbe unaotumwa kwa njia ya
    mashine inayoitwa faksi. Maelezo machache yanayofafanua ujumbe
    pekee hutumika.


    17.4 Kusikiliza na kuzungumza: Maigizo
    Katika makundi ya wanafunzi wanne wanne, igizeni mazungumzo mliyosoma
    hapo juu kati ya Baba na Mama.

    17.5 Sarufi

    Hali ya kuomba, tungo yakinishi

    A. Katika makundi ya wanafunzi watatu watatu, chunguzeni sentensi zinazofuata
    kisha mwelezane ugunduzi wenu na baadaye mjibu zoezi l7.3 linalofuata.

    1. Tafadhali nipigie simu unapofika nyumbani.
    2. Tafadhali imba wimbo wa taifa.
    3. Tafadhali cheza mpira wa miguu.
    4. Tafadhali pikeni mihogo kwa kuku.
    5. Tafadhali zungumza lugha ya Kiswahili sanifu pekee.

    B. Badilisheni sentensi mlizosoma hapo juu kwa kutumia ‘naomba’.

    Maelezo muhimu!

    Msamiati wa adabu ambao hutumika kuomba mtu akutendee hisani

    fulani ni kama vile: tafadhali, naomba, n.k.

    Zoezi la 17.3

    Katika makundi ya wanafunzi watatu watatu, tungeni sentensi tano sahihi

    katika hali ya kuomba, wakati uliopo.

    SOMO LA 18: Matumizi ya tarakilishi

    18.1 Kifungu kuhusu matumizi ya tarakilishi

    Katika makundi ya wanafunzi watatu watatu, jadilini kuhusu mnachokiona
    katika mchoro na picha ifuatayo na mwelezane maana na matumizi yake.
    Baada ya hapo, msome kifungu cha habari kilicho hapo chini na mjibu maswali

    yanayofuata.


    Maswali ya ufahamu
    1. Taja faida zozote mbili za mradi wa tarakilishi kwa wanafunzi.
    2. Taja faida zozote mbili za tarakilishi kwa watu kwa ujumla.
    3. Jina jingine la tarakilishi ni lipi?
    4. Mtandao hufanya ulimwengu kuwa kama kijiji kimoja. Kweli au la? Kivipi?
    Eleza.
    5. Jadili upungufu mkubwa wa watisapu kulingana na kifungu ulichosoma.
    6. Pendekeza anwani nyingine mwafaka kwa taarifa hii.
    7. Je, teknolojia ina manufaa gani kwa nchi? Taja manufaa matano.
    8. Eleza madhara yanayoweza kusababishwa na tarakilishi.
    9. Matumizi ya tarakilishi yanawezesha vipi utangamano wa wanajamii
    mbalimbali?
    10. Jadili matumizi, umuhimu na madhara ya:

    a) Fesibuku                             b) Watisapu            ch) Barua pepe

    18.2 Msamiati kuhusu matumizi ya tarakilishi

    Jipangeni katika makundi ya wanafunzi watatu watatu kisha mtafute maana
    ya msamiati mpya katika kifungu mlichosoma hapo awali. Tafuteni maana ya
    msamiati huo kulingana na matumizi yake katika kifungu hicho. Tumieni kamusi

    pale inapohitajika. 

    Zoezi la 18.1
    Katika makundi ya wanafunzi watatu watatu, chunguzeni sentensi hizi kisha
    mtunge sentensi zenu kwa kutumia maneno yaliyopigiwa mistari.

    1. Teknolojia imeufanya ulimwengu kuwa kama kijiji kidogo.
    2. Tarakilishi ina manufaa mengi kwa binadamu.
    3. Mtandao humwezesha mtafiti kupata taarifa nyingi.
    4. Mradi wa tarakilishi kwa kila mwanafunzi utafaulu.
    5. Mimi huisoma kamusi ya Kiswahili kwenye tarakilishi.
    6. Tunaweza kuzifahamu tamaduni za jamii jirani kupitia kwa mtandao.
    7. Wanajamii mbalimbali hutangamana kupitia kwa mtandao.
    8. Akaunti yangu ya fesibuku imefungwa.
    9. Watisapu yangu imejaa picha tele za harusi ya kaka yangu.
    10. Nimeipata barua pepe aliyonitumia Kamana. 

    18.3 Matumizi ya lugha: Majadiliano
    Katika makundi ya wanafunzi wanne wanne, tazameni picha hizi kisha mzijadili

    na kuziambatanisha na sentensi zilizo hapo chini kwa usahihi. 


    1. Barua pepe ya rais wa Marekani ina jumbe nyingi sana.
    2. Watisapu yangu ina jumbe nyingi sana.
    3. Barua pepe niliyomtumia mwalimu mkuu haijajibiwa.
    4. Ninataka kufungua akaunti yangu ya fesibuku. 

    Zoezi la makundi 

    Katika makundi ya wanafunzi wanne wanne, jadilini kuhusu umuhimu wa
    tarakilishi kwa kuwaeleza wenzako:
    1. Maana ya tarakilishi.
    2. Njia za mawasiliano kupitia tarakilishi unazozifahamu.
    3. Faida za tarakilishi kwa watumizi.

    4. Madhara ya tarakilishi kwa watumizi.

    18.4 Kusikiliza na kuzungumza: Majadiliano

    Katika makundi ya wanafunzi watatu watatu, someni tena kifungu kuhusu
    matumizi ya tarakilishi kisha mjadili kuhusu:
    1. Faida za mradi wa tarakilishi kwa kila mtoto nchini Rwanda.
    2. Kasoro za mradi wa tarakilishi kwa kila mtoto.
    3. Mapendekezo yako kuhusiana na namna ya kuuboresha mradi huu.
    4. Nchi nyingine ambazo zimewahi kutekeleza mradi huu wa tarakilishi kwa
    kila mtoto.
    5. Madhara na umuhimu wa kutumia:
    a) Fesibuku
    b) Barua pepe

    ch) Watisapu

    18.5 Sarufi
    Hali ya kuomba, tungo kanushi
    A. Katika makundi ya wanafunzi wanne wanne, chunguzeni sentensi zinazofuata
    kisha mwelezane ugunduzi wenu.
    1. Naomba uitoe simu hiyo kwenye chaji.
    2. Tafadhali iwashe tarakilishi hiyo.
    3. Tafadhali nunua mfuko wa kubebea tarakilishi yako.
    4. Tafadhali naomba uniazime kitabu chako.

    5. Naomba uniletee kalamu hiyo

    B. Katika makundi yenu, chunguzeni sentensi zinazofuata kisha mwelezane
    ugunduzi wenu.

    1. Naomba usiitoe simu hiyo kwenye chaji.
    2. Tafadhali usiiwashe tarakilishi hiyo.
    3. Tafadhali usinunue mfuko wa kubebea tarakilishi yako.
    4. Tafadhali usiniazime kitabu chako.
    5. Naomba usiniletee kalamu hiyo.
    5. Naomba usiniletee kalamu hiyo.

    Je, mmegundua nini?

    Maelezo muhimu!

    Tarakilishi  i ni chombo cha mawasiliano mbacho hufanana na runinga

    na hutuia iteaneti. Tarikiishi huhifadhi na kuchanganua taarifa

    zilizongizwa pamoja na kuongoza mitambo mbalimbali.


    Zoezi la 18.2


    Katika makundi ya wanafunzi watatu watatu, tungeni sentensi sahihi kwa
    kutumia msamiati wa teknolojia ufuatao katika hali ya kuomba, tungo kanushi.
    Kwa mfano:                    Tafadhali usiharibu tarakilishi ya baba.
    1. Mtandao
    2. Simu ya mkono
    3. Intaneti
    4. Kompyuta
    5. Televisheni
    6. Fesibuku
    7. Watisapu
    8. Baruapepe

    Zoezi la 18.3
    Katika makundi ya wanafunzi watatu watatu, badilisheni sentensi zifuatazo
    kutoka katika hali ya kuomba yakinishi hadi katika hali ya kuomba kanushi.
    Kwa mfano: Naomba unipigie simu usiku.
    Jibu:        Naomba usinipigie simu usiku.
    1. Tafadhali nunua televisheni nyingine.
    2. Naomba unitengenezee simu yangu.
    3. Naomba uninunulie bandali za intaneti.
    4. Tafadhali mtoto huyo atumie tarakilishi yangu.

    5. Naomba uniandikie baruapepe kesho asubuhi.

    SOMO LA 19: Redio na runinga

    19.1 Kifungu kuhusu matumizi ya redio na runinga

    Katika makundi ya wanafunzi watatu watatu, chunguzeni mchoro na picha
    zifuatazo kisha mjadili kuihusu. Baadaye, msome kifungu kilicho hapo chini

    kuhusu matumizi ya redio na runinga na mjibu maswali yanayofuata.




     

    Maswali ya ufahamu
    1. Eleza umuhimu wa redio na runinga kwa binadamu.
    2. Redio na runinga hufundisha lugha na fasihi kwa njia gani?
    3. Taja mifano mitatu ya msamiati wa redio na runinga.
    4. Habari za kimataifa ni habari gani?
    5. Taja mifano ya matangazo katika redio na runinga.
    6. Ni kazi gani ya mtangazaji kulingana na kifungu ulichosoma?
    7. Eleza maana ya ‘msikilizaji’ na ‘mtazamaji’ kwa kurejelea kifungu
    ulichosoma.
    8. Taja vituo vya redio na runinga unavyovijua nchini mwako.
    9. Eleza madhara ya redio na runinga kwa binadamu.

    10. Eleza tofauti iliyopo kati ya redio na runinga.

    19.2 Msamiati kuhusu matumizi ya redio na runinga

    Kutokana na kifungu cha habari mlichosoma hapo awali, katika makundi ya
    wanafunzi watatu watatu, jadilini kuhusu maana ya msamiati mpya uliojitokeza
    na unaohusiana na matumizi ya redio na runinga. Kamusi ya Kiswahili inaweza

    kutumika panapohitajika.

    Kwa mfano:

    redio: chombo kinachopokea mawimbi ya sauti kutoka hewani ili mtu

    asikie habari, ujumbe au muziki unaochezwa kupitia kituo cha redio

    Zoezi la 19.1

    A. Jigaweni katika makundi ya wanafunzi watatu watatu kisha mchunguze
    maana ya msamiati uliopigiwa mstari katika sentensi hizi. Tumieni kamusi
    inapohitajika.
    1. Watu wengi wanapenda kutazama runinga.
    2. Baba anasikiliza habari za kisiasa kwenye redio Rwanda.
    3. Taarifa za habari zimepeperushwa hewani kwa wasikilizaji na
    watazamaji.
    4. Kaka yangu ni mtangazaji katika kituo cha runinga cha Rwanda.
    5. Mawimbi ya sauti katika redio yetu yanasikika vizuri.
    6. Matangazo ya biashara yameshakamilika.
    7. Hawa ni watazamaji wa filamu ya watoto kwenye runinga.
    8. Mkuu wa redio katika kituo chao ametuzwa.
    9. Mimi ninapenda kutazama vipindi mbalimbali kwenye runinga.
    B. Katika makundi yenu, tungeni sentensi sahihi kwa kutumia maneno

    yaliyopigiwa mistari katika sentensi za Zoezi la kwanza A.

    19.3 Matumizi ya lugha: Majadiliano
    Jigaweni katika makundi ya wanafunzi watano watano kisha mjadili kuhusu

    matumizi ya redio na runinga kwa kuwaeleza wenzako:

    1. Vipindi ambavyo unapenda kutazama kwenye runinga.
    2. Vipindi ambavyo unapenda kusikiliza kwenye redio.
    3. Mafunzo unayoyapata kutokana na vipindi unavyopenda kutazama na
    kusikiliza.
    4. Watangazaji unaowapenda kwenye runinga na sababu za kuwapenda.
    5. Watangazaji unaowapenda kwenye redio na sababu za kuwapenda.

     619.4 Kusikiliza na kuzungumza: Maigizo

    Katika makundi ya wanafunzi watano watano, igizeni namna ya kutangaza

    habari au vipindi mbalimbali kwenye runinga na redio. Mzingatie lugha ya

    Kiswahili sanifu.

    19.5 Sarufi: Hali ya kuamrisha, tungo yakinishi

    Katika makundi ya wanafunzi watatu watatu, chunguzeni sentensi zinazofuata

    kwa kuzisoma kwa sauti kisha mwelezane ugunduzi wenu.

    1. Imba wimbo wa taifa.

    2. Cheza mpira wa miguu.

    3. Nenda usome kitabu hiki.

    4. Pika muhogo kwa kuku.

    5. Zungumza Kiswahili sanifu pekee.

    Je, mmegundua nini?. Madhara ya redio na runinga kwa binadamu.

    19.4 Kusikiliza na kuzungumza: Maigizo

    Katika makundi ya wanafunzi watano watano, igizeni namna ya kutangaza
    habari au vipindi mbalimbali kwenye runinga na redio. Mzingatie lugha ya
    Kiswahili sanifu.
    19.5 Sarufi: Hali ya kuamrisha, tungo yakinishi

    Katika makundi ya wanafunzi watatu watatu, chunguzeni sentensi zinazofuata
    kwa kuzisoma kwa sauti kisha mwelezane ugunduzi wenu.

    1. Imba wimbo wa taifa.
    2. Cheza mpira wa miguu.
    3. Nenda usome kitabu hiki.
    4. Pika muhogo kwa kuku.

    5. Zungumza Kiswahili sanifu pekee.

    Je, mmegundua nini?

    Maelezo muhimu!

    Kitendo cha kutoa maagizo ya kufanyika kwa tendo fulani huitwa
    kuamrisha.
    Kwa mfano:
    1. Nenda ukalale!
    Katika sentensi hii, kuna agizo la mzungumziwa kwenda kulala.
    2. Njoo hapa!
    Katika sentensi hii, kuna agizo la mzungumziwa kwenda aliko

    mzungumzaji.

    Zoezi la 19.3

    Tungeni sentensi sahihi kwa kutumia maneno yafuatayo kwa njia ya kuamrisha
    katika hali yakinishi.

    Kwa mfano: washa (televisheni)
    Jibu:                Nenda uiwashe televisheni ile.
    1. Andika (baruapepe)
    2. Tengeneza (tarakilishi)
    3. Jibu (simu)
    4. Tuma (arafa)
    5. Fundisha (teknolojia)
    6. Sikiliza (redio)
    7. Tazama (runinga)
    8. Soma (fesibuku)
    9. Fungua (watisapu)
    10. Nunua (gazeti)

    SOMO LA 20: Barua kwa mhariri

    20.1 Kifungu kuhusu barua kwa mhariri

    Katika makundi ya wanafunzi watatu watatu, tazameni mchoro na picha
    zifuatazo kisha mwelezane mnachokiona. Baadaye, msome kifungu kilicho hapo
    chini na mjibu maswali yanayofuata.