Topic outline

  • MADA YA 1: UANDISHI WA BARUA ZA KIRAFIKI, MWALIKO NA MATANGAZO

    Uwezo mahususi
    Kuandika barua za kirafiki, mwaliko na matangazo kwa watu mbalimbali

    Malengo ya ujifunzaji

    - Kutaja sehemu kuu za barua za kirafiki, mwaliko na matangazo 
    - Kuchunguza muundo wa barua za kirafiki, mwaliko na matangazo
    - Kutofautisha aina za barua za kirafiki, mwaliko na matangazo 
    - Kuelezea lugha inayofaa kutumiwa katika uandishi wa barua za kirafiki, 
    mwaliko na matangazo
    - Kutunga barua za kirafiki kwa watu mbalimbali, barua za mwaliko na 
    matangazo ya aina tofauti
    - Kuonyesha adabu na hehima kwa watu anaowaandikia

    - Kueleza matumizi ya aina za maneno

    KIDOKEZO
     Tazama kwa makini mchoro ufuatao kisha ujibu maswali  
    yaliyotolewa hapo chini:
    d

    Jibu maswali yafuatayo
    -- Ni nini unachoona kwenye mchoro?
    -- Ni mambo gani tunayotumia kwa kuwasiliana kimaandishi?
    SOMO LA 1: BARUA YA KIRAFIKI
    1.1. Kusoma na ufahamu: Wema Hauozi

    Soma barua ifuatayo kisha ujibu maswali ya ufahamu.


    Chuo cha Ualimu cha Amahoro
    S.L.P. 100,
    NGORORERO
    16/11/2019
    Mpendwa Amina,
    Salamu!
    Ninakuandikia waraka huu nikiwa nimejaa furaha ghaya kama mzazi aliyejifungua
    pacha salama salimini. Wewe u mzima? Wazazi wako hawajambo ? Nasi hapa
    nyumbani kwetu Ngororero mambo ni shwari.

    Nia yangu ya kukuandikia barua hii ni kukushukuru kwa dhati ya moyo wangu.

    Zaidi ya hayo ni kule kunialika kuja katika harusi ya dada yako huko kwenu. Harusi
    ile ilikuwa ya kukata na shoka kabisa. Ilinivutia sana, hasa nilivyoona kwamba
    harusi yenyewe ilionyesha utamaduni wetu wa Wanyarwanda bila kuchanganya
    mambo ya kizungu. Hilo ni jambo nadra sana siku hizi wakati ambapo watu wengi
    wamebobea uzunguni. Harusi ilionyesha mitindo ya asili na jadi. Bibi na bwana
    arusi walikuwa wakipendeza mno na wakachagua kufanana sana kama mboni za
    macho. Ninawaombea baraka za Bwana.

    Zaidi ya hayo, usafi uliokuwa nyumbani kwenu ulikuwa wa kuvutia. Ugani

    kulikuwa kunametameta na kupendeza kutokana na maua yaliyokuwa yakitoa
    harufu nzuri. Vyakula na vinywaji vilivyoandaliwa mezani vilikuwa safi kwenye
    kiwango kinachohitajiwa.

    Isitoshe, ninakushukuru tena kwa msaada ulionipatia ukanisaidia masomoni

    wakati tulipokuwa shuleni. Msaada wako ulinifaa zaidi kwa sababu niliweza
    kushinda vizuri. Jambo hili lilinionyesha kwamba u rafiki wa kweli. Unajua?
    Nilipofika nyumbani wazazi wangu walinichinjia jogoo! Nami wakati wowote ule
    utakapohitaji msaada kutoka kwangu niko tayari kukupatia kwa kuwa « wema
    hauozi ».

    Kisha nisalimie wazazi wako na ndugu zako, maana walinishughulikia kupita

    kiasi. Kwa hakika, ninashindwa niandike yapi hata waweze kuelewa upeo wa
    furaha yangu.
    Wako,
    gahamanjos

    GAHAMANYI Jonasi

    KAZI 1

    Maswali ya ufahamu :
    a) Ni nani aliyeandika barua hii?
    b) Taja jina la aliyeandikiwa barua.
    c) Mwandikaji wa barua anasomea katika shule gani?
    d) Mwandikajibarua anaishi wapi?

    e) Madhumuni ya barua hii ni yapi?

    1.2. Msamiati kuhusu barua

    KAZI 2

    Baada ya kusoma barua ya hapo juu eleza maneno yafuatayo
    -- Ghaya
    -- Shwari
    -- Nadra
    -- Wamebobea
    -- Dhati

    1.3. Sarufi : Aina za maneno ya Kiswahili

    KAZI 3
    Chunguza sentensi zifuatazo kisha utaje aina za maneno
    yaliyopigiwa mistari.
    -- Gahamanyi ni mwalimu wa chuo cha ualimu.
    -- Darasa linasafishwa na wanafunzi wale.

    -- Yeye atakuja kesho.

    Gahamanyi, ualimu : ni nomino/majina
    Ni, linasafishwa ni vitenzi
    Cha, wale ni vivumishi

    Yeye ni kiwakilishi

    Maelezo muhimu kuhusu aina za maneno
    Katika lugha ya Kiswahili kuna aina nane za maneno. Aina hizo ni kama vile
    nomino, kitenzi, kivumishi, kiwakilishi, kihusishi, kielezi, kiunganishi na kihisishi.
    Katika somo letu tutagusia kwenye aina nne yaani nomino, kivumushi, kiwakilishi
    na kitenzi.
    • Nomino (N)/ jina
    a) Maana ya nomino

    Nomino au jina ni neno linaloita kitu chenye uhai au kisicho hai kwa kukitoautisha
    na vingine.
    b) Aina za nonino
    -- Nomino za pekee : Butare, Nyanza, Ngororero , Gahamanyi, Ibilisi,
    Rukarara, Yesu, Akanyaru, …
    -- Nomino za kawaida : ndege, gari, nyumba, kiongozi, tarafa, gunia, kobe,
    miti …
    -- Nomino za dhana au za dhahania : unyama, uzalendo, ualimu, utu,
    ujinga, uroho…
    -- Nomino za jamii/ za makundi : umma, familia, jamii, bodi, baraza,
    genge, kikosi, jeshi, …
    -- Nomino za wingi : mate, maji, mafuta, amani, madaraka, …
    -- Nomino za kitenzi-jina : Kuishi kwingi kuona mengi. Kuimba kwake

    ni kuzuri.

    KAZI 4

    Baada ya kusoma maelezo ya hapo juu toa mifano mingine ya

    aina za nomino.

    KAZI 5

    Weka majina yafuatayo katika wingi

    s

    Vivumishi(V)
    a) Maan ya kivumishi
    Vivumishi au visifa ni maneno yanayotuelezea zaidi kuhusu nomino. Aghalabu
    vivumishi hutanguliwa na nomino.
    b) Aina za vivumishi
    • Vivumishi vya sifa

    Mifano:

    -- Mke mfupi yule ni mpole.
    -- Sauti nzuri humtoa nyoka mkali pangoni.
    • Vivumishi vimilikishi
    Vivumishi hivi hutumika kuonyesha nomino inayomiliki nyingine. Mizizi ya vivumishi
    hivi huundwa kulingana na nafsi mbalimbali. Mizizi hiyo ni: -angu, -ako, -ake,
    -etu, -enu, -ao.

    Mifano :

    -- Gari langu halina usukani.
    -- jamii yao inaishi vizuri.
    • Vivumishi vya idadi
    Hutueleza zaidi kuhusu kiasi, au idadi ya nomino. Kuna aina mbili za vivumishi
    vya idadi.

    a) Idadi kamili - hutumia nambari kuelezea idadi ya nomino.

    Mifano:
    -- Mmomonyoko wa ardhi ulibomoa nyumba tatu katika kijiji kimoja.
    -- Alipotaka kuoa wake wawili wanakijiji walimzuia.
    b) Idadi Isiyodhihirika - huelezea kiasi cha nomino kwa ujumla, bila kutaja
    idadi kamili.
    Mifano: Chache, nyingi, kadhaa, kidogo, wastani.

    Mifano
    :

    -- Watoto wengi waligeuka mayatima wakati wa mauaji ya kimbaridhidi ya
    Watusi yaliyotokea mnamo mwaka wa 1994.
    -- Mvua nyingi ilinyesha na kusababisha mmomonyoko wa ardhi.
    Vivumishi viulizi
    Vivumishi viulizi hutumika kuuliza swali.
    -ngapi?, -pi? wapi?, gani?
    Mifano:
    -- Mtu yule ana miguu mingapi?
    -- Ni mbuga ipi inayohifadhi simba nchini Rwanda?
    Vivumishi viashiria / vionyeshi
    Vivumishi viashiria hutumika kuonyesha au kuashiria nomino kulingana na mahali.
    Karibu: hapa, huyu, hiki, hili, huku, haya.
    Mbali kidogo: hapo, huyo, hiyo, hicho.
    Mbali zaidi: pale, lile, kile. ule, wale, pale.

    Mifano :

    -- Kaeni mahali hapa.
    -- Kijana yule ni mchezaji.
    Vivumishi visisitizi

    Husisitiza nomino fulani kwa kurudia rudia kivumishi kiashiria.

    Mifano:
    -- Amekuja pahali papa hapa.

    -- Kiongozi yuyu huyu anatutawala vizuri.

    • Vivumishi virejeshi
    Hivi ni vivumishi ambavyo hurejelea nomino. Vivumishi hivi vinaweza kuwa
    vivumishi vya O-/-ye rejeshi au vivumishi viashiria vinapotumika kurejelea nomino.

    Mifano:

    -- Raia ambaye atakamatwa akiuza au akinunua magendo ataadhibiwa.
    -- Wanyama ambao ni wakali sana ni simba na chui.

    Vivumishi vya A-unganifu
    Vivumishi hivi hutuelezea zaidi kuhusu nomino kwa kuonyesha kitu kinachomiliki
    nomino hiyo. Huundwa kwa kuambatanisha kiambishi cha nafsi/ngeli pamoja na
    kiambishi -a cha a-unganifu, kisha nomino.
    Mfano: cha, la, kwa, za, ya, wa, …

    -- Uchungu wa mwana aujuaye mzazi.

    KAZI 6

    Pigia mstari vivumishi katika sentensi zifuatazo:
    a) Jua kali hili husababishwa na uharibifu wa mazingira yetu.
    b) Maneno matamu yalimtoa nyoka yule pangoni mle.
    c) Koti hilo refu limekugeuza mzee.
    d) Usafi utafanywa na sisi sote wenyewe.

    e) Ni walimu gani watakaofundisha somo la Kiswahili?


    Viwakilishi (w)

    a) Maana ya viwakilishi
    Viwakilishi vya nomino ni maneno yanayotumika badala ya nomino. Kiwakilishi

    hakiwezi kuambatanishwa na nomino inayorejelewa.

    b) Aina za viwakilishi
    Viwakilishi vya nafsi
    -- Viwakilishi nafsi huru: Mimi, wewe, yeye, sisi, nyinyi, wao.
    -- Viwakilishi nafsi viambata : Ni-, u-, a-, tu-, m-, wa-, mi-, li-, ya-, ki-, vi-,

    i-, zi-, ku-, pa-

    • Viwakilishi viashiria

    Viwakilishi viashiria (vionyeshi) hutumika badala ya nomino kwa kutumia
    kuonyesha nomino inayorejelewa bila kuitaja.
    -- Haya ni madhara ya uharibifu wa mazingira.

    -- Wale wanahitaji amani.

    • Viwakilishi visisitizi

    Hutumika kwa niaba ya nomino kwa kutumia kiashiria chake mara mbili mfululizo.
    Kwa mfano: yuyu huyu, wawa hawa, kiki hiki, papo hapo, mumu humu, zizi hizi,
    → Yuyu huyu ndiye rafiki yangu.

    • Viwakilishi vya sifa

    Husimama badala ya nomino kwa kurejelea sifa yake.
    Kwa mfano: -chungu, -eupe, -dogo, -zuri, -tamu, -embamba, -rembo, -gumu,
    -kali, ekundu.
    → Cheupe Kinapendeza.
    • Viwakilishi vya idadi
    Hutumika kusimama badala ya nomino kwa kurejelea idadi yake.
    a) Idadi Kamili - hutumia nambari kuelezea idadi ya nomino
    -- Ukikata mmoja panda miwili.
    -- Anafuga watatu tu.

    b
    ) Idadi isiyodhihirika - huelezea kiasi cha nomino kwa ujumla, bila kutaja
    idadi kamili.
    Mifano:
    -- Tutasikiliza maoni ya wengi baada ya kuuratibu mpango huu.
    -- Mengi yalisemwa kuhusu maradhi ya UKIMWI.

    • Viwakilishi viulizi

    Viwakilishi viulizi hutumika kwa niaba ya nomino katika kuulizia swali.
    Baadhi ya viwakilishi viulizi huchukua viambishi vya ngeli.
    Mifano:
    -- Uko wapi?
    -- Unahitaji vingapi?

    • Viwakilishi vimilikishi

    Viwakilishi hivi hurejelea nomino kwa kutumia vimilikishi.
    -- Kwetu kuna maji safi.
    -- Zao zilibomolewa na mvua kali.

    • Viwakilishi virejeshi
    Hutumia O-/-ye-rejeshi kurejelea na kusimamia nomino.
    Kwa mfano: ambaye, ambao, ambalo, ambacho, huyo, yule.
    -- Ambao walizaliwa mwaka huu watapimwa.
    -- Ambaye anahitaji fedha za shule

    • Viwakilishi vya A-unganifu

    Huwakilishi nomino kwa kutaja kinachomilikiwa na nomino hiyo. Huundwa
    kwa kuambatanisha kiambishi cha nafsi/ngeli pamoja na kiambishi -a cha
    a-unganifu.

    Kwa mfano: cha, la, kwa, za, ya

    -- Cha mlevi huliwa na mgema.

    -- La kuvunda halina ubani.

    KAZI 7

    Taja aina za viwakilishi vinavyopatikana katika sentensi zifuatazo:
    -- Wao hawajafika kwangu.
    -- Yule mweusi aende nyumbani.
    -- La kuvunja halina rubani.

    -- Wengi walipanda miti kupambana na jangwa.

    1.4. Matumizi ya lugha

    KAZI 8

    Soma upya barua uliyopewa hapo awali kisha utoe maana ya

    barua ya kirafiki na uonyeshe sehemu zake kuu.

    Maelezo muhimu kuhusu barua ya kirafiki
    a) Maana ya barua
    Barua au waraka ni maandishi yaliyopangwa kwa utaratibu na mtiririko maalum
    kwa minajili ya kuwasilisha ujumbe fulani. Barua ni risala au mmjumbe mwepesi
    anayemwakilisha mtungaji wake kwa mtu mwingine na kuwasilisha taarifa yake

    kwa mtu huyo.

    Barua huandikwa kwa madhumuni mbalimbali kama kuarifu, kuomba kitu kama
    vile kazi, ruhusa; kuagiza bidhaa, n.k.

    Kuna aina nyingi za barua lakini katika kitabu hiki tutashuhulikia barua tatu tu

    ambazo ni:
    -- Barua za kikazi zenye madhumuni ya kazi.
    -- Barua za mwaliko zenye lengo la kualika mtu katika sherehe au sikukuu
    fulani
    -- Barua za kirafiki : ni zile ambazo huandikiwa na mtu au watu mbalimbali
    walio na uhusiano wa karibu na anayeandika; k.v rafiki, ndugu, n.k. Barua
    hizi zina uhuru mkubwa katika kuziandika. Hazidai utaratibu wa kipekee
    sana. Mtu huwa huru kuandika apendalo ilimradi halimvunjii mtu heshima
    yake.

    b) Sehemu za barua ya kirafiki

    c

    -- Anwani ya mwandikaji na tarehe: huandikwa kwenye pembe ya juu
    upande wa kulia wa karatasi. Mwandikaji anaandika mahali anapoandikia
    barua (au anapoishi). Anaweza kuongeza nambari za sanduku la posta
    (S.L.P.) na mji, nambari ya simu na akaunti ya barua pepe. Tarehe huandikwa
    chini ya anwani kwa kuacha nafasi ya mstari mmoja.
    -- Jina la mwandikiwa: huja chini ya tarehe lakini kwenye upande wa
    kushoto.
    -- Salamu: sehemu hii hutoa maamkizi kwa mwandikiwa na huandikwa
    chini ya jina la mwandikiwa.
    -- Utangulizi: hujitokeza katika aya ya kwanza. Mwandikaji humjulisha hali
    yake ilivyo,na kuuliza hali ya mwandikiwa na hata wenzake kwa jumla.
    -- Barua yeynyewe: huu ni ujumbe kamili wa barua. Mwandikaji anaweza
    kutumia aya moja au zaidi kulingana na urefu wa barua yake.
    -- Hitimisho la barua: ni sehemu ya mwisho ya barua. Sehemu hii
    huandikwa kwa aya moja na hujumlisha mambo ya kumuaga mwandikiwa.
    Kwenye sehemu hii unaongeza maneno ya kuvutia (Wako, Wako mpendwa,
    Mwanako, Wako mwaminifu, n.k.). Maneno haya huandikwa kwenye
    upande wa kulia kabla ya kutia sahihi.
    -- Sahihi ya mwandishi: huja chini ya hitimisho kwa upande wa kushoto.
    -- Jina la mwandikaji: huja chini ya sahihi ya mwandikaji.

    c) Aina za barua za kirafiki

    Barua za kirafiki zinaweza kuwa mwana kwa mzazi au mzazi kwa mwana, za
    mapenzi, za kindugu (kati ya ndugu), za kijamaa, n.k.


    1.5. Kusikiliza na kuzungumza
    KAZI 9
    Tunga barua kisha uisomee wenzako hadharani kwa kuonyesha vitabia
    1.6. Kuandika

    KAZI 10
    Mwandikie rafiki yako barua ukimwomba muende pamoja

    kutembelea Mbuga ya Wanyama ya Akagera.

    SOMO LA 2: BARUA YA MWALIKO
    2.1. Kusoma na ufahamu: Ndoa ya dadangu
    Soma kifungu cha habari kifuatacho kisha ujibu maswali ya ufahamu.

    NDOA YA DADANGU

    v

    Ilikuwa Jumamosi tarehe 15 mwezi wa Novemba wakati nilipohudhuria harusi ya
    dada yangu Mukashema Maria aliyefungana pingu za maisha na Mutabazi Joni.
    Harusi yenyewe ilikuwa ya kukata na shoka.

    Kabla ya wiki mbili za arusi kufanyika familia mbili zilikuwa katika pilikapilika za

    hapa na pale ili kuandaa sherehe hii ya harusi. Kwa upande wa familia yangu sisi
    watoto tulikuwa tukitumwa huku na kule kwa kuwaalika watu watakaohudhulia
    harusi hii. Wazazi wangu waliwaalika wazee majirani na dada yangu akawaalika
    wenzake hasa wa rika lake. Wote walikuwa wakipelekewa barua za mialiko.

    Siku moja kabla, nyumbani kwetu tulifanya usafi na majirani walikuwa wakimsaidia

    baba kutayarisha pombe ya mtama, ya ndizi na juisi. Wengine walikuwa
    wakipamba uga na kujenga nyumba za mahema.

    Siku hiyo ilipowadia watu walimiminika kuelekea nyumbani kwetu. Asubuhi

    majira ya saa nne hivi, familia ya bwana harusi ilifika kwetu na kukaribishwa kwa
    taadhima. Walikuwa wamekuja kuposa na kutoa mahari. Waliandaliwa vyakula
    na vinywaji mezani wakafurahi sana. Furaha yao ilipandishwa na nyimbo pamoja

    na ngoma za wachezaji waliokuwa hapo.

    Baada ya hapo bi harusi alivishwa veli. Bwana harusi alirudi kumchukua akiwa
    na gari la kifahari wakaenda kanisani ili kuvishana pete mbele ya Bwana. Nasi
    tuliandamana nao tukiwa katika magari kadhaa. Watu walipoona mlolongo wa
    magari hayo waliduwaa wakidhani kuwa kulikuwa na kongamano la kimataifa
    katika kijiji chetu.

    Tulipotoka kanisani, tulifurika bustanini kama ilivyoelezwa kwenye barua za

    mwaliko walizopewa watu. Watu walikuwa wengi sana na sherehe ilifana sana.
    Tuliandaliwa vinywaji na vyakula tele tele. Watu wote walifurahi sana na kucheza

    ngoma na nyimbo za utanaduni

    KAZI 1

    Maswali ya ufahamu
    a) Harusi inayosimuliwa ilifanyika lini ?
    b) Harusi hiyo ilikuwa ya kina nani ?
    c) Ni vinywaji gani vilivyotayarishwa siku moja kabla ya sherehe?
    d) Watu waliokuja harusini walipataje habari hizo?

    e) Kwa sababu gani watu walioona magari walishangaa?

    2.2. Msamiati

    KAZI 2

    Eleza maneno yafuatayo
    a) Aliyefungana pingu za maisha
    b) Pilikapilika
    c) Kifahari
    d) Mahema

    e) Veli

    2.3. Sarufi: Aina za maneno

    KAZI 3

    Tazama sentensi zifuatazo kisha ueleze maneno yaliyopigiwa
    mistari
    a) Nyumbani humu mna usafi.
    b) Tia taka nje.

    c) Simba anaishi ndani ya msitu ule.

    Maelezo muhimu kuhusu aina za maneno
    Katika lugha ya Kiswahili kuna aina nane za maneno. Aina hizo ni kama vile
    nomino, kitenzi, kivumishi, kiwakilishi, kihusishi, kielezi, kiunganishi na kihisishi.
    Katika somo letu tutagusia kwenye aina tatu yaani kitenzi, kielezi na kihusishi.
    • Kitenzi
    a) Maana ya kitenzi

    Kitenzi ni neno linaloeleza jambo linalotendwa au kufanywa na nomino au
    kiwakilishi chake.
    b) Aina za vitenzi
    -- Kitenzi halisi: Ni kitenzi kimoja kinachotumiwa katika sentensi.
    Mifano :
    -- Raia walifanya msaragambo.
    -- Meya amekuja hapa.
    -- Vitenzi vikuu na vitenzi visaidizi: Wakati vitenzi viwili hutumika pamoja
    kueleza kitendo kimoja, kitenzi cha kwanza huitwa kisaidizi na cha pili
    ndicho kitenzi kikuu.
    Mifano :
    -- Yeye alikuwa akicheza.
    -- Wao wanahitaji kula vizuri.
    Vitenzi vishirikishi: Vitenzi vishirikishi vina dhana ya kitenzi kuwa au
    kuwa na.
    Vitenzi vishirikishi huwa vya aina mbili kuu :
    Vitenzi vishirikishi vikamilifu: Hivi huchukua viambishi vya wakati
    na viambishi nafsi.
    Mifano :
    -- Wanafunzi wangali usingizini
    -- Yeye atakuwa mzembe.
    Vitenzi vishirikishi vipungufu : Hivi huchukua viambishi nafsi lakini
    havichukui viambishi wakati.
    -- Walozi si wazuri.
    -- Yeye yu mkweli.

    -- Nyinyi ni walimu wa kesho.

    KAZI 4

    Tunga sentensi ukitumia vitenzi vifuatavyo :
    • - yu
    • - kimuona
    • - u
    • - kaa

    • - ni

    • Vielezi
    Vielezi ni maneno yanayotoa habari zaidi kuhusu kitendo kilivyofanyika. Pia vielezi
    hutoa habari zaidi kuhusu hali, vivumishi na vielezi vingine.

    Kuna vielezi vya namna, vielezi vya wakati, vielezi vya mahali na vielezi vya kiasi.


    Mifano :

    -- Mwanafunzi-mwalimu yule ameshinda mtihani vizuri (Kielezi cha
    namna).

    -- Mvua ilinyesha jana (kielezi cha wakati).
    -- Samaki huishi baharini (kielezi cha mahali).

    -- Anamtembelea mara kwa mara (kielezi cha kiasi).

    KAZI 5

    Onyesha na utaje aina za vielezi vinavyopatikana katika sentensi
    zifuatazo:
    -- Simba huenda kimya anapowinda.
    -- Vijana wa siku hizi huvaa kizungu, kichina na kihindi mara chache.
    -- Wewe uliitwa mara kadhaa na hujaitika leo.
    -- Gunia hili limejaa sana inafaa lipakuliwe.

    -- Imenyesha mchana kutwa

    • Vihusishi (H)
    Vihusishi ni maneno yanayoonyesha uhusiano baina ya watu au vitu viwili au

    zaidi. Kuna vihusishi vya mahali na vya wakati.

    Mifano:
    -- Tutaonana baada ya wiki moja .
    -- Si vizuri kuishi kando ya mto.
    -- Ng’ombe hulala ndani ya zizi.
    -- Ameondoka hapa kabla ya mvua kunyesha.

    -- Wao wanaishi pamoja kwa amani.

    KAZI 6

    Tumia vihusishi vifuatavyo kwa kujaza mapengo: katika, kabla ya,
    mbele ya, baada ya, pembeni mwa.
    a) Miti ilipandwa................nyumba.
    b) .................mvua kunyesha unaona dalili zake.
    c) Watu wengi waliangamia ..............ajali ya ndege iliyotokea nchini
    Kongo.
    d) ...............kuondoka tulimfuata huko.

    e) Hakuna mtu anayeishi...............shimo siku hizi nchini Rwanda.

    2.4. Matumizi ya lugha

    KAZI 7

    Jibu maswali yafuatayo
    a) Mtu anapowakaribisha wengine karamuni anatumia nini?
    b) Mtu anaweza kuwaalika wengine kwa madhumuni gani?
    KAZI 7
    Maelezo muhimu kuhusu barua za mwaliko
    Maana ya barua za mwaliko
    Barua ya mwaliko ni ujumbe unaotolewa kwa kumkaribisha mtu kuhudhuria
    shughuli au hafla fulani. Barua za mwaliko zinaweza kuwa na madhumuni
    yafuatayo:
    Sherehe
    Karamu
    Harusi

    Ubatizo

    Sikukuu ya kufunga mwaka
    Sikukuu ya kupata cheti au digrii
    Kuadhimisha miaka fulani, n.k

    Mambo ya kuzingatiwa katika uandishi wa barua ya mwaliko

    Jina la mwalikwa
    Sababu ya mwaliko
    Mahali ukaribisho utakapofanyika, terehe na saa
    Jina na anwani ya mkaribishaji

    a) Mifano ya barua za mwaliko

    • Barua ya mwaliko kwenye harusi

    d

    Karibu sana!

                                                                                                                    RWEMA Eric

    2.5. Kusikiliza na Kuzungumza
    KAZI 8
    Shirikiana na wenzako mzungumzie kuhusu uandishi wa barua za mwaliko.

    2.6. Kuandika
    KAZI 9

    Mkaribishe mwenzako kwenye sikukuu yako ya kuzaliwa

    SOMO LA 3: MATANGAZO
    KAZI 1
    Tazama kwa makini mchoro ufuatao kisha ujibu maswali

    yaliyotolewa hapo chini:

    v

    Jibu maswali yafuatayo:
    –– Ni nini unachoona kwenye mchoro huu?

    –– Unafikiri kuwa mtu huyo mwenye kipazasauti anafanya nini?

    3.1. Kusoma na ufahamu: Tangazo la ajira
    Soma tangazo lifuatalo kisha ujibu maswali ya ufahamu.
    TANGAZO LA AJIRA
    Wilaya ya CHAPAKAZI inayo furaha ghaya ya kuwatangazia watu wote wenye
    uwezo kwamba ina nafasi za ajira za ufundishaji katika shule za chekechea na
    msingi. Nafasi hizo ni kama zifuatazo:
    1. Walimu wa Kiswahili katika shule za msingi (nafasi kumi)
    2. Walimu wa Kinyarwanda katika shule za msingi (nafasi tatu)
    3. Walimu wa Hisabati katika shule za msingi (nafasi tano)
    4. Walimu wa Kifaransa katika shule za msingi (nafasi tano)
    5. Walimu wa Kiingereza katika shule za msingi (nafasi tano)
    6. Walimu wa Mafunzo ya kijamii katika shule za msingi (nafasi tano)
    7. Walimu wa Sayansi katika shule za msingi (nafasi mbili)
    8. Walimu katika shule za chekechea (nafasi ishirini)

    Anayehitaji kazi hizo anapaswa kuwa na sifa zifuatazo:

    1. Kuwa Mnyarwanda,
    2. Kuwa na astashahada ya ukufunzi (A2),
    3. Kuwa na uwezo wa kutumia tarakilishi na vifaa vingine vya TEHAMA,
    4. Kuwa na uwezo wa kutumia Kinyarwanda na Kiingereza kwa ujumla.
    Kwa wakufunzi wa Kiswahili wanapaswa kuwa na uwezo wa kutumia
    kinyarwanda, Kiingereza na Kiswahili. Wakufunzi wa Kifaransa wanapaswa
    kuwa na uwezo wa kutumia Kinyarwanda, Kiingereza na Kifaransa.
    5. Kuwa na afya bora,
    6. Kuwa na umri usiozidi miaka thelathini,
    7. Kuwa na uwezo wa kufanyia kazi katika eneo na mazingira yoyote.

    Barua zenye maombi ya kazi pamoja na viambatisho vingine kama vile wasifu kazi,

    kitambulisho cha uraia na astashahada, vitapokelewa hadi tarehe 20/12/2019

    katika ofisi ya katibu wa wilaya. Tarehe ya kusailiwa mtaijuzwa baadaye.

    Tangazo limetolewa tarehe 1/12/2019.

    Meya wa Wilaya ya Chapakazi
    (Saini + mhuri)

    GAHIZI Musa

    KAZI 2
    Jibu maswali yafuatayo
    Tangazo hili ni la aina gani?
    Tangazo hili linalenga nani ?
    Tangazo hili linatangaza nini ?
    Neno TEKNOHAMA ni ufupisho wa nini ?

    Kwa sababu gani Meya wa wilaya alitia saini yake kwenye tangazo?

    KAZI 3
    3.2. Msamiati kuhusu tangazo
    Eleza maneno yafuatayo :
    -- Ajira
    -- Shule za chekechea
    -- Viambatisho
    -- Astashahada

    -- Mhuri

    3.3. Sarufi: Aina za maneno ya kiswahili
    KAZI 4
    Chunguza sentensi zifuatazo kisha utaje aina za maneno
    yaliyopigiwa mistari.

    -- Kobe na Kijumbamshale walikaa chini ya mti ili kuzungumza.
    -- Lo! Umemwona mshamba yule!

    -- Fisi wala Simba hawakucheza mchezo wa riadha.

    Maelezo muhimu kuhusu aina za maneno
    KAZI 5
    Soma maelezo yafuatayo kisha ujadili kuhusu matumizi ya maneno
    yanayounganisha sentensi:
    Katika lugha ya Kiswahili kuna aina nane za maneno. Aina hizo ni kama
    vile nomino, kitenzi, kivumishi, kiwakilishi, kihusishi, kielezi, kiunganishi na

    kihisishi. Katika somo letu tutaona aina mbili yaani kiunganishi na kihisishi.

    • Viunganishi (U)
    Viunganishi ni maneno yanayofanya kazi ya kuunganisha. Huonyesha uhusiano
    baina ya neno na neno, fungu moja la maneno na fungu jingine au sentensi na
    sentensi.

    Mifano:

    a) Unataka maji au juisi?
    b) Anasoma kitabu badala ya kupiga ubwana.
    c) Kufanikiwa maishani si bahati bali ni kujishughulisha na kujitolea.
    d) Alishinda mtihani ijapokuwa alipatwa na ugonjwa mkali.
    e) Alienda shuleni bila kupata chakula.

    KAZI 6

    Tunga sentensi sahihi kwa kutumia viunganishi vifuatavyo:

    a) Halafu
    b) Kisha
    c) Ili
    d) Ingawa

    e) Kama

    • Vihisishi (I)
    Vihisishi ni maneno ambayo yanaonyesha hisia za mtu za ndani kwa mujibu wa
    hali na muktadha. Yanaonyesha hangaiko la moyo ama kudokeza mguso wa

    moyo ama hata wa akili.

    Mifano:
    Mtume! Umefika asubuhi hii!
    Lo! Mvua imenyesha!

    Salaa! Inawezekana mtu kunywa chupa ishirini za juisi!

    KAZI 7
    Tunga sentensi sahihi kwa kutumia vihishi vifuatavyo:
    a) Mungu wangu!
    b) Mama wee!
    c) Ng’o!
    d) Barabara!

    e) Masalale

    3.4. Matumizi ya lugha
    KAZI 8
    Soma upya tangazo la hapo juu kisha ujadiliane na wenzako kuhusu muundo

    wa matanganzo.

    Maelezo muhimu kuhusu matangazo
    Maana ya tangazo
    Tangazo au ilani ni mpangilio wa maandishi kwa mtindo maalumu kwa lengo la
    kupasha habari ama kupokeza ujumbe fulani wa kidhalura au muhimu. Taarifa
    inayosambazwa kwa tangazo inaweza kuwa kifo, mkutano, taratibu za kutumia
    barabara vizuri, kazi na mengineyo.

    Aina za matangazo

    Zipo aina nyingi za matangazo
    Matangazo ya kibiashara
    Matangazo ya kifo
    Matangazo ya serikali, n.k.
    Mambo ya kuzingatiwa katika uandishi wa matangazo
    Kwa kuandika tangazo ni lazima kuzingatia mambo yafuatayo :
    Kichwa cha tangazo
    Kutaja anayetoa tangazo
    Kutaja walengwa wa tangazo
    Ujumbe wa tangazo

    Sahihi na jina la anayetoa tangazo (tangazo lisilokuwa na sehemu hii huitwa
    tetesi, fununu au uvumi)

    Mfano wa tangazo

    m

    3.5. Kusikiliza na Kuzungumza
    KAZI 9
    Sikiliza matangazo redioni kisha ujadiliane na wenzako kwa

    kuzingatia maudhui, aina ya matangazo na lugha iliyotumiwa.

    3.6. Kuandika
    KAZI 10

    Tunga tangazo la kibiashara

    Tathmini ya mada
    1. Eleza maana ya barua.
    2. Taja aina za barua tulizoona.
    3. Zitaje sehemu kuu za barua ya kirafiki.
    4. Ni mambo gani muhimu yanayopaswa kuonekana kwenye barua ya
    mwaliko?
    5. Tunga tangazo la kazi.
    6. Taja aina za meneno yanayojenga sentensi zifuatzo.
    -- Eeh! Unataka kitu gani?
    -- Wao walikufa hapa na kuondoka haraka.
    -- Mama alikuwa akipalilia maharagwe yake katika bonde lile.
    -- Ingawa mvua ilinyesha vizuri, mavuno yanaendelea kudidimia.

    -- Chukua hicho kizuri ila hakitoshi.

  • MADA YA 2: UTUNGAJI WA BARUA RASMI

    Uwezo mahususi
    Kuandika barua rasmi kwa ufasaha

    Malengo ya Ujifunzaji

    -- Kubainisha sehemu kuu za barua rasmi;
    -- Kutunga barua rasmi kwa ufasaha;
    -- Kutunga sentensi sahihi kwa kutumia kirejeshi – po - .

    SOMO LA 4: TARATIBU ZA KUTUNGA BARUA RASMI 
    KIDOKEZO
    n


    4.1. Kusoma na ufahamu: Barua ya kuomba kazi
    m
    n
    Maswali ya ufahamu
    KAZI 1

    Soma kifungu cha habari hapo juu na ujibu maswali ya ufahamu
    yafuatayo:
    1. Mwandishi wa barua hii ni nani?
    2. Mwandishi huyu anaishi wapi?
    3. Amemwandikia nani?
    4. Nini lengo la barua yake?
    5. Mwandishi amemshawishije mwandikiwa?

    KAZI 2
    Chagua jibu lililo sahihi kuliko mengine

    1. Mwandishi ana tajiriba ya:
    a) Miaka miwili
    b) Cheti cha ualimu
    c) Kuomba kazi
    d) Miaka miwili ya kufundisha katika shule za msingi.

    2. Baadhi ya vitambulisho vilivyoambatishwa kuna:

    a) Ombi la kazi
    b) Cheti cha ualimu pamoja na nakala ya kitambulisho cha uraia
    c) Kitambulisho cha mwajiri wa mwisho
    d) b na c ni sahihi

    3. Mwombaji kazi anaamini kuajiriwa kwa sababu:

    a) alijifunza ualimu.
    b) ana tajiriba ya kutosha katika ualimu na uwezo wa kutumia kompyuta.
    c) ana tajiriba katika ualimu katika shule za msingi pamoja na uwezo wa
    kutumia kompyuta.
    d) ana mbinu nzuri za kutimiza kazi yoyote.

    4. Kweli au uongo/sikweli

    a) Bila shaka Ndizeye ataajiriwa kwenye Shule ya Msingi Mukingi.
    b) Ndizeye ni mwalimu mwerevu sana na mwenye uwezo sana.
    c) Atakapoajiriwa kwenye alipoomba kazi wanafunzi wote watafaulu
    mitahani yao.
    d) Cheti cha ualimu ni kitambulisho pekee kinachofaa kupata ajira ya ualimu.
    e) Kufaulu mitihani kwa wanafunzi hutegemea jinsi mwalimu anavyotumia
    vizuri mbinu shirikishi za ujifunzaji na ufundishaji.

    4.2. Matumizi ya msamiati
    KAZI 3
    Jaza sentensi zifuatazo kwa kutumia msamiati huu: kuhitimu,
    uthibitisho, tarakilishi, kutimiza, feli, nakala

    1. Wanafunzi wanaombwa kufanya bidii ili wasi.............................majaribio
    na mitihani yao.
    2. ...............................ni kifaa cha kiteknolojia kinachorahisisha leo kazi ya
    mawasiliano kwa kupitia njia ya maandishi.
    3. Unapoomba kazi ni lazima kutoa ...................za vyeti na vitambulisho
    vingine muhimu vya..............................
    4. Katika barua yake ya kuomba kazi, Ndizeye aliahidi...........................
    wajibu wake ipasavyo.
    5. Baada ya .......................masomo yake ya ualimu, Ndizeye alipata kazi
    kwenye Shule ya Msingi Mukingi.

    4.3. Sarufi: Matumizi ya kirejeshi – po -
    KAZI 4
    Eleza matumizi ya mofimu yenye wino uliokolea
    i) Mahali tunapoishi ni pasafi.
    ii) Mahali ambapo panapatikana mbu ndipo panapoweza kuhatarisha
    maisha ya binadamu.
    iii) Mahali walipokaa palikuwa na utulivu.
    iv) Mahali wezi hujifichapo hapajulikani.

    MAELEZO MUHIMU

    - Po – ni kiambishi rejeshi cha mahali. Kwa kawaida hujihusisha na majina ya
    ngeli ya PA-M-KU na kutumiwa kama ifuatavyo:
    -- Katikati ya kiambishi nafsi cha kitenzi na mzizi wa kitenzi.
    -- Kwenye mzizi wa amba- na ndi-.
    -- Mwishoni mwa kitenzi.
    Tanbihi: Katika wakati ujao, kirejeshi –po- husababisha kiambishi –ka-.
    Mfano: Utakapofika utanipigia simu.
    Wakati wowote mtakapokata tamaa mtafeli mitihani yenu.

    Mifano mingine:

    i) Mahali nitakapoajiriwa nitafanya bidii.
    ii) Mahali ambapo panapatikana mbu panaweza kuhatarisha maisha ya
    binadamu.
    iii) Nipo tayari kuwasili wakati wowote nitakapohitajika.
    iv) Hapa ndipo patakapopandwa miti kwa ajili ya kuhifadhi mazingira.
    v) Mahali nitakapoajiriwa nitafanya bidii.
    vi) Mahali ambapo panapatikana mbu panaweza kuhatarisha maisha ya
    binadamu.
    vii) Nipo tayari kuwasili wakati wowote nitakapohitajika.
    viii) Hapa ndipo patakapopandwa miti kwa ajili ya kuhifadhi mazingira..,

    KAZI 5
    Unganisaha sentensi zifuatazo kwa kutumia kirejeshi –poi)

    Tunakaaa mahali pengi. Mahali papo ni penye raha.
    ii) Mahali pale panajulikana kama Eldorado. Ni pazuri sana.
    iii) Tulitembelea mahali penye mbugaza wanyama.
    iv) Walijenga nyumba mahali penye harufu nzuri.

    4.4. Matumizi ya lugha: Mwongozo wa kutunga barua
    rasmi

    Maelezo muhimu
    a) Maana ya barua rasmi:
    Barua rasmi au barua za kiofisi ni barua ambazo zinahusu mambo ya kiofisi kama
    vile taarifa za mikutano, kuomba kazi, kuagiza vifaa vya shughuli nyingine rasmi.

    b) Aina za barua rasmi

    Barua rasmi zipo za aina nyingi lakini zinaweza kugawanyika katika makundi au
    mafungu matatu makubwa yafuatayo:
    1. Barua za taarifa
    2. Barua za maombi mbalimbali
    3. Barua za upokeaji vifaa.

    c) Mtindo wa barua rasmi:

    Barua rasmi huandikwa kuelezea ujumbe maalumu, kwa hiyo huhitaji kuandikwa
    kwa uangalifu na umakini wa kutosha. Ni muhimu kuandika jambo husika waziwazi
    na kuepuka maelezo yasiyo muhimu, kama vile salamu na kadhalika. Mwandishi
    analazimika kuandika kwa ufupi na lugha nyepesi. Barua rasmi huwa na sentensi
    chache tena fupi, na ni lazima kufuata taratibu za uandishi, sentensi ziwe kamili.

    d) Lugha ya barua rasmi:

    Tofauti na lugha ya barua ya kirafiki, barua rasmi hutumia lugha fupi
    na mwandishi hulenga mada mara moja bila kuzungukazunguka. Kwa mfano,
    kama minajili yako ni kuomba hela za kulipa karo ya shule kama barua hii ya
    EssayVikings, hutazungukazunguka. Utayataja madhumuni ya barua mara moja.
    Lugha yenyewe huwa nyepesi kuelewa na haina misimu. Unapoandika barua
    ya kirafiki, waweza kutumia misimu ambayo mwandikiwa ataelewa kwa sababu
    ni rafiki yako. Katika barua rasmi, hili halifanyiwi. Mwandikiwa si rafiki yako na
    huenda ikawa humjui. Pia yafaa usome barua yako vizuri kabla ya kuituma ili
    isiwe na makosa ya tahajia au lugha.

    e) Mtindo wa barua rasmi:

    Barua rasmi huandikwa kueleza ujumbe maalumu, kwa hiyo huhitaji kuandikwa
    kwa uangalifu wa umakini wa kutosha. Ni muhimu kuandika jambo husika
    waziwazi na kuepuka maelezo yasiyo muhimu, kama vile salamu na kadhalika.
    Mwandishi analazimika kuandika kwa ufupi na lugha nyepesi. Barua rasmi huwa
    na sentensi chache tena fupi, na lazima kufuata taratibu za uandishi, sentensi
    ziwe kamili.

    f) Lugha ya barua rasmi: Tofauti na lugha ya barua ya kirafiki, barua
    rasmi hutumia lugha fupi na mwandishi hulenga mada mara moja bila
    kuzungukazunguka. Kwa mfano, kama minajili yako ni kuomba hela za
    kulipa karo ya shule kama barua hii ya Essay Vikings, hutazungukazunguka.

    Utayataja madhumuni ya barua mara moja. Lugha yenyewe huwa nyepesi

    kuelewa na haina misimu.

    Unapoandika barua ya kirafiki, unaweza kutumia misimu ambayo mwandikiwa

    ataelewa kwa sababu ni rafiki yako. Katika barua rasmi, hili halifanyiki. Mwandishi
    si rafiki yako na huenda ikawa humjui. Pia, yafaa usome barua yako vizuri kabla
    ya kuituma ili isiwe na makosa ya tahajia au lugha.

    KAZI 6
    Jadili muundo wa barua rasmi

    Muundo wabarua rasmi

    Anwani
    ya mwandishi huandikwa katika barua yake juu, kwenye pembe ya
    upande wa kulia wa karatasi.

    Tarehe
    : hii huandikwa upande wa kulia wa karatasi katika mstari uleule
    wa kumbukumbu namba ya barua kama ipo; tarehe iwe chini ya anwani ya
    mwandishi

    Kumbukumbu namba:
    hii ni namba ambayo huwa kama kitambulisho cha
    barua; mara nyingi huwa na tarakimu pamoja na herufi, kwa mfano: SRB MD 05.

    Anwani ya mwandikiwa
    : hii hutangulia na cheo cha mwandikiwa na huandikwa
    katika mkono wa kushoto, chini ya namba ya kumbukumbu.

    Mwanzo wa barua
    : huandikwa chini ya anwani ya mwandikiwa; mara
    nyingi neno ndugu hutumika kama salamu au mwanzo wa barua.

    Kichwa cha barua
    : Hutangulizwa na maneno kama vile KUHsadkuhusu),
    MINTsadmintarafu). Ni sharti kiachwe kiandikwe kwa herufi kubwa na kipigiwe
    mstari. Kichwa kinapaswa kuwa kifupi na kinachoelezea mada ya barua
    kiukamilifu.

    Barua yenyewe
    : hii huandikwa mambo yote muhimu kuhusu barua yenyewe,
    barua iwe fupi na taarifa muhimu tu.

    Mwisho wa barua
    huwa ni kimalizio cha barua: ni tamko la heshima la kumalizia
    barua; mara nyingi miisho ambayo hutamkwa ni kama vile, “wako mtiifu”, “wako
    katika kazi”, “wako katika kujenga taifa”, “wako mwanachama”.

    Saini au jina la mwandishi: baada ya kimalizio cha barua mwandishi atie
    saini yake, kisha jina lake kwa ukamilifu.

    Cheo cha mwandishi
    : mwisho wa barua, chini ya jina la mwandishi huandikwa
    cheo cha aliyeandika barua; cheo chaweza kuwa ni mwombaji, mwalimu wa
    darasa, mwanafunzi, kiranja mkuu, waziri wa elimu, mjumbe wa tawi, n.k.

    4.5. Kusikiliza na Kuzungumza
    KAZI 7
    Fikiria barua moja rasmi uliyowahi kuisoma na kuizungumzia
    hadharani.

    4.6. Kuandika
    KAZI 8
    Rejelea hapa chini mfano wa barua rasmi. Bainisha makosa ya
    kimuundo na kuyasahihisha.


    12/12/2019.

    GATETE, S.L.P. 2345,                                                                                   PAUL
    SIMU +2507345621876, KIGALI.
    Kumb.Nb 003
    KWA MKURUGENZI MKUU,
    SHAMBA LA MIKAHAWA LA USANASE, S.L.P. 3000,
    RUHANGO.
    Kwa Bi. Ituze,

    MINT: Kuomba Nafasi ya kuwa meneja wa uzalishaji kahawa


    Narejelea tangazo kutoka Gazeti la Mkulima Bora, toleo la siku ya Ijumaa

    tarehe 6, Desemba, 2019, kuhusu kuwepo kwa nafasi niliyotaja hapo juu
    nikiomba nizingatiwe. Mimi ni Mnyarwanda na ninapenda sana kilimo hasa
    cha mikahawa. Kwa miaka zaidi ya kumi, nimekuwa nikijihusisha katika
    kuwahamasisha wanakijiji kuhusu mbinu bora za kuimarisha kilimo cha
    mikahawa. Kwa sasa, kijiji chetu kinaongoza katika uzalishaji wa mikahawa
    mingi yenye thamani ya juu zaidi.
    Nimefanya utafiti kuhusu mbinu za kisasa za kuimarisha uzalishaji wa
    mikahawa na ninatumai kuwa maarifa niliyonayo yatakufaidi katika kukuza
    uzalishaji wa kahawa.

    Natazamia mawasiliano kutoka kwako wakati wowote.

                                                                                          wako mwaminifu,
                                                                                          Paul Gatete.
                                                                                          Saini
    KAZI 9
    Rejelea mfano wa barua rasmi kuhusu ombi la kazi ya hapo juu. Tunga barua

    yako kwa Waziri wa Elimu kwa ajili ya kuomba kuendendelea na masomo
    katika Chuo Kikuu cha Ualimu.

    Tathmini ya mada
    7. Nini maana ya barua rasmi?
    8. Jadili muundo wa barua rasmi.
    9. Zungumzia aina za barua rasmi.
    10. Andika barua rasmi kwa mkuu wa shule kuhusu ombi la maandalizi
    ya mazoezi ya ufundishaji.
    11. Tunga sentensi angalau mbili mbili kwa kila nafasi ya matumizi ya
    kirejeshi –po-, yaani katikati ya kiambishi nafsi cha kitenzi na mzizi
    wa kitenzi, kwenye mzizi wa amba- na ndi – pamoja na mwishoni
    mwa kitenzi.



  • MADA YA 3 :MIDAHALO

    Uwezo mahususi

    Kushiriki vilivyo katika midahalo, kuongoza na kutoa hoja kwa kutetea au

    kupinga mawazo yaliyotolewa.

    • Malengo ya ujifunzaji
    -- Kutoa maana ya mdahalo
    -- Kubainisha sifa za mdahalo mzuri
    -- Kuonesha mbinu au taratibu za mdahalo
    -- Kueleza umuhimu wa mdahalo
    -- Kutaja masuala mtambuka mbalimbali yaliyozungumziwa katika midahalo.
    -- Kueleza maana ya viambishi rejeshi

    -- Kuorodhesha viambishi rejeshi

    KIDOKEZO
    Tazama mchoro ufuatao kisha ujibu maswali yaliyo hapo chini yake
    x

    Maswali

    1. Elezea yale unayoyaona kwenye mchoro

    2. Watu hawa wanafanya nini?

    SOMO LA 5. MAANA YA MDAHALO
    5.1. Kusoma na ufahamu: Utekelezaji wa elimu ya

    kujitegemea kwa vijana
    Soma mdahalo ufuatao wenye mada “ Utekelezaji wa elimu ya
    kujitegemea kwa vijana wa leo ni dhaifu zaidi kuliko ule wa vijana wa
    miaka iliyopita ”, kisha ujibu maswali yaliyotolewa hapo chini.


    Mwenyekiti (anasimama
    ): Waheshimiwa mabibi na mabwana mliokusanyika
    hapa hivi leo, hamjambo? Mada ya mdahalo wetu wa leo ni kama mnavyoiona
    ubaoni ni“Utekelezaji wa elimu ya kujitegemea kwa vijana wa leo ni dhaifu zaidi
    kuliko ile ya vijana wa miaka iliyopita.”

    Mimi jina langu ni Kabatesi, mwenyekiti wa mdahalo. Niko pamoja na Gahizi

    kama katibu wa mdahalo wetu pamoja na Uwase atakayechunga muda. Vilevile
    tuna pande mbili hapa. Timu moja inatetea mada na nyingine inapinga mada.
    Bila ya kuchelewa Napenda kumkaribisha bwana (anataja jina lake) ambaye ni
    msemaji mkuu wa kwanza upande wa utetezi ili atoe hoja zake kuhusu mada
    yetu ( anakaa).

    Msemaji wa 1 (Utetezi):
    Mheshimiwa mwenyekiti na washiriki wote, ni wazi
    kabisa kwamba hali ya elimu ya kujitegemea si dhaifu kwa vijana wa leo kama
    mada isemavyo vijana wa leo wameenda shule, wameanza wakiwa wadogo,
    wameendelea na masomo hadi chuo kikuu na kuhitimu itakiwavyo kiasi kwamba
    wanaweza kufanya kazi katika nyanja mbalimbali zinazohitajika katika harakati za
    kulijenga taifa. Vijana wa leo wana mishahara minono. Mheshimiwa Mwenyekiti,
    waheshimiwa wote mnaoshiriki katika mdahalo huu; haya ni baadhi ya mambo
    mengi yanayoweza kututhibitishia kwamba vijana wa leo hushiriki vizuri katika
    kutekeleza elimu ya kujitegemea.

    Mwenyekiti:
    Naam, wasikilizaji washiriki. Nafikiri baada ya kusikiliza hoja za
    msemaji mkuu

    wa kwanza upande wa utetezi, sasa ningependa kumkaribisha msemaji mkuu

    wa kwanza upande wa upinzani naye atowe hoja zake. Karibu!

    Msemaji wa 1 (Upinzani): Asanteni sana mwenyekiti na wasikilizaji washiriki.
    kwa kunipa fursa hii. Sikubaliani na hoja za mtetezi wa mada hii. Msemaji
    aliyetangulia alisema kwamba vijana wa leo wanaanza kusoma wangali wadogo
    na kufikia viwango vikubwa na kupewa shahada za hali ya juu pamoja na
    mishahara minono kuliko wa miaka iliyopita. Vijana wa miaka iliyopita walikuwa
    na namna yao ya kufanya kazi walikuwa wanajituma na walifanya kazi bila
    usimamizi au unyampala, walikuwa si wavivu, vijana wa leo baadhi yao ni wavivu
    kazi haiwezi kufanyika bila kuwa na mtumishi nyumbani kwao, ambapo vijana wa
    miaka iliyopita walijituma kwa shughuli yoyote ile iliyohitaji ujenzi wa taifa, kama
    kuwinda, kwenda vitani, pia kuliwasidia wale wasiojiweza, n.k Nashukuru sana
    kwa kunisikiliza.

    Mwenyekiti:
    Naam! Mambo yameanza kupamba moto. Baada ya kusikiliza
    hoja za wasemaji wakuu wa kwanza kutoka pande zote mbili ningependa
    kumkaribisha msemaji mkuu wa pili kwa upande wa utetezi ili naye atoe hoja
    zake.

    Msemaji wa 2 (Utetezi)
    : Asante sana mwenyekiti, wenzangu watetezi na
    mahasimu wangu wapinzani pamoja nanyi wasikilizaji-washiriki. Ni wazi kwamba
    utekelezaji wa elimu ya kujitegemea kwa vijana wa leo ni dhaifu zaidi kuliko ile
    ya vijana wa miaka iliyopita. Hili ni kwa sababu vijana wa leo hawawezi kufanya
    kazi bila kulazimishwa. Lakini vijana wa zamani walikuwa wakijituma katika
    kutekelza kazi zote ili kuendeleza nchi. Kazi hizo hasa zilikuwa za kilimo, ujenzi
    na kazi nyingine za mikono. Vijana wa leo wao huogopa kutumia mikono yao. Je
    tutaendeaje? Haviwezekani. Asante sana.

    Mwenyekiti:
    Naam! Wapinzani mmekubali? Au mtashikilia shindano? Msemaji
    wa pili, fursa kwako!

    Msemaji wa 2 (upinzani):
    Asante sana mwenyekiti na nyinyi nyote ambao
    mmekusanyika hapa leo hii. Sisi wapinzani hatukubaliani na maoni ya watetezi
    hata kamwe! Je? Mnasema kuwa vijana wa leo hawafanyi kazi lakini siku hizi
    ndipo unaona kuwa kazi mpya zinabuniwa ilhali hapo zamani mtoto alikuwa
    akifuata kazi ya wazazi wake. Kama wahenga walivyosema “Mtoto wa mhunzi
    asiposana huvukuta”. Vilevile hapo zamani vijana waliokuwa wakitoka shuleni
    walikuwa wakisuburi kazi kutoka kwa serikali. Lakini leo mambo ni kinyume.
    Hatusubiri kazi za ofisini tunabuni nyingine mpya na kuajiri vijana wenzetu. Je
    huo si utekelezaji thabiti wa elimu ya kujitegemea? Asante sana.

    Mwenyekiti:
    Mambo yamekuwa shamrashamra kweli! Lakini ninaona kwamba
    muda hauturuhusu kusonga mbele. Hoja nzuri zimetolewa kwa kila upande
    lakini tunahitaji mshindi wa leo. Kwa hiyo ningependa kumkaribisha katibu
    aje atupigishe kura ili tujuwe mshindi wa leo. (Katibu anasimama na kuomba
    wanaotetea wanyoshe mikono na wanaopinga wafanye hivyo baadaye na
    kuhesabu kura).

    Katibu: Upande wa utetezi umepata kura kumi na tano. Upande wa upinzani
    umepata kura ishirini na moja. Kwa hiyo washindi wa mdahalo wa leo ni upande
    wa upinzani. (Wasikilizaji washiriki wanawapigia makofi.)

    Mwenyekiti
    : Mabibi na mabwana, baada ya matokeo haya sina budi kuwaambia
    kuwa huu ni mwisho wa mdahalo wa leo. Tukutane wakati ujao panapokuwa

    majaliwa ya Mungu.

    KAZI 1

    Maswali ya ufahamu
    1. Andika kichwa cha mada ya hapo juu.
    2. Ni pande gani zinazoonekana katika mdahalo huu?
    3. Eleza hoja za mtetezi wa kwanza katika mdahalo huu.
    4. Eleza jinsi vijana wa miaka iliyopita walivyoweza kujituma.

    5. Kwa sababu gani wapinzani walishinda ?

    5.2. Msamiati kuhusu mdahalo

    KAZI 2

    Unganisha maneno ya safu A na maana yake katika safu B

    kutokana na jinsi yalivyotumika katika kifungu cha habari .

    d

    KAZI 3

    Tunga sentensi zenye maana kamili kwa kutumia maneno
    yafuatayo yaliyotumika katika kifungu cha ufahamu:
    1. Kutetea
    2. Kujituma
    3. Katibu
    4. Mwenyekiti

    5. Kusikiliza

    5.3. Sarufi: Matumizi ya viambishi rejeshi kulingana na

    ngeli za majina

    KAZI 4

    Angalia mifano ya sentensi zifuatazo kisha ueleze viambishi
    vilivyopigiwa mistari.
    1. Mwenyekiti aliyeongoza mdahalo wa jana alikuwa msomi.
    2. Wanafunzi- walimu watakaoshinda vizuri watazawadiwa.
    3. Vijana waliokuwa wakitoka shuleni walikuwa wakisubiri kazi kutoka
    kwa serikali.
    4. Kazi nyingi zilizobuniwa ni za vijana.

    • Viambishi vilivyopigiwa mistari ni virejeshi au viambata.
    Maelezo muhimu kuhusu virejeshi/viambata

    Kirejesh
    i ni kiambishi kinachotiwa katika kitenzi ili kurejerea tendo kwa

    mtendaji. Ni kusema kuwa kirejeshi hujulisha kwamba jina/kiwakilisha
    kilichotajwa ndicho kilichofanya/kinachofanya/hufanya/kitakachofanya au
    kilichofanyiwa’kinachofanyiwa/hufanyiwa/kitakachofanyiwa jambo fulani. Jina/
    kiwakilishi kinachorejelewa hutangulia kitenzi.

    Isipokuwa kwenye ngeli ya A-WA katika umoja mahali ambapo kirejeshi huwa –

    ye mahali pengine kirejesshi ni –o kikabadilika kulingana na ngeli za majina kama

    jedwali lifuatalo linavyoeleza :

    x

    KAZI 5

    Jaza kwa kutumia kirejeshi kilicho mwafaka
    1. Kitabu uli…nipa kimenifurahisha.
    2. Mwendo una…kwenda utakuponza.
    3. Jino daktari ataka…ng’oa ni hili bovu.
    4. Saa ili------tundikwa ukutani imeanguka.

    5. Mwenyekiti ataka…ongoza mdahalo amefika.

    5.4. Matumizi ya Lugha: Maana ya Mdahalo

    KAZI 6

    Soma maelezo muhimu yafuatayo kisha ujibu maswali ya hapo
    chini
    Mdahalo ni majadiliano baina ya watu wengi juu ya jambo moja maalumu.
    Kuna mada inayozungumziwa, wazungumzaji wakuu wanaotetea mada
    (upande wa utetezi) na wazungumzaji wakuu wengine wanaopinga mada
    (upande wa upinzani). Aghalabu huwa wazungumzaji wakuu wawili kwa kila
    upande.

    Mwenyekiti wa mdahalo ana wajibu wa kufungua na kuendesha mdahalo,

    kuwapa wasemaji nafasi ya kuzungumza, kupigisha kura na kufunga mdahalo.

    Katibu wa mdahalo ndiye huandika hoja zinazotolewa na wazungumzaji

    mbalimbali, kufanya na kusoma muhtasari wa hoja zilizotolewa na pande
    mbili mwishoni mwa mdahalo na kutangaza matokeo ya kura zilizopigwa.
    Mdahalo ukifanyiwa darasani, mwalimu atatoa maoni yake juu ya mdahalo.

    Mdahalo mzuri unaonesha namna ya kuchagua mada inayoleta hoja nyingi

    tofauti (mada hii inapaswa kuwa ile inayoleta mchango fulani katika maisha
    ya jamii, uongozi mzuri wa mwenyekiti na umahiri wa wanaozungumza katika
    utafutaji na utoaji wa hoja ndivyo baadhi ya vipengele vinavyochangia katika
    kuboresha mdahalo.

    Jibu maswali yafuatayo:

    1. Ni lipi jukumu la mwenyekiti wa mdahalo?
    2. Katibu ana jukumu lipi katika mdahalo?
    3. Kuna aina ngapi za wazungumzaji katika mdahalo? Zitaje

    4. Ni zipi sifa za mdahalo mzuri?

    5.5. Kusikiliza na Kuzungumza
    KAZI 7
    Andaa mdahalo kisha uwasomee wenzako msimamo wako kuhusu

    mada isemayo:

    «Kazi za ofisini ndizo zinazoendeleza uchumi wa nchi yetu. »

    5.6. Kuandika
    KAZI 8

    Tunga mdahalo kuhusu mada ifuatayo :

    “Usawa wa jinsia ndiyo njia sahihi ya kuendeleza nchi yetu”

    SOMO LA 6: MWONGOZO WA MDAHALO

    v

    KAZI 1
    Tazama mchoro hapo juu kisha ujadili unayoyaona yakitendeka kwenye
    mchoro husika.


    6.1. Kusoma na ufahamu: Tutokomeze dawa za kulevya

    Soma mdahalo ufuatao kisha ujibu maswali ya ufahamu.

    “Wazazi wana wajibu mkubwa katika kutokomeza dawa za kulevya

    zinazoharibu vijana.”
    Mwenyekiti: Waheshimiwa wote mabibi na mabwana mliokusanyika hapa,
    kwanza ninataka niwakaribisheni kwenye mdahalo usemao kuwa “Wazazi wana
    wajibu mkubwa katika kutokomeza dawa ya za kulevya zinazoharibu
    vijana.” Karibuni sana nyote na bila kupoteza muda, ninamkaribisha mshiriki

    upande wa utetezi kutoa mchango wake.

    Msemaji wa 1 (Upande wa utetezi): Ninawashukuru sana viongozi,
    wasikilizaji na washiriki wenzangu. kuniruhusu kuzungumzia mada isemayo
    Wazazi wana wajibu mkubwa katika kutokomeza dawa za kulevya
    zinazoharibu vijana.
    ” Kama inavyojulikana elimu ya kwanza ya mtoto huanzia
    nyumbani. Nyumbani ndipo mtoto anapopata malezi ya msingi ambayo huanzia
    uimarishaji wa msingi wa malezi. Malezi haya ya kwanza ambayo hupatikana
    nyumbani humsaidia na kumuimarisha mtoto katika kufanikiwa katika maisha
    yake. Kwa hiyo wazazi wakitoa malezi bora vijana wataepukana na utumiaji wa
    madawa ya kulevya.

    Mwenyekiti
    : Asante sana kwa mazungumzo mazuri. Kama mlivyosikia, msemaji
    huyu ameeleza kwamba wazazi ndio wenye jukumu la kuwapatia watoto wao
    uimalishaji imara wa elimu ya mtoto kutokana na haya ndio wenye wajibu mkubwa
    katika kutokomeza madawa ya kulevya. Sasa ebu nitoe fursa kwa mshiriki wa
    upande wa upinzani.

    Msemaji wa 1 (Upande wa upinzani)
    : Asante sana kiongozi kwa fursa hii ya
    kuniruhusu kutoa mchango wangu. Kwa maoni yangu, ni kweli kwamba wazazi
    wana nafasi kubwa kwa watoto wao na hasa wale walio wadogo kuanzia
    chekechea . Lakini, kwa wale walio wakubwa kuna matatizo makuu ambayo
    wazazi hawawezi kutilia mkazo kwani watoto hao hawashindi na wazazi wao,
    wengine wako shule za sekondari wengine wanajipangia nyumba zao za kuishi
    wakati wa kusoma shule; kwa hiyo naona jukumu kubwa ni la walimu katika
    kutokomeza madawa ya kulevya yanayoharibu vijana. Hili ni kwa sababu walimu
    ndio wanaoshinda na watoto hao muda mrefu. Kwa hiyo walimu wakiwafuatilia
    karibu wanaweza kuepukana na madawa hayo nao wakatoa mchango wao
    katika kuendeleza nchi.

    Mwenyekiti:
    Ninamshukuru sana mshiriki upande wa upinzani. Ameelezea
    kwamba jukumu

    kubwa katika kutokomeza madawa ya kulevya yanayoharibu vijana ni kazi ya

    walimu ambao huwa na vijana hawa muda wote wa masomo. Hebu, tumsikilize
    pia mshiriki aliyenyosha mkono pale upande wa utetezi .

    Msemaji wa 2 (Upande wa utetezi):
    Ninawashukuru Mheshimiwa
    kiongozi,wasikilizaji na washiriki wenzangu. Watu ambao wako karibu sana
    na watoto ni wazazi wao ambao wana mchango wa kwanza katika malezi ya
    watoto hao. Wazazi huwatunza watoto wao, tangu wanapozaliwa na wakati
    wa kwenda shule unapofika, wao ndio wanapiga hatua ya kwanza kuwapeleka
    shuleni. Wajibu wa kila mzazi ni kupeleka mtoto wake shuleni kwani anapata
    mwenendo mwema utakaomsaidia maishani mwake. Watoto wanapofika
    shuleni, ni vyema wazazi wao wawajibike kufuatilia malezi, nidhamu na matendo
    ya watoto wao kwa kuwashauri, kuwafundisha kuwa na mienendo mizuri.
    Waheshimiwa wasikilizaji, kama mnavyoelewa, bila mchango wa wazazi, vita hivi
    dhihi ya dawa za kulevya vitatushinda. Je mtoto anapokuwa likizoni, atampata
    wapi mwalimu wa kumkanya? Au anapotoka shule jioni na kuelekea nyumbani
    mwalimu atamsindikiza? Tunaposema mzazi hatusemi yule aliyemzaa mtoto tu!
    Hapa tunataka kusema kila mtu mzima anayekutana na mtoto huyu. Akimwona
    katika matendo maovu vizuri amkanye. Wazazi wakifanya haya visa vile vya
    wizi, madawa ya kulevya, utovu wa nidhamu hautakuwepo kwa sababu wazazi
    watakuwa wakiwafuatilia karibu watoto wao. Asante sana kwa kunitega sikio,
    hayo ndiyo maoni yangu.

    Mwenyekiti:
    Baada ya kusikiliza hoja za msemaji mkuu wa pili kwa upande
    wa utetezi, ningependa kumpa fursa msemaji wa pili upande wa upinzani. Karibu
    ndugu!

    Msemaji wa 2 (Upande wa upinzani)
    : Asante sana mwenyekiti kwa kunipa
    fursa hii. Mimi sina mengi ya kusema kwa kuwa msemaji wa kwanza mwenzangu
    amesema mengi. Na ninafikiri kuwa yanatosha. Asante sana.

    Mwenyekiti
    : Naam! Baada ya kusikiliza hoja za wasemaji wakuu wa pande
    zote mbili yaani upande wa utetezi na upande wa upinzani, tutafanya uchaguzi ili
    tuone ni upande upi ambao umeshinda safari hii. Tutapiga kura kwa kunyoosha
    mikono kisha katibu atahesabu kura.

    Katibu
    : Upande wa utetezi umepata kura kumi na tano (aandike 15 ubaoni).
    Upande wa upinzani umepata kura kumi (anaandika 10 ubaoni).
    Mwenyekiti: Mabibi na mabwana, baada ya matokeo haya kura zinaonyesha
    kuwa ushindi katika mdahalo huu umeangukia upande wa utetezi (ukumbi
    uliwapigia makofi washindi na mwalimu wa somo akatoa maoni yake juu ya
    mdahalo huo. na ukawa mwisho wa mdahalo)

    KAZI 2
    Maswali ya ufahamu

    1. Taja mada inayozungumziwa katika mdahalo.
    2. Kuna makundi ya aina ngapi katika mdahalo huu ?
    3. Mtetezi wa pili alieleza kuwa mzazi ni nani ?
    4. Ni upande gani ulioshinda? Kwa sababu gani?
    5. Mdahalo ulimalizika kivipi?

    6.2. Msamiati Kuhusu mdahalo
    KAZI 3
    Tunga sentensi sahihi kwa kutumia maneno yafuatayo:
    -- Wajibu
    -- Kutokomeza
    -- Jukumu
    -- Mienendo
    -- Ukumbi

    6.3. Sarufi: Matumizi ya viambishi rejeshi kulingana na
    ngeli za majina
    .
    KAZI 4
    Chunguza sentensi zifuatazo kisha ueleze mabadiliko
    yanayojitokeza
    1. Mwenyekiti ambaye aliongoza mdahalo wa jana alikuwa msomi.
    2. Mwenyekiti aliyeongoza mdahalo wa jana alikuwa msomi.
    3. Binadamu ambao huishi kwa amani na wenzao pamoja na mazingira
    yao husifika.
    4. Binadamu waishio kwa amani na wenzao pamoja na mazinira yao
    husifika.

    Maelezo muhimu

    Kirejeshi ni kiambishi kinachotiwa katika kitenzi ili kurejerea tendo kwa mtendaji.
    Ni kusema kuwa kirejeshi hujulisha kwamba jina lililotajwa ndilo lililofanya au
    lililofanyiwa jambo fulani.

    Tunapotumia
    amba- haturuhusiwi kutumia kirejeshi hii ni kwa sababu ambainasimama
    sawasawa na kirejeshi. Kwenye vishirikishi vipungufu na kwenye
    kitenzi katika wakati wa mazoea, kirejeshi huja mwishoni.

    Mifano

    1. Mkufunzi ambaye alitufundisha Kiswahili mwaka jana amehama.
    2. Mkufunzi aliyetufundisha Kiswahili mwaka jana amehama.
    3. Mvua ambayo hunyesha kila siku si nzuri.
    4. Mvua inyeshayo kila siku si nzuri.
    5. Ni huku ambako tulikuwa tukizungumzia.
    6. Huku ndiko tulikokuwa tukizungumzia

    KAZI 5
    Ondoa amba- katika sentensi zifuatazo:

    1. Gari ambalo tulisafiria lilikuwa na hitilafu.
    2. Mchuzi ambao tulikunywa ulipikwa kwa ustadi.
    3. Amani ambayo sisi Wanyarwanda tunayo tuyatunze vyema.
    4. Nyumba ambazo tutazijenga ziwe na viwango vya kujengea nyumba.
    5. Mazingira ambayo tunastahili kuishi ndani ni yale yenye hewa safi.

    6.4. Matumizi ya lugha: Mwongozo na utekelezaji wa
    mdahalo
    KAZI 6
    Soma maelezo muhimu hapo chini kisha ujibu maswali yanayofuata:
    Maandalizi ya mdahalo

    a) Kuchagua mada ya kuzungumzia katika mdahalo: uchaguzi huu
    hufanyika kwa kupiga kura.
    b) Kumchagua mwenyekiti wa mdahalo: mwenyekiti huchaguliwa kwa
    kupiga kura na atakayechaguliwa ni yule mwenye uwezo wa kuongoza
    na kuendesha mdahalo.
    c) Kumchagua katibu wa mdahalo: mhusika huyu pia huchaguliwa, yeye
    ana wajibu wa kuandika na kuwasomea hadhira muhtasari na matokeo
    ya mdahalo.
    d) Kumchagua mtunzawakati: huyu ana jukumu la kuchunguza kwamba
    kila mhusika anatumia muda aliopewa katika kutoa hoja zake.
    e) Kupanga wahusika kwa upande wa utetezi na upande wa upinzani
    kama wasemaji wakuu wa pande hizo.
    f) Kupanga namna ya kukaa kwa wahusika wa mdahalo upande wa
    utetezi na upande wa upinzani na wasikilizaji pia. Kitendo hiki huweza
    kufanywa kwa kupanga watetezi na wapinzani kwenye pande mbili
    (upande wa kulia na upande wa kushoto) ambapo watabadilishana
    mawazo kwa urahisi.
    g) Kupanga muda utakaotumiwa na wahusika wa pande hizo mbili.

    • Mambo ya kuzingatia katika utekelezaji wa mdahalo :

    a) Kutumia vizuri muda uliopangwa.
    b) Kuepuka fujo, kelele na usumbufu wowote.
    c) Kutoa sauti inayosikika unaporuhusiwa kutoa hoja yako.
    d) Kutoa maoni kuendana na mada inayozungumziwa.
    e) Kutumia lugha rahisi na yenye adabu au heshima.
    f) Kuheshimu mawazo ya watu wengine wanapoongea
    g) Kuwa na mpangilio mzuri wa mawazo wakati wa kuzungumza
    h) Kukumbuka kuwa mdahalo ni mchezo si pambano.

    Jibu masali yafuatayo:

    1. Mtunzawakati ana jukumu gani?
    2. Mwenyekiti anapaswa kuwa na sifa gani?
    3. Jadili mambo mawili ya kuzingatia katika uandalizi wa mdahalo.

    4. Kwa sababu gani tunasema kuwa mdahalo si pambano?

    6.5. Kusikiliza na Kuzungumza
    KAZI 7
    Chunguza mada ifuatayo kisha utafute hoja za kuitetea na za
    kuipinga hatimaye uwasilishe darasani:

    “Nidhamu ya vijana wa leo ni bora kuliko nidhamu ya vijana wa zamani.”

    6.6. Kuandika
    KAZI 8
    Tunga mdahalo juu ya mada ifuatayo:
    “Madawa za kulevya hazina umuhimu katika maisha ya binadamu.”
    Tathmini ya mada
    1. Toa maana ya mdahalo.
    2. Eleza baadhi ya mambo ya kuzingatia katika utekelezaji wa mdahalo.
    3. Taja sifa za mdahalo mzuri.
    4. Eleza mambo ya kujiepusha katika mdahalo.
    5. Mdahalo huongozwa na nani? Anafanya kazi gani?
    6. Kwa sababu gani tunasema kuwa mdahalo si pambano?
    7. Taja masuala mtambuka yanayopatikana katika midahalo tuliyoona hapo juu.
    8. Jaza nafasi kwa kutumia kirejeshi kilicho mwafaka:

    i) vyakula viandaliwa-----vitafurahisha kila mtu.

    ii) Nguo wazishona ------ ni za bei nafuu.
    iii) Aisifu------ imemnyea.
    iv) Zimwi likujua------- halikuli likakwisha.
    v) Hamna hamna ndi----- mliwamo.

    9. Ondoa amba- katika sentensi zifuatazo:

    i) Mbunge ambaye hutuwakilisha bungeni atatutembelea kesho.
    ii) Kazi ambazo serikali inatuhamasisha kuunda ni zile zinazojenga nchi.
    iii) Vyakula na vinywaji ambavyo sisi hutumia huwa na viwango vya ubora.
    iv) Dawa za kupunguza ukali wa UKIMWI ambazo atapewa zitamsaidia sana.

    v) Umoja ambao sisi Wanyarwanda tunao tuulinde usije ukavunjika tena.

  • MADA YA 4: KISWAHILI NA TEKNOLOJIA

    Uwezo mahususi
    Kutumia kwa ufasaha msamiati maalum katika uwanja wa teknolojia

    Malengo ya Ujifunzaji

    -- Kubainisha vyombo vitumiwavyo katika mawasiliano ya kiteknolojia;
    -- Kujadili faida na hasara za mawasiiliano ya kiteknolojia;
    -- Kutunga barua mbalimbali za mawasiliano ya kiteknolojia kwa kutumia
    msamiati maalum
    -- Kutunga sentensi sahihi kwa kutumia viambishi vya masharti: -nge- -ngelina

    -ngali-

    KIDOKEZO

    Toa maoni yako kuhusu maswali yafuatayo:
    1. Ni vyombo vipi vya kiteknolojia vinavyoweza kutumiwa
    katika mawasiliano?

    2. Je, vyombo hivyo vina faida au hasara gani?

    SOMO LA 7: MAWASILIANO YA KITEKNOLOJIA

    b

    KAZI 1
    Tazama kwa makini picha hapa juu. Jadili moja kwa moja matumizi yake.

    7.1. Kusoma na ufahamu: Tahadhali vijana!
    Amina na Simeon ni wanafunzi wa Shule ya Ualimu wilayani Gatsibo.
    Wanazungumzia jinsi teknolojia ya habari na mawasiliano (TEHAMA) huweza
    kurahisisha mawasiliano na kupotosha akili ya watumiaji wake.
    y
    y
    g
    r
    KAZI 2
    Maswali ya ufahamu
    Chagua jibu sahihi
    1. Wahusika wanaozungumziwa ni:
    a) Amina na Simeon.
    b) Watumiaji wa vyombo vya mawasiliano ya kiteknolojia.
    c) Amina, Simeon pamoja na mpenzi wake Amina.

    d) Hakuna jibu sahihi

    2. Amina ameleta simu ya mkononi shuleni kwa sababu ya:
    a) kuwasiliana na mpenzi wake aliyeko ugenini.
    b) kutupia jicho wakati wa jaribio na mtihani.
    c) kupakua maelezo ya somo la Biolojia na Jiografi.
    d) burudani kwa mawasiliano na mpenzi wake pamoja na kuitupia jicho

    wakati wa jaribio na mtihani.

    3. Amina alipata anwani ya mpenzi wake kupitia:
    a) Watisapu.
    b) Fesibuku.
    c) Tovuti.
    d) barua pepe.

    4. Mpenzi wake Amina alimpelekea Amina simu ya mkononi kwa ajili ya:

    a) kurahisisha mawasiliano kati yao.
    b) kuendeleza hali ya teknolojia ya habari na mawasiliano barani Afrika.
    c) kumwondolea mpenzi wake aibu.
    d) Majibu mengine ni sahihi isipokuwa b.
    5. Simu ya mkononi hairuhusiwi shuleni kwani:
    a) inaweza kutumiwa katika vitendo tofauti vya upotovu.
    b) ni chombo cha bei ghali.
    c) inaweza kuleta fujo darasani.
    d) husababisha gharama nyingi.

    6. Wakati una mabawa maana yake ni:

    a) Ningekuwa na mabawa nigeruka mpaka Marekani.
    b) Wakati wa jambo kutendeka ni huu.
    c) Utakuwa na mabawa lini?

    d) Majibu yote ni sahihi.

    7.2. Matumizi ya msamiati
    KAZI 3
    Jaza sentensi zifuatazo kwa kutumia msamiati huu: kupekua,
    tovuti, kupiga marufuku, kutia aibu, ana kwa ana, kubakwa,
    uasherati, barua pepe.

    1. Kufeli mtihani wa taifa ni jambo la..........................kwa mwanafunzi
    binafsi na kwa wazazi wake.
    2. ...............huanzwa na https://www.
    3. Watu wengi hu.................picha kwa kutumia Youtube.
    4. ......................ni vitendo vya uzinifu, yaani kufanya mapenzi nje ya
    ndoa. Vitendo hivyo ni vya........................kwa ajili ya kupigana dhidi ya
    ugonjwa wa UKIMWI.
    5. .......................ni njia ya kuwasilisha ujumbe kwa mtu aliye mbali au
    karibu bila kuangaliana..............................
    6. Wakati wa mauaji ya kimbari dhidi ya Watutsi nchini Rwanda
    wanawake pamoja na wasichana wengi waliumizwa na vitendo vya

    .......................

    7.3. Sarufi: Matumizi ya kiambishi cha masharti –nge-
    KAZI 4
    Eleza dhana ya kiambishi –nge- katika sentensi zifuatazo:
    i) Ungejua athari ya mienendo mibaya hiyo kwa maisha yako,
    usingeendelea kupotoshwa na uongo wa mawasiliano kutoka
    mitandao ya intaneti au tovuti mbalimbali.

    ii) Nisingekuwa na simu ya mkononi, nisingekuwa kama nilivyo leo.

    MAELEZO YA KUZINGATIA
    Nge hutumika kuonesha uwezekano au majuto, yaani hutumika kuonyesha
    kwamba kitendo fulani hakijafanyika na kwa hiyo jambo fulani halijatokea lakini
    kuna uwezekano wa kufanya kitendo hicho na jambo hilo litokee.

    Mfano:

    1. Ningejua umuhimu wa elimu, ningewafundisha watoto wangu.
    → Sentensi hii inaonesha majuto: Sikujua umuhimu wa elimu, kwa hiyo
    sikuwafundisha watoto wangu.
    2. Ningekuwa na mchumba, angeninunulia simu ya mkononi aina ya Nokia.
    → Sentensi hii inaonyesha uwezekano: Bado sina mchumba wala simu ya
    mkononi aina ya Nokia, lakini nikimpata mchumba ataweza kuininunulia.
    Tanbihi: Katika hali kanushi nge hutanguliwa na kikanushi –si-
    Mfano:
    Nisingekuwa na simu ya mkononi, nisingekuwa kama nilivyo leo.

    KAZI 5
    Eleza ikiwa kiambishi -nge- kinaonyesha uwezekano au majuto.

    a) Angefanya bidii, asingeshindwa mtihani wa taifa.
    b) Wangewapatia watoto wao maadili, wangefaidika na matokeo mazuri.
    c) Tungejua kuwa mvua itanyesha leo, tungeleta miavuli.
    d) Mngetimiza wajibu wenu kazini, msingefukuzwa.

    7.4. Matumizi ya lugha: Vyombo na njia mbalimbali katika
    teknolojia ya habari na mawasiliano
    KAZI 6
    Zungumzia kuhusu vyombo vinavyotumiwa pamoja na njia za
    kuwasilisha ujumbe


    MAELEZO YA KUZINGATIA
    A. Vyombo vya uwasilishaji wa habari na mawasiliano.
    Kuna aina mbalimbali za vyombo ambavyo hutumiwa katika teknolojia ya habari
    na mawasiliano kama vile:
    • Redio.
    • Runinga au televisheni.
    • Simu.
    • Tarakilishi au kompyuta.
    • Posta.
    • Satalaiti, n.k.

    B. Njia za uwasilishaji wa habari na mawasiliano

    • Fesibuku
    • Watisapu
    • Twita
    • Skaipu
    • Faksi
    • Barua pepe
    • Tovuti
    • Telegramu

    • Instagramu

    KAZI 7

    Husisha ishara zifuatazo na maana yake

    r

    7.5. Kusikiliza na Kuzungumza
    KAZI 8

    Igiza mazungumzo kati ya Amina na Simeon.

    7.6. Kuandika
    KAZI 9

    Tunga kifungu cha habari chenye aya tatu kuhusu faida za TEHAMA.

    SOMO LA 8: MAWASILIANO KWA NJIA YA SIMU

    YA MKONONI

    s

    KAZI 1
    Tazama kwa makini mchoro hapo juu. Unadhani watu hawa

    wanashughulikia nini? .

    e

    d

    Maswali ya ufahamu
    KAZI 2
    Chagua jibu sahihi
    1. Wahusika wanaozungumza ni:
    a) Mkuu wa shule na Mkuu wa masomo.
    b) Viongozi wa shule.
    c) Fisto, Mkuu wa shule na Angela, Mkuu wa masomo.
    d) Majibu yote ni sahihi.

    2. Kifungu cha habari kinazungumzia:

    a) Mkuu wa shule na Mkuu wa masomo.
    b) Kupata hati kutoka tarakilishi kwa ajili ya mkutano.
    c) Matumizi ya simu ya mkononi.
    d) Kubonyeza vidude kwenye tarakilishi.

    3. Angela amepata matatizo ya:

    a) Kutomudu matumizi ya kompyuta.
    b) Kukatika kwa simu.
    c) Kufiuka kwa simu.
    d) Mtandao wa simu, kusanidi kicharazio na kielekezi pamoja na kusabidi

    kichapishi.

    4. Kabla ya kuzima tarakilishi inatubidi:
    a) Kuchapisha nakala.
    b) Kuhifadhi mabadiliko.
    c) Kusasaisha.

    d) Kubonyeza vidude.

    8.2. Matumizi ya msamiati

    KAZI 3

    Jaza sentensi zifuatazo kwa kutumia msamiati huu: kubonyeza
    vidude, kusasaisha, nakala bayana, kumemeka, kicharazo,
    kusanidua, kuamilisha, nakala laini.
    1. Hati iliyohifadhiwa katika kompyuta bila kuchapishwa huitwa...................
    wakati ambapo nakala iliyochapishwa huitwa...................
    2. Zoezi la kwanza kwenye kompyuta ni ...................................
    3. Unaweza .............programu matumizi za simu ya mkononi au tarakilishi
    wakati ambapo zinaonekana kama siyo muhimu.
    4. Ili uweze kuandika kwenye kompyuta ni lazima utumie .........................
    ....................
    5. Baada ya muda mrefu .hati kuhifadhiwa katika kompyuta inatubidi ....
    ..........................................
    6. Simu ya mkononi haiwezi ..................................bila kuchajiwa.
    7. Inatubidi ......................kingavirusi katika kompyuta zetu ili kulinda hati

    zetu dhidi ya virusi.

    8.3. Sarufi: Matumizi ya kiambishi cha masharti –ngeli- au–ngali-
    KAZI 4
    Eleza dhana ya kiambishi –ngeli- au –ngali- katika sentensi
    zifuatazo:
    -- Ningelikuwa na kingavirusi, ningeliiamilisha katika tarakilishi yako ili
    kuepuka uharibifu wa hati.

    -- Ningalifuata maonyo ya wazazi wangu, nisingalipata cha mtemakuni.

    MAELEZO YA KUZINGATIA
    Ngeli au ngali mara nyingi hutumiwa katika wakati uliopita kuonesha uwezekano
    au majuto, yaani hutumika kuonesha kwamba kitendo fulani hakijafanyika na kwa
    hivyo jambo fulani halijatokea lakini kuna uwezekano wa kufanya kitendo hicho
    na jambo hilo litokee.

    Mfano:

    Ningelikuwa na kingavirusi, ningeliiamilisha katika tarakilishi yako ili kuepuka
    uharibifu wa hati.
    Ningalifuata maonyo ya wazazi wangu, nisingalipata cha mtemakuni.

    Tanbihi:

    1. Ni kosa la kisarufi kuchanganya ngeli na ngali katika sentensi moja. Ikiwa
    kipande cha kwanza kimetumia ngeli, ni lazima ngeli itumiwe pia katika
    kipande cha pili n.k
    2. Katika hali kanushi ngeli au ngali hutanguliwa na kikanushi –si-

    Mfano: Ningalifuata maonyo ya wazazi wangu, nisingalipata cha mtemakuni.

    KAZI 5

    Weka sentensi hizi katika hali yakinishi au kanushi.
    a) Nisingelisoma, nisingeliwafundisha watoto wangu.
    b) Wangalihifadhi mazingira yao, wangaliishi kwa usalama.
    c) Mngeliepuka tabia ya uzinifu, msingeliambukizwa ugonjwa wa ukimwi.

    d) Ungalishughulikia kazi za ujasiliamali, ungalijiendeleza kiuchumi.

    8.4. Matumizi ya lugha: Vyombo na njia mbalimbali katika

    teknolojia ya habari na mawasiliano.

    KAZI 6
    Kwa kutegemea mchoro, onyesha vipengele muhimu vya

    kompyuta au tarakilishi

    m

    8.5. Kusikiliza na Kuzungumza
    KAZI 7

    Igiza mazungumzo kati ya Fisto na Angela.

    8.6. Kuandika
    KAZI 8
    Tunga kifungu cha habari chenye aya angalau tatu kuhusu hasara

    za TEHAMA.

    Tathmini ya mada
    I) Taja vyombo angalau vitano vya TEHAMA na kueleza matumizi yake.
    II) Chagua jibu sahihi:
    1. Ili ujumbe kutoka Fesibuku uwasilishwe ni lazima kuwe na vifaa
    vifuatavyo isipokuwa:
    a) tarakilishi au simu ya mkononi.
    b) mtandao wa intaneti.
    c) anwani ya mtumaji na mpokezi wa ujumbe.
    d) meza ya kuwekea tarakilishi pamoja na kiti cha kukalia.
    2. Mawasiliano kwa njia ya Watisapu huwezekana iwapo kuna:
    a) simu ya mkononi iliyounganishwa kwenye mtandao wa intaneti.
    b) simu kadi pamoja na chaji.
    c) simu ya mkononi pamoja na mtumiaji.
    d) simu ya mkononi iliyounganishwa kwenye mtandao wa intaneti pamoja
    na mtumiaji.
    3. Google ni aina ya:
    a) mtandao.
    b) tovuti.
    c) barua pepe.
    d) tarakilishi.
    4. Youtube hutumiwa:
    a) kupelekea mtu barua pepe.
    b) kubonyeza vidude.
    c) kupakua picha.
    d) kutangaza habari.
    5. Kielekezi kazi yake ni:
    a) kuonesha nafasi ya kuandikia kwenye tarakilishi.
    b) kufuta maandishi.
    c) kuchapisha nakala.
    d) kusanidua nakala laini.
    6. Badilisha sentensi zifuatazo kwa kutumia kiambishi –nge-, -ngeli- au–ngali-.
    a) Sikununua chai kwa sababu nilikosa pesa.
    b) Nikifanya kwa bidii sitafeli mtihani wa taifa.
    c) kama hukujua umuhimu wa kuhifadhi mazingira hukupanda miti karibu

    na nyumba yako.

    MAREJEO
    Waititu, F. na Wenzake (2008): Kiswahili Fasaha. Kitabu cha Mwanafunzi.
    Kidato cha Tatu. Oxford University Press, East Africa Ltd, Nairobi, Kenya.

    TUKI (2004): Kamusi ya Kiswahili Sanifu. Toleo la Pili. Oxford University Press.


    Bakhressa, S.K. na Wenzake (2008): Kiswahili Sanifu. Kitabu cha Mwanafunzi.

    Darasa la Saba. Oxford University Press, East Africa Ltd, Elgon Road, Upper
    Hill, Nairobi, Kenya.

    Nkwera F.M.V. (1978): Sarufi na Fasihi Sekondari na Vyuo. Tanzania Publishing

    House, Dar Es Salaam.

    HARERIMANA, F. (2017): Tujivunie Lugha Yetu. Kitabu cha Mwanafunzi, Kidato

    cha 5. MK Publishers (R) Ltd. Kigali, Rwanda.

    Ndalu, A. E. (2016): Masomo ya Kiswahili Sanifu. Kitabu cha Mwanafunzi.

    Kidato cha 2. Moran (E.A) Publishers Limited.

    Bakhressa, S.K. na Wenzake (2008): Kiswahili Sanifu. Kitabu cha Mwanafunzi.

    Darasa la 8. Oxford University Press, East Africa Ltd, Elgon Road, Upper Hill,
    Nairobi, Kenya.

    Ntawiyanga, S. na Wenzake (2017): Kiswahili kwa Shule za Rwanda. Mchepuo

    wa Lugha, Kidato cha 5. Longhorn Publishers (Rwanda) Limited. Kigali, Rwanda.

    Kenya Literature Bureau (2006): Kiswahili kwa Darasa la Nane. Kitabu cha

    Wanafunzi. Kenya Literature Bureau, Nairobi, Kenya.

    Ntawiyanga, S. na Wenzake (2017). Kiswahili kwa Shule za Rwanda. Mchepuo

    wa Lugha, Kidato cha 6. Longhorn Publishers (Rwanda) Limited. Kigali, Rwanda.

    Niyirora, E. na Ndayambaje, L. (2012): Kiswahili Sanifu kwa Shule za Sekondari.

    Kitabu cha Mwanafunzi Kidato cha Tano. Tan Prints (India) Pvt. Ltd.

    Massamba, D.P.B. na Wenzake (2009): Sarufi Miundo ya Kiswahili Sanifu,

    Sekondari na Vyuo. Taasisi ya Uchunguzi wa Kiswahili. Chuo Kikuu cha Dar es
    Salaam, Tanzania.

    Massamba, D.P.B. na Wenzake (2012): Sarufi Maumbo ya Kiswahili Sanifu,

    Sekondari na Vyuo. Taasisi ya Uchunguzi wa Kiswahili. Chuo Kikuu cha Dar es
    Salaam, Tanzania.

    Nkwera, F.M.V. (1979): Sarufi na Fasihi, Sekondari na Vyuo.Tanzania Publishing

    House, Dar es Salaam,Tanzania.