Main content blocks
Section outline
-
MADA KUU 1: LUGHA NA MAZINGIRA
MADA NDOGO: Utalii nchini Rwanda
1.1 Mazungumzo kati ya Mpokeaji na Mtalii
Katika makundi ya wanafunzi watatu watatu, tungeni sentensi sahihi kwakueleza kinachoendelea au mnachokiona katika mchoro huu.
Maswali ya ufahamu
Katika makundi ya wanafunzi watatu watatu, someni tena kifungu cha mazungumzo
kilicho hapo juu kati ya Mtalii na Mpokeaji, kisha mjibu maswali haya.
1. Mtalii anatoka katika nchi gani? Yeye anataka nini?
2. Taja vivutio vya utalii vilivyopo nchini Rwanda.
3. Mtalii atatembelea vivutio gani?
4. Mtalii atachukua muda gani nchini Rwanda?
5. Umuhimu wa mwelekezaji wa watalii ni upi?
6. Watu huruhusiwa kuingia katika mbuga za wanyama kuanzia saa ngapi
na hutoka saa ngapi?
7. Mtalii atatumia nambari za simu alizopewa kufanya nini?
8. Mtalii ataanza shughuli yake ya kuzuru maeneo mbalimbali lini?
9. Mtalii atatumia nini kusafiri hadi kwenye mbuga za wanyama?10. Huduma za hoteli kwa Mtalii ni zipi?
1.2 Msamiati kuhusu utalii
Katika makundi ya wanafunzi watatu watatu, tafuteni msamiati mpya katika
kifungu cha mazungumzo mlichosoma hapo juu kisha muutolee maelezo.
Zingatieni matumizi ya msamiati huo katika kifungu hicho na mtumie kamusipale panapohitajika.
Kwa mfano:
mbuga – sehemu maalum ya kuwahifadhia wanyamapori
Zoezi la 1.1
A. Katika makundi ya wanafunzi watatu watatu, elezeni maana ya msamiati
uliopigiwa mistari katika sentensi hizi kisha mtunge sentensi zenu sahihi
kwa kutumia msamiati huo.
1. Mtalii huyu kutoka nchi ya Ujerumani anataka kujua maeneo
mazuri ya kuzuru nchini.
2. Maeneo mengi ya nchi yetu yanavutia watalii wengi.
3. Mtalii huyu anataka kuzuru wilaya ya Korongi ili aweze kutazama
ziwa Kivu.
4. Simba wengi waliletwa katika mbuga ya wanyama ya Akagera.
5. Mbuga ya Wanyama ya Akagera ni kivutio muhimu cha utaliinchini Rwanda.
6. Mtalii huyu aliamua kufanya ziara ya kitalii ya siku tano nchini
mwetu.
7. Nchi yetu inatarajia kupokea watalii elfu themanini na watano
mwaka huu.
8. Mimi ninaona heri niondoke katika sehemu hii; sitaki wanyama
wakali wanipate hapa.
9. Unaweza kufanya ziara yako ya kitalii mjini Kigali kwa bei nafuu.10. Watalii hufurahia mazingira ya Akagera.
B. Katika makundi ya wanafunzi watatu watatu, tungeni sentensi sahihi kwakutumia maneno yaliyopigiwa mistari katika Zoezi la 1A
1.3 Matumizi ya lugha: Aina mbalimbali za pesa
Katika makundi ya wanafunzi watatu watatu, tazameni pesa zifuatazo kishamziambatanishe kwa usahihi na nchi zinakotumika.
Zoezi la 1.2
Katika makundi ya wanafunzi wawili wawili, ambatanisheni aina za pesazilizo katika sehemu A na nchi zinakotumika katika sehemu B kwa usahihi.
Kwa mfano: Faranga - Rwanda
Zoezi la 1.3
Katika makundi ya wanafunzi wawili wawili, onyesheni aina za pesa ambazohutumiwa katika nchi zifuatazo kwa kutunga sentensi sahihi.
Kwa mfano: Tanzania
Zoezi la utafiti
Katika makundi ya wanafunzi wawili wawili, badilisheni pesa za kigeni zifuatazo
ziwe katika faranga za Rwanda kama ilivyo sasa hivi.
Kwa mfano:
Shilingi elfu moja za Kenya = Faranga elfu saba na mia tano za Rwanda1. Dola hamsini za Marekani
2. Shilingi mia mbili za Uganda
3. Shilingi hamsini za Tanzania
4. Yuro tano za Ulaya
5. Naira mia moja za Naijeria1.4 Kusikiliza na kuzungumza: MaigizoKatika makundi ya wanafunzi wawili wawili, igizeni mazungumzo mliyosoma
hapo awali kati ya Mtalii na Mpokeaji.1.5 Sarufi: Viulizi ‘nani’ na ‘nini’
Katika makundi ya wanafunzi wawili wawili, someni sentensi zifuatazo kishamfanye mazoezi yanayofuata.
1. Nani atamaliza wiki mbili nchini Rwanda?
Jibu: Mtalii.
2. Nini kinavutia katika mbuga ya Akagera?
Jibu: Wanyamapori kwa mfano: simba.
3. Nani alimpa mtalii maelezo kuhusu hoteli ya kuishi?
Jibu: Mpokeaji wa watalii.
4. Nani atarudi mwaka ujao kwa shughuli za utalii?
Jibu: Mtalii.
5. Ni nini mtalii atalipa ili kuzuru mbuga ya wanyama?
Jibu: Pesa za kiingilio
Zoezi la 1.4
Katika makundi ya wanafunzi wawili wawili, ulizeni maswali mliyosoma hapo
juu kwa kuanza na kiulizi ‘je’.
Kwa mfano:
Je, ni nani atamaliza wiki mbili nchini Rwanda?
Zoezi la 1.5
Katika makundi ya wanafunzi wawili wawili, jazeni nafasi zilizoachwa wazi
katika sentensi hizi kwa jibu sahihi kutoka kwenye mabano.
Maelezo muhimu!
Maneno yaliyopigiwa mistari huitwa viulizi. Haya ni maneno
ambayo hutumiwa kuulizia maswali.
Kwa mfano:
i) Nani alikulipia karo ya muhula uliopita?
Neno ‘nani’ linauliza kuhusu mtu aliyetenda kitendo cha kulipa
karo.
ii) Nini kimekuhuzunisha?
Neno ‘nini’ linauliza kuhusu kitu au jambo ambalo limemhuzunisha
anayehusika.
• Maneno ‘nani’ na ‘nini’ hayaongezewi viambishi ngeli vyovyote.
Zoezi la 1.6
Tunga sentensi tano sahihi kwa kutumia kiulizi ‘nani’ na sentensi nyinginetano sahihi kwa kutumia kiulizi ‘nini’.
Somo la 2 : Mbuga za wanyama
2.1 Kifungu kuhusu mbuga za wanyama nchini RwandaKatika makundi ya wanafunzi wawili wawili, jadilini kuhusu mnachokiona
katika picha hizi kisha, mjitokeze mbele ya wanafunzi wenzenu ili muwaeleze.
Baadaye, msome kifungu kinachofuata cha habari kuhusu mbuga za wanyama
zinazopatikana nchini Rwanda.Maswali ya ufahamuKatika makundi ya wanafunzi wawili wawili, someni tena kifungu cha habari
kuhusu mbuga za wanyama kisha mjibu maswali yafuatayo.
1. Nchi ya Rwanda inapatikana wapi?
2. Je, ni vivutio gani vya utalii vinavyopatikana nchini Rwanda?
3. Mbuga ya wanyama ya Akagera inahifadhi wanyama gani?
4. Eleza sifa za mbuga ya Akagera.
5. Mbuga ya wanyama ya milima mirefu inapatikana katika sehemu gani?
Taja milima mirefu minne inayopatikana hapo.
6. Mbuga hii inasifiwa kwa sababu ya kuwa na wanyama gani? Kwa nini
wanyama hao wanapendwa sana na watalii?
7. Je, ni sherehe gani inayofanywa kila mwaka kuhusiana na wanyama hao?
8. Mbuga ya wanyama ya msitu wa Nyungwe inajulikana kwa sifa gani?
9. Je, ni faida gani tunazopata kutokana na shughuli ya utalii?
10. Ni mambo gani yanayostahili kukomeshwa ili utalii uweze kuendelea na
kustawi?2.2 Msamiati kuhusu mbuga za wanyamaKatika makundi ya wanafunzi wawili wawili, tafuteni msamiati mpya katika
kifungu cha habari mlichosoma kisha mueleze maana ya msamiati huo.
Zingatieni matumizi ya msamiati huo katika kifungu hicho na mtumie kamusi
pale panapohitajika.Kwa mfano:msitu – eneo kubwa lisilokuwa na watu lenye mimea mingiZoezi la 2.1Katika makundi ya wanafunzi wawili wawili, husisheni kwa usahihi maneno
yaliyoandikwa katika sehemu A na maelezo yake katika sehemu B. Zingatieni
mfano uliotolewa.Zoezi la 2.2Katika makundi ya wanafunzi wawili wawili, husisheni kwa usahihi sentensi
zilizo hapo chini na picha zifuatazo.1. Mlima huu ni mrefu kuliko milima mingine nchini Rwanda.
2. Mnyama huyu ana pembe ndefu.
3. Ziwa hili lina kisiwa kimoja kilicho na vibanda vingi.
4. Pundamilia na nyati huishi katika msitu huu.
5. Ziwa hili lina samaki wengi.2.3 Matumizi ya lugha: MajadilianoKatika makundi ya wanafunzi watatu watatu, jaribuni kujadiliana kuhusu
sifa za vivutio vya utalii mlivyojadili katika kifungu cha habari mlichosoma
hapo awali. Tajeni vivutio ambavyo mngependa kutembelea huku mkitoa
sababu za chaguo lenu.2.3.1 Kuandika ufupisho/ MuhtasariKatika makundi ya wanafunzi watatu watatu, elezeni mambo muhimu
yaliyozungumziwa katika kifungu cha habari mlichosoma. Msinakili sentensi
zilizotumiwa katika kifungu hicho, jaribuni kutumia maneno yenu na kuunda
sentensi zenu zilizofupishwa. Tumieni maneno yasiyozidi mia moja (100).Maelezo muhimuKabla ya kuandika ufupisho wenu ni vyema:1. Kusoma kwa makini kifungu kilichopo na kuandika mawazo muhimu.
Soma mara tatu ili kuelewa vizuri.
2. Kujibu maswali haya:
• Kifungu cha habari kinahusu nini? (Andika sentensi moja)
• Kifungu hiki kina aya ngapi? (Tambua aya zinazojenga kifungu hiki).
• Andikeni wazo moja kutoka kwa kila aya.
3. Kuunganisha mawazo mliyoorodhesha na kuandika habari kamili. Ili
mwandike vizuri ni vyema:
• Kutumia maneno yenu wenyewe (msitumie maneno pamoja na sentensi
zilizotumiwa katika kifungu cha habari mlichokisoma)
• Kutoa maelezo bila kupotosha ujumbe asilia.
• Kuhakikisha kuwa mmerejelea mawazo yote muhimu yanayopatikana
katika kifungu cha habari mlichokisoma.
• Kuhakikisha kuwa hakuna makosa ya kisarufi.
• Kuhakikisha kwamba mmezingatia urefu unaofaa.
• Kuzingatia matumizi ya alama za uandishi.
Habari hiyo mliyoandika kwa kuzingatia maelekezo hayo hapo juu ni
muhtasari au ufupisho wa habari asilia mliyosoma. Neno ‘ufupisho’
linatokana na kitenzi ‘fupisha’ lenye maana ya ‘kufanya maelezo kuwa
mafupi au kupunguza urefu wake’.Mfano wa ufupisho wa kifungu kuhusu mbuga za
wanyama
Rwanda ni nchi iliyo na vivutio vingi vya kitalii kama vile: mito
mbalimbali, mbuga za wanyama, misitu ya kiasili, hoteli nzuri, maziwa,
milima mirefu pamoja na nyumba za kuhifadhia vifaa vya utamaduni wetu.
Mbuga ya wanyama ya Akagera inapendwa na watu wengi. Mbuga hii ina
wanyama kama vile: pundamilia, swara, paa, twiga, vifaru, tembo, simba
pamoja na wanyama wengine. Pia, mbuga hii ina savana ya kupendeza.
Mbuga ya wanyama ya milima mirefu ya Virunga huvutia kwa milima yake
mirefu kama vile: Kalisimbi, Muhabura, Bisoke, Sabyinyo, Nyamuragira na
Nyiragongo. Mbuga hii pia inajulikana kwa wanyama wanaoitwa ‘sokwe
watu’.
Mbuga ya msitu wa Nyungwe inafahamika kwa miti yake mirefu sana
pamoja na ndege wa aina nyingi wasiopatikana kwingi ulimwenguni. Vivutio
hivi vina manufaa mengi ya kiuchumi kwa Wanyarwanda. Ni lengo la kila
Mnyarwanda kuhakikisha kuwa anatunza vivutio hivi ili utalii uendelee
kutufaidi. (Maneno 140 )
2.4 Kusikiliza na kuzungumza: Majadiliano
Katika makundi ya wanafunzi wawili wawili, jadilini kuhusu mbuga za wanyama
zinazopatikana nchini Rwanda na kuyaandika maelezo yenu kwa ufupi halafu
mjitokeze mbele ya wanafunzi wenzenu na kuwasomea kuhusu mbuga hizopamoja na sifa zao.
2.5 Sarufi: Kiulizi ‘lini’
Jigaweni katika makundi ya wanafunzi wawili wawili ili mchunguze sentensi
zifuatazo katika umoja na wingi kisha mfanye zoezi linalofuata.
Zoezi la 2.3
Katika makundi ya wanafunzi wawili wawili:
1. Jadilini aina ya neno lililopigiwa mstari katika sentensi mlizopewa.
2. Jadilini mabadiliko ya sentensi hizo yanayojitokeza katika umoja na wingi.
3. Tungeni sentensi tano sahihi kwa kutumia neno lililopigiwa mstari.
Zoezi la 2.4
Katika makundi yenu ya wanafunzi wawili wawili, jazeni nafasi zilizo wazikatika sentensi hizi kwa jibu sahihi kutoka kwenye mabano.
Maelezo muhimu!
Neno ‘lini’ ni kiulizi cha wakati. Hutumika katika sentensi kuuliziawakati wa kutendeka kwa kitendo fulani.
Kwa mfano: Utasafisha chumba cha mgonjwa lini?
Jibu: Kesho jioni.
Jibu linalotolewa kwa sentensi iliyo na neno ‘lini’ linaonyesha majira
mbalimbali ya wakati kama vile: majira ya siku (asubuhi, usiku, alasiri,
mchana, jioni), saa, siku, wiki, mwezi, mwaka miongoni mwa nyakatinyingine.
Zoezi la 2.5
Katika makundi ya wanafunzi watatu watatu, andikeni sentensi hizi upyakatika hali ya kuuliza kwa kufuata maagizo yaliyo kwenye mabano.
Kwa mfano: Mgeni ataondoka kesho jioni. (Tumia: lini)
Jibu: Mgeni ataondoka lini?
1. Mtalii alizuru mbuga ya wanyama. (Tumia: Nani)
2. Chakula hiki kitaliwa kesho. (Tumia: Nini)
3. Watalii kutoka Marekani watafika kesho asubuhi. (Tumia: lini)
4. Mwelekezaji atawapeleka watalii mjini Kigali. (Tumia: Nani)
5. Kisu kitanunuliwa sokoni. (Tumia: Nini)
Zoezi la 2.6
A. Tunga sentensi tano sahihi kwa kutumia kiulizi ‘lini’.B. Andika sentensi ulizotunga katika sehemu A katika umoja au wingi.
SOMO LA 3: Mwelekezaji na MtaliiSOMO LA 3: Mwelekezaji na Mtalii
3.1 Mazungumzo kati ya Mwelekezaji na MtaliiTazameni mchoro huu katika makundi ya wanafunzi watatu watatu kisha
mwelezane mnachokiona.
Maswali ya ufahamu
Katika makundi ya wanafunzi watatu watatu, someni tena kifungu cha
mazungumzo kati ya Mwelekezaji na Mtalii, kisha mjibu maswali haya.
1. Kwa nini wanyama hufurahia kuishi katika mazingira ya mbuga ya
Akagera?
2. Taja vitu vilivyomfurahisha mgeni wa kitalii.
3. Mgeni huyu alifika lini nchini Rwanda?
4. Mgeni huyu wa kitalii atarudi nchini kwao lini?
5. Ni wanyama gani wanaopatikana katika mbuga ya wanyama ya Akagera?
6. Ndovu mwenye umri mrefu kuliko wengine ana sifa gani?
7. Sungura hupenda nini?
8. Ili sungura wasitoroke mwelekezaji alifanya nini?
9. Ni wakati gani wanyama hujificha?10. Waharibifu wa mazingira hufanya nini?
3.2 Msamiati kuhusu ziara ya kitalii
Katika makundi ya wanafunzi watatu watatu, tafuteni msamiati mpya kutoka
katika kifungu cha mazungumzo mlichosoma hapo juu na kuueleza. Zingatieni
matumizi ya msamiati huo katika kifungu hicho na mtumie kamusi paleinapohitajika.
Zoezi la 3.1
Katika makundi ya wanafunzi wawili wawili, husisheni kwa usahihi msamiatikatika sehemu A na maelezo yake katika sehemu B. Zingatieni mfano uliopo.
Zoezi la 3.2
Katika makundi ya wanafunzi wawili wawili, husisheni kwa usahihi michorona picha hizi na sentensi zinazofuata.
1. Watalii wanawatazama wanyama katika mbuga ya Akagera.
2. Mtoto wa simba anaitwa shibli.
3. Msitu wa Virunga una miti mingi na sokwe wengi.
4. Walinzi wa mbuga za wanyama wamewashika wasasi waliokuwa
wakiwinda ndovu kwa ajili ya pembe zao.5. Wanafunzi walienda kuzuru mbuga ya Wanyama.
3.3 Matumizi ya lugha: Majadiliano
Katika makundi ya wanafunzi wawili wawili, jadilini kuhusu wanyamapori
ambao mmewahi kuwaona kwa kuelezana:
1. Majina ya wanyamapori hao.
2. Sifa za wanyamapori hao.
3. Chakula cha wanyamapori hao.
4. Maumbile ya wanyamapori hao.
5. Uliwaona wanyama hao wapi?6. Wanyamapori hao wanapenda kuishi katika mazingira ya aina gani?
A. Chunguza picha za wanyama hawa na kuzihusisha na majina yao sahihi
B. Katika makundi ya wanafunzi wawili wawili, onyesheni wanyama ambao
hufugwa na wanyamapori (wanyama wasiofugwa) kati ya wanyama waliohapo juu.
3.4 Kusikiliza na kuzungumza: Maigizo
Katika makundi ya wanafunzi wawili wawili, igizeni mazungumzo mliyosomakati ya Mwelekezaji na Mtalii wa kigeni.
3.5 Sarufi
Viulizi ‘wapi’ na ‘vipi’
Katika makundi ya wanafunzi wawili wawili, chunguzeni sentensi zifuatazo kisha
mjibu maswali haya.
Sentensi 1: Kila siku tunapokea watalii wengi kutoka Marekani.
Swali: Kila siku tunapokea watalii wengi kutoka wapi?
Sentensi 2: Mgeni alihudumiwa vizuri.
Swali: Mgeni alihudumiwa vipi?
Sentensi 3: Mgeni alifurahishwa na huduma ya hoteli.
Swali: Mgeni alifurahishwa na huduma ya wapi?
Sentensi 4: Ndovu alionekana mpole.
Swali: Ndovu alionekana vipi?Je, mmegundua nini?
Zoezi la 3.4
Katika makundi ya wanafunzi wawili wawili, tungeni sentensi tano kama hizo
zilizoandikwa hapo juu. Kutokana na sentensi utakazotunga, tunga maswaliyake kwa kutumia neno ‘wapi’
Maelezo muhimu!
Zoezi la 3.5
Tunga maswali kuhusu maneno yaliyopigiwa mstari katika sentensi hizi kwakutumia viulizi sahihi.
Kwa mfano:
1. Mwanafunzi huyu anasomea Uchina.Jibu: Mwanafunzi huyu anasomea wapi?
2.Mwanafunzi huyu anaandika vizuri
Jibu: Mwanafunzi huyu anaandika vipi?
1. Dereva huyu anatoka Afrika Kusini.
2. Sembare anaingia chumbani mwake haraka.
3. Gari la mtalii limesimama nje ya nyumba yetu.
4. Simba anajificha vichakani.5. Ndugu yangu anatembea polepole.
Zoezi la 3.6
Katika makundi ya wanafunzi wawili wawili, tungeni sentensi tano katikaumoja na wingi kwa kutumia viulizi ‘wapi’ na ‘vipi’
Zoezi la 3.7
Jaza nafasi zilizoachwa wazi kwa kutumia jibu sahihi kutoka kwa yaliyo
kwenye mabano.1. Kijana mmoja alienda _________ ? (nani, nini, wapi)
2. Waziri ataondoka _________ ? (nani, vipi, nini)
3. Mtumishi amepoteza ufagio wake ___________? (lini, nani, wapi)
4. Fundi hodari amejenga nyumba __________? (nani, vipi, nini)5. Mwalimu wetu ameenda __________? (nani, nini, wapi)
3.5.1 Kiulizi ‘kwa nini’
Katika makundi ya wanafunzi wawili wawili, chunguzeni sentensi zifuatazo.
Sentensi 1: Mtalii atatembelea mbuga ya wanyama ili kuwaona
wanyamapori.
Swali: Kwa nini mtalii atatembelea mbuga ya wanyama?
Sentensi 2: Mgeni alifurahi kwa sababu alipewa huduma nzuri.
Swali: Kwa nini mgeni alifurahi?
Zoezi la 3.8
1. Katika makundi ya wanafunzi wawili, tungeni sentensi mbili mbili kama
hizo zilizoandikwa hapo juu. (Sentensi 1 na 2)
2. Tunga maswali kwa sentensi mlizotunga katika swali la 1 hapo juu.
(Hakikisha kuwa mmetumia kwa nini katika maswali yenu).
Maelezo muhimu!
Maneno ‘kwa nini’ yanatumiwa kuulizia sababu ya kufanyika
kwa jambo fulani.
Kwa mfano:
Sentensi 1: Mwanafunzi huyu alipewa zawadi kwa sababu
anathamini mazingira yake.
• Swali: Kwa nini mwanafunzi huyu alipewa zawadi?
(Maneno ‘kwa nini’ yametumiwa kuulizia sababu ya kupewa zawadikwa mwanafunzi huyu).
• Sentensi 2: Waelekezaji walipewa mafundisho ili wajue namna
ya kuwapokea wageni.
• Swali: Kwa nini waelekezaji walipewa mafundisho?
(Maneno ‘kwa nini’ yametumiwa kuulizia sababu ya waelekezaji
kupewa mafundisho). Maneno ya kuulizia maswali huitwa viulizi.
Zoezi la 3.9
Katika makundi ya wanafunzi wawili wawili, ulizeni maswali kuhusu maneno
na vifungu vya maneno vilivyopigiwa mstari katika sentensi hizi.
Kwa mfano: Mtalii huyu hupenda kuja Rwanda kwa sababu Rwandani nchi nzuri.
Jibu: Kwa nini mtalii huyu hupenda kuja Rwanda
1. Mtoto huyu analia kwa sababu anataka chakula.
2. Mkulima huyu alichinja mbuzi mmoja kwa sababu ana wageni.
3. Mukandori anakaa katika nyumba hii kwa sababu alihamishwa kikazi.
4. Mtu huyu amepelekwa jela kwa sababu alihukumiwa kifungo cha miaka
miwili.
5. Mama na baba wamekaa sebuleni kwa sababu wanazungumza na
wageni wetu.
SOMO LA 4: Utamaduni na utalii
4.1 Kifungu kuhusu utamaduni na utalii
Katika makundi ya wanafunzi wawili wawili, chunguzeni picha hizi kisha mjadilikuhusu mnachokiona na kuwaelezea wenzenu.
Soma kifungu cha habari kinachofuata kuhusu utamaduni na utalii kisha mjibu
maswali yanayofuata. Kifungu hiki kinaeleza jinsi utamaduni unavyowezakutumiwa katika utalii na kuleta manufaa kwa nchi.
Maswali ya ufahamu
I. Katika makundi ya wanafunzi wawili wawili, someni tena kifungu cha
ufahamu kilichotangulia kisha mjibu maswali yafuatayo.
1. Kwa nini watu wengi hawaelewi umuhimu wa utamaduni?
2. Utamaduni unahusu nini?
3. Ni mambo gani yanayofanywa ili kuhifadhi utamaduni wetu?
4. Taja maeneo ambapo tunaweza kupata nyumba za kuhifadhia
utamaduni wetu?
5. Taja vitu tunavyoweza kupata katika nyumba ya kuhifadhi utamaduni
wetu iliyoko wilayani Huye.
6. Nyumba iliyoko wilayani Nyanza ilikuwa makazi ya nani?
7. Ni vitu gani vya kuvutia ambavyo tunaweza kukuta katika nyumba
hiyo?8. Kwa nini tunafaa kujivunia utamaduni wetu?
II. Katika makundi ya wanafunzi watatu watatu, andikeni kwa ufupi kifungucha habari mlichosoma hapo juu. Tumieni maneno sabini (70).
4.2 Msamiati kuhusu utamaduni
Katika makundi ya wanafunzi wawili wawili, tafuteni msamiati mpya kutoka
katika kifungu cha habari mlichosoma kilichotangulia na kuueleza. Zingatieni
matumizi ya msamiati huo katika kifungu hicho na mtumie kamusi palepanapohitajika.
Zoezi la 4.1
Katika makundi ya wanafunzi wawili wawili, husisheni maneno yaliyoandikwakatika sehemu A na maelezo yake katika sehemu B. Zingatieni mfano uliopo.
Zoezi la 4.2
Katika makundi ya wanafunzi wawili wawili,
husisheni mchoro na picha hizi na sentensi zifuatazo kwa usahihi.
1. Wageni hupokelewa katika sebule hii nzuri kwa mazungumzo.
2. Mama yangu huvaa taji la kitamaduni katika sherehe za harusi.
3. Babu anawasimulia wajukuu wake hadithi ya kusisimua.
4. Huu ni mtindo tofauti wa kukata nywele unaoitwa ‘Amasunzu’.5. Haya ni makazi yetu. Tuna nyumba nzuri ya kisasa.
4.3 Matumizi ya lugha: Zoezi la msamiati
Katika makundi ya wanafunzi wawili wawili, jazeni herufi zilizoachwa wazikatika visanduku vifuatavyo ili kuunda neno kamili.
4.4 Kusikiliza na kuzungumza: Majadiliano
Katika makundi ya wanafunzi watatu watatu, jadilini kuhusu utamaduni na
utalii halafu mjitokezee mbele ya wanafunzi wenzenu kuwaeleza kuhusu yale
mliyoafikiana. Jaribuni kuhakikisha kwamba mmejibu maswali haya katika
majadiliano yenu:
1. Utamaduni unahusu nini?
2. Utamaduni wa Wanyarwanda unatambulishwa na nini?
3. Utamaduni unaweza kuvutia watalii?
4. Ni faida gani tunaweza kupata kutokana na utamaduni?
5. Tunaweza kufanya nini ili kuhifadhi utamaduni wetu?6. Ni hasara gani tunaweza kupata iwapo hatutathamini utamaduni wetu?
4.5 Sarufi: Wakati wa mazoea, tungo yakinishi
Katika makundi ya wanafunzi wawili wawili, someni sentensi zinazofuata katikaumoja na wingi kisha mfanye zoezi lililo hapo chini.
Zoezi la 4.3
1. Katika makundi ya wanafunzi wawili wawili, tungeni sentensi moja moja
kwa kutumia neno kila siku na kitenzi pika katika nafsi zifuatazo: mimi,
wewe, yeye, sisi, nyinyi na wao.
2. Linganisheni sentensi zenu na zile ulizotolewa hapo juu kuhusu kitenzienda, chota na cheza.
Maelezo muhimu!
• Sehemu za kitenzi enda, chota na cheza zinaandikwa baada ya
kutumia hu.
• ‘hu’ inarudiwarudiwa katika vitenzi vyote baada ya nafsi mimi,
wewe, yeye sisi, nyinyi na wao.
• ‘hu’ inatumiwa kuonyesha kitendo kinachofanywa mara kwa mara,
kila wakati.
Kwa mfano: Mimi huchota maji kila asubuhi. (Kitendo cha kuchota
maji kinafanywa kila asubuhi)
• Kitenzi chota kimetumiwa katika wakati wa mazoea ili
kuonyesha kuwa kitendo hicho kinafanywa kila asubuhi.Zoezi la 4.4
Katika makundi ya wanafunzi wawili wawili, andikeni sentensi zifuatazo kwa
kutumia wakati wa mazoea.
Kwa mfano: Wachezaji hawa wanapenda kucheza kila jioni.
Jibu: Wachezaji hawa hupenda kucheza kila jioni.
1. Wagonjwa hawa wanapelekwa hospitalini kwa magari haya.
2. Waimbaji hawa wanapata fedha nyingi kila wiki.
3. Wageni wetu watafika kwenye uwanja wa ndege kabla ya saa kumi.
4. Mimi nitatembea kwa miguu hadi kanisani.
5. Mwalimu wetu ataondoka saa kumi na moja.
Zoezi la 4.5
Katika makundi ya wanafunzi wawili wawili, andikeni majibu ya sentensi
za Zoezi la 4.4 (lililo hapo juu) katika umoja au wingi.
Kwa mfano: Wachezaji hawa hupenda kucheza kila jioni.
Jibu: Mchezaji huyu hupenda kucheza kila jioni.
SOMO LA 5: Milima yetu
5.1 Kifungu kuhusu ‘Milima yetu’
Katika makundi ya wanafunzi wawili wawili, tazameni picha zifuatazo kisha
mjadili kuhusu kile kinachoendelea au mnachokiona katika picha hizi kwakujitokeza mbele ya wanafunzi wenzenu na kuwaelezea.
Katika makundi ya wanafunzi wawili wawili, someni kifungu cha habari
kinachofuata kuhusu ‘Milima yetu’ kisha mjibu maswali yanayofuata. Kifungu
hiki kinaelezea milima mbalimbali inayopatikana nchini Rwanda na mazingirayake mazuri yanayovutia sana.
Maswali ya ufahamu
I. Katika makundi ya wanafunzi wawili wawili, someni tena kifungu cha habari
kilichotangulia, kisha mjibu maswali haya.
1. Kwa nini watu wengi huita Rwanda ‘nchi yenye milima elfu moja’?
2. Ni faida gani tunazopata kutokana na misitu yetu?
3. Taja misitu mikubwa iliyozungumziwa katika kifungu hiki cha habari.
4. Taja milima minne mirefu iliyozungumziwa katika habari hii.
5. Milima hiyo hupatikana katika sehemu gani ya nchi yetu?
6. Taja wilaya mbili na mlima mmoja mmoja unaopatikana katika kila
wilaya.
7. Ni kwa nini Mlima Kageyo unajulikana?
8. Mwamba wa Ndaba una sifa gani?
9. Serikali ya Rwanda huomba Wanyarwanda kufanya nini?
10. Ni funzo gani tunalopata kutoka kwa viongozi wetu?
II. Katika makundi ya wanafunzi watatu watatu, andikeni habari hii kwa ufupi.
Tumieni idadi ya maneno mia moja.5.2 Msamiati kuhusu ‘Milima yetu’
Katika makundi ya wanafunzi wawili wawili, tafuteni msamiati mpya kutoka
katika kifungu cha habari kilicho hapo juu na kuueleza. Zingatieni matumizi yamsamiati huo katika kifungu hicho na mtumie kamusi pale panapohitajika.
Zoezi la 5.1
Katika makundi ya wanafunzi wawili wawili, chunguzeni sentensi zifuatazo
kisha mtunge sentensi zenu kwa kutumia maneno yaliyopigiwa mistari.
1. Miongoni mwa viumbe wote, binadamu ndiye mwenye akili.
2. Mjini Kigali kuna magari mengi mno.
3. Hapa kuna mteremko mrefu, jihadhari usianguke.
4. Watu wengi wananunua rangi hii kwa sababu inavutia sana.
5. Mvua haijanyesha kwa muda mrefu; kuna ukame na wanyama wetu
wamekosa maji na chakula.
6. Mtu huyu alishikwa na polisi kwa sababu anaharibu mazingira kwa
kuchoma misitu.
7. Huwezi kulima hapa kwa sababu kuna mwamba mkubwa.8. Ni lazima kila mwananchi afanye kazi ili kupambana na umaskini.
Zoezi la 5.2
Katika makundi ya wanafunzi wawili wawili, husisheni mchoro na pichapamoja na sentensi ulizopewa hapo chini kwa usahihi.
1. Mlima huu ni mrefu sana kuliko milima mingine.
2. Watu hawa wanapanda miti.
3. Msitu huu una ndovu wengi.4. Mteremko wa maji katika eneo hili unavutia sana.
5.3 Matumizi ya lugha: Zoezi la jedwali
Katika makundi ya wanafunzi wawili wawili, jazeni nafasi zilizoachwa wazi kwakuzingatia maelezo yaliyo chini ya jedwali.
Kwenda kulia
1. Mtu anayetembelea mahali pa kuvutia kwa kujifurahisha
4. Aina ya silaha inayotumiwa kukata mti
5. Muda wa saa ishirini na nne
8. Kujinyosha kitandani ili kupata usingizi
10. Ndege jike anayefugwa
12. Kupata kiumbe kichanga baada ya kukomaa kwa mimba
14. Mimea mikubwa iliyopandwa shambani au kuota mwituni15. Sarafu ya Marekani
Kwenda chini
1. Mtu anayefanya kazi ya kulinda
2. Azuru mbuga za wanyama
3. Sehemu yenye pori, vichaka na nyasi au mwitu
6. Kuangalia upande kilipo kitu fulani au kuenda mahali fulani
7. Sehemu ya ardhi inayoinuka juu sana
9. Safari ya kuzuru mahali kwa sababu maalumu
11. Ukosefu wa maji
13. Mnyama wa porini anayefanana na mbuzi5.4 Kusikiliza na kuzungumza: Majadiliano
Katika makundi ya wanafunzi watatu watatu, jadilini kuhusu faida za utalii kwa
wananchi halafu mjitokeze mbele ya darasa ili muwaeleze wanafunzi wenzenu
kuhusu hoja mlizozipata. Katika majadiliano yenu, hakikisheni mmejibu maswalihaya:
1. Utalii ni nini?
2. Ni sehemu zipi za utalii zilizo nchini mwetu?
3. Ni watu gani wanaokuja kutalii nchini mwetu?
4. Nchi yetu ina faida gani kwa kupokea watalii wengi?5. Wananchi wanapata faida gani kutokana na utalii?
5.5 Sarufi: Wakati wa mazoea, tungo kanushi
Katika makundi ya wanafunzi wawili wawili, someni sentensi zinazofuata katikaumoja na wingi kisha mfanye zoezi lililo hapo chini.
Zoezi la 5.3
Katika makundi ya wanafunzi wawili wawili, tungeni sentensi moja moja kwa
kutumia wakati wa mazoea (tungo yakinishi na tungo kanushi). Tumia nafsizifuatazo: mimi, wewe, yeye, sisi, nyinyi na wao.
Maelezo muhimu!
Kiambishi ‘hu’ kinarudiwarudiwa katika nafsi zote za tungo yakinishi.
Kikanushi ‘ha’ hutumiwa katika vitenzi vinavyoisha kwa irabu ‘i’
badala ya irabu ‘a’ katika tungo kanushi.
Kwa mfano: Sisi hupanda miti. (tungo yakinishi)
Sisi hatupandi miti. (tungo kanushi)
Viambishi vya nafsi hutumiwa baada ya kikanushi ‘ha’ na hubadilikakulingana na nafsi au ngeli inayohusika.
Kwa mfano:
Zoezi la 5.4
Katika makundi ya wanafunzi wawili wawili, andikeni vitenzi vilivyo kwenyemabano kwa kutumia wakati wa mazoea, tungo yakinishi.
Kwa mfano: Mtoto huyu _____ (kuchelewa) kufika shuleni kila asubuhi.
Jibu: Mtoto huyu huchelewa kufika shuleni kila asubuhi.
1. Wewe ______________ (kuandika) barua ndefu.
2. Sisi ______________ (kusaidia) walemavu katika kijiji hiki.
3. Watalii hawa ____________ (kufurahia) mazingira ya milima mirefu.
4. Mkulima huyu ____________ (kupanda) miti katika mashamba yake.
5. Mti huu ______________ (kuzaa) matunda mengi kila mwaka.
Zoezi la 5.5
Katika makundi ya wanafunzi wawili wawili, andikeni sentensi za zoezi la 5.4lililotangulia katika tungo kanushi.
Kwa mfano:
Sentensi: Mtoto huyu huchelewa kufika shuleni kila asubuhi.Jibu: Mtoto huyu hachelewi kufika shuleni kila asubuhi.
Zoezi la 5.6
Katika makundi ya wanafunzi wawili wawili, kanusheni tungo hizi kwakuziandika katika umoja na wingi.
Kwa mfano: Kitabu changu hupendwa na watu wengi.
Jibu: Umoja: Kitabu changu hakipendwi na watu wengi.
Wingi: Vitabu vyetu havipendwi na watu wengi.
1. Mwanafunzi yule hujibu vizuri maswali ya mwalimu.
2. Mtalii hutembelea mbuga zetu za wanyama kila siku.
3. Ukucha huu hupakwa rangi nyeupe baada ya mwezi mmoja.
4. Ndege yule hulala kwenye mti huu.5. Kitanda chako hutumiwa na wageni wetu.
SOMO LA 6: Maji yetu6.1 Kifungu kuhusu ‘Maji yetu’
Katika makundi ya wanafunzi wawili wawili, someni kifungu cha habarikinachofuata ambacho kinahusu ‘Maji yetu’ kisha mjibu maswali yanayofuata.
Maswali ya ufahamu
I. Katika makundi ya wanafunzi wawili wawili, someni tena kifungu cha habari
kilichotangulia kisha mjibu maswali haya.1. Maji yana umuhimu gani kwa afya yetu?
2. Maji huweza kutumiwa katika shughuli gani?
3. Ni mambo gani yanayoweza kutokea iwapo tutakosa maji?
4. Kwa nini nchi ya Rwanda ina maji ya kutosha?
5. Taja maziwa matatu yapatikanayo nchini Rwanda na ueleze sehemu
yanakopatikana.
6. Taja mito iliyozungumziwa katika kifungu hiki.
7. Ni vituo gani vilivyojengwa ili kutuletea nguvu za umeme?
8. Rwanda inahesabiwa katika ukanda upi?
9. Ukanda huo unazihusisha nchi gani?10. Taja mambo mawili ambayo watalii huyafurahia.
II. Katika makundi ya wanafunzi wawili wawili, fupisheni kifungu cha habari
mlichosoma hapo awali. Tumieni idadi ya maneno mia moja pekee.
6.2 Msamiati kuhusu ‘Maji yetu’
Zoezi la 6.1
katika kifungu cha habari kilicho hapo juu na kuueleza. Zingatieni matumizi yamsamiati huo katika kifungu hicho na mtumie kamusi pale panapohitajika.
1. Mwalimu wetu anatimiza kazi yake kwa kutufundisha vizuri.
2. Mimi hufua nguo zangu kila Jumamosi kwa kutumia maji safi na
sabuni.
3. Ukosefu wa mboga katika chakula unaweza kusababisha magonjwa
mengi katika mwili wa binadamu.
4. Rwanda inataka kuongeza vituo vya kutengeneza nguvu za umeme
kwa kutumia mito yake.5. Rwanda hupata gesi nyingi kutoka Ziwa Kivu.
Zoezi la 6.2
Katika makundi ya wanafunzi wawili wawili, chagueni neno linalofaa kati ya
maneno yafuatayo kisha mjaze nafasi zilizo wazi katika sentensi hizi.
Mtalii, Mto, Mbuga ya wanyama, ziwa, mbinu, Kisiwa
Kwa mfano: Mwalimu anatumia ________ nzuri kufundisha somo la
Kiswahili.
Jibu: Mwalimu anatumia mbinu nzuri kufundisha somo la Kiswahili.
1. _______ cha Ijwi kinapatikana ziwani Kivu.
2. _______ huyu alilipa pesa nyingi ili aweze kuingia katika nyumba hii
ya kitalii.
3. __________ ya Akagera inatembelewa na wageni wengi kutoka nchi
mbalimbali.
4. Walimu wetu wanatarajia kwenda Karongi ili kufurahia mazingira ya
______ la Muhazi.5. Watalii wawili walienda kwa gari zuri kutazama _______ Mukungwa.
6.3 Matumizi ya lugha: Majadiliano
Zoezi la 6.3
Je, umewahi kutembelea ziwa lolote nchini Rwanda? Umewahi kufika kwenye
kisiwa chochote nchini Rwanda? Jadilini kuhusu ziara zenu katika makundi yawanafunzi wanne wanne huku mkielezeana:
(a) Mliwaona wanyama gani wa majini? (b) Mliona mito gani?
(ch) Mlipanda vyombo vipi vya majini? (d) Mlivua samaki?
Zoezi la 6.4
Mkiwa wawili wawili, husisheni kwa usahihi maneno yaliyoandikwa katikasehemu A na maelezo yake katika sehemu B.
\
Zoezi la 6.5
Katika makundi ya wanafunzi wawili wawili, husisheni picha hizi na sentensizinazofuata kwa usahihi.
1. Hiki ni kituo cha kutengeneza nguvu za umeme katika Mto Nyabarongo.
2. Ziwani kuna chombo cha kusafiria.
3. Watalii wanatembea kwenye mchanga karibu na bahari hii.4. Mamba amelala kwenye ufuo wa mto huu.
6.4 Kusikiliza na kuzungumza: Majadiliano
Zoezi la 6.6
Katika makundi ya wanafunzi wawili wawili, jadilini kuhusu faida za kiutalii
tunazopata kutokana na maji halafu mjitokeze mbele ya darasa ili kuwaelezea
wenzenu. Hakikisheni kuwa mnajibu maswali haya katika majadiliano yenu:
1. Ni vivutio vipi vya utalii vyenye mazingira ya maji?
2. Ni mambo gani ya kuvutia tunayopata katika vivutio hivyo?3. Vivutio hivyo vinatumiwa vipi kuleta faida kwa nchi yetu?
6.4.1 Zoezi la imla
Funga kitabu chako kisha katika daftari lako, andika kwa usahihi kifunguambacho mwalimu wako atakusomea
6.5 Sarufi: Kiulizi ‘-pi’
Katika makundi ya wanafunzi wawili wawili, chunguzeni maswali yafuatayokatika umoja na wingi kisha mwelezeane ugunduzi wenu.
Zoezi la 6.7
Katika makundi ya wanafunzi wawili wawili, tungeni sentensi tano katikaumoja na wingi kwa kutumia kiulizi “-pi” katika ngeli mbalimbali za Kiswahili.
Zoezi la 6.8
Katika makundi ya wanafunzi wawili wawili, kamilisheni sentensi zifuatazokwa kutumia kiulizi ‘-pi’ kwa usahihi.
Kwa mfano: Kiti ______ kitakaliwa na mtalii?
Jibu: Kiti kipi kitakaliwa na mtalii?
1. Mtoto ______ anaweza kupika uji?
2. Viatu _______ vilinunuliwa na wageni hawa?
3. Ng’ombe ________ walichinjwa sokoni jana?
4. Kikombe _______ kilijazwa chai?5. Ubao _______ ulitengenezwa wiki iliyopita?
Zoezi la 6.9
Andika sentensi za zoezi la 8 (la hapo awali) katika umoja au wingi.
Kwa mfano:
Sentensi: (Umoja) Kiti kipi kitakaliwa na mtalii?Jibu: (Wingi) Viti vipi vitakaliwa na watalii?
Maelezo muhimu!
Kiulizi ‘-pi’ hutumika kuulizia swali kwa kumtaka mtu achague kitu
kimoja au vitu fulani miongoni mwa vitu vingine vilivyopo.Kwa mfano:
Swali: Mwanafunzi yupi ni mwerevu?
Jibu: Mwanafunzi mwerevu ni Kamaliza.
Wanafunzi ni wengi lakini mzungumzaji anauliza swali ili ajue
mwanafunzi mwerevu miongoni mwa wanafunzi wengi.
Swali: Wanafunzi wapi/ wepi ni werevu?
Jibu: Wanafunzi werevu ni Kamaliza na Iradukunda.
Wanafunzi ni wengi lakini mzungumzaji anauliza swali ili ajue
wanafunzi werevu tu miongoni mwa wanafunzi wote waliopo.Kiulizi ‘-pi’ kinatumika kulingana na ngeli inayohusika.
Kwa mfano:Umoja Wingi Ngeli
Mtoto yupi analia? Watoto wapi/wepi wanalia? A-WA
Kitabu kipi kinasomwa? Vitabu vipi vinasomwa? KI-VI
Mlima upi umepandwa? Milima ipi imepandwa? U-I
Nyumba ipi itajengwa? Nyumba zipi zitajengwa? I-ZI
Ukuta upi umebomoka? Kuta zipi zimebomoka? U-ZI
Tathmini ya mada ya 1
Zoezi la 1
Jibu maswali yafuatayo kwa usahihi.
1. Taja vivutio vya utalii vilivyopo nchini Rwanda.
2. Taja baadhi ya wanyama ambao hupatikana katika mbuga ya wanyama
ya Akagera.
3. Mbuga ya wanyama ya milima ya Virunga inajulikana kwa wanyama
gani?
4. Kwa nini sisi kama Wanyarwanda tunafaa kujivunia utamaduni wetu?Zoezi la 2
Andika sentensi hizi kwa kutumia wakati wa mazoea.
1. Wewe utaandika ubaoni wakati wa somo letu.
2. Mimi na ndugu yangu tutapika chakula baada ya somo letu.
3. Wewe na mtalii huyu mtafurahia kutazama mnyama yule.
4. Mkulima huyu na Semana watalima shamba lao katika mwezi wa
Februari.
5. Wanafunzi hawa wanaimba nyimbo za kufurahisha.
Zoezi la 3
Taja aina za pesa ambazo hutumiwa katika nchi zifuatazo.1. Naijeria
2. Japani
3. Malawi
4. Rwanda5. Kanada
Zoezi la 4
Kamilisha sentensi zifuatazo kwa kutumia kiulizi ‘-pi’ kwa usahihi.
1. Kioo ______ kilivunjika?
2. Mlima ______ una wanyamapori wengi?
3. Ufagio ______ uliharibika?
4. Ndizi ______ ni ya mtoto huyu?5. Mzigo ______ ni wa mgeni huyu?
Zoezi la 5
Jaza nafasi zilizo wazi kwa jibu sahihi kutoka kwenye mabano.1. __________ alizuru mbuga ya Akagera? (Nini, Nani)
2. __________ kitaliwa na wageni? (Nani, Nini)
3. __________ hajawahi kumwona simba? (Nini, Nani)
4. __________ kitaletwa na mhudumu wa hoteli? (Nani, Nini)5. __________ kilitumika kuwapiga picha wanyamapori? (Nani, Nini)
Zoezi la 6
Tunga sentensi tano sahihi kwa kutumia kiulizi ‘kwa nini’.Mfano: Kwa nini unamwogopa simba?