Topic outline

  • MADA YA 1 MATUMIZI YA KISWAHILI SHULENI

    Uwezo mahususi wa mada: Kuzungumza Kiswahili kwa ufasaha na kuandika matini fupifupi kwa kusisitizia msamiati maalum unaotumiwa katika 
    mazingira ya shuleni.

    Malengo ya ujifunzaji:

    • Kutumia kwa ufasaha msamiati unaotumiwa katika mazingira ya shule;
    • Kueleza kuhusu wafanyakazi wanaopatikana shuleni;
    • Kueleza kuhusu msamiati unaohusiana na shughuli zifanyikazo shuleni; 
    • Kutunga sentensi kwa kuzingatia matumizi ya umoja na wingi wa 

    majina ya ngeli ya LI-YA.

    Kidokezo

    cc

    Tazama mchoro huu na kueleza kinachofanyika hapa juu.

    SOMO LA 1: TARATIBU ZA SHULENI

    1.1. Kusoma na ufahamu: Shule ya Icyerekezo

    Soma kifungu cha habari hapa chini kisha ujibu maswali yanayofuata
    Shule yetu inaitwa Shule ya Sekondari ya Icyerekezo.

    Shule hii inapatikana 

    katika wilaya ya Kicukiro makao yake makuu yapo mjini Kigali. Shule hii 
    ya Ikerekezo ina walimu ishirini na madarasa kumi na mawili pamoja na 
    wafanyakazi wengine kumi ambao siyo walimu.

    Inapokuwa kipindi cha muhula kuanza, jumuiya nzima ya shule huchukua 
    muda wa saa mbili za mazungumzo kuelezea kuhusu taratibu za shule 
    kwa ujumla kabla ya kuanza shughuli yoyote shuleni.
    Mazungumzo haya huanzishwa na mkuu wa shule ambaye huanza kwa 

    kuelezea kama ifuatavyo: 
    Shughuli za shule huanza saa mbili kila siku, inapofika saa nne huwa kuna 
    mapumziko ya dakika ishirini. Baada ya hapo masomo huendelea hadi 
    saa sita,ambapo kunakuwepo mapumziko ya saa moja kwa chakula cha 
    mchana. Saa saba masomo yanaendelea hadi saa kumi.

    Baada ya masomo, wanafunzi hufanya usafi binafsi kwa muda wa saa 
    moja, kisha hujitayarisha kwa chakula cha jioni ambacho hupatikana saa 
    moja na baadaye huendelea na masomo binafsi darasani hadi saa tatu 
    ambao ni muda wa kwenda kulala.

    Saa moja asubuhi ni muda wa kupata kifunguakinywa (staftahi) hadi saa 
    moja na nusu huku wakijiandaa kuanza masomo. Utaratibu huu unaanzia 
    Jumatatu hadi Ijumaa.

    Shule hii ina madarasa kuanzia kidato cha kwanza hadi cha sita. Ina mikondo 
    miwili yaani mchepuo wa lugha na mchepuo wa sayansi.
    Shule hii ina maabara mbili. Maabara ya kidato cha kwanza hadi cha tatu na 
    maabara ya kidato cha nne hadi cha sita kwa kufanyia mazoezi ya vitendo 
    kwenye masomo ya lugha na sayansi.

    Idadi ya wanafunzi wote ni mia tano. Kuna ofisi ya naibu mkuu wa shule, 
    mkuu wa taaluma ambaye anashughulika na taratibu za mafunzo ya 
    wanafunzi ya kila siku, mkuu wa nidhamu na ofisi ya walimu kwa ujumla.
    Baada ya maelezo haya, mkuu wa shule alichukua fursa ya kuwatambulisha 
    walimu na wafanya kazi wengine.

    Mara baada ya mkuu wa shule kumaliza kuwatambulisha wafanyakazi wote 
    wa shule, alitoa fursa kwa wanafunzi kuuliza maswali huku akianzia kidato 

    cha kwanza ambao ndio waliokuwa wageni muhula huo.

    Mwanafunzi wa kidato cha kwanza alipewa fursa ya kuuliza swali na kuanza 
    kama ifuatavyo: Mimi naitwa Revocatus Kabayiza; mwanafunzi wa kidato 
    cha kwanza. Swali langu ni hili: “Mmetuelezea kuwa kufanya usafi binafsi 
    shuleni ni kuanzia saa kumi. Je, mbona hamkutuelezea shughuli za siku ya 

    Jumamosi na Jumapili ?”
    Mkuu wa shule alimshukuru kwa swali zuri, kisha akaendelea kuwaelezea 
    kuwa siku ya Jumamosi ni utawala binafsi, yaani wanafunzi hupata staftahi 
    kama kawaida baada ya hapo ni kufanya usafi wa mazingira kwa muda wa 
    saa moja. Wanafunzi hujigawa katika makundi ya kufanya usafi darasani, 
    kwenye mabweni na kwenye mazingira ya shule.

    Chakula cha mchana hupatikana saa za kawaida na siku ya Jumapili ni 
    utawala binafsi shuleni, pale ambapo itaonekana kuwa kuna mwanafunzi 
    mwenye matatizo siku za Jumamosi na Jumapili, ataweza kumwona 
    mwalimu wa zamu kupitia viranja wenu pamoja na viongozi wa madarasa.

    Baada ya maelezo mazuri haya, mkuu wa shule aliwatakia kila la heri na 
    fanaka kwa kuanza muhula mpya wa masomo. Wanafunzi walionyesha 
    furaha yao kwa kumpigia makofi mkuu wa shule wakionyesha walivyofurahia 
    mazumgumzo yake. Baadaye, mkutano ulimalizika na shughuli za shule 

    ziliendelea kama kawaida. 

    Kazi ya 1

    Maswali ya Ufahamu
    1. Ni wahusika gani wanaozungumziwa katika kifungu hiki?
    2. Mkuu wa shule alikuwa na lengo lipi kwa kufanya mkutano na 
    wanafunzi?
    3. Wanafunzi hao walikuwa katika kiwango gani cha elimu? 
    4. Nini maana ya mkuu wa taaluma?
    5. Unadhani wanafunzi hawa wamefurahia mazungumzo 
    waliyopewa na mkuu wa shule ? Eleza maoni yako. 
    6. Kifungu hiki cha habari kinazungumzia kuhusu:
    a. Maabara ya shule ya Icyerekezo.
    b. Utaratibu wa shule ya sekondari ya Icyerekezo.
    c. Ziara ya wanafunzi wa Shule jirani. 

    d. Masomo ya Shule.

    7. Ofisi ya Taaluma hujishughulisha na:
    a. Wafanyakazi wote shuleni.
    b. Wapishi shuleni.
    c. Masomo na kumbukumbu za kila siku za wanafunzi.
    d. Mwalimu wa zamu, viranja na viongozi wa madaras.
    8. Maabara ni sehemu ambayo walimu na wanafunzi hufanyia:
    a. Mchezo wa mpira wa miguu.
    b. Mazoezi ya chemshabongo.
    c. Sehemu ya kufanyia mazoezi ya sayansi kwa vitendo.
    d. Sehemu ya kufanyia mikutano.
    9. Ofisi ya walimu ni:
    a. Eneo la burudani na starehe.
    b. Mahali pa kuzungumzia na kupigia porojo.
    c. Sehemu ya kufanyia kazi na kutayarisha masomo ya wanafunzi.

    d. Hakuna shughuli yoyote ifanyikayo huko.

    1.2. Msamiati kuhusu mazingira ya shule

    Kazi ya 2

    Baada ya kusoma kifungu cha habari cha hapo juu,oanisha 

    msamiati ulio katika sehemu A na maelezo yake katika sehemu B.

    ff

    bb

    1.3. Sarufi: Matumizi ya umoja na wingi wa majina ya ngeli 

    ya LI-YA

    vv

    Mifano ya maneno yaliyomo katika ngeli ya LI-YA katika umoja na wingi: 

     Umoja wingi

    1. Kundi                    Makundi
    2. Shirika                  Mashirika
    3. Jani                       Majani
    4. Gari                       Magari
    5. Darasa                Madarasa

    Tanbihi : Kuna majina ya ngeli hii yasiyokuwa na umoja yaani hubaki katika 
    wingi kama vile:

    Maji, mate, maziwa (ya kunywewa), mateso, manukato, mazishi, matumizi, 

    manufaa, masafa.
    Katika sentensi, majina ya ngeli hii hufuatwa na kitenzi chenye kiambishi 

    awali li- katika umoja na ya- katika wingi.

    Mfano: 

     Umoja                                                                 Wingi
    1. Shirika liliundwa.                                    Mashirika yaliundwa.
    2. Koti lingesafishwa.                                 Makoti yangesafishwa.
    3. Chungwa liliangushwa.                        Machungwa yaliangushwa.

    Majina mengi ya ngeli ya li-ya hufanya wingi wake kwa kiambishi awali makama inavyoonekana kwenye mifano iliyotolewa hapa chini.

    bb

    Kazi ya 4:

    Tunga sentensi za umoja na za wingi kwa kutumia maneno haya: 

    jaribio, swali, jino, jembe, juma, jengo

    1.4. Matumizi ya lugha: Shughuli za Wafanyakazi Shuleni

    Kazi ya 5:

    Zungumzia kuhusu viongozi wote wa shule na wajibu wao.

    Kazi ya 6.

    cc

    1.5. Kusikiliza na kuzungumza
    Kazi ya 7:
    Itambulishe shule uliposomea katika kidato cha tatu
    1.6. Kuandika
    Kazi ya 8:
    Buni mazungumzo kati ya Mkuu wa Shule na wanafunzi wawili.
    Kazi ya 9:

    Iangalie ratiba hii kisha panga vipindi vyako inavyostahili kulingana 

    na ratiba yako ya kila siku.

    dd
    dd
    ddd

    SOMO LA 2: USAFI SHULENI

    Kidokezo

    ff

    Kazi ya 1:

    Tazama mchoro hapo juu kisha uzungumzie unayoyaona. 

    dd

    Soma kifungu cha habari hapa chini kisha ujibu maswali yanayofuata

    Usafi shuleni ni shughuli au kazi moja muhimu inayofanyika shuleni. 
    Usafi wa shule na vifaa vya shule ni njia ya kuendeleza afya kwa kuzuia 
    mawasiliano ya binadamu na athari za taka. Athari hizo zinaweza kuhusu 
    mwili wa binadamu.

    Uchafu unachangia pakubwa kuharibu maisha ya binadamu. Usafi shuleni 
    ni jambo ambalo linafaa kutiliwa maanani na wanafunzi, walimu, viongozi 
    wa shule na wafanyakazi wengine wa shule. Watu wa shuleni wachache 
    wanafikiri kuwa usafi unahusu miili na sare tu wakisahau kuwa usafi 
    huhusu kila kitu kinachopatikana na sehemu zote katika mazingira ya shule.

    Wanafunzi ni lazima wawe safi. Sare humfanya mwanafunzi aonekane 
    maridadi na apendeze. Mavazi ni hifadhi ya staha ya utu wa mtu. Mavazi 
    hukusudia pia kuficha utupu wa mtu. Wanaposafisha sare zao, wanajiepusha 
    na magonjwa yanayotokana na wadudu wanaoweza kuishi katika nguo chafu. 
    Wadudu hawa ni kama chawa, viroboto na kadhalika. Isitoshe, usafi wa sare 
    lazima uende sambamba na usafi wa mwili. Usafi wa mwili unahusiana na 
    kuoga, kunyoa nywele, kupiga mswaki na kukata kucha.

    Sehemu za shule zinazoshughulikiwa kusafishwa ni kama vile: darasani, 
    nje ya darasa, bweni, bwalo, vyoo, chumba cha wasichana, ofisi za walimu 
    na wakuu wa shule, viwanja vya michezo, n.k. Wanafunzi wanaposafisha 
    sehemu zote hizo wanatumia vifaa kama vile: ndoo ya maji, sabuni za 
    kawaida au sabuni za kemikali au dawa za kuulia wadudu wenye kuambukiza 
    watu, deke, n.k. 

    Wanafunzi au wafanyakazi wengine wanakata nyasi zinazozunguka 
    madarasa ili kuwafukuza mbu wanaosababisha ugonjwa wa malaria. Ni 
    lazima kuhifadhi mazingira. Katika bustani, wanatumia jembe kwa kupalilia 
    na panga kwa kukata nyasi. Wanafunzi au watu wengine wasitupe uchafu 
    ovyoovyo. Taka zote zinazotokana na vitu vyote vilivyotumiwa zinafaa 
    kutupwa mahali panapofaa kama vile pipa la taka au jalalani.

    Wanafunzi wasisahau usafi wa vifaa vya shule kama vile: vitabu, madaftari, 
    kalamu, kifutio, dawati, meza ya mwalimu, n.k. Wanafunzi wanaombwa 
    kuwa na vitabu na madaftari yenye vifuniko safi. Inakatazwa kuharibu vifaa 
    vya shule kwa kila mtu.

    Shuleni, maji yote ya kunywa na ya matumizi mengine yatoke kwenye vyanzo 
    salama au yachemshwe. Vyombo vya kubebea na kuhifadhi maji viwekwe 
    safi ndani na nje na kufunikwa ili kuepuka uchafuzi wa maji. Wanafunzi wawe 
    na tabia ya kunawa mikono kwa maji na sabuni kabla na baada ya chakula 

    na baada ya kutoka chooni.

    Kazi ya 2:
    Maswali ya Ufahamu
    1. Usafi shuleni unasadia nini binadamu?
    2. Usafi shuleni ni jambo ambalo linafaa kutiliwa maanani. Eleza. 
    3. Usafi shuleni unawahusu watu gani?
    4. Watu wachache wa shule wanafikiri nini kuhusu usafi?
    5. Kwa sababu gani wanafunzi wanaombwa kuvaa sare safi?
    6. Faida gani ya kusafisha sare za wanafunzi?
    7. Kuna umuhimu gani wa kukata nyasi zinazozunguka madarasa?
    8. Tunatumiaje pipa za taka na jalala?
    9. Wanafunzi wanatumia nini kusafisha bustani ?

    2.2. Matumizi ya msamiati

    Toa maana ya msamiati ufuatao na kuutumia katika sentensi sahihi
    1. Usafi
    2. Uchafu
    3. Athari 
    4. Maanani
    5. Bweni 
    6. Bwalo

    7. Mbu

    Kazi ya 4:
    Jaza sentensi kwa kutumia maneno yafuatayo kutoka kifungu cha 
    hapo juu: (yachemshwe, kunawa, jalalani, kunyoa, mswaki, hifadhi, 
    maridadi, unahusu, usafi, kuharibu)
    1. ……… ni jambo ambalo linafaa kutiliwa maanani shuleni.
    2. Watu wachache wa shuleni wanafikiri kuwa usafi ni…….mikono, 
    kuoga na kuvaa sare safi. 
    3. Sare humfanya mwanafunzi aonekane ……………..na apendeze.
    4. Mavazi ni …………..ya staha ya utu wa mtu.
    5. Usafi wa mwili unahusiana na kuoga, …….. nywele, kupiga ………. 
    na kukata kucha.
    6. Taka zote zinazotokana na vitu vyote vilivyotumiwa, zinafaa 
    kutupwa mahali panapofaa kama vile pipa la taka au..................... 
    7. Wanafunzi wana tabia ya……….. mikono kwa maji na sabuni 
    kabla na baada ya chakula.
    8. Maji yote ya kunywa na ya matumizi mengine lazima yatoke 
    kwenye vyanzo salama au ………………

    2.3. Sarufi: Ngeli ya LI – YA na vivumishi vya kumiliki
    Kazi ya 5:
    Chunguza mifano ya sentensi hapa chini na ueleze aina za maneno 
    yaliyopigiwa mstari.
    a. Jino langu linaniuma.
    b. Gazeti letu lina habari nyingi.
    c. Shamba lako limelimwa vizuri.
    d. Dawati lenu linavunjika.
    e. Soko lao linajaa watu
    Maelezo muhimu
    Vivumishi vya kumiliki ni -angu, -ako, -ake, -etu, -enu na -ao. Vivumishi 
    hivi katika ngeli ya Li-Ya huchukua kiambishi konsonanti l- katika umoja na 

    y- katika wingi.

    Kazi ya 6:

    Andika sentensi zifuatazo katika umoja au wingi
    1. Jiji letu linapata wageni kutoka Kigali.
    2. Ua langu linapamba mazingira.
    3. Dirisha lao linafunguliwa ili hewa iingie.
    4. Sikio langu lina shida ya kusikia.
    5. Gari lenu linatereza siku hii.
    6. Jino langu linaniuma.
    7. Gazeti letu lina habari nyingi.
    8. Shamba lako limelimwa vizuri.
    9. Dawati lenu limevunjika.
    10. Soko lao linajaa watu.

    2.4. Matumizi ya lugha
    Kazi ya 7:
    Mwambie mwenzako namna mnavyofanya usafi shuleni kwako.
    2.5. Kusikiliza na kuzungumza 
    Kazi ya 8:
    Jadili kuhusu “Uhifadhi wa vifaa vya shule” 
    2.6. Kuandika
    Kazi ya 7:
    Tunga kifungu cha habari kwa kutumia kichwa kifuatacho (maneno 
    yasiyopungua mia moja): “Uchafu shuleni ni asili ya maradhi mengi”

    SOMO LA 3: VIONGOZI WETU SHULENI

    fff

    Kazi ya 1:
    Tazama mchoro hapo juu kisha uzungumzie yale unayoyaona.
    3.1. Kusoma na ufahamu: Viongozi wa shule na wajibu wao
    Soma kifungu cha habari hapo chini kisha jibu maswali yanayofuata
    Mimi ninaitwa Kwizera. Ninasoma kidato cha nne. Shule yetu inaitwa shule 

    ya Sekondari ya Gikondo.

    Kayitare ni kiranja wa darasa letu. Yeye hutuwakilisha katika mikutano mingi 
    ya shule. Katika mikutano na mkuu wa shule, yeye huuliza maswali mazuri 
    kwa sababu yeye ni mwanafunzi hodari sana. Mimi ninaelewa vizuri masomo 
    yote; Kiswahili, Kinyarwanda, Kiingereza, Hisabati, Jiografia, Historia na 
    mengine kwani shule yetu ina viongozi wazuri. 

    Mkutubi hufanya kazi maktabani ambapo vitabu vyetu huhifadhiwa kwani. 
    Shule yetu ina vitabu vingi. Mwalimu wa taaluma kila asubuhi, hutukagua 
    ikiwa tumevaa sare. Yeye pia hutushauri kupenda masomo yetu, kusaidiana 
    na kufanya kazi kwa bidii. Yeye hupanga masomo ya kila muhula. Mwishoni 
    mwa kila muhula, sisi hufanya mitihani. Mhasibu wa shule hupokea karo 
    za wanafunzi. Mwalimu wa nidhamu huwaadhibu wanafunzi wanaofanya 
    makosa: wanafunzi watukutu, wanafunzi wanaotoroka shule na wale 
    wanaopiga kelele darasani. 

    Mwalimu mshauri wa wasichana, huchunguza nidhamu ya wasichana. 
    Yeye hutatua shida zao shuleni, hutushauri kuwa na mwenendo mzuri, 
    huchunguza wakati wa kuingia mabwenini na kadhalika. Mwalimu mshauri 
    wa wavulana huchunguza nidhamu ya wavulana na kupanga michezo 
    shuleni kwa kushirikiana na mwalimu mshauri wa wasichana. 
    Wakati wa chakula cha mchana na chakula cha jioni, walimu wa zamu 
    huingia bwaloni kuchunguza chakula chetu na kutushauri kuheshimiana 
    wakati wa kula. Mimi nawapenda sana viongozi wetu shuleni. 

    Kazi ya 2:
    Maswali ya ufahamu
    1. Kwizera anasomea wapi? 
    2. Yeye anasoma kidato gani?
    3. Fafanua umuhimu wa maktaba kwa mwanafunzi.
    4. Je, Kwizera anaelewa vizuri masomo yake? Eleza.
    5. Viongozi wao ni wepi?
    6. Eleza kazi zinazofanywa na mhasibu.
    7. Mwishoni mwa kila muhula wanafunzi hufanya nini?
    8. Nini wajibu wa kiranja?
    9. Mkuu wa shule anaitwa nani na ana majukumu gani?
    10. Walimu wa zamu huingia bwaloni kufanya nini?

    3.2. Msamiati kuhusu mazingira ya shule

    Kazi ya 3:xx

    3.3. Sarufi: Matumizi ya umoja na wingi wa majina ya ngeli 

    ya li-ya

    Kazi ya 4:

    Tazama sentensi zifuatazo na kuzungumzia mabadiliko yanayojitokeza 
    kutoka sehemu A kwenda sehemu B
    xx

    TNBH: Kuna majina ya ngeli hii yasiyokuwa na umoja kama vile :
    Maji, mate, maziwa (ya kunywewa), mateso, manukato, mazishi, matumizi, 
    manufaa, masafa.
    Katika sentensi, majina ya ngeli hii hufuatwa na kitenzi chenye kiambishi 
    awali li- katika umoja na ya- katika wingi.
    Mfano: 
     Umoja                                                Wingi
    1. Shirika liliundwa.                       Mashirika yaliundwa.
    2. Koti lingesafishwa.                    Makoti yangesafishwa.
    3. Chungwa liliangushwa.          Machungwa yaliangushwa.
    Maelezo muhimu 
    Majina mengi ya ngeli ya li-ya hufanya wingi wake kwa kuongeza kiambishi 
    awali ma- mwanzoni mwa neno. 

    Kazi ya 5:
    Weka sentensi hizi kati wingi au umoja:
    a. Zoezi hili halieleweki.
    b. Shamba la mjomba ni jipya.
    c. Yai lililoharibika halifai kwa afya ya mwanadamu.
    d. Gari lililoharibika halipendezi.
    e. Matope yamechafua nguo zangu.
    f. Jeshi limemshinda adui.
    g. Juma la kazi limemalizika.
    h. Magurudumu ya gari yanaviringika kasi.
    i. Hekalu limejengwa vizuri.

    j. Majamvi yaliliwa na panya.

    Kazi ya 6:

    Chunguza sentensi hizi kutoka sehemu A na sehemu B uziunganishe 

    ili ziwe sentensi kamili

    dd

    3.4. Matumizi ya lugha: Vyeo vya viongozi shuleni

    Kazi ya 7:

    Husisha maneno kutoka sehemu A kwenda sehemu B

    dd

    3.5. Kusikiliza na Kuzungumza
    Kazi ya 8:
    Zungumzia kuhusu shule uliposomea kidako cha tatu.
    3.6. Kuandika
    Kazi ya 9:
    Andika kuhusu umuhimu wa kuwa na viongozi katika jumuia zetu

    SOMO LA 4 : RATIBA YA WIKI YA MWANAFUNZI

    rr

    Kazi ya 1:
    Tazama michoro hapo juu, tambua kazi zinazofanywa na utaje 

    umuhimu wa kazi hizo

    4.1. Kusoma na ufahamu: Ratiba ya shughuli za kila siku 
    katika Shule ya Gasozi
    Soma kifungu cha habari hapo chini kisha jibu maswali yanayofuata
    Gasimba ni mwanafunzi wa kidato cha kwanza kwenye shule ya Gasozi. 
    Yeye ni mwanafunzi mwenye bidii na hachelewi shuleni. Jumatatu, Gasimba 
    huamka saa kumi na moja na nusu alfajiri na kuanza kujiandaa kwenda 
    shuleni. Baadaye, yeye hupiga meno yake mswaki, huchana nywele na 
    kuvaa sare yake.

    Mamake Gasimba huamka mapema zaidi ili kumwandalia mwanawe 
    kifunguakinywa. Gasimba hunywa chai kwa mkate kisha hubeba mkoba 
    wake wenye madaftari na vitabu vyake kuelekea shuleni. Gasimba humuaga 
    mamake na kuondoka. Gasimba hufika shuleni saa kumi na mbili na nusu na 
    kuingia darasani na kuanza kusoma. Yeye huwatangulia wanafunzi wengine.
    Saa mbili kasorobo kengele hulia na wanafunzi wote huenda kwenye gwaride 
    ambapo wao husali na baadaye wakaimba wimbo wa taifa la Rwanda. 
    Mwalimu mkuu huwahutubia wanafunzi kisha humpisha mwalimu wa zamu 
    kuwapa wanafunzi matangazo muhimu.

    Saa mbili kamili, somo la kwanza huanza. Baada ya vipindi viwili wanafunzi 
    hupewa dakika ishirini za mapumziko. Chakula cha mchana huliwa saa saba 
    kamili. Masomo huendelea kuanzia saa nane alasiri. Saa kumi na dakika 
    ishirini masomo ya siku huwa yamekamilika. Wanafunzi wote huenda 

    uwanjani kwa michezo mbalimbali kama kandanda, voliboli na kuruka kamba. 
    Ifikapo saa kumi na moja na nusu wanafunzi wote huelekea nyumbani.

    Gasimba afikapo nyumbani, yeye humsaidia mamake kufanya kazi za 
    nyumbani. Baadaye, yeye hufanya kazi zake za ziada na za shuleni. Saa 
    tatu na nusu usiku zifikapo huenda kulala. 

    Kila siku ya wiki huhusika na matukio haya ila siku ya Alhamisi jioni ambapo 
    Gasimba hufanya mazoezi ya kuogelea katika bwawa la kuogelea nyumbani 
    kwao. Ijumaa jioni, wanafunzi hushiriki katika mjadala kuhusu mada ambazo 
    walimu wao huwa wamewachagulia. Jumamosi, Gasimba humsaidia 
    mamake kufanya kazi za nyumbani. Jumapili, Gasimba huendelea na 
    mapumziko kama kawaida. Baada ya kupumzika, Gasimba hujitayarisha 
    kwa ajili ya kwenda shuleni Jumatatu.

    Kazi ya 2:
    Maswali ya Ufahamu

    1. Gasimba anasomea katika shule gani?
    2. Je, Gasimba yuko katika kidato kipi?
    3. Gasimba hufanya nini anapoamka kabla ya kustaftahi?
    4. Baina ya Gasimba na mamake, nani huamka mapema zaidi?
    5. Gasimba hufanya nini afikapo shuleni kabla wanafunzi wengine 
    wafike?
    6. Gasimba na wanafunzi wenzake hufanya nini Alhamisi na Ijumaa 
    jioni baada ya masomo yao?
    7. Gasimba hufanya nini Jumamosi?

    8. Taja shughuli za Gasimba za siku ya Jumapili?

    4.2. Matumizi ya msamiati
    Kazi ya 3:
    Tunga sentensi sahihi kwa kutumia maneno yafuatayo: (ratiba, 
    kuogelea, mjadala, huchana nywele na mapumziko)
    4.3. Sarufi: Matumizi ya vivumishi vya kuonyesha vya 

    ngeli ya LI-YA

    Kazi ya 4:

    Tazama sentensi zifuatazo na kuzungumzia mabadiliko 
    yanayojitokeza kutoka sehemu A kwenda sehemu B

    Sehemu A                                                                                    Sehemu B

    1. Bega hili limepambwa nyota za kijeshi.                 a. Mabega haya yamepambwa nyota za kijeshi.
    2. Gari hili ni jipya.                                                                b. Magari haya ni mapya.
    3. Jengo hili ni la hospitali.                                               c. Majengo haya ni ya hospitali.

    4. Pazia hili ni Safi .                                                              d. Mapazia haya ni safi.

    4.4. Matumizi ya lugha: Shughuli za kila siku za mwanafunzi

    Kazi ya 5:

    rr

    4.5. Kusikiliza na Kuzungumza
    Kazi ya 6:

    Eleza kwa ufupi kuhusu shughuli uzifanyazo shuleni unakosomea.

    4.6. Kuandika
    Kazi ya 7:
    Andika kwa ufupi kuhusu maendeleo ya shule yako.

    Tathmini ya mada

    Jibu maswali yafuatayo:

    1. Taja vitu angalau vitano ambavyo hupatikana katika mazingira ya 
    shule yenu.
    2. Zungumzia kuhusu shughuli tatu zinazofanyika shuleni kwenu. 
    3. Eleza majukumu ya wafanyakazi wanne wapatikanao shuleni. 
    4. Tunga sentensi kumi kwa kutumia ngeli ya LI-YA katika umoja 
    na uwingi.
    5. Eleza nafasi ya kila mwanafunzi katika harakati za kuzuia 
    ueneaji wa magonjwa shuleni.



  • MADA YA 2 MSAMIATI KUHUSU MAZINGIRA YA NYUMBANI

    Uwezo mahususi wa mada: Kuzungumza Kiswahili kwa ufasaha na 
    kuandika matini fupifupi kwa kutumia msamiati unaofaa katika mazingira ya 
    nyumbani.
    Malengo ya ujifunzaji:
    • Kutumia msamiati uhusuo mazingira ya nyumbani, mifugo na vifaa vya nyumbani,
    • Kuainisha watu wa nyumbani na uhusiano wa familia,
    • Kutumia majina ya ngeli ya LI- YA na vivumishi kwa ufasaha.
    Kidokezo
    1. Taja watu wote wanawopatikana nyumbani kwenu.
    2. Taja sehemu kuu za nyumba.
    3. Orodhesha vifaa na mifugo wanawopatikana nyumbani.
    SOMO LA 5: MAZINGIRA YA NYUMBANI
    ttt
    Kazi ya 1:
    Tazama mchoro hapo juu kisha jibu maswali yanayofuata: 
    a. Unaona nini kwenye picha hii? Eleza. 
    b. Kuna uhusiano gani kati ya mchoro huo na kichwa cha habari cha 
    hapa chini? 
    5.1. Kusoma na ufahamu: Makao ya Gakuba
    ccc
    Mimi na rafiki yangu Rurangwa tunazoea kutembea baada ya masomo ya 
    jioni. Siku moja tulipata gari na kuelekea kijijini.Tulipofika kijiji ambapo mzee 
    Gakuba anaishi tuliona nyumba yake na familia yake. Mzee Gakuba, mke 
    wake na watoto wao wawili walikuwa wanasimama mbele ya nyumba yao 
    katika bustani.Walikuwa wakizungumza.

     Tulipigwa na bumbuazi kwa sababu kabla ya kuenda likizoni hapo palikuwa 
    na nyumba ya msonge. Mapendekezo ya serikali ya Rwanda ni kuishi katika 
    nyumba za kisasa. Nyumba hii ina sehemu kuu zifuatazo: sebule,vyumba 
    vya kulala, chumba cha wageni, chumba cha vyombo, na jikoni. Nyumba hii 
    inajengwa kwa mchanga, saruji, vyuma, nondo, milango, madirisha, mawe, 
    matofali na mabati. Vifaa vyote hivi vinapatikana nchini Rwanda. Kwa kujenga 
    nyumba hii kuna: msingi, kuta, zege, paa, madirisha, milango, sakafu, dari, 
    bomba na kadhalika. Nyumba hii ina bustani na miti ya aina tofauti kama vile 
    mti wa machungwa na mti wa maembe. Tulitazama nyumba hiyo kwa makini 

    na kujiuliza mengi kuhusu mabadiliko ya muda mfupi.

    Tulichunguza gharama za ujenzi wa nyumba yake! Na kujiuliza Je, gharama 
    hizi zimetoka wapi? Gakuba na bibi yake, kwa ushirikiano wao walitumia 
    fedha za mkopo kutoka benki. Gharama za nyumba ni thamani ambayo 
    unapaswa kuilipa ili uweze kuipata nyumba hiyo unayoitaka! Sasa thamani 
    unaweza kuilipa kwa njia ya pesa, nguvu ya kazi yako, nguvu ya akili na 
    pesa. Ina maana kwamba bila kulipa gharama stahiki huwezi kupata thamani 
    ya nyumba ile unayoitaka. Gharama hizi unaweza kuwalipa watu wengine 
    wanaokufanyia kazi au wanaokuuzia bidhaa, lakini pia unaweza kuzilipa 
    wewe mwenyewe kama muda na nguvu zako. Bila kulipa gharama stahiki 
    huwezi kupata nyumba hiyo.

    Mara moja, Rurangwa alianza kuniuliza: “ je, unaona tofauti kati ya nyumba 
    za jadi na nyumba za kisasa?” Jibu langu lilikuwa hivi: “ kwanza ni vibaya 
    kwa maisha ya mtu anayeishi katika nyumba za msonge kwa sababu usafi 
    wa nyumba hizi si kazi rahisi. Nyingi zinajengwa kwa majani. Tena ni hatari 
    sana kuishi katika nyumba ya msonge: Nyumba hii inaweza kuangukia watu, 
    inaweza kuungua kwa sababu kunatumiwa majani kwa ujenzi wa nyumba 
    hii, na kadhalika. Tunahifadhi mazingira wakati tunapojenga nyumba 
    za kisasa kuliko ujenzi wa nyumba za jadi. Je, Rurangwa, unafahamu 
    umuhimu wa kuhifadhi mazingira wakati tunapojenga nyumba?” Rurangwa 
    anatoa jibu: “Hatuwezi kuorodhesha umuhimu wa mazingira kwa sababu 
    bila mazingira viumbe vyote haviwezi kuishi. Kuna mashirika mengi nchini 
    Rwanda yanayotetea uhifadhi wa mazingira. Bila mazingira hakuna maisha. 
    Binadamu na wanyama hupumua hewa nzuri kutoka kwenye mazingira. 
    Tunapata mvua kwa sababu mazingira yanahifadhiwa na kadhalika.” 

    Tulipomaliza matembezi yetu, tuliamua kuelezea wazazi wetu umuhimu wa 
    kuishi katika nyumba nzuri kwa kutumia vifaa ambavyo vinapatikana nchini 
    mwetu na kutumia fedha kutoka benki kwa njia ya mkopo. Na sisi kama 
    wanafunzi tutaunda klabu zitakazofundisha watu umuhimu wa kuishi mahali 

    pazuri na kuhifadhi mazingira.

    Kazi ya 2 :
    Maswali ya ufahamu 

    1. Taja majina ya watu wote wanaotajwa katika kifungu hiki.
    2. Familia ya Gakuba ina watu wangapi? Orodhesha watu hao.
    3. Kwa kujenga nyumba yao, walitumia vifaa gani? Kutoka wapi?
    4. Nyumba hii ilijengwa na nani? Toa maelezo.
    5. Je, Mtu mwenye uwezo mdogo wa kiuchumi anaweza kuishi katika 
    nyumba ya kisasa? Eleza.
    6. Kwa sababu gani tunatakiwa kuheshimu mazingira wakati 
    tunapojenga nyumba?
    7. Kama mwanafunzi wa mwaka wa kwanza, msaada wako ni upi 
    kwa kuhifadhi mazingira unamoishi?

    5.2. Matumizi ya msamiati 

    Kazi ya 3:
    Tumia maneno yafuatayo katika sentensi zako ukizingatia namna 
    yalivyotumiwa katika kifungu cha habari ulichosoma 

    1. Busitani
    2. Bumbuazi
    3. Mkopo 
    4. Kuhifadhi 
    5. Shirika
    6. Kupumua
    7. Kutetea
    8. Klabu

    Kazi ya 4:

    Oanisha maneno yaliyomo katika sehemu A na yale yaliyomo katika 

    sehemu B.

    ff

    5.3. Sarufi: Matumizi ya ngeli ya LI-YA.

    Kazi ya 5:

    Chunguza sentensi zifuatazo na kuandika viambishi nafsi 
    vinavyopatikana katika vitenzi

    1. Kundi la wanamuziki liliwatumbuiza watu jana. 
    2. Mashirika haya yaliundwa na vijana mbalimbali. 
    3. Koti hilo limeshonwa na mshonaji hodari. 
    4. Makabati yalitengenezwa na maseremala.

    5. Gari zuri lile lilitengenezwa nchini Rwanda

    Maelezo muhimu 

    • Vitenzi vilivyomo katika sentensi hapo juu, vinatumia viambishi nafsi LI-YA 
    • Matumizi ya viambishi hivi LI-YA yanategemea nomino zilizotumiwa katika sentensi hizo. 
    • Nomino hizo zikiwa katika umoja kitenzi huchukua LI; zikiwa katika wingi kitenzi huchukua YA. 
    • Nomino zilizopendekezwa katika umoja huchukua wingi wake kwa kuongeza ma- kwa jina hilo: 
    Mfano: 
    1. Kundi                   makundi 
    2. Shirika                mashirika 
    3. Jani                      majani 
    4. Gari                      magari 
    5. Darasa                 madarasa
    Tanbihi: Kuna majina ya ngeli hii yasiyokuwa na umoja. 
    Maji, mate, maziwa (ya kunywewa), mateso, mavi, manukato, mazishi, 
    matumizi, manufaa, masafa. Katika sentensi, majina ya ngeli hii hufuatwa 

    na kitenzi chenye kiambishi awali li- katika umoja na ya- katika wingi

    Mfano: 
    Umoja Wingi 
    1. Shirika liliundwa.                          Mashirika yaliundwa. 
    2. Koti lingesafishwa.                      Makoti yangesafishwa. 
    3. Chungwa liliangushwa.             Machungwa yaliangushwa.
    5.4. Matumizi ya lugha

    Kazi ya 6:
    Tunga sentensi sahihi kwa kutumia nomino hizi katika umuja na 
    wingi kisha ueleze kile ulichokigundua

     Umoja                                                                         Wingi 
    1. Kabati .......................................................... 
    2. Koti .............................................................. 
    3. Bega ............................................................ 
    4. Goti ............................................................. 
    5. Panga ......................................................... 
    6. Janga .......................................................... 
    7. Jangwa ....................................................... 
    8. Jina ............................................................. 
    9. Jibu ............................................................. 

    10. Jembe…………………………………………

    Kazi ya 7:
    Andika sentensi zifuatazo katika umoja au wingi. 
    1. Mimi nina lengo la kupambana na jangwa. 
    2. Wewe utaondoa jani kavu hilo. 
    3. Majani yalikauka. 
    4. Shavu linaniuma. 
    5. Kijana mrefu alibeba kasha kwenye bega. 
    6. Debe hilo linavuja kwa sababu limetoboka. 
    7. Watoto watano walilazwa hospitalini kwa sababu ya matatizo ya mapafu. 
    8. Madaftari yanapaswa kuhifadhiwa vizuri. 
    9. Tarumbeta lilitumiwa wakati wa burudani.

    10. Shirika la reli liliagiza garimoshi kubwa.

    5.5. Kusikiliza na kuzungumza
    Kazi ya 8:
    Simulia mbele ya darasa muhtasari wa kifungu “ Makao ya Gakuba.”
    5.6. Kuandika

    Kazi ya 9:
    Tunga kifungu cha mistari 12 kuhusu ujenzi wa nyumba ya wazazi 
    wako.

    SOMO LA 6: MSAMIATI KUHUSU WATU WANAOPATIKANA 
    NYUMBANI

    Kazi ya 1:

    Chunguza michoro hii kisha ujadili unachoona kwenye michoro hii.
    cc
    6.1. Kusoma na ufahamu: Watu wa nyumbani
    cc
    Familia ni jamaa ya watu wanaoishi pamoja yenye baba , mama na watoto. 
    Katika utamaduni wetu kama Wanyarwanda, watu hawa wana majukumu 
    tofauti katika familia.

    Baba pamoja na mama wana majukumu ya kutafuta maendeleo ya familia 
    yao. Baba kwa ushirikiano na mama wana wajibu wa kufanya juu chini ili 
    familia yao iweze kupiga hatua kimaendeleo na kujitegemea kikamilifu. 
    Kulinda usalama wa nyumbani ni mojawapo wa wajibu huo. Hapa mama na 
    baba ndio walinzi wa kwanza wa utaratibu nyumbani ili familia yao iwe na 
    amani kila wakati.

    Kuwalea watoto wao, wazazi wana majukumu makubwa sana kwa watoto 
    wao kama vile: kuwapenda, kuheshimu haki zote za mtoto na kukidhi mahitaji 
    yao yote kama vile kuwalisha, kuwasomesha, kuwalipia karo za shule na 
    kuwapeleka hospitalini wakati wanapoumwa, n.k. 

    Wazazi huwapa mawaidha mema na kuwafundisha mila na desturi za 
    Wanyarwanda kama vile: uzalendo, ushirikiano, kuheshimiana, n.k. Wazazi 
    pia huwasihi kuepukana na tabia za: ukatili, uongo, uovu, ulevi, uzembe, 
    kupiga marufuku itikadi ya mauaji ya kimbari, na mienendo yote isiyofaa. 
    Kwa upande wa watoto, nao wana majukumu ya kuwaheshimu wazazi wao, 
    kutimiza mipango ya wazazi kama ilivyopendekezwa na kutoa mchango 
    mwafaka wa maendeleo ya familia yao.

    Nyumbani, wageni wa aina yote hukaribishwa. Miongoni mwa wageni hao 
    ni kama babu, bibi, mjomba, shangazi, mpwa na shemeji. Wageni hawa 
    wanalakiwa vizuri.

    Kazi ya 2:

    Maswali ya ufahamu
    1. Kwa maoni yako, eleza maana ya familia.
    2. Kwa kawaida familia hujengwa namna gani?
    3. Katika utamaduni wetu kama Wanyarwanda, baba na mama 
    wanashirikiana vipi?
    4. Je, mchango wa watoto ni upi katika familia? 

    5. Eleza mila na desturi ambazo wazazi wanafundisha watoto wao.

    6.2. Msamiati kuhusu watu wa nyumbani
    Kazi ya 3:
    Baada ya kusoma kifungu cha habari, toa maana ya msamiati 
    unaofuata, kisha utunge sentensi zenye maana kamili kwa kutumia 
    msamiati huo.

    1. Majukumu
    2. Ushirikiano
    3. Usalama
    4. Uzalendo 

    5. Mienendo 

    Kazi ya 4:

    Oanisha maneno kutoka sehemu A na maana yake katika B

    xxx

    6.3. Sarufi: Matumizi ya vivumishi vya idadi katika ngeli ya 
    LI-YA

    Kazi ya 5:

    Chunguza sentensi zifuatazo, kisha ueleze muundo wa vivumishi 
    vilivyotumiwa

    1. Jibu moja limepatikana.
    2. Mawe sita yameanguka chini.
    3. Matunda saba yameiva.
    4. Madarasa tisa yanasafishwa.
    5. Makoti kumi yatashonwa.

    Maelezo muhimu 

    Katika matumizi ya ngeli ya li-ya na vivumishi vya idadi, idadi mbili ambayo 
    hugeuka -wili, tatu, nne, tano pamoja na nane huchukua kiambishi makatika wingi. Vivumishi hivyo huwa mawili, matatu, manne, matano na
    manane. 
    Kinyume na matumizi ya ngeli ya li-ya na vivumishi vya idadi tulivyoona 
    hapo juu, idadi, sita, saba, tisa na kumi havichukui kiambishi ma- katika 
    wingi. Vivumishi hivyo hubaki vile vilivyo yaani, sita, saba, tisa, na kumi. 
    Nomino za ngeli ya “li-ya” huweza kutumiwa na vivumishi vya idadi ya jumla 
    /isiyo kamili / isiyo dhahiri: 
    Kwa mfano
    Matendo mengi mazuri yamefanywa na watu hawa.

    Kazi ya 6:

    Andika sentensi zifuatazo kwa kutumia vivumishi vilivyomo ndani 
    ya mabano. 

    1. Mawe .................... yamewekwa kando ya barabara (tatu). 
    2. Madirisha ........................... yamefunguliwa (tano). 
    3. Meno ...................... yameng’oka (mbili). 
    4. Matunda ....................... yameiva (nane).
    5. Makundi ................................. ya wanafunzi yameshiriki vilivyo (nne). 
    6. Madarasa .............................. yamejengwa (tatu). 
    7. Taja mambo .............. yanayozingatiwa katika kazi ya fasihi (tatu). 

    8. Makoti ...................... yameuzwa na mfanyabiashara huyu (tano).

    Kazi ya 7:

    Chunguza vivumishi vya idadi isiyo dhahiri vya ngeli ya “li-ya” 
    vifuatavyo kisha utunge sentensi zenye vivumshi hivyo. 

    1. Machache 
    2. Mengi 
    3. Kadhaa 
    4. Tele 

    5. Kidogo

    6.4. Matumizi ya lugha

    Kazi ya 8:
    Kamilisha tungo zifuatazo kwa kutumia vivumishi vya idadi: toka 
    moja hadi arubaini (Andika kwa maneno) 

    1. Kanuni za Mungu ni ........................ 
    2. Mwaka una miezi ............................. 
    3. Ni rahisi kujua kwamba wiki moja ina siku ..................... 
    4. Watu wa zamani walipika kwa kuweka chungu juu ya mafiga 
    ........................... 
    5. Wanyarwanda huwapa majina watoto wao kwenye siku ya ..........
    ......................... 
    6. Nchi ya Rwanda ina majimbo/ mikoa................. na mji wa Kigali.
    7. Nchi yetu inapakana na nchi........................ 
    8. Dunia ina mabara............................ 
    9. Rwanda ina milima ya volkano.................. 
    10. Katika mchezo wa soka, timu moja huwa na wachezaji...................
    uwanjani. 
    11. Siku moja ina saa........................... 

    6.5. Kusikiliza na kuzungumza

    Kazi ya 9:
    Soma kifungu cha habari hapo juu “watu wa nyumbani” baadaye 
    utoe muhtasari kimazungumzo.
    Kazi ya 10:
    Kwa njia ya mazungumzo, zungumzia wanafunzi wenzako ushirikiano 
    uliopo baina ya watu wa familia yenu.
    6.6. Kuandika 
    Kazi ya 11:
    Buni, kwa kuandika, mazungumzo ya watu nyumbani wakishirikiana 
    katika kazi fulani unayoitaka.
    SOMO LA 7: UHUSIANO WA KIFAMILIA
    Kazi ya 1:
    Tazama mchoro huu. Unaona nini kwenye mchoro huu? 
    vvv


    gggfff
    Bi. Nyiranzage aliolewa na Bw. Rutebuka. Sasa, Bi Nyiranzage 
    anaitwa bibi Rutebuka. Wengine humwita Bi. Nyiranzage. Bwana 
    Rutebuka ni mume wa bibi Nyiranzage. Bibi Nyiranzage na 
    bwana Rutebuka, ni mke na mume. Bwana na bibi Rutebuka 
    walizaa watoto wawili tu. Kifunguamimba wao ni mwanamume. 
    Jina lake ni Matabaro. Mtoto wa pili ni mwanamke. Yeye anaitwa 
    Nyiratabaro. Kwa upande mwingine Rutabagisha ambaye ni jirani 
    yao amemuoa Nyiramavugo; hivyo wote huitana mume na mke. 
    Bw. Rutabagisha na Nyiramavugo nao walizaa watoto wawili 
    tu, mmoja wa kike anayeitwa Mukabutera ndiye aliyetangulia 
    kuzaliwa na mwingine wa kiume Butera alifuata baadaye. Wototo 
    wa familia hizi mbili husomea kwenye Chuo cha Ualimu cha 
    Gacuba II.
    Watoto wote ni wanafunzi wa shule za sekondari. Vifunguamimba 
    husoma katika mwaka wa tatu katika chuo cha Ualimu cha Gacuba II.

    Ilhali vifungamimba husoma katika mwaka wa pili. 

    Baada ya muda mfupi, majirani hawa walikata shauri ya 
    kushirikiana kimasomo. Vifunguamimba walitangulia kushirikiana 
    na kusaidiana kati yao na hata kuwasaidia wadogo wao kimasomo 
    na kuwahimiza kuwaiga. Walikuwa wakishika nafasi ya kwanza 
    kwa kila muhula wa masomo. Baada ya kuona matunda ya 
    kushirikiana kimasomo, wote waliamua kuwasaidia wanafunzi 
    wenzao waliokuwa wakishindwa shuleni wakifanya marudio nao. 
    Jambo hili lilishamiri sana na kujulikana shuleni kote. Ilitokea 
    Mkurugenzi wa shule akapata habari hii na kuwakabidhi zawadi 
    ya kusoma mwaka mzima bila kulipa ada ya shule. 

    Jambo hili liliwafurahisha wazazi na kuwapongeza watoto wao 
    kwa zawadi nono. Shuleni, walimu wote walikuwa wanatumia 
    mfano wao ili kuwahimiza wanafunzi wengine kuwaiga.

    Mwishowe, wanafunzi hawa walimaliza masomo yao na kuachia 
    shule yao makumbusho ya milele. Walianza maisha mapya 
    wakawa walimu mashuhuri. Baada ya miaka miwili, Matabaro na 
    Mukabutera walifunga ndoa na kuzaa mtoto anayeitwa Rubangura. 
    Punde si punde, Butera na Nyiratabaro walioana wakazaa mtoto 
    anayeitwa Rubaduka. Familia hizi ziliendelea kuishi pamoja na 
    kushirikiana katika shughuli zote za nyumbani.

    Kazi ya 2:
    Maswali ya ufahamu:
    1. Taja uhusiano uliopo baina ya Butera na Mukabutera.
    2. Bi. Nyiramavugo atamwitaje Mukabutera?
    3. Bw. Rutebuka atamwitaje Matabaro?
    4. Jaza mapengo kwa neno faafu:
    a. Bw. Rutebuka ni …………… wa Bi. Nyiranzage.
    b. Mukagatera ni ………….. yake Butera.
    c. Rutebuka ni ………….. yao Matabaro na Nyiratabaro.

    5. Nyiramavugo atamwitaje mke wa Butera?

    Kazi ya 3:
    Kamilisha sentensi zifuatazo kwa kutumia msamiati wa uhusiano wa 
    kifamilia unaofaa.

    1. Mama ya mama yangu anaitwa………………………. 
    2. Ndugu wa kike wa baba yangu anaitwa ……………….
    3. Baba ya mume wangu anaitwa …………………………
    4. Mtoto wa mtoto wangu anaitwa…………………………
    5. Baba ya baba yangu anaitwa ……………………………..
    6. Mtoto wa mjukuu wako anaitwa …………………………. 
    7. Mama ya mke wako anaitwa ……………………………..
    8. Mwanamke aliyeolewa na babako, na ambaye si mama yako wa 
    damu anaitwa …………………………………………………….
    9. Mtoto wa kwanza kuzaliwa anaitwa …………………………….
    10. Mtoto wa mwisho kuzaliwa anaitwa………………………… 
    Maelezo muhimu kuhusu uhusiano wa kifamilia
    • Mjomba: Mvulana aliyezaliwa na dada yako au kaka ya mama yako.
    • Shangazi: Msichana aliyezaliwa pamoja na baba yako au ndugu wa kike wa baba yako. 

    • Mpwa: Mtoto wa dada yako.

    • Binamu: Mtoto wa mjomba wako au wa shangazi yako. 
    • Shemeji: Ni ndugu zote wa mkeo au ndugu za kiume wa mumeo.
    • Wifi: Jina wanaloitana dada zako na mkeo. 
    • Mkaza mjomba: Mke wa mjomba wako. 
    • Mkaza mwana: Mke wa mtoto wako. 
    Mavyaa: Jina linalotumiwa katika kuitana baina ya mke na mama mkwe wake. 
    Kifunguamimba: Mtoto wa kwanza kuzaliwa. 
    • Kitindamimba:Mtoto wa mwisho kuzaliwa. 
    • Mapacha: Watoto wawili waliozaliwa siku moja kutokana na mimba moja. 
    • Baba wa kambo: Mwanaume aliyeoa mamako na ambaye si baba yako wa damu. 
    • Mama wa kambo: Mwanamke aliyeolewa na babako, na ambaye si mama yako wa damu. 
    • Kitukuu: Mtoto wa mjukuu. 
    • Kilembwe: Mtoto wa kitukuu. 
    Kilembwekeza/Kinying’inya: Mtoto wa kilembwe. 
    Kitojo: Mtoto wa kilembwekeza.
    7.2. Msamiati kuhusu uhusiano wa kifamilia
    Kazi ya 4:
    Eleza maneno yalopigiwa mistari katika sentensi hizi:
    1. Watoto wanaheshimu wazazi wao.
    2. Tunampokea nyanya yetu nyumbani.
    3. Kifunguamimba kutoka familia ya mjomba wetu anahifadhi mazingira.
    4. Baba wa kambo wa Juma anamsadia mtoto mwenzake mwenye matatizo ya kutembea.
    5. Binamu yenu anaunda shirika la kutetea watoto wenye matatizo.

    7.3. Sarufi: Matumizi ya vivumishi vya kuuliza katika ngeli ya LI-YA 

    Kazi ya 5:
    Chunguza sentensi zifuatazo kisha ueleze muundo wa vivumishi 
    vilivyotumiwa.

    1. Jengo lipi ni kubwa? 
    2. Mapapai yapi yameiva? 
    3. Tukupe magunia mangapi? 
    4. Mashirika gani yanasaidia wakulima? 
    5. Wewe unataka nikupe jembe lipi?
    Maelezo muhimu kuhusu vivumishi viulizi
    Vivumishi viulizi hutumika kuuliza swali kuhusu nomino. Vivumishi hivi 
    vinapotumiwa katika sentensi ni sharti sentensi hiyo ikamilishwe kwa alama 
    ya kiulizi. Vivumishi viulizi ni vitatutongueouti?, -ngapi? na -gani? Vivumishi viulizi 
    -ngapi? na -pi? huchukua viambishi vya ngeli lakini kiulizi “gani” hakichukui 
    kiambishi chochote cha ngeli.
    Kwa mfano: 
    1. Gari lipi linatembea? 
    2. Magari yapi yanatembea? 
    3. Je, nyumba yako ina madirisha mangapi? 
    4. Unapenda shirika gani? – 
    5. Unapenda mashirika gani?
    Kazi ya 6:
    Tumia vivumishi viulizi vilivyomo mabanoni ili kujaza sentensi 
    zifuatazo: 

    1. Jibu .............. limeishapatikana? (-pi) 
    2. Mawe ................. yamewekwa kando ya barabara? (-ngapi) 
    3. Madirisha .............. yamefunguliwa? (gani) 
    4. Meno ................ yameng’oka? (-pi) 
    5. Tunda ................ limeiva? (gani)

    Kazi ya 7:

    Andika sentensi zifuatazo katika umoja ama wingi. 
    1. Jengo lipi ni kubwa? 
    2. Mapapai yapi yameiva? 
    3. Tukupe magunia yapi? 
    4. Mashirika gani yanasaidia wakulima? 
    5. Wewe unataka nikupe jembe lipi?
    7.4. Matumizi ya lugha
    Kazi ya 8:
    Soma maelezo hapo juu kuhusu uhusiano wa kifamilia kisha umwambie 
    mwenzako hali halisi ya kila mtu katika familia yako binafsi.
    7.5. Kusikiliza na Kuzungumza
    Kazi ya 9:
    Baada ya kusoma maelezo kuhusu uhusiano wa kifamilia, zungumzia 
    darasa ukoo wako.
    7.6. Kuandika 
    Kazi ya 10:
    Tunga mazungumzo kuhusu 
     “ uhusiano wa kifamilia” ( angalau misitari 15)

    SOMO LA 8: VIFAA VYA NYUMBANI NA USAFI WAKE

    Kazi ya 1:

    Orodhesha vifaa mnavyotumia nyumbani kwenu mnapofanya usafi.

    8.1. Kusoma na ufahamu: Vifaa vya nyumbani na usafi wake 

    bb

    Usafi wa nyumbani na vifaa vyake ni njia ya kuendeleza afya kwa kuzuia 
    maradhi yanayotokana na athari za taka kwa binadamu. Athari hizo zinaweza 
    kuhusu miili yetu. 

    Usafi wa nyumbani ni jambo ambalo linafaa kutiliwa maanani na kila mtu, 
    kwani uchafu unachangia pakubwa kuharibu maisha ya binadamu. Jambo 
    la kushangaza ni kwamba watu wengi wanafikiri kuwa usafi unahusu miili na 
    mavazi tu, wakisahau kuwa usafi huhusu kila kitu kinachopatikana katika 
    mazingira wanamoishi.

    Tunapozungumzia usafi wa nyumbani, watu wengi huelewa shughuli 
    muhimu zinazostahili kufanywa katika kusafisha vyumba vya nyumbani na 
    kutengeneza bustani zinazozunguka nyumba hiyo. Lakini, ni lazima kujua 
    kwamba usafi huchunguzwa kupitia vifaa vya nyumbani vinavyotumiwa 
    kama vile: sahani, vikombe, vijiko, sufuria,vijiko, nguo, meza, kabati, 
    runinga, redio,na kadhalika. Tena inafaa kusafisha sehemu zote za nyumba 
    kama vile vyumba vya kula, sebule, jikoni, chooni, bila ya kusahau bustani.

    Kabla ya kufanya usafi wa vifaa na sehemu za nyumba, sisi wenyewe 
    tunaombwa kuwa na usafi ipasavyo. Kama vile: Kunawa mikono kwa maji 
    na sabuni hupunguza kwa kiasi kikubwa maambukizo ya ugonjwa wa 
    kuhara. Wazazi na walezi wengine wanapaswa kunawa mikono kwa sabuni 
    kila baada ya kumhudumia mtoto mchanga au mtoto mdogo aliyejisaidia, 
    kumpeleka mtoto msalani, kutoka msalani wao wenyewe, kabla ya kuandaa 
    chakula, kabla ya kulisha watoto wadogo na baada ya kuondoa takataka.
    Wazazi na walezi wengine wanapaswa kuwajengea watoto tabia ya kunawa 
    mikono kwa maji safi na sabuni kabla ya chakula na baada ya kutoka 
    msalani. Kinyesi cha wanyama na binadamu kisiruhusiwe kukaa ndani ya 
    nyumba, njiani, kwenye vyanzo vya maji na katika maeneo ya kuchezea 
    watoto. Matumizi ya vyoo pamoja na tabia ya usafi, hasa unawaji wa mikono 
    kwa sabuni ni mambo muhimu kwa afya ya jamii. Hutoa kinga kwa watoto 
    na kwa kaya kwa gharama nafuu pamoja na kuwapatia watoto haki yao ya 
    kuwa na afya njema na lishe bora.

    Tunaposafisha nyumba tunatumia maji, sabuni za kawaida, na sabuni za 
    majimaji au dawa za kuulia wadudu wenye kuambukiza watu magonjwa 
    mbalimbali.Tunawaonya watu wasitupe uchafu ovyoovyo. Taka ambazo 
    zinaweza kusababisha matatizo ya afya ni kinyesi cha binadamu na cha 
    wanyama, taka ngumu, maji machafu, taka za viwandani, na za kilimo, n.k. 
    Taka zote zinazotokana na vitu vyote vilivyotumiwa zinafaa kutupwa mahali 
    panapofaa kama vile jalalani au zikachomwa kupitia njia zinazokubaliwa. 
    Nyasi nazo zinazozunguka nyumba zetu zinafaa kufyekwa ili kuwafukuza 
    mbu wanaosambaza ugonjwa wa malaria.

    Maji yote ya kunywa na ya matumizi mengine yatoke kwenye vyanzo salama 
    na yachemshwe baadaye au yanyunyiziwe dawa ya kuulia vijidudu. Vyombo 
    vya kuwekea na kuhifadhia maji vitunzwe vizuri ndani na nje na kufunikwa ili 
    kuepukana na uchafu wa maji. Ni lazima iwepo mikakati rahisi ya kusafisha 
    maji yawe safi nyumbani kama vile kuyachemsha, kunyunyizia dawa ya maji 
    (klorini) ili kuua vijidudu. Vyakula vibichi au mabaki ya vyakula vilivyopikwa 
    yanaweza kuwa hatari. Vyakula vibichi visafishwe kwa maji safi kabla ya 
    kupikwa. Chakula kilichopikwa kiliwe kikiwa moto na kiporo kipashwe moto 
    vizuri kabla ya kuliwa. Chakula, vyombo na eneo la kutayarishia chakula 
    halina budi kuwa safi na mbali na wanyama.

    Chakula kihifadhiwe kwenye vyombo vilivyofunikwa. 

    Upungufu wa usafi wa mazingira ni sababu kuu ya maradhi kote duniani. 
    Uboreshaji wa mazingira una manufaa makubwa kwa afya ya watu katika 
    kaya na katika jamii.

    Kazi ya 2:
     Maswali ya ufahamu 
    1. Ni sehemu zipi za nyumba ambazo huhitaji usafi?
    2. Taja vifaa vya nyumbani vilivyotajwa katika kifungu hiki.
    3. Kwa sababu gani watoto wanapaswa kuepukana na uchafu?
    4. Tunatumia nini katika kufanya usafi wa nyumbani?
    5. Wazazi au walezi wengine wanafundisha watoto wao nini kuhusu 
    usafi?
    6. Ni umuhimu gani wa kuwa na maji safi?
    7. Ni dosari zipi za upungufu wa usafi kwa binadamu?
    8.2. Msamiati
    Kazi ya 3:
     Tunga sentensi sahihi kwa kutumia maneno yafuatayo:
    1. Athari
    2. Maanani
    3. Kuhara 
    4. Kinga
    5. Takataka
    6. Kaya
    Kazi ya 4:
    Baada ya kusoma kifungu cha habari hapo juu, kamilisha sentensi 
    zifuatazo kwa kutumia maneno yafuatayo: runinga, redio, kijiko, 
    sufuria, meza, malaria, usafi, tabia, sabuni, linafaa, vifaa.
    1. Mama anapika chakula ndani ya……………….
    2. Tunaposoma kiswahili nyumbani tunaandikia kwenye………..
    3. Nyanya yangu anatumia………….. wakati mimi ninatumia uma.
    4. Tunasikiliza habari za mpira kwenye………………
    5. Wanafunzi hupenda kutazama filamu kwenye…………
    6. Usafi nyumbani ni jambo ambalo ………..kutiliwa maanani.
    7. Watu wengi wanafikiri kuwa ……..unahusu miili na mavazi tu. 
    8. Usafi nyumbani huonekana kupitia ………. vinavyotumiwa nyumbani.
    9. Kunawa mikono kwa maji na …………hupunguza kwa kiasi kikubwa 
    magonjwa.
    10. Wazazi na walezi wengine wanapaswa kuwazoeza watoto ……….
    ya kunawa mikono kwa maji safi.
    11. Nyasi nazo zinazozunguka nyumba zetu zinafaa kukatwa ili 

    kuwafukuza mbu wanaosababisha ugonjwa wa…………..

    8.3. Sarufi: Nomino za ngeli ya LI-YA na vivumishi vya 

    kumiliki 
    Kazi ya 5:
    Chunguza mifano ya sentensi hapa chini, kisha ueleze aina za 
    maneno yaliyopigiwa mstari. 

    1. Koti langu limechafuka.
    2. Shirika lako linajulikana sana.
    3. Gari lake ni la kifahari. 
    4. Jumba letu linapendeza
    Maelezo muhimu kuhusu matumizi ya nomino za ngeli ya LI-Ya na 
    vivumishi vya kumiliki
    Vivumishi vya kumiliki ni -angu, -ako, -ake, -etu, -enu na -ao. Vivumishi 
    hivi katika ngeli ya Li-Ya huchukua kiambishi konsonanti l- katika umoja na 
    y- katika wingi. 
    Kazi ya 6:
    Andika wingi wa sentensi za hapa chini.
    Umoja                                                                                Wingi 
    1. Jembe langu limepotea. ------------------------------------------- 
    2. Janga kubwa limesababisha maafa. ----------------------------------
    3. Jaribio la leo limesahihishwa. ------------------------------------------- 
    4. Jeshi lao lina askari wengi. ------------------------------------------- 
    5. Jeraha lake lina uchafu sana. ------------------------------------------- 
    6. Jambo hili liliwafurahisha wengi. ----------------------------------------
    7. Jicho lake linaona mbali sana. ------------------------------------------
    8. Jiwe langu lina thamani kubwa. -----------------------------------------
    9. Jino lako limeng’oka? ------------------------------------------- 
    10. Jiko langu limeharibika. -------------------------------------------
    8.4. Matumizi ya lugha
    Kazi ya 7:
    Katika makundi ya wanafunzi wawili wawili jadilini kuhusu “Umuhimu 
    wa usafi na madhara ya kutokuwa na usafi.”
    Kazi ya 8:
    Eleza umuhimu wa vifaa hivi vya usafi:
    1. Bafu 
    2. Sabuni
    3. Deki 
    4. Ufagio 
    5. Taulo 
    8.5. Kusikiliza na Kuzungumza
    Kazi ya 9:
    Mwambie mwenzako namna mnavyofanya usafi nyumbani kwenu 
    na usafi wa vifaa vya nyumbani.
    8.6. Kuandika
    Kazi ya 10:
    Tunga kifungu cha habari kwa kutumia kichwa kifuatacho (maneno 
    yasiyopungua mia moja): “Uchafu ni asili ya maradhi mengi.”

    SOMO LA 9: MSAMIATI KUHUSU MIFUGO

    gg

    Kazi ya 1:
    Jiunge na mwanafunzi mwenzako. Kumbushaneni majina ya mifugo 

    mbalimbali mnayoyajua.

    9.1. Kusoma na ufahamu: Kazi nzuri ya ufugaji.

    cc

    Huyu ni Ikirezi. Ikirezi ni mfugaji wa nyuki. Ikirezi anarina asali. Baada ya 
    kurina, yeye husafisha asali yake na kuiuza. Asali hiyo hutumiwa kama 

    chakula au hutengenezewa dawa.vv

    vvvv

    Huyu ni Ituze. Ituze anakama ng’ombe. Kabla ya kukama, aliosha chuchu 
    kwa maji vuguvugu na kuzikausha kwa kitambaa safi. Anatumia mkebe safi 

    kuwekea maziwa. Ituze huwapandisha madume kwa mitamba au mpira.

    cc

    Hili ni josho. Ng’ombe hawa wanaogeshwa kwa dawa ndani ya josho. 
    Wafugaji huosha mifugo katika josho ili kuwakinga dhidi ya kupe. Dawa 

    huua viroboto wanaoishi kwenye ngozi za mifugo.

    cc

    Hawa ni Mudenge na Gatera. Mudenge anawalisha kuku kwa mahindi. Pia, 
    huwapa kuku mtama, ugali, wadudu na vyakula vinavyopatikana kwa urahisi. 
    Wakati mwingine, yeye huwapa kuku chakula maalumu kilichotengenezewa 
    katika viwanda. Mudenge anawafuga kuku wa mayai na wa nyama. Yeye 
    huuza baadhi ya mayai ili kujipatia riziki. Mudenge, pia, huwaatamisha 
    baadhi ya kuku wake ili apate vifaranga wa kuuza na kufuga. 

    Gatera, naye, anawalisha ng’ombe kwa nyasi. Gatera anawafuga ng’ombe 
    wake ndani kwa ndani. Anawapa lishe, maji na dawa humo humo zizini. 
    Gatera hukata pembe za ng’ombe wake. Ng’ombe hukatwa pembe ili 

    kumzuia kumdhuru mtu au kuharibu vitu.

    bb

    Huyu ni Kaliza. Kaliza anapenda kuchunga farasi. Anawachunga farasi 
    penye maji safi na nyasi nyingi. Kulisha mifugo ni shughuli muhimu ya 
    ufugaji. Mifugo wanapolishwa vizuri hukua kwa haraka, huwa na afya nzuri 

    na hutupatia mapato mazuri.

    vvv

    Kaliza anafagia zizi la ng’ombe. Mfugaji bora husafisha makao ya mifugo na 
    vyombo vyao vya kulia, kunywea na kulalia. Mifugo wanaolala katika mahali 

    safi na kulia katika vyombo safi huwa na afya njema.

    fff

    Daktari wa mifugo anamtibu kuku kwa kumdunga sindano. Kutibu mifugo 
    ni muhimu kwa mfugaji. Ni vizuri kutambua dalili ya ugonjwa ili watibiwe 
    mapema.
    Kazi ya 2:
    Maswali ya ufahamu
    1. Andika majina yote ya mifugo yaliyotajwa hapo juu.
    2. Asali ina umuhimu gani kwa maisha ya binadamu?
    3. Kwa sababu gani tunakata sufu ya kondoo?
    4. Kabla ya kukama ng’ombe, tunaombwa kufanya nini kwanza?
    5. Chagua mifugo watano katika vifungu vya habari hapo juu kisha 
    utaje umuhimu wao kwa binadamu.
    6. Kwa maoni yako, ufugaji unaleta matunda gani kwa maendeleo 
    ya nchi?
    9.2. Msamiati kuhusu mifugo 
    Kazi ya 3:
    Baada ya kusoma kifungu cha habari hiki, toa maana ya msamiati 
    unaofuata:

    • kurina 
    • kukata sufu 
    • kukama 
    • kupandisha madume kwa mtamba 
    • kufuga ng’ombe ndani kwa ndani 
    • kuwapeleka ng’ombe katika josho 
    • kuatamisha kuku 
    • kuchunga 

    • kukata pembe

    bbb

    9.3. Sarufi: Ngeli ya LI –YA na Vivumishi vya kuonyesha. 
    Kazi ya 5:

    Tazama sentensi zifuatazo na kujadili mabadiliko ya kisarufi yanayojitokeza.

    vvv

    Maelezo muhimu 
    Vivumshi vya kuonyesha hili, hilo, lile hufuata nomino katika umoja. 

    Vivumishi vya kuonyesha haya, hayo, yale hufuata nomino katika wingi. 

    Kazi ya 6:
    Chagua neno sahihi katika mabano na kujaza pengo.
    1. Debe ………….. lilitoboka (hii, haya, hili, hiyi). 
    2. Jambazi ……….liliadhibiwa (yule, hii, lile, hiyo). 
    3. Tafadhali kunja majamvi………..(ayo, hizo, hayo, halo). 
    4. Anakuomba umnunulie machungwa ………….(hizo, hayo, yayo). 
    5. Jahazi …….ni kubwa (lili, hile, jile, lile). 

    Kazi ya 7:
    Sahihisha sentensi zifuatazo: 
    1. Kabati kale kalivunjwa na wezi. 
    2. Maji haya alimwagwa ovyo sakafuni. 
    3. Alipotaka kujenga nyumba alitafuta majiwe makubwa. 
    4. Mafuta haya haamwagwi ziwani kwa sababu anaweza kuua samaki. 

    5. Maboga haya yana manufaa nyingi kwa mwili wako. 

    9.4. Matumizi ya lugha 
    Kazi ya 8:

    Husisha majina haya na mifugo wanaopatikana hapo chini: mbuzi, 

    mbwa, kuku, paka, na sungura.

    dd

    9.5. Kusikiliza na Kuzungumza: Majadiliano
    Kazi ya 9:
    Zungumzia wanafunzi jinsi mnavyofanya ufugaji wengine namna 
    gani nyumbani kwenu au kwa babu yako mnavyofanya ufugaji.
    9.6. Kuandika 
    Kazi ya 10:

    Tunga kifungu kifupi cha maneno yasiyozidi 100 kuhusu “Umuhimu 
    wa ufugaji nchini Rwanda.”

    Tathmini ya mada
    1. Tumia maneno yafuatayo ya ngeli ya LI-YA na vivumishi vya 
    kumiliki au vya kuonyesha katika sentensi sahihi katika 

    umoja. 
    a. Azimio
    b. Ini
    c. Jiko
    d. Ua
    e. Shamba
    2. Tumia sentensi za hapo juu katika wingi.
    3. Jaza sentensi zifuatazo kwa kutumia maneno: baba, wifi, 
    mama, shangazi, mjomba, mjukuu, binamu, mpwa, mapacha, 
    baba wa kambo. 
    a. Mke wa baba yako ni ……………………………….. yako.
    b. Mume wa mama yako utamuita……………………… yako.
    c. Mtoto wa mjomba au shangazi yako ni……………..
    d. Mtoto wa mtoto wako utamuita…………..
    e. Bwana ya mama yako ambaye si baba yako utamuita……..
    f. Dada ya baba yako utamuita……………………………….
    g. Kaka ya mama yako utamuita………………………………..
    h. Mke wa ndugu yako utamuita…………………………….
    i. Watoto wawili waliozaliwa siku moja na mama mmoja 
    tutawaita……..
    j. Mtoto wa dada yako utamuita……….

    4. Andika umuhimu wa vifaa vya nyumbani vifuatavyo:

    vv

    5. Tunga insha ndogo ya maneno yasiyozidi 100 kuhusu “Umuhimu 

    wa kuishi katika nyumba ya kisiasa kwa maisha ya binadamu”



  • MADA YA 3 MSAMIATI KATIKA MAZINGIRA YA HOSPITALI

    Uwezo mahususi katika mada hii: 
    Kuzungumza na kuandika kwa ufasaha matini fupifupi kwa kutumia msamiati 
    unaofaa katika mazingira ya hospitalini.
    Malengo ya Ujifunzaji:
    • Kutumia kwa ufasaha msamiati maalum wa mazingira ya hospitali katika mawasiliano;
    • Kueleza vifaa vya hospitalini na umuhimu wake,
    • Kubainisha wafanyakazi wa hospitalini na majukumu yao,
    • Kusikiliza kwa makini na kusoma kwa ufasaha kifungu cha habari kinachohusika,

    • Kunyambua vitenzi kwa kuzingatia kauli mbalimbali.

    Kidokezo
    1. Hospitali ni nini?
    2. Orodhesha angalau hospitali tatu muhimu zinazojulikana nchini Rwanda.
    3. Taja vifaa vitano vinavyotumiwa hospitalini na kueleza umuhimu wake.
    4. Bainisha wafanyakazi angalau wanne wapatikanao hospitalini na kuainisha kazi au majukumu yao.

    SOMO LA 10: SEHEMU ZA HOSPITALI

    vvv

    Tazama kwa makini mchoro hapa juu. Zungumzia vitu muhimu 
    unavyoona vyenye uhusiano na hospitali.

    10.1. Kusoma na ufahamu: Ziara yetu hospitalini

    vv

    Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Maadili wamefanya ziara kwenye hospitali 
    moja wilayani Huye. Shabaha yao ni kuielewa vyema hospitali. Wamekaribishwa 

    na mpokezi wageni ambaye amewaongoza kwa Daktari Mkuu.

    Daktari: Hamjambo vijana!
    Vijana: Hatujambo Daktari! 

    Aminata: Jina langu ni Aminata na mimi ndimi kiranja wa darasa letu. Hawa 
    ni wanafunzi wenzangu.
    Tumefurahia fursa hii ya kuitembelea hospitali yenu kwa ajili ya kuyaelewa 
    vyema mazingira ya hospitali. 

    Daktari: Asante sana kwa nia yenu. Kwa hiyo, karibuni nyote! 
    Mimi ni Birashoboka, Daktari Mkuu wa hospitali hii. Na huyu ni muuguzi 
    wetu, jina lake Veneranda. 
    Nifuateni sasa niwatembeze sehemu mbalimbali za hospitali.

    Muuguzi: Tuanzie kwenye sehemu ambapo mmekaribishiwa na kupata kiti. 
    Sehemu hiyo huitwa pambajio. Ni sehemu ya kuwapokelea wagonjwa. 
    Pascal: Samahani Daktari! Sisi siyo wagonjwa, msije mkatudunga sindano!

    Daktari: Hahaaaa! Usiwe na wasiwasi kijana! Tafadhali tuendelee. Sehemu 
    hii ni chumba cha matibabu ya dharura, yaani chumba cha kuwatibia 
    wagonjwa wanaohitaji matibabu ya haraka sana kama vile majeruhi wa ajali. 

    Muuguzi: Samahani Daktari! Ni vizuri kuelewa kwamba chumba cha 
    dharura ni tofauti na wodi kwani wodi ni chumba cha kushughulikia maradhi 
    ambayo si ya kawaida kama vile maradhi ambayo yamezuka ghafla na bado 
    hayaeleweki vizuri. 

    Daktari: Asante sana Muuguzi! Kama nyongeza, kuna wodi nyingine 
    ambayo ni sehemu ya kuwalaza wagonjwa wanaoendelea na matibabu.

    Samilla: Samahani Daktari! Kwenye mlango ule nimesoma neno maabara. 
    Je, nini maana ya neno hili?

    Daktari: Vizuri sana! Maabara ni chumba cha kufanyia uchunguzi wa 
    magonjwa. Kwa kuwa hatuna muda wa kutosha wa kuizunguka hospitali 
    yote, inafaa kusimamia hapa na kumwomba Muuguzi awaelezee sehemu 
    nyingine za hospitali.

    Muuguzi: Asante sana Daktari! Kuna chumba cha kuhifadhia dawa; 
    kuna kungawi, yaani chumba cha kujifungulia kwa kina mama wajawazito; 
    chumba cha upasuaji; chumba cha uangalizi maalum ambacho ni chumba 
    cha matibabu ya kiwango cha juu sana. Hususan chumba hiki hutumiwa 

    kwa wagonjwa walio katika hali mahututi. 

    Daktari: Chumba hiki huwa na mitambo na mashine za hali ya juu sana za kumsaidia mgonjwa. 
    Muuguzi: Chumba cha mwisho ni ufuoni au makafani ambacho hutumiwa kuhifadhia maiti. 
    Jado: Asante sana kwa maelezo haya. Ningependa sasa mtuelezee kuhusu vifaa muhimu vinavyotumiwa humu.

    Kazi ya 2:
    Maswali ya ufahamu
    a. Soma kifungu cha habari hapa juu na kujibu maswali ya ufahamu yafuatayo:
    1. Habari hii imetokea wapi?
    2. Ni lengo gani la wanafunzi kuitembelea hospitali?
    3. Ni watu gani wanaozungumziwa katika kifungu cha habari hiki?
    4. Ni sehemu zipi za hospitali zilizotajwa?
    5. Aminata alikuwa na wajibu gani?
    b. Chagua jibu lililo sahihi kuliko mengine 
    1. Kifungu hiki cha habari kinazungumzia:
    a. Wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Maadili na Daktari.
    b. Vifaa na wafanyakazi wa hospitali wilayani Huye.
    c. Ziara ya wanafunzi wa Shule ya Sekondari Maadili kwenye hospitali moja wilayani Huye.
    d. Mazungumzo kati ya wanafunzi wa Shule ya Sekondari Maadili kuhusu uchaguzi wa mchepuo wa udaktari.

    2. Walipofika hospitalini, wanafunzi walikaribishwa na

    a. Muuguzi.
    b. daktari mkuu.
    c. nesi.
    d. mpokeaji.
    3. wanafunzi walitembezwa sehemu za hospitali na
    a. daktari mkuu.
    b. muuguzi pamoja na daktari mkuu.
    c. mpokezi.
    d. majibu yote ni sahihi.
    4. Wanafunzi walielezewa vyumba vingapi ?
    a. vyumba tisa.
    b. vyumba vitatu.
    c. vyumba kumi.
    d. vyumba vitano.
    e. hakuna jibu sahihi.
    5. Kungawi ni chumba cha:
    a. kuwapasulia wajawazito.
    b. kuzalia wajawazito.
    c. kununulia dawa.
    d. kulalia wagonjwa.

    10.2. Matumizi ya msamiati kuhusu mazingira ya hospitali

    Kazi ya 3:

    Kwa kutumia Kamusi ya Kiswahili Sanifu au njia nyingine tofauti, toa 
    maana ya msamiati ufuatao na kuutungia sentensi sahihi.

    1. Kudunga                                 6. Kuhifadhi
    2. Matibabu                                7. Uchafu
    3. Mgonjwa                                8. Mjamzito
    4. Hali mahututi                      9. Kujifungua
    5. Kupenyeza                           10. Dharura

    Kazi ya 4:

    Oanisha maneno katika sehemu A na maana zake kutoka sehemu B.

    vv

    10.3. Sarufi: Matumizi ya kauli za vitenzi
    Kazi ya 5:
    Soma sentensi zifuatazo na kutofautisha viambishi vilivyokolea
    Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Maadili walikuwa wanapendana sana. 
    Waliandaa mpango wa kumwandikia Daktari Mkuu wa Hospitali kwa ajili 

    ya kuitembelea hospitali yake.

    Maelezo muhimu
    Viambishi vilivyokolea ni viambishi vya mnyambuliko wa vitenzi. 
    Mnyambuliko wa vitenzi ni jinsi vitenzi vinavyobadilika kulingana na kauli/

    hali mbalimbali.

    Hapo juu, kauli za vitenzi zilizotumiwa ni tatu kama ifuatavyo:
    i. Kauli ya kutenda.
    ii. Kauli ya kutendana.
    iii. Kauli ya kutendea.
    Yafuatayo ni maelezo kwa kila aina ya kauli: 
    1. Kauli ya Kutenda - kitendo katika hali yake ya kawaida (bila kunyambuliwa).
    2. Kauli ya Kutendana - unamfanya mtu kitendo, naye anakufanya vivyo hivyo.
    3. Kauli ya Kutendea - kufanya kitendo kwa niaba (au kwa ajili) ya mtu mwingine.

    Kazi ya 6:

    Onyesha mnyambuliko wa vitenzi ulivyochagua kisha uviweke katika 
    hali ya kutendea na kutendeana.

    Kazi ya 7:
    Tunga sentensi ambazo vitenzi vyake vinabeba kauli ya kutenda, 
    kutendea na kutendana 

    Kazi ya 8:
    Andika vitenzi vifuatavyo katika hali ya kutendea kwa kuzingatia 
    mabadiliko ya kimaana.
    1. Tumeandika barua kwa ajili ya rafiki zetu.
    2. Wazazi walifanya mema kwa niaba ya watoto wao
    3. Baba yake ameweka pesa kwenye akaunti kwa manufaa ya mtoto wake.

    10.4. Matumizi ya lugha: Sehemu muhimu za hospitali
    Maelezo muhimu kuhusu sehemu muhimu za hospitali
    Hospitali ni mahali pa kutibia wagonjwa. Kuna hospitali kubwa na nyingine 

    ndogo. Hospitali ndogo huitwa dispensali au zahanati.

    Hospitali ina sehemu muhimu zifuatazo:
    1. Pambajio: Sehemu ya kuwapokelea wagonjwa.
    2. Wodi: Sehemu ya kuwalaza wagonjwa wanapoendelea kupokea 
    matibabu.
    3. Kungawi: Chumba cha kujifungulia kwa waja wazito.
    4. Chumba cha upasuaji: Chumba cha kufanyiwa upasuaji wa wagonjwa.
    5. Wodi wa matibabu maalum: Chumba cha kushughulikia maradhi ambayo si ya kawaida k.m. maradhi ambayo yamezuka ghafla na bado hayaeleweki vizuri.
    6. Chumba cha matibabu ya dharura: Chumba cha kuwatibia wale wanaohitaji matibabu ya haraka sana k.m. waathiriwa wa ajali.
    7. Chumba cha matibabu ya kina: Chumba cha matibabu ya kiwango cha juu sana. Hususan hutumiwa kwa wale walio katika hali 
    mahututi. Chumba hiki huwa na mitambo na mashine za hali ya juu za kumsaidia mgonjwa.
    8. Maabara: Chumba cha kufanyia utafiti.
    9. Chumba cha dawa: Chumba cha kuhifadhia dawa zitolewazo kwa wagonjwa.
    10. Ufuoni/makafani: Mahali pa kuhifadhia maiti.

    10.5. Kusikiliza na Kuzungumza

    Kazi ya 10:
    Sikiliza taarifa ya habari moja kutoka redio au runinga juu ya mambo 
    ya afya. Isimulie mbele ya darasa.
    Kazi ya 11:
    Kwa ushirikiano na wenzako, igiza mazungumzo hapo juu
    Kazi ya 12:
    Fikiria zahanati au hospitali moja uliyoitembelea, kisha zungumzia 

    chumba kimoja ambamo uliingia na sababu za kuitembelea.

    10.6. Kuandika
    Kazi ya 13:

    Chora hospitali moja na kuonyesha sehemu zake angalau nne na 

    kueleza umuhimu wake

    bb

    Kazi ya 1:
    Tazama kwa makini mchoro hapa juu. Zungumzia vitu muhimu unavyoona 

    vyenye uhusiano na hospitali.

    11.1. Kusoma na ufahamu: Vifaa vya hospitalini

    vv

    Daktari: Kabla ya kutembelea vyumba vyote ambamo mmepatikana vifaa 
    mbalimbali, tazameni picha hizi za vifaa vipatikanavyo hospitalini. Picha hii ni ya 
    eksrei au uyoka ambayo ni mashine ya kutazamia viungo vya ndani ya mwili. 
    Muuguzi: Hii ni machela, yaani kigari au kitanda cha kubebea wagonjwa. 
    Aminata: Tafadhali Muuguzi. Je, naweza kuwasaidia? Picha inayofuata 
    ninajua jina lake.
    Muuguzi: Vizuri sana! Kushirikiana katika kazi zote ni jambo muhimu sana. 
    Fursa ni yako kiongozi wa darasa.
    Aminata: Ile ni mikroskopu au hadubini. Inatumiwa kuangalia vijidudu 
    vidogo sana ambavyo haviwezi kuonekana kwa macho tu. 
    Daktari: Hongera Aminata! Tuendelee. Hii ni dipfriza ambayo ni chombo 
    cha kuhifadhia dawa katika kipimo cha baridi kali sana. 
    Muuguzi: Jiko lile hutumiwa kuchemshia vyombo ili kuulia vijidudu na bakteria. 
    Kifaa hiki chenye umbo sawa na soksi kinaitwa glovu. Kinavaliwa mkononi 
    kumkinga muuguzi dhidi ya uchafu au kuambukizwa na maradhi. 
    Daktari: Vifaa hivi ninadhani vinafahamika kwa kila mtu. Vijana, nani ambaye anaweza kutuelezea?
    Bugingo: Hizi ni sindano. Zinatumiwa kupenyezea dawa mwilini. Pembeni 
    kuna makasi ambazo hutumiwa kwa kukatia vitu mbalimbali. 
    Muuguzi: Vijana, mpigieni makofi! Bendeji hii ni kitambaa cha kufungia 
    jeraha au kidonda kisichafuliwe. 
    Na hii ni plasta ambayo ni kitambaa kigumu sana cha kufungia sehemu ya 
    mwili iliyovunjika. 
    Daktari: Mwishoni, koleo hii husaidia kama kifaa cha kushikia vitu 
    vinavyotumiwa na daktari.

    Kazi ya 2:
    Maswali ya ufahamu
    a. Soma kifungu cha habari hapa juu na kujibu maswali ya 
    ufahamu yafuatayo:

    1. Mazungumzo haya yametokea wapi?
    2. Ni madhumuni gani ya wanafunzi kuitembelea sehemu hii?
    3. Ni wahusika gani waliowasiliana?
    4. Baadhi ya vifaa vilivyoonyeshwa, ni kifaa kipi ambacho kingeweza kuwatia hofu wanafunzi?
    5. Daktari ametumia mbinu gani ya kuonyesha na kuelezea vifaa? 
    b. Chagua jibu lililo sahihi kuliko mengine
    1. Kifungu hiki cha habari kinazungumzia:
    a. Vifaa vitumiwavyo hospitalini
    b. Daktari na wanafunzi
    c. Ziara ya wanafunzi hospitalini
    d. Hakuna jibu sahihi

    2. Katika maelezo yake, Daktari ameungwa mkono na

    a. muuguzi
    b. kiongozi wa darasa
    c. wanafunzi
    d. muuguzi pamoja na wanafunzi wawili.
    3. Dipfriza ni mojawapo ya:
    a. Wafanyakazi wa hospitalini
    b. Dawa za hospitalini
    c. Sehemu za hospitali
    d. Vifaa vya hospitalini.
    4. Machela inatumiwa kubeba
    a. Dawa za wagonjwa
    b. Walemavu
    c. Vifaa vya hospitalini
    d. Wagonjwa hospitalini.
    5. Daktari au Muuguzi anatumia bendeji
    a. Kumfunga kamba mgonjwa
    b. Kufungia kidonda
    c. Kufungia sehemu iliyovunjika
    d. Kumwezesha mgonjwa kutembeatembea.

    11.2. Matumizi ya msamiati

    Kazi ya 3:
    Kwa kutumia Kamusi ya Kiswahili Sanifu au njia nyingine tofauti, toa 
    maana ya msamiati ufuatao na kuutungia sentensi sahihi.
    i. Vidudu
    ii. Bakteria
    iii. Kuhifadhi 
    iv. Jeraha

    v. Kidonda

    Kazi ya 4:
    Jaza nafasi iliyoachwa wazi kwa kutafuta msamiati unaofaa kwenye 

    upande wa maneno na maana kwenye upande wa maelezo

    v

    Kazi ya 5:
    Kamilisha sentensi zifuatazo ili zilete maana kamili kwa kutumia 
    msamiati huu: eksirei, plasta, sindano, kuhifadhia baadhi ya dawa.
    1. Kitambaa kigumu sana cha kufungia sehemu iliyovunjika 
    huitwa.......................................................
    2. Dipfriza ni chombo...................................
    3. .......................ni kifaa cha kupenyezea dawa mwilini.
    4. ..................ni mashine ya kuonea viungo vya ndani ya mwili.

    11.3. Sarufi: Matumizi ya kauli za vitenzi
    Kazi ya 6:
    Soma sentensi zifuatazo na kutofautisha viambishi vilivyokolea
    Baada ya mpango kukamilika, walifikisha hoja zao kwa Mkuu wa shule 
    ambaye aliridhika na nia hiyo ya wanafunzi wake.
    Baadaye, walitumiwa barua na Daktari Mkuu wa hospitali ya kuwakubalia 
    ziara yao. 
    Maelezo muhimu
    Kauli za vitenzi zilizotumiwa katika sentensi hapo juu ni zifuatazo:
    i. Kauli ya kutendeka
    ii. Kauli ya kutendesha
    iii. Kauli ya kutendewa
    Yafuatayo ni maelezo kwa kila aina ya kauli: 
    1. Kauli ya Kutendeka - kitendo kukamilika au kuwa katika hali timilifu.
    2. Kauli ya Kutendewa - kitendo kufanywa kwa niaba yako au kwa ajili yako.

    3. Kauli ya Kutendesha - kumfanya mtu atende jambo fulani.

    Kazi ya 7:
    Onyesha mnyambuliko wa vitenzi vifuatavyo katika hali ya kutendeka 
    na kutendewa 
    Vitenzi ni kunywa, kuzaa, kupenda, kutaja na kujenga.
    Kazi ya 8:
    Tunga sentensi 3 ambazo vitenzi vyake vinabeba kauli ya kutendeka, 
    kutendesha na kutendewa

    Kazi ya 9:
    Soma kisa kifuatacho na kuweka vitenzi husika katika hali ya 
    kutendewa
    Baba alimpatia mtoto wake elimu kuhusu uhifadhi wa mazingira, 
    uzalishajimali pamoja na usawa wa kijinsia. Alimwelezea pia faida za 
    kupiga marufuku uvivu, ulevi pamoja na ukatili. Alimtungia hadithi za 
    kumwongoza na kumwelekeza katika njia nzuri za kimaisha. Baadaye, 
    alimpelekea wajibu wa kuzitetea haki za binadamu na kuishi kwa amani na 
    watu wote mahali popote atakapokuwepo. 
    11.4. Matumizi ya lugha: Vifaa vya hospitalini
    Kazi ya 10:

    Taja majina ya vifaa vifuatavyo na kueleza umuhimu wa kila kifaa.

    vvv

    Kazi ya 11:
    Tafuta vifaa vingine vinavyotumiwa hospitalini na kueleza umuhimu wake.
    Maelezo muhimu
    Hospitali hutumia vifaa mbalimbali wakati wa kuhudumia wagonjwa. Baadhi 
    ya vifaa hivyo ni hivi vifuatavyo:
    1. Eksrei/uyoka: mashine ya kuonea viungo vya ndani ya mwili.
    2. Machela: kigari au kitanda cha kubebea wagonjwa. 
    3. Mikroskopu/hadubini: kifaa kitumiwacho kuangalia vitu vidogo.
    4. Dipfriza: chombo cha kuhifadhia baadhi ya dawa zinazohitaji kuhifadhiwa katika kiwango cha baridi sana.
    5. Jiko: chombo cha kuchemshia vyombo ili kuulia viini na bakteria.
    6. Glovu: kitu kama soksi kitengenezwacho kwa mpira na huwekwa mkononi kukingia uchafu.
    7. Sindano: kifaa cha kupenyezea dawa mwilini.
    8. Sirinji: kifaa chenye umbo la bomba ambapo madaktari na wauguzi huchopeka sindano ili kumdunga mgonjwa au kufyonza sampuli ya damu.
    9. Makasi: kifaa ambacho hutumiwa kwa kukatia 
    10. Bendeji: kitambaa cha kufungia jeraha au kidonda
    11. Plasta: kitambaa kigumu sana cha kufungia sehemu iliyovunjika
    12. Koleo: kifaa cha kushikia vitu vinavyotumiwa na daktari.

    11.5. Kusikiliza na Kuzungumza

    Kazi ya 12:
    Kwa ushirikiano na wenzako, igiza mazungumzo yanayohusu vifaa 
    vya hospitalini.
    Kazi ya 13:
    Itembelee zahanati au hospitali moja, kisha uzungumzie vifaa 

    ulivyowahi kuviona.

    Kazi ya 14:
    Simulia hisia ulizokuwa nazo au ulizosikia kutoka mtu mwingine 
    kuhusu siku yako au yake ya kwanza kudungwa sindano hospitalini.
    11.6. Kuandika
    Kazi ya 15:
    Kamilisha sentensi zifuatazo kwa kuongozwa na muktadha wa vifaa vya hospitalini
    a. Nilipokuwa bado mtoto nilikuwa na woga wa kuenda hospitalini kwa sababu....................................
    b. Inasemekana leo kuwa Hospitali ya Roi Faisal ni maarufu sana kwa sababu....................................
    c. Hospitali au zahanati nyingi hushindwa kutoa huduma bora kwa sababu ya..................................
    d. Sindano hospitalini hutumiwa mara moja kwa mgonjwa kwa ajili ya.............................................

    SOMO LA 12: WAFANYAKAZI WA HOSPITALINI

    hh
    Kazi ya 1:
    Tazama kwa makini mchoro hapo juu kisha uzungumzie vitu muhimu 

    unavyoviona

    12.1. Kusoma na ufahamu: Kazi nzuri ya udaktari

    bb

    Wanafunzi wameendelea na matembezi yao hospitalini. Sasa ni wakati 
    wa kuongea na wafanyakazi.
    Muuguzi: Shukrani Daktari, ningependa tuelekee sehemu ambapo 
    tutawapata wafanyakazi mbalimbali ili niwaelezee kazi zao. Daktari au 
    tabibu mnayemwona hapa ndiye anayewatibu wagonjwa. Mimi ni Muuguzi 
    au nesi. Kazi yangu ni kumsaidia daktari katika kazi yake. 
    Mkunga: Jina langu ni Liberata. Mimi ni Mkunga. Kazi yangu ni kutoa 
    huduma kwa wajawazito wakati wa kujifungua. 
    Mhazigi: Ninaitwa Jean Paul. Mimi ni mhazigi. Wajibu wangu ni 
    kuwashughulikia waliovunjika viungo kama vile miguu au mikono. 
    Msaidizi: Ninaitwa Francoise, Msaidizi katika maabara. Mimi hutoa huduma 
    kwa wagonjwa. 
    Karani: Jina langu ni Shema, Karani wa hospitali. Jukumu langu ni kufanya 
    rekodi za wagonjwa. 
    Mfamasia: Mimi ni mfamasia na jina langu Pascasie. Kazi yangu ni kuziweka 
    dawa na kuzitoa kwa wagonjwa. 
    Daktari wa meno: Byiringiro Charles, daktari wa meno. Jukumu langu ni 
    kuwashughulikia wagonjwa walio na matatizo ya meno.

    Aminata: Kwa mujibu wa wanafunzi wenzangu, tumenufaika zaidi kutokana 

    na safari hii. Kwa kweli, tungeliitembelea hospitali hii mwaka jana, tungelijua 
    haya yote tayari. Wahenga walisema kwamba asiyefika kwa mfalme 
    hudanganywa mengi. Tumebahatika kufika hapa na mengi tumeyaelewa. 
    Mireille: Sisi sote tumeridhika na maelezo tuliyopewa. Kwa upande wetu, 
    tunaahidi kuwaunga mkono kama iwezekanavyo kwa kuchagua mchepuo 
    wa udaktari ili kuwahudumia wagonjwa hospitalini.
    Daktari: Asanteni sana vijana. Kwa heri ya kuonana, tunawatakia kila la kheri!
    Aminata: Asante sana Daktari pamoja na Muuguzi, na sisi tunawatakia kazi 
    njema!
    Kazi ya 2:
    Soma kifungu cha habari hapo juu na kujibu maswali ya ufahamu 
    yafuatayo:

    1. Ni watu gani wanaozungumziwa katika mazungumzo haya?
    2. Matembezi haya yamekuwa na lengo lipi?
    3. Jadili faida pamoja na hasara kutoka ziara ya wanafunzi iliyozungumziwa.
    4. Wanafunzi wameridhika na ziara yao. Je, unakubaliana na ukweli huu? Eleza msimamo wako.

    12.2. Matumizi ya msamiati kuhusu mazingira ya hospitali
    Kazi ya 3:
    Kwa kutumia Kamusi ya Kiswahili Sanifu au njia nyingine tofauti, 
    toa maana ya msamiati ufuatao na kutungia sanifu sentensi sahihi.
    a. Kutibu
    b. Jukumu
    c. Mujibu
    d. Wahenga
    e. kuahidi
    Kazi ya 4:
    cc
    Kazi ya 5:

    Husisha wafanyakazi wafuatao na vifaa wanavyotumia

    vv

    12.3. Sarufi: Matumizi ya kauli za vitenzi
    Kazi ya 6:
    Soma sentensi zifuatazo na kutofautisha viambishi vilivyokolea
    Walipowasili hospitalini walikaribishwa na kupokelewa vizuri. Walielezewa
    mambo mengi sana na kuongezewa ujasiri wa kuchagua mchepuo wa 

    udaktari. Waliahidi kwamba kazi yao itafanywa kwa bidii.

    Maelezo muhimu
    Viambishi vilivyopigiwa mstari vinaonyesha kauli ya kutendwa ambayo 
    huathirika moja kwa moja na kitendo
    Kazi ya 7:
    Andika vitenzi vifuatavyo katika hali ya kutendewa kwa kuzingatia 
    mabadiliko ya kimaana.

    1. Wezi wameniiba pesa zangu.
    2. Tulimzaa mtoto wa kike miaka sita iliyopita.
    3. Dawa imewaua nzi wengi kutoka chooni.
    4. Kampuni ilimfikisha meneja wake mahakamani kwa sababu ya 
    uporaji mali.
    5. Tumekula chakula kitamu kwa wingi.
    6. Tulivua samaki wengi kutoka ziwa Kivu.
    7. Si vizuri kunywea pombe hospitalini.
    8. Wilaya itatengeneza barabara za lami nyingi.
    9. Dobi amefua nguo za aina mbalimbali.

    12.4. Matumizi ya lugha: Aina za kazi
    Kazi ya 8:
    Katika jozi, jadilini kuhusu kazi za watu mbalimbali mnazozijua.
    Maelezo muhimu
    Zipo kazi za aina nyingi duniani. Kazi hizi hutofautiana kulingana na ujuzi, 
    elimu na tajiriba ya kiwango cha juu. 
    Ifuatayo ni baadhi ya mifano mbalimbali ya kazi:
    Mhasibu: Mtaalamu wa kuweka hesabu ya fedha.
    Mhandisi/injinia: Mjuzi wa kutengeneza, kuhudumia na kuunda mitambo.
    Tarishi/Katikiro: Anayehudumu ofisini kwa kutumwa kupeleka habari au ujumbe.
    Bawabu: Alindaye mlangoni.
    Topasi/chura: Asafishaye choo.

    Tabibu/daktari/mganga: Mwenye ujuzi wa kutibu.
    Muuguzi/mualisaji: Ahudumiaye wagonjwa.
    Msarifu: Anayesimamia na kuidhinisha matumizi mazuri ya fedha katika 
    shirika.
    Dereva: Aendeshaye vyombo vya nchi kavu k.v. gari.
    Nahodha: Aendeshaye na kuongoza vyombo vya majini k.v. meli.
    Rubani/Mwanahewa: Aendeshaye na kuongoza vyombo vya angani 
    k.v.ndege.
    Utingo/taniboi: Mpakiaji na mpakuaji wa mizigo katika gari.
    Hamali/mpagazi/mchukuzi: Abebaye mizigo kwa malipo.
    Malenga: Mtunzi stadi wa mashairi na nyimbo.
    Manju: Stadi wa kutunga na kuimba nyimbo katika ngoma.
    Kuli: Apakiaye na kupakua shehena za forodhani.
    Dobi: Afuaye na kupiga nguo za watu pasi kwa malipo
    Sogora: Fundi wa kupiga ngoma
    Saisi: Atunzaye wanyama wanaopandwa k.v. punda na farasi.
    Msajili: Awekaye orodha ya kazi, vitu au viumbe.
    Mkalimani/mtarijumani: Afasiriaye lugha moja hadi nyingine.
    Sonara: Atengenezaye mapambo kwa kutumia madini.
    Kinyozi: Anyoaye nywele.
    Msusi/msosi: Asukaye watu nywele.
    Ngariba: Mtu anayefanya kazi ya kutahiri katika jando.
    Mkunga: Awasaidiaye wajawazito kujifungua.
    Kungwi: Afundishaye mwari wa kike au kiume.
    Mshenga: Atumwaye kupeleka habari za ndoa (posa).
    Refa: Mwamuzi katika mchezo k.v. soka
    Kasisi: Kiongozi wa kidini katika madhehebu fulani ya kikristo
    Imamu: Kiongozi wa kidini katika madhehebu fulani ya kiislamu.
    Hakimu: Aamuaye kesi katika mahakama.
    Kadhi: Hakimu wa kiislamu
    Mwekezaji: Anayeweka mali au pesa katika mradi au biashara.
    Meneja: Msimamizi au kiongozi katika kampuni au shirika.
    Karani: Afanyaye kazi ya kuandika k.m. barua na majarida.
    Kocha: Mwalimu wa mchezo k.v. soka, voliboli, n.k.
    Mkutubi: Ahifadhiye vitabu maktabani na kuviazima kwa wasomaji.
    Mnajimu: Mwenye elimu ya nyota. Hutabiri mambo.
    Mpigaramli: Abashiriaye kwa kupiga bao.
    Mwajiri: Aandikaye mtu kwa kazi ya malipo au mshahara.
    Mzegazega: Achotaye maji na kuyauza.
    Dalali: Auzaye bidhaa katika mnada (soko la kushindania bei)
    Manamba: Mfanyakazi wa muda katika shamba kubwa.
    Mnyapara: Msimamizi wa kazi.
    Mhazili: Sekretari - Atunzaye barua na majarida na kuandika kwa mashine ofisini.
    Mhadhiri: Mwalimu katika chuo kikuu.
    Mwashi: Fundi wa kujenga nyumba.
    Mhunzi: Afuaye vitu vya madini ya chuma au bati.
    Seremala : Atengenezaye samani za mbao au miti.
    Mfinyanzi: Atengenezaye vyombo vya udongo k.m. vyungu.
    Mvuvi: Afanyaye kazi ya kuvua samaki.
    Mwanaanga: Afanyaye utafiti wa hali ya anga.
    Mkabidhi: Mtu atunzaye mali kwa ajili ya mwingine
    Diwani: Anayewakilisha watu wake katika serikali za wilaya
    Mzoataka: Anayeokota takataka
    Kaimu: Anayeshikilia cheo au wadhifa fulani kwa muda.

    12.5. Kusikiliza na Kuzungumza
    Kazi ya 9:
    Kwa kushirikiana na wenzako,buni na uigize mazungumzo kuhusu 
    kazi za ufundi mbalimbali.
    Kazi ya 10:
    Itembelee zahanati au hospitali moja, kisha zungumzia wafanyakazi 
    uliowaona hapo.
    Kazi ya 11:
     “Daktari ni muhimu sana kuliko mwalimu”. Jadili na wenzako kauli hii.
    12.6. Kuandika
    Kazi ya 12:

    Kamilisha sentensi hizi kulingana na ujuzi wako
    a. Ili uwe na cheti cha udaktari, unapaswa kuwa na weledi katika 
    mchepuo wa...............................
    b. Baada ya kuhitimu masomo ya................................ mtu huweza 
    kupatiwa cheti cha urubani
    c. Hakimu ni mfanyakazi ambaye alihitimu masomo ya...................
    d. Kasisi huwa ameyazingatia masomo ya ........................
    e. Keshia huteuliwa baada ya masomo ya.....................................
    f. Katibu ni lazima awe na stadi katika elimu ya.........................
    cc
    Kazi ya 1:

    Tazama mchoro huu kwa makini na kuzungumzia unachoona.

    cc

    Daktari Mkuu pamoja na Muuguzi kutoka hospitali moja wilayani Gatsibo 
    wamepata fursa ya kuwatolea wagonjwa maonyo kuhusu umuhimu wa usafi 
    katika maeneo ya hospitali na mahali pengine.
    Daktari:                               Hamjambo wote!
    Wagonjwa:                         Hatujambo Daktari!
    Daktari:                              Haya! Kabla ya kuwatolea huduma mbalimbali, ningetaka tuongee 
    kidogo kuhusu usafi hapa hospitalini.
    Nani anayeweza kutuelezea kwa nini usafi hospitalini ni muhimu sana?
    Mgonjwa wa 1:          Usafi hospitalini ni lazima utiliwe maanani kwa sababu 
    pasipokuwa na usafi afya ya wagonjwa pamoja na 
    wafanyakazi wa hospitalini huwa katika hali mbaya sana.
    Daktari:                      Vizuri sana! Nani mwingine ambaye anaweza kutaja mahali ambapo 
    usafi unastahili kuliko pengine?
    Mgonjwa wa 2:            Mahali muhimu pakushughulikia mno ni kama vile vyooni, 
    vyumbani pamoja na nje ya hospitali.
    Muuguzi:                      Asante sana! Je, mnafikiri nini kwa mtu ambaye anakuja 
    hospitalini bila usafi wa mwili pamoja na mavazi yake?
    Mgonjwa wa 3:                           Kwa ukweli, watu kama hao wapo lakini tabia hiyo ni ya 
    kuepuka sana.
    Daktari:                  Ndiyo. Lakini ni lazima kujua kwamba usafi hospitalini 
    huchunguzwa kupitia vifaa vyote vinavyotumiwa, dawa 
    zinazotunzwa na kupewa wagonjwa, mahali pa kutolea 
    huduma tofauti bila kusahau usafi wa mwili na nguo kwa 
    wafanyakazi wa hospitalini.
    Muuguzi           :Sasa, nani ambaye anaweza kueleza hasara inayotokana 
    na ukosefu wa usafi kwa ujumla?
    Mgonjwa wa 4            : Si hospitalini tu, ukosefu wa usafi mahali popote huweza 
    kuambukiza magonjwa kadhaa kama vile ugonjwa wa 
    kipindupindu, kuhara, minyoo, n.k.
    Daktari                       : Asante sana! Basi, nani wa kueleza njia au jinsi magonjwa hayo yanavyosambazwa?
    Mgonjwa wa 5        :  Kwa mfano, kama vyoo havisafishwi vizuri, nzi huweza 
    kujitafutia makazi humo. Wadudu hawa wanapogusa
    kinyesi cha mgonjwa na kutua kwenye chakula cha watu 
    wazima vilelevile huwaambukiza ugonjwa wa kipindupindu 
    au kuhara. Lakini na matumizi ya maji machafu huweza 
    kuwa chanzo cha magonjwa haya.
    Muuguzi:                  Je, hakuna ugonjwa mwingine unaosababishwa na ukosefu 
    wa usafi kwenu nyumbani?
    Mgonjwa wa 6:                Taka zikitupwa mahali pasipofaa, madimbwi pamoja na 
    vichaka karibu na nyumba huwakaribisha mbu ambao 
    husababisha ugonjwa wa malaria.
    Daktari:                     Asante sana kwa mchango wenu. Kumbukeni kwamba 
    usafi ni ufunguo wa afya njema. Inatubidi kuushughulikia 
    mahali popote kwa ajili ya kuboresha maisha yetu mema.

    Kazi ya 2:

    Maswali ya Ufahamu
    Chagua jibu sahihi kuliko mengine 
    1. Tunatakiwa kuwa na usafi mahali popote kwa sababu
    a. usafi ni mzuri
    b. usafi wa mwili hulinda magonjwa
    c. penye ukosefu wa usafi maisha ya binadamu pamoja na ya 
    mazingira yake huathirika vibaya.
    d. Mbu huweza kujificha katika vichaka na kuambukiza ugonjwa wa 
    malaria. 
    2. Ugonjwa wa kipindupindu au kuhara husababishwa na 
    a. nzi
    b. uchafu kutoka kinyesi unaosambazwa na nzi pamoja na matumizi 
    ya maji machafu
    c. chakula kichafu na ambacho hakikuiva vizuri
    d. ukosefu wa vyoo safi na vya kutosha.

    3. Taka zote ni lazima

    a. zichomwe
    b. zitupwe shambani
    c. zitupwe jalalani baada ya kutofautisha zinazooza na zisizooza
    d. zihifadhiwe katika mashimo mbali na nyumba.
    4. Inastahili kuvaa glovu na bwelasuti wakati wa
    a. kula
    b. kupiga deki
    c. kuingia hospitalini
    d. kufanya usafi kwa ajili ya kujikinga na uchafu.
    5. Usafi hospitalini ni jukumu la 
    a. wagonjwa
    b. wagonjwa, wafanyakazi wa hospitali pamoja na yeyote anayekwenda hapo
    c. wafanyakazi wa hospitali

    d. hakuna jibu sahihi.

    13.2. Matumizi ya msamiati
    Kazi ya 3:

    Eleza maana ya maneno yafuatayo:
    1. Madimbwi 
    2. Kupiga deki 
    3. Huduma 
    4. Kuambukiza 
    5. Kipindupindu
    6. Kichaka
    7. Minyoo

    8. Bwelasuti

    Kazi ya 4:

    Kamilisha sentensi zifuatazo kwa kutumia choo, kuhara, deki, 
    kutiliwa maanani, taka.

    1. .....................ni kifaa chenye majimaji kinachotumiwa kuosha 
    sakafu ili kuondoa uchafu.
    2. Baada ya kujisaidia ni lazima umwage maji 
    katika........................................................................................
    3. Matumizi ya maji machafu yanaweza kuwa chanzo cha 
    kuambukizwa ugonjwa wa......................................
    4. Kila jamii inalazimishwa kuwa na jalala la 
    kutupia......................................................
    5. Usafi ni jambo la...........................mahali popote.
    13.3. Sarufi: Matumizi ya kauli ya kutendeshana
    Kazi ya 5:
    Soma sentensi zifuatazo na kueleza maana ya kitenzi baada ya 
    kuongezewa viambishi vilivyopigiwa mstari.

    1. Martha na Peter wanaelimishana mambo ya kujitegemea.
    2. Walikaribishana na kutoa hoja zao.

    3. Si vuzuri kugombanishana watu.

    Maelezo muhimu
    Kauli ya Kutendeshana - mtu anakufanya utende jambo fulani, nawe 
    unamfanya atende jambo hilo hilo.
    Kazi ya 6:
    Weka vitenzi vifuatavyo katika hali ya kutendeshana
    a. Wamepikiana chakula kitamu.
    b. Tumefanyana mambo mema ya kuieleza jamii yetu.
    c. Wamelimiana shamba la maharage.

    d. Mmechora michoro inayoeleza wazi usawa wa kijinsia

    13.4. Matumizi ya lugha: Msamiati kuhusu aina za magonjwa
    Kazi ya 7:
    Zungumzia aina mbalimbali za magonjwa yanayoweza kuhatarisha 
    maisha ya binadamu
    Maelezo ya kuzingatia
    a. Maana ya ugonjwa
    Ugonjwa ni hali au kitu kinachomfanya mtu, mnyama au mmea kuwa katika 
    afya duni. Pia ugunjwa huitwa maradhi, uele, ukongo. Kuna maradhi chungu 
    nzima yanayoweza kumwathiri mtu. Mengine yana tiba mengine hayana. 
    Mengine yanaambukizwa.
    Maradhi ya kuambukiza ni yale yanayoenea kutoka kwa mtu mmoja hadi 
    mwingine.
    b. Aina za maradhi
    Kuna aina mbalimbali za ugonjwa au maradhi. Ifuatayo ni miongoni mwa mifano.
    Saratani/kansa: ugonjwa usio na tiba kwa sasa. Ni ukuaji usio wa kawaida wa seli katika mwili.
    Malale: ugonjwa wa usingizi unaoambukizwa na mbung’o.
    Homa ya matumbo: taifodi
    Kwashakoo/ukosandisha: uele wa watoto unaosababishwa na uhaba wa chakula hususan protini.
    Surua/shurua/firangi/ukambi: ugonjwa wa watoto unaofanya ngozi kuwa na vipele. Hatua za kwanza huwa ni homa kali.
    Mafua/bombo: maradhi ya kuambukiza yanayosababisha mgonjwa kuumwa na koo na kichwa. Mgonjwa hutokwa na kamasi na kuwa na homa.
    Kaputula: uele wa kuhara. Tumbo la kuendesha.
    Baridi yabisi: maumivu ya mifupa au viungo yanayosababishwa na baridi 
    shadidi.
    Ukoma: uele wa kuambukiza wa mabatomabato ambao unaharibu mishipa 
    ya fahamu na kukata viungo vya mwili.
    Matumbwitumbwi / machibwichibwi: ugonjwa wa kuvimba mashavu hadi chini ya taya hususan kwa watoto
    Kisunzi/kizunguzungu / masua / gumbizi: uele wa kuhisi kichwa kikizunguka.
    Kipwepwe: ugonjwa wa ngozi unaosababisha madoa mekundu unaodaiwa kuletwa na chawa.
    Ndui: ugonjwa unaosababisha pele nyingi zenye majimaji na usaha.
    Kororo: uele wa kuvimba kooni.
    Ngiri: ugonjwa wa kukazana kwa mishipa iliyo sehemu za chini ya kitovu.
    Zongo: ugonjwa wa kuvimba tumbo kwa watoto wadogo.
    Vimbizi: hali ya kutoweza kupata pumzi kutokana na chakula kutosagika tumboni.
    Mbalanga / barasi: uele unaobadilisha rangi ya ngozi na kuwa na mabaka au matone.
    Rovu: ugonjwa wa kuvimba tezi kwenye shingo.
    Tetekuwanga / galagala / tetemaji: ugonjwa wa pele na homa kali wa kuambukizwa 

    13.5. Kusikiliza na kuzungumza

    Kazi ya 8:
    Igiza mazungumzo hapo juu kati ya Daktari na wagonjwa.
    Kazi ya 9:
    “Usafi ni ufunguo wa afya njema.” Jadili kauli hii.
    13.6. Kuandika
    Kazi ya 10:
    Tunga sentensi nne kwa kutumia vitenzi kama vile kuondoa, safisha, 
    kunawa, kuambukiza.

    SOMO LA 14: ADABU HOSPITALINI 
    Kazi ya 1:
    Eleza adabu inayotakiwa hospitalini na utoe sababu za adabu hiyo.
    14.1. Kusoma na ufahamu: Utaratibu hospitalini
    Yafuatayo ni mazungumzo mbele ya darasa ya wanafunzi walioitembelea 
    hospitali ya Girubuzima
    Mwalimu: Hamjambo vijana!
    Wanafunzi: Hatujambo mwalimu!
    Mwalimu: Kuna kundi la wanafunzi waliopewa kazi ya nyumbani kwenda 
    kuitembelea hospitali moja. 
    Nawaomba wafike mbele ya darasa na kutusimulia juu ya ziara 
    yao.
    Kiongozi wa kundi: Asante sana mwalimu kwa fursa hii. Kazi 
    tuliyoshughulikia ilikuwa inahusu mwenendo 
    hospitalini.
    Tuliitembelea hospitali moja inayoitwa Girubuzima. 
    Ningetaka niwashirikishe wenzangu katika 
    masimulizi haya.
    Mwanafunzi wa kwanza: Tulipoingia katika maeneo ya hospitali, tuliwakuta 
    watu wamekaa kimya mbele ya ofisi tofauti 
    kwa ajili ya kutaka kuhudumiwa.
    Mwanafunzi wa pili: Kwenye ukuta wa hospitali palikuwa pameandikwa 
    maonyo au maadili mbalimbali kuhusu utaratibu 
    unaofaa hospitalini kama ifuatavyo: 
    Mwanafunzi wa tatu: Hapa ni eneo la Hospitali. Inakatazwa kutenda 
    yafuatayo:Kuvuta sigara.
    Mwanafunzi wa nne: Kuchafua majengo ya hospitali na mazingira yake.
    Mwanafunzi wa tano: Kujisaidia pasipofaa.
    Mwanafunzi wa sita: Kutema mate hadharani.
    Mwanafunzi wa saba: Kupiga kelele.
    Mwanafunzi wa nane: Kuharibu vifaa vya hospitalini kama vile kuvunja vioo, viti, mlango, n.k.
    Mwanafunzi wa tisa: Kutumia pombe pamoja na dawa za kulevya.
    Mwanafunzi wa kumi: Kuonyesha tabia ya ukatili, ugomvi, chuki pamoja 
    na ubaguzi.
    Kiongozi wa kundi: Hii ndiyo miiko ya kupiga marufuku ndani ya hospitali tuliyoorodheshewa.
    Mwalimu: Asante sana kwa kazi hii! Darasa, pigieni makofi kundi hili.Maswali ya Ufahamu
    Kazi ya 2:
    Jibu maswali yafuatayo
    1. Habari hii imetokea wapi?
    2. Ni mbinu gani ya ufundishaji na ujifunzaji inayozungumziwa?
    3. Kwa nini maonyo yale yalitolewa hospitalini?
    4. Ni wahusika wangapi wanaojitokeza?

    5. Unadhani maonyo yale yalitolewa na nani?

    14.2. Matumizi ya msamiati
    Kazi ya 3:

    Oanisha msamiati kutoka sehemu A na maana yake katika sehemu B

    dd

    cc

    14.3. Sarufi: Matumizi ya kauli za vitenzi
    Kazi ya 4:
    Soma sentensi zifuatazo na kueleza maana ya kitenzi baada ya 
    kuongezewa viambishi

    1. Mama na shangazi wamepikiana chakula kitamu sana.
    2. Kagina na Amina waliimbiana nyimbo za kuvutia.
    3. Mimi na binamu yangu tulitembeleana mwishoni mwa mwaka uliopita.
    Maelezo muhimu
    Viambishi vilivyopigiwa mstari vinaonyesha kauli ya kutendeana yaani 
    unafanya kitendo kwa niaba ya mtu, naye anafanya kitendo hicho kwa niaba yako.
    14.4. Matumizi ya lugha: Muhtasari kuhusu kauli za vitenzi
    Kazi ya 5:
    Unganisha kauli za vitenzi vifuatavyo: fanya, lima, piga, cheza, lipa, 
    penda, omba, dunga katika jedwali moja na kutoa mifano husika kwa 
    kila kauli.

    1. Kauli ya Kutenda: Kitendo katika hali yake ya kawaida (bila 
    kunyambuliwa)
    2. Kauli ya Kutendea: Kufanya kitendo kwa niaba(au kwa ajili) ya 
    mtu mwingine
    3. Kauli ya Kutendana: Unamfanya mtu kitendo, naye anakufanya 
    vivyo hivyo
    4. Kauli ya Kutendeana: Unafanya kitendo kwa niaba ya mtu, naye 
    anafanya kitendo hicho kwa niaba yako.
    5. Kauli ya Kutendwa: Kuathirika moja kwa moja na kitendo
    6. Kauli ya Kutendewa : Kitendo kufanywa kwa niaba yako au kwa 
    ajili yako.
    7. Kauli ya Kutendeka: Kitendo kukamilika au kuwa katika hali timilifu
    8. Kauli ya Kutendesha : Kumfanya mtu atende jambo fulani
    9. Kauli ya Kutendeshana: Mtu anakufanya utende jambo fulani, 
    nawe unamfanya atende jambo lilo hilo

                  vv
    f

    14.5. Kusikiliza na kuzungumza
    Kazi ya 6:
    Simulia mbele ya darasa muhtasari wa mazungumzo hapo juu baina 
    ya mwalimu na wanafunzi
    Kazi ya 7:
    Kwa ushirikiano na wenzako, igiza mazungumzo hayo.
    14.6. Kuandika
    Kazi ya 8:

    Buni mazungumzo mafupimafupi baina ya mwanafunzi na mzazi wake 
    kuhusu umuhimu wa usafi na uandike maneno yasiyopungua 100.Tathmini ya mada
    1. Taja vifaa angalau vinne vya hospitalini na kueleza umuhimu wake
    2. Baadhi ya sehemu muhimu za hospitali, chagua tatu na kueleza umuhimu wake.
    3. Kamilisha sentensi zifuatazo:
    i. Kazi ya muuguzi ni..................................................................
    ii. Karani hospitalini hushughulikia...............................................
    iii. Tabibu ni mfanyakazi wa hospitalini anaye..................................
    iv. Mfanyakazi wa hospitalini anayeshughulikia waliovunjika viungo vya mwili huitwa................ 
    v. Anayetoa huduma kwa wajawazito wakati wa kujifungua huitwa..............................................
    4. Jadili hasara zinazoweza kujitokeza kwa sababu ya ukosefu wa usafi.
    5. Zungumzia kasoro angalau tano ambazo zinachukuliwa kama mwiko hospitalini.
    6. Weka vitenzi vinavyopatikana katika sentensi zifuatazo katika hali ya kutendwa.
    a. Tumesafisha vyumba, vyoo pamoja na jikoni kwa ajili ya kujilinda uchafu.
    b. Jana wageni walikula chakula kwa wingi.
    c. Si vizuri kupiga kelele hospitalini.
    d. Tunakunywa maji baada ya kuchemka.
    e. Sisi huvaa tai shingoni.



  • MADA YA 4 MSAMIATI KUHUSU MAENEO YA UTAWALA

    Uwezo mahususi : Kuzungumza na kuandika kwa ufasaha matini fupifupi 
    kwa kutumia msamiati unaofaa katika maeneo ya utawala.Malengo ya ujifunzaji:
    • Kutoa msamiati utumiwao katika maeneo ya utawala, ngazi za utawala na viongozi wakuu wa kiserikali,
    • kutaja aina za vitambulisho vinavvotumiwa na sikukuu za kitaifa,
    • Kuainisha makazi ya watu mbalimbali, 
    • Kutumia kwa usahihi vivumishi vya majina ya ngeli ya U-ZI,
    • Kuzungumza na kuandika kwa ufasaha Kiswahili kwa kutumia msamiati kuhusu utawala.Kidokezo
    • Katika mazingira unamoishi kuna viongozi wa aina gani?
    • Je, tarehe ya 1 Februari inakukumbusha nini kila mwaka? 

    • Taja aina tatu za vitambulisho unavyovijua.

    tt

    Kazi ya 1:
    Jengo hili linakuonyesha nini?
    15.1. Kusoma na ufahamu: Ofisi za kiutawala
    Soma mazungumzo yaliyo hapa chini baina ya Abayo, Baba, Gloriose 
    na Anezerwe.

    (Abayo alikubaliana na babake kwenda kuwashawishi rafiki zake ili 
    waambatane kumpokea rais wa jamhuri katika ziara yake wilayani kwao) 
    Abayo: Shikamoo baba!
    Baba: Marahaba mwanangu. U safi leo kabisa!
    Abayo: Ndiyo, leo tutampokea rais wetu wa jamhuri hapa kwetu.
    Baba: Hilo ni jambo muhimu sana. Kila mtu ataenda kumpokea.
    Abayo: Unajua atazuru miundombinu kadhaa wilayani humu kama vile: 
    kuanzisha mradi wa umwagiliaji, kuzindua mradi wa ukarabati wa 
    nyumba kwa familia zilizokumbwa na mvua kali na ukarabati wa 
    barabara ya lami.
    Baba: Nenda uwajulishe rafiki zako Gloriose na Anezerwe ili wasikose kuhudhuria. 
    Abayo: Kweli kabisa! Ebu niende. 
    Baba: Haya, safari njema.
    Abayo: Hamjambo rafiki zangu.
    Gloriose: Hatujambo sana! Karibu kwetu.
    Abayo: Ningetaka kuwakumbusha ziara ya rais wa jamhuri katika wilaya 
    yetu. Sherehe za kumpokea zinatarajiwa kufanyika kwenye uwanja 
    wa michezo Ituze.
    Gloriose: Uwanja huo unapatikana wapi?
    Abayo: Unapatikana katika kijiji cha Kinini, kata ya Gitabi, tarafa ya Bwiza, 
    wilaya Bikombe, mkoa wa Mashariki.
    Anezerwe: Haaa! Nyinyi mmeisha kuwa wanasiasa! Hayo yote mimi siyajui.
    Abayo: Ni kusema kwamba hujui hata wilaya yetu pamoja na mkoa?
    Gloriose: Tafadhali, acha Abayo aendelee na habari yake ya ziara ya rais.
    Abayo: Nimekuja kuwaalika ili msije mkakosa bahati ya kuwaangalia viongozi mbalimbali.
    Anezerwe: Kweli? Viongozi wepi? Jamaa, tupatie mfano.
    Abayo: Mawaziri mbalimbali akiwemo wa elimu, wabunge na maseneta, 
    gavana wa mkoa wetu, wakuu wa wilaya mbalimbali, viongozi wa tarafa, wakuu wa jeshi na polisi kwenye ngazi mbalimbali, n.k.
    Gloriose: Ehee! Viongozi wanapaswa kuweko ili wananchi wakiuliza swali lo lote watoe mchango wao katika kujibu au kumfafanulia rais.
    Anezerwe: Hii ndiyo fursa yangu kuuliza swali kiongozi wa tarafa 
    aliyetunyang’anya mabati yetu ya kutujengea nyumba baada ya dhoruba kali kuiangusha nyumba yetu.
    Gloriose: Rais wetu ni mzuri atawauliza viongozi walichokifanya ili tusiteswe namna hii.
    Abayo: Jamani! Naona saa za kuenda zimefika. Twende tufike mapema ili umati wa watu usitukataze kumwona rais.
    Anezerwe: Eeeh!Twende. Asante sana Abayo kutujulisha.
    Gloriose: Mienendo bora ya wananchi ni kujiendeleza, uzalendo na ushikamano, n.k.

    Abayo: vizuri, twende.

    Kazi ya 2:
    Maswali ya ufahamu
    A. Baada ya kusoma mazungumzo hapo juu, jibu maswali yafuatayo:
    1. Ni wahusika gani wanaozungumza?
    2. Kwa sababu gani Abayo aliamua kwenda nyumbani kwao Gloriose 
    na Anezerwe?
    3. Sherehe zinatarajiwa kufanyika wapi?
    4. Raia wamealikwa kuwapokea viongozi gani?
    5. Eleza miundombinu zilizotajwa katika kifungu cha habari.
    6. Andika baadhi ya mienendo bora uliyoisoma katika mazungumzo.
    B. Jaza sentensi zifuatazo kwa kutegemea mazungumzo hapo juu
    i. ……….. ndiye alikwenda kuwaarifu………………ziara 
    ya……………………..
    ii. Ziara hii inatarajiwa kuhudhuriwa na viongozi kadhaa kama 
    vile………………..
    iii. Lengo kuu la ziara hii ni kuanzisha miradi ya kimaendeleo kama 
    vile……………..
    15.2. Matumizi ya msamiati 
    Kazi ya 3:
    Fafanua msamiati ufuatao:
    Rais 
    Mbunge
    Waziri 
    Umwagiliaji 
    Dhoruba 

    Miundombinu 

    Kazi ya 4:

    Oanisha msamiati wa sehemu A na viongozi katika sehemu B

    rr

    rr

    Kazi ya 6:
    Tazama sentensi zifuatazo zilizo katika sehemu A na sehemu B na 

    kueleza mabadiliko ya kisarufi yanayojitokeza.

    cc

    Maelezo ya kuzingatia
    Ngeli hii inajumuisha nomino za vitu visivyo na uhai ambazo zinajigawa 
    katika makundi matano yafuatayo:
    1. Nomino ambazo umoja huanza kwa u- na wingi Ø-.
    Kwa mfano: unywele, ukuta, ufagio, ufunguo, unyasi, utepe, utosi, ukoo, 
    upote, upenu, upondo, upongoo, upanga, upepeo, n.k.
    2. Nomino ambazo umoja huanza kwa u- na wingi wake huanza kwa ny-
     Kwa mfano: uta, ufa, uwanja, uso, uwayo, uzi, uwalio, ugwe.
    3. Nomino ambazo umoja huanza kwa w- na wingi huanza kwa ny-
    Kwa mfano
    : waraka, wakati, wembe, wimbo, wayo, waya, wavu, wanja, 
    wanda, wadhifa, waadhi.
    4. Nomino ambazo umoja huanza kwa u- na wingi huanza kwa nd-
    Kwa mfano: ulimi, uele.
    5. Nomino ambazo umoja huanza kwa u- na wingi huanza kwa mb-
    : ubao, ubavu, ubati, ubale.
    Mifano zaidi katika sentensi:
    Umoja: 

    1. Ukuta huu umebomolewa na Umutoni.
    2. Ufunguo wake utafungua vizuri.
    3. Ukurasa wenyewe si mrefu.
    4. Ukucha ule umechorwa na Nikuze.
    5. Uso wa Solange ni mzuri 
     Wingi:
    1. Kuta hizi zimebomolewa na Umutoni
    2. Funguo zao zitafungua vizuri
    3. Kurasa zenyewe si ndefu
    4. Kucha zile zimechorwa na Nikuze
    5. Nyuso za solange ni nzuri
    ff

    Vivumishi katika ngeli ya U-ZI
    1. Vivumishi vya kuonyesha
    Mfano:
     Umoja                                                     Wingi
    Wimbo huu unapendeza.                      Nyimbo hizi zinapendeza.
    Uzi huu umetoka wapi?                          Nyuzi hizi zimetoka wapi?
    Ukurasa huo umeandikwa vizuri.      Kurasa hizo zimeandikwa vizuri.
    Utepe ule umenunuliwa leo.                Tepe zile zimenunuliwa leo.
    Maelezo:
    Maneno ule,zile,hizo na huo ni vivumishi vya kuonyesha katika ngeli ya U-ZI, 
    kwa sababu vinaonyesha jina au nomino fulani. Katika umoja: huu,huo na

    ule hutumiwa na hizi,hizo,zile hutumiwa katika wingi.

    Kazi ya 8:
    Jaza sentensi hizi kwa kutumia jibu sahihi kutoka mabanoni.

    1. Ufito ……………utakatwa upya.(huyu,huu,hii).
    2. Fizi ……….zilijeruhiwa kutokana na ajali ya baiskeli (hio,huo,hizo).
    3. Ufunguo…………unaweza kufungua nyumba yangu (ule,ile,zile).
    4. Mwanafunzi ataandika ukurasa…………. vizuri(hio,huo,hizo).
    5. Nyufa ……………. zitazibwa na mwashi hodari (huu,hizi,hii).

    2. vivumishi vya pekee

    Kazi ya 9:
    Soma kifungu cha habari kifuatacho na kueleza matumizi ya maneno 
    yaliyopigiwa mstari 

    Bwana Kamali ni Mwalimu kwenye shule ya Mahoro. Siku moja akiwa 
    njiani kuelekea shuleni alipoteza funguo zake pamoja na ufunguo 
    wenyewe wa gari lake. 

    Kwa bahati nzuri funguo zile zote zilipatikana na kumwezesha kufika 
    shuleni. Alipofikapo aliwapa wanafunzi wake kazi ya kuandika kurasa 
    kumi za insha. Binti mmoja aitwaye Tamari aliandika ukurasa mmoja tu. 
    Kwenye ukurasa wenyewe alichora picha za wanyama wenye kucha 
    ndefu. Kucha zenyewe zilikuwa chafu mno. Mwalimu alimwonyesha 
    mfano mzuri wa kufuata. Kwa hiyo, binti alikubali mfano wa mwalimu.
    Uso wa mwalimu ulionekana kuwa na furaha vilevile na uso huo wa binti 
    Tamari ukaonyesha furaha tele.
    Maelezo
    Maneno wenyewe na zenyewe ni vivumishi vya pekee vyenye dhana 
    kurejesha katika ngeli ya U-ZI, kwa sababu vina uaminifu wa kulirejea lile jina 
    linalowakilishwa.Katika umoja wenyewe hutumiwa na zenyewe ikatumiwa katika  wingi.
    Mfano:                 Umoja                                               Wingi
                    Uzi wenyewe                                    Nyuzi zenyewe
                    Ukurasa wenyewe                           Kurasa zenyewe
                    Mifano katika sentensi
    Umoja                                                               Wingi
    Uso wenyewe umeharibika.              Nyuso zenyewe zimeharibika
    Ufagio wenyewe umepotea.              Fagio zenyewe zimepotea.

    15.4. Matumizi ya lugha: Ngazi za utawala
    Kazi ya 10:
     Jadili maswali yafuatayo:
    a. Maeneo ya utawala nchini Rwanda yanaonekana katika muundo gani?
    b. Panga viongozi wa utawala nchini Rwanda kulingana na ngazi zao
    Maelezo muhimu
    1. Muundo wa ngazi za utawala nchini Rwanda
    Kijiji
    kata 
    Tarafa
    Wilaya
    Mkoa
    Taifa/nchi
    2. Ngazi za viongozi
    Mkuu wa kijiji
    Katibu mtendaji wa kata
    Katibu mtendaji wa tarafa
    Meya/mkuu wa wilaya
    Gavana
    Viongozi wakuu wa taifa (Rais, waziri mkuu, mawaziri,wabunge, maseneta)
    Nchi ya Rwanda ina jumla ya Mikoa 5, Wilaya 30, Tarafa 416 na Kata 2 148 
    na Vijiji 14 837.

    Mji wa Kigali huongozwa na Meya wa mji. Viongozi wengine wanaopatikana 
    katika ngazi za utawala ni wale wanaosimamia ngazi za usalama kama 
    vile jeshi na polisi pamoja na viongozi wa vyeo mbalimbali vya kiserikali. 
    Maseneta, Wabunge, Makatibu katika wizara tofauti, wakuu wa jeshi, wakuu 
    wa polisi,…….Wote hushirikiana ili kuliendeleza taifa na kumsaidia rais wa 
    jamhuri kuyafikia majukumu yake.Hii inamaanisha kwamba viongozi wote 
    wakitimiza majukumu yao, nchi itaweza kuendelea haraka na kuukuza 
    uchumi wake.
    Kazi ya 11:
    Oanisha sehemu A na sehemu B
    cc

    Kazi ya 12:
    Kamilisha sentensi zifuatazo:
    1. Karongi ni mojawapo ya …………………...zinazounda …………….
    wa Magharibi.
    2. ………………………wa jamhuri ya Rwanda alihutubia raia wote.
    3. Nishati, umeme, ukarabati wa barabara ni baadhi ya …………………
    4. Gavana ni kiongozi mkuu wa ………………………………………….
    5. a.Idadi fulani ya kata inaunda …………………………………………
    b. Jamhuri ya Rwanda inaongozwa na ……………………………
    c. Rwanda imegawanyika katika mikoa ifuatayo:…………………
    15.5. Kusikiliza na Kuzungumza
    Kazi ya 13:
    Igiza na wenzako mazungumzo kuhusu kifungu cha habari 
    kilichosomwa awali “Ofisi za kiutawala.”
    Kazi ya 14:
    Iandae ziara kwenye kituo cha utawala kilichoko karibu yako na 

    kusimulia mbele ya darasa kuhusu ziara yako.

    Kazi ya 15:
    Jitambulishe kwa mwenzako kwa kuzingatia maeneo ya utawala 
    unamoishi pamoja na viongozi wake.
    15.6. Kuandika 
    Kazi ya 16:
    Tunga mazungumzo kati ya raia mmoja na kiongozi wilayani juu ya 
    huduma ya kuomba kitambulisho fulani. 
    Kazi ya 17:
    Tunga kifungu cha habari kifupi kwa kutumia msamiati ufuatao:
    a. Mkoa
    b. Jamhuri
    c. Kata

    d. Wilaya

    SOMO LA 16: MAKAZI YA WATU

    ccc

    Chunguza mchoro huu, kisha ueleze ikiwa unayoyaona yanahusiana 

    na makazi ya watu

    16.1. Kusoma na ufahamu: Makazi ya watu

    Makazi ni eneo au  mazingira ambayo ni makao ya mnyama au mmea fulani 
    au aina nyingine ya  viumbe hai. Ni mazingira ya asili ambapo kiumbe 
    huishi, au mazingira ambayo yanazunguka idadi ya jamii. Kuhusu makazi 
    ya bianadamu, haya ni mazingira ambayo binadamu huishi na kuingiliana. 
    Kwa mfano, nyumba ni makazi ya binadamu, ambapo binadamu hulala na 
    kula. Haya yanaweza kuwa mjini au vijijini. Makazi ya mjini ni aina ya makazi 
    ambayo watu wanajenga nyumba zao mijini, karibu na wenzao wengi. Mji 
    wenye wakaaji wengi ni mji mkuu wa Kigali na miji kama Musanze, Huye, 
    Rubavu, Rusizi, Muhanga na Nyagatare inayosaidia jiji la Kigali. Miji hii yote 
    ina miundombinu mbalimbali kama vile umeme, maji safi, viwanda kadhaa, 
    hospitali, barabara za lami, n.k.

    Makazi ya vijijini ni aina ya makazi ambayo watu hujenga nyumba zao 
    sehemu za vijijini. Asilimia kubwa ya Wanyarwanda huishi sehemu hii lakini 
    serikali inaendelea kuwapa miundombinu tofauti kama inavyofanyia miji. 

    Nchini kwetu, serikali imewakataza raia kujenga na kuishi katika maeneo 
    hatari kama vile vinamasini, mabondeni, milimani na sehemu nyingine zote 
    zinazoweza kuhatarisha maisha yao. Serikali imetoa mchango mkubwa 
    kulitatua tatizo hili kwa kuhamisha raia wote waliokuwa katika maeneo haya 
    ya hatari ikiwapatia maeneo mazuri pia salama na kuwajengea nyumba bora 
    vilevile. Hii inalenga wale wanaoishi katika mabonde chini ya milima mirefu 
    kuepuka mmomonyoko wa ardhi na watu waliokuwa wamejenga kando ya 

    mito na maziwa. 

    Kazi ya 2:
    Maswali ya ufahamu
    1. Taja aina za makazi bora kwa binadamu? 
    2. Eleza maeneo yasiyokubaliwa kuishi nchini Rwanda.
    3. Serikali ya Rwanda ilifanya nini kuwaokoa waliokuwa wanaishi katika maeneo ya hatari?
    4. Taja miundombinu ambayo serikali ilifikisha vijijini ili kusaidia raia kuishi vema.
    5. Je, mmomonyoko wa ardhi husababishwa na nini?

    6. Je, ungependa kuishi wapi kati ya mjini na kijijini? Kwa nini?

    7. Jibu “NDIYO au HAPANA” kwa sentensi zifuatazo:
    a. Binadamu hukaa katika nyumba.
    b. Mji wa Kigali ni mji wenye wakaaji wengi duniani.
    c. Sehemu za vijijini nchini Rwanda zina miundombinu mbalimbali.
    d. Nchini Rwanda raia wanaweza kujenga nyumba zao sehemu 
    yoyote.
    16.2. Msamiati kuhusu makazi
    Kazi ya 3:
    Fafanua maneno yafuatayo:
    a. Nyumba 
    b. Bondeni 
    c. Mmomonyoko wa ardhi: 
    d. Kinamasi 

    e. Mjini 

    Kazi ya 4:

    Oanisha maneno katika kundi A na maana yake katika kundi B

    bb

    16.3. Sarufi: Matumizi ya ngeli ya U-ZI
    Vivumishi vya idadi 
    Kazi ya 5:
    Tazama sentensi hizi na kujadili mabadiliko ya kisarufi yaliyojitokeza:
    Ufagio mmoja umetumiwa kwetu.
    Ukurasa mmoja umeandikwa vizuri.
    Kuta mbili zitajengwa lini?
    Fagio tatu zimeletwa na wavulana.
    Nyufa chache zimezibwa na Ishimwe.
    Maelezo 
    Maneno mmoja, mbili, tatu, nne, chache,…. ni vivumishi vya idadi katika 
    ngeli ya U-ZI, kwa sababu vinaonyesha idadi au hesabu ya vitu. Aina hii ya 
    vivumishi tunaweza kuigawa katika makundi mawili:
    • Vivumishi vya idadi vinavyoonyesha idadi kwa jumla.
    • Vivumishi vya idadi vinavyoonyesha idadi kwa hesabu.
    Vivumishi vya idadi vinavyoonyesha idadi kwa jumla. Mifano ya vivumishi 
    vya idadi vya kundi la kwanza ni kama:
    i. chache
    ii. ingi
    iii. maridhawa
    iv. pungufu
    v. haba
    vi. kidogo, n.k.
    • Vivumishi vya idadi vinavyoonyesha idadi dhahiri: ni vya idadi isiyo kikomo 
    kwani vinahusu hesabu ya nambari kuanzia moja na kuendelea.
    Mfano:
    i. moja
    ii. mbili 
    iii. tatu 
    iv. nne
    v. kumi
    vi. miavii. 
    vi.elfu

    viii. milioni, n.k.

    Kazi ya 6:

    Weka sentensi hizi katika umoja au wingi:

    cc

    Kazi ya 7:
    Jaza nafasi zilizoachwa wazi kwa kutumia kivumishi kinachofaa mabanoni.
    a. Upondo ……………….. umewekwa ndani ya mtumbwi (moja, mmoja, mbili).
    b. Petero aliandika kurasa…………………..(zitano,tano,moja).
    c. Umutoni na Abayo walipokea fagio………………. Siku ile (nyingi, moja, wengi).
    d. Mtoto aliwaandikia wazazi wake nyaraka……………katika muhula wa tatu. (nyingi, zingi, lingi).
    e. Wembe ……………ulimkata kidole (moja, mmoja, wumoja).
    16.4. Matumizi ya lugha: Makazi ya watu
    Kazi ya 8:
    Jadili maswali yafuatayo:
    a. Makazi ni muhimu sana kwa binadamu.
    b. Serikali ya Rwanda iliwakataza raia kujenga na kuishi katika maeneo hatarishi.

    Maelezo muhimu

    Kama ilivyoandikwa katika kifungu cha habari, makazi  ni eneo 
    au mazingira ambayo ni makao ya mnyama au mmea fulani au aina nyingine 
    ya viumbe hai. Ni mazingira ya asili ambapo kiumbe huishi, au mazingira 
    ambayo yanazunguka idadi ya  jamii. Binadamu anaweza kuishi katika 
    nyumba kubwa au ndogo kulingana na uwezo wake. Nyumba hizi lazima 
    ziwe safi ili kujiepusha na magonjwa yatokanayo na uchafu. Ghorofa ni aina 
    ya nyumba pia ambayo familia moja au nyingi huweza kuishi.
    16.5. Kusikiliza na kuzungumza: Majadiliano kuhusu makazi
    Kazi ya 9:
    Zungumzia wenzako umuhimu wa kuishi katika maeneo yasiyo hatari.
    Kazi ya 10:
    Simulia wenzako kuhusu picha au video ulizoziona zinazohusu 
    makazi nchini Rwanda hasa hasa mji wa Kigali. 
    16.6. Kuandika: Utungaji wa insha kuhusu makazi
    Kazi ya 11:
    Tunga insha yenye aya 3 (Maneno yasiyopungua mia moja) ukielezea 
    umuhimu wa kuishi katika maeneo yasiyo hatari.

    SOMO LA 17: SIKUKUU ZA KITAIFA
    ccc

    17.1. Kusoma na ufahamu: Sikukuu za kitaifa

    Mwaka jana Yusufu alikuja kututembelea kwenye sikukuu ya Krismasi. 
    Alipofika nyumbani kwetu tulimpokea vizuri kwa chakula pamoja na vinywaji 
    mbalimbali. Tulipomaliza sherehe zetu, mwalimu wetu aliingia ndani na 
    kutuuliza sababu tulikuwa tunafurahi sana. Bila kukawia nilimwambia kuwa 
    nchini Rwanda kuna sikukuu za kitaifa nyingi zinazosherehekewa na kwamba 
    siku hiyo tulikuwa tukisherehekea Krismasi. Mwalimu alituomba kumfafanulia 
    sikukuu nyingine za kitaifa zinazosherehekewa nchini Rwanda. Tulianza 
    kukodoleana macho tukingoja mmoja kati yetu ajibu swali hilo. Mwalimu 
    alipoona kuwa kimya kimetutawala alianza kutufafanulia sikukuu hizo ili mara 
    nyingine tusije tukatatizika. Yusufu alimwambia kwamba hakukumbuka na 
    habari. Mwalimu alianza kumfafanulia sikukuu hizo ili mara nyingine asije 
    akaziuliza tena. “Tarehe ya 1 Januari kila mwaka ni sikukuu ya mwaka 
    mpya, tarehe 1 Februari sikukuuu ya mashujaa, tarehe 7 Aprili kila mwaka ni 
    kumbukumbu ya mauaji ya kimbari dhidi ya watutsi, siku ya kuwakumbuka 
    jamii ya Wanyarwanda iliyoangamia mwaka 1994,” alisema mwalimu. Nami 
    niliongeza kuwa tarehe 1 Mei ni sikukuu ya kazi ulimwenguni, sikukuuu ya 
    uhuru wa Rwanda ikasherehekewa kwenye tarehe 1 Julai na tarehe 4 Julai 
    kila mwaka ikawa sikukuuu ya ukombozi wa Rwanda. 

    Yusufu alituomba kutosahau sikukuu za kidini kama vile Idi kwa waumini wa 
    kiislamu, sikukuu ya Bikira Maria kwa wakatoliki, sikukuu ya pasaka katika 
    mwezi Machi au Aprili, n.k. 

    Kitu kingine alichotuambia mwalimu ni kwamba sikukuu hizi huwapa viongozi 
    fursa ya kukutana na wananchi, kuwajulisha mipango ya serikali, pia hupata 
    fursa ya kupumzika na kuwatembelea jamii na marafiki.

    Kazi ya 1:

    Maswali ya ufahamu
    1. Yusufu alikuja kututembelea kwenye sikukuu ipi?
    2. Nani aliingia baada ya chakula na kinywaji? Alisema nini?
    3. Ni kwenye tarehe gani ulimwengu mzima husherehekea sikukuu ya kazi?
    4. Andika majina matatu ya sikukuu za kidini zinazosherehekewa 
    nchini Rwanda.

    5. Ni kitu gani kinachowanufaisha viongozi kwenye sikukuu hizi?
    17.2. Msamiati kuhusu sikukuu za kitaifa
    Kazi ya 2:
    Eleza maneno yafuatayo ukiyahusisha na kifungu hicho.Tumia 
    kamusi ya Kiswahili Sanifu pale panapohitajika.

    1. Krismasi
    2. Mashujaa 
    3. Kukomboa
    4.Kimbari
    5. Fursa 
    Kazi ya 3:
    Jaza sentensi kwa kutumia msamiati huu: Uhuru, mashujaa, kimbari, 
    makazi, kuikomboa, Krismasi, Idi.

    1. Katika mwezi wa Februari sisi husherehekea sikukuu ya ……………
    lakini ile ya ………….. wa taifa ni mwezi wa Julai.
    2. Mauaji ya …………nchini Rwanda yaliacha watu wengi 
    bila………………
    3. Majeshi ya RPF Inkotanyi yaliwahi…………………..nchi ya 
    Rwanda.
    4. …………………….huanza kulingana na kalenda ya waislamu.
    5. Kwenye sikukuu ya ………..wao walikula chakula kizuri sana.

    17.3. Sarufi: Matumizi ya ngeli ya U-ZI na vivumishi vya sifa

    Kazi ya 4:
    Tazama sentensi hizi na kueleza maneno yaliyopigiwa kistari:
    • Ufunguo mpya unafungua mlango vizuri.
    • Funguo nzuri zinafungua milango vizuri.
    • Ukurasa mbaya umeandikwa na Irakiza. 
    • Kurasa nyekundu zimeandikwa na Irakiza 
    • Mugabekazi ametuagizia ufagio mzito.
    • Mugabekazi ametuagizia fagio nzito.
    Maelezo muhimu
    Vivumishi vya sifa ni vivumishi vinavyotaja tabia au namna vitu vilivyo au 
    vinavyoonekana. Vivumishi vinavyoonyesha tabia hii ni kama hivi vifuatavyo:
    i. -ema                        v. -nyenyekevu
    ii. -pevu                      vi. -danganyifu
    iii. -nyamavu            vii. -changamfu   
    iv. -pumbavu            viii. -ovu, n.k
    Katika mfano hapo juu tunaona kuwa kuna vivumishi vya sifa vinavyoonyesha 
    tabia hasa ya viumbe hai. Ifuatayo ni mifano ya vivumishi vya sifa 
    vinavyoonyesha jinsi vitu vilivyo hai au vinavyoonekana:
    i. -zuri                       v. -nene      
    ii. -baya                    vi. -eusi
    iii. -gumu                 vii. -pya 
    iv. -zito                     viii. -kongwe, n.k

    Kazi ya 5:

    Jaza nafasi zilizoachwa wazi kwa kutumia kivumishi kinachofaa kutoka mabanoni.
    a. Ukucha wake ……………….. umekatwa na Ahirwe (mbaya, baya, mabaya).
    b. Mbwa huyu ana nyayo……………… (msafi, safi, usafi).
    c. Kalisa aliandika kurasa…………………..(refu, ndefu, urefu).
    d. Ufunguo ………………. umepotea njiani (ndogo, mdogo, wadogo).
    Kazi ya 6:
    Andika sentensi mbili zenye vivumishi vya sifa vinavyoonyesha 
    tabia na nyingine mbili za vivumishi vya sifa vinavyoonyesha jinsi 

    vitu vilivyo au vinavyoonekana katika jedwali hili:

    vv

    17.4. Matumizi ya lugha: Sikukuu za kitaifa
    Kazi ya 7:
    Chagua maneno haya na kuyapanga katika kundi A au B
    Pasaka
    Sikukuu ya mashujaa 
    Sikukuu ya ukombozi
    Sikukuu ya kazi ulimwenguni
    Krismasi
    Sikukuu ya uhuru wa taifa
    Sikukuu ya watakatifu wote

    Idi

    Maelezo muhimu
    Sikukuu ni siku yenye shamrashamra ya kuadhimisha tukio fulani. Hii ni siku 
    maalumu ya kukumbuka, kusheherekea au kufurahia jambo fulani. Kati ya 

    sikukuu za umma kuna sikukuu za kidini na sikukuu za kiserikali.

    dd

    17.5. Kusikiliza na kuzungumza: Sikukuu za kitaifa
    Kazi ya 8:
    Jadili kuhusu sikukuu za kitaifa na kutoa matokeo yako hadharani.
    Kazi ya 9:
    Ukitumia sikukuu uliyoisherehekea siku moja au zaidi, zungumzia 
    wenzako jinsi ilivyokuwa.
    17.6. Kuandika 
    Kazi ya 10:
    Tunga kifungu cha habari kuhusu sikukuu fulani uliyoisherehekea 

    siku moja au zaidi kisha uonyeshe vile ulivyoona pale. 

    cc

    vvv

    Kitambulisho cha shule

    18.1. Kusoma na ufahamu: Ombi la vitambulisho
    Uwera, Aline na Rwema walienda kwenye ofisi ya tarafa ili kutafta vitambulisho mbalimbali
    Uwera: Shikamoo Katibu Mtendaji!
    Katibu Mtendaji: Marahaba bibi. Nikusaidie nini?
    Uwera: Nimekuja hapa ili nipate cheti cha kuzaliwa.
    Katibu Mtendaji: Karibu ofisini. Nipe kibali cha Katibu Mtendaji wa Kata.
    Uwera : Hiki hapa Katibu.
    Katibu Mtendaji: Naona wewe namaliza kukupa huduma yako. Mwambie mwingine aingie.
    Uwera: Kwaheri. (Mwingine anayehitaji huduma aingie).
    Rwema: Mimi nataka kadi ya uraia nimetimiza miaka kumi na sita.
    Katibu Mtendaji: Ndiyo. Na wewe?
    Aline: Nimekuja mniandikie kibali niende kwenye wilaya kutafuta pasipoti kwani nitaenda Marekani mwezi ujao.
    Katibu Mtendaji: Barabara kabisa. Rwema, nenda ukamkute mtumishi 
    wa mtandao Irembo atakusaidia haraka. Na wewe Aline mwambatane kwa sababu mna shida sawa.
    Aline& Rwema: Asante sana katibu. Nchi yetu imepiga hatua kiteknolojia.
    Katibu Mtendaji: Asante kushukuru.
    Kazi ya 1:
    Maswali ya ufahamu
    1. Mazungumzo haya yametokea wapi? 
    2. Kwa nini raia walitembelea ofisi ya katibu mtendaji wa tarafa?
    3. Kiongozi yule aliwapokeaje raia?
    4. Rwema aliambiwa kupata alichokitaka wapi?
    5. Ni kwa nyanja gani Rwanda ina maendeleo?
    18.2. Msamiati kuhusu aina ya vitambulisho
    Kazi ya 2:
    Toa maana ya msamiati huu na uutumie katika sentensi
    i. Cheti
    ii. Ofisi
    iii. Huduma
    iv. Kibali
    v. Kuambatana
    Kazi ya 3:
    Jaza sentensi kwa kutumia msamiati ufuatao: pasipoti, huduma, ofisi, cheti
    i. Nilipoingia kazini ilinibidi nitafute………………cha kuzaliwa.
    ii. Mujawase ataulizwa………………..kabla ya kuenda nchini 
    Ujerumani.
    iii. Katibu mtendaji wa tarafa anawapa raia …………….nzuri sana.
    iv. ……………ya wilaya yetu inapatikana mbali na nyumba yangu.

    18.3. Sarufi: Matumizi ya ngeli ya U-ZI na vivumishi vya kumiliki
    Kazi ya 4:
    Tazama sentensi hizi na kujadili mabadiliko ya kisarufi yanayojitokeza.
    1. Wimbo wake unapendeza mno (umoja).
    2. Nyimbo zoo zinapendeza mno (wingi).
    3. Upinde wangu umevunjika (umoja).
    4. Pinde zetu zimevunjika (wingi)
    Maelezo muhimu
    Majina ya ngeli ya U-ZI yametumiwa pamoja na vivumishi vya kumiliki.
    Vivumishi vya kumiliki ni maneno yanayoonyesha kitu ni cha nani, mtu fulani 
    ni wa nani au kitu kina nini . Navyo ni sita: –angu, -etu -ako,-enu -ake,-ao
    Mifano zaidi
     Umoja                                                                                Wingi
    Uso wangu ni mzuri sana.                                   Nyuso zetu ni nzuri sana
    Ufunguo wako ni mchafu kabisa                     Funguo zenu ni chafu kabisa
    Ukuta wake utajengwa upya                            Kuta zao zitajengwa upya
    Kazi ya 5:
    Jaza sentensi hizi kwa kutumia vivumishi vya kumiliki vinavyofaa 
    kulingana na kiambishi cha nafsi ambacho kimeandikwa katika mabano:
    1. Ukucha …………………umerefuka sana (yeye).
    2. Uzi …………………..ni mweusi sana (Kagorora na mimi).
    3. Kazeneza na Mwami waliibiwa funguo ………….zote (wao).
    4. Usikose kupaka rangi ukuta ………..ule kwani umechafuka sana 
    (wewe).

    Kazi ya 6:

    Soma kifungu hiki cha habari na kueleza matumizi ya maneno 
    yaliyopigiwa kistari

    Habari gani Dusabe? Mbona umenunua kufuli lenye ufunguo mmoja? 
    Bila shaka utalirudisha sokoni. “Funguo zipi baba?” Dusabe aliniuliza. 
    “Funguo nyingine nimeziweka kabatini,” Dusabe aliendelea kueleza. 
    Baada ya maelezo yake nilifungua kabati na kuziona zote ndani. Nilikosa 
    cha kusema na kumwambia maneno haya: Samahani binti yangu 
    sitakusumbua tena nimeziona. Uwineza ndiye alikuwa amezichukua. 
    Niliendelea kumwuliza, “umeleta wembe upi?” Tuliongea mengi na 
    kumruhusu aende kula chakula cha mchana. Tokea siku hiyo, Dusabe na 
    Uwineza ni wasichana wapole wenye ukweli.

    Maelezo muhimu: 

    Vivumishi vya kuuliza hutumika kwa kuuliza swali. Badhi ya vivumishi viulizi 
    huchukua viambishi vya ngeli wakati ambapo vingine havichukui viambishi 
    hivyo vikitumiwa pamoja na nomino za ngeli ya U-ZI.
    Kivumishi kinachochukua kiambishi ngeli nitongueouti? Wakati ambapo viulizi –
    ngapi? na gani? Havichukui viambishi vya ngeli.
    Mfano:
     Umoja                                                                                                  Wingi
    Ukuta upi umejengwa ?                                                Kuta zipi zimejengwa ?
    -                                                                                               Kuta ngapi zimejengwa?
    Ukuta gani umejengwa?                                               Kuta gani zimejengwa?
    Kazi ya 7:
    Uliza maswali matatu ukitumia vivumishi –pi au gani katika ngeliya U-ZI
    Kazi ya 8:
    Jaza sentensi hizi ukitumia kivumishi cha kuuliza kinachofaa.
    i. Uwineza alichukua funguo…………….?
    ii. Mchana huo Dusabe aliambiwa habari…………..?
    iii. Ni wembe…………….ambao binti yangu atauleta?
    iv. Tumbili wanapenda kuparamia ukuta………….?
    v. Karatasi …………..zilitengenezwa katika miti ya kwetu?

    18.4. Matumizi ya lugha
    Kazi ya 9:
    Jibu maswali yafuatayo:
    1. Je, raia anaweza kupata vitambulisho vifuatavyo katika ngazi zipi 
    za kiutawala?
     Pasipoti, cheti cha kuzaliwa, Cheti cha ndoa na leseni ya udereva.
    2. Ikiwa kitambulisho fulani kimepotea au kimeibiwa, raia aliyekipoteza 
    atafanya nini?
    3. Je, kuna kosa lolote la utumiaji mbaya wa vitambulisho vya kitaifa? 
    Eleza.
    Maelezo muhimu: Vitambulisho.
    Kitambulisho ni cheti au kadi, aghalabu yenye picha inayotumiwa kwa ajili ya 
    kumtambulisha mtu na mahali pa kazi au mahali pengine ambapo kitu kama 
    hicho kinahitajika. Baadhi ya vitambulisho hivyo ni kama:
    1. Kitambulisho cha utaifa
    2. Cheti cha kuzaliwa
    3. Cheti cha elimu ya msingi,
    4. Pasi ya kusafiria (Pasipoti)
    5. Cheti cha elimu ya sekondari (kidato cha vi)
    6. Leseni ya udereva
    7. Kadi ya bima ya afya
    8. Kadi ya mpigakura
    9. Nambari ya mlipa kodi (Tin. No)
    10. Cheti cha ndoa 
    11. Cheti cha kufariki
    • Nchini Rwanda, idadi kubwa ya vitambulisho hupatikana kupitia 
    mtandao rasmi wa kiteknolojia -IREMBO na kumwangalia kiongozi 
    husika baadaye.

    UMUHIMU WA KITAMBULISHO
    Vitambulisho vya Taifa ni msingi wa maendeleo ya kiuchumi, kijamii 
    na kisiasa.
    1. Vitasaidia kuongeza wigo wa mapato ya Serikali
    2. Vitasaidia kumtambua mhusika kwa urahisi anapohitaji huduma 
    katika taasisi mbalimbali kama vile benki, taasisi za mikopo na huduma za afya.
    3. Vitarahisisha kuwatambua wakwepaji wa kurejesha mikopo kutoka 
    kwenye benki na asasi mbalimbali za fedha nchini.
    4. Vitasaidia kuweka kumbukumbu za matukio ya uhalifu katika daftari la kumbukumbu la kielektroniki.
    5. Vitawezesha kumtambua mtu anapofanya biashara au shughuli nyingine kwa kutumia majina tofauti.
    6. Vitafanikisha kuhakikisha kuwa mtu anapata stahili zake za jamii. 
    Kwa mfano, kupata malipo ya pensheni, haki za matibabu, haki za 
    kujiunga na masomo ikiwa ni pamoja na stahili zozote ambazo raia 
    wa Rwanda anastahili kupata kwa urahisi kwani kupitia kitambulisho 
    mtu atatambulika kwa urahisi (fulani ni nani?, yuko wapi?, na anafanya nini? katika taifa hili.
    7. Vitasaidia  kuondoa watumishi hewa kwenye mfumo wa malipo ya mishahara ya Serikali.
    8. Vitaimarisha utendajikazi Serikalini kwa kuwa na kumbukumbu sahihi 
    za watumishi na malipo ya stahili zao, hasa pale wanapostaafu.
    9. Vitarahisisha zoezi la kuhesabu watu (sensa).
    10. Vitarahisisha zoezi la kusajili wapigakura
    18.5. Kusikiliza na Kuzungumza
    Kazi ya 10:
    Zungumzia umuhimu wa kuwa na kitambulisho cha taifa na hasara za 
    kutokuwa nacho.
    18.6. Kuandika
    Kazi ya 11:
    Andika umuhimu wa vitambulisho vya kitaifa. Kwa kutumia maneno 
    yasiyopungua 100

    Tathmini ya mada

    Jibu maswali yafuatayo:
    1. Jamhuri ya Rwanda inaongozwa na nani?
    2. Jaza nafasi zilizoachwa wazi kwa kutumia vivumishi vilivyotolewa mabanoni:
    a. Ukuta ………………..ulioanguka ulikuwa haukujengwa vizuri 
    (moja,mmoja,mbili).
    b. Habimana hakuvunja ufunguo……………….(ndogo, mdogo, wadogo).
    c. Nyuzi…………………..ni nyeusi na nyekundu, pia (zao, wangu, yake).
    3. Taja majina ya kiutawala yanayotumiwa kwa viongozi wa ngazi zifuatazo:
    a. Wilaya b. Kijiji c. Tarafa
    4. Andika aina tano za vitambulisho vya kitaifa.
    5. Ni nini kinachowanufaisha viongozi wakati wa kusherehekea sikukuu za kitaifa?
    6. Taja mifano minne ya umuhimu wa vitambulisho kwa jamii ya Wanyarwanda.















  • MADA YA 5 KISWAHILI KATIKA SHUGHULI ZA KIBIASHARA

    Uwezo mahususi wa mada: Kuzungumza na kuandika kwa ufasaha matini 
    fupifupi kwa kutumia msamiati unaofaa katika shughuli za kibiashara.
    Malengo ya ujifunzaji:
    • Kufanya mazungumzo kati ya mfanyabiashara na mteja, 
    • Kutumia kwa ufasaha mizani au vipimo katika hesabu,
    • Kuainisha pesa zitumiwazo katika shughuli za kibiashara, 
    • Kuainisha bidhaa mbalimbali zipatikazo sokoni,
    • Kutumia kwa ufasaha ngeli ya I-ZI katika sentensi sahihi,
    Kidokezo

    Taja baadhi ya msamiati maalumu unaotumiwa katika mazingira ya 

    biashara

    SOMO LA 19: MAWASILIANO SOKONI

    cc

    Kazi ya 1:
    Tazama mchoro hapa juu na kueleza kinachofanyika hapo.
    19.1. Kusoma na ufahamu: Safari ya Niwemwiza na Kayigi sokoni
    dd


    Siku moja nilitembea sokoni na kaka yangu Kayigi ili kununua vifaa vya 
    shule. Soko hilo linaloitwa Gatare lilikuwa katika kilomita kumi na tano kutoka 
    kwetu. Mama alitupatia pesa za nauli na nyingine za kununua vifaa tofauti 
    vya shule na bidhaa nyingine za kutumia nyumbani.
    Tulitoka nyumbani saa tatu za asubuhi na kufika sokoni saa nne. Tulipokuwa 
    garini, Kayigi aliniuliza kama ninakumbuka vifaa ambavyo mama alituambia 
    kununua. Nilimkumbusha kwamba alituambia kununua vifaa vifuatavyo: 
    shati, jaketi, jozi ya viatu, sidiria, madaftari kumi, kalamu nane, soksi mbili 
    na sabuni vilevile.

    Kayigi aliniuliza kama hakuna vitu vingine amabavyo nimesahau ili 
    anikumbushe tusije tukasahau na vile vilivyokuwa vinahusu matumizi ya 
    nyumbani. Kwa kusema hayo nilianza kuangalia kulia na kushoto, mbele 
    na nyuma kwa ajili ya kuchunguza aina mbalimbali za bidhaa tofauti ili nisije 
    nikasahau chochote nilichoambiwa na mama.
    Nilikumbuka kuwa, mama alikuwa ameniambia kununua nyama, viazi vitamu, maharagwe na sukari. Tulipofika sokoni, tulishangaa kuona watu wengi wa marika tofauti wakijaa sehemu zote. Kelele nyingi za watu sokoni zilikuwa zimehanikiza si huku si kule.

     Kayigi alinishika mkono na kunielekeza pahali panapouzwa bidhaa tofauti. Sauti hizo zilikuwa za wauzaji wakisema: Mia bei! Mia bei! ….karibu mteja… bei rahisi…..chagua….chagua…..kaptula hii ni mia tatu, jaketi hii ni mia tano. Karibu mteja wangu. Karibu katika kibanda changu. Bidhaa ni nyingi utachagua zile utakazo. Tulianzia sehemu panapouzwa nguo.

     Kayigi nami tulifika mbele ya kibanda cha nguo tukaanza kuuliza bei ya vile tulivyokuwa tunataka. Kwanza niliuliza bei ya jaketi niliyokuwa nimechagua. Muuzaji alinijibu kuwa jaketi ilikuwa elfu moja. Nilimwambia apunguze kidogo kwa kuwa bei ilikuwa ghali. Tulijadiliana bei mpaka akakubali mia tisa.
     Baada ya kununua nguo, tuliendelea kutembea sokoni tukanunua vifaa vya shule. Kwenye kibanda cha vifaa vya shule, tulinunua madaftari na kalamu. Bei za kila bidhaa zilikuwa ni bei nafuu. Daftari moja tulilinunua kwa mia moja na hamsini na kalamu kwa mia tu.

    Kabla ya kurudi nyumbani, tulikumbuka kuwa mama alitutuma kununua nyama kwenye bucha. Nilichunguza mfukoni mwangu pesa nilizokuwa nabaki nazo nikaona mnabaki dola mia tano za Marekani tu. Niliuliza dada yangu jambo la kufanya akanishauri kwenda kwenye duka la kubadilisha pesa za kigeni. Tulikwenda mbio na kufika kwenye nyumba ya ghorofa kubwa ambapo pamekuwa maduka mengi ya kubadilisha pesa.

     Tuliingia duka moja ambamo tulikaribishwa na kijana mmoja aliyetubadilishia pesa zetu katika pesa za Rwanda tukarudi sokoni.
    Kwenye bucha, bei ilikuwa ghali pia kwani kilo moja ya nyama ilikuwa mbili elfu mia tano. Kayigi alijaribu kupunguzisha bei. Muuza nyama alikataa kuipunguza akisema kuwa hawezi kupata faida akipunguza. Je, mnataka nipate hasara? Muuza nyama aliuliza. Nilimwomba kupunguza bei kidogo kufika mbili elfu mia tatu.

     Aidha, tulinunua kifungu kimoja cha mboga za sukumawiki, vifungu viwili vya nyanya na kilo moja ya chumvi.
    Ilipofika saa saba za mchana tulichukua basi tukarudi nyumbani. Tulipofika nyumbani mama alitushukuru kwa kuwa hatukukawia kurudi na kuwa
    tulitumia pesa vizuri. Kila mmoja alimwahidi kumpa tuzo ya peremende mbili.

    Kazi ya 2:
    Maswali ya ufahamu
    a. Taja aina mbili za bidhaa ambazo mama aliwatuma wanawe sokoni.
    b. Ni kwenye sehemu gani ya soko ambapo Kayigi na Niwemwiza walinunua madaftari na kalamu?
    c. Nini kilichosababisha Kayigi na Niwemwiza kushangaa walipofika sokoni?
    d. Kwa sababu gani mchinjaji alikataa kupunguza bei ya kilo moja ya nyama?
    e. Ni kwa sababu gani mama aliwapongeza wanawe walipotoka sokoni?
    19.2. Matumizi ya msamiati
    Kazi ya 3: Toa maana ya msamiati ufuatao:
    a. Faida
    b. Bei ghali
    c. Kununua
    d. Kuuza
     e. Bucha
     f. Hasara

    19.3. Sarufi: Matumizi ya ngeli ya I-ZI
    Kazi ya 4:
    Tazama sentensi zifuatazo na kujadili mabadiliko ya kisarufi yanayojitokeza.
    a. Biashara imetajirisha watu wengi duniani na kuendeleza hali yao ya 
    maisha (Umoja).
    • Biashara zimetajirisha watu wengi duniani na kuendeleza hali yao 
    ya maisha (Wingi).
    b. Nguo ambayo imechafuka imemuambukiza magonjwa (Umoja).
    • Nguo ambazo zimechafuka zimewaambukiza magonjwa (Wingi).
    Maelezo muhimu
    Ngeli hii ya I-ZI inajumuisha nomino za vitu visivyo na uhai. Nomino hizi 
    umoja na wingi wake huwa ni sawa. Isitoshe, nomino hizi ni za vitu ambavyo 
    vinaweza kuhesabika k.m kalamu, meza, sahani, rafu, linga, saa, rula, soksi, 
    nyumba, karatasi, kamusi, wiki, siku, chaki, chupa, ndizi, kamba, bawaba, 
    pete, n.k.
    Majina ya ngeli hii hutumia kiambishi nafsi “I” katika umoja na kiambishi nafsi 
    “ZI” katika wingi kufuatana na upatanisho wa kisarufi.
    Matumizi ya majina ya ngeli ya I-ZI na vivumishi vya sifa
    • Vivumishi “-baya” na”-pya” huchukua kiambishi “m-“ badala ya “n-“.
    Mfano: 
    Umoja: Barabara mpya ilijengwa Kiramuruzi na kurahisisha 
    mawasiliano baina ya raia huko. 
    Wingi: Barabara mpya zilijengwa Kiramuruzi na kurahisisha 
    mawasiliano baina ya raia huko. 
    Umoja:Tabia mbaya inakemewa na wengi
    Wingi: Tabia mbaya zinakemewa na wengi
    Vivumishi vinavyoanza na “r” herufi hiyo hugeuka “nd” inapotanguliwa na 
    kiambishi “n”.
    Mfano:
    Umoja: Ndoo ndefu imewekwa bafuni ili kuogea mikono.
    Wingi: Ndoo ndefu zimewekwa bafuni ili kuogea mikono. 
    • Vivumishi vinavyoanza na “ch, f, p, k, t” havipachikwi viambishi katika 
    umoja wala wingi.
    Mfano:
    Umoja: Meza chafu imetupwa nje.
    Wingi: Meza chafu zimetupwa nje.
    Umoja: Nyumba kubwa na ya kisasa inahitajika mjini.
    Wingi: Nyumba kubwa na za kisasa zinahitajika mjini.
    Umoja: Sketi fupi inakatazwa shuleni.
    Wingi: Sketi fupi zinakatazwa shuleni.
    Umoja: Meza kubwa imewatosha watu wengi harusini.
    Wingi: Meza kubwa zimewatosha watu wengi harusini.
    Umoja: Ndizi tamu imenunuliwa sana sokoni.
    Wingi: Ndizi tamu zimenunuliwa sana sokoni.
    Umoja: Nyumba pana iliwatosha wageni wote wakati wa mkutano wa 
    kimataifa.
    Wingi: Nyumba pana ziliwatosha wageni wote wakati wa mkutano wa 
    kimataifa.

    Kazi ya 5:

    Chagua neno linalofaa na kuliandika katika nafasi iliyoachwa wazi.
    1. Barabara hii ni ……….lakini imepasuka kwa sababu haikujengwa 
    vizuri. (Zipya, kipya, mpya)
    2. Tafadhari nipe Kamusi ya Kiswahili ……… kuna msamiati mgumu 
    ninaotaka kuchunguza ( kisanifu, jisanifu, sanifu)
    3. Karatasi …………zimetupwa jalalani ( mchafu, wachafu, chafu).
    4. Meza …………imewekewa bidhaa nyingi sokoni (vipana, pana, 
    kipana)
    5. Pombe ………iliwalevya watoto na kusababisha kutohudhuria 
    masomo (mtamu, litamu, tamu)
    Kazi ya 6:
    Kwa kutumia vivumishi vya sifa, tunga sentensi sahihi kwa kutumia 
    maneno yafuatayo:

    a. Nyumba 
    b. Shule 
    c. Karatasi 
    d. Baiskeli 
    e. Nyumba
    19.4. Matumizi ya lugha: Msamiati maalumu katika uwanja 
    wa kibiashara

    Kazi ya 7:
    Taja istilahi tano zitumiwazo katika shughuli za kibiashara na kueleza 
    maana yake.

    Maelezo muhimu kuhusu msamiati unaotumiwa katika shughuli za 
    kibiashara. 

    • Biashara: ununuzi na uuzaji wa bidhaa na/au huduma.
    • Faida/tijara/kivuno/chumo/ziada - Pato libakialo baada ya kuondoa 
    gharama za kufanya biashara k.v. ununuzi na usafirishaji.
    • Hasara: Ukosefu wa faida; hali ya kupoteza pato au mali katika biashara. 
    • Bei: Kiwango cha pesa kununulia au kuuzia bidhaa au huduma fulani. 
    • Bei: Kiwango cha pesa kununulia au kuuzia bidhaa au huduma fulani. 
    • Uuzaji wa rejareja: Uuzaji wa kiasi kidogo kidogo. 
    • Uuzaji wa jumla: Uuzaji wa kwa pamoja 
    • Bei rafi: Bei ambayo haipunguzwi. 
    • Kipimo rafi: Kipimo ambacho hakipunguzwi. 
    • Bei ya kuruka: Bei isiyokubalika kisheria/haramu.
    • Rasilimali: Jumla ya mali inayomilikiwa na mtu au nchi.
    • Malighafi: Mali inayotumika kutengeneza vitu vingine k.m. pamba ni 
    malighafi ya kutengenezea nguo.
    • Maliasili: Utajiri kama vile madini, misitu, maziwa, mito, anga 
    vinavyopatikana katika mazingira. 
    • Uwekezaji: Kutumia pesa / mali ili kuzalisha fedha/mali zaidi (ilikupata 
    faida).
    • Kitegauchumi: Rasilimali k.v. kiwanda inayotumika kuzalisha mali. 
    • Ujasiriamali: Uwekezaji mtaji katika biashara.
    • Mtaji: Mali ya kuanzisha biashara au kuipanulia.
    • Ulanguzi: Ufichaji wa bidhaa ili bei yake iruke.
    • Magendo: Upigaji biashara kwa njia haramu/isiyo halali. 
    • Chenji: pesa inayobaki baada ya kununua kitu 
    • Maduhuli: Bidhaa ambazo hununuliwa kutoka nchi za nje.
    • Mahuruji: Bidhaa zinazouzwa nchi za nje.
    • Ushuru: Kodi ya kuingiza bidhaa nchini au kuziuza/Ada ya forodha. 
    • Ruzuku: Pesa inayotolewa na serikali kwa idara mbalimbali ili 
    kujiendeleza. 
    • Mshitiri: Mnunuzi. 
    • Mteja: Mtu aendaye kununua bidhaa au huduma.

    • Wakala: Ajenti

    • Utandawazi: Utaratibu wa mataifa kushirikiana katika nyanja mbalimbali 
    k.v. biashara.
    • Ubinafsishaji: Hali ya kusababisha mali ya umma imilikiwe na watu 
    binafsi. 
    • Ubia: Ushirikiano wa watu wawili au zaidi katika shughuli k.v. ya 
    biashara. 
    • Hawala: Hundi/ cheki yaani cheti maalumu cha benki kinachotumiwa 
    kuidhinisha aliyetajwa kwenye cheti hicho apewe fedha za mwenye 
    hesabu. 
    • Amana: Kitu unachomwekea mwenzako hadi atakapokihitaji.
    • Turuhani: Kiwango kinachotolewa kutoka katika bei iliyotangazwa. 
    • Iktisadi: Uangalifu katika kutumia fedha/mali. 
    • Ubepari: Mfumo wa uchumi ambao unawawezesha watu wachache 
    kumiliki rasilimali na vitegauchumi.
    • Ukiritimba: Hali ya kuzuia wengine kufanya biashara au kushindana 
    katika biashara.
    • Dukakuu: Duka kubwa ambapo wateja hujichukulia bidhaa watakazo 
    kutoka rafuni.

    • Hisa: Sehemu ya mtaji katika biashara.

    Kazi ya 8:
    Tunga sentensi sahihi kwa kutumia maneno yafuatayo
    a. Hundi
    b. Mteja
    c. Ruzuku
    d. Magendo
    e. Rasilimali

    19.5. Kusikiliza na kuzungumza
    Kazi ya 9:
    Tega sikio habari inayosimuliwa na mwanafunzi mwenzako kuhusu 
    safari yake sokoni na kusimulia hali ya safari hiyo mbele ya darasa.
    19. 6. Kuandika
    Kazi ya 10:
    Tunga kifungu cha habari chenye aya tatu kuhusu safari yako sokoni.
    SOMO LA 20: MAJADILIANO DUKANI
    Kazi ya 1:
    Taja mahali fulani panapofanyiwa biashara na huduma zinazotolewa hapo.

    20.1. Kusoma na ufahamu: Muuzaji na mteja

    vv

    Mazungumzo yafuatayo yanahusu Kalisa ambaye ni mteja na Uwera ambaye 

    ni muuzaji. Wanajadiliana bei dukani. 

    Kalisa : Habari za asubuhi bibi !
    Uwera : Nzuri. Nikusaidie nini ?
    Kalisa : Nataka kununua bidhaa tofauti tofauti katika duka lako. Naona duka 
    lako lina bidhaa mbali mbali zinazovutia macho. 
    Uwera : Ndiyo. Mimi ninaagiza bidhaa kufuatana na mahitaji ya wateja ili 
    waweze kufaidika na kile wanachokinunua.
    Kalisa : Mimi nahitaji sabuni, kilo moja ya chumvi, kilo mbili za sukari, nusu 
    ya vitunguu, lita ya mafuta ya kupikia na sufuria moja.
    Uwera : Vyote hapa Kalisa. 
    Kalisa :Kila bidhaa ambayo nimekutajia inauzwa kwa bei gani ?
    Uwera : Bidhaa hizi zote zinauzwa kwa bei nafuu. Sabuni moja ni faranga 
    mia moja, kilo moja ya chumvi ni faranga mia tatu, nusu ya vitunguu ni 
    faranga mia moja hamsini, lita ya mafuta ya kupikia ni mia tano na sufuria 
    hii ni moja elfu. 
    Kalisa : Mbona sufuria ni bei ghali ? Je, unaweza kupunguza kidogo ?
    Uwera : Hiyo ni bei rafi bwana. Ungenunua sufuria mbili ningekupunguzia.
    Kalisa : Nipunguzie faranga mia moja nitaendelea kununulia hapa.
    Uwera : Ninakupunguzia faranga hamsini tu kwa sababu sufuria hii ni kubwa.
    Kalisa : Asante. lakini chukua mizani unipimie kilo ya chumvi na nusu ya 
    vitunguu.
    Uwera : Ndiyo. Angalia hapa vipimo vinaenea. Kwa uhakika mizani yangu 
    ni mpya sikunyang’anyi.
    Kalisa : Hakuna nyongeza bibi ?
    Uwera : Nitakupatia nyongeza ya kutosha siku ijayo.
    Kalisa : Ni pesa ngapi ya kulipa kwa jumla?
    Uwera : Mbili elfu kwa jumla.
    Kalisa : Ahsante sana bibi.
    Uwera : Asante kwa kushukuru. Karibu tena.

    Kalisa :Kwaheri !

    Kazi ya 2:
    Maswali ya ufahamu
    1. Taja bidhaa zinazozungumziwa katika mazungumzo haya.
    2. Kalisa alinunua nini dukani ?
    3. Nini umuhimu wa mizani ?
    4. Ni kwa sababu gani Uwera huuza bidhaa zinazovutia macho ya watu ?

    5. Uwera alimwahidi Kalisa kumfanyia nini siku ijayo ?

    20.2. Matumizi ya msamiati
    Kazi ya 3:
     Toa maelezo ya bidhaa zifuatazo:
    a. Kekee
    b. Patasi 
    c. Chungu 
    d. Jiko la mkaa 
    e. Almasi 
    f. Dhahabu 
    g. Maziwa 
    h. Kuku
    i. Maparachichi 

    j. Tikitimaji

    20.3. Sarufi: Matumizi ya ngeli ya I-ZI na vivumishi vya a-unganifu
    Kazi ya 4:
    Tazama sentensi katika sehemu A na sentensi katika sehemu B na 

    kueleza mabadiliko ya kisarufi yanayojitokeza.

    cc

    Maelezo muhimu kuhusu matumizi ya vivumishi vya a-unganifu
    Majina ya ngeli ya I-ZI yakitumiwa pamoja na vivumishi vya a-Unganifu, 
    umoja wake huchukua ya na wingi huchukua za.
    Mfano: 
    Umoja: Runinga ya Gakire ilinipasha habari kuhusu nanma ya kuleta umoja na maridhiano kwetu
    Wingi: Runinga za Gakire zilinipasha habari kuhusu nanma ya kuleta umoja na maridhiano kwetu.
    Umoja: Rafu ya mama inajaa bidha nyingi.
    Wingi: Rafu za mama zinajaa bidha nyingi.

    Kazi ya 5:
    Tunga sentensi 5 kwa kutumia majina ya ngeli ya I-ZI na kiambishi 
    cha -a unganifu

    20.4. Matumizi ya lugha: Aina za bidhaa zinazopatikana 
    sokoni

    Kazi ya 6
    Bainisha aina kumi za bidhaa zinazopatikana sokoni.
    Maelezo muhimu
    Kuna aina mbalimbali za bidhaa zinazouzwa na kununuliwa sokoni. Baadhi 
    ya bidhaa hizo hutokana na kilimo, ufugaji, vifaa vya ufundi na vile ambavyo 
    hutengenezewa viwandani.
    Kazi ya 7:
    Toa mifano miwili miwili ya bidhaa zinazoweza kupatikana katika mazingira 
    ya sokoni (Bidhaa zitokanazo na viwanda, mazao, ufugaji, madini)
    20.5. Kusikiliza na kuzungumza
    Kazi ya 8:
    Buni mazungumzo kati yako na mwenzako kuhusu majadiliano 
    kati ya muuzaji na mnunuzi. Majadiliano haya yafanyike sokoni na 
    yaonyeshe kutokubaliana kwenye bei ya bidhaa zinazouzwa.
    20.6. Kuandika
    Kazi ya 9:
    Tunga mazungumzo yasiyopungua ukurasa mmoja kuhusu 

    majadiliano ya bei dukani.

    cc

    Kazi ya 1:
    Tazama mchoro hapo juu na kueleza kinachofanyika.

    21.1. Kusoma na ufahamu: Matumizi bora ya mizani

    vv

    Bwana Muhire ni mfanyabiashara katika soko linaloitwa Maridadi. Biashara 
    yake inahusu uuzaji wa matunda, bidha za kula, na mafuta ya kupikia. Mara 
    nyingi raia humlalamikia wakisema kuwa yeye hatumii vipimo sahihi.
     

    Siku moja, Amina alikwenda sokoni kununua bidhaa tofauti za matumizi 
    ya nyumbani. Soko hilo lilikuwa kwenye umbali wa kilomita mbili kutoka 
    kwake. Alipofika sokoni, alikaribishwa na muuzaji aitwae Muhire. Muhire 
    anajulikana sana katika soko hili la Maridadi. Muhire alimwomba kutaja vitu 
    vyote alivyokuwa anataka kununua. 

    Baadhi ya bidhaa alizokuwa anahitaji kulikuwa kilo kumi za maharage, 
    kilo moja na nusu ya chumvi, lita tano za mafuta ya kupikia, gramu mia 
    mbili hamsini ya nyama za kupikia ndugu yake mdogo, mafungu mawili ya 
    sukumawiki na fungu moja la nyanya.

    Baada ya kuorodhesha bidhaa hizo zote, aliomba Muhire kuchukua mizani 

    na kupima ili kuhakikisha kwamba hamnyang’anyi. Muhire alichukua 
    mizani na kuanza kupima maharagwe. Alipomaliza kupima, Amina aliona 
    kuwa maharagwe yaliyokuwa yamepimwa yalikuwa machache akaanza 
    kumlalamikia. Mbona unanipa maharagwe kidogo? “Mizani yako si sahihi,” 
    Amina alisema. Amina alienda nyuma ya kibanda akapigia simu mfanyakazi 
    katika Bodi ya Mapato Rwanda. 

    Katika dakika thelathini viongozi wanaohusika na ushuru nchini walitembelea 
    soko hilo na kuwakagua wafanyabiashara halamu. Walitembelea watu 
    ishirini na kukagua jumla ya mizani ishirini na miwili. Baadhi ya mizani hiyo, 
    iliyokutwa sahihi ni ishirini na jumla ya mizani miwili ilikutwa na kasoro. 
    Tokea hapo, mizani hii haikuruhusiwa katika biashara mpaka itengenezwe 
    na mafundi na kuhakikiwa upya na wakala wa Vipimo ili iweze kuruhusiwa 
    kutumiwa katika biashara.

    Wafanyabiashara waliotuhumiwa ni Muhire na Kazimoto ambao walikubali 
    kosa lao la kutaka faida nyingi mno kwa njia isiyo halali. Bila kusita , viongozi 
    waliwashawishi raia na wafanyabiashara kutumia mizani iliyopimwa tu yaani 
    iliyo sahihi.

    Katika hatua nyingine, kiongozi mkuu aliwaonya wafanyabiashara 
    wanaolalamikiwa kuweka mawe, kokoto pamoja na mchanga,vipande vya 
    vyuma na aina nyingine za vitu kwenye mizani kwa ajili ya kuongeza uzito 
    waache tabia mbaya hiyo mara moja kwani wakikamatwa watapata hasara. 
    Alieleza kwamba sheria ya vipimo ipo na inafanyakazi kwa pande zote mbili 
    yaani kwa muuzaji na mnunuzi. 

    Wote hawatakiwi kufanya udanganyifu wowote katika biashara. Alisisitiza 
    kuwa wale watakaobainika kuchezea mizani kwa ajili ya kuwaiba wananchi 
    adhabu ni kubwa sana kwawo kama vile kifungo au kutozwa faini au vyote 
    kwa pamoja ; shabaha ikiwa ni kumlinda mlaji ili apate faida na thamani ya 
    kile alichozalisha ama kukinunua na siyo tu kupunjwa na wafanyabiashara 
    wajanjawajanja.

    Baada ya mkutano, mbele ya watu wote waliokuwa wamekusanyika hapo 
    sokoni, viongozi walitoa tuzo ya mizani nne kwa wafanyabiashara ambao 
    hawakuwa na makosa yoyote katika shughuli zao za kibiashara. Hii ilikuwa 
    ni kutoa mfano kwa watu wote ili kusipatikane tena kosa lile la kuiba watu. 

    Watu waliokuwepo walifurahi na kuwapigia makofi viongozi wao. Viongozi 
    nao waliwapongeza kwa kuwa waliwajulisha hali ya makosa yanayofanywa 
    na wafanyabiashara wakiwanyonya raia.

    Kazi ya 2:

    Maswali ya ufahamu
    1. Nani ambaye alilalamikiwa kuwa na matumizi ya mizani isiyo sahihi?
    2. Bainisha aina mbili za adhabu ambazo hupewa mtuhumiwa anayehusika na matumizi ya mizani isiyo sahihi.
    3. Ni onyo gani lililotolewa na kiongozi mkuu kwa wafanyabiashara wanaotumia mizani kinyume na sheria? 
    4. Eleza lengo la ziara ya viongozi wanaohusika na ushuru katika soko la Maridadi.
    5. Afanyaye vizuri hutuzwa. Eleza kauli hii kwa kutoa mfano kutoka katika kifungu hiki cha habari.
    21.2. Matumizi ya msamiati
    Kazi ya 3:

    Oanisha maneno katika sehemu A na maana yake katika sehemu B.

    ccc

    21.3. Sarufi: Matumizi ya ngeli ya I-ZI na vivumishi vya kurejesha
    Kazi ya 4
    Soma sentensi katika sehemu A na kujadili mabadiliko ya kisarufi 

    yanayojitokeza katika sehemu B:

    vv

    Maelezo muhimu
    Majina ya ngeli ya I-ZI, katika sentensi hutumia kirejeshi -yo katika umoja 
    na kirejeshi -zo katika wingi. Vivumishi hivi kuwa vinarejelea nomino.
    Mfano: 
    Umoja: Pikipiki ambayo amenunua imemtajirisha.
    Wingi: Pikipiki ambazo wamenunua zimewatajirisha.
    Kazi ya 5
    Kwa kutumia kirejeshi amba-, tunga sentensi katika umoja na wingi 
    kwa kutumia maneno yafuatayo:

    a. Klabu
    b. Chupa
    c. Redio
    d. kaptula
    e. suruali

    21.4. Matumizi ya lugha: Matumizi ya mizani katika hesabu na aina za pesa
    Kazi ya 6
    Taja aina za mizani au vipimo unavyovijua
    Maelezo muhimu
    A. Matumizi ya mizani au vipimo
    Kipimo ni kiasi au kadiri. Kuna vipimo vya aina tofauti.
    Jedwali lifuatalo linaonyesha aina mbalimbali za vipimo.
    vv
    B. Hesabu

    Mifano ya hesabu kwa tarakimu na kwa maneno kutoka 1-1,000,000

    vvv

    cc

    Kazi ya 7:
     Andika kwa tarakimu 
    a. Kumi na sita
    b. Thelathini na moja
    c. Sabini na saba
    d. Mia tatu hamsini
    e. Moja elfu mia mbili na saba
    f. Laki tano
    g. Moja elfu mia mbili ishirini na sita
    C. Alama za hesabu
    Alama ni mchoro wa kutambulisha kitu (Ishara)

    Jedwali lifuatalo linaonyesha alama za hesabu na maana zake.

    vv

    Kazi ya 8:
    Andika kwa tarakimu
    a. Sitini jumlisha kumi ni sawa na sabini.
    b. Mia moja arobaini toa ishirini na saba ni sawa na mia moja na kumi na tatu.
    c. Mia nane na themanini gawanya kwa nane ni sawa na mia moja na kumi.
    d. Sabini na moja ni kubwa kuliko kumi na nne.
    e. Mia moja ni ndogo kuliko laki moja.
    f. Tisini mara tatu ni sawa na mia mbili na sabini.
    D. Aina za pesa zitumiwazo katika shughuli za kibiashara
    Kazi ya 9:

    Tazama mchoro ufuatao na kueleza shughuli zinazofanyiwa hapo.

    ccc

    Maelezo muhimu
    Pesa ni nini?
    Pesa ni chombo cha kubadilishana bidhaa na huduma kati ya watu. Pesa 
    zenyewe hazina faida na hazitoshelezi mahitaji ya binadamu ila zimekubalika 
    katika jamii kama njia ya kujipatia mahitaji mengine. Kuna majina mengine 
    ya pesa katika Kiswahili, kama kwa mfano: hela, fedha, dirhamu, darahima, 
    fulusi au sarafu, n.k.

    Pesa hutolewa na serikali ya nchi au na taasisi kama vile benki kuu inayofanya 
    kazi hii kwa niaba ya serikali.

    Kuna aina nyingi za pesa zinazotumiwa duniani katika biashara. Jedwali 
    lifuatalo linatuonyesha baadi ya aina tofauti za pesa na nchi au bara 
    zinakotumiwa.
    cc
    Kazi ya 10:
    Kamilisha sentensi hizi kwa kutumia aina ya pesa zinazotumiwa 
    katika nchi au bara husika.
    a.       Wanyarwanda wengi hutumia …………………..katika shughuli 
                   nyingi za biashara ya ndani.
    b.          Mjomba wangu alikwenda kumtembelea rafiki yake anayeishi 
                Uganda. Kabla ya kuvuka mpaka alikwenda kwenye duka la 
                  kubadilisha pesa ili wampe ………..za Uganda.
    c.            Mama aliniahidi kwamba nikishika nafasi ya kwanza katika kidato 
                 cha kwanza atanitembeza Marekani. Katika safari yetu tutatumia 
                 ………………… mia nne za kimarekani.
    d.         Shughuli za biashara anazozifanya mama yangu huhusisha 
               uagizaji wa bidhaa kutoka Japani. Kila wiki hulipa ……..elfu tano.
    e.       Je, uliwahi kufika katika duka la kubadilisha pesa? Mimi nilifikapo 
               nikaona faranga za Rwanda, Shilingi za Kenya, Dola za Marekani 
               na Kanada na ………..za Uingereza.
    Kazi ya 11:
    Tafuta aina tofauti za pesa zinazotumiwa katika nchi nyingine ambazo 
    hazikushughulikiwa katika somo hili.
    21.5. Kusikiliza na kuzungumza
    Kazi ya 12:
    Katika jozi, simulia mwenzako sifa za soko fulani uliyoitembelea na 
    kueleza bidhaa ulizoziona.
    21.6. Kuandika
    Kazi ya 13:
    Tunga kifungu cha habari kifupi kuhusu umuhimu wa biashara
    Tathmini ya mada
    1. Taja angalau vifaa kumi vinavyouzwa sokoni.
    2. Chagua neno linalofaa katika mabano na kukamilisha sentensi 
    zifuatazo:
    a. Mwalimu wetu huvaa suti nzuri sana. Wanafunzi wote hufikiri 
    kwamba suti zake hununuliwa kwa bei ………. (ghali, rahisi, rafi).

    b. Dada yangu amekwenda sokoni …………………….sare ya shule ili arudi 
    shuleni kesho kuanza masomo ya muhula wa tatu( kununua, kuuza).
    c. Uwantege anauza matunda katika soko la Nyagasambu. Kwenye kibanda 
    chake kuna ,………….,………,……… na ………….( maembe, ndizi 
    mbivu, machungwa, viazi vitamu, tikitimaji, mchele, madaftari, mananasi).
    d. Mwenye duka la vitabu alitoa ………………………………. ya kitabu 
    kimoja cha hadithi za Kiswahili kwa wateja wote ambao hununua kwake 
    kila wiki (nyongeza, mtaji).
    e. Wakati wa uhaba wa …………… sokoni, bei hupanda sana (wateja, 
    wanunuzi, bidhaa).
    3. Kwa kuzingatia matumizi ya ngeli ya I-ZI, tunga sentensi sahihi kwa 
    kutumia maneno yafuatayo:
    a. Nchi
    b. Tarafa 
    c. Serikali 
    d. Barabara
    e. Shule
    4. Kamilisha kifungu cha habari hiki kwa kutumia maneno sahihi.
    Mama Mutoni ni mfanyabiashara katika soko la Nyarugenge. Mara nyingi 
    huagiza bidhaa kutoka nchi zinazopakana na Rwanda. Anapoagiza 
    bidhaa kutoka Uganda inambidi abadilishe …………za Rwanda katika 
    ……………..za Uganda. Ni sawa na kuagiza bidhaa kutoka Tanzania na 
    Kenya.
     

    Ikiwa Mama anahitaji bidhaa zinazotengenezewa katika nchi za Ulaya 
    kama Vile Uingereza, inambidi kutumia ………………Mwezi uliopita 
    rafiki yake ambaye anaishi Marekani alimwambia kuwa kuna bidhaa 
    nzuri zinazoweza kumletea faida nyingi anapoziuza kwa Wanyarwanda. 
    Mama aliamua kumtumia ………….elfu tatu za Marekani ili amnunulie 
    bidhaa hizo.

    Kazi ya biashara naipenda sana. Kuna wakati amabapo naenda pamoja 
    na mama yangu Zambia na Libya kufanya biashara huko nikaona namna 
    anavyobadilisha faranga zake katika …………….. Libya au ……….za 
    Zambia nikawa na motisha ya kufanya biashara ya kubadilisha pesa siku 
    moja. Mimi nafikiri kwamba aina hii ya biashara itachangia kuongeza 
    mapato yetu nyumbani.
    5. Buni mazungumzo yenye ukurasa mmoja kati ya muuzaji na 
    mnunuzi katika duka la vitabu.


  • MADA YA 6 UIGIZAJI WA MAZUNGUMZO

    Uwezo mahususi katika mada hii: Kuigiza mazungumzo mbalimbali kwa 
    kutumia Kiswahili sanifu.
    Malengo ya ujifunzaji:

    • Kuzungumza Kiswahili Sanifu kwa ufasaha;
    • Kujiamini katika mazungumzo ya hadharani au jukwaani;
    • Kukuza stadi za kusikiliza, kukariri na kuzungumza hadharani;
    • Kuendeleza weledi wa kubuni mazungumzo mbalimbali.
    Kidokezo
    1. Nini maana ya mazungumzo?
    2. Ni faida gani zinazopatikana kutoka mazungumzo?
    3. Mazungumzo hujadili mada gani?
    4. Katika mazungumzo, inawabidi wahusika kuwa na sifa gani? 

    5. Mazungumzo huweza kutokea wapi?

    SOMO LA 22: KUIGIZA MAZUNGUMZO

    vv

    Kazi ya 1:
    Unaona nini kwenye mchoro huu?
    22.1. Kusoma na ufahamu: Mazungumzo kati ya mwalimu 

    mkuu wa shule na mzazi


    cc
    Mwalimu mkuu wa shule: Karibu bibi! Habari za asubuhi?
    Bibi: Si nzuri hedimasta! Ahsante sana kwa kunikaribisha.
    Mwalimu mkuu wa shule: Shida gani bibi? Nikusaidieje?
    Bibi: Labda ni makosa ya mwanangu kutumwa mzazi.
    Mwalimu mkuu wa shule: Jina lake ni nani?
    Bibi: Gasagara Peter, mwanafunzi wa mwaka wa kwanza. 
    Mwalimu mkuu wa shule: Kwa nini umeitwa na shule?
    Bibi: Kwa sababu ya utovu wa nidhamu wa mtoto wangu. Sababu hii 
    niliisoma kwenye barua aliyopewa na shule ya kuniita mimi mzazi wake nije 
    hapa shuleni haraka.
    Mwalimu mkuu wa shule: Ndiyo! Mtoto huyo namkumbuka. Ni yapi 
    yaliyomsibu? Je, alikuelezea kilichotokea?
    Bibi: Alikuwa na makosa! Aliyakiri makosa matatu hivi: Kosa la kuchelewa 
    shuleni, kuja shuleni bila vifaa vya shule na kukosa usafi mwilini.
    Mwalimu mkuu wa shule: Ni kweli. Ilitubidi tumwite mzazi wake aje shuleni 
    kwa sababu ya mwenendo wa mtoto wako ulikuwa unaendelea kuzorota 
    sana. Bibi, unaweza kunielezea kwa nini mtoto wako hufanya kinyume na 
    wenzake?
    Bibi: Ushahidi ni kwamba sisi wazazi ndisi tuliokuwa chanzo cha matatizo 
    haya yote. Kulingana na shughuli za kimaisha, tulidharau fursa ya kumchunga 
    mwanetu na kuongea naye kila siku. Maana yake tulisahau jukumu letu 
    kama wazazi. Kwa hiyo, naomba msamaha. Toka leo nimeahidi kurekebisha 
    mienendo yetu na ya mtoto ili kuimarisha sura ya familia yetu.
    Mwalimu mkuu wa shule: Ahsante sana kwa uamuzi mzuri huu. Kwa 
    mujibu wa shule, tutashirikiana bega kwa bega kwa njia ya mawasiliano ya 
    kila siku. 
    Bibi: Asante sana kwa makubaliano haya. 
    Mwalimu mkuu wa shule: Kumbuka kuwa ahadi ni deni. 
    Bibi: Ndiyo, usijali yote yatatimizwa.
    Kazi ya 2:
    Jibu maswali ya ufahamu yafuatayo:
    1. Kifungu cha habari cha hapo juu kinazungumzia nini?
    2. Habari hii imetokea wapi?
    3. Kwa nini mzazi ameitwa shuleni?
    4. Ni makosa yapi yanayojitokeza katika kifungu cha habari?
    5. Ni makubaliano gani yaliyofikiwa kati ya wahusika wawili?
    6. “Harakati za maisha ya leo ni changamoto kubwa kwa elimu ya 
    watoto katika jamii.” Husisha maoni haya na kifungu cha habari.

    22.2. Matumizi ya msamiati
    Kazi ya 3:
    Kwa kutumia Kamusi ya Kiswahili Sanifu au njia nyingine tofauti, toa 
    maana ya msamiati ufuatao na kuutungia sentensi sahihi.
    a. Utovu wa nidhamu
    b. Kuja
    c. Kukiri 
    d. Kuzorota
    e. Chanzo
    f. Kuahidi
    g. Kurekebisha
    h. Kuimarisha
    i. Uamuzi
    j. Kushirikiana bega kwa bega

    Kazi ya 4:
    Jaza nafasi iliyoachwa wazi kwa kutumia msamiati unaofaa kutoka 
    kifungu cha habari

    i. ............. kosa ni njia ya kusamehewa.
    ii. Ukosefu wa mwenendo mzuri ni ..........................cha kushindwa 
    masomo shuleni.
    iii. Ni lazima kuepuka vita kwa sababu bila usalama amani na utulivu 
    ..................................
    iv. Tunaombwa .....................tabia mbaya ili tujenge jamii nzuri.
    v. Tumechukua ................huu shuleni kwa ajili ya kugombana dhidi 
    ya uvivu miongoni mwa wanafunzi

    Kazi ya 5:

    Toa kinyume cha msamiati ufuatao
    a. Kumkaribisha mtu
    b. Utovu wa nidhamu
    c. Kushirikiana bega kwa bega
    d. Kuzungumza
    e. Kuheshimu
    22.3. Sarufi: Matumizi ya “nini”, “nani” na “lini’ katika 
    kuuliza maswali

    Kazi ya 6:
    Soma sentensi zifuatazo na kuzungumzia matumizi ya maneno 
    yaliyopigiwa mstar
    i
    i. Jina lako ni nani?
    ii. Kifungu cha habari kinazungumzia nini?
    iii. Nchi yetu ilijinyakulia uhuru lini?
    Maelezo muhimu
    Maneno yaliyopigiwa mstari huitwa viulizi, yaani maneno yanayotumiwa 
    kuulizia swali. 
    Viulizi huweza kutumiwa mwanzoni mwa sentensi au mwishoni mwake.
    Kwa mfano:
    Nani amepiga hodi?
    • Umesema bwana huyo anaitwa nani?
    Matumizi maalum ya viulizi
    a. Nani
    Neno hili hutumiwa kuulizia mtu, Mwenyezi Mungu, mnyama, ndege au 
    wadudu.

    Mfano:

    • Nani amezungumziwa hapa?
    • Jina lake ni nani?
    • Nani aliyeumba binadamu?
    • Baadhi ya sungura na fisi, nani mjanja kuliko mwingine?
    b. Nini
    Hutumiwa kwa kuulizia kitu.
    Mfano: Mmejifunza nini leo?
    c. Lini
    Neno hili hutumiwa kuuliza majira, kipindi cha muda (tarehe au mwaka)
    Mfano: Ulizaliwa lini?
     Wageni wako waliwasili nyumbani lini?
    Kazi ya 7:
    Uliza swali linalofaa kwa kila sentensi kulingana na maneno 
    yaliyopigiwa mstari
    a. Shule yetu ilijengwa miaka thelathini iliyopita.
    b. Ukosefu wa usafi huweza kusababisha magonjwa.

    c. Mgeni amewasili nyumbani.

    22.4. Matumizi ya lugha: Mazungumzo na uigizaji wake
    Kazi ya 8:
    Kwa kuzingatia mfano wa mazungumzo hapo juu, eleza maana ya 
    neno ‘mazungumzo’ pamoja na aina zake.

    Maelezo muhimu ya kuzingatia
    Maana ya mazungumzo

    Mazungumzo au dayolojia ni utanzu mojawapo wa fasihi simulizi. Ni utaratibu 
    wa kuongea baina ya watu wawili au miongoni mwa watu zaidi ya mmoja au 
    pande mbili tofauti kuhusu mada mbalimbali zinazobadilikabadilika. 
    Baadhi ya vipera vya mazungumzo, vipera vitatu vifuatavyo ndivyo 
    vinavyojulikana na kutumiwa sana. 
    Malumbano ya utani: Ni mashindano ya kuongea jukwaani baina ya watu 
    wa makundi au jamii mbili ambayo hutumia kejeli na chuku kukejeli tabia 
    mbaya katika jamii au kundi fulani. Watu husimama jukwaani na kushindana 
    kwa maneno. Mazungumzo haya hutumia mzaha na vichekesho pamoja na 
    kejeli ili kuangazia ukweli fulani katika jamii.
    Ulumbi: Ni uwezo wa kipekee wa kuzungumza mbele ya hadhira. Mtu 
    mwenye uwezo huo wa kipekee wa kuzungumza jukwaani huitwa mlumbi. 
    Walumbi husifika sana kwa kuzungumzia mambo yanayoathiri jamii.
    Soga: Ni mazungumzo baina ya watu wawili au zaidi ambayo aghalabu huwa 
    hayana mada maalum. Aghalabu soga huwa na vichekesho vingi, mzaha 
    na kejeli. Nia yake huwa kuburudisha na kupitisha wakati. Soga huwa na 
    vichekesho na mzaha mwingi. Mada hubadilikabadilika kutoka wakati mmoja 
    hadi mwingine. Haihitaji taaluma yoyote ya kisanaa na inaweza kufanyika 
    pahali popote - njiani, sebuleni, katika vyumba vya burudani, n.k. 
    22.5. Kusikiliza na kuzungumza
    Kazi ya 9
    Sikiliza mazungumzo kutoka video zifuatazo na kusimulia mbele ya 
    darasa mambo yafuatayo:

    https=//
    https=//
    a. Dhamira kuu iliyozungumziwa
    b. Maudhui
    Kazi ya 10
    Kwa kushirikiana na wenzako, igiza mazungumzo kati ya mwalimu 
    mkuu wa shule na mzazi wa mwanafunzi

    22.6. Kuandika
    Kazi ya11:
    Buni mazungumzo (yenye ukurasa mmoja) kati ya mwalimu na mwanafunzi.

    Kazi ya12:

     Tunga sentensi sita kwa kuzingatia viulizi “nani” na “nini”.

    SOMO LA 23: UMUHIMU WA UIGIZAJI WA MAZUNGUMZO

    Kazi ya1:
    Unaona nini kwenye mchoro huu? 
    23.1. Kusoma na ufahamu: Tujivunie lugha yetu
    Kamana na Zaninka ni wanafunzi wanaosomea darasa moja kwenye Shule 
    ya Sekondari ya Tarubwenge. Wanazungumzia faida za kujizoeza uigizaji 
    wa mazungumzo kama mojawapo ya njia za kupata weledi na umahiri wa 
    lugha fulani.
    Kamana: Dada, unakumbuka jinsi tulivyokuwa miaka mitatu iliyopita?
    Zaninka: Unataka kumaanisha nini? Unadhani nilihifadhi matukio yote 
    katika miezi thelathini na sita yote?
    Kamana: Nimetaka kuzungumzia mchakato wa kukuza ujuzi wetu katika 
    stadi nne za lugha ya Kiswahili.

    Zaninka: Aa! Kuna mambo tele ya kuongea kuhusu mafanikio tuliyonayo

    Kamana: Kiwango cha matumizi ya Kiswahili leo ni cha juu mithili ya 
    Waswahili wenyewe.
    Zaninka: Acha! Haya ni majivuno! Nakubali tumepiga hatua kubwa lakini 
    hatujashindana na wale wakazi wa pwani.
    Kamana: Mimi nina ushahidi mkubwa sana. 

    Zaninka: Ushahidi wako unautoa wapi? 
    Kamana: Weledi wangu katika kuizungumza kwa ufasaha lugha ya Kiswahili 

    ulitokana na mazoezi darasani kwa kuigiza mazungumzo mbalimbali. 
    Zaninka: Si hayo tu. Kwa nini huzungumzii faida nyingine?
    Kamana: Kwa mfano?
    Zaninka: Kama kujiamini katika masimulizi hadharani.

    Kamana: Huo ni ukweli mtupu. Wiki iliyopita niliingia katika mashindano ya 
    mdahalo pamoja na wanafunzi kutoka shule tofauti za mjini ambao nilikuwa 
    ninawaogopa kulingana na tajriba yao ya kuitumia lugha ya Kiswahili kwa 
    ufasaha.
    Zaninka: Matokeo ya mashindano yalikuwaje?
    Kamana:Bila shaka nilijinyakulia ushindi na kutunukiwa kombe la almasi!
    Zaninka: Mimi nimeishafanya maajabu kijijini kwetu! Wakati wa sherehe 
    mbalimbali watu hunialika kwa ajili ya kuwaburudisha kupitia uigizaji wa 
    mazungumzo. Mwishowe hunipatia zawadi ya pesa zaidi ya elfu kumi. 

    Kamana: Hatuwezi kuorodhesha faida zote, ndiyo sababu tunapaswa 

    kujivunia lugha yetu tukufu.

    Kazi ya 2:
    Jibu maswali ya ufahamu yafuatayo:
    1. Kifungu cha habari kinazungumzia nini?
    2. Ni wahusika gani wanaozungumziwa kifunguni?
    3. Mafanikio ya wanafunzi hawa yalisababishwa na nini?
    4. Je, majivuno ya wanafunzi hawa yana sababu ya kuwepo? Eleza.

    23.2. Matumizi ya msamiati

    Kazi ya3:
    Kwa kutumia kamusi ya Kiswahili sanifu au njia nyingine uzipendazo, 
    toa maana ya msamiati ufuatao:
    a. Kujivunia
    b. Mchakato
    c. Tele 
    d. Mafanikio
    e. Kujiamini
    Kazi ya4:
    Jaza nafasi iliyoachwa wazi kwa kutumia msamiati huu: majivuno, pwani, ushahidi, tajriba, kujinyakulia
    i. Zaninka na Kamana wametoa..............................kwamba uigizaji 
    wa mazungumzo ulikuwa chanzo cha mafanikio yao.
    ii. Inahakikishwa kuwa asili ya Kiswali ni sehemu za................... au 
    mwambao wote wa Afrika Mashariki.
    iii. .......................ni tabia ya kujisikia bora kuliko wengine; maringo.
    iv. Baada ya kuishambulia timu B, timu A iliweza .........................ushindi wa mabao mawili kwa nunge.
    23.3. Sarufi: Matumizi ya “nini”, “wapi” na “kwa nini’ katika kuuliza maswali
    Kazi ya 5:
    Soma sentensi zifuatazo na kuzungumzia matumizi ya maneno yaliyopigiwa mstari
    i. Je, miti itapandwa wapi?
    ii. Kwa nini vijana hawajaelewa hasara ya kutumia dawa za kulevya?

     Maelezo muhimu

    a. Wapi
    Tunatumia neno hili kuulizia mahali au sehemu fulani
    Mfano: Unaishi wapi? ; Umesema uliniona juzi. Je, uliniona wapi?
    Tanbihi: Matumizi ya neno ‘pahali’, kiulizi ‘wapi’ hugeuka ‘papi’
    Mfano: Pahali papi panapotembelewa sana nchini humu?
    b. Kwa nini/ mbona
    Kiulizi hiki hutumiwa kuulizia sababu.
    Mfano: Kwa nini/ mbona mmechelewa kufika shuleni?
    c. Namna gani
    Neno hili hutumiwa kuulizia namna au jinsi jambo lilivyotendeka
    Kwa mfano:
    Mlifanya kazi hii namna gani?
    Kazi ya 6:
    Toa swali sahihi kutegemea maneno au kundi la maneno yaliyopigiwa mstari
    i. Sokwe mtu hupatikana katika mbuga ya wanyama iliyoko kaskazini 
    mwa Rwanda.
    ii. Taka zote hutupwa jalalani.
    iii. Hali ya hewa ilikuwa nzuri mwaka huu kwani raia walipanda miti 
    pahali pengi.
    iv. Mauaji ya kimbari dhidi ya Watutsi yaliwezekana nchini Rwanda 
    kwa sababu ya itikadi ya ubaguzi wa kikabila iliyofundishwa miaka mingi.

    23.4. Matumizi ya lugha: Mazungumzo na uigizaji wake
    Kazi ya 7:

     Jadili maswali yafuatayo:
    a. Nini maana ya uigizaji wa mazungumzo?
    b. Uigizaji wa mazungumzo una umuhimu gani?
    Maelezo muhimu
    a. Kuigiza mazungumzo ni nini?
    Ni kuyakariri mazungumzo yaliyosimuliwa na mtu mwingine na kuyarudia 
    kwa kumwiga mtu huyo kimatendo kwa njia au namna ya mchezo; yaani 
    kuvaa uhalisia wa mtu huyo. Ni karibu na maigizo au michezo ya kuigiza.

    b. Umuhimu wa kuigiza mazungumzo
    • Huunganisha watu katika jamii
    • Hutumiwa kama chombo cha kuburudisha katika jamii.
    • Vilevile huelimisha kuhusu mambo fulani
    • Pia huleta umoja na utangamano
    • Hutumiwa kuonya dhidi ya matendo mabaya.
    • Hutumiwa kupitisha wakati.
    • Hukuza stadi za kuzungumza lugha kwa ufasaha
    23.5. Kusikiliza na kuzungumza
    Kazi ya 8:
    Kwa ushirikiano na wenzako, igiza mazungumzo kati ya Zaninka na 
    Kamana.
    23.6. Kuandika
    Kazi ya 9:
    Buni kifungu cha habari kwa kutilia mkazo juu ya umuhimu wa 
    uigizaji wa mazungumzo
    Kazi ya 10:
     Tunga sentensi nne kwa kutumia viulizi ‘’wapi’’ na ‘’kwa nini’’.

    SOMO LA 24: VIFAA KATIKA UIGIZAJI WA MAZUNGUMZO

    vv

    Kazi ya 1:
    Unaona nini kwenye mchoro huu? 
    24.1. Kusoma na ufahamu: Majukumu yetu katika uigizaji wa mazungumzo
    Egide na Liliane ni wanafunzi wanaosomea kidato kimoja kwenye Shule 
    ya Sekondari ya Mazungumzo. Wanazungumzia vifaa vinavyowasaidia 

    katika uigizaji wa mazungumzo pamoja na sifa za mwigizaji bora

    Egide: Liliane, unayakumbuka mashindano tutakayoshuhudia wiki ijayo?
    Liliane: Bila shaka nayakumbuka na nilazima tuanze maandalizi yake
    Egide: Hayo ni kweli. Je, ni vifaa gani tutakavyohitaji ili tuliambulie kombe?
    Liliane: Baadhi ya vifaa muhimu ni lazima kuwepo na simu ya mkononi, 
    kofia, aina tofauti za pesa, chupa, tarumbeta, n.k.
    Egide: Usisahau aina za mavazi mbalimbali kama suti, kimono, tarubushi 
    pamoja na bombo.
    Liliane: Aa! Hatukutaja vuvuzela, barakoa za ucheshi, mkongojo pamoja na 
    miwani.
    Egide: Asante sana kwa nyongeza. Sasa ni wakati wa kuzungumzia sifa 
    zinazofaa kwa kila mwigizaji wa mazungumzo.
    Liliane: Hizo ni mboga! Kwanza, mwigizaji bora ni lazima ajiamini katika 
    mazungumzo yake.
     Pili, anapaswa kutumia lugha ya ishara kama vile kusugua mikono, kutikisa 
    kichwa, kugusa pua, kupiga vidole, kuinua nyushi, n.k. 
    Tatu, kuwa na ucheshi wa kutosha
    Nne, kutumia vihisishi ili kufanya mazungumzo yawe ya kusisimua.
    Egide: Si hayo tu, sifa zifuatazo sharti zizingatiwe pia:
                    Kutumia matamshi au lafudhi bora
                    Kuzungumza kwa ufasaha Kuonyesha moyo wenye huruma
                   Kuwa na mazungumzo ya mkato na yasiyozidiana sana kati ya 
                   wahusika. Mhusika mmoja asitawale mazungumzo kupita wengine.
    Liliane: Naam! Egide, tujipigie makofi kabisa! Ushindi ni wetu bila shaka.
    Egide: Lakini kumbuka lililosemwa na wahenga kwamba chelewa chelewa utamkuta mtoto si wako.
    Liliane: Usijali kaka yangu! Nimekupata wazi, ni lazima maandalizi yaanze leo bila kungoja kesho. 
    Egide: Naam, liwezekanalo leo lisingoje kesho.

    Maswali ya ufahamu

    Kazi ya 2:
    Jibu maswali ya ufahamu yafuatayo:
    1. Kifungu cha habari kinazungumzia nini?
    2. Ni wahusika gani wanaozungumza?
    3. Ni vifaa gani vilivyotajwa?
    4. Onyesha angalau sifa tatu muhimu anazostahili mwigizaji bora.
    5. Bila shaka wanafunzi hawa watajinyakulia ushindi. Tetea ukweli 
    huu kulingana na ushahidi kutoka mazungumzo.
    24.2. Matumizi ya msamiati
    Kazi ya 3:

    Kwa kutumia Kamusi ya Kiswahili Sanifu au njia nyingine tofauti, toa 
    maana ya msamiati ufuatao na kuutungia sentensi sahihi.
    a. Kombe
    b. Kujali
    c. Maandalizi
    d. Mkongojo
    e. Ucheshi
    f. Kimono
    g. Tarubushi
    h. Bombo
    i. Barakoa

    Kazi ya 4:
    Oanisha michoro hii na majina yake, kisha eleza umuhimu wa kila 
    aina: tarumbeta, vuvuzela, suti, miwani, barakoa.
    vv

    cc


    24.3. Sarufi: Matumizi ya “gani” na “-ngapi’ katika kuuliza maswali
    Kazi ya 5:
    Soma sentensi zifuatazo na kuzungumzia matumizi ya maneno yaliyopigiwa mstari 
    i. Swali gani ambalo halikutolewa jibu?
    ii. Miti mingapi mliyoipanda nyumbani kwenu?
    Maelezo muhimu
    a. Gani
    Neno hili hutumiwa kuulizia aina ya mtu au vitu.
    Mfano: Tatizo gani linalojitokeza hapa?
    Tanbihi: 
    1. Kiulizi gani huweza kuwakilishwa na kiwakilishi -pi
    Mfano: 
    • Tatizo lipi ambalo halijatatuliwa?
    • Vitambulisho vipi vinavyotakiwa kwa kila mwanafunzi?
    • Darasani mpi mnapatikana uchafu?
    2. Viulizi mbalimbali huweza kuchukua nafasi ya viwakilishi viulizi.
    Mfano:
    Zipi zimenunuliwa?
    Papi pamesafishwa?
    • Mpi mmesafishwa?
    b. -ngapi
    Hiki ni kiulizi cha kuulizia idadi ya watu au vitu.
    Kwa mfano:
    • Ng’ombe wangapi walitolewa kwa raia kwa ajili ya kujitegemea? 
    • Ni wanafunzi wangapi wanaoomba mahitaji maalum ya ujifunzaji?
    Tanbihi: Kiulizi hiki huweza kuchukua nafasi ya viwakilishi viulizi.

    Mfano: Vingapi vinahitajika?

    Kazi ya 6:
    Toa swali sahihi kulingana na maneno au kundi la maneno 
    linalopigiwa mstari
    i. Tumetumia vifaa vya aina nyingi katika maigizo yetu
    ii. Sabuni kadhaa zimewekwa nje ya choo kwa ajili ya usafi.
    iii. Wanafunzi kumi wamezawadiwa kwa sababu ya kuimarisha amani 
    na umoja darasani mwao.

    iv. Mwigizaji bora anapaswa kuwa na sifa kama vile kujiamini, 
    kuzungumza kwa ufasaha, kuzungumza kwa kutoa sauti, n.k.
    24.4. Matumizi ya lugha
    Kazi ya 7:
    Jadili mada zifuatazo:
    a. Umuhimu wa uigizaji wa mazungumzo
    b. Wahusika wanaoshiriki katika uigizaji wa mazungumzo
    c. Maigizo na aina zake
    Maelezo muhimu
    a. Kuigiza mazungumzo ni nini?

    Ni kuyakariri mazungumzo yaliyosimuliwa na mtu mwingine na kuyarudia 
    kwa kumwiga mtu huyo kimatendo kwa njia au namna ya mchezo; yaani, 
    kuvaa uhalisia wa mtu huyo. Ni karibu sawa na maigizo au michezo ya 
    kuigiza
    b. Wahusika katika uigizaji wa mazungumzo

    Kwa kawaida wahusika huwa ni binadamu. Wahusika ndio wanaozungumza 
    katika sehemu zao mbalimbali. Kulingana na aina ya mazungumzo, wahusika 
    wanaweza kuwa wawili au zaidi. Katika uigizaji wa mazungumzo, majukumu 
    ya watu wa marika au viwango mbalimbali huigizwa kama vile wazee, rais, 
    waziri, askari jeshi, mbunge, mwalimu, mfanyabiashara, mfalme, daktari, 
    hakimu, n.k.
    Maigizo ni sanaa katika fasihi simulizi ambayo watendaji huwa ndio wahusika. 
    Maigizo hayasimuliwi kama mbinu nyingine za fasihi. Wahusika ndio 
    huzungumza katika sehemu zao mbalimbali. Ifuatayo ni mifano ya maigizo.
    1. Michezo ya kuigiza ( agh. huletwa jukwaani): Haya ni maigizo ya 
    jukwaani ambapo watendaji huiga maneno na matendo ya wahusika 
    mbele ya hadhira.
    2. Miviga: Sherehe mbalimbali katika jamii fulani. Watu hujumuika na 
    sherehe hizi kulingana na tamaduni zao
    3. Ngomezi: Ni sanaa ya ngoma. Midundo mbalimbali ya ngoma 
    hutumika kuwasilisha jumbe mbalimbali.
    4. Malumbano ya utani: Mashindano ya kuongea jukwaani baina ya 
    watu wa makundi au jamii mbili ambayo hutumia kejeli na chuku 
    kukejeli tabia mbaya katika jamii au kundi fulani
    5. Ulumbi: Uwezo wa kipekee wa kuzungumza mbele ya hadhira. Mtu 
    mwenye uwezo huo wa kipekee wa kuzungumza jukwaani huitwa 
    mlumbi.
    6. Soga : Mazungumzo baina ya watu wawili au zaidi ambayo aghalabu 
    huwa hayana mada maalum.
    7. Vichekesho: Aina ya sanaa ya fasihi simulizi ambayo watu hutoa 
    vihadithi vifupi au sentensi zenye uwezo wa kuwafanya wasikilizaji 
    wacheke.
    8. Maonyesho ya sanaa: Maonyesho huhusisha watu wa jamii au kundi 
    fulani wanaoonesha taaluma, ujuzi au sanaa yao kwa watazamaji.
    24.5. Kusikiliza na kuzungumza
    Kazi ya 8:
    Kwa ushirikiano na wenzako, igiza mazungumzo kati ya Egide na Liliane.
    24.6. Kuandika
    Kazi ya 9:
    Buni kifungu cha habari ambapo vifaa tofauti pamoja na sifa 
    mbalimbali zimeonekana kwa wahusika wanaoigiza mazungumzo.
    Kazi ya 10:
    Tunga sentensi nne kwa kutumia viulizi “gani” na “-ngapi”.
    Tathmini ya mada
    1. Taja aina tatu za mazungumzo na kuzieleza
    2. Nini umuhimu wa uigizaji wa mazungumzo?
    3. Mwigizaji wa mazunguzo anastahili kuwa na sifa gani? Toa angalau tano
    4. Kwa kutegemea mifano mitatu, onyesha mandhari au pahali panapoweza kuigiziwa mazungumzo.
    5. Toa maswali sahihi kwa sentensi zifuatazo:
    i. Barabara hii ilijengwa kabla ya Wazungu kufika nchini humu.
    ii. Mtoto wangu hakuweza kufika shuleni jana kwani alikuwa mgonjwa.
    iii. Tunakuja shuleni kwa miguu.
    iv. Maswali kumi yametolewa na washiriki.
    v. Wazazi pamoja na walimu ndio watu muhimu katika jitihada za kuimarisha elimu bora.
    vi. Mgeni amepiga hodi.












  • MADA YA 7 UTUNGAJI WA INSHA

    Uwezo mahususi wa mada : Kutunga insha fupifupi kwa kuzingatia kanuni 
    za utungaji na masimulizi.
    Malengo ya ujifunzaji:
    • Kueleza maana ya insha,
    • Kutofautisha aina za insha,
    • Kujadili umuhimu wa insha,
    • Kutunga insha kwa kuzingatia kanuni za utungaji wa insha, 

    • Kutumia kwa usahihi alama za vituo husika.

    Kidokezo
    Zungumzia aina mbalimbali za maandishi au masimulizi unazozijua.
    SOMO LA 25: DHANA YA INSHA 

    25.1. Kusoma na ufahamu: Mchuano wa fainali

    cc

    Wiki iliyopita nilibahatika kutazama mchuano wa fainali ya kuwania kombe 
    la Agaciro kati ya shule ya wasichana ya Elimu Bora na Tusonge Mbele

    kwenye uwanja wa michezo Amahoro. 

    Nilipofika nyumbani, wazazi wangu waliniuliza kwa mapana na marefu 
    kuhusu mchezo huo kwa sababu mmoja kati ya wachezaji ni dada yangu, 
    jina lake Umutesi Marie Alice.
     

    Nilianza kuelezea wazazi kwanza historia ya timu hizo. Timu hizi mbili ni 
    wapinzani sugu tangu jadi na jadi. Elimu Bora inajivunia historia nzuri kwa 
    kushinda kombe hili mara kumi. Wao ndio mabingwa watetezi. Tusonge 
    Mbele imeshinda kombe hili mara tatu. Mwaka jana walitimuliwa katika nusu 
    fainali. Katika awamu hii, wana rekodi ya kutoshindwa katika mechi zote 
    hadi kufikia fainali.

    Timu zote mbili ziliingia uwanjani tayari kwa mapambano. Kwa ufupi, kila timu 
    ilikuwa na golikipa mmoja. Elimu Bora waliweka wachezaji watatu katika safu 
    ya ulinzi wao Wakati ambapo tusone mbele walichezesha wachezaji wanne 
    katika safu hiyo hiyo. Timu ya Elimu Bora walitia wachezaji watano katika 
    kiungo cha kati nao Tusonge Mbele waliwachezesha wachezaji watatu. 
    Elimu Bora walikuwa na washambulizi wawili nao wakati ambapo tusonge 
    mbere walikuwa na washambulizi watatu katika safu ya mashambulizi. 
    Timu zote mbili zilikuwa na wachezaji wa akiba watano. Refa mkuu alipuliza 
    kipenga nao wasaidizi wake wawili walikimbia pembeni mwa uwanja kuinua 
    kijibendera. Mmoja alikimbia kushoto naye mwingine alikimbia kulia. 

    Manahodha wa timu zote mbili walisimama katikati ya uwanja kurusha sarafu 
    ili kuamua timu inayoanzisha mpira. Mashabiki wa timu zote mbili walikuwa 
    wanaimba nyimbo za kushangilia timu zao. Makochi wao walikaa pembeni 
    mwa uwanja kushuhudia wasichana wao wakimenyana. 

    Naam, refa alipuliza kipenga. Mpira ulianzishwa pale na Ikirezi na Umutesi 
    Marie Alice wa timu ya Elimu Bora. Elimu Bora walianza mchuano huo 
    kwa kasi mno. Walitafuta bao la mapema. Tusonge Mbele nao walifanya 
    shambulizi la kujibu. Kipindi cha kwanza kilimalizika bila goli kwa timu zote. 

    Katika kipindi cha pili, kila timu ilicheza vizuri. Kwenye dakika ya sabini 
    kulikuwa hatari katika lango la Tusonge Mbele. Kayitesi alinawa mpira. 
    Naam, kipenga kilipulizwa. Refa aliwapa Elimu Bora penalti. Shangwe na 
    vifijo vikahanikiza huku na huko kutoka kwa mashabiki wa Elimu Bora. 
    Kayitesi alionyeshwa kadi ya manjano. Ikirezi alisimama nyuma ya mpira 
    ule tayari kufyatua mkwaju wa penalti. Kabatesi akaruka na kuupiga mpira 
    ule ukapitia juu ya mtambaapanya wa goli hadi nje. Ilikuwa konakiki.

    Konakiki hiyo ilipigwa na Umulisa. Uwamwiza alikimbilia mpira ule. Alipiga 
    kichwa! Hatimaye Elimu Bora walipata goli la kwanza. Mashabiki wote wa 
    Elimu Bora na makochi wao waliacha viti vyao huku wakijirusharusha kwa 

    nderemo kama kulungu. Mashabiki wa Tusonge Mbele waliviinamisha vichwa 

    vyao mithili ya kondoo. Wachezaji wa Tusonge Mbele walipandwa na mori 
    kwa goli walilofungwa. Walimzingira refa mkuu. Walidai kuwa Uwamwiza 
    alikuwa ameotea. Nahodha wao, Mutoni, ambaye ni beki wa kupanda na 
    kushuka alimiminia refa maneno makali. Refa alitia mkono katika mfuko wa 
    nyuma ya kaptula na kuchomoa kadi nyekundu. Mutoni alionyeshwa kadi 
    nyekundu kwa kukosa adabu. Alisindikizwa nje ya uwanja. Timu ya Tusonge 
    Mbele walibaki na wachezaji kumi pekee. 

    Mchezo ulimalizika ikiwa ni goli moja la Elimu Bora kwa bila. 

    Kazi ya 1:
    Maswali ya ufahamu
    1. Timu hizi mbili ni zipi?
    2. Timu hizo mbili zinagombania kombe gani?
    3. Timu hizo zilikuwa marafiki? Eleza.
    4. Historia ya timu hizo ilikuwa namna gani katika mchezo wa 
    kandanda?
    5. Mchezo ulimalizika vyema? Eleza. 
    6. Kwa sababu gani wazazi walitaka kusikiliza matokeo ya mchezo huo?
    7. Kwa sababu gani Mutoni alipewa kadi nyekundu?
    8. Kwa maoni yako, michezo ina umuhimu gani?
    9. Ni vizuri kwa wasichana kucheza mchezo wa kandanda?
    25.2. Matumizi ya msamiati kuhusu kifungu cha habari
    Kazi ya 2:
    Eleza maana ya maneno yafuatayo kutoka katika kifungu cha habari 
    ulichokisoma hapo juu kuhusu “Mchuano wa fainali”
    Kabumbu 
    Mchuano 
    Fainali
    Kuwania kombe 
    Wapinzani 
    Bingwa tetezi
    Nusu fainali
    Safu ya ulinzi 
    Kiungo cha kati 
    Washambulizi
    Kazi ya 3:
    Kamilisha sentensi kwa kutumia maneno yanayofaa kati ya haya 
    yafuatayo: kabumbu, mchuano, fainali, kuwania kombe, washambulizi, 
    kuinua kijibendela, mabingwa watetezi, refa, mashabiki, penalti. 
    1. Elimu Bora ndiyo …………… kwa sababu walishinda mara 
    nyingi.
    2. ………anachomoa kadi nyekundu na kumuonyesha Mutoni. 
    3. Kulikuwepo mashabiki wengi katika mchezo wa …………..la 
    Agaciro nchini Rwanda
    4. ………….. ndio wanaofungia timu yao magoli mengi.
    5. Mara nyingi …………husababisha goli.
    6. Wasaidizi wa refa wanamsaidia katika mchezo kwa………………..
    7. Timu ya Arsenal ina ……….. wengi nchini Rwanda.
    8. Siku hizi wachezaji wa ………….hulipwa hela nyingi.
    9. Nchini Rwanda, …………wa APR FC na Rayon Sport unatazamwa 
    na watu wengi sana.
    10. Katika mchezo wa ………….kila timu hutakiwa kuwa bingwa.
    25.3. Sarufi: Matumizi ya herufi kubwa
    Kazi ya 4:

    Tazama herufi zinazopigiwa mstari na kueleza sababu ya kutumia 
    herufi kubwa
    a. Mjini Kigali panajulikana kuwa na usalama pamoja na usafi.
    b. Shule ya Mtakatifu Yohana inawapokea wasichana na wavulana.
    c. Jina lako ni nani? Ninaitwa Peter. Jina jingine ?
    Maelezo ya matumizi ya herufi kubwa 
    a. Hutumiwa kuanzishia sentensi: Tazama mfano ufuatao:
    Nilikuona jana. 
    b. Herufi kubwa hutumiwa mwanzoni mwa majina au nomino pekee 
    kama vile: majina ya watu, mahali, milima, mito, maziwa, nchi, 
    mabara, siku za wiki, miezi ya kalenda, sikukuu, dini mbalimali, 
    barabara, majina ya vitabu, visiwa, n.k.
    c. Hutumiwa kuandikia anwani: 
    Mfano: 
    JINSI YA KUPANDA MITI
    Kazi ya 5:

    Chunguza makosa ya kisarufi katika sentensi zifuatazo na 
    kuyasahihisha.
    1. musanze ni mji mkubwa.
    2. kalisa na uwineza ni wanafunzi wenye bidii.
    3. miti hutupatia kivuli cha kupumzikia.
    4. mwalimu anafundisha.
    5. berwa anacheza mpira. 
    25.4. Matumizi ya Lugha: Dhana ya insha na utungaji wake
    Kazi ya 6:
     Jadili maswali yafuatayo:
    a. Insha ni nini?
    b. Toa umuhimu wa kujifunza insha.
    c. Insha nzuri inastahili kuwa na sifa gani?
    d. Kifungu hiki cha habari ni cha aina gani ya insha ?
    Maelezo muhimu kuhusu insha
    Maana ya insha:
    Insha ni mtungo wa kinathari unaozungumzia suala au kusimulia kisa 
    fulani. Utungo huu huwa na urefu wa wastani. Kisa hicho au suala hilo 
    ndilo mada ya utungo huo. Insha hutumiwa kueleza maoni ya mwandishi 
    kuhusu masuala au mambo tofauti. Utungaji ni neno linalotokana na kitenzi 
    “tunga”. Kitenzi hiki kwa mujibu wa Kamusi ya Kiswahili Sanifu (2004: 414) 
    kinamaanisha “Kutoa mawazo kutoka ubongoni na kuyakusanya, kisha 
    kuyadhihirisha kwa maandishi, kwa kusimulia, kwa kuyaimba au kwa 
    muziki.»
    Kwa hiyo, tunaweza kusema kuwa utungaji ni utoaji wa mawazo binafsi 
    kutoka akilini mwa mtu kuhusiana na mambo mbalimbali katika jamii, kisha 
    kuyaweka wazi kwa njia ya mdomo au maandishi. 
    Sehemu kuu za insha: Insha hugawika katika sehemu kuu tatu ambazo ni 
    pamoja na: 
    • Utangulizi (mwanzo) 
    Katika sehemu hii inampasa mwandishi/ mtungaji atoe maelezo mafupimafupi 
    na maana ya habari aliyopewa. 
    • Kiini cha insha (Kati au mwili) 
    Inamlazimu mwandishi afafanue kwa mapana na marefu mada 
    anayoishughulikia huku akitoa mifano hai inayoendana na hali halisi ya 
    maisha ya mtu kijamii. Kwa kawaida sehemu hii hueleza kwa ukamilifu kila 
    hoja iliyodokezwa katika utangulizi. 
    • Hitimisho na mwisho 
    Inampasa mwandishi kutoa mapendekezo (maoni) ya msingi au kusisitiza 
    kwa ufupi yale aliyoyaeleza katika habari yenyewe. Mwisho wa insha 
    huonesha uhusiano uliopo kati ya utangulizi na maelezo yaliyomo katika 
    mwili. 
    25.5. Kusikiliza na kuzungumza 
    Kazi ya 7:
    Fikiria juu ya insha moja uliyoisikiliza au kusoma na kuisimulia 
    mbele ya darasa
    176
    25.6. Kuandika: Utungaji wa insha
     
    Kazi ya 8:
    Kutokana na mfano wa insha uliotolewa hapo juu, andika insha
    kuhusu mada ifuatayo:
    “Umoja wa Afrika ni Msingi Muhimu kwa Maendeleo ya Afrika”

    SOMO LA 26: AINA ZA INSHA

    vv

                          cc

    b

    Kazi ya 1:
    Jadili michoro hii kwa kuelekea kwenye insha

    26.1. Kusoma na ufahamu: Usafi wa mavazi yetu

    ff

    Vazi ni nguo ya aina yoyote inayovaliwa mwilini. Binadamu huhitaji mavazi 
    kujikinga dhidi ya hali ya hewa ya aina mbalimbali. Wakati wa joto huhitaji 
    vazi jepesi na wakati wa baridi huhitaji vazi linaloweza kumtilia joto mwilini. 
    Hii ndiyo sababu wakati wa baridi watu hujifunika mavazi kama migolole, 
    makoti, makabuti, kaniki, vikoi, na sweta . 

     Mavazi ni pambo kwa binadamu. Vazi humfanya mtu aonekane maridadi na 
    apendeze zaidi. Labda, hii ndiyo sababu ya kuwepo kwa aina mbalimbali za 
    mavazi na mitindo tofauti inayomfanya mtu avutie.

    Mavazi huonesha utamaduni wa watu. Kusema kwamba mtu akivaa nguo 
    ya mtindo fulani mara nyingi utamaduni wake au asili yake hutambulika 
    waziwazi. Hata mtu awe mweupe anayetoka Ulaya au Marekani, akivaa 
    mgolole, kanga, kitenge, atakuwa akiiga vazi la utamaduni wa Afrika kwa 
    ujumla. Hadi leo, kuna mavazi unayoweza kusema kuwa ni ya Kichina, 
    Kihindi, Kiarabu, Kizungu, Kinyarwanda, Kiganda, Kimasai na kadhalika. 

    Tena mtu anaweza kuvaa nguo kwa mtindo wa aina fulani akafikiriwa kuwa ni 
    Mkongomani, Mganda, Mmasai, raia kutoka Afrika Magharibi na kadhalika. 
    Mavazi ni ya aina nyingi na mitindo tofauti. Lakini mavazi hayo yote huweza 
    kupangwa katika aina kuu tatu: mavazi ya kike, ya kiume na mavazi mahususi.

    Kwa upande wa kwanza, mavazi ya kike ni mavazi ambayo kwa kawaida

    huvaliwa na watu wa jinsia ya kike. Kuna mavazi au nguo za ndani, ambazo 
    huvaliwa na wanawake na hazipaswi kuonekana ovyo. Na hizo ni kama 
    chupi, fulana, sidiria na shimizi. 
    Tena, kuna nguo za nje ambazo ndizo zionekanazo mara nyingi. Hizo ni 
    kama sketi, blauzi, shati, jaketi, gauni, kanga, kaniki, kitenge, kaptula, suruali 
    na kadhalika.
    Kwa upande mwingine, wanaume nao huwa na nguo za staha yaani nguo 
    za ndani kama chupi na fulana. Pia, wana nguo zinazoonekana nje kama 
    kaptula, suruali, shati, koti, tai, suti, kanzu na kadhalika. 
    Zaidi ya hayo, kuna mavazi mahususi ambayo ni mavazi rasmi kwa ajili ya 
    shughuli maalum au kazi maalum. Mfano wa mavazi haya ni kama mavazi 
    ya viongozi wa kidini, masista, makasisi, mapadri na mashehe. Kundi la 
    aina hii huwa na nguo zao maalum kwa ajili ya kazi zao na pia huwasaidia 
    kujitambulisha kwa urahisi kwa umma au jamii. Baadhi ya nguo hizo ni kama 
    kasiki, joho, kanzu, kilemba na nguo zinazofanana na hizo. 
    Mfano mwingine ni mavazi rasmi kama ya askari jeshi, askari polisi, askari 
    magereza, wafanyakazi wa forodha, walinda usalama wa mashirika ya 
    kujitegemea, waganga na wauguzi, wafanyakazi wa mashirika ya ndege, 
    wachezaji na hata wanafunzi. Hawa wote wana mavazi yao rasmi kwa ajili 
    ya shughuli zao. Mtu akivaa nguo ya aina fulani, hujitokeza kuwa yeye ni 
    mtu wa namna fulani au kazi fulani. 

    Mavazi yetu yote ni lazima yawe na usafi. Usafi wa mavazi yetu ni muhimu 
    sana kwa sababu jambo hili husaidia mambo mengi maishani mwetu. 
    Kwanza tunaposafisha nguo zetu, tunajiepusha na magonjwa yanayotokana 
    na wadudu wanaoweza kuishi katika nguo chafu. 
    Wadudu hawa ni kama chawa, viroboto na kadhalika. 
    Nguo chafu hasa zile za ndani huweza kusababisha madhara katika sehemu 
    za uzazi na kuleta magonjwa mbalimbali kutokana na vidudu ambavyo 
    vinaweza kusababishwa na uchafu.
    Pili, mtu akiwa na nguo chafu hutoa harufu mbaya ambayo husumbua 
    wenzake wanapomsogelea. 

    Kwa ujumla, mavazi yetu ni ya aina nyingi na mitindo tofauti. Mavazi 
    haya yana umuhimu sana katika maisha yetu. Ndiyo maana tunalazimika 
    kuyatunza vizuri na kuyasafisha ili tuwe na usafi wa kutosha. Usafi huu 
    lazima uende bega kwa bega na usafi wa miili yetu. 
    (Kifungu hiki msingi wake ni kutoka: Ndalu A. (1997) Mwangaza wa Kiswahili, 

    East African Educational Publishers Ltd, Nairobi, Kenya.

    Kazi ya 2:
    Maswali ya Ufahamu: 
    1. Vazi ni nini ? 
    2. Kwa sababu gani vazi ni kifaa muhimu sana kwa binadamu? 
    3. Taja aina kuu tatu za mavazi. 
    4. Ni kwa namna gani vazi linavyoweza kutambulisha utamaduni wa 
    anayevaa vazi hilo? Eleza kwa kutoa mifano ya kutosha. 
    5. Taja mifano mitatu ya nguo mahususi. 
    6. Veli linaweza kutambulika kama vazi la aina gani miongoni mwa 
    aina za mavazi tulizotaja hapo juu? 
    7. Eleza jinsi ambavyo mavazi hutegemea sana utamaduni wa jamii husika? 
    8. Taja majina ya wadudu wanaoishi ndani ya mavazi machafu. 
    9. Kwa sababu gani nguo zilizofuliwa ni lazima zipigwe pasi baada 
    ya kukaushwa na jua? 
    10. Ni ushauri gani unaoweza kutoa kulingana na kifungu hiki?
    26.2. Msamiati kuhusu kifungu cha hatari
    Kazi ya 3:
    Tazama kwa makini jedwali hili. Bainisha msamiati mbalimbali na 

    kueleza maana yake. 

    vv

    Kazi ya 4:

    Unganisha msamiati kutoka sehemu A na maana yake kutoka sehemu B.

    xx

    26.3. Sarufi: Matumizi ya alama za vituo
    a. Matumizi ya nukta ( . )

    Kazi ya 5:
    Tazama sentensi zifuatazo na kuzungumzia matumizi ya alama 
    yanayojitokeza.

    i. Usafi ni muhimu sana kwa maisha ya binadamu. 
    ii. Kalisa alienda sokoni. Alikutana na rafiki yake sokoni.
    iii. Tunasoma ili tupate elimu.
    Maelezo muhimu 
    Nukta

    a. Huwekwa mwishoni mwa sentensi sahili sahihi. Kwa mfano
    i. Tunakula mboga kwa ajili ya afya nzuri
    ii. Inatubidi kusafisha mahali tunapoishi. 
    b. .Hutumiwa kuonyesha ufupisho wa maneno. Kwa mfano:
    i. S.L.P. – Sanduku la Posta
    ii. Bi. – Bibi
    182
    c. Hutumika kubainisha saa na dakika au tarehe. Kwa mfano:
    i. 3.20 – saa tisa na dakika ishirini
    ii. 14.5.2016- tarehe kumi na nne, mwezi wa tano, mwaka wa mbili elfu 
    kumi na sita
    d. Hutumiwa kuonyesha vipashio vya pesa. Kwa mfano:
     sh.10.50- shilingi kumi na thumuni hamsini
    e. Zikitumiwa mara tatu mfululizo (…) huonyesha kutokamilika kwa 
    sehemu husika
    Kwa mfano: Nitakupa lakini ni sharti...
    Kazi ya 6:
    Chunguza sentensi hizi na kusahihisha makosa ya kisarufi. 
    1. mwalimu anaandika ubaoni
    2. mifano ya ndege ni kv kuku, mwewe na bata
    3. tulianza mitihani yetu tarehe 12122017
    4. bi mutoni anaendesha gari
    5. wanafunzi wanasoma darasani
    b. Matumizi ya koma / mkato ( , )
    Kazi ya 7:
    Tazama sentensi zifuatazo na kuzungumzia matumizi ya alama 
    yanayojitokeza.

    1. Nimemkuta mzee, nikamwuliza shida zake, nikamsaidia kupata 
    gari la kumpeleka nyumbani.
    2. Tumekuja kwa ajili ya akili, si kwa ajili ya pesa.
    3. Baadhi ya maadili na thamani Mnyarwanda anatakiwa kuwa na zo 
    ni kama vile utu, unyarwanda, ushirikiano na ushujaa.
    Maelezo muhimu
     Mkato / koma
    a. Hutumiwa kuonyesha pa kutua kwa muda mfupi katika sentensi. 
    Kwa mfano: 
    ii. Nilipowasili nyumbani, nilienda kuteka maji kisimani. 
    iii. Kwa kuwa tulijiandaa vilivyo kwa mtihani wa kitaifa, tulipita. 
    b. Hutumiwa kutenga maneno yaliyo katika orodha: 
    i. Nenda sokoni ununue mboga, nyama, mafuta, na unga. 
    ii. Mwanafunzi huyu ni mtiifu, mwerevu, mtanashati, na mwenye bidii. 
    c. Hutumiwa kubainisha sehemu mbili za sentensi zilizo kinyume: 
    i. Umoja ni nguvu, utengano ni udhaifu. 
    ii. Aliniambia atakuja, hakuja. 
    d. Hutumiwa kabla ya alama za mtajo. 
    Kwa mfano:
    Mama akasema, “Niletee chumvi.” 
    e. Hutumiwa wakati sentensi inapoanza kwa kiunganishi. 
    Kwa mfano: 
    Kweli, alikuwa mtu mwovu. 
    f. Hutumiwa unapoita mtu ili kupata usikivu wake kabla hujamwambia 
    chochote. Kwa mfano: 
    Nkusi, niletee kalamu. 
    g.Hutumiwa unapokubali au unapokataa kitu. Mfano: 
    i. Ndiyo, nitakuja. 

    ii. Hapana, sitakulipa.

    Kazi ya 8:
    Sahihisha makosa ya kisarufi katika sentensi zifuatazo
    1. Baba alinunua daftari kalamu rula na kifutio
    2. Mama alipofika sokoni alinunua nanasi mkate chungwa na 
    parachichi
    3. Familia yetu ina watoto wafuatao: Kabanda Kabalisa na Mukandoli
    4. Mwalimu wetu anatufundisha masomo ya Kiswahili Kiingereza na 
    Historia
    5. Katika lugha ya Kiswahili kuna alama za uandishi kama vile: nukta 
    mkato alama ya kuuliza ….
     26.4. Matumizi ya lugha: Ainaza insha
    Kazi ya 9:
    Jibu maswali yafuatayo: 
    1. Kifungu “ Usafi wa mavazi” ni aina gani ya insha?
    2. Kifungu “Mchuano wa fainali” ni aina gani ya insha?
    Maelezo muhimu kuhusu aina za insha 
    Insha ni za aina nyingi kulingana na namna zilivyoandikwa au kufuatana na 
    kusudi lake. Katika utungaji wa insha kuna :
    1. Insha za wasifu 
    Insha za wasifu ni aina ya utungaji ambao huchora picha ya kitu 
    kinachozungumziwa. Huonyesha waziwazi hisia za msanii. Aghalabu, kuna 
    vitu vingi ambavyo tunaviona kila siku kama vya kawaida lakini mtungaji 
    anaweza akavitungia insha za wasifu na tukaviona katika mtazamo tofauti 
    kabisa. Katika insha za wasifu kuna usanii wa kueleza sifa za mtu, mahali 
    au kitu fulani. 
    2. Insha ya mjadala au ya mdahalo 
    Inalenga mara nyingi kulieleza jambo na vile vile kuhimiza mtazamo fulani. 
    Hata hivyo, jambo lililo muhimu zaidi si kueleza bali ni kujibidiisha kushawishi. 
    Katika mdahalo shawishi, mwandishi hulenga katika kuathiri hisia na maoni 
    ya msomaji kwa njia ya kumfanya achukue hatua. Insha hii huhusisha mada 
    ambayo mwanafunzi anapaswa kuitetea au kuipinga katika kisa chake. Hoja 
    nyingi na nzito hutolewa kwenye upande anaounga mkono. 

    3. Insha fafanuzi 
    Katika aina hii ya insha, mwandishi hutumia mifano kufafanua au kutilia 
    mkazo hoja yake. Anaweza kutumia mfano mmoja wenye uzito au mifano 
    mingi yenye kuhusiana. 
    Mfano: Rushwa imepigwa marufuku nchini Rwanda. 
    4. Insha ya methali 
    Insha ya methali ni utungo unaoandikwa kwa kuzingatia methali. Kisa au 
    maelezo yatolewayo huwa yanaongozwa na maana iliyomo katika methali 
    husika. Kabla ya kuanza kuandika insha, ni bora kwanza kuielewa vyema 
    maana ya methali au maudhui yake. Mbali na kufahamu maana ya kijuujuu 
    ya methali, inambidi mtunzi wa insha kuelewa mazingira (miktadha mingine 
    ambapo methali husika inaweza kutumiwa). Kwa mfano: Akili ni nywele kila 
    mtu ana zake. Hapa, anayetunga insha hii lazima aeleze maana ya juu na 
    ya ndani ya methali. Pia, msamiati uliotumiwa hufafanuliwa.
    5. Insha ya mdokezo 
    Insha ya mdokezo ni aina ya utungo ambao huandikwa kwa kuongozwa 
    na maneno aliyopewa mtunzi wake. Maneno hayo yaliyotolewa ndiyo 
    mwongozo wa kumwelekeza mwandishi kuhusu maudhui atakayoandika. 
    Lililo muhimu ni kuhakikisha kuwa mtungo utakaoandikwa unaoana vizuri na 
    maneno yaliyotolewa kama mwongozo. 
    Mfano: Nilipofika katika eneo la tukio hilo, sikuamini niliyoyaona ………………
    Hapa, unaweza kuendeleza kidokezi hiki kwa kukitungia kisa mwafaka. 
    6. Insha za picha 
    Insha za picha ni zile ambazo msingi wake wa kuzitunga ni picha ambazo 
    huwa zimechorwa na ambazo humwongoza mwandishi kubuni hadithi au 
    kisa kinachooana na picha hizo. Kimsingi, huhitaji ufasiri wa picha zilizo 
    kwenye ukurasa na kuibuni hadithi kuzihusu. 
    Hivyo basi huwa ni insha za kusimulia. 
    7. Insha ya mawazo au ya kubuni 
    Insha hizi zinahusu jambo la kufikiriwa. Jambo linalojadiliwa katika aina hii ya 
    insha huwa halitokani na hali au tukio halisi katika maisha. Vipengele vyote 
    vinavyoijenga hubuniwa na mtunzi wake. Maudhui, wahusika, mandhari vya 
    mtungo wa aina hii vyote hubuniwa katika fikra ya mtunzi. 

    8. Insha ya kitawasifu (Insha elezi/ ya maelezo) 
    Insha hii huwasilisha sifa za vitu, watu, hali, matendo, mahali au hata 
    sherehe uliyohudhuria. Inalenga kutoa picha ya kitu katika akili zetu jinsi 
    ambavyo kinamdhihirikia anayekiona. Ili kuandika insha ya maelezo, 
    mwandishi wake anahitaji kwanza kabisa kukusanya habari za kina kuhusu 
    jambo analoliandikia. Hategemei tu yale ambayo yanaonekana kwa macho 
    bali pia aina nyingine za hisi kama vile kugusa, kuonja, kunusa, kusikia na 
    kadhalika. Hali hii humwezesha msomaji kupata taswira kamilifu kuhusu 
    jambo linaloelezewa kupitia viungo vya kuona, kuonja, kugusa na kusikia. 
    9. Insha ya masimulizi 
    Insha ya masimulizi ni insha yenye kuhadhiria tukio au hali fulani. Ni utungo 
    ambao husimulia au kueleza kisa. Dhima yake ni kuburudisha au kuteka 
    umakini wa msomaji. Kwa kuwa inalenga hadhira ni muhimu kufahamu na 
    kuitambua hadhira yako kabla ya kuandika utungo wako
    26.5. Kusikiliza na kuzungumza 
    Kazi ya 10:
    Jadili mada zifuatazo
    1. Mavazi ya kigeni yana athari kubwa katika utamaduni wa 
    Wanyarwanda
    2. Matumizi ya mtumba (mavazi) huleta hasara kwa Wanyarwanda.
    26.6. Kuandika
    Kazi ya 11:
    Tunga insha ya wasifu unayotaka yenye ukurasa mmoja.

    SOMO LA 27: INSHA YA MASIMULIZI

    cc

    Kazi ya 1:
    Unaona nini kwenye mchoro hapa juu?
    27.1. Kusoma na ufahamu: Mafanikio ya kudumu 

    Ilikuwa tafrija ya kijiji kizima, tuliposherehekea siku ya kupata tuzo kwa kijana 
    hodari ambaye aliyamudu maisha yake kiasi cha kuigwa na vijana wengine. 
    Kabatesi, kijana aliyezaliwa mwanapekee katika familia yake hakubahatika 
    kulelewa na wazazi wake kwani walifariki angali mdogo akachukuliwa na 
    kulelewa na shangazi yake. 

    Alipomaliza masomo yake katika shule za sekondari, Kabatesi alipata cheti 
    cha kuhitimu masomo ya sekondari huku akiwa na alama nzuri. Jambo hili 
    liliwafurahisha watu wengi: walimu na majirani zake. Alikuwa mwanafunzi 
    mwenye bidii tangu shule za chekechea hadi kiwango alichofikia. Muda mfupi 
    baadaye, alijiunga na vijana wenzake kufuata masomo ya muda mfupi yaliyokuwa 
    yakitolewa kijijini mwake. Masomo hayo ni kuandaa miradi midogo midogo ya 
    kujiendeleza na jinsi ya kuifanikisha. 

    Alipokubaliwa kufuata mafunzo pamoja na vijana wengine alielewa kwamba hiyo 
    ilikuwa njia nzuri ya kupata suluhisho na ufumbuzi wa tatizo lililokuwa likimkera 
    kwa muda mrefu. Mafunzo yalifanyika kwa muda wa mwaka mzima, akapewa 
    cheti katika fani ya maandalizi na utekelezaji wa miradi ya kimaendeleo.

    Mwezi mmoja uliofuata, Bodi ya Maendeleo Rwanda ilihitaji kuajiri vijana 
    waliokuwa wamemaliza masomo yao katika mkondo wa lugha ili wasaidie katika 
    kazi za ukalimani na uongozaji wa watalii kwenye vivutio vya utalii. 
    Kabatesi alipeleka ombi lake na baada ya muda mfupi akaitwa kwa mtihani. Hili 
    lilikuwa jambo jepesi kwake kwani aliufaulu vizuri mtihani na hivyo akaajiriwa na 
    bodi hiyo. Alifanya kazi yake kwa bidii kiasi kwamba watalii wengi walifurahia 
    huduma yake, wakampenda kwa uwezo wake wa kuzungumza lugha nyingi 
    tofauti na bidii aliyoonesha kazini. 

    Kabatesi alifungua akaunti kwenye benki moja na kuanza kuhifadhi sehemu 
    ya mshahara wake. Kwa kweli, alikuwa msichana asiyekata tamaa na kila 
    aliposhikilia jambo alilifuatilia mpaka lilipokamilika. Kwa hivyo, alipoona akaunti 
    yake imeshakua na pesa za kutosha, aliamua kuomba mkopo ili aweze 
    kutekeleza mengi aliyokuwa amejifunza katika maandalizi na utekelezaji wa 
    miradi ya kimaendeleo. Mawazo yake yalikuwa kwenye shamba lake kubwa 
    aliloachiwa na wazazi ambalo mpaka wakati huo lilikuwa halijatumiwa vizuri. 
    Aliandaa vizuri mradi wa kilimo na ufugaji, akajenga vibanda vya mifugo yake, 
    akawaajiri baadhi ya vijana waliokuwa pamoja katika mafunzo ya muda ule 
    mfupi, kila mmoja akapewa jukumu lake. 

    Pamoja na kazi yake ya ukalimani, Kabatesi alifuata vizuri mradi wake 
    akanunua vifaa vilivyohitajika. Ninakumbuka kuwa mwaka jana, serikali yetu 
    ilipotoa tuzo kwa watu waliochangia kubadilisha maisha ya watu wengine, 
    Kabatesi alikuwa miongoni mwa watu waliochangia kuyaboresha maisha ya 
    majirani zake. Kwa sasa ameanza kuendelea na masomo yake katika Chuo 
    kikuu cha Rwanda. 

    Kabatesi amekuwa mfano mzuri kwa vijana wengine wengi ambao 
    wanayakumbuka maisha yake, huyaamini yaliyosemwa na wahenga 
    kwamba” Mchumia juani hulia kivulini” na “mvumilivu hula mbivu”. 

     Wema kwa kila mtu, utulivu na upendo ni baadhi ya sifa zinazomtambulisha 
    kijana huyu ambaye amewashangaza wengi wanaofahamu alipotoka.

    Kazi ya 2:
    Maswali ya ufahamu 

    1. Eleza hali ya maisha ya Kabatesi alipokuwa mtoto mdogo. 
    2. Kwa nini Kabatesi alipewa zawadi nyingi baada ya kumaliza 
    masomo yake ya shule za Sekondari? 
    3. Masomo ya muda mfupi aliyoyafuata yalikuwa yanahusu nini? 
    4. Eleza jinsi ambavyo Kabatesi aliweza kufaidika kutokana na 
    masomo ya muda mfupi. 
    5. Eleza jinsi ambavyo Kabatesi aliweza kufaidika kutokana na 
    masomo yake ya Sekondari. 
    6. Ni mambo gani yanayokudhihirishia kwamba Kabatesi alikuwa 
    kijana asiyekata tamaa? 
    7. Eleza jinsi ambavyo Kabatesi aliweza kuboresha maisha ya watu 
    wengine. 
    8. Kwa nini Kabatesi alipewa tuzo? 
    9. Kwa kifupi, eleza tabia na mienendo ya Kabatesi. 
    10. Kwa nini Kabatesi anachukuliwa kuwa mfano kwa vijana wengine? 
    11. Umepata funzo gani kutokana na kifungu hiki? 
    12. .Kulingana na kifungu hiki, eleza maana ya methali hizi: 
    a. Mvumilivu hula mbivu.
    b. Mchumia juani hulia kivulini.
    27.2. Matumizi ya msamiati kuhusu kifungu
    Kazi ya 3:
    Tunga sentensi kwa kutumia maneno yafuatayo: 
    1. Kuandaa
    2. Karo
    3. Tafrija
    4. Ajira 
    5. Hodari
    6. Kukata tamaa 
    7. Akaunti
    8. Tuzo
    9. Mradi

    Kazi ya 4:
    Husisha maneno kutoka sehemu A na maana yake kwenye sehemu B.
     

    cc

    ff

    Kazi ya 5:
    Kamilisha sentensi kwa kutumia maneno unayoona yanafaa kati ya 
    yafuatayo:
    Bidii, inawapongeza, utulivu, majukumu, vibanda, shule za 
    chekechea, ukalimani 
    1. Nchini Rwanda watoto wengi wanaanzia masomo yao katika……
    2. Wanafunzi wanalazimishwa kusoma kwa ............ ili waweze 
    kufaulu mtihani wa taifa.
    3. Kuna uhusiano wa karibu wa kazi ya ………. na tafsiri. 
    4. Wanafunzi wenye tabia ya …….. wanapata alama nzuri katika 
    masomo yao. 
    5. Serikali ya Rwanda ………. na kuwahimiza wasichana wanaosoma 
    sayansi na teknolojia. 
    6. Wazazi wana ……. ya kuwalisha na kulipa karo za watoto wao. 
    7. Mjomba wangu alijenga ……… vitatu vya kuku wake
    27.3. Sarufi: Matumizi ya alama za vituo
     a. Matumizi ya alama ya kuuliza/ ulizo ( ? )
    Kazi ya 6:
    Tazama sentensi zifuatazo na kuzungumzia matumizi ya alama 
    inayojitokeza.

    i. Unasema nini?
    ii. Mnafanya nini hapa ?
    iii. Je, jina lako nani ?
    iv. Kwa sababu gani wototo wanapaswa kuheshimu wazazi wao ?
    Maelezo muhimu
    Alama ya kuuliza au ulizo hutumiwa mwishoni mwa sentensi kuonyesha 
    kuwa sentensi hiyo ni swali. 
    Kwa mfano: Unaitwa nani?
    Kazi ya 7:
    Sahihisha sentensi zifuatazo:

    1. Unasoma kitabu kipi
    2. Mwalimu wako wa Kiswahili anaitwa nani
    3. Je, unakunywa chai
    4. Kwa nini unapiga kelele darasani
    5. Unachora nini
    b. Matumizi ya alama ya mshangao ( ! )
    Kazi ya 8:
    Tazama sentensi zifuatazo na kuzungumzia matumizi ya alama 
    inayojitokeza.

    i. O lalala! Baba yako amekufa!
    ii. Gooooo ! Amefunga goli!
    Maelezo muhimu
    Alama ya mshangao hutumiwa kuashiria mahangaiko ya moyo kama vile 
    hasira, hofu, mshangao na kadhalika. 
    i. Lo! Mwanafunzi ameangusha kitabu cha mwalimu matopeni. 
    ii. Wamefungwa mabao kumi kwa nunge!
    Kazi ya 9:
     Chunguza sentensi zifuatazo na kuzisahihisha

    1. Ala umebeba mzigo huo pekee yako
    2. Hoyee wanariadha wametunzwa medali
    3. Pesa zangu zimeibiwa
    4. Nimepita mtihani wangu wa kitaifa
    5. Lo Akimana ameanguka chini
    27.4. Matumizi ya lugha: Sifa za inshe ya masimulizi
    Kazi ya 10:
    Je, kifungu “Mafanikio ya kudumu” ni aina gani ya insha? Toa maelezo.
    Maelezo muhimu
    Sifa kuu za aina hii ya insha:

    • Matamshi na lafudhi ni lazima yawe sahihi. 
    • Ni lazima mazungumzo haya yagawanyike katika sehemu kuu tatu: 
    mwanzo, kati, na mwisho. 
    • Utungaji wa masimulizi ni lazima uzungumzie ukweli wa jambo 
    linalozungumziwa. 
    • Uwasilishaji wa hali, matukio, na mazingira yanayodhihirika waziwazi. 
    • Mtiririko wa mawazo wenye mshikamano. 
    • Msimuliaji ni lazima azungumze kwa nidhamu na kwa lugha sanifu 
    inayoeleweka kwa watu wote. 
    Mfululizo wa matukio ya haraka haraka. 
    • Masimulizi yawe ya kupendeza sana, pengine ya kuchekesha na yenye 
    kuteka hisia kwa maelezo ya kushangaza au yenye kujaa taharuki. 
    • Kutoa funzo maalumu kutokana na hadithi yenyewe, yaani maadili 
    fulani kuhusu maisha kwa ujumla. 
    27.5. Kusikiliza na kuzungumza: Majadiliano 
    Kazi ya 11:
    Serikali ya Rwanda inawahimiza wananchi kujitafutia ajira kutokana 
    na uhaba wa kazi. Jadili kuhusu namna ya kujitafutia kazi. 

    27.6. Kuandika: Utangazaji wa insha ya masimulizi 
    Kazi ya 12:
    Baada ya kusoma kifungu kuhusu insha za masimulizi “Mafanikio 
    ya kudumu,” tunga insha ya masimulizi kuhusu tukio fulani, kisa au 
    tukio la kweli au la kubuni kwa kuheshimu vipengele muhimu vya 
    insha ya msimulizi na taratibu zake.


    SOMO LA 28: MWONGOZO WA KUTUNGA INSHA

    xx

    Kazi ya 1:
    Unaona nini kwenye mchoro hapa juu?
    28.1. Kusoma na kufahamu: Siku yangu ya kwanza katika 

    shule za mabweni

    cc

    Mwanzo wa masomo yetu ulipokaribia kufika, wazazi wote walianza 
    kujiandaa kwa kutimiza wajibu wao wa kuwanunulia watoto wao mahitaji 
    kwa ajili ya masomo yao katika shule za sekondari. Wazazi wangu nao 
    waliwajibika kuninunulia mahitaji yote muhimu yaliyohitajika.

    Ulikuwa wakati wa mwanzo wa mwaka, shule za msingi na za sekondari 
    zilifungua tayari kwa kuanza masomo. Mimi niliamka asubuhi na mapema 
    nikatoka nyumbani saa kumi na mbili kamili. Baba, mama, dada na kaka 
    zangu wawili walinisindikiza umbali wa takribani kilomita mbili toka nyumbani 
    kabla ya wengine kurudi nyumbani isipokuwa baba. Baba yangu alichukua 
    begi langu lililokuwa zito nami nikachukua ndoo na godoro langu tukaendelea 
    mpaka kituo cha basi. 

    Tulipofika njiani, baba yangu aliniambia kwa sauti ya upole akisema: 
    “Mwanangu, nenda ukasome kwa bidii. Wakati ni mali, kamwe usiuatili. 
    Kumbuka kuwa tumewauza mbuzi wetu wawili ili tuweze kukutafutia vifaa 
    vyote unavyohitaji. Huko shuleni utakutana na vijana wengi wenye tabia 
    tofauti. Tafadhali, usishabihiane na wanafunzi wabaya ambao hawazingatii 
    maonyo na mawaidha ya wazazi wao na walimu”. Nami nilifikiria kidogo ili 
    niweze kumpa baba yangu jibu kutokana na yale aliyoniambia. Hatimaye 
    nilipata cha kumuambia baba. “Baba! Sitakusaliti kamwe! Malezi uliyonipa 
    tangu utotoni mwangu nitayatilia maanani; nitajifunza kwa bidii kama 
    unavyonitakia. Sitalandana na vijana hao wasio na maadlili mema.” Baada 
    ya kusikia hayo, baba yangu alitikisa kichwa kuonyesha kukubaliana nami 
    kuhusu mwelekeo wangu wa maisha katika mazingira niliyokuwa natarajia 
    kuingia. 
    Tuliendelea na safari mpaka tulipofika kwenye kituo cha basi. Huo ulikuwa 
    mwendo wa saa moja tu kwa miguu. 

    Kwenye kituo cha basi, kulikuwa na wanafunzi wengi lakini mabasi yalikuwa 
    machache. Baada ya dakika thelathini, basi lilikuja tukaingia sote. Mimi 
    nilikaa upande wa dirisha na baba alikaa karibu nami.Tuliendelea na safari 
    yetu mpaka shuleni. Kufika hapo, tulielekea kwenye ofisi ya mwalimu mkuu 
    wa shule ili tujitambulishe na kujisajilisha. Hapo nje palikuwa na umati wa 
    wanafunzi waliokuwa wakielekezwa kwenye mabweni yao na wengine 
    wakifanya shughuli za usafi. Labda hao walikuwa wenyeji wa shule hiyo 
    kwani walikuwa wakizungumza na kucheka kwa furaha kubwa pasipo 
    wasiwasi wowote

    Tulipiga hodi ofisini tukapokelewa vyema. Hedimasta alituuliza habari kamili, 
    tukamwelezea yote halafu nilielekezwa kwa katibu ambaye alinisajili baada 
    ya kuonyesha stakabadhi ya malipo ya karo ya shule. Mfanyakazi huyu 
    alimwita afisa wa nidhamu ili anipeleke bwenini na kunionyesha kitanda 
    changu. Hapo hapo nilimuaga baba yangu, naye akarudi nyumbani baada 
    ya kunitakia kila heri na fanaka katika masomo yangu. 

    Nilipofika bwenini nilishangaa sana kuona vitanda vingi katika ukumbi 
    mkubwa ambapo kila kitanda kilikuwa na sehemu mbili za kulala, moja chini 
    na nyingine juu yake. Nilitandika godoro langu kwenye sehemu ya chini ya 
    kitanda. Hata hivyo, nilikuwa na hofu kubwa moyoni kuwa yule atakayelala 
    juu yangu siku moja anaweza kuniangukia. Lakini nilijikaza kiume nikafikiria 
    kwamba hayo yalikuwa mazoea yao na kwamba shule haingekubali 
    kuendeleza hali hiyo kama kungetokea tatizo kama hilo. 
    Baadaye, kengele ililia kuwaita wanafunzi wote kuingia bwaloni kupata 
    chakula cha jioni. Chakula kilikuwa kizuri. Siku hiyo tulikula wali, maharagwe, 
    mboga na matunda.

    Tulipomaliza kula tuliambiwa kuingia madarasani mwetu kwa masomo ya 
    kibinafsi. Sisi sote tuliingia darasani, kila mwanafunzi alichukua daftari fulani 
    alilotaka na kuanza kujikumbusha yale tuliyokuwa tumesoma hapo awali. 
    Mimi nilichukua daftari langu la somo la Kiswahili nikaanza kupitia masomo 
    yote tuliyojifunza katika kidato cha tatu. Shughuli hii iliendelea mpaka saa 
    tatu za jioni ambapo kengele ililia tena kuashiria kuenda mabwenini kulala. 
    Mumo humo, tulilala kwa utulivu mpaka asubuhi tulipoamka kuanza masomo 
    yetu. 

    Kwa hakika, siku hiyo ya kwanza ya masomo yangu katika shule za mabweni 
    ilikuwa siku ya furaha na ugunduzi wa mambo mengi yanayohusu mazingira 
    ya shule hizo ambayo sikuyajua. Nilifurahia maonyo niliyopewa na wazazi 
    wangu na jinsi nilivyopokelewa na kuelekezwa na kila mmoja niliyemkuta 

    katika shule yangu.

    Kazi ya 2:
    Maswali ya Ufahamu 
    1. Eleza shughuli za wazazi kila wanapokaribia mwanzo wa masomo 
    ya watoto wao. 
    2. Mwanafunzi anayezungumziwa katika kifungu hiki anakwenda 
    kujifunza katika aina gani ya shule? 
    3. Nani ambaye alimsindikiza mwanafunzi hadi shuleni? 
    4. Ni mawaidha gani aliyompatia baba yake walipokuwa njiani?
    5. Eleza sifa za mwanafunzi anayezungumziwa katika kifungu hiki. 
    6. Ni nini kinachokuonyesha kwamba mwanafunzi huyu alipokelewa 
    vizuri mara tu alipofika shuleni? 
    7. Kwa nini alishangaa alipofika bwenini? 
    8. Wanafunzi walipewa chakula gani wakati wa jioni? 
    9. Walipoingia darasani mwanafunzi huyu alifanya nini? 
    10. Wanafunzi walitakiwa kulala saa ngapi? 
    28.2. Matumizi ya msamiati 
    Kazi ya 3:
    Tunga sentensi fupi kwa kutumia maneno yafuatayo kama 
    yalivyotumiwa katika kifungu ulichokisoma hapo juu.

    1. kujiandaa                                                       6. maadili 
    2. kusaliti                                                            7. heri na fanaka 
    3. kuuza                                                               8. ukumbi 
    4. bidii                                                                  9. kusajili 

    5. tabia                                                                10. kuashiria

    Kazi ya 4:

    Tumia mshale kwa kuonyesha maana ya maneno yafuatayo:

    c

    28.3. Sarufi: matumizi ya alama za vituo
    a. Nuktambili / koloni ( : )
    Kazi ya 5:
    Tazama sentensi zifuatazo na kuzungumzia matumizi ya alama 
    nuktambili inayojitokeza.

    i. Tunaenda sokoni kununua vitu vifuatavyo: nyanya, mahindi,… 
    ii. Katika familia yetu kuna watoto kama: Karangwa, Mukamurenzi…
    iii. Jimbo la kusini kuna wilaya kama: Ruhango, Kamonyi, Huye

    Maelezo muhimu

    Nukta mbili 
    a. Hutumiwa kutanguliza maneno yaliyo katika orodha. 
    Kwa mfano: 
    i. Nenda ukaniletee: kalamu, karatasi na kifutio. 
    ii. Amenunua: machungwa, sukari, na ndizi. 
    b. Hutumiwa kuashiria maneno ya msemaji badala ya alama za mtajo 
    hasa katika uandishi wa mazungumzo au tamthilia. 
    i. Mama: Lazima uniambie ulikokuwa tangu jana. 
    ii. Mwalimu alisema: Ingieni darasani. 
    c. Hutenganisha nambari za saa (saa na dakika). 
    Kwa mfano: 
    4: 10 – saa kumi na dakika kumi
    Kazi ya 6:
    Sahihisha sentensi zifuatazo
    1. Mifano ya ndege wanaofugwa ni kuku, bata, na njiwa
    2. Baba yangu hutengeneza meza, kiti, kitanda na kabati.
    3. Familia huwa na baba, mama, nyanya, babu na watoto
    4. Mimi huamka saa 2: 00 asubuhi kila siku
    5. Mchezo wa kandanda ulianza saa10: 00 jioni
    b. Nuktamkato / nukta na kituo / semikoloni ( ; )
    Kazi ya 7:
    Tazama sentensi zifuatazo na kuzungumzia matumizi ya alama 
    nuktamkato inayojitokeza.
    a. Sikwenda Kayonza; nilienda Kirehe.
    b. Usiwe na wasiwasi; nitakuwa pamoja nawe siku zote.
    c. Harusi hiyo ilihudhuriwa na watu wengi: wanawake kwa wanaume; 
    wadogo kwa wakubwa; wazee kwa vijana. 
     
    Maelezo muhimu
    Nukta na kituo 
    a. Hutumiwa kuunganisha vishazi vikuu bila kutumia kiunganishi.
     Kwa mfano: 
    • Tuliwasili darasani tukiwa tumechelewa; mwalimu alitukaribisha kwa 
    kutuuliza tulipokuwepo. 
    b. Hutumiwa kumpumzisha msomaji katika sentensi iliyo ndefu ili 
    apumzike zaidi kuliko pale inapotumiwa koma. 
    Kwa mfano: 
    Alipofikiri sana, alitanabahi kuwa hakikuwepo cha kutorokwa; yeye angeweza 
    kuondoka nyumbani au kumwacha mumewe, aende popote kufanya lolote.
    c. Kuorodhesha vitu hasa vinapokuwa na zaidi ya neno moja
    Mfano:
    Wakati wa likizo tulitembelea sehemu kadhaa: Mombasa, Kenya; Dodoma, 
    Tanzania; Kampala, Uganda na tukamalizia hapa Nairobi, Kenya.
    Kazi ya 8:
     Sahihisha sentensi zifuatazo: 
    1. Kabla ya kupata chakula ni lazima kunawa mikono hii ni tabia nzuri
    2. Akili ni mali kila mtu ana zake.
    28.4. Matumizi ya lugha: Taratibu za kutunga insha
    Kazi ya 9:
    Jibu maswali yafuatayo:
    1. Kwa sababu gani utangulizi mzuri ni muhimu katika insha? 
    2. Jadili sehemu kuu za insha. 
    3. Jadili mambo ya kuzingatia katika uandishi wa insha.
    Maelezo muhimu: Taratibu za kutunga insha: 
    • Soma kwa makini mada/ kichwa/ anwani uliyopewa zaidi ya mara moja, 
    ili uielewe vizuri. 

    • Ifikirie mada/ kichwa/ anwani kwa muda. 
    • Yaandike mambo muhimu yatakayokuongoza katika kuiandika insha .
    • Maelezo yote yatolewe kwa undani na kwa njia ya kuvutia. 
    • Kutumia vizuri alama za uakifishaji. 
    • Kupanga mawazo katika mtiririko wenye mantiki. 
    • Kutumia msamiati mwafaka kwa kutegemea mada. 
    • Lugha iwe ya adabu na isiyo ya matusi. 
    • Andika methali, misemo na nahau ambazo unadhania zinaweza 
    kukufaa katika utungaji. 
    Mambo ya kuzingatia katika uandishi wa insha 
    Bila kujali ni aina gani ya insha mtu anayoiandika, yapo mambo kadhaa ya 
    kuzingatia wakati wa uandishi wa insha. Mambo hayo ni pamoja na: 
    1. Kubaini ni mada gani ya kuandikia insha na kuielewa vyema, 
    2. Kupanga mawazo katika mtiririko wenye mantiki, 
    3. Kutumia mtindo unaoendana na kusudi la insha. 
    Kwa mfano: Mtindo wa masimulizi unafaa kwa hadithi au insha nyingine za 
    kisanaa.
    4. Kutumia lugha fasaha na inayoeleweka,
    5. Kufuata kanuni za uandishi. 
    Kwa mfano:
    Matumizi ya alama za uandishi, aya, herufi kubwa na herufi ndogo. 
    Kupanga insha katika muundo wake, yaani kichwa, utangulizi, kiini na 
    hitimisho. 
    1. Kichwa cha habari 
    Kichwa cha habari cha insha ni maneno machache, takribani matano, 
    ambayo ndiyo jina la insha. Kichwa cha habari huandikwa juu, katikati 
    kwenye ukurasa wa kwanza wa insha. Mara nyingi, huandikwa kwa herufi 
    kubwa na hubeba wazo kuu la insha. 
    2. Utangulizi wa insha 
    Utangulizi wa insha ni sehemu ya mwanzo yenye urefu usiozidi aya moja. 
    Utangulizi hudondoa kwa ufupi kabisa kile kinachoelezwa kwenye insha. 

    3. Kiini cha insha / mwili 
    Hii ni sehemu tunayoweza kusema ndiyo insha yenyewe. Kwenye kiini ndipo 
    ufafanuzi wote hutolewa. Ufafanuzi huu hupangwa katika aya moja au zaidi. 
    Hapa ndipo mwandishi hubainisha mawazo yake, huthibitisha, hushawishi, 
    huhimiza na hufafanua kiundani kabisa. 
    4. Hitimisho la insha 
    Hii ni sehemu ya mwisho ya insha ambayo nayo haizidi aya moja. 
    Katika sehemu hii, mwandishi anaweza kurejelea kwa ufupi sana yale 
    aliyozungumzia kwenye insha yake, anaweza kuonyesha msimamo wake, 
    anaweza kutoa mapendekezo, au kuwahimiza walengwa wake kuchukua 
    hatua fulani.
    28.5. Kusikiliza na kuzungumza
    Kazi ya 10:
    Chagua mada moja kati ya hizi, kisha uizungumzie kwa mapana na 
    marefu na kuiwasilisha mbele ya darasa.

    1. Harusi uliyoihudhuria
    2. Mchezo uliohudhuria
    28.6. Kuandika: Utungaji wa insha
    Kazi ya 11:
    Andika insha ya ukurasa mmoja kuhusu “Siku yangu ya kwanza shuleni.” 

    Tathmini ya mada
    A. Sahihisha makosa ya kimaandishi katika mazungumzo hapa chini
    Mgonjwa: hujambo daktari 
    Daktari: sijambo Karibu uketi. 
    Mgonjwa: asante daktari 
    Daktari: nikusaidie vipi 
    Mgonjwa: Jina langu ni kayitesi ninaumwa na tumbo sana. 
    Daktari: pole sana kayitesi tumbo lilianza kukuuma lini 
    Mgonjwa: Tangu jana usiku hata sijalala ninaendesha na kutapika sana
    Daktari: pole sana Ulikula nini jana usiku 
    Mgonjwa: Nilikula wali kwa kitoweo cha samaki
    Daktari Mmmmhh!Wewe hunywa maji yaliyochemshwa
    Mgonjwa Si kila siku daktari Mimi hunywa maji yoyote bora yanaonekana 
    kuwa safi.
    B. Andika insha ya masimulizi kuhusu mada zifuatazo: 
    i. Siku ya kuadhimisha mwaka mpya. 
    ii. Safari yangu mjini Kigali. 
    iii. Utoto wangu. 
    iv. Likizo iliyopita.



    

  • MADA YA 8 DHIMA YA LUGHA YA KISWAHILI KATIKA JAMII

    Uwezo mahususi katika mada hii: 
    Kuonyesha dhima ya lugha ya Kiswahili kwa jamii ya nchi zinazozungumza 
    lugha hii.
    Malengo ya ujifunzaji:
    • Kutoa maana na umuhimu wa lugha,
    • Kusoma na kuelewa kifungu kuhusu lugha kama chombo cha 
    mawasiliano,
    • Kusikiliza kwa makini na kusimulia kwa ufasaha kifungu cha habari 
    kinachohusika,
    • Kujadili namna ya kuitunza lugha na mwenendo unaofaa.
    Kidokezo
    1. Taja lugha zote zinazozungumzwa nchini Rwanda.

    2. Andika dhima nne za lugha ya Kiswahili.

    SOMO LA 29: TUONGEE KISWAHILI SANIFU

    cc

    Kazi ya 1:
    Tazama mchoro hapa juu na kujadili kazi mbalimbali zinazoendelea.
    29.1. Kusoma na ufahamu: Kiswahili nchini Rwanda
    Soma kifungu cha habari kifuatacho kisha ujibu maswali 
    yanayoambatana nacho: 

    Lugha ya Kiswahili ni mojawapo ya lugha nne zinazozungumzwa nchini 
    Rwanda. Hizi ni Kinyarwanda, Kiingereza, Kifaransa na Kiswahili vilevile. 
    Hapo mwanzo, lugha ya Kiswahili ilikuwa lugha ya kibiashara lakini polepole 
    mambo yalibadilika kutokana na ushirikiano wa Rwanda pamoja na nchi 
    jirani zake ambazo ni Kenya, Tanzania, Uganda, Jamhuri ya Kidemokrasia 
    ya Kongo na Burundi zinazotumia lugha ya Kiswahili katika shughuli 
    mbalimbali. 

    Lugha ya Kiswahili ambayo ni chombo cha mawasiliano kwa kupashana 
    habari, nchini Rwanda, imeshamiri na kupata nguvu nyingi baada ya Rwanda 
    kuwa mwanachama wa Jumuiya ya nchi za Afrika Mashariki, Kiswahili 
    kikiwemo lugha rasmi.

    Lugha ya Kiswahili hufundishwa nchini katika shule za sekondari na vyuo 
    vikuu. Vituo vya utangazaji habari kama vile redio na vituo vya televisheni 
    pia hutumia Kiswahili katika baadhi ya matangazo vinavyorusha. 

    Aidha, lugha ya Kiswahili hutunza, hukuza, na huendelezautamaduniwajamii, 
    bila ya kusahau kwamba ni alama ya utambulisho wa jamii au taifa fulani.
    Kazi ya 2:
    Maswali ya ufahamu

    1. Ni lugha gani zinazozungumzwa nchini Rwanda ?
    2. Kwa sababu gani, nchini Rwanda, lugha ya Kiswahili imekua 
    sana siku hizi?
    3. Onyesha dhima mbili za Kiswahili.
    4. Taja shule zinazofundisha Kiswahili nchini Rwanda .
    5. Je, lugha ya Kiswahili ni lugha ya mawasiliano nchini? Eleza jibu 
    lako kwa kutumia mifano sahihi kutoka kifungu.

    29.2. Matumizi ya msamiati
    Kazi ya 3:
    Toa maana ya maneno yafuatayo:

    1. Dhima 
    2. Ushirikiano
    3. Kupashana 
    4. Maarifa
    5. Utamaduni 
    6. Jamii

    7. Mzawa

    29.3. Sarufi: Matumizi ya hali ya kuamuru

    dd

    Kazi ya 4:
     Tazama michoro hapo juu na kueleza kinachofanyika pale.
    Kazi ya 5:
    Tunga sentensi tano kwa kutumia hali ya kuamuru.
    Maelezo muhimu

    • Katika hali ya kuamuru au ya kushurutisha, vitenzi vya silabi zaidi 
    ya moja na vyenye kiambishi tamati -a, huondolewa tu kiambishi 
    cha kitenzi ku- katika umoja hali yakinishi. Katika wingi, vitenzi hivi 
    huondolewa kiambishi ku- pamoja na kiambishi tamati-a, halafu 
    vikachukua kiambishi -eni badala ya kiambishi -a cha mwishoni.
    Mfano:Kitenzi: kusimama
    Umoja: (Wewe) Simama!
    Wingi: (Nyinyi/ Ninyi) Simameni!
    Kazi ya 6:
    Zikamilishe sentensi zifuatazo kwa kutumia hali ya kushurutisha 
    kwa vitenzi ambavyo vimo katika mabano. 

    Kwa mfano: Swali: Mwalimu aliwaambia wanafunzi: “…….madaftari 
    yenu”. (kuchukua)
     Jibu: Mwalimu aliwaambia wanafunzi: “Chukueni madaftari yenu.”
    1. “…………… kazi yako ya shule kuhusu dhima ya Kiswahili.” Mama 
    alimwamrisha mtoto wake. (fanya)
    2. Mwalimu alimwomba mwanafunzi akisema: “…………… ubao 
    tufanye mazoezi!”(Kufuta)
    3. Baada ya kujiunga na nchi nyingine za Afrika Mashariki viongozi 
    wa Rwanda walituambia: “……… Kiswahili!” (kuzungumza).
    4. Kwa kuwa wewe ni mkazi wa nchi ya Rwanda …………. vizuri 
    lugha ya Kinyarwanda! (ongea)
    5. Mwalimu ameniambia kuwa mtafanya jaribio la Kiswahili kesho; 
    kwa hiyo……… (kurudia) masomo yenu.
    6. Mwalimu aliwaambia wanafunzi: “…………..runinga kuna mchezo 
    wa kuigiza uhusuo uhifadhi wa mazingira!” (kutazama).

    7. Katibu aliombwa na mwenyekiti: “……………….mawazo yote 
    yatakayotolewa mkutanoni!” (kuandika).
    8. Kama unataka kukuza stadi zako za kuzungumza na kusikiliza 
    lugha ya Kiswahili, ……………..matangazo ya redioni na utazame 
    runinga! (kusikiliza)
    29.4. Matumizi ya Lugha: Maana na umuhimu wa lugha 
    katika jamii

    Kazi ya 7:
    Panga maneno yafuatayo kwa utaratibu unaofaa ili yaweze kuleta 
    maana kamili

    1. ni -ya -Kiswahili- Mashariki- muhimu -lugha -Jumuia -ya -Afrika 
    -katika -sana
    2. Kiswahili -mwanzoni -kama- lugha -ilikuwa -ya- hapo- biasharalugha-ikitumiwa -ya.
    3. Walifurahi- rasmi- Wanyarwanda- kusikia- sana- mojawapo- lugha 
    ya- nchini- Kiswahili- kwamba- ni- Rwanda- ya- lugha.
    Kazi ya 8:
    Tunga sentensi kwa kutumia maneno yafuatayo:

    1. Jumuiya
    2. Utamaduni
    3. Matangazo
    4. Jamii
    29.5. Kusikiliza na Kuzungumza: Umuhimu wa lugha ya 
    Kiswahili katika jamii
    Kazi ya 9:

    Jadili kuhusu dhima za lugha ya Kiswahili

    29.6 Kuandika: Utungaji wa kifungu cha habari 

    Kazi ya 10:
    Tunga kifungu kifupi (mistari kumi) ukionyesha faida ya Rwanda 
    kutumia lugha ya Kiswahili

    SOMO LA 30: MAWASILIANO YETU.

    vv


    Kazi ya 1:
    Eleza kinachofanyika kwenye mchoro wa hapo juu.
    30.1. Kusoma na ufahamu: Ziara ya mjini

    Soma kifungu cha habari hiki na kujibu maswali yanayokifuata:
    Siku moja Bwana Mugisha aliondoka zake kijijini Kirenge kuelekea mjini. 
    Alichukua mkoba wake mweusi na kuujaza kila kitu cha kumsadia njiani na 
    mjini vilevile. Alipofika mjini, aliwakuta jamaa wawili mmoja aitwaye Rukundo 
    na mwingine Ruhara.Walisalimiana kwa hamu kubwa kwani siku zilikuwa 
    nyingi bila ya kuonana. 

    Wakati huo huo wasichana watatu Ange, Lidia na Isimbi walipita karibu nao 
    wakiwa wametoka kabisa. Lugha waliyokuwa wanaongea ilimshangaza 
    Mugisha sana kwani ilikuwa mara yake ya kwanza kuisikia.  « Mbona watu 
    hawa siwaelewi hata kidogo, wametoka wapi  ?  » Alitamka haya akiwa 
    na mshangao mkubwa sana. Ruhara ambaye alizoea maisha ya mjini 

    alimwambia, ‘’hii ni lugha ya Kiswahili, lugha nzuri yenye asili ya upwa 
    wote wa Afrika Mashariki.’’ Aliendelea kumsimulia yaliyompata alipokwenda 
    sehemu za Arusha huko Tanzania. ‘’Miaka miwili iliyopita, nilikwenda mjini 
    Arusha katika mkutano wa waumini wa dini moja huko, nilipoingia mjini 
    lugha ilikuwa hiyo, mitaani na migahawani, misikitini na makanisani, kweli 
    sikuwa na tamko lolote isipokuwa kimya tu na kutumia ishara. Kwa bahati 
    nzuri, nilipata usaidizi kutoka kwa raia wa huko kwani baadhi yao walijua 
    lugha nyingi ikiwemo yangu. Baada ya wiki moja, tulirudi kwetu nikiwa na 
    fikra moja kichwani mwangu ya kujifunza Kiswahili na kukizungumza vizuri. 
    Leo nina hatua nzuri. ’’

    Kuyasikia hayo, Mugisha aliunga mkono Ruhara na kusema kuwa naye 
    angepata mwalimu angejifunza Kiswahili. Wote waliendelea na safari zao 
    kwa makubaliano ya kujua lugha zaidi ya moja, msingi wa maendeleo na 
    ushirikiano na wengine.
    Punde si punde mabinti wale Ange, Lidia na Isimbi walimwita Mugisha 
    ambaye alionekana kuwa mgeni mjini. Walisema ‘’ Mzee njoo hapa, tunahitaji 
    kuongea na wewe.’’ Mugisha bila kusita alianza mbio kinyumenyume 
    akihofia kuibiwa au usumbufu mwingine. Yeye aliona wasichana hao kama 
    wakware ambao wanataka awape pesa zake alizokuwa ameficha mkobani 
    chini ya nguo. Ange alimfuata kwa hatua ndefu na maneno ya upole, jambo 
    lililopunguza wasiwasi wake Mugisha na kusimama. 

    Mazungumzo yalianza katika lugha ya Kinyarwanda Ange na wenzake 
    wakimwonyesha umuhimu wa lugha kama chombo cha mawasiliano kati 
    ya jamii fulani. Bwana Mugisha aliwajulisha uamuzi wake ili mara ijayo 
    asije akakabiliana na shida hiyo tena. Walimfundisha maneno machache 
    na kumshauri aendelee kuvifuata vipindi vya redio na televisheni katika 
    Kiswahili. Mugisha aliwaomba namba zao za simu ili kila mara atakapopata 
    shida au atahitaji msaada awapigie simu. Wasichana walimnunulia chakula 
    na chai akala na kushiba. Baadaye, kundi la watatu lilimuaga Mugisha. Tangu 
    siku hiyo, Mugisha hawezi kuidharau lugha na umuhimu wa mawasiliano.

    Kazi ya 2:
    Maswali ya ufahamu
    1. Toa majina ya wahusika katika kifungu cha habari hiki.
    2. Mgeni huyu alishangazwa na nini alipofika mjini?
    3. Kwa sababu gani Ruhara alikuwa kimya na kutumia ishara tu 
    alipokuwa mjini Arusha ? Alisaidiwa na nini ?
    4. Je, mabinti waliokutana na Mugisha walizungumza lugha zaidi ya 
    moja ? Fafanua jibu lako.
    5. Kwa nini Mugisha alianza kukimbia alipoitwa na wasichana ?
    6. Nini kilimridhisha Mugisha katika ziara yake mjini ?
    7. Ingekuwa wewe ungefanya nini baada ya kupata shida ya 
    kimawasiliano ? Jadili.
    30.2. Matumizi ya msamiati kuhusu mawasiliano yetu
    Kazi ya 3:
    Toa kinyume cha maneno haya:
    1. Mzee
    2. Mji
    3. Haraka
    4. Lugha nzuri
    5. Karibu
    Kazi ya 4:
    Jaza sentensi hizi kwa kutumia msamiati unaofaa ulioko katika 
    kifungu

    1. Bwana Mugisha alisaidiwa na……………………….wawili 
    waliomnunulia ………….akala akashiba.
    2. Miaka miwili iliyopita ……………..alikwenda mjini……………..
    katika …….wa waumini.
    3. Ange na ……..waliongea lugha ya………….na lugha ya..... 
    4. Mugisha alidhani wasichana walikuwa ……………..na kukimbia.

    Kazi ya 5:
    Eleza maana ya maneno yanayofuata: 

    a. Mkoba
    b. Jamaa
    c. Mkutano
    d. Kutoka
    e. Fikra
    f. Binti
    g. Mbio
    h. Kuaga
    Kazi ya 6:
    Kamilisha sentensi zifuatazo ili zilete maana kamili kwa kutumia 
    msamiati huu:
    lugha, jumuia, televisheni, simu, ishara.
    1. Kiswahili ni................................ambayo inatumiwa katika 
    ………………….ya afrika Mashariki.
    2. Jamila hufuata vipindi vya………………………kila siku.
    3. Wasichana watapigiwa …………………….. na mzee Karinda.
    4. Mtu asiye na ujuzi wa lugha lazima atumie……..……………….

    30.3. Sarufi: Hali ya kuamuru
    Kazi ya 7:
    Soma mazungumzo yafuatayo na kubainisha vitenzi vilivyotumiwa 
    katika hali ya kuamuru
    Baba: Waambaje, Nikuze?
    Nikuze: Salama babangu. Naona umechoka leo! Tafadhali nenda bafuni.
    Baba: Ehee! Leo nimefanya kazi nyingi bila kupumuzika. Nenda ukaniletee 
    maji na sabuni ya kuogea.
    Nikuze: Ndiyo. Jitayarishe, uchukue taulo na kandambili halafu uende 
    bafuni.
    Baba: Asante sana binti yangu. Niandalie chakula haraka iwezekanavyo 
    nina njaa.
    Nikuze: Chakula kimeiva na ninakaribia kukiweka mezani. Nimekupikia 
    ugali na kitoweo kitamu sana bila shaka utakifurahia. Karibu ndani mama.
    Mama: Asante binti yangu. Habari za nyumbani?
    Nikuze: Nzuri mama. Baba amekuja akiwa amechoka na hivi sasa yumo 
    bafuni.
    Mama: Ni kweli kabisa. Leo amefanya kazi isiyo rahisi. 
    Nikuze : Namwona baba anatoka bafuni usisahau kumpa pole kwa 
    uchovu alio nao.
    Mama: Wewe mwekee chakula na kinywaji mezani, mengine ni yangu. 
    Fanya haraka binti yangu.

    Nikuze: Barabara kabisa.

    Kazi ya 8:
    Tunga sentensi tatu kwa kutumia hali ya kuamuru tungo yakinishi.

    Kazi ya 9:
    Tunga sentensi tatu zenye vitenzi vilivyoko katika hali ya kuamuru 
    tungo kanushi.

    Maelezo muhimu kuhusu hali ya kuamuru / hali ya amri
    Hali ya kuamuru ni ya vitenzi ambavyo vimo katika hali shurutishi au ya 
    kulazimisha yaani mtendaji wa tendo halitendi kwa hiari yake bali ni kwa 
    sharti ya mtu mwingine.
    Huonyesha kuwa mtu analazimishwa kufanya jambo fulani. Hutumiwa kwa 
    nafsi ya pili tu (umoja na wingi).
    Tunafuata kanuni zifuatazo :
    • Vitenzi vyenye silabi nyingi, hupoteza ku- ya kitenzi. Kwa wingi, kitenzi 
    huongezwa «-ni» mwishoni, katika hali yakinishi.
    Mfano: Nyamaza! (Umoja)
     Nyamazeni! (Wingi)
     shukuru! (umoja)
     shukuruni! (wingi)
    • Katika hali kanushi, vitenzi huishia na «-e» isipokuwa vitenzi vya asili 
    ya kigeni.
    Mfano: Usinyamaze! (Umoja)
     msinyamaze! (Wingi)
    • Usirudi! (umoja)
    • Msirudi! (wingi)
    • Vitenzi vyenye silabi moja hubaki na «ku-» ya kitenzi (katika hali 
    yakinishi) na huongezwa «-ni», kwa wingi.
    Mfano: - Kunywa! (umoja)
    • Usinywe!
    • Kunyweni! (wingi)
    • Msinywe!
    • Vitenzi: kuja, kwenda (kuenda) na kuleta, havifuati kanuni hizi.
    Mifano:
    a. Kuja:
    Njoo! (umoja hali yakinishi)
     Usije! (hali yakinishi)
    Njooni! (wingi hali yakinishi)
    Msije! (wingi hali kanushi)
    b. Kwenda/kuenda :
    Nenda! (Umoja hali yakinishi)
     Usiende! (Umujo hali kanushi)
    Nendeni! (Wingi hali yakinishi)
    Msiende! (Wingi hali kanushi)
    c. Kuleta:
    Lete! (Umoja hali yakinishi)
    Usilete! (Umoja hali kamushi)
    Leteni! (Wingi hali yakinishi)
    Msilete! (Wingi hali kanushi)
    d. Kupa:
    Nipe! (Umoja hali yakinishi)
    usinipe! (Umoja hali kanushi)
    Nipeni! (Wingi hali yakinishi)
    Msinipe! (Wingi hari kanushi)
    Kazi ya 10:
    Badilisha sentensi zifuatazo ziwe katika hali ya kuamuru katika wingi. 

    1. Njoo hapa utusalimu!
    2. Kimbia ili usichelewe shuleni!
    30.4. Matumizi ya lugha: Mawasiliano yetu
    Kazi ya 11:
    Jadili maswali yafuatayo: 
    Mawasiliano ni nini?
    Je,ndege na wanyama huwasiliana kwa njia gani?
    Mawasiliano yana umuhimu gani ?

    Maelezo muhimu
    Mawasiliano ni mchakato wa kuhawilisha taarifa kwa njia ya ubadilishanaji wa 
    mawazo, hisia, malengo, tabia, matarajio, mitazamo kupitia mazungumzo, 
    ishara na maandishi. Ni ubadilishanaji wa taarifa unaoleta maana baina ya 
    pande mbili au zaidi ambazo zinaweza kuwa viumbe hai au kinyume chake. 

    Lugha ni chombo cha mawasiliano ambacho amejaliwa binadamu tu na 
    kwamba hakuna kiumbe mwingine ambaye si binadamu mwenye uwezo 
    wa kuzungumza na kutumia lugha. Hii ina maana kuwa kuna sifa fulani za 
    lugha za binadamu ambazo hazipatikani kwa kiumbe mwingine yeyote yule 
    isipokuwa mwanadamu.

    Ingawa ndege, mbwa, nyuki, tumbili wanaweza kuwasiliana, mawasiliano 
    yao huwa ni ya sauti au ishara ambazo kimsingi siyo lugha, pia huwa 
    yanadhibitiwa na hisia tu kama hofu, njaa, na ishara za kutoa taarifa. 

    Binadamu ana uwezo wa kujifunza lugha mbalimbali na kuzitumia katika 
    mazingira yake na kitu ambacho wanyama hawawezi. Kwa mfano, 
    ukimchukua paka wa Uchina na kumleta Rwanda atatoa sauti ile ile sawa 
    na paka wa Rwanda kwa kueleza shida ile ile au kutoa ishara ile ile. 

    Ulishawahi kujiuliza kwamba mawasiliano yangekuwaje pasipokuwepo 
    lugha? Mwalimu angekuwa anatumia mtindo gani kukufundisha darasani au 
    wewe ungemwombaje kalamu rafiki yako? (Unasema ungewasiliana kama 
    wanavyowasiliana watu wasiosikia au kuzungumza?) Hao pia wanawasiliana 
    hivyo kwa sababu wana maarifa ya lugha. Watu wasiosikia au kuzungumza 
    wanawasiliana kwa lugha ya ishara, lugha ambayo inafundishwa katika 
    baadhi ya shule za sekondari na vyuo vikuu nchini Rwanda. 

    Ufumbuzi wa kisayansi na kiteknolojia usingewezekana pasipo kuitumia 
    lugha, usingeweza kusogoa na marafiki zako kwenye fesibuku, usingeweza 
    kumwandikia ujumbe rafiki yako kupitia simu yako na kadhalika. Kiswahili 
    kinatarajiwa kutumika kama chombo cha mawasiliano katika taaluma 
    mbalimbali kama vile utawala na taasisi mbalimbali kama vile bungeni, 
    mahakamani na penginepo.
    Kazi ya 12:
    Jibu maswali yafuatayo:

    1. watu wasiosikia au kuzungumza huwasiliana kwa njia ipi?
    2. Ni tofauti gani kati ya mawasiliano ya binadamu na yale ya viumbe 
    wengine?
    3. Andika njia nne ambamo Kiswahili kinaweza kutumiwa na 
    kurahisisha mawasiliano.
    Kazi ya 13:
    Pamoja na picha hizi, sema ikiwa kuna mawasiliano ya lugha, ya 

    ishara au ya sauti na kujaza jedwali hapo chini:

    vv

    cc

    30.5. Kusikiliza na Kuzungumza: Majadiliano
    Kazi ya 14:
    ”Mawasiliano ya lugha ni bora kuliko mawasiliano ya ishara na 
    sauti.” jadili kauli hii. 
    30.6. Kuandika: Utangaji wa insha
    Kazi ya 15:
    Tunga insha fupifupi ukionyesha umuhimu wa lugha ya Kiswahili 
    nchini Rwanda.
    Kazi ya 16:

    Andika aya mbili kuhusu “umuhimu wa mawasiliano.”

    SOMO LA 31: UMUHIMU WA LUGHA

    cc

    Kazi ya 1:
    Eleza yale unayoyaona kwenye mchoro huu. 
    31.1. Kusoma na ufahamu: Umuhimu wa lugha
    Soma kifungu kifuatacho kuhusu “Umuhimu wa lugha” kisha, jibu 

    maswali uliyopewa hapo chini. 

    Familia ya mzee Yakobo inaishi katika kijiji cha Nyamugari. Kila mara Mzee 
    Yakobo huwahimiza watoto wake Maria na Maria kujifunza lugha mbalimbali 
    kwa madhumuni ya maisha yao ya usoni. Yeye anajua kwamba lugha, kama 
    mfumo wa ishara au sauti nasibu zinazowezesha jamii kuwasiliana, ina 

    umuhimu sana katika maisha ya kila siku. Tangu Maria alipoyasikia maneno 
    ya baba yake aliyazingatia sana mawaidha aliyopewa na kujifunza vizuri 
    lugha zote zilizopatikana kwenye ratiba yake ya masomo. Kwa sasa, yeye ni 
    mkuu wa kitengo cha utalii katika taasisi inayoshughulikia masuala ya utalii na 
    mazingira. Petro ni tofauti na ndugu yake Petro aliyeonyesha mtazamo hasi 
    kuhusu ujifunzaji wa lugha. Yeye alipenda kusema: « Siwezi kupoteza muda 
    wangu kujifunza lugha za watu wengine, lugha ninayozungumza inanitosha». 
    Kwa kweli, alikuwa mtoto mtukutu asiyejali maonyo na mawaidha ya wazazi 
    wake. Kwake, kujisomea hata sentensi fupi za Kiswahili lilikuwa jambo la 
    ajabu! Alikuwa amesitisha masomo yake alipomaliza darasa la pili katika 
    shule ya Sekondari ya Nyamugari ingawa baba yake hakuacha kumuonya 
    kuhusu umuhimu wa elimu na nafasi ya lugha katika maisha ya binadamu. 

    Siku moja, Mzee Yakobo aliamua kwenda kumtembelea binti yake aliyeishi 
    katika nchi jirani. Petro alimsihi waende pamoja kuwasalimia binamu zake 
    ambao ni Kamugisha na Kana. Mzee Yakobo aliposikia maneno ya mtoto 
    wake, hakusita kukubali wazo lake. Alifikiria kwamba mtoto wake angekutana 
    na binamu zake wangemuuliza mengi kuhusiana na masomo yake. Kwa 
    hivyo, Mzee Yakobo alimwomba mtoto wake Petro ajiandae kwa safari. 
    Gari lao lilitoka Nyabugogo saa kumi na moja alfajiri. Walipofika njiani, Petro 
    alishindwa kuvumilia njaa iliyokuwa ikimuuma kutokana na safari ndefu. Kwa 
    bahati nzuri, walipofika katika mji mmoja, dereva aliamua kusimamisha gari 
    ili wasafiri waweze kwenda haja na wengine waweze kujinunulia chakula na 
    kinywaji kabla hawajaendelea na safari yao. Baba yake Yakobo alimwonea 
    huruma mtoto wake na kumpa shilingi mia mbili ili aweze kwenda kujinunulia 
    chakula. Petro alifurahi sana. Alikuwa na hamu ya kula mkate na kunywa 
    juisi ya matunda iliyotengenezewa katika nchi jirani. Alienda haraka na 
    kuingia dukani. Dukani alimkuta Bi Hassani aliyemkaribisha na kumuuliza 
    alichotaka kununua dukani humo. 

    Lo ! Petro alikosa neno. Alisimama akimkodolea macho kama aliyejiingiza 
    baharini bila kujua kuogelea. Kweli alishindwa kuulizia kile kilichomleta 
    pale. Alijitahidi kutumia ishara kumwonyesha sehemu palipowekwa mikate 
    na vyakula vingine lakini mfanyabiashara hakuelewa alichokuwa anahitaji 
    miongoni mwa vyakula vilivyokuwemo dukani. Petro aliposhindwa kusema 
    alichukua shilingi zote alizokuwa nazo na kumkabidhi Bi. Hassani. Hapo 
    ndipo alipewa mkate na maji. Petro alipokea kwa shingo upande alichopewa 
    na mwenye duka na kurudi haraka na kuziacha shilingi mia moja zilizobaki 
    kwenye jumla ya bei ya mkate na maji. Kama angekwenda shuleni 
    asingefanyiwa hayo. 

    Mara moja, dereva alianza kugeuza gari ili waendelee na safari. Petro 
    alikuwa ameketi kwenye kiti chake karibu na baba yake. “Salaalaa!” Yakobo 
    alishikwa na bumbuazi alipoona mtoto wake ameleta chakula kilichokuwa 
    kimepitisha tarehe ya kukila mwaka uliopita. “Wewe hujui kusoma wala 
    kuhesabu! Tazama tarehe iliyoandikwa hapa! Huoni kuwa chakula hiki 
    kingepaswa kuliwa kabla ya mwezi uliopita?” Kwa kweli, alianza kujiuliza 
    mengi kuhusu maisha ya mtoto wake. Alisikitika sana na kumwomba 
    asithubutu kula chakula hicho kwani kingeweza kuharibu afya yake. Petro 
    alikunywa maji tu aliyoleta na kuvumilia njaa iliyokuwa ikimbana wakati huo. 
    Alianza kujuta kwa kutofuata mawaidha aliyopewa na wazazi wake. Alifikiri, 
    “Nisingepuuza mawaidha ya baba yangu, nisingekutana na matatizo haya”. 

    Walipofika Dar-es-salaam, walifurahi kuonana na shangazi na binamu zake. 
    Walipokelewa vizuri na kupata muda wa kutembelea mazingira mazuri ya jiji 
    hilo. Tangu alipofika, Petro alifuatana na binamu zake kila wakati walipotoka 
    kununua vitu ili asikilize walivyoweza kuwasiliana na watu wengine katika 
    lugha ya Kiswahili. Hapo, aliweza kuelewa umuhimu wa kujifunza lugha na 
    aliamua kwamba angeanza kujifunza kwa bidii mara wakirudi nyumbani. Kwa 
    sasa, Petro amemaliza kidato cha tatu katika shule ya Sekondari ya Museta 
    ambapo walimu wake wanampenda kwa uwezo wake wa kuzungumza lugha 
    ya Kiswahili na lugha nyingine anazojifunza. 
    Kazi ya 2:
    Maswali ya Ufahamu
    1. Taja majina ya watu wanaozungumziwa katika kifungu hiki.
    2. Ni mawaidha gani mzee Yakobo aliyokuwa anawapa watoto 
    wake ?
    3. Maria amefaidika vipi kutokana na ujuzi wake wa lugha 
    mbalimbali ?
    4. Safari ya mzee Yakobo ilikuwa na lengo gani ?
    5. Ni hasara gani aliyoipata Petro aliposhindwa kuwasiliana na 
    mfanyabiashara ?
    6. Eleza tabia za mfanyabiashara Bi Hassani mbele ya mteja wake. 
    7. Ni jambo lipi lingetokea ikiwa mzee Yakobo hakumkataza mtoto 
    wake Petro kula chakula alichokinunua ? 
    8. Petro alikuwa na majuto gani? Kwa nini alijuta?
    9. Aliporudi nyumbani alifanya nini?
    10. Unajifunza nini kutokana na kifungu hiki cha habari?
    31.2. Msamiati kuhusu umuhimu wa lugha
    Kazi ya 3:
    Tunga sentensi sahihi kwa kutumia maneno yafuatayo huku ukizingatia 
    matumizi yake katika kifungu cha habari ulichosoma hapo juu.

    1. Kuhimiza
    2. Madhumuni
    3. Mawaidha
    4. Mtazamo
    5. Mtukutu
    6. Utalii 
    7. Kwenda haja
    8. Kwa shingo upande
    9. Bidii

    10. Bumbuazi

    Kazi ya 4:

    Oanisha maneno katika sehemu A na maana zake zilizopo katika sehemu B.

    cc

    Kazi ya 5:
    Jaza nafasi kwa kutumia maneno mwafaka yafuatayo: bidii, 
    madhumuni, kupuuza, maarufu, mawaidha, mtazamo, bumbuazi, 
    ratiba, kwenda haja, shingo upande.

    1. Nilianzisha mradi huu kwa ...................................ya kuhifadhi 
    mazingira yetu.
    2. Kila mwanafunzi analazimishwa kuwa na .........................ya 
    masomo yake ya kila siku.
    3. Usipojifunza kwa............................. basi hutafaulu mitihani yako. 
    4. Aliposikia habari hiyo alipigwa na ............................... na kukosa 
    la kufanya.
    5. Anaanza kujuta kwa kutofuata ....................................ya baba 
    yake.
    6. Baada ya kufanya safari ndefu, wasafiri wamesimamisha dereva 
    ili waweze ....................
    7. Sikubaliani na ...............................wako kuhusu uhifadhi mwafaka 
    wa mazingira.
    8. Alipokea zawadi hiyo kwa.................................................
    9. Amekuwa mchezaji.....................................kutokana na ustadi 
    wake wa kusakata mpira.
    10. Si vizuri ...............................fikra za mwenzako kabla hujamsikiliza.
     31.3. Sarufi: Matumizi ya hali ya kuamuru
    Kazi ya 6:
    Soma kifungu cha habari kifuatacho na kubainisha vitenzi 
    vilivyotumiwa katika hali ya kuamrisha

    Ona kwenye gazeti hili viongozi wa mataifa mbalimbali wamekusanyika 
    mjini Kigali. Lengo lao ni maendeleo ya lugha yetu. Soma habari yote 
    uelewe vizuri yanayoendelea pale na usiendelee kusimama kwenye 
    barabara. Kimbia nyumbani uwashe runinga yako ili uweze kuwaona 
    na uandike matangazo hayo kwa ufupi. Lakini jaribu kujifunza Kiswahili 
    kitakuwezesha kushirikiana na jamii, nchi zote za kanda hii hasa hasa 
    Jumuiya yetu ya Afrika Mashariki kwani Kiswahili ni lugha rasmi.

    Kazi ya 7:
    Tunga sentensi tano zenye vitenzi mbalimbali katika hali ya kuamuru.
    Kazi ya 8:

    Tazama picha hizi kisha utunge sentensi katika hali ya kuamuru 

    kulingana na vitendo vinavyoendelea kwenye picha hizi:

    cc

    Kazi ya 9:
    Andika vitenzi vilivyopigiwa msitari katika hali ya kuamuru tungo 
    yakinishi na kanushi:
    Nchi yetu ni nzuri sana,ina milima na mabonde,viongozi bora na sehemu 
    mbalimbali za utalii. Mutesi hutembelea maziwa mengi naye Bugingo 
    husafisha kwake akipanda maua na miti ili kuhifadhi mazingira. Yeye 
    huwazuru wenzake akiwashawishi watende mema kila siku. Benita 
    aliamua kujenga nchi yake kwa kufanya kazi za umuganda, vilevile 

    akiwajengea wasiojiweza na kutengeneza barabara.

    Kazi ya 10:
    Weka sentensi zifuatazo katika hali ya kuamuru katika umoja na 
    kuzingatia mabadiliko ya kisintaksia katika sentensi. 

    a. Sauti ya pili,ingieni tuimbie Bwana.
    b. Teteeni maendeleo ya lugha ya kiswahili.
    c. Kuleni nyama yote pia osheni vyombo.
    d. Lieni kwa sauti ndogo majambazi yasituvamie.
    31.4. Matumizi ya lugha: Umuhimu wa lugha
    Kazi ya 11:
    Soma maelezo yafuatayo, kisha ujibu maswali hapo chini.
    Maelezo muhimu: Umuhimu wa lugha
    Lugha ni mojawapo ya vipengele vya utamaduni wa jamii na tena ni chombo 
    cha utamaduni. Hili ni kwa sababu chombo hiki hutumiwa kuwasilisha amali, 
    mila na desturi zote za jamii. Lugha ndio uti wa mgongo wa utamaduni. 
    Lengo kuu la lugha katika jamii ni pamoja na kuwafanya watu wawasiliane 
    kwa kupashana habari. Kujua lugha fulani kunamwezesha mtu kujipatia 
    marafiki, kukuza ujuzi kwa kusoma maandishi mbalimbali au kwa kufuata 
    vipindi mbalimbali kwenye redio, runinga na tovuti

    Kutumia lugha moja katika jamii kunaweza kuwa na faida pamoja na 
    hasara mbalimbali kutokana na mazingira ya jamii. Rwanda kama nchi 
    inayozungukwa na nchi zinazotumia Kiswahili, itanufaika kwa kutumia 
    lugha ya Kiswahili. Vilevile, lugha ya Kiswahili ina umuhimu mkubwa sana 
    katika Jumuiya ya Afrika Mashariki kwa kuwa lugha hii ndiyo lugha rasmi 
    inayotumiwa katika Jumuiya hii.
    Maswali:
    1. “Lugha ndio uti wa mgongo wa utamaduni.” Eleza.
    2. Lipi ni lengo kuu la kuijua lugha?
    3. Jadili: “Kutumia lugha moja katika jamii kunaweza kuwa na faida 
    pamoja na hasara mbalimbali”.

    31.5. Kusikiliza na Kuzungumza: Majadiliano
    Kazi ya 12:

    Jadili kuhusu mambo yafuatayo: 
    1. Matatizo yawezayo kujitokeza baina ya watu wawili wanaposhindwa 
    kusikilizana kimawasiliano
    2. Umuhimu wa lugha katika jamii 
    3. Mambo mbalimbali yanayoweza kukwamisha mawasiliano yenye 
    kutumia lugha
    31.6. Kuandika: Utungaji wa kifungu cha habari
    Kazi ya 13:
    Kwa kutoa hoja zenye mifano, tunga kifungu chako kwa kutumia 
    mada ifuatayo: 

    “Lugha inapotumiwa vizuri hujenga jamii na ikitumiwa vibaya huangamiza 
    jamii”.
    Kazi ya 14:
    Chagua mada moja kati ya hizi zifuatazo na kuzitungia insha 
    isiyopungua maneno 100.

    • Lugha ni kitambulisho cha jamii
    • Lugha hurahisisha mawasiliano katika jamii
    • Lugha hukuza utamaduni
    • Lugha huburudisha

    Tathmini ya mada
    Jibu maswali yote.

    1. Je, ushirikiano wa Rwanda pamoja na nchi nyingine za kikanda 
    ulisaidia nini Kiswahili?
    2. Toa lugha rasmi nchini Rwanda.
    3. Ni vituo gani vya utangazaji habari vinavyotumia Kiswahili katika 
    baadhi ya matangazo vinavyorusha?
    4. Fafanua maneno haya: - Malighafi, chatu, mawaidha.
    5. Jaza sentensi zifuatazo kwa kutumia neno lililo mabanoni:
    i. “…………… kazi yako ya shule kuhusu dhima ya kiswahili!”. 
    Mama alimuamrisha mtoto wake (kurekebisha).
    ii. Mwalimu alimwomba mwanafunzi akisema: “…………… kurasa 
    mbili za kifungu!”(Kuandika).
    iii. Baada ya kujiunga na nchi nyingine za Afrika Mashariki viongozi 
    wa Rwanda walituambia: “……… Kiswahili!” (jifunza)

    6. Onyesha umuhimu wa lugha ya Kiswahili katika jamii.

    MAREJEO
    1. Ntawiyanga, S. na Wenzake (2016). Kiswahili kwa Shule za Rwanda, 
    Kidato cha Kwanza. Longhorn Publishers (K) Ltd.
    2. Ndalu, A. E. (2016). Masomo ya Kiswahili Sanifu, Kidato cha 2. Moran 
    (E.A.) Publishers Ltd.
    3. Rwanda Education Board (2019). Kiswahili kwa Shule za Rwanda, 
    Mchepuo wa Lugha, Kidato cha 4. Rwanda Education Board.
    4. Rwanda Education Board (2019). Kiswahili kwa Shule za Rwanda, 
    Michepuo Mingine, Kidato cha 6. Rwanda Education Board.
    5. TUKI (2004). Kamusi ya Kiswahili Sanifu, Toleo la Pili. Oxford University 
    Press.
    6. NKWERA, F.M.V. (1979). Sarufi na Fasihi, Sekondari na Vyuo. Tanzania 
    Publishing House Dar-es-salaam, Tanzania.
    7. https://sw.wikipedia.org/wiki/Kito_(madini)
    8. ;
    9. ;
    10. http://swa.gafkosoft.com/maigizo

    11. https://www.facebook.com/1416762588414463/posts/hali-yakuamuru-hali-hii-ilichambuliwa-kwenye-tawi-la-mutanga-jumapili-hiikidat/1823486384408746