Topic outline

 • General

 • Sura 1:Mazungumzo na majadiliano


  Mada ndogo: Msamiati na mawasiliano katika shughuli za kilimo na ufugaji


  A . Msamiati wa msingi kuhusu mazao na shughuli za kilimo na ufugaji nchini Rwanda.
  i) Msamiati wa mazao nchini Rwanda
  Tazama mazao yafuatayo na usome maneno chini yake.

  Bidhaa zilizopo kwenye michoro zinaitwa mazao. Mazao ni vitu tunavyovuna
  baada ya kupanda mbegu zake.Ni vitu vinavyozaliwa na mimea iliyopandwa. Hapa
  nchini Rwanda, udongo wetu ungali na rutuba ya kutoa mazao mema. Tunapanda
  mimea mbalimbali inayotupatia mazao.

  Tazama mifano zaidi ya mazao yanayopatikana hapa nchini Rwanda na
  usome vifungu kando yake.                                                               Kahawa ni zao la mkahawa au mbuni. Kahawa
                              hukaushwa na kusagwa ili kutoa ungaunga.
                              Ungaunga huo hutumiwa kwa kutengenezea
                              kinywaji cha kahawa. Kinywaji cha kahawa
                              kina ladha nzuri. Kahawa pia huuzwa katika
                              nchi za nje na kuletea nchi yetu pesa za kigeni.


                                                                                                                    
    Haya ni
    majani ya mchai. Majani ya mchai hukaushwa
    na kusagwa. Majani haya hutumiwa kutengenezea
    kinywaji cha chai. Nchi yetu huuza majani ya
    mchai katika nchi za kigeni. Majani ya mchai
    pia huletea nchi yetu pesa za kigeni.
                                                                                                 


           
    

                                                                                       
                                                                                              Hizi ni ndizi. Ndizi 
                                                                                              ni zao la mgomba.  
                                                                                              Ndizi humea kwenye      
                                                                                              mkungu. Ndizi
                                      inaweza kuivishwa na kuliwa moja kwa moja. Baadhi ya
                                     ndizi hupikwa na kuliwa.Ndizi pia huuzwa na kutuletea
                                     mapato.

                                                                   

  Haya ni maharagwe. Maharagwe ni zao la mharagwe.
  Nafaka hii ni muhimu sana kwa chakula chetu. Hii ni
  kwa kuwa virutubishi vyake vya protini huhitajika sana
  miilini mwetu. Wale ambao hawali nyama mara kwa mara
  huweza kupanda miharagwe na kupata protini zao kutoka
  kwayo.

             Huu ni mtama. Mtama huzaa punje ndogo ndogo. Punje  
  za mtama hukaushwa na kuchanganywa na mihogo au mahindi. Baadaye husagwa ili kupata unga. Unga huu hutengenezewa  uji au sima (ugali).
                                                              
              
  Haya ni mahindi.Mahindi ni mazao
  ya mhindi. Mahindi hukaushwa na
  kusagwa ili kutoa unga wa dona.
  Unga wa mahindi hutengenezewa
  sima au ugali.Mahindi pia yanaweza kupikwa pamoja na
  maharagwe kutengenezea pure au kande. Pure ni chakula kitamu kinachoshibisha vilivyo. Ama hindi linaweza kuchomwa au kuchemshwa na likawa chakula kwetu. Mafuta ya mahindi hutumiwa kutengenezea mafuta ya kupikia. Mbali na mahindi, njugu pia hutengenezewa mafuta ya kupaka kwenye mkate. Njugu ni zao la karanga. Njugu hukaangwa na kuliwa. Baadhi ya watu hutwanga njugu na kutengeneza borohoa ya kuungia kitoweo.


              
                            Haya ni mananasi. Nanasi ni zao la mnanasi.   
                            Nanasi huivishwa na kuliwa.
                            Nanasi hutoa maji matamu yanayomaliza kiu.
                            Maji hayo hutumiwa kutengenezea sharubati au soda.                                                                                                       
                                 Hii ni mihogo. Muhogo ni mzizi wa muhogo.
                                 Muhogo huweza kuchemshwa au kukaangwa na kuliwa.
                                 Muhogo pia huweza kukaushwa, ukasagwa na kutengenezewa
                                 sima.


                                                                                     
                     

                                                                                                    Hizi ni mbatata. Mbatata  
                                                      ni viazi vya mviringo. Viazi hivi havina sukari. Mbatata
                                                      huweza kupikwa kama kiungo. Pia, huchemshwa na
                                                      kuliwa na vinywaji au vyakula vinginevyo. Mbatata pia
                                                      hukatwakatwa kwa vipande vyembamba na kutiwa ndani           
                                                      ya mafuta ili kutengenezea vibanzi au chipsi.
  Hivi ni viazi vitamu. Viazi hivi hupandwa katika matuta au sesa.
  Viazi vitamu huchemshwa na kunywewa kwa chai au kahawa.
  Viazi vitamu huwa na sukari kiasi cha haja.

  Zoezi

  1. Angalia maana ya maneno yaliyokolezwa kwa wino katika kamusi.
     Tunga sentensi sahihi kwa kila neno.
  2. Taja mazao zaidi yanayopatikana nchini Rwanda lakini hayajatajwa katika kifungu.
       Je, mazao hayo yana faida gani?
  3. Tunga sentensi sahihi ukitumia maneno yafuatayo:
      a) ndizi           b) mahindi           c) kahawa 
      d) mbatata     e) maharagwe     f ) chai
  4. Taja majina ya mazao haya na faida zake.

  Kazi ya wanafunzi wawili wawili
  Jiunge na mwanafunzi mwenzako. Jadilianeni kuhusu majina na faida ya mazao mbalimbali katika maeneo mnakoishi

  Kazi ya kikundi
  Katika vikundi, kila mwanafunzi ataje mazao yasiyopatikana katika eneo anamoishi.
  Jadilianeni kuhusu faida za mazao mliyoyataja.

  ii) Msamiati kuhusu shughuli za kilimo nchini Rwanda
  Jiunge na mwanafunzi mwenzako. Jadilianeni kuhusu shughuli mbalimbali za kilimo kwenye michoro.
  Mfano
                 

  Soma kifungu kilichopo hapa chini na ujibu maswali chini yake.
  HABIMANA:  Habari za asubuhi wenzangu?
  KAREKEZI
  na ITUZE:       Nzuri sana Habimana.
  HABIMANA:   Wenzangu, naomba mnieleze maana ya kilimo.
  KAREKEZI:    Kilimo au zaraa ni kazi ya kulima shamba na kukuza mimea hadi
                          kufikia kiwango cha kuvunwa.
  HABIMANA:   Wenzangu, naomba mnitajie shughuli hizi za kilimo.
  KAREKEZI:    Kwanza, kuna kufyeka. Sisi hufyeka shamba letu kwa kutumia
                          upanga na fyekeo. Baadaye, kuna kulima shamba ili kuandaa konde.
                          Katika kijiji chetu, tunatumia jembe la mkono kuandalia konde.
  HABIMANA:   Kwa nini mnatumia jembe la mkono?
  KAREKEZI:    Kwa sababu mashamba katika kijiji chetu ni madogomadogo.
                          Vilevile, wakulima katika kijiji chetu hawawezi kumudu mbinu
                          nyinginezo za kulima. Je, Ituze, wakulima katika eneo lenu
                          hutumia mbinu zipi kuandaa mashamba yao?
  ITUZE:            Wakulima katika eneo letu hutumia plau inayovutwa na ng’ombe au punda.
                          Wakulima katika eneo jirani nao hutumia plau inayovutwa na trekta. Wakulima
                          hao wanamiliki mashamba makubwa. Pia wanaweza kulipia gharama za trekta.
                          Karekezi, hebu tueleze namna nyingine ya ukulima katika eneo lenu.
  KAREKEZI:    Sisi hulima sesa. Tunapojiandaa kupanda mbegu, huchanganya mbolea ya samadi
                          na udongo. Udongo wetu hauna rutuba ya kutosha. Baada ya kuweka mbolea,
                          tunapanda mbegu za mahindi na maharagwe ndani ya udongo na kuzifukia.
                          Mbegu zinapoota, tunapalilia miche ili kuondoa magugu au kwekwe. Baadhi ya
                          wakulima huweza kupiga dawa za kuwaua wadudu waharibifu.Wakati wa kiangazi,
                          kuna kunyunyizia mimea maji. Baada ya mimea kukua na kukomaa, tunavuna. Viazi
                          na mihogo yetu ndiyo hutuletea pesa za matumizi nyumbani kwetu. Tunakula baadhi
                          ya mazao hayo na kuyauza mengine.
  HABIMANA:   Kumbe kazi hii ya kilimo ni nzuri mno! Nilisoma juzi kuwa nchi yetu hupata pesa
                          za kigeni kwa kuuza chai na kahawa katika nchi za kigeni.
  ITUZE:            Kweli kabisa. Uchumi wa Rwanda umeimarika kwa sababu ya kilimo.
                          Maisha ya wakulima wengi yameimarika pia. Watu wengi
                          wameajiriwa kutokana na kilimo.
  HABIMANA:   Hata mimi nitaanza kufanya shughuli hizi za kilimo. Tuna shamba
                          dogo lakini lina rutuba nyingi. Nitapanda mboga na njugu.
                          Asanteni kwa kunifunza kuhusu kilimo. Kushauriana katika kazi
                          ya kilimo ni jambo lililo muhimu mno.
  KAREKEZI:     Pia, tusome kwa bidii hadi chuo kikuu ndipo tuwe wakulima bora zaidi.
                          Tukisoma kwa bidii, tutajifunza na kutumia mbinu za kisasa za kilimo.
                          Mbinu hizi zitatusaidia na kusaidia jamii. Kilimo kitaimarika.
  ITUZE:            Taibu! Pia tukisoma, tutabuni mbinu mpya za kurahisisha kilimona kujiongezea mazao.
                          Ni lazima tufanye juu chini kupata elimu na kufanya utafiti zaidi. Asanteni wenzangu.

  Maelezo ya msamiati
  kufyeka      – kusafisha shamba kwa kukata miti au majani
  kulima        – kutayarisha shamba kwa kutifua ardhi
  konde         – sehemu ya shamba iliyolimwa
  sesa           – ukulima usiokuwa wa matuta katika ardhi tambarare
  kuzifukia     – kuzificha mbegu ardhini
  zinaota        – zinachipuka kutoka ardhini
  kupalilia       – kulima kwa kuondoa magugu katikati ya mimea au miche
  kunyunyizia – kumwagilia maji au dawa ya maji
  kukua           – kuongezeka ukubwa au kimo
  kukomaa      – kuwa tayari kuvunwa/kutolewa shambani
  kuvuna         – kutoa mazao shambani

  Maswali
  1. Angalia maana ya maneno haya katika kamusi na uyatungie sentensi sahihi.
      a) upanga                    b) fyekeo                   c) plau                             d) trekta                                        e) mbolea    
      f ) samadi                     g) udongo                 h) rutuba                           i) kwekwe                                     j) mbegu
       k) mche                        l) pampu
  2. Andika manufaa ya kilimo yaliyotajwa kwenye kifungu. Ongezea manufaa matano zaidi.
  3. Karekezi na Ndoli hawapendi kilimo. Je, kauli hii ni kweli? Toa sababu zako.
  4. Je, masomo ya kilimo yana umuhimu gani?
  5. Tumia maneno uliyopewa kutaja shughuli kwenye michoro.
       (kufyeka, kulima, kupanda mbegu, kupalilia, kupiga dawa, kunyunyizia maji, kuvuna)
  6. a) Taja majina na matumizi ya vifaa vilivyopo hapa chini.
     
      b) Tunga sentensi sahihi kuhusu kilimo ukitumia jina la kila kifaa hapo juu.
  7. Andika maneno kumi ya shughuli na zana za kilimo kutoka kwenye mraba huu.
      Tunga sentensi sahihi ukitumia kila neno.
       
  Kazi ya wanafunzi wawili wawili
  Jiunge na mwanafunzi mwenzako. Jadilianeni kuhusu shughuli za kilimo katika nchi
  ya Rwanda na manufaa ya shughuli hizo.

  iii) Msamiati kuhusu shughuli za ufugaji nchini Rwanda
  Ufugaji hasa ni kazi ya kutunza wanyama, ndege na hata wadudu. Kazi hii ina faida
  kubwa sana kama kilivyo kilimo cha mimea. Mfugaji anaweza kufuga wanyama ama wadudu.

  Kazi ya wanafunzi wawili wawili
  Jiunge na mwanafunzi mwenzako. Kumbushaneni majina ya mifugo mbalimbali
  mliyosoma katika kidato cha kwanza na umuhimu wake.

  Tazama michoro iliyopo hapa chini na usome kifungu cha maneno kando yake.
   


  Huyu ni Ikirezi. Ikirezi ni mfugaji wa nyuki. Ikirezi
  anarina asali.Baada ya kurina, yeye husafisha
  asali yake na kuiuza. Asali hiyo hutumiwa kama
  chakula au hutengenezewa dawa.
              
  Huyu ni Gabiro. Gabiro anakata sufu. Sufu ya kondoo
  hutumiwa kutengenezea nyuzi za kufumia nguo.

                                                                 


  Huyu ni Ituze. Ituze anakama
  ng’ombe.Kabla ya kukama, aliosha chuchu kwa
  maji vuguvugu na kuzikausha kwa kitambaa safi.
  Anatumia mkebe safi kuwekea maziwa. Ituze
  huwapandisha mitamba kwa dume au mpira.

  Hili ni josho. Ng’ombe hawa wanaogeshwa kwa dawa ndani ya josho. Wafugaji huosha mifugo katika josho ili kuikinga dhidi ya kupe. Dawa huua viroboto wanaoishi kwenye ngozi za mifugo.


  Hawa ni Mudenge na Gatera.
  Mudenge anawalisha kuku kwa mahindi. Pia,
  huwapa kuku mtama, ugali, wadudu na vyakula
  vinavyopatikana kwa urahisi. Wakati mwingine,
  yeye huwapa kuku chakula maalumu
  kilichotengenezwa katika viwanda. Mudenge anawafuga
  kuku wa mayai na nyama. Yeye huuza baadhi ya mayai ili kujipatia riziki. Mudenge pia huwaatamisha baadhi ya kuku wake ili apate vifaranga wa kuuza na kufuga. Gatera naye anawalisha ng’ombe kwa nyasi. Gatera anawafuga ng’ombe wake ndani kwa ndani. Anawapa lishe, maji na dawa humohumo zizini. Gatera hukata pembe za ng’ombe wake. Ng’ombe hukatwa pembe ili kumzuia kumdhuru mtu au kuharibu vitu.

  Huyu ni Kaliza. Kaliza anapenda kuchunga punda. Anawachunga punda penye maji safi na nyasi nyingi. Kulisha mifugo ni shughuli muhimu ya ufugaji. Mifugo wanapolishwa vizuri hukua kwa haraka, huwa na afya nzuri na hutupatia mapato mazuri.

  Kaliza anafagia zizi la ng’ombe. Mkulima
  bora husafisha makao ya mifugo na vyombo
  vyao vya kulia na kulalia. Mifugo wanaolala
  katika mahali safi na kula katika vyombo safi
  huwa na afya njema.

  Daktari wa mifugo anamtibu kuku kwa kumdunga sindano. Kutibu mifugo ni muhimu kwa mkulima. Ni vizuri kutambua dalili ya ugonjwa ili watibiwe mapema.


  Msamiati
  kurina         – kufukuza nyuki kutoka kwenye mzinga na kukata masega ili kupakua asali.
  kukata sufu – kunyoa manyoya ya kondoo kutoka kwenye ngozi yake
  kukama       – kuminya chuchu za mnyama kama vile ng’ombe ili maziwa yatoke
  kupandisha mtamba                     – kumpa ng’ombe wa kike mbegu za kiume ili kuzalisha ndama
  kufuga ng’ombe ndani kwa ndani – kufuga ng’ombe ndani ya eneo au jengo fulani na
                                                           kuwapa mahitaji yote humo bila kuwatoa nje
  kuwapeleka ng’ombe katika josho – kuwapelekea ng’ombe katika dimbwi maalumu lililotiwa dawa ya kuulia kupe
  kuatamisha kuku – kumfanya kuku kulalia mayai
  kuchunga            – kuwapeleka wanyama malishoni na kuwalinda wasiibwe
  kukata pembe     – kutoa pembe kwa kutumia kisu au chuma moto
  kulisha   – kupea chakula na maji

  Maswali
  1. Andika majina yote ya mifugo waliotajwa katika ufahamu hapo juu.
      Taja umuhimu wao.
  2. Eleza faida za shughuli za ufugaji ulizosoma katika kifungu.
  3. Jaza mapengo haya kwa shughuli sahihi ya ufugaji.
     
   
   
  4. Tunga sentensi sahihi ukitumia maneno hapo chini.
      a) rina asali
      b) chunga
      c) kata pembe
      d) kama
      e) lisha
      f ) fagia zizi
      g) tibu ng’ombe
      h) pandisha mtamba
       i) atamisha

  Kazi ya wanafunzi wawili wawili
  Jiunge na mwanafunzi mwenzako na mfanyeni zoezi hili:
  1) Kwa pamoja, andikeni shughuli mbalimbali za ufugaji na mifugo nchini Rwanda katika karatasi.
  2) Kunjeni karatasi hizo na kuziweka pamoja.
  3) Kila mwanafunzi achukue karatasi moja kwa zamu, asome shughuli ya ufugaji
      au mifugo katika karatasi aliyochukua na atunge sentensi sahihi kwa kutumia
      neno katika karatasi yake. Atakayekosea asahihishwe.

  Kazi ya kikundi
  Kama darasa zima, fanyeni mjadala kuhusu: Njia za kisasa za ufugaji zinaleta mapato
  makubwa zaidi kuliko njia za kienyeji.

  B . Majira ya mwaka nchini Rwanda
  Tazama michoro iliyopo hapa chini. Je, nini kinafanyika?
   

   Soma kifungu hiki na ujibu maswali yaliyoulizwa chini yake.
  Majira ni kipindi maalumu cha hali ya hewa. Majira haya ndiyo huelekeza upanzi
  wa mimea na uvunaji wa mazao hapa kwetu.
  Tupo na majira mbalimbali. Yapo majira ya mvua nyingi. Majira ya mvua nyingi ya
  mfululizo huitwa masika. Majira haya hutokea kuanzia mwezi wa Machi hadi Mei
  kila mwaka. Shughuli za kupanda mimea kama vile maharage, mtama, mbatata,
  mahindi,na kadhalika hutokea mwanzoni mwa majira ya masika. Mimea hiyo    
  huota na kupaliliwa katika majira haya ya masika.
  Vilevile, mimea mbalimbali kama vile mikahawa, mipareto, migomba, minanasi na
  kadhalika hustawishwa mnamo majira haya.
  Msimu huu wa masika hufuatwa na majira ya kiangazi au ukame. Huu ni wakati
  ambapo jua kali huwaka, mvua hukosa kunyesha na ardhi hukauka. Yapo majira
  mafupi ya kiangazi ambayo hutokea kuanzia Juni hadi Septemba. Mifugo na mimea
  hukosa chakula na maji ya kutosha na huanza kuwa na afya mbaya mnamo majira haya.
  Baadhi ya wakulima huanza kuvuna mazao yao katika majira ya kiangazi.
  Wengine hulima na kuandaa makonde yao mnamo majira haya kabla ya mvua
  kuanza kunyesha.
  Mbali na majira haya, yapo majira ya vuli. Huu ni wakati ambapo huwepo mvua
  ndogo ndogo tu. Majira haya hutokea kati ya mwezi wa Novemba na Februari.
  Wakati wa vuli, wakulima hupanda vyakula vinavyochukua muda mfupi kukua na kukomaa.
  Hata hivyo, shughuli nyingi za upanzi hazifanyiki kwa kuwa mvua inyeshayo huwa haitoshi
  kukuza baadhi ya mimea.
  Hali kadhalika, yapo majira ya kipupwe. Kipupwe ni majira ya baridi ambayo hutokea katika
  miezi ya Septemba na Novemba nchini Rwanda. Wakati huu wa mwaka huwepo baridi kali
  na hubidi watu kuvaa sweta, makoti na hata makabuti.
  Kwa ufupi, wakulima wengi nchini Rwanda huzingatia majira mbalimbali
  wanapofanya shughuli zao za kilimo. Wao hutegemea mvua na jua katika kukuza mimea.

  Msamiati
  masika               – majira ya mvua nyingi ya mfululizo
  kiangazi/ukame  – majira ya jua kali
  vuli                      – majira ya mvua ndogo ndogo
  kipupwe              – majira ya baridi kali

  Maswali
  1. Taja miezi na majira ambapo shughuli hizi za kilimo hufanywa hapa kwetu Rwanda.
      a) kulima shamba kavu
      b) kuandaa konde lenye unyevunyevu
      c) kupanda mimea mingi
      d) kupalilia
      e) kustawisha mimea
      f ) kuvuna
      g) kupanda mimea michache inayokua na kukomaa haraka
  2. Ipo tofauti gani kati ya vuli na kipupwe?3. Tazama mraba ufuatao na uandike maneno manne ya majira.
        

  Kazi ya wanafunzi wawili wawili
  Jiunge na mwenzako. Chunguzeni michoro ifuatayo na mjaze mapengo kando yake.
   
   

  C . Msamiati wa msingi kuhusu wanyama wa porini na umuhimu wake

  i) Msamiati wa wanyama wa porini nchini Rwanda
  Tazama wanyama hawa. Je, hawa ni wanyama gani? Wanyama hawa
  wanapatikani katika mbuga na sehemu ipi ya Rwanda?

  Kisome kifungu kifuatacho ili kujifunza msamiati wa wanyama wa porini.
  Mnyama wa porini ni mnyama anayeishi katika pori. Pori ni mahali penye miti na nyasi nyingi.
  Mnyama wa porini hafugwi na binadamu. Wanyama wengi wa porini hupatikana katika mbuga
  za wanyama. Mbuga za wanyama ni sehemu zilizotengwa na serikali kuwa ndio makazi ya
  wanyama hao wa porini. Je, unafahamu mbuga gani za wanyama nchini Rwanda?
                                                                                                                            

  Nchi ya Rwanda ina wanyama wengi wa porini.
  Nchi yetu ya Rwanda inasifika sana kutokana
  na masokwe. Sokwe ni mnyama mkubwa zaidi
  katika jamii ya nyani. Mnyama huyu hana
  mkia. Sokwe ana akili nzuri inayokaribiana
  na ile ya binadamu. Wana uwezo wa
  kumwiga binadamu. Nchi yetu inajulikana
  sana kutokana na masokwe. Masokwe hawa
  wanapatikana katika mbuga zetu za wanyama.
  Masokwe wengi wanapatikana katika Mbuga
  ya Wanyama ya Volcanoes (Volkano).

  Nyani ni mnyama wa jamii ya sokwe na tumbiri.
  Nyani ni mdogo kuliko sokwe lakini ana akili nyingi zaidi.
  Ana masikio makubwa nao mwili wake una rangi ya kaki ya
  kijivu na ngoko nyekundu makalioni. Nyani huishi katika
  vikundi vya majike na madume. Wana uwezo wa kuishi
  kwa miaka zaidi ya arubaini.
                                                                                                                    

             Pia kuna tumbiri porini. Tumbiri ni mnyama mdogo
             zaidi katika jamii ya nyani. Tumbiri hupenda sana
             kukaa mitini. Hula vyakula mbalimbali kama vile
             matunda, mazao ya mimea mbalimbali na kadhalika.  Simba ni mnyama mkubwa wa jamii ya paka.
  Simba hula nyama. Anaitwa mfalme wa wanyama
  au nyika. Simba huishi kwenye vikundi. Vikundi
  hivyo huongozwa na simba dume.       
                 


                               Ndovu ndiye mnyama mkubwa zaidi wa porini.
                               Ndovu ana mkonga pamoja na pembe mbili
                               kubwa zenye thamani. Ndovu wana masikio
                               makubwa na miguu mifupi minene. Ndovu hula
                               nyasi, mizizi, matunda na mashina ya miti. Pia,
                               huishi katika vikundi. Kila kikundi huongozwa na
                               ndovu jike ambaye ana umri mkubwa zaidi kuliko
                               wote. Uwindaji wa ndovu na kuuza pembe
                                zake ni hatia. Sisi sote tunafaa kuwatunza ndovu na wanyama wote wa porini.


  Chui pia hupatikana katika mbuga zetu. Chui ni
  mnyama wa jamii ya paka lakini aliye mkubwa na
  mkali na mwenye madoadoa ya manjano na meusi.
  Chui hula wanyama wadogo wadogo wanaoishi porini.
  Baada ya kuwinda, wao huficha nyama kwenye matawi
  ya mti. Wao hupenda sana kutembea na kuwinda wakati
  wa usiku na kupumzika wakati wa mchana.  Pundamilia pia ni mnyama wa porini wa jamii ya farasi.
  Ana milia myeusi na myeupe katika mwili mzima.
  Inaaminika kuwa milia hiyo huwawezesha kujificha
  nyikani ili wasionekana na wanyama wanaowawinda.
  Pundamilia hutembea na kula nyasi katika vikundi vikubwa.                                                                                                                                                    

                        Twiga naye ana shingo ndefu, rangi ya kahawia na madoadoa meusi.
                        Twiga  ndiye mnyama mrefu zaidi. Yeye hula majani ya miti.
  Kifaru pia hupatikana katika mbuga zetu. Ni mnyama
   mkubwa afananaye na kiboko na mwenye kipusa usoni.


                                                                     
                                        
                                
   Nyati pia ni mnyama mkubwa sana. Hufanana na ng’ombe. Pembe zake zimepinda kwa mbele. Nyati hula nyasi. Wao pia huishi katika vikundi kutegemea jinsia. Nyati pia huitwa mbogo.                                    
   


  Swara ni mnyama mdogo anayefanana na mbuzi.
  Swara anaweza kukimbia haraka. Yeye hula nyasi.  Wanyama hawa wa porini hupatikana katika mbuga zetu kama vile Akagera,
  Nyungwe na Volcanoes. Wanyama hawa ni vivutio vikubwa vya watalii wanaotoka
  ndani na nje ya nchi yetu.

  Maswali
  1. Andika orodha ya majina ya wanyama wa porini wanaokula:
      a) nyama
      b) nyasi
  2. Eleza tofauti zilizopo kati ya sokwe na nyani.
  3. Jaza kila pengo kwa jina sahihi la mnyama wa porini.
       a) Mwenye tamaa kama______________.
       b) _________ ana mkonga na pembe mbili.
       c) _______ haoni kundule.
       d) Ndovu pia huitwa_____________.
       e) Nimemwona mnyama mwenye milia myeusi na myeupe mwilini.
           Nimemwona__________.
  4. Tunga sentensi sahihi ukitumia majina haya ya wanyama wa porini.
       a) pundamilia             b) simba               c) tumbir
      id) swara                     e) nyati                  f ) ndovu
  5. Taja majina ya wanyama hawa:


  6. Jiunge na mwanafunzi mwenzako. Fanyeni utafiti kuhusu majina na sifa
      za wanyama wa porini wanaopatikana ndani na nje ya Rwanda na ambao
      hawajatajwa katika ufahamu.

  ii) Umuhimu wa wanyama wa porini nchini Rwanda
  Kufikia sasa, umesoma mengi kuhusu wanyama wa porini. Wanyama hao wana
  umuhimu mbalimbali.
  Tazama mchoro huu na usome kifungu chini yake.
                                                
  KANYANA:  Karibuni katika mbuga yetu ya Volcanoes.
  UWASE
  na HIRWA:   Asante.
  KANYANA: Hapa, mtaona wanyama wengi wa porini.
  UWASE:      Wanyama hao wana umuhimu gani?
  NGABO:     Wanyama hao wana umuhimu mkubwa sana kwa nchi hii yetu ya
                      Rwanda. Wanyama hao kama vile masokwe ni vitega uchumi. Kila
                      mwaka, watalii kutoka nchi za mbali huja hapa kwetu kuwaona
                      wanyama. Wajapo hivyo, huja na pesa za kigeni ambazo huinua sana
                      uchumi wetu.
  KANYANA: Nyinyi pia ni watalii wetu hapa. Pesa mnazolipa mkiingia hujenga
                      uchumi wetu. Pesa hizo pia hutumiwa kutulipia mshahara. Mimi na
                      wenzangu tumeajiriwa kwa sababu ya wanyama wa porini.
  HIRWA:       Je, nchi yetu hunufaika na pesa za kiingilio peke yake?
  NGABO:      Hapana. Wageni wanapokuja, wanaleta manufaa mengi zaidi. Wao
                       hulipia huduma mbalimbali. Kwanza kuna malazi yao. Sisi
                       huwakaribisha katika hoteli kubwa kubwa na nzuri nzuri. Hoteli
                       hizo zimepanuka na kuwaajiri watu wengi kwa sababu ya wageni
                       hao wanaokuja kuangalia wanyama wa porini. Wageni hao pia
                       hulipia usafiri wao uwe ni wa ndege au gari. Usafiri huo huwapeleka
                       huko wanakopenda kwenda kuwaona wanyama.
  KANYANA: Mbali na hayo, zipo bidhaa nyingi sana za hapa ambazo watalii hao
                      hununua kuwa ni ushahidi kwao kwamba kweli walikuwa hapa. Kwa
                      njia hiyo pia nchi hufaidika kiuchumi.
  UWASE:      Mbali na faida hizo za kifedha, zipo faida gani tena za wanyama hawa?
  NGABO:      Wanyama hawa hukuza elimu yetu. Wanafunzi, na hata watu wazima
                       huzuru mbuga zetu za wanyama ili kuwaona na kujifunza mengi
                       kuwahusu.
  KANYANA:  Isitoshe, wanyama wa porini ni hazina kwa vizazi vyetu vya baadaye.
                       Sisi sote tumewaona wanyama hawa. Vivyo hivyo, litakuwa jambo
                       zuri sana ikiwa wanetu, wajukuu, watukuu, vilembwe na hata
                       vilembwekeza wetu kuwaona wanyama wa porini pia. Hii ndiyo
                        sababu ya serikali yetu kuwatunza na kuwalinda wanyama wa porini.
  UWASE
  na HIRWA:  Asanteni kwa maelezo yenu.

  Maswali
  1. Taja faida za wanyama wa porini.
  2. Taja njia mbili ambazo serikali hutumia kuhifadhia wanyama wa porini.

  Kazi ya kikundi
  Jiunge na wanafunzi wenzako. Jadilianeni kuhusu umuhimu wa wanyama wa porini nchini Rwanda.

  D . Matini ya Kiswahili kuhusu kilimo na ufugaji pamoja na vipengele vya kisarufi
  Nomino
  Je, unakumbuka maana na aina za nomino ulizosoma katika kidato cha kwanza?
  Zitaje.
  Nomino ni neno linalotaja mtu, kitu, hali au jambo. Zipo aina mbalimbali za nomino.
  Zifuatazo ni baadhi ya nomino hizo.

  a) Nomino za pekee
  Nomino za pekee hutaja vitu au watu wenye sifa za kipekee. Zinapoandikwa katika
  sentensi, lazima zianze kwa herufi kubwa hata zikiwa katikati au mwishoni mwa
  sentensi. Kumbuka hapa ya kuwa majina haya hayachukui hali ya wingi.
    Mifano ya nomino za pekee katika sentensi.
  i) Rwanda ni nchi yenye wanyama wengi wa porini.
  ii) Mukangango ananyoa sufu ya kondoo.
  iii) Mwenyezi Mungu atujalie mvua nyingi ili tulime.
  iv) Kigali ni jiji linalopendeza.


  Zoezi

  a) Andika sentensi sahihi ukitumia nomino hizi za pekee:
      i) Munyana        ii) Kamana          iii) Mola
    iv) Mei                 v) Mto Kivu          vi) Msitu wa Nyungwe
  b) Tambua makosa katika sentensi hizi na uyarekebishe.
      i) Mimi na kayitesi tunapenda somo la kilimo.
      ii) Nitavuna mihogo yangu mwezi wa februari.
      iii) Ng’ombe anaitwaje kwa kinyarwanda?

  b) Nomino za kawaida
  Nomino za kawaida hutaja vitu vya kawaida vinavyoweza kuchukua umoja na
  wingi kama jina lolote lile. Nomino hizo zinapoandikwa, huchukua herufi ndogo
  isipokuwa pale zinapojitokeza mwanzoni mwa sentensi.

  Mifano ya nomino za kawaida:
  i) Nomino za viumbe wenye uhai:
    
  ii) Nomino zinazomtambulisha mtu na kazi yake:
       

  iii) Nomino za vitu vya kawaida
     
  iv) Nomino za mahali: shambani, uwanjani, mbugani, zizini, porini
  Kumbuka hapa kuwa nomino hizi za mahali huundwa kwa kuongeza ‘ni’ mwishoni
  mwa nomino husika.

  Mifano ya matumizi ya nomino za kawaida katika sentensi.
  i) Mavuno ya mwaka huu ni mazuri.
  ii) Niletee jembe hilo.
  iii) Sufu za kondoo hutumiwa kutengenezea sweta.
  iv) Mkulima hodari hupata mazao mengi.
  v) Ndovu ni mnyama mkubwa wa porini.

  Zoezi

  Tunga sentensi kumi sahihi ukitumia nomino za kawaida.

  c) Nomino za jamii
  Nomino za jamii pia huitwa nomino za makundi. Hizi ni nomino ambazo hutaja
  jumla ya vitu vingi au vitu katika makundi.

  Mifano ya nomino za jamii:


  Mifano katika sentensi
  i) Makole ya ndizi yamevunwa.
  ii) Matuta yamepigwa shambani.
  iii) Matita ya kuni yatatumika kuchomea nyama.
  iv) Mitumba ya aina hii haifai wakulima.
  v) Bunge letu limetenga pesa nyingi kwa wizara ya kilimo.
  vi) Baraza la wafuga farasi limevunjwa.
  vii) Hili ni robota la pamba.

  Zoezi

  Fanya utafiti kupata nomino kumi zaidi za jamii. Tunga sentensi ukitumia kila
  nomino hizo katika umoja na wingi.

  d) Nomino za dhahania
  Katika kikundi hiki hupatikana nomino ambazo ni za kufikirika tu na wala
  haziwezi kuguswa. Chukua nomino kama urafiki. Urafiki ni neno la kufikirika au
  kudhaniwa tu na wala haliwezi kuonekana wala kushikika. Nomino hizi haziwezi
  pia kuhesabika.
  Mifano katika sentensi
  i) Upanzi hufanywa mvua inapoanza kunyesha.
  ii) Kilimo kinasaidia kumaliza umaskini nchini Rwanda.
  iii) Ushirikiano wao katika kupalilia unawafaidi.
  iv) Fikira za wafugaji hao ni za hekima.
  v) Tutafanya uvunaji mwezi ujao.

  Zoezi

  Tunga sentensi zozote kumi kuhusu kilimo na ufugaji ukitumia nomino za jamii.

  e) Nomino za wingi
  Hizi nazo ni nomino za vitu ambavyo daima hupatikana kwa wingi pekee au umoja
  pekee. Vitu vinavyotajwa na nomino hizi haviwezi kugawika.

  Mifano ya nomino za wingi:
  maziwa, sukari, chumvi, uji, chai, manukato, mvua na kadhalika.

  Mifano katika sentensi:
  i) Sukari ni zao la miwa.
  ii) Maua yale hutumiwa kutengenezea manukato.
  iii) Chai hii ni tamu.
  iv) Maji yanyunyiziwayo hapa ni ya mto huo.

  Zoezi

  Soma kifungu kilichopo hapa chini. Tambua na uanishe nomino mbalimbali kifunguni.
  Hapa nchini Rwanda, Mwenyezi Mungu ametujalia mazingira mazuri yenye
  kufanikisha ufugaji. Ufugaji ni kazi ya kutunza wanyama, ndege na hata wadudu.
  Mfugaji anaweza kufuga wanyama ama wadudu. Ikiwa ni wanyama, anaweza
  kutunza ng’ombe, mbuzi, kondoo, farasi, nguruwe, na kadhalika. Ikiwa nia yake ni
  kufuga ndege, anaweza kuwatunza kuku, bata na kadhalika. Hata hivyo, akichagua
  wadudu huweza kuwafuga nyuki.
  Ufugaji una kazi nyingi sana. Kwa mfano, mfugaji wa ng’ombe anapotaka matokeo
  ya kuridhisha, itambidi atumie njia za kisasa katika ufugaji wake. Kwanza kabisa, ni
  lazima awatafute ng’ombe bora wa maziwa. Ng’ombe hawa huleta mapato ya juu.
  Mbali na hayo ni sharti ahakikishe kwamba wanyama wake wana lishe ya kutosha
  hasa kwa ng’ombe wanaokaa ndani kwa ndani. Ng’ombe hawa, hasa ng’ombe jike,
  wa kukaa ndani kwa ndani hulishiwa zizini na kulala humo humo zizini. Hata hivyo,
  ni lazima zizi hilo liwe safi na ng’ombe huyo alale pahali safi. Kukosa kufanya hivyo
  ni kukaribisha magonjwa ya namna kwa namna.
  Iwapo mfugaji atawalisha wanyama wake vizuri, atafaidika pakubwa. Ataweza
  kupata maziwa ya kutosha. Atauza maziwa hayo na kujinunulia bidhaa nyinginezo
  kama vile chumvi, sukari, chane za ndizi na kadhalika. Umaskini pia utaisha.

  Vivumishi
  Je, unakumbuka vivumishi mbalimbali mlivyosoma katika kidato cha kwanza?
  Kwa kawaida, kivumishi ni neno linaloongezea nomino maana. Zipo aina mbalimbali za
  vivumishi. Baadhi ya vivumishi hivyo ni:

  a) Vivumishi vya sifa
  Haya ni maneno yatajayo tabia au sifa za kitu, mtu ama jambo.
  Zipo aina mbili za vivumishi vya sifa: vivumishi vya sifa vinavyochukua viambishi na
  vivumishi vya sifa visivyochukua viambishi.

  Mifano ya vivumishi vya sifa vinavyochukua viambishi:
  -aminifu         -zuri
  -pana             -kubwa
  -pya               -dogo
  -bovu             -fupi

  Kumbuka kuwa kiambishi au viambishi vinavyochukuliwa na vivumishi hivi hutegemea ngeli.
  Mifano katika sentensi:

  ii) Vivumishi vya sifa visivyochukua viambishi
  Hivi ni vivumishi ambavyo havibadiliki katika umoja na wingi au kutoka ngeli moja
  hadi nyingine; hubakia jinsi vilivyo.
  Mifano: bora, safi, hodari, bandia, haba, duni, laini na kadhalika.

  Mfano katika sentensi.
   


  Zoezi

  a) Tunga sentensi sahihi kuhusu kilimo na ufugaji katika umoja na wingi ukitumia vivumishi hivi vya sifa.
      i) -baya          ii) -fupi           iii) -dogo
     iv) -ingi           v) -chache
  b) Tunga sentensi sahihi ukitumia vivumishi hivi katika umoja na wingi.
     i) bora           ii) dhalimu       iii) duni
    iv) tele            v) laini
  c) Andika sentensi hizi katika umoja au wingi.
     i) Nipe ndizi chache.
    ii) Mhindi mrefu unafaa.
   iii) Farasi wakubwa watatubeba.
   iv) Zizi safi halileti magonjwa.
    v) Upanzi bora ni huu.
   vi) Mkulima nadhifu anapita.
  d) Tunga sentensi zozote kumi kuhusu wanyama wa porini na kilimo zenye
       vivumishi vya sifa katika umoja na wingi.

  b) Vivumishi vya pekee
  Vivumishi vya pekee hutoa habari kuhusu nomino au kiwakilishi chake kwa njia ya
  kipekee. Vivumishi vya peke ni sita katika Kiswahili kama ifuatavyo:

  i) -enye
  Huonyesha hali ya ‘kuwa na’ au ‘kumiliki’. Ni sharti kivumishi hiki kifuatwe na nomino wala si kitenzi.

  ii) -enyewe
  a) Hutumika mwanzoni mwa sentensi kuonyesha jambo au kitu kinachotarajiwa.

  b) Hutumika mwishoni mwa sentensi kuonyesha kuwa jambo limetokea bila
      kusababishwa na yeyote au chochote.
    
  iii) -ote
  Huleta maana mbili:
  a) Kuonyesha kila sehemu ya kitu hasa katika umoja.
   
  b) Kuonyesha kila kitu; bila kubakisha lolote hasa katika wingi.

  Zoezi

  Eleza maana ya sentensi ikiwa ni ‘kila sehemu’ au ‘kila kitu’.
  i) Zizi lote limefagiliwa.
  ii) Mazao yote yamevunwa.
  iii) Paka amekunywa maziwa yote.
  iv) Ndizi yote imeiva.
  v) Simba wote wamepita.

  iv) -o-ote
  Huonyesha mojawapo ya vitu au baadhi ya vitu bila kubagua.

  Zoezi

  Tumia ‘-ote’ au ‘-o-ote’ pamoja na viambishi sahihi vya ngeli kujazia pengo katika sentensi zifuatazo.
  1. Nitatumia jembe _____ nitakalopewa.
  2. Miharagwe _________ imemea.
  3. Kuku ______ wamepewa chakula.
  4. Sitachukua nanasi ____________.
  5. Fyeka nyasi____________.

  v) -ingine
  Kivumishi hiki cha pekee huweza kuwa na maana tatu:
  a) Kuonyesha kitu tofauti na kile kilichotajwa au kilichopo.
   

  b) Kuonyesha kitu zaidi/nyongeza


  c) Kuonyesha ‘baadhi ya’


  vi) -ingineo
  Kivumishi hiki hutumika kuleta maana mbili:
  a) 'zaidi ya'

  b) Kuonyesha hitimisho ya orodha ambayo haikukamilika.
    

  Zoezi

  a) Tumia ‘-ingine’ au ‘-ingineo’ pamoja na viambishi sahihi vya ngeli kujazia mapengo.
      i. Amevuna mananasi ____________.
      ii. Sitaki panga hili, nipe panga _____________.
     iii. Mama amepanda mbegu za maharagwe, mtama, mahindi na _____________.
     iv. Usiwakame ng’ombe __________. Maziwa haya yametosha.
     v. Mpe migomba hiyo na ______________.
  b) Tunga sentensi tano sahihi kuhusu kilimo na ufugaji katika umoja na wingi
       ukitumia nomino zozote na kivumishi cha ‘-ingine’.
  c) Tunga sentensi tano sahihi kuhusu wanyama wa porini na mifugo katika
       umoja na wingi ukitumia nomino zozote na kivumishi cha ‘-ingineo’.

  c) Vivumishi vionyeshi
  Vivumishi vionyeshi au viashiria ni maneno ya kuonyesha alipo mtu au kitu, yaani
  ujirani. Kuonyesha huko kunaweza kuwa kwa ujirani wa karibu – hapa, ujirani wa
  mbali kidogo – hapo, na ujirani wa mbali – pale.

  Mifano ya vivumishi hivi ni hii ifuatayo:

  Mfano katika sentensi:
  i) Kijijini humu mna mfugaji hodari.
  ii) Hizi juhudi zenu za kulima zitamaliza umaskini.
  iii) Ng’ombe wale wanakunywa maji.
  iv) Fyekeo hilo halikati majani.
  v) Shambani pale pamepaliliwa.

  i) Vivumishi vionyeshi radidi
  Vivumishi hivi hutokana na kurudia vivumishi vionyeshi. Huleta maana ya kutilia mkazo.

  ii) Vivumishi vionyeshi visisitizi
  Hutumiwa kusisitiza jambo.

  Zoezi

  a) Jaza kila pengo kwa vivumishi sahihi vilivyowekwa katika mabano.
      i. Mazao __________ yatajaza guni. (vionyeshi visisitizi vya karibu)
      ii. Mkulima _________ analima. (vionyeshi vya mbali)
     iii. Twiga __________ ni wengi. (vionyeshi viradidi vya mbali kidogo)
     iv. Nyama __________ ni tamu. (vionyeshi vya karibu)
     v. Wafugaji _________ wana bidii. (vionyeshi vya mbali kidogo)
  b) Tunga sentensi tano tano kuhusu kilimo na ufugaji katika umoja na wingi
       ukitumia vivumishi vionyeshi, vivumishi vionyeshi rejeshi na vivumishi
       vionyeshi visisitizi.

  d) Vivumishi vya idadi
  Vivumishi vya idadi ni maneno yanayoonyesha idadi ya watu ama vitu.
  Vipo vivumishi vya idadi kamili, vivumishi vya idadi ya jumla na vivumishi
  vya idadi ya matokeo.

  i) Vivumishi vya idadi kamili
  Pia huitwa vivumishi vya idadi halisi au bainifu. Huonyesha hesabu halisi ya nomino
  husika.Baadhi ya vivumishi hivi huchukua viambishi vya ngeli kutegemea nomino
  inayohesabiwa.
  Mfano: -moja, -wili, -tatu, -nne, -tano na -nane.

  Baadhi ya vivumishi vya idadi kamili havichukui viambishi vyovyote vya ngeli.
  Yaani hutumika jinsi vilivyo bila kubadilika.
  Mfano: sita, saba, tisa na kumi, makumi, mia na kadhalika

  ii) Vivumishi vya idadi ya jumla/isiyo kamili
  Huonyesha idadi ambayo ujumla wake haujulikani. Baadhi ya vivumishi hivi
  huchukua viambishi vya ngeli ya nomino.

  Mfano: -chache na –ingi

  Mfano katika sentensi:
  1. Kuku hawa wametaga mayai machache.
  2. Mwaka huu tumepanda mbegu nyingi.
  3. Wakulima wengi wamevuna.
  4. Wao huuza maziwa mengi sana.
  Baadhi ya vivumishi vya idadi ya jumla havichukui viambishi vya ngeli.
  Yaani hubakia vivyo hivyo.
  Mfano: kadhaa, tele, kiasi, kidogo na haba.


  iii) Vivumishi vya idadi ya matokeo
  Pia huitwa vivumishi vya nafasi katika orodha. Vivumishi hivi huonyesha nafasi ya
  nomino katika orodha.

  Zoezi

  a) Jaza kila pengo kwa kivumishi sahihi katika mabano.
     i. Sungura ________ wanakimbia. (chache)
    ii. Masokwe __________ wanacheza. (sita)
   iii. Mkulima __________ atapewa mbolea. (moja)
   iv. Amenunua maembe_________. (ingi)
    v. Tumelima mashamba___________. (nane)
  b) Tunga sentensi kumi sahihi kuhusu kilimo na ufugaji ukitumia vivumishi vya
       idadi jumla na isiyo jumla.

  e) Vivumishi viulizi
  Hili ni kundi la vivumishi ambalo lina maneno yatumiwayo kuulizia maswali.
  Baadhi ya mifano ya vivumishi viulizi ni:

  i) Kiulizi -pi?

  ii) Kiulizi -ngapi?

  iii) Kiulizi gani?
  Kiulizi hiki hakichukui kiambishi chochote cha ngeli.

  Tanbihi
  Kivumishi kiulizi kinastahili kuandamana na nomino au kiwakilishi cha nomino.
  Viulizi ambavyo havitumiwi pamoja na nomino au viwakilishi vya nomino haviwezi
  kuitwa vivumishi bali ni viulizi.
  Mfano: lini, nani, nini, vipi. Hivi si vivumishi viulizi kwa sababu havitumiwi pamoja
  na nomino au kiwakilishi cha nomino.

  Zoezi

  a) Tumia kiulizi ‘-pi’ kwa usahihi kujazia kila pengo.
     i. Mashirika _________ yanasaidia wakulima?
    ii. Mkahawa __________ unakatwa?
   iii. Dawa _________ zinanyunyiziwa mimea?
   iv. Niwaite wafugaji ________?
   v. Kufyeka _______ kunafaa?
  b) Tumia kivumishi kiulizi ‘-ngapi’ kwa usahihi kujazia kila pengo.
   i. Tukupe magunia __________?
  ii. Pembe _________ zimekatwa?
  iii. Mbwa _________ wamechanjwa?
  iv. Mipera ___________ inapandwa?
  v. Vibuyu _________ vina maziwa?

  f) Vivumishi vimilikishi
  Maneno katika kundi hili la vivumishi hujibu swali mtu, kitu au jambo ni la nani au
  lina nini? Vivumishi hivi huwa sita pekee katika Kiswahili.
  -angu            -etu
  -ako              -enu
  -ake              -ao

  Kutokana na haya, unapata maneno kama vile:
  wangu               wetu
  chako                chenu
  kwake                kwao

  Unaweza kutunga sentensi hizi ukitumia vivumishi vimilikishi:
  1. Jibini hii ni yangu.
  2. Mawele yako yameliwa na fukusi.
  3. Mbatata zenu zinauzwa Zambia.
  4. Njugu za kwao ni tamu mno.
  5. Huwezi kusema kuwa huu ni mchicha wako!

  Zoezi

  Jaza kila pengo kwa kivumishi kiwakilishi sahihi.
  1. Nyinyi mna mihogo. Mihogo ni ___________.
  2. Sisi tuna maembe. Maembe ni _____________.
  3. Wao wana sufu. Sufu ni _____________.
  4. Mimi nina sukari. Sukari ni ____________.
  5. Yeye ana kole la ndizi. Kole ni __________.
  6. Wewe una muhogo. Muhogo ni _____________.

  Kazi ya wanafunzi wawili wawili
  Jiunge na mwanafunzi mwenzako. Someni kifungu kifuatacho huku mkitambua jinsi
  vivumishi vilivyotumiwa.
  Mimi ni mwanafunzi mwenye bidii. Nia yangu kuu maishani mwangu ni kuridhika
  na shughuli za kilimo cha kisasa kama mojawapo ya njia nzuri za kupigana dhidi
  ya umaskini. Lengo langu kuu la kwenda shuleni hasa ni kupata maarifa mema ya
  kuniwezesha kuishi maisha ya kitajiri. Maarifa hayo yataniwezesha kuwa mkulima
  bora.
  Nitaendelea na masomo hadi chuo kikuu. Nitafanya somo la Kilimo katika chuo
  kikuu. Hata hivyo, hilo pekee halitatosha. Nitafanya kazi ndogo ndogo kwa muda
  ili kutafuta pesa za kuanzisha kilimo. Kufikia hapo, nitakuwa nimepiga hatua lakini
  bado sitakuwa nimefikia lengo langu.
  Kuanzisha kilimo cha kisasa kutakuwa ni hatua kubwa lakini bado kutakuwa
  na kazi kubwa ya kufanywa. Ni sharti niupige vita vikali umaskini kupitia kilimo
  hicho. Umaskini ni adui mbaya ambaye lazima niangamize. Njia moja ya kumaliza
  umaskini ni kuweka uvivu kando.
  Mbali na kulima, nitafuga mifugo wengi. Nitahakikisha ya kuwa nina vifaa vyote
  vinavyohitajika kwa kufanyia kazi hizo mbili. Kutakuwa na trekta kubwa kubwa
  na mashine za kukamua. Nitanunua magari mazuri ya kusafirisha mazao mengi
  nitakayovuna. Nitawapa vijana wenzangu kazi ili nao wawe na kipato kizuri. Kwa
  jumla, nitahakikisha kuwa vitu vyote anavyohitaji mkulima wa kisasa vipo.
  Mwisho, nitatafuta masoko mazuri na ya kuaminika. Nia yangu hapa ni kuuza
  bidhaa zangu katika masoko yaya haya ya hapa kwetu. Baadaye nitaziuza katika
  masoko, nje ya nchi yetu. Hizi zote zitakuwa ni juhudi za kuendeleza vita vikali dhidi
  ya umaskini au uchochole.

  Zoezi

  1. Orodhesheni vivumishi vyote vilivyomo kifunguni humu kwa kuzingatia aina
      ya kila kivumishi husika.
  2. Tunga sentensi fupi fupi na sahihi ukitumia vivumishi mlivyoorodhesha hapo juu.

  Viwakilishi
  Viwakilishi ama vibadala ni maneno ama viambata (sehemu za maneno)
  vinavyosimama badala ya majina. Kundi hili la maneno huweza kugawika katika
  sehemu mbalimbali ifuatavyo.

  a) Viwakilishi nafsi
  Husimamia nafsi za nomino inayozungumziwa katika umoja au wingi. Kuna aina
  mbili kuu za viwakilishi vya nafsi:

  i) Viwakilishi nafsi huru
  Huwakilisha nafsi iliyo huru, yaani isiyounganishwa na kitenzi katika umoja na
  wingi kwenye sentensi.
  Mfano: nafsi ya kwanza (mimi, sisi), nafsi ya pili (wewe, nyinyi), nafsi ya tatu (yeye, wao).

  Zoezi

  Umoja                                                    Wingi
  1. Mimi ninalima.                                   Sisi tunalima.
  2. Wewe unavuna.                               Nyinyi mnavuna.
  3. Yeye anafyeka.                                Wao wanafyeka.

  ii) Viwakilishi nafsi viambata
  Viwakilishi hivi huambatanishwa na vitenzi.
  Mfano: nafsi ya kwanza (ni-, tu-), nafsi ya pili (u-, m-) nafsi ya tatu (a-, wa-)
  ii) Pia, vipo viwakilishi ambata vya ngeli. Navyo ni:
  b) Viwakilishi vitokanavyo na vivumishi
  Je, unakumbuka vivumishi ulivyosoma hapo juu? Endapo kivumishi husika
  kimetumika badala ya nomino, kivumishi hicho kinakuwa kiwakilishi. Nacho
  kiwakilishi hicho huchukua jina la kivumishi hicho. Mfano:
  i) Viwakilishi vionyeshi
  Hutokana na vivumishi vionyeshi. Tazama vivumishi vionyeshi. Unapoondoa
  nomino katika vivumishi hivyo, unapata viwakilisihi vionyeshi.
  Kumbuka kwamba hufai kutumia nomino na kiwakilishi katika sentensi moja.

  ii) Viwakilishi viulizi
  Viwakilishi hivi vinatokana na vivumishi viulizi.
  iii) Viwakilishi vimilikishi
  Viwakilishi hivi hutokana na vivumishi vimilikishi. Tazama mifano hapa chini.

  Zoezi A

  Tunga sentensi ukitumia viwakilishi mbalimbali.

  Zoezi A

  Soma kifungu kifungu kifuatacho huku ukitambua jinsi viwakilishi vilivyotumiwa.
  Zama hizo, fisi alikuwa jirani ya binadamu aliyependa kulima. Binadamu alimiliki
  shamba kubwa la mihogo. Naye Fisi alikuwa mvivu aliyependa kumtembelea
  binadamu kwake. Alidhani kuwa huyo binadamu naye alimpendana sana. Hata
  hivyo, binadamu hakumpenda sana fisi. Fisi hakupenda kulima bali alipenda sana
  kula.    
                                     
  Siku moja jioni, fisi alimuaga binadamu na kusema,    “Kesho nitaamkia huku kwako ili uniandalie kiamshakinywa! ”Kwa roho ya ndani, mwanadamu alijisemea, ‘Huyu hapendi kufanya kazi, anapenda tu kula. Kwa nini haoni kuwa simpendi?’Akamwambia fisi, “Labda utanipata, labda utanikosa.”
  Fisi kuona kuwa anaweza kukosa mlo alisema, “Basi nitajaribu nije hata mapema zaidi. Kwa namna hiyo tunaweza kula halafu wewe uende shambani. Napenda sana namna unavyopika nyama.” Bila kungoja jawabu, alitoka na kujiendea zake.
  Keshoye, mwendo wa saa kumi na moja asubuhi, fisi alibisha hodi kwa mwanadamu. Naye mwanadamu hakusita kumfungulia mlango. Mwanadamu aliazimia kumfunza fisi adabu.
  “Karibu, karibu kwangu rafiki yangu,” mwanadamu alijibu.
  Naye fisi kwa kusukumwa na njaa yake ya asubuhi pamoja na ulafi wake, alimpita
  tu na kuingia ndani. Harufu ya nyama mle ndani ilimfanya fisi ameze mafunda ya mate.
  “Karibu, karibu kaa,” mwanadamu alimlaki fisi. “Nipe dakika chache tu na chakula
  kitamu na kingi kitakuwa mezani hapa.”
  “Basi fanya haraka. Ninakufa kwa njaa,” fisi alisema.
  Baada ya muda usiokuwa mrefu vile, mwanadamu alikuwa ameandika meza
  kwa kila namna ya nyama ya mifupa. Ohoo! Fisi kuona hivyo, nusura kuirukia
  lakini mwanadamu akamzuia kwa kusema, “Bwana fisi, ili leo ushibe vya kutosha,
  tumbukiza kila sahani mdomoni mwako na umeze tu bila kutafuna.
  ”Hata kabla ya mwanadamu kumaliza usemi wake, fisi alikuwa ametumbukiza
  sahani mbili kinywani mwake!
  “Mbona hiki cha leo ni kikali jinsi hii? Lo! Kinawasha sana! Loooooooooo!”
   Fisi alilalamika.
  Kumbe mwanadamu alijaza pilipili kwenye nyama. Tangu siku hiyo, fisi hakurudi
  tena kwa mwanadamu.

  Maswali
  1. Je, fisi alikuwa mnyama wa aina gani?
  2. Ni kwa nini mwanadamu hakumpenda fisi?
  3. Mwanadamu aliikomeshaje tabia mbaya ya fisi?
  4. Unadhani ni yapi yaliyompata fisi?
  5. Jiunge na mwanafunzi mwenzako. Bainisheni viwakilishi vyote vilivyomo
      katika kifungu mlichosoma hapo juu. Tungeni sentensi sahihi mkitumia
      vivumishi hivyo.

  Vielezi
  Vielezi pia huitwa viarifa. Ni maneno yafafanuayo vitenzi, vivumishi au vielezi
  vingine. Mathalan, ukisema Anatembea haraka, neno 'haraka' linaeleza jinsi
  anavyotembea mhusika. Kwa hivyo, neno hilo linalokuarifu mengi kuhusu
  kutembea ni kielezi.
  Maneno haya hujigawa katika vikundi mbalimbali kama ifuatavyo:

  a) Vielezi vya namna au jinsi
  Haya ni maneno ambayo huarifu jinsi ya kutendeka mambo.
  Mfano: sana, bure, kitoto, vizuri, upesi, kwa miguu, kwa bidii, bwe!
  b) Vielezi vya wakati
  Nayo haya ni maneno yanayofafanua ama kueleza wakati wa kutokea tendo.
  Mathalan, ukisema Mgeni alifika jioni neno jioni ni kielezi cha wakati.
  Vipo vielezi vya wakati vya aina mbili:

  i) Vielezi vya wakati maalumu.
  Mfano: Januari, Disemba, Jumamosi, saa tatu, kesho, leo, mtondo na kadhalika.
  ii) Vielezi vinavyotaja wakati kwa jumla
  Mfano: baadaye, zamani, daima, milele, awali, punde, karibuni, zama hizo.

  c) Vielezi vya kiasi/idadi
  Vielezi vya kiasi ni namna ya maneno ambayo hufafanua vitenzi kwa kujulisha
  limetokea mara ngapi tendo linalotajwa.

  d) Vielezi vya mahali
  Haya nayo ni maneno ama mafungu ya maneno yanayofafanua panapotokea kitendo.
  Mara nyingi, maneno haya huwa ni majina ya mahali.

  Zoezi

  Jiunge na wenzako watatu na mworodheshe vielezi vyote vilivyomo kifunguni humu
  huku mkivitungia sentensi fupi na sahihi.
  Gakwerere alikuwa mfugaji mwenye bidii nyingi sana tangu zamani. Mwanzoni,
  Gakwerere alikuwa akifuga ng’ombe wa kienyeji. Aliwalisha ng’ombe hao uwanjani
  na pembeni mwa mashamba. Hata hivyo, ng’ombe hao hawakuwa wakimpa kiasi
  cha maziwa alichotarajia. Angewakamua mara moja tu kwa siku. Alikata shauri
  kuanzisha ufugaji wa ng’ombe bora wa maziwa.
  Mfugaji huyu aliwapeleka ng’ombe wake wa kienyeji sokoni na kuwauza mnamo
  Novemba. Baada ya kuwauza, aliamka alfajiri na kufunga safari ya kuzuru shamba
  la kisasa la Nyinawumuntu. Bi. Nyinawumuntu alikuwa mfugaji na mkulima
  mashuhuri sana katika eneo hilo alilokaa Gakwerere. Alipofika huko, alimpata
  bibiye yupo na wakaanza kupiga bei. Baada ya kukubaliana bei, alinunua mitamba
  wawili kwa bei nafuu. Alilipa papo hapo kwa sababu hakutaka kuwa na deni.
  Kumaliza hivi tu, yule bibi alimpa Gakwerere gari lake ili alitumie kuwasafirisha
  ng’ombe wake. Gakwere alimshukuru kwa wema wake na akawasafirisha hao
  mitamba wake hadi kwake.
  Alipofika nyumbani kwake, mfugaji huyo alianza kuwalisha ng’ombe wake kwa njia
  za kisasa. Kwa kuwa walikuwa wakilishwa kwa lishe bora ya ng’ombe, haukuchukua
  muda mrefu kuwapandisha. Muda ulipowadia, walizaa ndama wawili wenye afya
  nzuri.
  Baada ya muda usio mrefu, Gakwerere alianza kuvuna matokeo ya jasho lake la kila
  siku. Hakuamini kiasi cha maziwa alichokuwa akikama kila asubuhi na jioni.
  Aliweka akiba kwa muda. Hatimaye, mfugaji huyu alinunua gari. Alitumia gari hilo
  kuwatafutia na kuwabebea chakula ng’ombe hao wake wa gredi.

  E . Matumizi ya wakati uliopo na uliopita na vitenzi vya silabi moja
  i) Matumizi ya wakati uliopo (-na-) na vitenzi vya silabi moja
  Wakati uliopo -na-unaweza kuwa katika hali mbili: Hali hizo ni hali yakinishi na hali
  kanushi. Hali yakinishi ni ya ukubali na hali kanushi ni ya ukatavu.
  Soma sentensi hizi.

  Hali yakinishi
  Hali yakinishi ni hali ya kukubali. Tazama tena mifano iliyopo hapo juu. Vitenzi
  unakufa, anakula, anakunywa, anakuja, anampa na inanyesha vimo katika hali
  yakinishi, yaani hali ya kukubali.
  Hali kanushi
  Nayo hali kanushi ni hali ya kukataa. Itazame tena mifano hapo juu. Vitenzi haufi,
  hali, hanywi, haji, hampi na hainyeshi vipo katika hali kanushi, yaani hali ya kukataa.

  Unaweza kutunga sentensi zaidi za namna hii kama ifuatavyo:

  Kazi ya wanafunzi wawili wawili
  Jiunge na mwenzako. Tafuteni vitenzi zaidi vyenye silabi moja katika kamusi huku
  mkijadiliana mabadilko ambayo hutokea vitenzi hivyo vinapotumiwa katika hali
  kanushi na yakinishi.

  ii) Matumizi ya wakati uliopita -li- na vitenzi vya silabi moja
  Wakati uliopita huonyesha kuwa kitendo kilifanyika muda mrefu uliopita. Wakati
  huu huwakilishwa na -li-. Vitendo husika vinaweza kuwa katika hali yakinishi au
  kanushi. Kama ujuavyo, hali yakinishi ni ya kukubali na hali kanushi ni kukataa.

  Tazama mifano ifuatayo:

  Vitenzi hivyo vipo katika wakati uliopo. Tunaweza kuvigeuza viwe katika wakati
  uliopita kwa kuweka ‘-li-‘ mahali pa ‘-na-‘. Tunapofanya hivyo, tunamaanisha kuwa
  vitendo hivyo vilifanyika muda au wakati uliopita. Tazama jedwali hili.

  Tazama mifano ifuatayo:


  Katika jedwali lililopo hapo juu, vitenzi ulikufa, alikula, alikunywa, alikuja, alimpa,
  na ilimnyeshea vimo katika hali yakinishi au kukubali kwa wakati uliopita. Navyo
  vitenzi haukufa, hakula, hakunywa, hakumpa, haikumnyeshea vimo katika hali ya
  kukataa yaani hali kanushi.

  Mazoezi ya ziada

  Zoezi A

  Jiunge na mwanafunzi mwenzako na mworodheshe vitenzi vinane vya silabi moja
  huku mkivitungia sentensi sahihi katika wakati uliopita. Sentensi zenu zihusiane na
  kilimo na ufugaji. Someaneni vitenzi na sentensi huku mkisahihishiana.

  Zoezi B

  Jiunge na wanafunzi wenzako katika kikundi. Msomeane tungo au hadithi
  mbalimbali zilizopo katika kitabu hiki na vitabu vingine. Mbainishe na kuainisha aina
  za maneno katika tungo hizo (vivumishi, viwakilishi na vielezi) kama vinavyotokea
  katika umoja na wingi pamoja na matumizi ya wakati uliopo na wakati uliopita.
   
                            Maswali ya marudio
  li kujikumbusha mengi ya yale uliyojifunza katika sehemu hii, yajibu vilivyo maswali
  haya yafuatayo yote.
  1. Bila ya kuangalia popote, taja maneno kumi yanayohusu mazao na kumi
      yanayohusu ufugaji huku ukiyaeleza.
  2. Ipo misimu mingapi hapa Rwanda? Ieleze huku ukirejelea upanzi na uvunaji
      wa mimea.
  3. Tazama picha zifuatazo. Eleza misimu kulingana na kila mchoro.

  4. Tunga sentensi sahihi ukitumia msamiati ufuatao:
      a) mahindi
      b) ndizi
      c) kahawa
      d) viazi mviringo
      e) maharagwe
      f ) njugu
  5. a) Jaza kila pengo kwa jina sahihi la kifaa cha kilimo.
       i) Ndoli anafyeka shamba kwa ______________.
      ii) Mkulima yule anatumia _________ la mkono kulimia shamba lake.
     iii) Shamba kubwa hulimwa kwa _______________.
     iv) __________ hutumiwa kukata matawi ya miti shambani.
  6. Tunga sentensi tano fupi ukitumia vifaa mbalimbali vya kilimo ambavyo vinatumiwa katika eneo utokako.
  7. Eleza jinsi unavyopanga kupiga vita uchochole kwa kilimo cha kisasa.
  8. Taja majina kumi ya mifugo nchini Rwanda na uyatungie sentensi sahihi.
  9. Taja chuo cha kilimo hapa nchini ambacho ungependa kukiingia baada ya
       masomo yako huku ukieleza ni kwa nini unakistahi chuo hicho.
  10. Eleza umuhimu wa ufugaji katika jamii unapotoka.
  11. Zipo tamaduni zozote za kikwenu zihusuzo kilimo na ufugaji? Zitaje
       huku ukieleza huo uhusiano.
  12. Taja wanyama kumi wa porini wanaopatikana nchini Rwanda.
  13. Andika majina na sifa za wanyama wafuatao wa porini:

  14. Eleza faida za wanyama wanaoishi porini.
  15. Pendekeza njia zinazoweza kutumiwa kuwavutia watalii wanaozuru mbuga
        zetu za wanyama wa porini.
  16. Eleza maana ya:
       a) nomino
       b) vivumishi
       c) vielezi
       d) viwakilishi
  17. Huku ukitoa mifano, eleza aina nne nne za:
      a) nomino
      b) vivumishi
      c) vielezi
  18. a) Je, vitenzi vya silabi moja ni maneno ya aina gani?
        b) Andika mifano minne ya maneno yenye silabi moja na uyatungie sentensi sahihi.
  19. a) Huku ukitoa mifano, eleza tofauti zilizopo kati ya:
         i) wakati uliopo na wakati uliopita
        ii) hali kanushi na yakinishi
  b) Andika sentensi zifuatazo katika hali yakinishi au kanushi.
      i) Baba anakula mahindi.
     ii) Mahindi hayafi wakati wa kiangazi.
    iii) Ng’ombe hakunywa maji jana.
    iv) Mkulima alimpa ndizi nyingi.
  c) Andika sentensi zifuatazo katika wakati uliopo au uliopita.
     i) Ndoli anakula mihogo.
    ii) Mimi sinywi maziwa.
   iii) Mama alinipa jembe.
   iv) Kuku hao hawakufa.
  20. Kwa ufupi, elezea mambo muhimu uliyojifunza katika sura hii na useme jinsi
        yatakavyokufaidi na jamii.
  Files: 3
 • Sura 2: Utungaji

   

  Mada ndogo: Barua kuhusu matembezi, Barua za kirafiki,

                        Barua za mwaliko, Simu,Tangazo/Ilani.


  A Barua
  Barua ama waraka ni maandishi yaliyopangwa kwa utaratibu na mtiririko maalumu
  kwa minajili ya kuwasilisha ujumbe fulani. Zipo aina mbili kuu za barua: Ipo barua
  ya kirafiki ambayo pia huitwa barua ya kindugu na ipo barua rasmi.
  a) Barua za kirafiki
  Barua ya kirafiki ni barua ambayo huandikiwa mtu ama watu mbalimbali walio na
  uhusiano wa karibu na anayeandika; kama vile rafiki, mzazi, dada na kadhalika.

  Kazi ya wanafunzi wawili wawili
  Jiunge na mwenzako na mjadili barua zenu mlizoandika. Je, waandikiwa walikuwa
  kina nani? Ujumbe ulikuwa upi na ni lugha gani uliyotumia?

  Mifano ya barua za kirafiki
  i) Barua ya mwana kwa mzazi

                                                   

  Ukimwandikia mama barua, barua hiyo ni ya kirafiki

  Zoezi

  Mwandikie ndugu yako barua ukimweleza maendeleo yako katika masomo.
  ii) Barua ya mapenzi

                                    

                

  Barua ya kindugu inaweza kuwa ya mapenzi pia.

  Zoezi

  Jifanye kuwa una zaidi ya miaka kumi na minane. Mwandikie mchumba wako barua
  ukimweleza sababu ya kumpenda na kutaka kumwoa.

  ii) Barua ya kutoa ushauri
  Isitoshe, barua ya kirafiki inaweza kuwa ni ya mzazi anayetoa ushauri kwa mwanawe.


  Zoezi

  Wewe ni mzazi ambaye mwanao amepotoka. Mwandikie barua ya
  kumwelekeza kuepukana na upotovu huo na arudie wema wake wa awali.
  Someni barua zenu mbele ya darasa.

  Sehemu kuu za barua za kirafiki

  Barua za kirafiki huwa na sehemu au muundo fulani maalumu.

  Kazi ya kikundi

  Jiunge na wanafunzi wenzako katika kikundi. Tazameni mifano ya barua za kirafiki iliyotolewa na mingineyo. Jadilianeni kuhusu sifa zinazofanana katika barua zote. 

  Tazama mfano wa muundo wa barua ya kirafiki. Kuna uhusiano gani kati ya yaliyomo na barua za kirafiki ulizosoma? 

           Anwani

          Tarehe 

          Kutaja mwandikiwa

          Utangulizi/salamu 

          Mwili wa barua           

          Hitimisho  

          Jina la mwandishi.

  Barua ya kirafiki huwa na sehemu kuu zifuatazo:
  i) Anwani moja ya mwandishi: Huandikwa juu, pembeni.
  ii) Tarehe: Huandikwa chini ya anwani kwa kuacha nafasi ya mstari mmoja.
  iii) Kutaja mwandikiwa: Huja chini ya tarehe kwa kuacha nafasi ya mstari mmoja.
  iv) Utangulizi: Hujitokeza katika aya ya kwanza. Mwandishi humjulia hali mtu
       anayeandikiwa na wenzake. Pia, husema hali yake.
  v) Mwili wa barua: Mwandishi hupitisha ujumbe wa barua/kuelezea kiini cha
      kuandikwa kwa barua husika.
  vi) Hitimisho/Kufunga barua: Mwandishi huhitimisha barua yake kwa kumtakia
       heri aliyeandikiwa. Jina la mwandishi wa barua huja chini ya hitimisho.

  Zoezi

  Tazama barua iliyopo hapa chini. Je, barua hii ina makosa gani? Andika upya barua
   hii kwa kusahihisha makosa yaliyopo na kuongezea sehemu zinazokosekana.

  Kwa Shangazi Mpendwa,
  S.L.P, 45
  Kigali
  Rwanda

  Wako Mpendwa,

  Ninajua wewe unapenda sana kilimo cha ndizi. Juzi tulisoma kuhusu kilimo bora
  cha ndizi. Mwalimu wetu alitufunza mbinu mpya za kupanda ndizi. Tukifunga,
  nitakutembelea ili nikufunze mbinu hii mpya itakayokupa mavuno mengi zaidi.

  Unisalimie wote waliopo nyumbani. Waambie nitawatembelea wakati wa likizo.

  Kwanza, ningependa kukueleza kuwa ninazidi kutia bidii katika masomo. Juzi
  tulifanya majaribio na niliibuka nafasi ya tatu katika darasa letu. Ninatia bidii zaidi.
  U hali gani? Mimi nipo salama. Nia yangu kuu ya kukuandikia barua hii ni kukujulisha
  kuhusu mambo mawili makuu.

  Kanuni za kuzingatiwa katika uandishi wa barua za kirafiki
  Zipo kanuni mbalimbali za kuzingatiwa wakati wa kuandika barua ya kirafiki.
  Soma kifungu kifuatacho ili kubainisha baadhi ya kanuni hizo.

                

  USANASE: Hujambo, Gabiro?
  GABIRO:     Sijambo Usanase.
  USANASE: Unaonekana mwingi wa huzuni. Pana jambo linalokutatiza?
  GABIRO:    Ni kweli. Ninataka kuandika barua kwa mjomba. Sijui endapo pana
                      kanuni zozote ninazofaa kuzingatia.
  USANASE: Ahaa! Zipo kanuni za kufuatwa wakati wa kuandika barua ya kirafiki.
  GABIRO:    Kanuni hizo ni gani?
  USANASE: Kwanza, hufai kuandika kichwa.
  GABIRO:    Niandike tu moja kwa moja?
  USANASE: Naam. Kabla ya kuandika kiini au mwili wa barua, hakikisha kuwa
                      umeandika anwani yako kama mwandishi.
  GABIRO:    Anwani moja inatosha?
  USANASE: Naam. Chini ya anwani, andika tarehe kisha umtambulishe unayemwandikia.
  GABIRO:    Ninaweza kumtambulisha vipi?
  USANASE: Mtambulishe kwa kudhihirisha uhusiano uliopo baina yenu. Kwa
                      mfano, Kwa Mjomba Mpendwa.
  GABIRO:    Ahaa! Ninakupata vizuri sana. Je, ninafaa kujikita katika ujumbe
                      mmoja mkuu?
  USANASE: Hapana. Una uhuru wa kuzungumzia maudhui mengi. Unaweza
                      kutaja mambo mengi yasiyohusiana. Mfano, unaweza kumwambia
                      kuhusu hali ya anga na masomo shuleni. Baadaye, unaweza
                      kumwuliza kuhusu mazao yake yalivyo shambani na mambo mengi.
                      Uhakikishe kuwa kila maudhui au ujumbe upo katika aya yake.
  GABIRO:    Ninafaa nitumie kiwango gani cha lugha?
  USANASE: Hujafungwa katika kiwango fulani cha lugha. Lugha utakayotumia
                      inategemea uhusiano uliopo kati yako na mjomba au yeyote
                      unayemwandikia.
  GABIRO:    Kwa hivyo si lazima lugha yangu iwe rasmi?
  USANASE: Naam. Si lazima uzingatie kiwango cha juu cha adabu kama ilivyo
                      katika barua rasmi. Hilo halimaanishi kuwa unaruhusiwa kutumia lugha chafu au
                      lugha isiyokuwa na tasfida.
  GABIRO:    Kwa hivyo ninaweza kutumia lugha yenye utani, vichekesho na yenye
                      kuibua hisia ya huzuni, furaha au huruma.
  USANASE: Naam.
  GABIRO:    Je, ninafaa kuzingatia urefu kiasi gani?
  USANASE: Kama nilivyosema hapo mbeleni, una uhuru wa kuzungumzia
                      mambo mengi utakavyo katika barua ya kirafiki. Urefu utategemea
                      jumla ya mambo hayo. Una uhuru wa kuandika barua ndefu au fupi
                     utakavyo. Hakuna urefu maalumu.
  GABIRO:    Nikimaliza, ninafaa kutia sahihi?
  USANASE: La hasha! Barua ya kirafiki si lazima itiwe sahihi.
  GABIRO:     Asante sana rafiki yangu kwa maelezo hayo. Sasa ninaweza kuandika
                      barua yangu.
  USANASE: Karibu. Ukiwa na swali lingine, utaniuliza.

  Zoezi

  Jiunge na mwenzako na muigize mazungumzo yaliyopo hapo juu. Andikeni kanuni za kuzingatiwa katika uandishi wa barua za kirafiki zilizopo kwenye ufahamu.

  Kazi ya kikundi

  Jiunge na wanafunzi wenzako katika kikundi. Andikianeni barua za kirafiki kuhusu mada yoyote mpendayo. Someni barua zenu huku mkisahihishiana.

  b) Barua rasmi

  Tazama michoro hii. Je, mwalimu na wanafunzi hawa wanajadiliana kuhusu nini?
  Je, unajua jinsi ya kuandika barua rasmi?

                          

  Barua rasmi ni barua zinazoandikiwa mtu au watu wenye nyadhifa kwa lengo
  maalumu la kuwasilisha ujumbe rasmi.Mifano ya barua rasmi.

  i) Barua ya kuomba kazi

  Hii ni aina ya barua ambayo mtu huandika wakati anapotaka kuajiriwa mahali. Kuna aina mbalimbali za barua za kuomba kazi.

  Kazi ya wanafunzi wawili wawili

  Jiunge na mwenzako. Jadilianeni kuhusu jinsi ya kuandika barua ya kuomba kazi. Andikeni barua hiyo kwa msingi wa majadiliano hayo.


  Zoezi

  Andika barua ya kuomba kazi yoyote upendayo. Angazia mambo yafuatayo katika barua yako:

  i) jinsi ulivyopata kuwepo kwa nafasi ya kazi hiyo,
  ii) tajiriba yako, wasifu wako mfupi,
  iii) sababu ya kutaka kazi hiyo,
  iv) mambo mapya ambayo utafanya ukipewa nafasi hiyo na kadhalika.                                                                                                                                                                                                                                                                                      

  ii) Barua ya kuomba ruhusa

  Hii ni aina ya barua ambayo mwandishi huomba kupewa fursa ya kutoshiriki katika shughuli fulani muhimu. Unaweza kusema kwa nini hutakuwepo au usiseme.   Zoezi

  Mwandikie mwalimu wako barua ukiomba ruhusa yoyote. Mweleze sababu za kuomba ruhusa hiyo.                                              

  iii) Barua ya huduma

  Barua ya huduma ni aina ya barua ambayo humhitaji mtu, kundi la watu, shirika lisilo la kiserikali au idara ya serikali au kampuni kutoa huduma fulani katika jamii. Wakati mwingine huandikwa kutoa maoni kuhusu hatua ambazo jamii ingependa kuchukuliwa, kwa mfano, idara ya polisi ama hospitali kuweka visanduku vya kupokea maoni kutoka kwa wananchi kuhusu namna wangependa kuhudumiwa kwa ubora zaidi.

  Kazi ya kikundi
  Jiunge na wanafunzi wenzako katika kikundi. Nyinyi ni vijana wanaojihusisha katika
  kufanya utafiti wa mbinu bora za kilimo katika wilaya yenu. Kipeni kikundi chenu
  jina na mchague katibu mkuu. Andikeni barua kwa shirika lolote linalojihusisha
  na kilimo katika eneo lenu. Elezeni shirika hilo kuhusu utafiti mliofanya wa kukuza
  kilimo katika wilaya yenu na msaada mnaohitaji kutoka kwao.

  Aina zaidi za barua rasmi
  Mbali na mifano iliyotolewa, zipo aina zaidi ya barua rasmi. Barua hizo ni kama vile:
  i) Barua ya kuomba nafasi katika shule fulani
  ii) Barua ya kuomba msamaha
  iii) Barua ya shukrani
  iv) Barua ya malalamiko
  v) Barua kwa mhariri
  vi) Barua ya mapendekezo
  vii) Barua ya uteuzi
  viii)Barua ya kusimamishwa au kufutwa kazi.

  Kazi ya wanafunzi wawili wawili
  Jiunge na mwanafunzi mwenzako. Fanyeni utafiti kuhusu jinsi barua zilizotajwa
  hapo juu huandikwa. Kila mwanafunzi aandike mojawapo ya barua hizo kuhusu
  mada yoyote kisha amsomee mwenzake. Sahihishianeni.

  Sehemu kuu na kanuni za barua rasmi
  Barua rasmi huwa na sehemu au muundo fulani maalumu kama ufuatao:
  Anwani ya mwandishi
  Tarehe
  Anwani ya mwandikiwa
  Mtajo/Kutaja mwandikiwa kwa heshima
  Kichwa
  Utangulizi/Kutajwa kwa kiini
  Mwili wa barua
  Hitimisho
  Wako mwaminifu/mtiifu
  Sahihi
  Jina la mwandishi
  Cheo cha mwandishi (ikiwa mwandishi anaandika
  kwa niaba ya shirika fulani, kikundi au kampuni)

  Soma mazungumzo haya na ujibu maswali chini yake.
                                        

  UMUHIRE: Mwenzangu, nieleze kuhusu jinsi ya kuandika barua rasmi.
  NDOLI:       Lazima uandike anwani yako na ile ya mwandikiwa. Anwani yako
                     kama mwandishi huja juu. Unapoandika anwani ya mwandikiwa, ni
                     sharti uandike cheo chake kwanza kabla ya kuandika jina na anwani
                     ya kampuni chini ya cheo chake kama vile,  'MKURUGENZI MKUU,
                     MWENYEKITI, MWALIMU MKUU’ na kadhalika.
  UMUHIRE: Baada ya anwani, ninaandika nini?
  NDOLI:      Unaandika ufunguzi wa barua kama vile Kwa Mbunge Mheshimiwa,
                     Kwa Mheshimiwa, Kwa Meneja Mkuu, Kwa Meneja, Kwa Mgeni wa
                     Heshima na kadhalika. Unaweza kuandika jina lake la pili baada ya
                     Bw au Bi.
  UMUHIRE: Naam! Kwa hivyo, baada ya kutambulisha mwandikiwa, ninaandika
                     kichwa au vipi?
  NDOLI:       Naam, rafiki yangu. Kichwa hudokeza kiini cha kuandika barua yako.
                     Unapoandika kichwa, unaanza kwa kutumia kifupisho MINT: au KUH:
  UMUHIRE: MINT na KUH vinasimamia nini?
  NDOLI:       MINT husimamia Mintaarafu au kwa mintaarafu ya, KUH husimamia
                     kuhusu. Kichwa au mada yako haifai kuzidi maneno sita isipokuwa
                     pale ambapo pana lazima.
  UMUHIRE: Ninapoanza kuandika mwili, ninafaa kusema nini?
  NDOLI:      Ikiwa ni barua ya kuomba kazi, ni vizuri uanze kwa kurejelea tangazo
                    la kazi hiyo au jinsi ulivyopokea kuwepo kwa nafasi hiyo. Baadaye,
                    andika moja kwa moja kiini cha barua hiyo.
  UMUHIRE: Hakuna salamu?
  NDOLI:       Naam. Barua rasmi haina salamu. Unaeleza moja kwa moja kiini
                     cha kuandika barua. Unafaa kujikita katika ujumbe mmoja mkuu,
                     yaani jambo linalokufanya uiandike barua hiyo. Ikiwa unaomba kazi,
                     toa maelezo muhimu kukuhusu. Maelezo hayo yawe na uhusiano na
                     kazi unayolenga kupata. Epuka maelezo mengi yasiyokuwa na manufaa.
  UMUHIRE: Lugha yangu inafaa kuwa ya namna gani?
  NDOLI:       Lugha yako sharti izingatie adabu ya hali ya juu na kiwango cha juu cha urasmi.
                     Lugha yako iwe sahihi. Ikiwa unaandika kwa kalamu, tumia hati nadhifu. Usitaje
                     chochote cha kuonyesha mambo au hisia za kibinafsi au uhusiano wa kibinafsi
                     na unayemwandikia.
  UMUHIRE: Nini huandikwa katika hitimisho la barua hii rasmi?
  NDOLI:       Unaandika tumaini lako la majibu mazuri. Chini yake, unaandika:
                     Wako Mwaminifu au Wako Mtiifu kisha unaweka sahihi. Chini ya sahihi yako,
                     andika jina lako kamili. Ikiwa unaandika kwa niaba ya shirika au kampuni au kikundi,
                     andika cheo chako chini ya jina lako.
  UMUHIRE: Asante kwa maelezo haya.

  Maswali
  i) Je, barua rasmi ina kanuni zipi za kuzingatiwa?
  ii) Linganisheni sehemu na kanuni za kuandika barua za kirafiki na zile za
      kuandika barua rasmi. Jadilianeni kuhusu tofauti zilizopo kati ya barua za
      kirafiki na barua rasmi.

  Kazi ya kikundi
  Jiunge na wanafunzi wenzako. Tazameni mifano ya barua rasmi iliyotolewa na
  mingineyo. Jadilianeni kuhusu miundo ya barua hizo. Andikianeni barua rasmi
  kuhusu mada yoyote.
      
    B. Matangazo mbalimbali                             
  Tangazo ni mpangilio wa maandishi
  kwa mtindo maalumu kwa lengo la
  kupasha ama kupokeza ujumbe fulani
  wa kidharura au muhimu.
  Zipo aina mbalimbali za matangazo:

  i) Matangazo ya biashara
  Matangazo ya biashara ni maandishi
  ambayo yanalenga kutoa maelezo fulani
  kuhusu kitu, bidhaa, mahali au jambo
  kwa ajili ya kuwashawishi wasomaji
  kununuana kutumia bidhaa husika au

  kuzuru mahali husika. Matangazo haya yanaweza pia kuwajulisha watu kuhusu bidhaa mpya zilizoingia sokoni au kuimarishwa kwa bidhaa zilizopo kwa sasa.

  Kazi ya kikundi
  Jiunge na wanafunzi wenzako katika kikundi. Tajeni matangazo mbalimbali
  yaliyomo katika redio, televisheni, magazeti na vibango mbalimbali karibu na
  maeneo mnapoishi. Jadilianeni kuhusu jinsi istilahi au msamiati ulivyotumika
  katika matangazo hayo na malengo ya matangazo hayo. Je, istilahi hizo zimefaulu
  katika kuafikia malengo husika?  Jinsi ya kufika huko
  Unaweza kusafiri angani kwa ndege hadi uwanja wa ndege wa Gisenyi. Hapo,
  waajiri wetu watakupokea kwa tabasamu na unyenyekevu.
  Ikiwa una gari, pitia barabara kuu ya Kaskazini Magharibi kutoka jijini Kigali.
  Itakuchukua saa tatu pekee.
  Tembelea hoteli ya Sabyinyo leo upate uhondo wa burudani.

  Kazi ya wanafunzi wawili wawili
  Jiunge na mwanafunzi mwenzako. Someni tena matangazo yaliyopo hapo juu kwa
  makini huku mkitambua sifa na miundo ya matangazo hayo.

  Sifa na miundo ya matangazo ya biashara
  Soma kifungu hiki na ujibu maswali chini yake.
  Matangazo ya biashara huwa na utangulizi wenye mvuto na hitimisho lenye
  ushawishi. Kumbuka kuwa lengo kuu la tangazo lolote la biashara ni kuwavutia
  wasomaji.
  Yapo matumizi ya takriri. Takriri ni kurudiarudia neno au maneno fulani. Kwa kuwa
  matangazo ya biashara hulenga kutambulisha bidhaa fulani au mahali fulani, bidhaa
  au mahali husika hurudiwarudiwa katika mwili wa tangazo ili wasomaji au wateja
  lengwa wazikumbuke. Pia, jina la bidhaa na kampuni hutajwa na kurudiwarudiwa.
  Watu hupenda sana kusoma maneno mafupi na ni rahisi kuyakumbuka. Maneno
  marefu kwa upande mwingine huchosha na huchukua nafasi kubwa. Matangazo
  ya biashara huandikwa kwa maneno mafupi mafupi yenye mnato na ujumbe mzito.
  Maneno mafupi hupunguza gharama ya matangazo hayo.
  Katika matangazo ya biashara kwenye redio na televisheni, matangazo hayo
  huambatana na sauti ya kimuziki. Sauti hiyo hulenga kuwavutia wanaosikiza
  matangazo hayo. Pia, huchangia katika kupitisha ujumbe uliokusudiwa.
  Wakati mwingine, matangazo hufuata mtindo wa dayalojia. Hapa, watu
  wanaohusika katika kutangaza bidhaa fulani huulizana maswali na kupashana
  ujumbe. Kwa mfano
  MTU I: Je, umejaribu sabuni hii?
  MTU II: Bado
  MTU I: Ijaribu leo. Hii ndiyo suluhisho ya kudumu kwa madoa sugu.
  Matangazo ya biashara pia hutumia lugha ya kushawishi. Lugha hiyo huwa sahihi
  au hukosa usahihi. Lugha inayotumika hutegemea umri, jinsia ya wanunuzi
  wanaolengwa.
  Matangazo ya biashara hueleza ubora wa bidhaa pekee na manufaa yake. Hutilia
  mkazo mambo haya kwa undani na wakati mwingine hutilia chumvi ubora na
  manufaa ya bidhaa husika.
  Matangazo mengi ya biashara hayataji bei ya bidhaa. Pia, hueleza zinakopatikana
  bidhaa zenyewe au jinsi ya kuzipokea mahali unapoishi. Wakati mwingine, hutoa
  mwito wa kutembelewa kampuni husika.

  Zoezi

  1. Taja sehemu kuu za matangazo ya biashara kwa mujibu wa kifungu na
       matangazo ya biashara uliyosoma au kusikia.
  2. Taja kanuni au sifa kuu za kuzingatiwa katika uandishi wa matangazo ya
       biashara.

  Kazi ya kikundi
  Jiunge na wanafunzi wenzako katika kikundi. Fanyeni mradi wa kuandika
  matangazo mbalimbali ya biashara kuhusu bidhaa mtakazojichagulia.

  ii) Matangazo ya mkutano
  Katika matangazo haya, mwandishi hutaja kiini au ajenda za mkutano, mahali pa
  mkutano, tarehe na wakati ambapo mkutano utaandaliwa na maelezo mengine
  muhimu.


  iii) Matangazo kuhusu ziara ya rais
  Ziara ni tendo la kwenda mahali kwa sababu fulani kama vile kuzindua ujenzi wa
  barabara, kuwahutubia wananchi na kadhalika. Nalo tangazo lake linaweza kuwa
  kama hili lifuatalo:


  Zoezi

  Liandike tangazo kwa watu wote waliomo shuleni mwenu kuhusu ziara ya
  waziri wa elimu shuleni humo. Liandike tangazo hilo kwa niaba ya mwalimu mkuu.

  iv) Matangazo ya kuwachagua watu kujiunga na kikosi cha polisi
  Huweza kutokea kwamba serikali inataka kuchagua watu kujiunga na kikosi cha
  polisi. Basi, huweza kulitangaza jambo kwa wananchi.

  Kazi ya wanafunzi wawili wawili
  Jiunge na mwanafunzi mwenzako. Someni tangazo lililopo hapo juu na matangazo
  mengineyo ya mikutano. Jadilianeni kuhusu sehemu muhimu za matangazo ya
  mikutano na kanuni za kuzingatiwa katika uandishi wa matangazo maalumu.

  v) Matangazo kuhusu nafasi za kazi
  Hutolewa kwa lengo la kufahamisha watu kuhusu kuwepo kwa nafasi fulani ya/za
  kazi katika kampuni, shirika ama idara fulani.

  Mfano

  HALMASHAURI YA WILAYA YA NYAGATARE
  Tarehe 3/07/2016.
  NAFASI ZA KAZI
  Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Nyagatare anatangaza kuwepo
  kwa nafasi zifuatazo za kazi:
  1. MWENYEKITI WA BODI YA AJIRA (Nafasi 1)
  Sifa za Mwombaji kazi
  Ni sharti awe:
  i) mkazi wa muda mrefu wa Wilayani Nyagatare,
  ii) na shahada ya uzamifu katika usimamizi,
  iii) mwenye umri wa miaka 35 au zaidi,
  iv) na tajiriba ya miaka 5 katika kusimamia watu katika shirika kubwa tajika,
  v) na rekodi nzuri ya utendakazi,
  vi) mwenye uwezo wa kuwatia motisha wafanyakazi ili kuinua hadhi ya bodi hii,
  vii) mtu mwenye kutoshawishika katika misimamo sahihi yake na ile ya
        halmashauri.
  Wajibu na majukumu
  i) Kutangaza nafasi za ajira,
  ii) Kupendekeza kupandishwa vyeo kwa wafanyakazi,
  iii) Kutoa mafunzo au maelekezo kwa waajiriwa wapya,
  iv) Kupendekeza nyongeza ya mishahara kwa wafanyakazi,
  v) Kutekeleza majukumu mengineyo kama itakavyopendekezwa mara kwa mara.

  Kiwango cha mshahara
  Kitajadiliwa wakati wa mahojiano.
  2. MAAFISA WA UCHUKUZI DARAJA LA II ( Nafasi 5)

  Sifa za mwombaji kazi
  Ili kufuzu katika nafasi hii, unahitajika kuwa na:
  i) shahada katika masuala ya usimamizi wa kibiashara,
  ii) tajiriba ya miaka 3 katika kitengo hiki,
  iii) uelewa wa masuala ya uchukuzi katika forodha na kanuni za barabara,
  iv) rekodi nzuri ya utendakazi,
  v) ufahamu wa matumizi ya kompyuta na mtandao.

  Majukumu
   i) Kutayarisha bajeti na kuendesha uchukuzi,
  ii) Kuhakikisha kuwa takwimu, stakabadhi na kumbukumbu zinazohusu vyombo
      vya usafiri pamoja na mitandao yake zinatunzwa vyema,
  ii) Kukusanya na kuandaa takwimu kuhusu maendeleo ya sekta ya uchukuzi na
      kuziwasilisha kwa wadau ndani na nje ya wilaya,
  iv) Kuweka faili za uchukuzi nchini,
  v) Kukadiria na kushauri juu ya utendaji wa miradi mbalimbali ya sekta ya
      uchukuzi.

  Kiwango cha mshahara
  Kitajadiliwa wakati wa mahojiano.

  Ikiwa una sifa hizi na ungependa kujiunga nasi, tuma barua ukionyesha kazi
  unayoomba na uambatanishe wasifukazi wako wa hivi karibuni, nambari ya/za
  simu na warejelewa watatu kwa mawasiliano wakati wa mchana. Tuma kwa anwani
  hii kabla ya usiku wa manane ya tarehe 23/08/2016.
  J.M. Gatete,
  Halmashauri ya Wilaya ya Nyagatare,
  S.L.P. 3013,
  NYAG ATA R E .    
  Tanbihi
  Halmashauri hii ni huru katika utoaji wa nafasi sawa za kazi bila kubagua yeyote.
  Ombi litakataliwa moja kwa moja endapo anayeomba kazi atahonga afisa yeyote
  kwa ajili ya kupendelewa.

  Zoezi

  Tafuta matangazo mbalimbali kuhusu nafasi za kazi katika magazeti, mabango na
  kadhalika. Soma matangazo hayo na ubainishe sifa zayo na kanuni zilizozingatiwa
  katika uandishi huo.

  Kazi ya kikundi
  Jiunge na wanafunzi wenzako katika kikundi. Huku mkirejelea matangazo
  mbalimbali, jadilianeni kuhusu tofauti zilizopo katika matangazo hayo mkizingatia:
  i) sifa
  ii) sehemu kuu
  iii) kanuni
  iv) msamiati
  v) malengo

  C . Ilani
  Ilani ni tangazo ambalo hutahadharisha au kuarifu kuhusu aina ya jambo ama tukio
  ambalo linastahili kuepukwa, lau sivyo madhara hutokea.
  Ilani huwa na wazo moja tu maalumu. Hutolewa mahali penye shughuli nyingi ama
  palipo na watu wengi kama vile shuleni, chuoni, kanisani msikitini na kadhalika.
                    
  Ilani mara nyingi huwa na mtindo rasmi. Ilani nyingi huwekwa katika mabango
  makubwa, magazetini, kwenye majarida na kadhalika.

  Mifano

  i) Ilani kuhusu mkurupuko wa ugonjwa
  ILANI
  WIZARA YA AFYA, KUPITIA HOSPITALI KUU YA MKOA,
  INAWATANGAZIA KUZUKA KWA UGONJWA HATARI WA
  KIPINDUPINDU.
  WATU WOTE WANASHAURIWA KUZINGATIA USAFI WA MWILI NA MAZINGIRA.
  ILI KUJIKINGA KUTOKANA NA MAAMBUKIZI YA UGONJWA HUU
  HATARI, MAMBO YAFUATAYO NI SHARTI YAZINGATIWE:
  i) KILA MTU AHAKIKISHE ANATUMIA CHOO.
  ii) KILA MTU ANAWE MIKONO KWA MAJI SAFI NA SABUNI BAADA YA KUTOKA CHOONI.
  iii) HAKIKISHA UNAKULA KATIKA MAHALI SAFI
  iv) WATU WASILE KWENYE MIKAHAWA.
  v) ALIYE NA DALILI ZA KUENDESHA NA KUTAPIKA AKIMBIZWE MARA
      MOJA HOSPITALINI KWA UCHUNGUZI NA MATIBABU.
  vi) ALIYEAMBUKIZWA APEWE MAJI MENGI YA KUNYWA WAKATI
       ANAPOPELEKWA HOSPITALINI.
  vii) KILA MTU ACHEMSHE MAJI YA KUNYWA.
  viii)MTU YEYOTE ALIYEAMBUKIZWA ATENGWE NA WATU WENGINE.
        ONYO:
  MTU YEYOTE ATAKAYEPATIKANA AKIUZA CHAKULA KATIKA
  MAENEO WAZI ATASHTAKIWA.

  ii) Ilani kuhusu unywaji wa pombe

  Mfano

  POMBE HATARI
  Serikali, kupitia wizara ya afya, inawatahadharisha wananchi kuhusu kuzuka kwa
  pombe hatari ya SUMEDA inayonywewa sana katika sehemu mbalimbali nchini.
  SUMEDA ni pombe hatari kwa afya yako kwa kuwa inatengenezwa kwa kutumia
  dawa ya kuhifadhi maiti na kemikali nyingine hatari.
  Pombe hii hatari imesababisha vifo vya watu zaidi ya 50, kuwapofusha
  wengine wengi pamoja na kutoa mimba.
  Atakayepatikana akiuza ama kunywa aina hii ya pombe atakamatwa.
  Ofisi ya mkuu wa wilaya.

  iii) Ilani ya kutokanyaga nyasi

  Mfano

                                                ILANI
                        HAPANA RUHUSA KUKANYAGA NYASI
                                           NA MENEJIMENTI

  Zoezi

  i) Tazama mifano ya ilani zilizotolewa hapo juu. Je, ilani hizo zina sifa gani?
  ii) Andika ilani kuhusu mada yoyote upendayo.

  Kazi ya wanafunzi wawili wawili
  Jiunge na mwanafunzi mwenzako. Andikeni ilani kuhusu mada hizi na mziweke
  kwenye maeneo husika shuleni.
  i) Kutokanyagwa kwa sehemu fulani zenye nyasi.
  ii) Kuwepo kwa mjadala kuhusu: mbinu za kisasa za kilimo ni bora kuliko mbinu
      za jadi za kilimo.
  iii) Kuwafahamisha wanafunzi kunawa mikono watokapo msalani.
  iv) Kuzingatia usafi jikoni

  D. Mialiko
  Mwaliko ni mwito wa kumtaka mtu au watu kuhudhuria shughuli au hafla fulani.
  Wito wa namna hii huweza kufanywa kwa njia ya barua ya kirafiki au barua rasmi
  na hata kwa matangazo.

  Kazi ya kikundi
  Jiunge na mwanafunzi mwenzako na mchunguze mchoro huo uliopo hapo chini.
  Jadilianeni kuhusu mambo yaliyomo ubaoni.
                                       
  Mifano ya mialiko
  i) Mwaliko wa harusi
  Je, umewahi kualikwa katika harusi au kuona kadi ya mwaliko wa harusi? Je,
  mwaliko huo ulikuwa na mambo gani?
  Mwaliko wa harusi huwaomba jamaa na marafiki kuhudhuria sherehe ya harusi.
  Kadi za mialiko ya harusi huchukua miundo na sura tofautitofauti. Miundo ya
  kadi hizo hutegemea ubunifu wa anayeziunda au mapendekezo ya maarusi au
  waandalizi wa harusi.

  Kazi ya kikundi
  Jiunge na wanafunzi wenzako. Tazameni mialiko ya harusi iliyotolewa hapa chini.
  Jadilianeni kuhusu mambo yaliyomo katika mialiko hiyo.

  Mfano
              

    
              A .                    B. 


  Kanuni za kuzingatiwa katika uandishi wa mwaliko wa harusi
  Unapoandika mwaliko wa harusi, ni sharti utaje majina ya watu wanaofunga ndoa,
  tarehe ya harusi, mahali pa harusi na wakati sherehe itakapoanza.
  Watu mbalimbali huandika mialiko ya harusi kwa njia tofauti tofauti. Mara
  nyingi, kadi hutumika. Wao hurembesha kadi za harusi ili kuwavutia wasomaji
  na kuonyesha mapenzi yaliyopo kati ya maharusi. Wengine hunukuu maandiko
  takatifu yanayotaja mapenzi na ndoa. Almuradi, kila mwaliko wa harusi huwa na
  umbo lake maalumu.

  Kazi ya kikundi
  Jiunge na wanafunzi wenzako na mchukulie kuwa nyinyi ni wanachama wa kamati
  inayoandaa harusi. Mna nia ya kutengeneza kadi nzuri ya mwaliko wa harusi. Kila
  mmoja achore kadi ya mwaliko na aweke ujumbe wake. Linganisheni mialiko yenu
  na mchague mwaliko bora zaidi kisha muufanye urembeke zaidi. Onyesheni na
  mlisomee darasa zima kadi yenu.

  ii) Mwaliko wa kutembelea mbuga ya wanyama
  Mwaliko kama huu huchukua umbo la barua rasmi.

  ii) Mwaliko wa maonyesho ya vitabu

                      

    Zoezi

  i) Soma tena barua za mialiko hapo juu. Taja mambo muhimu yaliyozingatiwa
     katika uandikaji wazo.
  ii) Mwandikie aliyekuwa mwalimu wako barua ya kumwalika kwenu kwa
      sherehe ya kukuaga kwa safari ya kwenda ng’ambo kusoma.

  Zoezi la ziada
  Andika barua za mialiko kuhusu mada yoyote.

  E . Aina za alama za uandishi na matumizi yake
  Wenzetu wanapozungumza, tunaweza kutambua wanapomaliza usemi wao kwa
  kusikia sauti zao. Lakini katika uandishi, hakuna sauti. Badala ya sauti, zipo alama
  za uandishi ambazo hutumiwa kuwakilisha sauti katika uandishi. Kutokana na
  alama hizo, tunatambua kama usemi umekwisha, kuulizwa swali, kushangaa na
  kadhalika. Pia, tunaposoma, tunajua wapi tunafaa kupumua kidogo, kushusha au
  kupandisha sauti na kadhalika.
  Alama hizi huitwa viakifishi. Hivyo basi, viakifishi ni alama zinazotumiwa katika
  maandishi ili kuleta maana ikusudiwayo katika matini mbalimbali kama vile
  sentensi, aya, mtungo, barua, mialiko, matangazo, ilani na kadhalika.

  Aina za viakifishi
  Nukta (.)
  a) Huwekwa mwishoni mwa sentensi. Kwa mfano:
     i) Nimechoka.
     ii) Waziri mkuu wa Uchina amewasili mjini Kigali.
  b) Hutumiwa kuonyesha ufupisho wa maneno. Kwa mfano:
     i) S.L.P. – Sanduku la Posta
     ii) Bi. – Bibi
  c) Hutumika kubainisha saa na dakika au tarehe. Kwa mfano:
     i) 3.20 – saa tisa na dakika ishirini
     ii) 14.5.2016- tarehe kumi na nne, mwezi wa tano, mwaka wa elfu mbili na kumi na sita
  d) Hutumiwa kuonyesha vipashio vya pesa. Kwa mfano:
      Sh. 10.50 – shilingi kumi na thumuni hamsini
  e) Zikitumiwa mara tatu mfululizo (...), huonyesha kutokamilika kwa sehemu
      husika. Kwa mfano:
                      Nitakupa lakini ni sharti...
  Mkato/koma ( , )
  a) Hutumiwa kuonyesha pa kutua kwa muda mfupi katika sentensi. Kwa mfano:
      i) Nilipowasili nyumbani, nilienda kuteka maji kisimani.
     ii) Kwa kuwa tulijiandaa vilivyo kwa mtihani wa kitaifa, tulipita.
  b) Hutumiwa kutenga maneno yaliyo katika orodha:
      i) Kwenda sokoni ununue mboga, nyama, mafuta, na unga.
      ii) Mwanafunzi huyu ni mtiifu, mwerevu, mtanashati, na mwenye bidii.
  c) Hutumiwa kubainisha sehemu mbili za sentensi zilizo kinyume:
      i) Umoja ni nguvu, utengano ni udhaifu.
      ii) Aliniambia atakuja, hakuja.
  d) Hutumiwa kabla ya alama za mtajo. Kwa mfano:
      Mama akasema, “Niletee chumvi.”
  e) Hutumiwa wakati sentensi inapoanza kwa kiunganishi. Kwa mfano:
      Kweli, alikuwa mtu mwovu.
  f ) Hutumiwa unapoita mtu ili kupata usikivu wake kabla hujamwambia
      chochote. Kwa mfano:
      Nkusi, niletee kalamu.
  g) Hutumiwa unapokubali au unapokataa kitu. Mfano:
     i) Ndio, nitakuja.
     ii) Hapana, sitakulipa.

  Nukta mbili/koloni (smile
  a) Hutumiwa kutanguliza maneno yaliyo katika orodha.

  Kwa mfano:
      i) Nenda kaniletee: kalamu, karatasi na kifutio.
      ii) Amenunua: machungwa, sukari, na ndizi.
  b) Hutumiwa kuashiria maneno ya msemaji badala ya alama za mtajo hasa katika
       uandishi wa mazungumzo au tamthilia.
      i) Mama: Lazima uniambie ulikokuwa tangu jana.
     ii) Mwalimu alisema: Ingieni darasani.
  c) Hutenganisha numerali za saa.

  Kwa mfano:
         4:10 – saa kumi na dakika kumi
  Nukta na kituo (;)
  a) Hutumiwa kuunganisha vishazi vikuu bila kutumia kiunganishi. Kwa mfano:
      Sikwenda Kayonza; nilienda Kirehe.
  b) Hutumiwa kumpumzisha msomaji katika sentensi iliyo ndefu ili apumzike
      zaidi kuliko pale inapotumiwa koma. Kwa mfano:
      Alipofikiri sana, alitanabahi kuwa hakikuwepo cha kutorokwa; yeye angeweza
      kuondoka nyumbani au kumwacha mumewe, aende popote kufanya lolote.
  Kistari kifupi (-)
  a) Hutumiwa kuonyesha kuwa neno linakatwa kwa vile limefika ukingoni mwa
       mstari husika na bado linaendelea katika mstari unaofuatia.
       Tanbihi: Neno la silabi moja halikatwi.
  b) Hutumiwa kuunga maneno yanayojenga neno moja. Mtindo
       huu aghalabu hujitokeza katika maneno yenye asili ya kigeni. Kwa mfano:
      i) Idd-el-Fitri
      ii) Dar-es-Salaam
  c) Huweza kutumiwa badala ya koma. Kwa mfano:
      Nyimbo za asili-hasa rumba-zinapendwa na wengi.

  Alama ya mshangao (!)
  Hutumiwa kuashiria mahangaiko ya moyo kama vile hasira, hofu, mshangao na
  kadhalika.
         i) Lo! Mwanafunzi ameangusha kitabu cha mwalimu matopeni.
         ii) Wamefungwa mabao kumi kwa nunge!
  Alama ya kuulizia/kiulizi (?)
  a) Hutumiwa mwishoni mwa sentensi kuonyesha kuwa sentensi hiyo ni swali.

  Mwa mfano:
  Unaitwa nani?
  b) Hutumiwa kuonyesha ukosefu wa uhakika kuhusu jambo kama vile mwaka.
      Kwa mfano:
      Shule hii ya Tumaini ilianzishwa 1992 (?)

  Mabano/parandesi egg
  a) Hutumiwa kufunga maneno ya ziada katika sentensi. Kwa mfano:
      Nyamata (makao makuu ya Bugesera) inakua kwa kasi.
  b) Hutumiwa mwandishi anapotaka kutoa ufafanuzi kwa lugha nyingine tofauti
       na ile anayoitumia.
  Kwa mfano: Walowezi (settlers) walifukuzwa
  c) Hutumiwa kufungia herufi za kuorodhesha. Kwa mfano:
       (a) huelimisha,                  (b) huburudisha,                (c) huonya

  Mkato (/)
  Hutumiwa kuonyesha kuwa mojawapo ya vitu vilivyotajwa chaweza kutumiwa
  badala ya hivyo vingine.
  Tazama: Abera alishangaa/aliduwaa
  Mtajo: (“ ” au ‘ ’)
  Hutumiwa kuonyesha maneno halisi ya mzungumzaji. Kwa mfano:
  “Nitafika kesho jioni,” alisema mdogo wake.
  Herufi kubwa (H)
  Hizi ndizo alama za uandishi zinazotumiwa sana kuliko nyingine zote. Hutumiwa
  kila baadaya herufi kubwa.
  Mama anapika.

  Zoezi

  Kiakifishe kifungu kifuatacho
  Ilikuwa asubuhi na mapema bw butera alipotoka kwake kwenda kazini fikirani
  mwake alijikumbusha pindi nikifika ofisini nitaomba ruhusa niende nimlipie binti
  yangu karo
  aliabiri gari linaloelekea ruhango baada ya mwendo mfupi tu lo gari hilo lilipata
  ajali liligongana na lori japo ng'ombe waliokuwemo njiani walikufa takriban wote
  abiria walipata majeraha madogo madogo lakini ililazimu wapelekwe hospitalini
  hivyo butera hakutimiza azma yake

  Mazoezi ya ziada

  Zoezi A

  Andika kifungu cha habari kuhusu mada yoyote ukitumia alama za uandishi kwa
  usahihi.


  Zoezi B

  Jiunge na mwanafunzi mwenzako na msome vifungu mbalimbali vya habari
  vilivyomo katika kitabu hiki, magazeti, na vitabu vinginevyo. Bainisheni na kuainisha
  alama mbalimbali za kuakifisha zilizotumika na jinsi zilivyotumiwa.

                                              Maswali ya marudio
  1. Eleza maana ya barua ya kirafiki.
  2. a) Taja watu watano wanaoweza kuandikiwa barua ya kirafiki.
      b) Mwandikie mmoja wa hao uliowatajia barua ya kirafiki.
  3. Zitaje sehemu zote kuu za barua ya kirafiki huku ukizieleza.
  4. Eleza maana ya barua rasmi.
  5. Taja aina tano za barua rasmi.
  6. Mwandikie Mwalimu Mkuu wa shule ya msingi ulikosomea ukiomba nafasi ya
       kufunza katika shule hiyo.
  7. Zitaje sehemu kuu za barua rasmi.
  8. Eleza kanuni za kuzingatiwa wakati wa kuandika barua rasmi.
  9. Eleza tofauti zilizopo kati ya barua rasmi na barua ya kirafiki.
  10. Kwa maneno yako mwenyewe, eleza tangazo ni nini.
  11. Ipo tofauti gani kati ya matangazo na barua rasmi?
  12. Eleza tofauti kati ya tangazo la tanzia na tangazo la mkutano.
  13. a) Ilani ni nini?
        b) Andika ilani utakayoweka msalani ili kuwatahadharisha wanafunzi
             wenzako kuhusu madhara ya kutonawa mikono baada ya kutoka msalani.
  14. a) Eleza sifa za matangazo ya biashara.
        b) Andika tangazo la biashara kuhusu bidhaa upendayo.
  15. Eleza umuhimu wa mwaliko.
  16. Je, kuakifisha ni kufanya nini?
  17. Eleza umuhimu wa uakifishaji.
  18. Yataje kwa mifano matumizi matano ya nukta.
  19. a) Eleza maana ya mtajo.
        b) Andika mifano miwili ya matumizi ya mtajo.
  20. Eleza kwa ufupi mambo muhimu uliyojifunza katika sura hii. Taja jinsi mambo
        hayo yatakavyokusaidia na kuisaidia jamii yako. • Sura 3: Matumizi ya lugha katika mazingira mbalimbali

  Mada ndogo: Rejesta za mpira na burudani

  A   Rejesta mbalimbali nchini Rwanda 
  Rejesta au sajili ni lugha inayotumiwa mahali ama katika hali fulani na wala haiwezi
  kuhamishwa kutoka mazingira yale na kutumiwa katika mahali pengine. Lugha hizi
  hutofautiana kwa misingi ya msamiati, muundo wa sentensi na kadhalika. Kutokana
  na tofauti hizi, tunapata rejesta za aina mbalimbali. Baadhi ya rejesta hizo ni kama
  hizi zifuatazo.

  i) Rejesta ya mpira wa miguu
  Mpira wa miguu pia huitwa kandanda, soka au kambumbu. Huu ni mchezo
  maarufu sana hapa nchini Rwanda na duniani kote. Kwa mfano, mashindano ya
  kombe la dunia hutazamwa na watu wengi sana kote duniani. Mashindano hayo
  huandaliwa kila baada ya miaka minne. Pia, yapo mashindano ya Bara la Afrika,
  Kombe la Kagame, ligi mbalimbali na kadhalika.
  Baadhi ya watu hufuatilia mechi mbalimbali kupitia redio au televisheni. Wapo
  wanahabari ambao hutangaza mpira kupitia vyombo hivyo. Rejesta ya mchezo
  hujitokeza kupitia matangazo hayo.

  Kazi ya wanafunzi wawili wawili
  Jiunge na mwanafunzi mwenzako. Tazameni mchoro huu. Jadilianeni kuhusu
  yaliyomo michoroni na myahusishe na mazingira yenu.

                                  

                  

  Soma kifungu hiki na ujibu maswali chini yake. 

  Matangazo ya kandanda sehemu I

  Hujambo msikilizaji. Karibu katika matangazo haya ya moja kwa moja ya kabumbu.
  Ni mimi mtangazaji wako, Teta. Huu ni mchuano wa fainali ya kuwania kombe la
  Fahari ya Rwanda kati ya shule ya wasichana ya Elimu Bora na Tusonge Mbele.
  Timu hizi mbili ni wapinzani sugu tangu jadi. Elimu Bora inajivunia historia nzuri
  kwa kushinda kombe hili mara kumi. Wao ndio bingwa tetezi. Tusonge Mbele
  imeshinda kombe hili mara tatu. Mwaka jana walitimuliwa katika nusu fainali.
  Katika awamu hii, wana rekodi ya kutoshindwa katika mechi zote hadi kufikia
  fainali. Je, rekodi hiyo itavunjwa na Elimu Bora?
  Naona timu zote mbili zikiingia uwanjani tayari kwa pambano. Kwa sababu ya muda
  sitataja majina ya wachezaji wote. Nitayataja kadri wanavyozidi kucheza. Kwa ufupi,
  kila timu ina golikipa mmoja. Elimu Bora wameweka wachezaji watatu katika safu
  ya ulinzi nao Tusonge wanawachezesha wachezaji wanne katika safu hiyo hiyo.
  Timu ya Elimu Bora wametia wachezaji watano katika kiungo cha kati nao Tusonge
  wanawachezesha wachezaji watatu. Elimu Bora wana washambulizi wawili nao
  Tusonge wana washambulizi watatu katika safu ya mashambulizi. Timu zote mbili
  zina wachezaji wa akiba watano. Refa mkuu anapuliza kipenga nao wasaidizi wake
  wawili wanakimbia pembeni mwa uwanja kuinua kijibendera. Mmoja anakimbia
  kushoto naye mwingine anakimbia kulia.
  Manahodha wa timu zote mbili wapo pale katikati ya uwanja kurusha sarafu ili
  kuamua timu inayoanzisha mpira. Mashabiki wa timu zote mbili wanaimba nyimbo
  za kushangilia timu zao. Nao makocha wao wamekaa pembeni mwa uwanja
  kushuhudia wasichana wao wakimenyana.
  Naam, refa anapuliza kipenga. Mpira unaanzishwa pale na Ikirezi na Uwamwiza
  wa timu ya Elimu Bora. Ikirezi anapiga pasi kwake Gwiza. Gwiza anapiga chenga.
  Anaangalia aupige wapi. Anapiga pasi safi kwake Umuliza. Umuliza na mpira.
  Umuliza anakwenda. Anapiga shoti ndefu kuelekea lango la Tusonge. Munyana
  anajibu kombora kwa kichwa. Mpira unakuwa mwingi na kutoka nje.
  Hee! Hee! Elimu Bora wameanza mchuano huu kwa kasi mno. Wanatafuta bao
  la mapema. Kamaliza anarusha ngoma ile kwake Muteteri. Muteteri anateleza
  na kuanguka. Refa anasema twendelee. Mutoni anachukua mpira. Tusonge
  wanafanya shambulizi la kujibu. Kamiza kwake Umuhire. Umuhire...Umuhire na
  mpira. Umuhire anakwenda. Umuhire anavuka mstari wa katikati. Anatoa pasi safi..
  go..go..ah! Kijibendera kipo juu. Tona amejenga kibanda katika ardhi ya wenyewe
  pasi ruhusa. Lo! Leo kuna kazi hapa.
  Msamiati
  kabumbu – mchezo wa mpira wa mguu/kandanda
  mchuano – mashindano baina ya timu mbili
  fainali – shindano la mwisho kabisa la kutafuta mshindi
  kuwania kombe – kushindania kombe/tuzo katika mchezo
  wapinzani – kikundi cha watu wanaoshindana na wengine
  bingwa tetezi – timu ambayo iliibuka mshindi/kuchukua kombe katika awamu
                           iliyopita ya shindano fulani.
  nusu fainali – mchezo unaotangulia fainali ambapo washindi hucheza katika fainali
  safu ya ulinzi – wachezaji ambao huzuia wapinzani kufunga bao
  kiungo cha kati – wacheza ambao hucheza sana katikati ya uwanja
  washambulizi – wachezaji ambao hucheza karibu na lango la wapinzani ili wafunge bao
  wachezaji wa akiba – wachezaji ambao hukaa nje ya uwanja na ambao huingizwandani kuchukua nafasi
                                      za wenzao waliopata jeraha au kuchoka
  kuinua kijibendera – kuonyesha kuwa mchezaji amekiuka kanuni za mchezo
  kurusha sarufi – kuamua timu gani inaanzisha mchezo kwa kurusha sarafu juu.
  anapiga pasi – mchezaji mmoja kumpigia mwenzake mpira
  anapiga chenga – kumhepa au kumpita mpinzani kwa mpira
  anapiga shoti – kupiga mpira kuelekea lango la mpinzani
  anajibu kombora – kuzuia mpira kwa kuupiga kuelekea upande wa pili
  mpira unakuwa mwingi – mpira kukosa kuthibitiwa na wachezaji
  mpira umetoka nje – mpira kuenda nje ya mstari wa nje uwanjani
  bao – mpira kuingia ndani ya lango
  shambulizi la kujibu – wachezaji kuelekeza mpira kwa kasi kuelekea lango la
                                      wapinzani punde tu baada ya mpira kuelekezwa
                                      langoni mwao
  kujenga kibanda/kuotea – kuvunja kanuni za ushambulizi kwa kushambulia
                                            ghafla nyuma ya mchezaji wa mwisho wa timu pinzani

  Zoezi

  1. Tunga sentensi sahihi ukitumia msamiati uliotolewa maelezo hapo juu.
  2. a) Orodhesha na utoe maana ya maneno yote katika rejesta ya kandanda
          kifunguni humu lakini ambayo hayakuelezwa hapo juu.
      b) Tunga sentensi ukitumia msamiati uliotaja hapo juu.

  Kazi ya kikundi
  Wewe ni mtangazaji wa mpira wa miguu. Andika matangazo ya mchezo kati ya
  timu zozote mbili upendazo. Baada ya kuandika, jiunge na mwanafunzi mwenzako.
  Kila mmoja amsomee mwenzake matangazo yake.

  Sifa za rejesta ya mpira wa miguu
  Tazama matangazo ya mpira katika kifungu ulichosoma. Je, pana sifa gani katika
  rejesta hiyo?
  Zifuatazo ni orodha ya sifa za rejesta ya mpira wa miguu.
  i) Hujaa jadhba hasa baada ya mchezo kuanza,
  ii) Hujaa mazungumzo ya kuhamisha ndimi ambapo baadhi ya maneno ya
      Kiingereza na hata kienyeji hutumiwa,
  iii) Huwa na lugha ya kuchekesha na kuburudisha wanaoisikiliza,
  iv) Hujaa maoni mbalimbali kuhusu nani atashinda, nani mchezaji bora zaidi,
       na kadhalika,
  v) Huwepo kurudiarudia maneno kama vile majina ya wachezaji, dakika zilizopita,
      mabao yaliyofungwa na kadhalika,
  vi) Huwa na lugha ya kuibua hisia na kumfanya mtu kuingiwa na mahangaiko ya moyo,
  vii) Sentensi fupi fupi huweza kutumika pamoja na taswira ya kuchora picha kamili ya
       yanayotendeka.

  Kazi ya wanafunzi wawili wawili
  Jiunge na mwenzako mmoja. Someni kifungu hiki ili mbainishe rejesta ya mpira wa
  miguu na sifa zao.
  Matangazo ya kandanda sehemu II
  Mlinda lango wa Elimu Bora anaenda kupiga mpira wa madhambi. Anapiga kombora
  ndeeeefu na kutoka nje. Munyana anarusha ngozi iliyowambwa na kutengenezwa mpira.
  Kamiza anapiga chenga. Anatoa pasi kwake Usanase. Usanase anakwenda.
  Anaingia ndani ya kijisanduku. Hatari katika lango la Tusonge. Hatariiiii! Lo! Kayitesi
  ananawa mpira. Refa anasemaje. Naam, kipenga kinapulizwa. Refa anawapa Elimu
  Bora penalti. Shangwe na vifijo kutoka kwa mashabiki wa Elimu Bora. Kayitesi
  anaonyeshwa kadi ya manjano. Kayitesi amecheza rafu. Achunge asionyeshwe kadi
  nyingine ya manjano kwani atatolewa uwanjani.

  Haya! Tuone jinsi mambo yatakavyokuwa hapa. Refa anahesabu miguu kumi na
  miwili kutoka lango la Tusonge. Anaweka mpira chini. Ikirezi amesimama nyuma
  ya mpira ule tayari kupiga mkwaju wa penalti. Mlinda lango wa Tusonge, Kabatesi,
  amesimama mbele ya wavu. Refa anapuliza kipenga. Ikirezi anapiga hatua mbili
  tatu nyuma. Anapiga...go...goo... Nje! Heeee! Heee! Ikirezi ameshindwa kutikisa
  wavu. Alipiga kombora zito. Kabatesi akaruka na kuupiga mpira ule ukapitia juu ya
  mtambaa panya wa goli hadi nje. Kona! Kona ile inapigwa kutoka kushoto wa goli
  la Tusonge.
  Dakika zilizokatika hapa ni dakika kumi na tano. Bado dakika thelathini kipindi
  cha kwanza kikamilike. Tutakupa nafasi ya kuwasiliana nasi wakati wa mapumziko
  ambao utachukua dakika kumi na tano. Baadaye tutarudi hapa kwa kipindi cha
  pili ambacho kitachukua dakika nyingine arubaini na tano pamoja na dakika za
  nyongeza kutoka kwa refa mkuu. Ikiwa timu hizi zitatoka sare baada ya kipindi
  cha lala salama, dakika thelathini za ziada zitaongezwa. Ikiwa bado mshindi
  hatapatikana, watapiga penalti ya kuamua mshindi. Mshindi na mshinde sharti
  wapatikane leo kwa sababu hii ni fainali.
  Umuliza anapiga kona safi pale. Uwamwiza anakimbilia mpira ule. Anapiga kichwa..
  go..goo...goooooool! Mpenzi msikilizaji, hayawi hayawi huwa! Hatimaye Elimu
  Bora wamepata goli la kwanza. Uwamiza amecheka na wavu. Yeye ndiye mfungaji
  bora kufikia sasa. Mashabiki wote wa Elimu Bora na makochi wao wameacha viti
  vyao. Mashabiki wa Tusonge wameinamisha vichwa vyao. Wachezaji wa Tusonge
  wamepandwa na mori. Wamemzingira refa mkuu. Wanadai kuwa Uwamwiza
  alikuwa ameotea. Nahodha wao, Mutoni, ambaye ni beki wa kupanda na kushuka
  anammiminia refa maneno makali. Refa anatia mkono katika mfuko wa nyuma
  ya kaptura na kuchomoa kadi nyekundu. Salaale! Mutoni ameonyeshwa kadi
  nyekundu kwa kukosa adabu. Anasindikizwa nje ya uwanja. Timu ya Tusonge
  wamebaki na wachezaji kumi pekee. Je, itakuaje?

  i) Rejesta ya burudani
  Kama ujuavyo, burudani ni shughuli ifanywayo kwa ajili ya kuchangamsha na
  kufurahisha watu. Nayo mazingira ya namna hii yana msamiati wake ambao ndio
  lengo la sehemu hii.
  Tazama mchoro huu na ueleze mambo yanayojiri katika mchoro wenyewe.
                                                       
  Soma kifungu hiki cha habari na ujibu maswali chini yake.
  MFAWIDHI:Leo ni leo! Asemaye kesho....?
  WATU:        Ni mwongo!
  MFAWIDHI:Hapana! Asemaye kesho hayuko hapa. (Watu wanacheka) Leo showhii itakuwa ya kukata na shoka.
                     Kama huna shoka sijui utakata na nini.
  MTU I:        Tutakata na wembe.
  MFAWIDHI: Wembe utavunjika. (Watu wanacheka) Tuna wasanii wanaotajika ambao wamefika hapa kututumbuiza.
                      Mko tayari kuvunjika mbavu?
  WATU:        Ndiyooooo!
  MFAWIDHI: Shauri yenu. Mimi sitagharamia matibabu ya mbavu zitakazovunjika.
                      (Watu wanacheka) Mabibi na mabwana, sote tumkaribishe mwimbaji
                       katika jukwaa kwa makofi na vigelegeleeeeee!
                      (Watu wanapiga makofi. Mwimbaji anaingia.)
  MFAWIDHI: Kwenu mnanunua sindano kweli?
  MWIMBAJI: Hapana.
  MFAWIDHI: Ningeshangaa. Wewe ni sindano tayari. (Watu wanacheka)
  MWIMBAJI: Kwetu tuko wengi sana.
  MFAWIDHI: Mko wengi hadi mnapika chapati moja kisha mnapiga chapa.
                      (Kicheko). Kabla hatujaanza, ebu tupe historia fupi kuhusu safari
                      yako katika muziki.
  MWIMBAJI: Nilianza kwa kucheza kayamba kanisani.Hapo ndipo bendi ya
                      Umoja Jazz wakatambua kipawa changu. Wakanichukua kuwachezea
                       tarumbeta. Baada ya muda mfupi, nikaanza kujisimamia. Nikatunga
                      na kurekodi nyimbo zangu kama na kujichezea gitaa.
                      Hivi karibuni nitaunda bendi yangu.
  MFAWIDHI: Usikose kunijumuisha katika kwaya yako. Nitakuimbia soprano.
                      (Watu wanacheka) Leo umetuandalia nini?
  MWIMBAJI: Leo nitawatumbuiza kwa taarabu.
  MFAWIDHI: Haya haya! Wakati wa burudani umewadia. Kila mtu atafute nafasi
                      na mwandani wake. Muwe wawili wawili. Kama huna wako, eleka
                      jiwe. Kuna mawe mengi hapa. (Kicheko) Hakuna kukanyagana mguu.
                      (Watu wanacheka). Kama hujui kucheza miondoko ya taarabu,
                      kuja hapa mbele nikufunze. (Watu wanacheka). Haya twende kazi.
                      (Mwimbaji anaimba. Watu wanacheza.)

  Maelezo ya msamiati

  kukata na shoka – kufana
  kuvunjika mbavu – kucheka
  kayamba – ala ya muziki yenye umbo la kisanduku ambayo
                     hutengenezwa kwa matete na kutiwa punje kavu au
                     changarawe na hutikiswatikiswa wakati wa kuimba
  bendi – kikundi cha waimbaji wanaoimba pamoja
  tarumbeta – ala ya muziki ya kupuliza ambayo hutengenezwa kwa shaba na
                        hutoa sauti mbalimbali
  gitaa – ala ya muziki ambayo kwa kawaida huwa na nyuzi sita
  kwaya – uimbaji wa pamoja katika kikundi maalamu cha kuimba
  taarabu – muziki wenye mahadhi ya mwambao wa Afrika Mashariki
                  unaotumia mchanganyiko wa ala za Kiarabu, Kihindi na Kizungu

  Zoezi

  1. Tunga sentensi sahihi ukitumia msamiati uliotolewa maelezo hapo juu.
  2. Toa mifano zaidi ya rejesta ya burudani. Andika msamiati wa kimsingi
       unaotumika katika rejesta hizo.
  3. Eleza sifa ya lugha iliyotumika kifunguni.

  Sifa za rejesta ya burudani

  Rejesta ya burudani huwa na sifa mbalimbali. Tazama baadhi ya sifa hizo katika orodha ifuatayo:
  i) Kuwa na maneno ya raha,
  ii) Huibua hali za kutuliza na kupumbaza mshiriki,
  iii) Kuwepo na uwezekano wa washirika wake kukesha hadi che huku
       wakijifurahisha kwa namna wapendavyo,
  iv) Kuwepo bendi ya muziki na wanasarakasi,
  v) Hali ya kusahau shida na mahangaiko aliyonayo mshiriki angalau kwa wakati mfupi tu.

  Kazi ya wanafunzi wawili wawili
  Jiunge na mwanafunzi mwenzako. Fanyeni mazoezi haya:
  1. Toeni mifano zaidi ya rejesta za burudani.
  2. Jadilianeni sifa za lugha inayotumika katika rejesta mlizotaja.
  3. Linganisheni na mtofautishe msamiati uliotumika katika rejesta hizo mbalimbali za burudani.

  Umuhimu wa michezo na burudani
  a) Umuhimu wa michezo
  Michezo ni shughuli za kushindana kati ya timu au watu tofauti tofauti ili kutafuta ushindi.
  Je,wewe unapenda kucheza mchezo gani?

  Kazi ya wanafunzi wawili wawili
  Jiunge na mwanafunzi mwenzako. Tazameni michoro iliyopo hapo chini na mtaje yanayotendeka.
    

  Soma kifungu na ujibu maswali yaliyoulizwa chini yake.
  Michezo ina umuhimu mkubwa kwetu kutokana na sababu mbalimbali. Kwanza,
  mchezo huimarisha afya yetu. Wachezaji hufanya mazoezi ya viungo. Mazoezi
  hayo ya viungo husaidia miili yetu kuyeyusha mafuta ya ziada, kunyosha misuli,
  kuimarisha mapigo ya moyo na kadhalika.
  Pili, michezo huleta umoja miongoni mwa jamii. Watu wanapoenda kutazama
  mchezo kama vile kandanda, hujumuika pamoja kushabikia timu fulani. Pale,
  wao hujenga urafiki. Mathalan, timu yetu ya taifa inapocheza, Wanyarwanda
  wote huja pamoja kuishabikia. Tunapofanya hivyo, tunajenga umoja wetu kama
  Wanyarwanda. Baadhi ya mashabiki pia husafiri pamoja na timu yetu ya taifa
  wanapocheza nje ya Rwanda. Safari kama hizo huchangia kujenga umoja na
  urafiki miongoni mwa mashabiki hao.
  Tatu, michezo huleta fahari. Mchezaji mashuhuri, timu bora na taifa bingwa katika
  michezo fulani hujulikana kwingi na kusifiwa. Sifa hizi huinua hadhi ya mtu binafsi,
  timu na taifa kwa jumla. Nchi inayosifika kwa mchezo au michezo fulani huwa
  katika hali nzuri ya kuvutia watalii.
  Michezo huleta pato la kuridhisha. Pato hili huwa kwa mchezaji binafsi, kwa
  kilabu na hata kwa taifa. Wachezaji wa vilabu mbalimbali na timu ya taifa hulipwa
  mshahara na marupurupu mengi. Baadhi ya wachezaji hawa hasa wanaochezea
  vilabu vya kimataifa ni matajiri wa kutajika kutokana na michezo.
  Vilabu mbalimbali pia hunufaika pakubwa. Wao hukusanya pesa nyingi kutokana na
  mauzo ya tikiti, matangazo ya biashara katika viwanja vyao, kuuzwa kwa wachezaji
  wao kwa vilabu vinginevyo na kadhalika. Taifa zima pia hunufaika kutokana na
  ushuru mbalimbali unaolipwa na wachezaji pamoja na vilabu husika.
  Michezo huburudisha na kutuliza roho. Baada ya shughuli nyingi za siku au wiki,
  mashabiki hujipumzisha akili kwa kutazama michezo wanayopenda. Pia, kushabikia
  timu na kusherehekea ushindi huleta uchangamfu.

  Maswali
  1. Taja umuhimu wa michezo kulingana na kifungu hiki.
  2. Michezo ni njia bora kuu ya kuimarisha afya yetu. Tetea kauli hii.
  3. Eleza jinsi michezo huleta ushirikiano kati yetu.
  4. Jadilianeni kuhusu jinsi mnavyoweza kutumia michezo kukuza ushirikiano,
       kuboresha afya na kutatua matatizo yanayokumba jamii yenu.

  b) Umuhimu wa burudani
  Tazama michoro iliyopo hapa chini. Je, mambo gani yanafanyika?