adimika – kosa kupatikana kwa urahisi
ambukiza – enezea ugonjwa
andaa - tayarisha
ankra – orodha ya vitu vilivyouzwa pamoja na bei ya kila bidhaa
anuani – maelezo ya mahali mtu anapoishi ambayo huandikwa katika barua
asali – namna ya kitu kioevu na kitamu sana kitengenezwacho na nyuki
azma – lengo au shabaha
bainisha – tambua jambo
bao – mpira kuingia katika lango katika mchezo wa kandanda (goli)
baridi kali – hali isiyokuwa na joto na isisimuayo sana mwili
bei – kiasi cha pesa kinachotumiwa kununulia ama kuuzia bidhaa fulani
burudani - starehe
burudisha – sababishia raha
chai – zao la mchai
dumisha – endeleza
faranga – pesa, fedha, dirhamu, senti, fulusi
filisika – ishiwa na mali
fyeka – kata nyasi
gharamia – lipia gharama
harage/haragwe– nafaka ya jamii ya kunde
haramu – -siyoruhusiwa, -siyokuwa halali
Hisabati – sayansi ya tarakimu ijumuishayo aljebra
hitaji – kuwa na haja ya kitu
huzuni – hisia za majonzi
ibuka – tokeza
idadi – hesabu au jumla ya vitu
ilani – tangazo la kuonya watu wasifanye jambo fulani hasa lenye
kuleta madhara
ingawa – hata ikiwa
jadhba/jazba – hisia isababishayo kujisahau
jamii – watu wanaoishi pamoja
jangili – mwindaji haramu
jedwali – orodha ya maelezo kuhusu mambo fulani kwa namna
yatakavyofuatana
jibini – chakula kinachotengezwa kwa kuyagandisha maziwa na kuyatoa
maji
jukumu – wajibujumuiya– mkusanyiko wa watu
kabuti – koti zito la kuzuia baridi
kagua – chunguza kwa makini
kahawa – zao la mkahawa ama mbuni
kandanda – mchezo wa miguu
kauli – usemi
kiasili – kienyeji
kifaa – chombo
kikao – mkutano
kipindi – muda
kipusa – pembe ndogo ya kifalu
kivuna nafaka – mashine kama trekta ambayo huvuna ngano huku
ikiitoa wishwa
kiwanda – mahali panapotengenezwa bidhaa
kodi ya mapato – fedha zinazolipwa serikali kama ushuru wa mapato ya mtu
kupanda– tia mbegu mchangani ili ziote
limbikiza – weka vitu kidogo kidogo ili viwe vingi
lishe bora – chakula kinachohitajika kwa afya nzuri ya mwili
maabara – mahali mnamofanyiwa majaribio ya kisayansi
maalumu – -enye sifa ya kipekee
mada– kiini cha jambo linalozungumziwa
majira– wakati au kipindi
majira ya kiangazi – kipindi cha kiangazi
majira ya kipupwe – kipindi cha baridi
majira ya mvua– kipindi cha mvua
majira ya vuli– kipindi cha mvua chache
majivuno – hali ya kujiona
manufaa – faida
mapato – kitu kinachopatikana kama vile baada ya kufanya kilimo ama
kufanya biashara.
masuala mtambuka – mambo muhimu yanayoiathiri jamii katika kipindi cha
sasa
matini – kifungu cha habari iliyoandikwa
mazingira – mambo yanayotuzunguka mahali tunapoishi
maziwa – kitu kioevu kitokacho ndani ya titi la mnyama
mbatata – namna ya viazi vilivyo mviringo na visivyo na ladha
mbinu – njia au namna ya kufanyia jambo
mbuga – eneo lililotengewa wanyama wa porini
mchele – mpunga uliokobolewa,yaani kuondolewa mashuke
mfawidhi – mtu aliyepewa wajibu wa kuendesha shughuli fulani, kama vile
mkutano au sherehe fulani
mfugaji tajiri – mfugaji ambaye ana mali nyingi
mifugo – wanyama wanaotunzwa nyumbani
mikahawa – mimea izaayo kahawa
mkulima tajiri – mkulima ambaye ana mali nyingi
mmomonyoko – kuchukuliwa kwa udongo wenye rutuba
mori – hasira kali
mshinde – aliyeshindwa
mshindi – aliyeshinda
msimu – majira
mtama – zao la mtama
muhogo – mzizi wa muhogo unapokuwa umekomaa tayari kwa kuliwa
ndama – mtoto wa ng’ombe
ndizi – tunda la mgomba linalomea kwenye mkungu.
ngeli – kikundi cha majina au nomino zinazofuata kanuni sawa za kisarufi
njugu – mbegu zitengenezewazo mafuta ya karanga
nyama – sehemu laini ya mwili ambayo ikikatwa hutoka damu
pandwa – ingiwa na
pekee – pweke; bila ya -ingine
pesa – noti na sarafu zinazotolewa na kuidhinishwa na serikali kuwa ni
fedha rasmi za kubadilishana na bidhaa.
pori – mahali palipo na miti mingi, nyasi na vichaka
ratiba – mpango wa mfululizo wa shughuli fulani
refa – mwamuzi katika mchezo wa mpira
rejesta – lugha inayotumiwa katika mahali maalum, kama vile hospitalini, hotelini, msikitini na kwingineko
rutuba – mbolea ya kukuzia mimea ardhini
sajili – rejesta
shabiki – apendaye sana timu
sheria – kanuni za kuongoza watu
shime – neno la kuhimizia mtu
shiriki – husika au kuungana na watu katika kufanya shughuli fulani
soseji – namna ya chakula kinachotengenezwa kutoka kwa nyama ya
nguruwe au ya ng’ombe
suala – jambo au hoja
sufu – manyoya ya kondoo
takwimu – nambari zinazoeleza ukweli kuhusu matukio ya mambo, kwa
mfano idadi ya watu katika eneo fulani
tambua – fahamu au maizi
tanbihi – maelezo yanayotoa habari muhimu
tathmini – pima
tegemea– weka matumaini kupata kitu
tia mdomoni– kumsema ama kumsengenya mtu
ulinzi – ulindaji, hali ya kulinda
upanzi – upandaji (uwekaji mbegu ardhini)
utafiti – uchunguzi wa kisayansi
vanila – kiungo kiyafanyayo maziwa yaliyoganda kuwa na ladha ya
kupendeza
viazi vitamu– namna ya viazi vikubwa na vilivyo vitamu
wadau – mtu mwenye maslahi katika shughuli fulani
wadhifa – madaraka au cheo fulani
waligonga ndipo – walisema ukweli
wasifukazi – maandishi yanayoeleza kuhitimu kwa mtu katika
kutekeleza kazi fulani, aghalabu, kimasomo, tajiriba ya kazi
na ujuzi wake
wishwa – takataka za nafaka kama vile mtama au ngano
yakinishi – hali ya kukubali
zao – kile kinachozaliwa na mmea
zaraa – kilimo