Topic outline

 • Label: 1
 • Tazama mchoro huu kwa makini, kisha ujishughulishe na mazoezi yanayofuata.

  kj

  Zoezi la 1: Chunguza mchoro huu, kisha ueleze unayoyaona yanayohusiana na

  usafi.

  2.1. Kusoma na Ufahamu: Umuhimu wa Usafi wa Mazingira Hospitalini

  Soma kifungu cha habari kuhusu “Umuhimu wa Usafi wa Mazingira Hospitalini” ili

  ujibu maswali uliyopewa.

  Usafi wa mazingira ni jambo ambalo linafaa kutiliwa maanani na kila mtu kwani

  uchafu unachangia pakubwa kuharibu maisha ya binadamu yeyote yule. Jambo la

  kusikitisha ni kwamba watu wengi hujitahidi kuwa safi kwenye miili na mavazi yao

  tu huku wakisahau kuwa usafi huhusu kila kitu kinachopatikana katika mazingira

  wanamoishi. Watu wengi wangeliepuka na kupatwa na magonjwa mbalimbali

  yanayotokana na uchafu kama wangelizingatia usafi wa mazingira yao.

  Tunapozungumzia usafi hospitalini, watu wengi huelewa shughuli muhimu

  zinazostahili kufanywa katika kusafisha vyumba vya wagonjwa na kutengeneza

  bustani zinazozunguka hospitali hiyo.

  Lakini, ni lazima kujua kwamba usafi hospitalini huchunguzwa kupitia vifaa

  vinavyotumiwa, dawa zinazotunzwa na kupewa wagonjwa, mahali pa kutolea

  huduma tofauti, usafi wa wagonjwa na hata watumishi wote wanaoshughulikia na

  kuhudumia wagonjwa hao na watu wengine wanaofika kwenye hospitali hiyo.

  Mazingira ya hospitali huweza kusafishwa kwa kutumia dawa za kuulia wadudu

  wenye kuambukiza watu magonjwa mbalimbali. Ufikapo katika hospitali yoyote

  hutakosa kuwakuta watumishi wanaopiga deki na kusafisha mazingira mengine

  ya hospitali hiyo. Watu hawa nao huvaa bwelasuti ili waweze kujikinga uchafu na

  huhakikisha kuwa vyoo vinavyotumiwa ni safi kwa kuwaonya wagonjwa wasitupe

  uchafu ovyoovyo. Kama vyoo havisafishwi vizuri, nzi huweza kujitafutia makazi

  yao humo na kusambaza magonjwa mbalimbali kama vile kipindupindu ambacho

  ni ugonjwa hatari. Wadudu hawa huweza kugusa kinyesi cha mgonjwa na kutua

  kwenye chakula cha watu wazima na kuwaambukiza ugonjwa huo.Wadudu wengine

  hatari kwa maisha ya watu ni kama kombamwiko na viroboto ambao hupatikana

  jikoni, mahali ambapo chakula hutayarishiwa.

  Taka zote zinazotokana na vitu vyote vilivyotumiwa zinafaa kutupwa mahali

  panapofaa kama vile jalalani au zikachomwa. Nyasi nazo zinazozunguka hospitali

  zetu zinafaa kukatwa ili kuwafukuza mbu wanaosababisha ugonjwa wa malaria.

  Panya wanaobeba viroboto wanaosababisha ugonjwa wa tauni hujificha humo pia.

  Aidha, nyoka wanaweza kujificha humo na kutambaa hadi vyumbani. Mikebe na

  chupa zilizotumiwa zinafaa kutupwa shimoni na kufukiwa ili kuzuia mbu kuzalia

  ndani mwake na viluwiluwi vyake kukulia humo, hasa maji ya mvua yanapoingia

  kwenye vyombo hivyo.

  Hali hii ya usafi wa mazingira ya hospitali inafaa kuzingatiwa ili kuzuia magonjwa

  yanayoweza kujitokeza. Shughuli za usafi ni nyingi na kila mtu anayefika hospitalini

  ni lazima ajaribu kuimarisha usafi katika mazingira anamoingia. Wagonjwa na watu

  wote wanaowaangalia au kuwasaidia wanapaswa kutunza usafi kila mahali walipo

  kwa manufaa ya watu wanaoishi katika maeneo hayo. Wauguzi na madaktari pamoja

  na wafanyakazi wote lazima wachunguze kama usafi umezingatiwa katika hospitali

  nzima.

  Maswali ya ufahamu

  1. Chagua jibu moja kati ya haya. Mazingira ni:

  a. Sehemu ya nje au ya ndani ya nyumba iliyotengenezwa maalumu kwa watu

  kukaa na kuzungumza.

  b. Hali au mambo yanayomzunguka kiumbe katika sehemu anapoishi au

  maisha yake.

  c. Sehemu ambapo kitu au mtu huweza kukaa.

  2. Usafi wa mazingira unachangia nini katika maisha ya binadamu?

  3. Usafi wa mazingira utatusaidiaje kutumia rasilimali zetu vizuri?

  4. Wadudu hawa husababisha magonjwa yapi?

  1. nzi

  2. mbu

  6. Ugonjwa wa kipindupindu husababishwa na nini?

  7. Ni nini maana ya maneno haya kama yalivyotumiwa katika kifungu?

  1. jalala

  2. bwelasuti

  8. Taja wadudu wengine wanne uwajuao wanaosababishwa na uchafu.

  2.2. Msamiati kuhusu Usafi Hospitalini

  1. Kutiliwa maanani

  2. Kupiga deki

  3. Huduma

  4. Kuambukiza

  5. Kipindupindu

  Zoezi la 3: Oanisha maneno katika kundi A na maana yake kutoka kundi B.

  j

  Zoezi la 4: Kamilisha sentensi zifuatazo kwa kutumia maneno yafuatayo

  (viroboto, bwelasuti, mbu, huchangia parefu, viroboto wa panya, vifaa, nyasi,

  nyoka, wangezingatia, nzi):

  1. Usafi wa mazingira.........................kurefusha umri wa kuishiwa binadamu.

  2. Watu wengi wangeelimishwa vizuri, .....................usafi wa mazingira, .

  3. Ni lazima.................vya.hospitalini visafishwe vizuri.

  4. Mara nyingi wadudu kama ................na hujenga makao yao sakafuni.

  5. Watu wanapaswa kuvaa .................................. ili waweze kujikinga na

  uchafu.

  6. .................................zinafaa kukatwa ili kuwafukuza mbu wanaosababisha

  ugonjwa wa malaria.

  7. Wadudu wanaosababisha ugonjwa wa tauni huitwa .....................................

  8. ........................................ni mnyama anayetambaa ambaye hujificha nyasini.

  Zoezi la 5: Wanafunzi wawili wawili, tajeni majina ya vifaa vifuatavyo ambavyo

  hupatikana katika mazingira ya hospitali pamoja na umuhimu wake.

  k

  2.3. Sarufi: Matumizi ya Kiambishi -ngeli-

  Zoezi la 6: Andika upya sentensi zifuatazo kwa kutumia kiambishi -ngeli- badala

  ya kiambishi -nge-. Fananisha sentensi unazozipata na sentensi za awali.

  Mfano: Sisi tungeshirikiana ipaswavyo, tungejenga nchi imara

  Sisi tungelishirikiana ipaswavyo, tungelijenga nchi imara.

  • Sentensi hizi ingawa zinatumia -ngeli- badala ya -nge- hazitofautiani kimaana

  na zile za awali.

  1. Wanafunzi wangesoma vizuri, wangefaulu mtihani wa taifa.

  2. Mungu huwapenda watu; asingewapenda, asingewaumba.

  3. Tusingeandika vitabu, tusingepata vitabu vya kufundishia.

  4. Wao wangekuwa Wakristo, wangewasaidia walemavu.

  • Kiambishi -ngeli- kinaweza kutumiwa katika hali kanushi na vilevile katika hali

  yakinishi.

  l

  Tanbihi: Katika matumizi ya kiambishi hiki, tunaweza kukanusha kwa kutumia kikanushi

  -si- kama ilivyoonyeshwa kwenye mifano hapo juu

  Chunguza maelezo muhimu kuhusu matumizi ya kiambishi -ngeli-

  Kiambishi -ngeli ni kiambishi ambacho hutuarifu juu ya hali ya masharti.

  Kinapotumiwa humaanisha kuwa tendo moja ni lazima lifanyike ndipo tendo jingine

  nalo lifanyike.

  Hali kadhalika, kiambishi nge hutumiwa kuonyesha majuto au kuwa kama tendo

  fulani halifanyiki, tendo jingine nalo haliwezi kutokea. Lakini katika hali hii ya mwisho

  tunaelewa kwamba kuna uwezekano wa kufanyika kwa tendo hilo na kisha jambo

  hilo nalo litokee.

  Katika hali ya kuonyesha uwezekano

  Mifano:

  • Ningelikuwa na pesa, ningelimjengea mzazi nyumba nzuri. Maana yake ni kuwa

  mimi sina pesa wala sikujengea mzazi nyumba nzuri, lakini nikipata pesa sasa hivi

  ninaweza kumjengea nyumba nzuri.

  • Ningelimjua msichana yule, ningelimshauri kuacha tabia mbaya. Maana yake ni

  kwamba simjui msichana yule, lakini kumjua kwangu kwasababisha kumpa ushauri

  wa kuacha tabia yake mbaya.

  Katika hali ya kuonyesha majuto

  Mifano:

  1. Ningelikuwa msichana mwenye moyo wa utulivu, ningelijilinda kujiunga na

  vijana wenye tabia mbaya za uasherati.

  • Maana yake ni kuwa mimi sikuwa msichana mwenye moyo wa utulivu ijapokuwa

  ningelihitaji kuwa msichana mwenye moyo wa utulivu ili nijiepushe na urafiki na

  vijana wenye tabia mbaya za uasherati, lakini ninajuta kwa sababu sikuweza kuwa

  na moyo wa utulivu.

  2. Ningelikuwa mkristo wa kweli, ningeliacha kuvuta sigara au kuchukua dawa za

  kulevya ambazo zimeniharibia afya.

  • Maana yake ni kuwa mimi si mkristo wa kweli na ninajuta kuwa uvutaji wa sigara

  na kuchukua dawa za kulevya kumeniharibia afya.

  Zoezi la 7: Zikamilishe sentensi zifuatazo ili zilete maana kamili

  Mifano: - Angelikuwa mfalme, angeliishi raha mustarehe.

  - Asingelikuwa mfalme, asingeliishi raha mustarehe.

  1. Chumba hiki kingelikuwa kikubwa, …………………....………..…….....

  2. Chumba hiki kisingelikuwa kikubwa, …………………………..................

  3. Wali usingelikuwa mtamu, ……………………………….............................

  4. Minazi ingelizaa madafu mengi, …………………………….......................

  5. Minazi isingezaa madafu mengi, ……………………………………........

  6. 6. Mwanafunzi angelisoma kwa bidii, ……………………………….........

  7. 7.Ningelikuwa daktari, .......…………………………………..........................

  8. 8. Tungelikuwa na pesa, …………………………………………................

  9. 9. Ungelikuwa na ujuzi kamili, ……………………………….......................

  10. Wapishi wangelikuwa na viungo, ………....……………..................................

  2.4. Matumizi ya Lugha

  Zoezi la 8: Chagua maneno haya kufuatana na maana zake na kuyaandika katika

  makundi yake halisi.

  k

  Zoezi la 9:Oanisha maneno yafuatayo hapo chini na maana zake:

  j

  2.5. Kusikiliza na Kuzungumza: Majadiliano na Mawasilisho

  Zoezi la 10: Soma kifungu kuhusu “Umuhimu wa Usafi wa Mazingira Hospitalini”,

  kisha uwasilishe mawazo makuu hadharani.

  2.6. Kuandika: Utungaji wa Kifungu

  Zoezi la 11: Tunga kifungu kifupi kuhusu umuhimu wa usafi hospitalini kwa

  kutumia maneno yafuatayo: (usafi, kuhara, wadudu, vyoo, mazingira, uchafu).
  • Zoezi la 1: Tazama mchoro ufuatao kisha ueleze vitendo vinavyofanywa na watu

   waliopo katika mchoroi.

   kj

   3.1. Kusoma na Ufahamu: Maelekezo na Kanuni Hospitalini

   Soma kifungu cha habari kinachofuata kuhusu maelekezo na kanuni zinazofaa

   kuzingatiwa hospitali, kisha jibu maswali yanayofuata hapo chini.

   Jina langu ni Mugisha juzi nilikuwa ninahisi homa kali.Hivyo nilienda katika hospitali

   moja iliyopo mjini Rubavu. Nilikuwa na ndugu yangu mdogo Semana aliyekuwa

   amenisindikiza hospitalini. Wakati nilipokuwa nangoja usaidizi wowote kutoka kwa

   daktari, nikikaa kwenye benchi moja mbele ya ofisi yake, nililiona tangazo lililokuwa

   limebandikwa kwenye ukuta na kumwomba ndugu yangu anisomee kilichoandikwa

   pale. Nilihofia kuvunja sheria yoyote ya hospitali kutokana na kutosoma kile

   kilichoandikwa.. Ndugu yangu alikubali kunisomea. Hivyo alianza kunisomea

   tangazo hilo kuanzia mwanzo hadi mwisho. Tangazo lilisomeka ifuatavyo:

   Kwa manufaa ya wagonjwa na watu wengine wanaotembelea mazingira ya hospitali

   hii, uongozi wa hospitali hii unataka kuwajulisha mambo yafuatayo:

   1. Wagonjwa wanapaswa kuonyesha maadili mema ya kuwaheshimu wenzao

   pamoja na wafanyakazi wa hospitali.

   2. Inakatazwa kugombana, kutukana, kuiba na kuwadharau watu wengine.

   3. Mtu yeyote wa nje haruhusiwi kuingia katika kungawi wala chumba cha

   upasuaji.

   4. Kila mgonjwa inambidi aheshimu masharti ya daktari ya kutumia dawa

   kama ilivyoagizwa.

   5. Usafi ni msingi wa afya. Mazingira yatahifadhiwa ipaswavyo na kila mtu

   anapaswa kuwajibika katika utunzaji wa usafi kila mahali alipo.

   6. Ni mwiko kuvuta sigara katika eneo la hospitali.

   7. Wagonjwa waliolazwa hospitalini na wengine wanaowahudumia

   wanaombwa kutopiga kelele wakiwa katika wodi.

   8. Hairuhusiwi kamwe kuingiza na kutumia pombe pamoja na dawa za kulevya

   katika eneo la hosptitali.

   9. Mienendo mibaya isiyoendana na maadili mema imepigwa marufuku katika

   eneo la hospitali.

   10. Kila mtu anatakiwa kuwa na moyo wa huruma kwa kusaidia wale

   wasiojiweza na wenye udhaifu.

   Mimi nilifurahia maonyo na mawaidha hayo yaliyotolewa na Dakatari Mkuu wa

   hospitali. Zamu yangu ilifika nikaingia kwa daktari na nikahudumiwa vizuri. Baada

   ya kupewa dawa, nilianza kutembea kuelekea nyumbani. Ghafla nilisikia sauti za

   watu wengi: «Piga…, jichoni, mtupe chini wee…, ngumi nyingine!…». Nilipogeuka

   kuangalia nini kilikuwa kikiendelea pale sikuamini macho yangu! Vijana wawili

   walikuwa wanapigana! Nilisikitika sana na kumwambia ndugu yangu, «Kwa nini watu

   wengine wanawatazama bila kuwatenganisha ili wasiendelee kugombana? Kwa

   kweli, watu hao wangaliwa amua kabla ya kupigana, wasingaliweza kuumizana».

   Mmoja alikuwa amemuumiza mwenzie vibaya sana akisingizia kuwa amemwibia

   chupa ya pombe.

   Baada ya muda, Polisi waliitwa ili kutatua tatizo hili. Ilibidi kwanza vijana hao

   watibiwe majeraha waliyokuwa nayo usoni na miguuni kabla ya kuwapeleka kwenye

   kituo cha polisi ili kuwahoji kuhusu ugomvi wao. Hapo niliendelea kumwambia

   ndugu yangu, «Kwa nini vijana hawa watumie nguvu zao kwa kupigana badala ya

   kuzitumia kwa kuzalisha mali? Wangalisoma tangazo la Daktari Mkuu wa Hospitali

   hii kuhusu maadili mema, wasingalishambuliana namna hii! Wao walikiuka maagizo

   yaliyotolewa na kuvunja kanuni za hospitali».

   Mimi na ndugu yangu tuliendelea na safari yetu ya kurudi nyumbani na kushauriana

   kuhusu maadili na mienendo mizuri inayofaa kumtambulisha kila mgonjwa na mtu

   yeyote anayetembelea mazingira ya hospitali. Tulifurahia jinsi uongozi wa hospitali

   yetu ulivyotilia mkazo kuwahimiza watu kuwa na maadili na mienendo mizuri. Tangu

   siku hiyo, niliamua kuwaonya watu wote waheshimiane na kuzingatia maagizo

   ya Madaktari wetu ili wasipate adhabu zisizostahili. Ndugu yangu naye aliendelea

   kwa kusema,»Vijana wale wasingaligombana, wasingalipelekwa kituo cha polisi

   kuadhibiwa.»

   Maswali ya ufahamu

   1. Taja watu wanaozungumziwa katika kifungu hiki.

   2. Watu hawa walikuwa wapi?

   3. Tangazo linalozungumziwa linahusu nini?

   4. Tangazo hilo lilikuwa wapi? Ni nani aliyelisoma?

   5. Taja vitu angalau vitano ambavyo haviruhusiwi hospitalini.

   6. Unadhani ni kwa sababu gani mtu yeyote wa nje haruhusiwi kuingia katika

   kungawi wala chumba cha upasuaji?

   7. Ni kitu gani kilichosababisha vijana wawili kugombana?

   8. Wao walivunja sheria zipi kutokana na tangazo la Daktari Mkuu?

   9. Vijana hao waliamuliwa nini kutokana na ugomvi wao?

   10. Ni jambo gani linalokudhihirishia kuwa Mugisha alisikitishwa na mapigano ya

   vijana hao?

   11. Kwa nini Mugisha na nduguye walifurahia uongozi wa hospitali yao?

   12. Ni maonyo gani anayoyatoa ndugu yake Mugisha ili watu wasipate adhabu

   zisizostahili?

   3.2. Msamiati kuhusu Adabu Hospitalini

   Zoezi la 2: Eleza maana ya maneno yafuatayo na baadaye uyatumie kwa kuunda

   sentensi zenye maana:

   1. Mwiko                            5. Afya

   2. Marufuku                        6. Mhudumu

   3. Benchi                             7. Kujeruhi

   4. Ghafla                               8. Kugombana

   Zoezi la 3: Jaza sentensi zifuatazo kwa kutumia maneno uliyopewa: kupiga kelele,

   heshima, kuvunja sheria, maadili mema, kugombana, kuheshimu.

   1. Kila mtu anapaswa kuwa na hofu ya .............................................mahali popote

   alipo.

   2. Mtoto huyu anafurahisha kwa sababu anaonyesha .....................................kwa watu

   wakubwa.

   3. Mgonjwa alipewa ushauri kuhusu.......................................... na daktari alipokuwa

   hospitalini.

   4. Unapokuwa katika wodi unakatazwa .........................................kwa sababu kuna

   wagonjwa ambao wako katika hali mbaya.

   5. .......................................... ni kufanya matata kwa kutoa maneno makali.

   Zoezi la 4: Jaza sentensi zifuatazo kwa kutumia maneno kutoka kifunguni

   : sheria, kuvuta, hawakuwatenganisha, pombe, benchi, wasingalipigana,

   kuhudumiwa, kutazama.

   1. Vijana wawili walipokuwa wanapigana watu .....................................................

   .....

   2. Wagonjwa sana huhitaji ..............................................................................................

   ......

   3. Si vizuri ................................................tu watu wanapopigana.

   4. Vijana wawili waliingiza .........................................................................hospitalini.

   5. Vijana wake wawili wangalisoma tangazo lile, ....................................................

   6. Nchini Rwanda hairuhusiwi .................................sigara mahali ambapo

   hukutania watu wengi.

   7. ...................................................ni kifaa cha kukalia.

   8. Wagonjwa waliopigana hawakujua .........................................................................

   za hospitali.

   Zoezi la 5: Jaza jedwali lifuatalo kufuatana na mada zilizotolewa hapa chini:

   j

   3.3. Sarufi: Matumizi ya Kiambishi chenye Dhana ya Masharti -ngali-

   Zoezi la 6: Jadilini kuhusu matumizi ya -ngali-katika sentensi zinazofuata:

   1. Ninyi mngalikuwa na muda wa kutosha, tungalizungumzia mengine mengi

   kuhusu adabu.

   2. Watoto wale wangalijifunza vizuri, wangalipewa zawadi nyingi.

   3. Wanafunzi wasingalikuwa na alama za kutosha, wasingalifanya mtihani wa

   taifa.

   4. Sisi tusingalifika mapema, tusingalifanya kazi nyingi.

   Linganisheni maoni yenu kutoka makundi tofauti na maelezo hapa chini.

   Viambishi -nge-, na -ngeli-: mzungumzaji au mwandishi anaweza kuvitumia katika

   nafasi ya kiambishi -ngali- katika nyakati tofauti. Viambishi hivi hubeba dhana

   ya masharti. Dhana hii inalifanya tendo fulani litegemee tendo jingine katika

   kutendeka kwake. Kwa mfano, kama umetumia -ngali- katika sehemu ya kwanza ya

   sentensi yako endelea kutumia pia -ngali- katika sehemu ya pili. Ndani ya sentensi

   zinazobeba hali ya masharti, ni lazima kuelewa maana ya sentensi nzima kutokana

   na kutegemeana kwa vitendo. Ikumbukwe kuwa viambishi vya hali ya masharti

   hutumiwa katika hali yakinishi na hali kanushi. Katika hali kanushi -si- huwekwa

   baada ya kiambishi nafsi cha kitenzi cha hali yakinishi.

   Zoezi la 7: Kamilisha sentensi zifuatazo ili zilete maana kamili.

   1. Raia wote wangalifuata mashauri ya usafi na kuhifadhia mazingira,

   magonjwa yanayosababishwa na uchafu ………..........................................

   sana.

   2. ………………………………………..., tusingalipata hasara hii.

   3. Ningaliepuka unyanyasaji wa kijinsia dhidi ya mke wangu, …………….

   msiba huu.

   4. Nisingaliponda mali yangu yote katika mahitaji yasiyo muhimu,

   .....................

   5. Serikali ya Rwanda isingalichukua mikakati thabiti kuhusu unyanyasaji

   wa kijinsia, ................

   6. Wangalijua nia yangu katika kutetea haki za wanawake, ..............................................

   7. Ungalionana na daktari, .............................................................................................................

   8. Vijana wangaliepuka dawa za kulevya, bila shaka ...........................................................

   9. Barabara zote zingalikuwa za lami, kila eneo nchini Rwanda .....................................

   Zoezi la 8: Kanusha sentensi zifuatazo:

   1. Tungalipanda miti ya kutosha, tungalizuia mmomonyoko kupasua

   mlima huu.

   2. Bwana yule angalijua usawa wa kijinsia, angalikuwa na maendeleo katika

   familia yake.

   3. Ungalikuwa na moyo wa kiutu, ungalimhudumia mwanafunzi mlemavu yeyote

   darasani.

   4. Wanafunzi wangalisoma kwa bidii , wangalishinda mitihani kwa urahisi.

   3.4. Matumizi ya Lugha: Msamiati wa Adabu

   Zoezi la 9: Yafuatayo ni baadhi ya maneno ya adabu yanayoweza kutumiwa

   nyumbani, shuleni au sokoni. Tunga sentensi moja kwa kila neno.

   1. Tafadhali

   2. Asante

   3. Samahani

   4. Karibu!

   5. Shukrani

   6. Naomba

   7. Pole

   8. Hodi!

   9. Shikamoo!

   10. Maraha

   Mienendo mizuri hospitalini humtaka kila mtu azingatie mambo yafuatayo:

   •Kuonyesha maadili mema;

   •Kuwaheshimu wengine pamoja;

   •Inakatazwa kugombana, kutukana, kuiba na kuwadharau wengine, kuvuta sigara;

   •Kuheshimu masharti ya daktari na wafanyakazi wa hospitali

   •Kuwa na usafi;

   •Kutopiga kelele katika wodi;

   3.5. Kusikiliza na Kuzungumza: Majadiliano

   Zoezi la 10: Jadili mada zifuatazo:

   1. Namna watoto wanaweza kuimarisha adabu mbele ya wazazi

   nyumbani kwao.

   2. Adabu ni msingi wa uhusiano mwema kati ya mtu na mtu mwingine.

   Eleza.

   3.6. Kuandika: Sifa za Aya katika Uandishi

   Zoezi la 11: Kila mwanafunzi aandike mambo muhimu matatu ya kuzingatiwa

   katika kukuza adabu hospitalini na kuyajadili katika aya tatu

   TATHMINI KUHUSU MADA YA KWANZA

   Jibu maswali yafuatayo:

   1. Taja anghalau vitu vitano muhimu vinavyopatikana katika mazingira ya hospitali

   au zahanati.

   2. Taja sehemu tatu za hospitali na kueleza shughuli zinazofanyiwa katika sehemu

   hizo.

   3. Eleza majukumu ya wafanyakazi angalau wanne wanaopatikana hospitalini.

   4. Thathmini shughuli za kuboresha usafi zinazofanywa katika moja ya hospitali

   ulizowahi kutembelea.

   5. Jadili mwenendo unaofaa katika mazingira ya hospitali au zahanati kwa mijajili ya

   kujilinda na magonjwa.

   6. Kwa kutumia viambishi nge, ngeli au ngali, andika aya nne kwa kujadili hasara

   zinazoweza kujitokeza kutokana na matumizi ya taulo moja kwa watu zaidi ya

   mmoja; kisha, toa suluhisho ili kuepukana na madhara yanayoweza kujitokeza.