Topic outline
Sura 1:Mazungumzo na majadiliano
Mada ndogo: Msamiati na mawasiliano katika shughuli za kilimo na ufugaji
A . Msamiati wa msingi kuhusu mazao na shughuli za kilimo na ufugaji nchini Rwanda.
i) Msamiati wa mazao nchini Rwanda
Tazama mazao yafuatayo na usome maneno chini yake.
Bidhaa zilizopo kwenye michoro zinaitwa mazao. Mazao ni vitu tunavyovunabaada ya kupanda mbegu zake.Ni vitu vinavyozaliwa na mimea iliyopandwa. Hapanchini Rwanda, udongo wetu ungali na rutuba ya kutoa mazao mema. Tunapandamimea mbalimbali inayotupatia mazao.Tazama mifano zaidi ya mazao yanayopatikana hapa nchini Rwanda na
usome vifungu kando yake.
Kahawa ni zao la mkahawa au mbuni. Kahawahukaushwa na kusagwa ili kutoa ungaunga.Ungaunga huo hutumiwa kwa kutengenezeakinywaji cha kahawa. Kinywaji cha kahawakina ladha nzuri. Kahawa pia huuzwa katikanchi za nje na kuletea nchi yetu pesa za kigeni.Haya nimajani ya mchai. Majani ya mchai hukaushwana kusagwa. Majani haya hutumiwa kutengenezeakinywaji cha chai. Nchi yetu huuza majani yamchai katika nchi za kigeni. Majani ya mchaipia huletea nchi yetu pesa za kigeni.Hizi ni ndizi. Ndizini zao la mgomba.Ndizi humea kwenyemkungu. Ndiziinaweza kuivishwa na kuliwa moja kwa moja. Baadhi yandizi hupikwa na kuliwa.Ndizi pia huuzwa na kutuleteamapato.Haya ni maharagwe. Maharagwe ni zao la mharagwe.Nafaka hii ni muhimu sana kwa chakula chetu. Hii nikwa kuwa virutubishi vyake vya protini huhitajika sanamiilini mwetu. Wale ambao hawali nyama mara kwa marahuweza kupanda miharagwe na kupata protini zao kutokakwayo.Huu ni mtama. Mtama huzaa punje ndogo ndogo. Punjeza mtama hukaushwa na kuchanganywa na mihogo au mahindi. Baadaye husagwa ili kupata unga. Unga huu hutengenezewa uji au sima (ugali).Haya ni mahindi.Mahindi ni mazaoya mhindi. Mahindi hukaushwa nakusagwa ili kutoa unga wa dona.Unga wa mahindi hutengenezewasima au ugali.Mahindi pia yanaweza kupikwa pamoja namaharagwe kutengenezea pure au kande. Pure ni chakula kitamu kinachoshibisha vilivyo. Ama hindi linaweza kuchomwa au kuchemshwa na likawa chakula kwetu. Mafuta ya mahindi hutumiwa kutengenezea mafuta ya kupikia. Mbali na mahindi, njugu pia hutengenezewa mafuta ya kupaka kwenye mkate. Njugu ni zao la karanga. Njugu hukaangwa na kuliwa. Baadhi ya watu hutwanga njugu na kutengeneza borohoa ya kuungia kitoweo.Haya ni mananasi. Nanasi ni zao la mnanasi.Nanasi huivishwa na kuliwa.Nanasi hutoa maji matamu yanayomaliza kiu.Maji hayo hutumiwa kutengenezea sharubati au soda.Hii ni mihogo. Muhogo ni mzizi wa muhogo.Muhogo huweza kuchemshwa au kukaangwa na kuliwa.Muhogo pia huweza kukaushwa, ukasagwa na kutengenezewasima.Hizi ni mbatata. Mbatatani viazi vya mviringo. Viazi hivi havina sukari. Mbatatahuweza kupikwa kama kiungo. Pia, huchemshwa nakuliwa na vinywaji au vyakula vinginevyo. Mbatata piahukatwakatwa kwa vipande vyembamba na kutiwa ndaniya mafuta ili kutengenezea vibanzi au chipsi.Hivi ni viazi vitamu. Viazi hivi hupandwa katika matuta au sesa.Viazi vitamu huchemshwa na kunywewa kwa chai au kahawa.Viazi vitamu huwa na sukari kiasi cha haja.Zoezi
1. Angalia maana ya maneno yaliyokolezwa kwa wino katika kamusi.Tunga sentensi sahihi kwa kila neno.2. Taja mazao zaidi yanayopatikana nchini Rwanda lakini hayajatajwa katika kifungu.Je, mazao hayo yana faida gani?3. Tunga sentensi sahihi ukitumia maneno yafuatayo:a) ndizi b) mahindi c) kahawad) mbatata e) maharagwe f ) chai4. Taja majina ya mazao haya na faida zake.Kazi ya wanafunzi wawili wawili
Jiunge na mwanafunzi mwenzako. Jadilianeni kuhusu majina na faida ya mazao mbalimbali katika maeneo mnakoishiKazi ya kikundi
Katika vikundi, kila mwanafunzi ataje mazao yasiyopatikana katika eneo anamoishi.Jadilianeni kuhusu faida za mazao mliyoyataja.ii) Msamiati kuhusu shughuli za kilimo nchini Rwanda
Jiunge na mwanafunzi mwenzako. Jadilianeni kuhusu shughuli mbalimbali za kilimo kwenye michoro.Mfano
Soma kifungu kilichopo hapa chini na ujibu maswali chini yake.
HABIMANA: Habari za asubuhi wenzangu?KAREKEZIna ITUZE: Nzuri sana Habimana.HABIMANA: Wenzangu, naomba mnieleze maana ya kilimo.KAREKEZI: Kilimo au zaraa ni kazi ya kulima shamba na kukuza mimea hadikufikia kiwango cha kuvunwa.HABIMANA: Wenzangu, naomba mnitajie shughuli hizi za kilimo.KAREKEZI: Kwanza, kuna kufyeka. Sisi hufyeka shamba letu kwa kutumiaupanga na fyekeo. Baadaye, kuna kulima shamba ili kuandaa konde.Katika kijiji chetu, tunatumia jembe la mkono kuandalia konde.HABIMANA: Kwa nini mnatumia jembe la mkono?KAREKEZI: Kwa sababu mashamba katika kijiji chetu ni madogomadogo.Vilevile, wakulima katika kijiji chetu hawawezi kumudu mbinunyinginezo za kulima. Je, Ituze, wakulima katika eneo lenuhutumia mbinu zipi kuandaa mashamba yao?ITUZE: Wakulima katika eneo letu hutumia plau inayovutwa na ng’ombe au punda.Wakulima katika eneo jirani nao hutumia plau inayovutwa na trekta. Wakulimahao wanamiliki mashamba makubwa. Pia wanaweza kulipia gharama za trekta.Karekezi, hebu tueleze namna nyingine ya ukulima katika eneo lenu.KAREKEZI: Sisi hulima sesa. Tunapojiandaa kupanda mbegu, huchanganya mbolea ya samadina udongo. Udongo wetu hauna rutuba ya kutosha. Baada ya kuweka mbolea,tunapanda mbegu za mahindi na maharagwe ndani ya udongo na kuzifukia.Mbegu zinapoota, tunapalilia miche ili kuondoa magugu au kwekwe. Baadhi yawakulima huweza kupiga dawa za kuwaua wadudu waharibifu.Wakati wa kiangazi,kuna kunyunyizia mimea maji. Baada ya mimea kukua na kukomaa, tunavuna. Viazina mihogo yetu ndiyo hutuletea pesa za matumizi nyumbani kwetu. Tunakula baadhiya mazao hayo na kuyauza mengine.HABIMANA: Kumbe kazi hii ya kilimo ni nzuri mno! Nilisoma juzi kuwa nchi yetu hupata pesaza kigeni kwa kuuza chai na kahawa katika nchi za kigeni.ITUZE: Kweli kabisa. Uchumi wa Rwanda umeimarika kwa sababu ya kilimo.Maisha ya wakulima wengi yameimarika pia. Watu wengiwameajiriwa kutokana na kilimo.HABIMANA: Hata mimi nitaanza kufanya shughuli hizi za kilimo. Tuna shambadogo lakini lina rutuba nyingi. Nitapanda mboga na njugu.Asanteni kwa kunifunza kuhusu kilimo. Kushauriana katika kaziya kilimo ni jambo lililo muhimu mno.KAREKEZI: Pia, tusome kwa bidii hadi chuo kikuu ndipo tuwe wakulima bora zaidi.Tukisoma kwa bidii, tutajifunza na kutumia mbinu za kisasa za kilimo.Mbinu hizi zitatusaidia na kusaidia jamii. Kilimo kitaimarika.ITUZE: Taibu! Pia tukisoma, tutabuni mbinu mpya za kurahisisha kilimona kujiongezea mazao.Ni lazima tufanye juu chini kupata elimu na kufanya utafiti zaidi. Asanteni wenzangu.Maelezo ya msamiati
kufyeka – kusafisha shamba kwa kukata miti au majanikulima – kutayarisha shamba kwa kutifua ardhikonde – sehemu ya shamba iliyolimwasesa – ukulima usiokuwa wa matuta katika ardhi tambararekuzifukia – kuzificha mbegu ardhinizinaota – zinachipuka kutoka ardhinikupalilia – kulima kwa kuondoa magugu katikati ya mimea au michekunyunyizia – kumwagilia maji au dawa ya majikukua – kuongezeka ukubwa au kimokukomaa – kuwa tayari kuvunwa/kutolewa shambanikuvuna – kutoa mazao shambaniMaswali
1. Angalia maana ya maneno haya katika kamusi na uyatungie sentensi sahihi.a) upanga b) fyekeo c) plau d) trekta e) mboleaf ) samadi g) udongo h) rutuba i) kwekwe j) mbeguk) mche l) pampu2. Andika manufaa ya kilimo yaliyotajwa kwenye kifungu. Ongezea manufaa matano zaidi.3. Karekezi na Ndoli hawapendi kilimo. Je, kauli hii ni kweli? Toa sababu zako.4. Je, masomo ya kilimo yana umuhimu gani?5. Tumia maneno uliyopewa kutaja shughuli kwenye michoro.(kufyeka, kulima, kupanda mbegu, kupalilia, kupiga dawa, kunyunyizia maji, kuvuna)6. a) Taja majina na matumizi ya vifaa vilivyopo hapa chini.b) Tunga sentensi sahihi kuhusu kilimo ukitumia jina la kila kifaa hapo juu.7. Andika maneno kumi ya shughuli na zana za kilimo kutoka kwenye mraba huu.Tunga sentensi sahihi ukitumia kila neno.Kazi ya wanafunzi wawili wawili
Jiunge na mwanafunzi mwenzako. Jadilianeni kuhusu shughuli za kilimo katika nchiya Rwanda na manufaa ya shughuli hizo.iii) Msamiati kuhusu shughuli za ufugaji nchini Rwanda
Ufugaji hasa ni kazi ya kutunza wanyama, ndege na hata wadudu. Kazi hii ina faidakubwa sana kama kilivyo kilimo cha mimea. Mfugaji anaweza kufuga wanyama ama wadudu.Kazi ya wanafunzi wawili wawili
Jiunge na mwanafunzi mwenzako. Kumbushaneni majina ya mifugo mbalimbalimliyosoma katika kidato cha kwanza na umuhimu wake.Tazama michoro iliyopo hapa chini na usome kifungu cha maneno kando yake.
Huyu ni Ikirezi. Ikirezi ni mfugaji wa nyuki. Ikirezianarina asali.Baada ya kurina, yeye husafishaasali yake na kuiuza. Asali hiyo hutumiwa kamachakula au hutengenezewa dawa.Huyu ni Gabiro. Gabiro anakata sufu. Sufu ya kondoohutumiwa kutengenezea nyuzi za kufumia nguo.Huyu ni Ituze. Ituze anakamang’ombe.Kabla ya kukama, aliosha chuchu kwamaji vuguvugu na kuzikausha kwa kitambaa safi.Anatumia mkebe safi kuwekea maziwa. Ituzehuwapandisha mitamba kwa dume au mpira.Hili ni josho. Ng’ombe hawa wanaogeshwa kwa dawa ndani ya josho. Wafugaji huosha mifugo katika josho ili kuikinga dhidi ya kupe. Dawa huua viroboto wanaoishi kwenye ngozi za mifugo.Hawa ni Mudenge na Gatera.Mudenge anawalisha kuku kwa mahindi. Pia,huwapa kuku mtama, ugali, wadudu na vyakulavinavyopatikana kwa urahisi. Wakati mwingine,yeye huwapa kuku chakula maalumukilichotengenezwa katika viwanda. Mudenge anawafugakuku wa mayai na nyama. Yeye huuza baadhi ya mayai ili kujipatia riziki. Mudenge pia huwaatamisha baadhi ya kuku wake ili apate vifaranga wa kuuza na kufuga. Gatera naye anawalisha ng’ombe kwa nyasi. Gatera anawafuga ng’ombe wake ndani kwa ndani. Anawapa lishe, maji na dawa humohumo zizini. Gatera hukata pembe za ng’ombe wake. Ng’ombe hukatwa pembe ili kumzuia kumdhuru mtu au kuharibu vitu.Huyu ni Kaliza. Kaliza anapenda kuchunga punda. Anawachunga punda penye maji safi na nyasi nyingi. Kulisha mifugo ni shughuli muhimu ya ufugaji. Mifugo wanapolishwa vizuri hukua kwa haraka, huwa na afya nzuri na hutupatia mapato mazuri.Kaliza anafagia zizi la ng’ombe. Mkulimabora husafisha makao ya mifugo na vyombovyao vya kulia na kulalia. Mifugo wanaolalakatika mahali safi na kula katika vyombo safihuwa na afya njema.Daktari wa mifugo anamtibu kuku kwa kumdunga sindano. Kutibu mifugo ni muhimu kwa mkulima. Ni vizuri kutambua dalili ya ugonjwa ili watibiwe mapema.Msamiati
kurina – kufukuza nyuki kutoka kwenye mzinga na kukata masega ili kupakua asali.kukata sufu – kunyoa manyoya ya kondoo kutoka kwenye ngozi yakekukama – kuminya chuchu za mnyama kama vile ng’ombe ili maziwa yatokekupandisha mtamba – kumpa ng’ombe wa kike mbegu za kiume ili kuzalisha ndamakufuga ng’ombe ndani kwa ndani – kufuga ng’ombe ndani ya eneo au jengo fulani nakuwapa mahitaji yote humo bila kuwatoa njekuwapeleka ng’ombe katika josho – kuwapelekea ng’ombe katika dimbwi maalumu lililotiwa dawa ya kuulia kupekuatamisha kuku – kumfanya kuku kulalia mayaikuchunga – kuwapeleka wanyama malishoni na kuwalinda wasiibwekukata pembe – kutoa pembe kwa kutumia kisu au chuma motokulisha – kupea chakula na majiMaswali
1. Andika majina yote ya mifugo waliotajwa katika ufahamu hapo juu.Taja umuhimu wao.2. Eleza faida za shughuli za ufugaji ulizosoma katika kifungu.3. Jaza mapengo haya kwa shughuli sahihi ya ufugaji.4. Tunga sentensi sahihi ukitumia maneno hapo chini.a) rina asalib) chungac) kata pembed) kamae) lishaf ) fagia zizig) tibu ng’ombeh) pandisha mtambai) atamishaKazi ya wanafunzi wawili wawili
Jiunge na mwanafunzi mwenzako na mfanyeni zoezi hili:1) Kwa pamoja, andikeni shughuli mbalimbali za ufugaji na mifugo nchini Rwanda katika karatasi.2) Kunjeni karatasi hizo na kuziweka pamoja.3) Kila mwanafunzi achukue karatasi moja kwa zamu, asome shughuli ya ufugajiau mifugo katika karatasi aliyochukua na atunge sentensi sahihi kwa kutumianeno katika karatasi yake. Atakayekosea asahihishwe.Kazi ya kikundi
Kama darasa zima, fanyeni mjadala kuhusu: Njia za kisasa za ufugaji zinaleta mapatomakubwa zaidi kuliko njia za kienyeji.B . Majira ya mwaka nchini Rwanda
Tazama michoro iliyopo hapa chini. Je, nini kinafanyika?Soma kifungu hiki na ujibu maswali yaliyoulizwa chini yake.Majira ni kipindi maalumu cha hali ya hewa. Majira haya ndiyo huelekeza upanziwa mimea na uvunaji wa mazao hapa kwetu.Tupo na majira mbalimbali. Yapo majira ya mvua nyingi. Majira ya mvua nyingi yamfululizo huitwa masika. Majira haya hutokea kuanzia mwezi wa Machi hadi Meikila mwaka. Shughuli za kupanda mimea kama vile maharage, mtama, mbatata,mahindi,na kadhalika hutokea mwanzoni mwa majira ya masika. Mimea hiyohuota na kupaliliwa katika majira haya ya masika.Vilevile, mimea mbalimbali kama vile mikahawa, mipareto, migomba, minanasi nakadhalika hustawishwa mnamo majira haya.Msimu huu wa masika hufuatwa na majira ya kiangazi au ukame. Huu ni wakatiambapo jua kali huwaka, mvua hukosa kunyesha na ardhi hukauka. Yapo majiramafupi ya kiangazi ambayo hutokea kuanzia Juni hadi Septemba. Mifugo na mimeahukosa chakula na maji ya kutosha na huanza kuwa na afya mbaya mnamo majira haya.Baadhi ya wakulima huanza kuvuna mazao yao katika majira ya kiangazi.Wengine hulima na kuandaa makonde yao mnamo majira haya kabla ya mvuakuanza kunyesha.Mbali na majira haya, yapo majira ya vuli. Huu ni wakati ambapo huwepo mvuandogo ndogo tu. Majira haya hutokea kati ya mwezi wa Novemba na Februari.Wakati wa vuli, wakulima hupanda vyakula vinavyochukua muda mfupi kukua na kukomaa.Hata hivyo, shughuli nyingi za upanzi hazifanyiki kwa kuwa mvua inyeshayo huwa haitoshikukuza baadhi ya mimea.Hali kadhalika, yapo majira ya kipupwe. Kipupwe ni majira ya baridi ambayo hutokea katikamiezi ya Septemba na Novemba nchini Rwanda. Wakati huu wa mwaka huwepo baridi kalina hubidi watu kuvaa sweta, makoti na hata makabuti.Kwa ufupi, wakulima wengi nchini Rwanda huzingatia majira mbalimbaliwanapofanya shughuli zao za kilimo. Wao hutegemea mvua na jua katika kukuza mimea.Msamiati
masika – majira ya mvua nyingi ya mfululizokiangazi/ukame – majira ya jua kalivuli – majira ya mvua ndogo ndogokipupwe – majira ya baridi kaliMaswali
1. Taja miezi na majira ambapo shughuli hizi za kilimo hufanywa hapa kwetu Rwanda.a) kulima shamba kavub) kuandaa konde lenye unyevunyevuc) kupanda mimea mingid) kupaliliae) kustawisha mimeaf ) kuvunag) kupanda mimea michache inayokua na kukomaa haraka2. Ipo tofauti gani kati ya vuli na kipupwe?3. Tazama mraba ufuatao na uandike maneno manne ya majira.Kazi ya wanafunzi wawili wawili
Jiunge na mwenzako. Chunguzeni michoro ifuatayo na mjaze mapengo kando yake.C . Msamiati wa msingi kuhusu wanyama wa porini na umuhimu wake
i) Msamiati wa wanyama wa porini nchini Rwanda
Tazama wanyama hawa. Je, hawa ni wanyama gani? Wanyama hawawanapatikani katika mbuga na sehemu ipi ya Rwanda?Kisome kifungu kifuatacho ili kujifunza msamiati wa wanyama wa porini.Mnyama wa porini ni mnyama anayeishi katika pori. Pori ni mahali penye miti na nyasi nyingi.Mnyama wa porini hafugwi na binadamu. Wanyama wengi wa porini hupatikana katika mbugaza wanyama. Mbuga za wanyama ni sehemu zilizotengwa na serikali kuwa ndio makazi yawanyama hao wa porini. Je, unafahamu mbuga gani za wanyama nchini Rwanda?Nchi ya Rwanda ina wanyama wengi wa porini.Nchi yetu ya Rwanda inasifika sana kutokanana masokwe. Sokwe ni mnyama mkubwa zaidikatika jamii ya nyani. Mnyama huyu hanamkia. Sokwe ana akili nzuri inayokaribianana ile ya binadamu. Wana uwezo wakumwiga binadamu. Nchi yetu inajulikana
sana kutokana na masokwe. Masokwe hawawanapatikana katika mbuga zetu za wanyama.Masokwe wengi wanapatikana katika Mbugaya Wanyama ya Volcanoes (Volkano).Nyani ni mnyama wa jamii ya sokwe na tumbiri.Nyani ni mdogo kuliko sokwe lakini ana akili nyingi zaidi.Ana masikio makubwa nao mwili wake una rangi ya kaki yakijivu na ngoko nyekundu makalioni. Nyani huishi katikavikundi vya majike na madume. Wana uwezo wa kuishikwa miaka zaidi ya arubaini.Pia kuna tumbiri porini. Tumbiri ni mnyama mdogozaidi katika jamii ya nyani. Tumbiri hupenda sanakukaa mitini. Hula vyakula mbalimbali kama vilematunda, mazao ya mimea mbalimbali na kadhalika.Simba ni mnyama mkubwa wa jamii ya paka.Simba hula nyama. Anaitwa mfalme wa wanyamaau nyika. Simba huishi kwenye vikundi. Vikundihivyo huongozwa na simba dume.Ndovu ndiye mnyama mkubwa zaidi wa porini.Ndovu ana mkonga pamoja na pembe mbilikubwa zenye thamani. Ndovu wana masikiomakubwa na miguu mifupi minene. Ndovu hulanyasi, mizizi, matunda na mashina ya miti. Pia,huishi katika vikundi. Kila kikundi huongozwa nandovu jike ambaye ana umri mkubwa zaidi kulikowote. Uwindaji wa ndovu na kuuza pembezake ni hatia. Sisi sote tunafaa kuwatunza ndovu na wanyama wote wa porini.Chui pia hupatikana katika mbuga zetu. Chui nimnyama wa jamii ya paka lakini aliye mkubwa namkali na mwenye madoadoa ya manjano na meusi.Chui hula wanyama wadogo wadogo wanaoishi porini.Baada ya kuwinda, wao huficha nyama kwenye matawiya mti. Wao hupenda sana kutembea na kuwinda wakatiwa usiku na kupumzika wakati wa mchana.Pundamilia pia ni mnyama wa porini wa jamii ya farasi.Ana milia myeusi na myeupe katika mwili mzima.Inaaminika kuwa milia hiyo huwawezesha kujifichanyikani ili wasionekana na wanyama wanaowawinda.Pundamilia hutembea na kula nyasi katika vikundi vikubwa.Twiga naye ana shingo ndefu, rangi ya kahawia na madoadoa meusi.Twiga ndiye mnyama mrefu zaidi. Yeye hula majani ya miti.Kifaru pia hupatikana katika mbuga zetu. Ni mnyamamkubwa afananaye na kiboko na mwenye kipusa usoni.Nyati pia ni mnyama mkubwa sana. Hufanana na ng’ombe. Pembe zake zimepinda kwa mbele. Nyati hula nyasi. Wao pia huishi katika vikundi kutegemea jinsia. Nyati pia huitwa mbogo.Swara ni mnyama mdogo anayefanana na mbuzi.Swara anaweza kukimbia haraka. Yeye hula nyasi.Wanyama hawa wa porini hupatikana katika mbuga zetu kama vile Akagera,Nyungwe na Volcanoes. Wanyama hawa ni vivutio vikubwa vya watalii wanaotokandani na nje ya nchi yetu.Maswali
1. Andika orodha ya majina ya wanyama wa porini wanaokula:a) nyamab) nyasi2. Eleza tofauti zilizopo kati ya sokwe na nyani.3. Jaza kila pengo kwa jina sahihi la mnyama wa porini.a) Mwenye tamaa kama______________.b) _________ ana mkonga na pembe mbili.c) _______ haoni kundule.d) Ndovu pia huitwa_____________.e) Nimemwona mnyama mwenye milia myeusi na myeupe mwilini.Nimemwona__________.4. Tunga sentensi sahihi ukitumia majina haya ya wanyama wa porini.a) pundamilia b) simba c) tumbirid) swara e) nyati f ) ndovu5. Taja majina ya wanyama hawa:6. Jiunge na mwanafunzi mwenzako. Fanyeni utafiti kuhusu majina na sifaza wanyama wa porini wanaopatikana ndani na nje ya Rwanda na ambaohawajatajwa katika ufahamu.ii) Umuhimu wa wanyama wa porini nchini Rwanda
Kufikia sasa, umesoma mengi kuhusu wanyama wa porini. Wanyama hao wanaumuhimu mbalimbali.Tazama mchoro huu na usome kifungu chini yake.
KANYANA: Karibuni katika mbuga yetu ya Volcanoes.UWASEna HIRWA: Asante.KANYANA: Hapa, mtaona wanyama wengi wa porini.UWASE: Wanyama hao wana umuhimu gani?NGABO: Wanyama hao wana umuhimu mkubwa sana kwa nchi hii yetu yaRwanda. Wanyama hao kama vile masokwe ni vitega uchumi. Kilamwaka, watalii kutoka nchi za mbali huja hapa kwetu kuwaonawanyama. Wajapo hivyo, huja na pesa za kigeni ambazo huinua sanauchumi wetu.KANYANA: Nyinyi pia ni watalii wetu hapa. Pesa mnazolipa mkiingia hujengauchumi wetu. Pesa hizo pia hutumiwa kutulipia mshahara. Mimi nawenzangu tumeajiriwa kwa sababu ya wanyama wa porini.HIRWA: Je, nchi yetu hunufaika na pesa za kiingilio peke yake?NGABO: Hapana. Wageni wanapokuja, wanaleta manufaa mengi zaidi. Waohulipia huduma mbalimbali. Kwanza kuna malazi yao. Sisihuwakaribisha katika hoteli kubwa kubwa na nzuri nzuri. Hotelihizo zimepanuka na kuwaajiri watu wengi kwa sababu ya wagenihao wanaokuja kuangalia wanyama wa porini. Wageni hao piahulipia usafiri wao uwe ni wa ndege au gari. Usafiri huo huwapelekahuko wanakopenda kwenda kuwaona wanyama.KANYANA: Mbali na hayo, zipo bidhaa nyingi sana za hapa ambazo watalii haohununua kuwa ni ushahidi kwao kwamba kweli walikuwa hapa. Kwanjia hiyo pia nchi hufaidika kiuchumi.UWASE: Mbali na faida hizo za kifedha, zipo faida gani tena za wanyama hawa?NGABO: Wanyama hawa hukuza elimu yetu. Wanafunzi, na hata watu wazimahuzuru mbuga zetu za wanyama ili kuwaona na kujifunza mengikuwahusu.KANYANA: Isitoshe, wanyama wa porini ni hazina kwa vizazi vyetu vya baadaye.Sisi sote tumewaona wanyama hawa. Vivyo hivyo, litakuwa jambozuri sana ikiwa wanetu, wajukuu, watukuu, vilembwe na hatavilembwekeza wetu kuwaona wanyama wa porini pia. Hii ndiyosababu ya serikali yetu kuwatunza na kuwalinda wanyama wa porini.UWASEna HIRWA: Asanteni kwa maelezo yenu.Maswali
1. Taja faida za wanyama wa porini.2. Taja njia mbili ambazo serikali hutumia kuhifadhia wanyama wa porini.Kazi ya kikundi
Jiunge na wanafunzi wenzako. Jadilianeni kuhusu umuhimu wa wanyama wa porini nchini Rwanda.D . Matini ya Kiswahili kuhusu kilimo na ufugaji pamoja na vipengele vya kisarufi
Nomino
Je, unakumbuka maana na aina za nomino ulizosoma katika kidato cha kwanza?Zitaje.Nomino ni neno linalotaja mtu, kitu, hali au jambo. Zipo aina mbalimbali za nomino.Zifuatazo ni baadhi ya nomino hizo.a) Nomino za pekee
Nomino za pekee hutaja vitu au watu wenye sifa za kipekee. Zinapoandikwa katikasentensi, lazima zianze kwa herufi kubwa hata zikiwa katikati au mwishoni mwasentensi. Kumbuka hapa ya kuwa majina haya hayachukui hali ya wingi.Mifano ya nomino za pekee katika sentensi.
i) Rwanda ni nchi yenye wanyama wengi wa porini.ii) Mukangango ananyoa sufu ya kondoo.iii) Mwenyezi Mungu atujalie mvua nyingi ili tulime.iv) Kigali ni jiji linalopendeza.Zoezi
a) Andika sentensi sahihi ukitumia nomino hizi za pekee:i) Munyana ii) Kamana iii) Molaiv) Mei v) Mto Kivu vi) Msitu wa Nyungweb) Tambua makosa katika sentensi hizi na uyarekebishe.i) Mimi na kayitesi tunapenda somo la kilimo.ii) Nitavuna mihogo yangu mwezi wa februari.iii) Ng’ombe anaitwaje kwa kinyarwanda?b) Nomino za kawaidaNomino za kawaida hutaja vitu vya kawaida vinavyoweza kuchukua umoja nawingi kama jina lolote lile. Nomino hizo zinapoandikwa, huchukua herufi ndogoisipokuwa pale zinapojitokeza mwanzoni mwa sentensi.Mifano ya nomino za kawaida:i) Nomino za viumbe wenye uhai:ii) Nomino zinazomtambulisha mtu na kazi yake:iii) Nomino za vitu vya kawaidaKumbuka hapa kuwa nomino hizi za mahali huundwa kwa kuongeza ‘ni’ mwishonimwa nomino husika.Mifano ya matumizi ya nomino za kawaida katika sentensi.i) Mavuno ya mwaka huu ni mazuri.ii) Niletee jembe hilo.iii) Sufu za kondoo hutumiwa kutengenezea sweta.iv) Mkulima hodari hupata mazao mengi.v) Ndovu ni mnyama mkubwa wa porini.Zoezi
Tunga sentensi kumi sahihi ukitumia nomino za kawaida.c) Nomino za jamiiNomino za jamii pia huitwa nomino za makundi. Hizi ni nomino ambazo hutajajumla ya vitu vingi au vitu katika makundi.Mifano ya nomino za jamii:
Mifano katika sentensi
i) Makole ya ndizi yamevunwa.ii) Matuta yamepigwa shambani.iii) Matita ya kuni yatatumika kuchomea nyama.iv) Mitumba ya aina hii haifai wakulima.v) Bunge letu limetenga pesa nyingi kwa wizara ya kilimo.vi) Baraza la wafuga farasi limevunjwa.vii) Hili ni robota la pamba.Zoezi
Fanya utafiti kupata nomino kumi zaidi za jamii. Tunga sentensi ukitumia kilanomino hizo katika umoja na wingi.d) Nomino za dhahaniaKatika kikundi hiki hupatikana nomino ambazo ni za kufikirika tu na walahaziwezi kuguswa. Chukua nomino kama urafiki. Urafiki ni neno la kufikirika aukudhaniwa tu na wala haliwezi kuonekana wala kushikika. Nomino hizi haziwezipia kuhesabika.Mifano katika sentensi
i) Upanzi hufanywa mvua inapoanza kunyesha.ii) Kilimo kinasaidia kumaliza umaskini nchini Rwanda.iii) Ushirikiano wao katika kupalilia unawafaidi.iv) Fikira za wafugaji hao ni za hekima.v) Tutafanya uvunaji mwezi ujao.Zoezi
Tunga sentensi zozote kumi kuhusu kilimo na ufugaji ukitumia nomino za jamii.e) Nomino za wingiHizi nazo ni nomino za vitu ambavyo daima hupatikana kwa wingi pekee au umojapekee. Vitu vinavyotajwa na nomino hizi haviwezi kugawika.Mifano ya nomino za wingi:
maziwa, sukari, chumvi, uji, chai, manukato, mvua na kadhalika.Mifano katika sentensi:
i) Sukari ni zao la miwa.ii) Maua yale hutumiwa kutengenezea manukato.iii) Chai hii ni tamu.iv) Maji yanyunyiziwayo hapa ni ya mto huo.Zoezi
Soma kifungu kilichopo hapa chini. Tambua na uanishe nomino mbalimbali kifunguni.
Hapa nchini Rwanda, Mwenyezi Mungu ametujalia mazingira mazuri yenyekufanikisha ufugaji. Ufugaji ni kazi ya kutunza wanyama, ndege na hata wadudu.Mfugaji anaweza kufuga wanyama ama wadudu. Ikiwa ni wanyama, anawezakutunza ng’ombe, mbuzi, kondoo, farasi, nguruwe, na kadhalika. Ikiwa nia yake nikufuga ndege, anaweza kuwatunza kuku, bata na kadhalika. Hata hivyo, akichaguawadudu huweza kuwafuga nyuki.Ufugaji una kazi nyingi sana. Kwa mfano, mfugaji wa ng’ombe anapotaka matokeoya kuridhisha, itambidi atumie njia za kisasa katika ufugaji wake. Kwanza kabisa, nilazima awatafute ng’ombe bora wa maziwa. Ng’ombe hawa huleta mapato ya juu.Mbali na hayo ni sharti ahakikishe kwamba wanyama wake wana lishe ya kutoshahasa kwa ng’ombe wanaokaa ndani kwa ndani. Ng’ombe hawa, hasa ng’ombe jike,wa kukaa ndani kwa ndani hulishiwa zizini na kulala humo humo zizini. Hata hivyo,ni lazima zizi hilo liwe safi na ng’ombe huyo alale pahali safi. Kukosa kufanya hivyoni kukaribisha magonjwa ya namna kwa namna.Iwapo mfugaji atawalisha wanyama wake vizuri, atafaidika pakubwa. Atawezakupata maziwa ya kutosha. Atauza maziwa hayo na kujinunulia bidhaa nyinginezokama vile chumvi, sukari, chane za ndizi na kadhalika. Umaskini pia utaisha.Vivumishi
Je, unakumbuka vivumishi mbalimbali mlivyosoma katika kidato cha kwanza?Kwa kawaida, kivumishi ni neno linaloongezea nomino maana. Zipo aina mbalimbali zavivumishi. Baadhi ya vivumishi hivyo ni:a) Vivumishi vya sifa
Haya ni maneno yatajayo tabia au sifa za kitu, mtu ama jambo.Zipo aina mbili za vivumishi vya sifa: vivumishi vya sifa vinavyochukua viambishi navivumishi vya sifa visivyochukua viambishi.Mifano ya vivumishi vya sifa vinavyochukua viambishi:
-aminifu -zuri-pana -kubwa-pya -dogo-bovu -fupiKumbuka kuwa kiambishi au viambishi vinavyochukuliwa na vivumishi hivi hutegemea ngeli.Mifano katika sentensi:
ii) Vivumishi vya sifa visivyochukua viambishi
Hivi ni vivumishi ambavyo havibadiliki katika umoja na wingi au kutoka ngeli mojahadi nyingine; hubakia jinsi vilivyo.Mifano: bora, safi, hodari, bandia, haba, duni, laini na kadhalika.Mfano katika sentensi.
Zoezi
a) Tunga sentensi sahihi kuhusu kilimo na ufugaji katika umoja na wingi ukitumia vivumishi hivi vya sifa.i) -baya ii) -fupi iii) -dogoiv) -ingi v) -chacheb) Tunga sentensi sahihi ukitumia vivumishi hivi katika umoja na wingi.i) bora ii) dhalimu iii) duniiv) tele v) lainic) Andika sentensi hizi katika umoja au wingi.i) Nipe ndizi chache.ii) Mhindi mrefu unafaa.iii) Farasi wakubwa watatubeba.iv) Zizi safi halileti magonjwa.v) Upanzi bora ni huu.vi) Mkulima nadhifu anapita.d) Tunga sentensi zozote kumi kuhusu wanyama wa porini na kilimo zenyevivumishi vya sifa katika umoja na wingi.b) Vivumishi vya pekee
Vivumishi vya pekee hutoa habari kuhusu nomino au kiwakilishi chake kwa njia yakipekee. Vivumishi vya peke ni sita katika Kiswahili kama ifuatavyo:i) -enye
Huonyesha hali ya ‘kuwa na’ au ‘kumiliki’. Ni sharti kivumishi hiki kifuatwe na nomino wala si kitenzi.ii) -enyewe
a) Hutumika mwanzoni mwa sentensi kuonyesha jambo au kitu kinachotarajiwa.b) Hutumika mwishoni mwa sentensi kuonyesha kuwa jambo limetokea bilakusababishwa na yeyote au chochote.iii) -ote
Huleta maana mbili:a) Kuonyesha kila sehemu ya kitu hasa katika umoja.b) Kuonyesha kila kitu; bila kubakisha lolote hasa katika wingi.Zoezi
Eleza maana ya sentensi ikiwa ni ‘kila sehemu’ au ‘kila kitu’.i) Zizi lote limefagiliwa.ii) Mazao yote yamevunwa.iii) Paka amekunywa maziwa yote.iv) Ndizi yote imeiva.v) Simba wote wamepita.iv) -o-ote
Huonyesha mojawapo ya vitu au baadhi ya vitu bila kubagua.Zoezi
Tumia ‘-ote’ au ‘-o-ote’ pamoja na viambishi sahihi vya ngeli kujazia pengo katika sentensi zifuatazo.1. Nitatumia jembe _____ nitakalopewa.2. Miharagwe _________ imemea.3. Kuku ______ wamepewa chakula.4. Sitachukua nanasi ____________.5. Fyeka nyasi____________.v) -ingine
Kivumishi hiki cha pekee huweza kuwa na maana tatu:a) Kuonyesha kitu tofauti na kile kilichotajwa au kilichopo.b) Kuonyesha kitu zaidi/nyongezac) Kuonyesha ‘baadhi ya’vi) -ingineo
Kivumishi hiki hutumika kuleta maana mbili:a) 'zaidi ya'b) Kuonyesha hitimisho ya orodha ambayo haikukamilika.Zoezi
a) Tumia ‘-ingine’ au ‘-ingineo’ pamoja na viambishi sahihi vya ngeli kujazia mapengo.i. Amevuna mananasi ____________.ii. Sitaki panga hili, nipe panga _____________.iii. Mama amepanda mbegu za maharagwe, mtama, mahindi na _____________.iv. Usiwakame ng’ombe __________. Maziwa haya yametosha.v. Mpe migomba hiyo na ______________.b) Tunga sentensi tano sahihi kuhusu kilimo na ufugaji katika umoja na wingiukitumia nomino zozote na kivumishi cha ‘-ingine’.c) Tunga sentensi tano sahihi kuhusu wanyama wa porini na mifugo katikaumoja na wingi ukitumia nomino zozote na kivumishi cha ‘-ingineo’.c) Vivumishi vionyeshi
Vivumishi vionyeshi au viashiria ni maneno ya kuonyesha alipo mtu au kitu, yaaniujirani. Kuonyesha huko kunaweza kuwa kwa ujirani wa karibu – hapa, ujirani wambali kidogo – hapo, na ujirani wa mbali – pale.Mifano ya vivumishi hivi ni hii ifuatayo:
Mfano katika sentensi:
i) Kijijini humu mna mfugaji hodari.ii) Hizi juhudi zenu za kulima zitamaliza umaskini.iii) Ng’ombe wale wanakunywa maji.iv) Fyekeo hilo halikati majani.v) Shambani pale pamepaliliwa.i) Vivumishi vionyeshi radidi
Vivumishi hivi hutokana na kurudia vivumishi vionyeshi. Huleta maana ya kutilia mkazo.ii) Vivumishi vionyeshi visisitizi
Hutumiwa kusisitiza jambo.Zoezi
a) Jaza kila pengo kwa vivumishi sahihi vilivyowekwa katika mabano.i. Mazao __________ yatajaza guni. (vionyeshi visisitizi vya karibu)ii. Mkulima _________ analima. (vionyeshi vya mbali)iii. Twiga __________ ni wengi. (vionyeshi viradidi vya mbali kidogo)iv. Nyama __________ ni tamu. (vionyeshi vya karibu)v. Wafugaji _________ wana bidii. (vionyeshi vya mbali kidogo)b) Tunga sentensi tano tano kuhusu kilimo na ufugaji katika umoja na wingiukitumia vivumishi vionyeshi, vivumishi vionyeshi rejeshi na vivumishivionyeshi visisitizi.d) Vivumishi vya idadi
Vivumishi vya idadi ni maneno yanayoonyesha idadi ya watu ama vitu.Vipo vivumishi vya idadi kamili, vivumishi vya idadi ya jumla na vivumishivya idadi ya matokeo.i) Vivumishi vya idadi kamili
Pia huitwa vivumishi vya idadi halisi au bainifu. Huonyesha hesabu halisi ya nominohusika.Baadhi ya vivumishi hivi huchukua viambishi vya ngeli kutegemea nominoinayohesabiwa.Mfano: -moja, -wili, -tatu, -nne, -tano na -nane.Baadhi ya vivumishi vya idadi kamili havichukui viambishi vyovyote vya ngeli.Yaani hutumika jinsi vilivyo bila kubadilika.Mfano: sita, saba, tisa na kumi, makumi, mia na kadhalikaii) Vivumishi vya idadi ya jumla/isiyo kamili
Huonyesha idadi ambayo ujumla wake haujulikani. Baadhi ya vivumishi hivihuchukua viambishi vya ngeli ya nomino.Mfano: -chache na –ingiMfano katika sentensi:
1. Kuku hawa wametaga mayai machache.2. Mwaka huu tumepanda mbegu nyingi.3. Wakulima wengi wamevuna.4. Wao huuza maziwa mengi sana.Baadhi ya vivumishi vya idadi ya jumla havichukui viambishi vya ngeli.Yaani hubakia vivyo hivyo.Mfano: kadhaa, tele, kiasi, kidogo na haba.iii) Vivumishi vya idadi ya matokeo
Pia huitwa vivumishi vya nafasi katika orodha. Vivumishi hivi huonyesha nafasi yanomino katika orodha.Zoezi
a) Jaza kila pengo kwa kivumishi sahihi katika mabano.i. Sungura ________ wanakimbia. (chache)ii. Masokwe __________ wanacheza. (sita)iii. Mkulima __________ atapewa mbolea. (moja)iv. Amenunua maembe_________. (ingi)v. Tumelima mashamba___________. (nane)b) Tunga sentensi kumi sahihi kuhusu kilimo na ufugaji ukitumia vivumishi vyaidadi jumla na isiyo jumla.e) Vivumishi viulizi
Hili ni kundi la vivumishi ambalo lina maneno yatumiwayo kuulizia maswali.Baadhi ya mifano ya vivumishi viulizi ni:i) Kiulizi -pi?
ii) Kiulizi -ngapi?
iii) Kiulizi gani?
Kiulizi hiki hakichukui kiambishi chochote cha ngeli.Tanbihi
Kivumishi kiulizi kinastahili kuandamana na nomino au kiwakilishi cha nomino.Viulizi ambavyo havitumiwi pamoja na nomino au viwakilishi vya nomino haviwezikuitwa vivumishi bali ni viulizi.Mfano: lini, nani, nini, vipi. Hivi si vivumishi viulizi kwa sababu havitumiwi pamojana nomino au kiwakilishi cha nomino.Zoezi
a) Tumia kiulizi ‘-pi’ kwa usahihi kujazia kila pengo.i. Mashirika _________ yanasaidia wakulima?ii. Mkahawa __________ unakatwa?iii. Dawa _________ zinanyunyiziwa mimea?iv. Niwaite wafugaji ________?v. Kufyeka _______ kunafaa?b) Tumia kivumishi kiulizi ‘-ngapi’ kwa usahihi kujazia kila pengo.i. Tukupe magunia __________?ii. Pembe _________ zimekatwa?iii. Mbwa _________ wamechanjwa?iv. Mipera ___________ inapandwa?v. Vibuyu _________ vina maziwa?f) Vivumishi vimilikishi
Maneno katika kundi hili la vivumishi hujibu swali mtu, kitu au jambo ni la nani aulina nini? Vivumishi hivi huwa sita pekee katika Kiswahili.-angu -etu-ako -enu-ake -aoKutokana na haya, unapata maneno kama vile:wangu wetuchako chenukwake kwaoUnaweza kutunga sentensi hizi ukitumia vivumishi vimilikishi:1. Jibini hii ni yangu.2. Mawele yako yameliwa na fukusi.3. Mbatata zenu zinauzwa Zambia.4. Njugu za kwao ni tamu mno.5. Huwezi kusema kuwa huu ni mchicha wako!Zoezi
Jaza kila pengo kwa kivumishi kiwakilishi sahihi.1. Nyinyi mna mihogo. Mihogo ni ___________.2. Sisi tuna maembe. Maembe ni _____________.3. Wao wana sufu. Sufu ni _____________.4. Mimi nina sukari. Sukari ni ____________.5. Yeye ana kole la ndizi. Kole ni __________.6. Wewe una muhogo. Muhogo ni _____________.Kazi ya wanafunzi wawili wawili
Jiunge na mwanafunzi mwenzako. Someni kifungu kifuatacho huku mkitambua jinsivivumishi vilivyotumiwa.Mimi ni mwanafunzi mwenye bidii. Nia yangu kuu maishani mwangu ni kuridhikana shughuli za kilimo cha kisasa kama mojawapo ya njia nzuri za kupigana dhidiya umaskini. Lengo langu kuu la kwenda shuleni hasa ni kupata maarifa mema yakuniwezesha kuishi maisha ya kitajiri. Maarifa hayo yataniwezesha kuwa mkulimabora.Nitaendelea na masomo hadi chuo kikuu. Nitafanya somo la Kilimo katika chuokikuu. Hata hivyo, hilo pekee halitatosha. Nitafanya kazi ndogo ndogo kwa mudaili kutafuta pesa za kuanzisha kilimo. Kufikia hapo, nitakuwa nimepiga hatua lakinibado sitakuwa nimefikia lengo langu.Kuanzisha kilimo cha kisasa kutakuwa ni hatua kubwa lakini bado kutakuwana kazi kubwa ya kufanywa. Ni sharti niupige vita vikali umaskini kupitia kilimohicho. Umaskini ni adui mbaya ambaye lazima niangamize. Njia moja ya kumalizaumaskini ni kuweka uvivu kando.Mbali na kulima, nitafuga mifugo wengi. Nitahakikisha ya kuwa nina vifaa vyotevinavyohitajika kwa kufanyia kazi hizo mbili. Kutakuwa na trekta kubwa kubwana mashine za kukamua. Nitanunua magari mazuri ya kusafirisha mazao menginitakayovuna. Nitawapa vijana wenzangu kazi ili nao wawe na kipato kizuri. Kwajumla, nitahakikisha kuwa vitu vyote anavyohitaji mkulima wa kisasa vipo.Mwisho, nitatafuta masoko mazuri na ya kuaminika. Nia yangu hapa ni kuuzabidhaa zangu katika masoko yaya haya ya hapa kwetu. Baadaye nitaziuza katikamasoko, nje ya nchi yetu. Hizi zote zitakuwa ni juhudi za kuendeleza vita vikali dhidiya umaskini au uchochole.Zoezi
1. Orodhesheni vivumishi vyote vilivyomo kifunguni humu kwa kuzingatia ainaya kila kivumishi husika.2. Tunga sentensi fupi fupi na sahihi ukitumia vivumishi mlivyoorodhesha hapo juu.Viwakilishi
Viwakilishi ama vibadala ni maneno ama viambata (sehemu za maneno)vinavyosimama badala ya majina. Kundi hili la maneno huweza kugawika katikasehemu mbalimbali ifuatavyo.a) Viwakilishi nafsi
Husimamia nafsi za nomino inayozungumziwa katika umoja au wingi. Kuna ainambili kuu za viwakilishi vya nafsi:i) Viwakilishi nafsi huru
Huwakilisha nafsi iliyo huru, yaani isiyounganishwa na kitenzi katika umoja nawingi kwenye sentensi.Mfano: nafsi ya kwanza (mimi, sisi), nafsi ya pili (wewe, nyinyi), nafsi ya tatu (yeye, wao).Zoezi
Umoja Wingi1. Mimi ninalima. Sisi tunalima.2. Wewe unavuna. Nyinyi mnavuna.3. Yeye anafyeka. Wao wanafyeka.ii) Viwakilishi nafsi viambata
Viwakilishi hivi huambatanishwa na vitenzi.Mfano: nafsi ya kwanza (ni-, tu-), nafsi ya pili (u-, m-) nafsi ya tatu (a-, wa-)ii) Pia, vipo viwakilishi ambata vya ngeli. Navyo ni:
b) Viwakilishi vitokanavyo na vivumishi
Je, unakumbuka vivumishi ulivyosoma hapo juu? Endapo kivumishi husikakimetumika badala ya nomino, kivumishi hicho kinakuwa kiwakilishi. Nachokiwakilishi hicho huchukua jina la kivumishi hicho. Mfano:i) Viwakilishi vionyeshi
Hutokana na vivumishi vionyeshi. Tazama vivumishi vionyeshi. Unapoondoanomino katika vivumishi hivyo, unapata viwakilisihi vionyeshi.Kumbuka kwamba hufai kutumia nomino na kiwakilishi katika sentensi moja.ii) Viwakilishi viulizi
Viwakilishi hivi vinatokana na vivumishi viulizi.iii) Viwakilishi vimilikishi
Viwakilishi hivi hutokana na vivumishi vimilikishi. Tazama mifano hapa chini.Zoezi A
Tunga sentensi ukitumia viwakilishi mbalimbali.Zoezi A
Soma kifungu kifungu kifuatacho huku ukitambua jinsi viwakilishi vilivyotumiwa.Zama hizo, fisi alikuwa jirani ya binadamu aliyependa kulima. Binadamu alimilikishamba kubwa la mihogo. Naye Fisi alikuwa mvivu aliyependa kumtembeleabinadamu kwake. Alidhani kuwa huyo binadamu naye alimpendana sana. Hatahivyo, binadamu hakumpenda sana fisi. Fisi hakupenda kulima bali alipenda sanakula.Siku moja jioni, fisi alimuaga binadamu na kusema, “Kesho nitaamkia huku kwako ili uniandalie kiamshakinywa! ”Kwa roho ya ndani, mwanadamu alijisemea, ‘Huyu hapendi kufanya kazi, anapenda tu kula. Kwa nini haoni kuwa simpendi?’Akamwambia fisi, “Labda utanipata, labda utanikosa.”Fisi kuona kuwa anaweza kukosa mlo alisema, “Basi nitajaribu nije hata mapema zaidi. Kwa namna hiyo tunaweza kula halafu wewe uende shambani. Napenda sana namna unavyopika nyama.” Bila kungoja jawabu, alitoka na kujiendea zake.Keshoye, mwendo wa saa kumi na moja asubuhi, fisi alibisha hodi kwa mwanadamu. Naye mwanadamu hakusita kumfungulia mlango. Mwanadamu aliazimia kumfunza fisi adabu.“Karibu, karibu kwangu rafiki yangu,” mwanadamu alijibu.Naye fisi kwa kusukumwa na njaa yake ya asubuhi pamoja na ulafi wake, alimpitatu na kuingia ndani. Harufu ya nyama mle ndani ilimfanya fisi ameze mafunda ya mate.“Karibu, karibu kaa,” mwanadamu alimlaki fisi. “Nipe dakika chache tu na chakulakitamu na kingi kitakuwa mezani hapa.”“Basi fanya haraka. Ninakufa kwa njaa,” fisi alisema.Baada ya muda usiokuwa mrefu vile, mwanadamu alikuwa ameandika mezakwa kila namna ya nyama ya mifupa. Ohoo! Fisi kuona hivyo, nusura kuirukialakini mwanadamu akamzuia kwa kusema, “Bwana fisi, ili leo ushibe vya kutosha,tumbukiza kila sahani mdomoni mwako na umeze tu bila kutafuna.”Hata kabla ya mwanadamu kumaliza usemi wake, fisi alikuwa ametumbukizasahani mbili kinywani mwake!“Mbona hiki cha leo ni kikali jinsi hii? Lo! Kinawasha sana! Loooooooooo!”Fisi alilalamika.Kumbe mwanadamu alijaza pilipili kwenye nyama. Tangu siku hiyo, fisi hakuruditena kwa mwanadamu.Maswali
1. Je, fisi alikuwa mnyama wa aina gani?2. Ni kwa nini mwanadamu hakumpenda fisi?3. Mwanadamu aliikomeshaje tabia mbaya ya fisi?4. Unadhani ni yapi yaliyompata fisi?5. Jiunge na mwanafunzi mwenzako. Bainisheni viwakilishi vyote vilivyomokatika kifungu mlichosoma hapo juu. Tungeni sentensi sahihi mkitumiavivumishi hivyo.Vielezi
Vielezi pia huitwa viarifa. Ni maneno yafafanuayo vitenzi, vivumishi au vielezivingine. Mathalan, ukisema Anatembea haraka, neno 'haraka' linaeleza jinsianavyotembea mhusika. Kwa hivyo, neno hilo linalokuarifu mengi kuhusukutembea ni kielezi.Maneno haya hujigawa katika vikundi mbalimbali kama ifuatavyo:a) Vielezi vya namna au jinsi
Haya ni maneno ambayo huarifu jinsi ya kutendeka mambo.Mfano: sana, bure, kitoto, vizuri, upesi, kwa miguu, kwa bidii, bwe!b) Vielezi vya wakati
Nayo haya ni maneno yanayofafanua ama kueleza wakati wa kutokea tendo.Mathalan, ukisema Mgeni alifika jioni neno jioni ni kielezi cha wakati.Vipo vielezi vya wakati vya aina mbili:i) Vielezi vya wakati maalumu.
Mfano: Januari, Disemba, Jumamosi, saa tatu, kesho, leo, mtondo na kadhalika.ii) Vielezi vinavyotaja wakati kwa jumla
Mfano: baadaye, zamani, daima, milele, awali, punde, karibuni, zama hizo.c) Vielezi vya kiasi/idadi
Vielezi vya kiasi ni namna ya maneno ambayo hufafanua vitenzi kwa kujulishalimetokea mara ngapi tendo linalotajwa.d) Vielezi vya mahali
Haya nayo ni maneno ama mafungu ya maneno yanayofafanua panapotokea kitendo.Mara nyingi, maneno haya huwa ni majina ya mahali.Zoezi
Jiunge na wenzako watatu na mworodheshe vielezi vyote vilivyomo kifunguni humuhuku mkivitungia sentensi fupi na sahihi.Gakwerere alikuwa mfugaji mwenye bidii nyingi sana tangu zamani. Mwanzoni,Gakwerere alikuwa akifuga ng’ombe wa kienyeji. Aliwalisha ng’ombe hao uwanjanina pembeni mwa mashamba. Hata hivyo, ng’ombe hao hawakuwa wakimpa kiasicha maziwa alichotarajia. Angewakamua mara moja tu kwa siku. Alikata shaurikuanzisha ufugaji wa ng’ombe bora wa maziwa.Mfugaji huyu aliwapeleka ng’ombe wake wa kienyeji sokoni na kuwauza mnamoNovemba. Baada ya kuwauza, aliamka alfajiri na kufunga safari ya kuzuru shambala kisasa la Nyinawumuntu. Bi. Nyinawumuntu alikuwa mfugaji na mkulimamashuhuri sana katika eneo hilo alilokaa Gakwerere. Alipofika huko, alimpatabibiye yupo na wakaanza kupiga bei. Baada ya kukubaliana bei, alinunua mitambawawili kwa bei nafuu. Alilipa papo hapo kwa sababu hakutaka kuwa na deni.Kumaliza hivi tu, yule bibi alimpa Gakwerere gari lake ili alitumie kuwasafirishang’ombe wake. Gakwere alimshukuru kwa wema wake na akawasafirisha haomitamba wake hadi kwake.Alipofika nyumbani kwake, mfugaji huyo alianza kuwalisha ng’ombe wake kwa njiaza kisasa. Kwa kuwa walikuwa wakilishwa kwa lishe bora ya ng’ombe, haukuchukuamuda mrefu kuwapandisha. Muda ulipowadia, walizaa ndama wawili wenye afyanzuri.Baada ya muda usio mrefu, Gakwerere alianza kuvuna matokeo ya jasho lake la kilasiku. Hakuamini kiasi cha maziwa alichokuwa akikama kila asubuhi na jioni.Aliweka akiba kwa muda. Hatimaye, mfugaji huyu alinunua gari. Alitumia gari hilokuwatafutia na kuwabebea chakula ng’ombe hao wake wa gredi.E . Matumizi ya wakati uliopo na uliopita na vitenzi vya silabi moja
i) Matumizi ya wakati uliopo (-na-) na vitenzi vya silabi moja
Wakati uliopo -na-unaweza kuwa katika hali mbili: Hali hizo ni hali yakinishi na halikanushi. Hali yakinishi ni ya ukubali na hali kanushi ni ya ukatavu.Soma sentensi hizi.Hali yakinishi
Hali yakinishi ni hali ya kukubali. Tazama tena mifano iliyopo hapo juu. Vitenziunakufa, anakula, anakunywa, anakuja, anampa na inanyesha vimo katika haliyakinishi, yaani hali ya kukubali.Hali kanushi
Nayo hali kanushi ni hali ya kukataa. Itazame tena mifano hapo juu. Vitenzi haufi,hali, hanywi, haji, hampi na hainyeshi vipo katika hali kanushi, yaani hali ya kukataa.Unaweza kutunga sentensi zaidi za namna hii kama ifuatavyo:
Kazi ya wanafunzi wawili wawili
Jiunge na mwenzako. Tafuteni vitenzi zaidi vyenye silabi moja katika kamusi hukumkijadiliana mabadilko ambayo hutokea vitenzi hivyo vinapotumiwa katika halikanushi na yakinishi.ii) Matumizi ya wakati uliopita -li- na vitenzi vya silabi moja
Wakati uliopita huonyesha kuwa kitendo kilifanyika muda mrefu uliopita. Wakatihuu huwakilishwa na -li-. Vitendo husika vinaweza kuwa katika hali yakinishi aukanushi. Kama ujuavyo, hali yakinishi ni ya kukubali na hali kanushi ni kukataa.Tazama mifano ifuatayo:
Vitenzi hivyo vipo katika wakati uliopo. Tunaweza kuvigeuza viwe katika wakatiuliopita kwa kuweka ‘-li-‘ mahali pa ‘-na-‘. Tunapofanya hivyo, tunamaanisha kuwavitendo hivyo vilifanyika muda au wakati uliopita. Tazama jedwali hili.Tazama mifano ifuatayo:
Katika jedwali lililopo hapo juu, vitenzi ulikufa, alikula, alikunywa, alikuja, alimpa,na ilimnyeshea vimo katika hali yakinishi au kukubali kwa wakati uliopita. Navyovitenzi haukufa, hakula, hakunywa, hakumpa, haikumnyeshea vimo katika hali yakukataa yaani hali kanushi.Mazoezi ya ziada
Zoezi A
Jiunge na mwanafunzi mwenzako na mworodheshe vitenzi vinane vya silabi mojahuku mkivitungia sentensi sahihi katika wakati uliopita. Sentensi zenu zihusiane nakilimo na ufugaji. Someaneni vitenzi na sentensi huku mkisahihishiana.Zoezi B
Jiunge na wanafunzi wenzako katika kikundi. Msomeane tungo au hadithimbalimbali zilizopo katika kitabu hiki na vitabu vingine. Mbainishe na kuainisha ainaza maneno katika tungo hizo (vivumishi, viwakilishi na vielezi) kama vinavyotokeakatika umoja na wingi pamoja na matumizi ya wakati uliopo na wakati uliopita.Maswali ya marudio
li kujikumbusha mengi ya yale uliyojifunza katika sehemu hii, yajibu vilivyo maswalihaya yafuatayo yote.1. Bila ya kuangalia popote, taja maneno kumi yanayohusu mazao na kumiyanayohusu ufugaji huku ukiyaeleza.2. Ipo misimu mingapi hapa Rwanda? Ieleze huku ukirejelea upanzi na uvunajiwa mimea.3. Tazama picha zifuatazo. Eleza misimu kulingana na kila mchoro.4. Tunga sentensi sahihi ukitumia msamiati ufuatao:a) mahindib) ndizic) kahawad) viazi mviringoe) maharagwef ) njugu5. a) Jaza kila pengo kwa jina sahihi la kifaa cha kilimo.i) Ndoli anafyeka shamba kwa ______________.ii) Mkulima yule anatumia _________ la mkono kulimia shamba lake.iii) Shamba kubwa hulimwa kwa _______________.iv) __________ hutumiwa kukata matawi ya miti shambani.6. Tunga sentensi tano fupi ukitumia vifaa mbalimbali vya kilimo ambavyo vinatumiwa katika eneo utokako.7. Eleza jinsi unavyopanga kupiga vita uchochole kwa kilimo cha kisasa.8. Taja majina kumi ya mifugo nchini Rwanda na uyatungie sentensi sahihi.9. Taja chuo cha kilimo hapa nchini ambacho ungependa kukiingia baada yamasomo yako huku ukieleza ni kwa nini unakistahi chuo hicho.10. Eleza umuhimu wa ufugaji katika jamii unapotoka.11. Zipo tamaduni zozote za kikwenu zihusuzo kilimo na ufugaji? Zitajehuku ukieleza huo uhusiano.12. Taja wanyama kumi wa porini wanaopatikana nchini Rwanda.13. Andika majina na sifa za wanyama wafuatao wa porini:14. Eleza faida za wanyama wanaoishi porini.15. Pendekeza njia zinazoweza kutumiwa kuwavutia watalii wanaozuru mbugazetu za wanyama wa porini.16. Eleza maana ya:a) nominob) vivumishic) vielezid) viwakilishi17. Huku ukitoa mifano, eleza aina nne nne za:a) nominob) vivumishic) vielezi18. a) Je, vitenzi vya silabi moja ni maneno ya aina gani?b) Andika mifano minne ya maneno yenye silabi moja na uyatungie sentensi sahihi.19. a) Huku ukitoa mifano, eleza tofauti zilizopo kati ya:i) wakati uliopo na wakati uliopitaii) hali kanushi na yakinishib) Andika sentensi zifuatazo katika hali yakinishi au kanushi.i) Baba anakula mahindi.ii) Mahindi hayafi wakati wa kiangazi.iii) Ng’ombe hakunywa maji jana.iv) Mkulima alimpa ndizi nyingi.c) Andika sentensi zifuatazo katika wakati uliopo au uliopita.i) Ndoli anakula mihogo.ii) Mimi sinywi maziwa.iii) Mama alinipa jembe.iv) Kuku hao hawakufa.20. Kwa ufupi, elezea mambo muhimu uliyojifunza katika sura hii na useme jinsiyatakavyokufaidi na jamii.Files: 3Sura 2: Utungaji
Mada ndogo: Barua kuhusu matembezi, Barua za kirafiki,
Barua za mwaliko, Simu,Tangazo/Ilani.
A Barua
Barua ama waraka ni maandishi yaliyopangwa kwa utaratibu na mtiririko maalumukwa minajili ya kuwasilisha ujumbe fulani. Zipo aina mbili kuu za barua: Ipo baruaya kirafiki ambayo pia huitwa barua ya kindugu na ipo barua rasmi.a) Barua za kirafiki
Barua ya kirafiki ni barua ambayo huandikiwa mtu ama watu mbalimbali walio nauhusiano wa karibu na anayeandika; kama vile rafiki, mzazi, dada na kadhalika.Kazi ya wanafunzi wawili wawili
Jiunge na mwenzako na mjadili barua zenu mlizoandika. Je, waandikiwa walikuwakina nani? Ujumbe ulikuwa upi na ni lugha gani uliyotumia?Mifano ya barua za kirafiki
i) Barua ya mwana kwa mzazi
Ukimwandikia mama barua, barua hiyo ni ya kirafikiZoezi
Mwandikie ndugu yako barua ukimweleza maendeleo yako katika masomo.
ii) Barua ya mapenzi
Barua ya kindugu inaweza kuwa ya mapenzi pia.
Zoezi
Jifanye kuwa una zaidi ya miaka kumi na minane. Mwandikie mchumba wako baruaukimweleza sababu ya kumpenda na kutaka kumwoa.ii) Barua ya kutoa ushauri
Isitoshe, barua ya kirafiki inaweza kuwa ni ya mzazi anayetoa ushauri kwa mwanawe.Zoezi
Wewe ni mzazi ambaye mwanao amepotoka. Mwandikie barua yakumwelekeza kuepukana na upotovu huo na arudie wema wake wa awali.Someni barua zenu mbele ya darasa.Sehemu kuu za barua za kirafiki
Barua za kirafiki huwa na sehemu au muundo fulani maalumu.
Kazi ya kikundi
Jiunge na wanafunzi wenzako katika kikundi. Tazameni mifano ya barua za kirafiki iliyotolewa na mingineyo. Jadilianeni kuhusu sifa zinazofanana katika barua zote.
Tazama mfano wa muundo wa barua ya kirafiki. Kuna uhusiano gani kati ya yaliyomo na barua za kirafiki ulizosoma?
Anwani
Tarehe
Kutaja mwandikiwa
Utangulizi/salamu
Mwili wa barua
Hitimisho
Jina la mwandishi.
Barua ya kirafiki huwa na sehemu kuu zifuatazo:
i) Anwani moja ya mwandishi: Huandikwa juu, pembeni.ii) Tarehe: Huandikwa chini ya anwani kwa kuacha nafasi ya mstari mmoja.iii) Kutaja mwandikiwa: Huja chini ya tarehe kwa kuacha nafasi ya mstari mmoja.iv) Utangulizi: Hujitokeza katika aya ya kwanza. Mwandishi humjulia hali mtuanayeandikiwa na wenzake. Pia, husema hali yake.v) Mwili wa barua: Mwandishi hupitisha ujumbe wa barua/kuelezea kiini chakuandikwa kwa barua husika.vi) Hitimisho/Kufunga barua: Mwandishi huhitimisha barua yake kwa kumtakiaheri aliyeandikiwa. Jina la mwandishi wa barua huja chini ya hitimisho.Zoezi
Tazama barua iliyopo hapa chini. Je, barua hii ina makosa gani? Andika upya baruahii kwa kusahihisha makosa yaliyopo na kuongezea sehemu zinazokosekana.Kwa Shangazi Mpendwa,S.L.P, 45KigaliRwandaWako Mpendwa,Ninajua wewe unapenda sana kilimo cha ndizi. Juzi tulisoma kuhusu kilimo boracha ndizi. Mwalimu wetu alitufunza mbinu mpya za kupanda ndizi. Tukifunga,nitakutembelea ili nikufunze mbinu hii mpya itakayokupa mavuno mengi zaidi.Unisalimie wote waliopo nyumbani. Waambie nitawatembelea wakati wa likizo.Kwanza, ningependa kukueleza kuwa ninazidi kutia bidii katika masomo. Juzitulifanya majaribio na niliibuka nafasi ya tatu katika darasa letu. Ninatia bidii zaidi.U hali gani? Mimi nipo salama. Nia yangu kuu ya kukuandikia barua hii ni kukujulishakuhusu mambo mawili makuu.Kanuni za kuzingatiwa katika uandishi wa barua za kirafiki
Zipo kanuni mbalimbali za kuzingatiwa wakati wa kuandika barua ya kirafiki.Soma kifungu kifuatacho ili kubainisha baadhi ya kanuni hizo.
USANASE: Hujambo, Gabiro?GABIRO: Sijambo Usanase.USANASE: Unaonekana mwingi wa huzuni. Pana jambo linalokutatiza?GABIRO: Ni kweli. Ninataka kuandika barua kwa mjomba. Sijui endapo panakanuni zozote ninazofaa kuzingatia.USANASE: Ahaa! Zipo kanuni za kufuatwa wakati wa kuandika barua ya kirafiki.GABIRO: Kanuni hizo ni gani?USANASE: Kwanza, hufai kuandika kichwa.GABIRO: Niandike tu moja kwa moja?USANASE: Naam. Kabla ya kuandika kiini au mwili wa barua, hakikisha kuwaumeandika anwani yako kama mwandishi.GABIRO: Anwani moja inatosha?USANASE: Naam. Chini ya anwani, andika tarehe kisha umtambulishe unayemwandikia.GABIRO: Ninaweza kumtambulisha vipi?USANASE: Mtambulishe kwa kudhihirisha uhusiano uliopo baina yenu. Kwamfano, Kwa Mjomba Mpendwa.GABIRO: Ahaa! Ninakupata vizuri sana. Je, ninafaa kujikita katika ujumbemmoja mkuu?USANASE: Hapana. Una uhuru wa kuzungumzia maudhui mengi. Unawezakutaja mambo mengi yasiyohusiana. Mfano, unaweza kumwambiakuhusu hali ya anga na masomo shuleni. Baadaye, unawezakumwuliza kuhusu mazao yake yalivyo shambani na mambo mengi.Uhakikishe kuwa kila maudhui au ujumbe upo katika aya yake.GABIRO: Ninafaa nitumie kiwango gani cha lugha?USANASE: Hujafungwa katika kiwango fulani cha lugha. Lugha utakayotumiainategemea uhusiano uliopo kati yako na mjomba au yeyoteunayemwandikia.GABIRO: Kwa hivyo si lazima lugha yangu iwe rasmi?USANASE: Naam. Si lazima uzingatie kiwango cha juu cha adabu kama ilivyokatika barua rasmi. Hilo halimaanishi kuwa unaruhusiwa kutumia lugha chafu aulugha isiyokuwa na tasfida.GABIRO: Kwa hivyo ninaweza kutumia lugha yenye utani, vichekesho na yenyekuibua hisia ya huzuni, furaha au huruma.USANASE: Naam.GABIRO: Je, ninafaa kuzingatia urefu kiasi gani?USANASE: Kama nilivyosema hapo mbeleni, una uhuru wa kuzungumziamambo mengi utakavyo katika barua ya kirafiki. Urefu utategemeajumla ya mambo hayo. Una uhuru wa kuandika barua ndefu au fupiutakavyo. Hakuna urefu maalumu.GABIRO: Nikimaliza, ninafaa kutia sahihi?USANASE: La hasha! Barua ya kirafiki si lazima itiwe sahihi.GABIRO: Asante sana rafiki yangu kwa maelezo hayo. Sasa ninaweza kuandikabarua yangu.USANASE: Karibu. Ukiwa na swali lingine, utaniuliza.Zoezi
Jiunge na mwenzako na muigize mazungumzo yaliyopo hapo juu. Andikeni kanuni za kuzingatiwa katika uandishi wa barua za kirafiki zilizopo kwenye ufahamu.
Kazi ya kikundi
Jiunge na wanafunzi wenzako katika kikundi. Andikianeni barua za kirafiki kuhusu mada yoyote mpendayo. Someni barua zenu huku mkisahihishiana.
b) Barua rasmi
Tazama michoro hii. Je, mwalimu na wanafunzi hawa wanajadiliana kuhusu nini?Je, unajua jinsi ya kuandika barua rasmi?
Barua rasmi ni barua zinazoandikiwa mtu au watu wenye nyadhifa kwa lengomaalumu la kuwasilisha ujumbe rasmi.Mifano ya barua rasmi.i) Barua ya kuomba kazi
Hii ni aina ya barua ambayo mtu huandika wakati anapotaka kuajiriwa mahali. Kuna aina mbalimbali za barua za kuomba kazi.
Kazi ya wanafunzi wawili wawili
Jiunge na mwenzako. Jadilianeni kuhusu jinsi ya kuandika barua ya kuomba kazi. Andikeni barua hiyo kwa msingi wa majadiliano hayo.
Zoezi
Andika barua ya kuomba kazi yoyote upendayo. Angazia mambo yafuatayo katika barua yako:
i) jinsi ulivyopata kuwepo kwa nafasi ya kazi hiyo,ii) tajiriba yako, wasifu wako mfupi,iii) sababu ya kutaka kazi hiyo,iv) mambo mapya ambayo utafanya ukipewa nafasi hiyo na kadhalika.ii) Barua ya kuomba ruhusa
Hii ni aina ya barua ambayo mwandishi huomba kupewa fursa ya kutoshiriki katika shughuli fulani muhimu. Unaweza kusema kwa nini hutakuwepo au usiseme.
Zoezi
Mwandikie mwalimu wako barua ukiomba ruhusa yoyote. Mweleze sababu za kuomba ruhusa hiyo.
iii) Barua ya huduma
Barua ya huduma ni aina ya barua ambayo humhitaji mtu, kundi la watu, shirika lisilo la kiserikali au idara ya serikali au kampuni kutoa huduma fulani katika jamii. Wakati mwingine huandikwa kutoa maoni kuhusu hatua ambazo jamii ingependa kuchukuliwa, kwa mfano, idara ya polisi ama hospitali kuweka visanduku vya kupokea maoni kutoka kwa wananchi kuhusu namna wangependa kuhudumiwa kwa ubora zaidi.
Kazi ya kikundi
Jiunge na wanafunzi wenzako katika kikundi. Nyinyi ni vijana wanaojihusisha katikakufanya utafiti wa mbinu bora za kilimo katika wilaya yenu. Kipeni kikundi chenujina na mchague katibu mkuu. Andikeni barua kwa shirika lolote linalojihusishana kilimo katika eneo lenu. Elezeni shirika hilo kuhusu utafiti mliofanya wa kukuzakilimo katika wilaya yenu na msaada mnaohitaji kutoka kwao.Aina zaidi za barua rasmi
Mbali na mifano iliyotolewa, zipo aina zaidi ya barua rasmi. Barua hizo ni kama vile:i) Barua ya kuomba nafasi katika shule fulaniii) Barua ya kuomba msamahaiii) Barua ya shukraniiv) Barua ya malalamikov) Barua kwa mharirivi) Barua ya mapendekezovii) Barua ya uteuziviii)Barua ya kusimamishwa au kufutwa kazi.Kazi ya wanafunzi wawili wawili
Jiunge na mwanafunzi mwenzako. Fanyeni utafiti kuhusu jinsi barua zilizotajwahapo juu huandikwa. Kila mwanafunzi aandike mojawapo ya barua hizo kuhusumada yoyote kisha amsomee mwenzake. Sahihishianeni.Sehemu kuu na kanuni za barua rasmi
Barua rasmi huwa na sehemu au muundo fulani maalumu kama ufuatao:Anwani ya mwandishiTareheAnwani ya mwandikiwaMtajo/Kutaja mwandikiwa kwa heshimaKichwaUtangulizi/Kutajwa kwa kiiniMwili wa baruaHitimishoWako mwaminifu/mtiifuSahihiJina la mwandishiCheo cha mwandishi (ikiwa mwandishi anaandikakwa niaba ya shirika fulani, kikundi au kampuni)Soma mazungumzo haya na ujibu maswali chini yake.UMUHIRE: Mwenzangu, nieleze kuhusu jinsi ya kuandika barua rasmi.NDOLI: Lazima uandike anwani yako na ile ya mwandikiwa. Anwani yakokama mwandishi huja juu. Unapoandika anwani ya mwandikiwa, nisharti uandike cheo chake kwanza kabla ya kuandika jina na anwaniya kampuni chini ya cheo chake kama vile, 'MKURUGENZI MKUU,MWENYEKITI, MWALIMU MKUU’ na kadhalika.UMUHIRE: Baada ya anwani, ninaandika nini?NDOLI: Unaandika ufunguzi wa barua kama vile Kwa Mbunge Mheshimiwa,Kwa Mheshimiwa, Kwa Meneja Mkuu, Kwa Meneja, Kwa Mgeni waHeshima na kadhalika. Unaweza kuandika jina lake la pili baada yaBw au Bi.UMUHIRE: Naam! Kwa hivyo, baada ya kutambulisha mwandikiwa, ninaandikakichwa au vipi?NDOLI: Naam, rafiki yangu. Kichwa hudokeza kiini cha kuandika barua yako.Unapoandika kichwa, unaanza kwa kutumia kifupisho MINT: au KUH:UMUHIRE: MINT na KUH vinasimamia nini?NDOLI: MINT husimamia Mintaarafu au kwa mintaarafu ya, KUH husimamiakuhusu. Kichwa au mada yako haifai kuzidi maneno sita isipokuwapale ambapo pana lazima.UMUHIRE: Ninapoanza kuandika mwili, ninafaa kusema nini?NDOLI: Ikiwa ni barua ya kuomba kazi, ni vizuri uanze kwa kurejelea tangazola kazi hiyo au jinsi ulivyopokea kuwepo kwa nafasi hiyo. Baadaye,andika moja kwa moja kiini cha barua hiyo.UMUHIRE: Hakuna salamu?NDOLI: Naam. Barua rasmi haina salamu. Unaeleza moja kwa moja kiinicha kuandika barua. Unafaa kujikita katika ujumbe mmoja mkuu,yaani jambo linalokufanya uiandike barua hiyo. Ikiwa unaomba kazi,toa maelezo muhimu kukuhusu. Maelezo hayo yawe na uhusiano nakazi unayolenga kupata. Epuka maelezo mengi yasiyokuwa na manufaa.UMUHIRE: Lugha yangu inafaa kuwa ya namna gani?NDOLI: Lugha yako sharti izingatie adabu ya hali ya juu na kiwango cha juu cha urasmi.Lugha yako iwe sahihi. Ikiwa unaandika kwa kalamu, tumia hati nadhifu. Usitajechochote cha kuonyesha mambo au hisia za kibinafsi au uhusiano wa kibinafsina unayemwandikia.UMUHIRE: Nini huandikwa katika hitimisho la barua hii rasmi?NDOLI: Unaandika tumaini lako la majibu mazuri. Chini yake, unaandika:Wako Mwaminifu au Wako Mtiifu kisha unaweka sahihi. Chini ya sahihi yako,andika jina lako kamili. Ikiwa unaandika kwa niaba ya shirika au kampuni au kikundi,andika cheo chako chini ya jina lako.UMUHIRE: Asante kwa maelezo haya.Maswali
i) Je, barua rasmi ina kanuni zipi za kuzingatiwa?ii) Linganisheni sehemu na kanuni za kuandika barua za kirafiki na zile zakuandika barua rasmi. Jadilianeni kuhusu tofauti zilizopo kati ya barua zakirafiki na barua rasmi.Kazi ya kikundi
Jiunge na wanafunzi wenzako. Tazameni mifano ya barua rasmi iliyotolewa namingineyo. Jadilianeni kuhusu miundo ya barua hizo. Andikianeni barua rasmikuhusu mada yoyote.B. Matangazo mbalimbaliTangazo ni mpangilio wa maandishikwa mtindo maalumu kwa lengo lakupasha ama kupokeza ujumbe fulaniwa kidharura au muhimu.Zipo aina mbalimbali za matangazo:i) Matangazo ya biashara
Matangazo ya biashara ni maandishiambayo yanalenga kutoa maelezo fulanikuhusu kitu, bidhaa, mahali au jambokwa ajili ya kuwashawishi wasomajikununuana kutumia bidhaa husika aukuzuru mahali husika. Matangazo haya yanaweza pia kuwajulisha watu kuhusu bidhaa mpya zilizoingia sokoni au kuimarishwa kwa bidhaa zilizopo kwa sasa.
Kazi ya kikundi
Jiunge na wanafunzi wenzako katika kikundi. Tajeni matangazo mbalimbaliyaliyomo katika redio, televisheni, magazeti na vibango mbalimbali karibu namaeneo mnapoishi. Jadilianeni kuhusu jinsi istilahi au msamiati ulivyotumikakatika matangazo hayo na malengo ya matangazo hayo. Je, istilahi hizo zimefaulukatika kuafikia malengo husika?Jinsi ya kufika huko
Unaweza kusafiri angani kwa ndege hadi uwanja wa ndege wa Gisenyi. Hapo,waajiri wetu watakupokea kwa tabasamu na unyenyekevu.Ikiwa una gari, pitia barabara kuu ya Kaskazini Magharibi kutoka jijini Kigali.Itakuchukua saa tatu pekee.Tembelea hoteli ya Sabyinyo leo upate uhondo wa burudani.Kazi ya wanafunzi wawili wawili
Jiunge na mwanafunzi mwenzako. Someni tena matangazo yaliyopo hapo juu kwamakini huku mkitambua sifa na miundo ya matangazo hayo.Sifa na miundo ya matangazo ya biashara
Soma kifungu hiki na ujibu maswali chini yake.Matangazo ya biashara huwa na utangulizi wenye mvuto na hitimisho lenyeushawishi. Kumbuka kuwa lengo kuu la tangazo lolote la biashara ni kuwavutiawasomaji.Yapo matumizi ya takriri. Takriri ni kurudiarudia neno au maneno fulani. Kwa kuwamatangazo ya biashara hulenga kutambulisha bidhaa fulani au mahali fulani, bidhaaau mahali husika hurudiwarudiwa katika mwili wa tangazo ili wasomaji au watejalengwa wazikumbuke. Pia, jina la bidhaa na kampuni hutajwa na kurudiwarudiwa.Watu hupenda sana kusoma maneno mafupi na ni rahisi kuyakumbuka. Manenomarefu kwa upande mwingine huchosha na huchukua nafasi kubwa. Matangazoya biashara huandikwa kwa maneno mafupi mafupi yenye mnato na ujumbe mzito.Maneno mafupi hupunguza gharama ya matangazo hayo.Katika matangazo ya biashara kwenye redio na televisheni, matangazo hayohuambatana na sauti ya kimuziki. Sauti hiyo hulenga kuwavutia wanaosikizamatangazo hayo. Pia, huchangia katika kupitisha ujumbe uliokusudiwa.Wakati mwingine, matangazo hufuata mtindo wa dayalojia. Hapa, watuwanaohusika katika kutangaza bidhaa fulani huulizana maswali na kupashanaujumbe. Kwa mfanoMTU I: Je, umejaribu sabuni hii?MTU II: BadoMTU I: Ijaribu leo. Hii ndiyo suluhisho ya kudumu kwa madoa sugu.Matangazo ya biashara pia hutumia lugha ya kushawishi. Lugha hiyo huwa sahihiau hukosa usahihi. Lugha inayotumika hutegemea umri, jinsia ya wanunuziwanaolengwa.Matangazo ya biashara hueleza ubora wa bidhaa pekee na manufaa yake. Hutiliamkazo mambo haya kwa undani na wakati mwingine hutilia chumvi ubora namanufaa ya bidhaa husika.Matangazo mengi ya biashara hayataji bei ya bidhaa. Pia, hueleza zinakopatikanabidhaa zenyewe au jinsi ya kuzipokea mahali unapoishi. Wakati mwingine, hutoamwito wa kutembelewa kampuni husika.Zoezi
1. Taja sehemu kuu za matangazo ya biashara kwa mujibu wa kifungu namatangazo ya biashara uliyosoma au kusikia.2. Taja kanuni au sifa kuu za kuzingatiwa katika uandishi wa matangazo yabiashara.Kazi ya kikundi
Jiunge na wanafunzi wenzako katika kikundi. Fanyeni mradi wa kuandikamatangazo mbalimbali ya biashara kuhusu bidhaa mtakazojichagulia.ii) Matangazo ya mkutano
Katika matangazo haya, mwandishi hutaja kiini au ajenda za mkutano, mahali pamkutano, tarehe na wakati ambapo mkutano utaandaliwa na maelezo menginemuhimu.iii) Matangazo kuhusu ziara ya rais
Ziara ni tendo la kwenda mahali kwa sababu fulani kama vile kuzindua ujenzi wabarabara, kuwahutubia wananchi na kadhalika. Nalo tangazo lake linaweza kuwakama hili lifuatalo:Zoezi
Liandike tangazo kwa watu wote waliomo shuleni mwenu kuhusu ziara yawaziri wa elimu shuleni humo. Liandike tangazo hilo kwa niaba ya mwalimu mkuu.iv) Matangazo ya kuwachagua watu kujiunga na kikosi cha polisi
Huweza kutokea kwamba serikali inataka kuchagua watu kujiunga na kikosi chapolisi. Basi, huweza kulitangaza jambo kwa wananchi.Kazi ya wanafunzi wawili wawili
Jiunge na mwanafunzi mwenzako. Someni tangazo lililopo hapo juu na matangazomengineyo ya mikutano. Jadilianeni kuhusu sehemu muhimu za matangazo yamikutano na kanuni za kuzingatiwa katika uandishi wa matangazo maalumu.v) Matangazo kuhusu nafasi za kazi
Hutolewa kwa lengo la kufahamisha watu kuhusu kuwepo kwa nafasi fulani ya/zakazi katika kampuni, shirika ama idara fulani.Mfano
HALMASHAURI YA WILAYA YA NYAGATARETarehe 3/07/2016.NAFASI ZA KAZIMkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Nyagatare anatangaza kuwepokwa nafasi zifuatazo za kazi:1. MWENYEKITI WA BODI YA AJIRA (Nafasi 1)Sifa za Mwombaji kaziNi sharti awe:i) mkazi wa muda mrefu wa Wilayani Nyagatare,ii) na shahada ya uzamifu katika usimamizi,iii) mwenye umri wa miaka 35 au zaidi,iv) na tajiriba ya miaka 5 katika kusimamia watu katika shirika kubwa tajika,v) na rekodi nzuri ya utendakazi,vi) mwenye uwezo wa kuwatia motisha wafanyakazi ili kuinua hadhi ya bodi hii,vii) mtu mwenye kutoshawishika katika misimamo sahihi yake na ile yahalmashauri.Wajibu na majukumui) Kutangaza nafasi za ajira,ii) Kupendekeza kupandishwa vyeo kwa wafanyakazi,iii) Kutoa mafunzo au maelekezo kwa waajiriwa wapya,iv) Kupendekeza nyongeza ya mishahara kwa wafanyakazi,v) Kutekeleza majukumu mengineyo kama itakavyopendekezwa mara kwa mara.Kiwango cha mshaharaKitajadiliwa wakati wa mahojiano.2. MAAFISA WA UCHUKUZI DARAJA LA II ( Nafasi 5)Sifa za mwombaji kaziIli kufuzu katika nafasi hii, unahitajika kuwa na:i) shahada katika masuala ya usimamizi wa kibiashara,ii) tajiriba ya miaka 3 katika kitengo hiki,iii) uelewa wa masuala ya uchukuzi katika forodha na kanuni za barabara,iv) rekodi nzuri ya utendakazi,v) ufahamu wa matumizi ya kompyuta na mtandao.Majukumui) Kutayarisha bajeti na kuendesha uchukuzi,ii) Kuhakikisha kuwa takwimu, stakabadhi na kumbukumbu zinazohusu vyombovya usafiri pamoja na mitandao yake zinatunzwa vyema,ii) Kukusanya na kuandaa takwimu kuhusu maendeleo ya sekta ya uchukuzi nakuziwasilisha kwa wadau ndani na nje ya wilaya,iv) Kuweka faili za uchukuzi nchini,v) Kukadiria na kushauri juu ya utendaji wa miradi mbalimbali ya sekta yauchukuzi.Kiwango cha mshaharaKitajadiliwa wakati wa mahojiano.Ikiwa una sifa hizi na ungependa kujiunga nasi, tuma barua ukionyesha kaziunayoomba na uambatanishe wasifukazi wako wa hivi karibuni, nambari ya/zasimu na warejelewa watatu kwa mawasiliano wakati wa mchana. Tuma kwa anwanihii kabla ya usiku wa manane ya tarehe 23/08/2016.J.M. Gatete,Halmashauri ya Wilaya ya Nyagatare,S.L.P. 3013,NYAG ATA R E .Tanbihi
Halmashauri hii ni huru katika utoaji wa nafasi sawa za kazi bila kubagua yeyote.Ombi litakataliwa moja kwa moja endapo anayeomba kazi atahonga afisa yeyotekwa ajili ya kupendelewa.Zoezi
Tafuta matangazo mbalimbali kuhusu nafasi za kazi katika magazeti, mabango nakadhalika. Soma matangazo hayo na ubainishe sifa zayo na kanuni zilizozingatiwakatika uandishi huo.Kazi ya kikundi
Jiunge na wanafunzi wenzako katika kikundi. Huku mkirejelea matangazombalimbali, jadilianeni kuhusu tofauti zilizopo katika matangazo hayo mkizingatia:i) sifaii) sehemu kuuiii) kanuniiv) msamiativ) malengoC . Ilani
Ilani ni tangazo ambalo hutahadharisha au kuarifu kuhusu aina ya jambo ama tukioambalo linastahili kuepukwa, lau sivyo madhara hutokea.Ilani huwa na wazo moja tu maalumu. Hutolewa mahali penye shughuli nyingi amapalipo na watu wengi kama vile shuleni, chuoni, kanisani msikitini na kadhalika.Ilani mara nyingi huwa na mtindo rasmi. Ilani nyingi huwekwa katika mabangomakubwa, magazetini, kwenye majarida na kadhalika.Mifano
i) Ilani kuhusu mkurupuko wa ugonjwa
ILANIWIZARA YA AFYA, KUPITIA HOSPITALI KUU YA MKOA,INAWATANGAZIA KUZUKA KWA UGONJWA HATARI WAKIPINDUPINDU.WATU WOTE WANASHAURIWA KUZINGATIA USAFI WA MWILI NA MAZINGIRA.ILI KUJIKINGA KUTOKANA NA MAAMBUKIZI YA UGONJWA HUUHATARI, MAMBO YAFUATAYO NI SHARTI YAZINGATIWE:i) KILA MTU AHAKIKISHE ANATUMIA CHOO.ii) KILA MTU ANAWE MIKONO KWA MAJI SAFI NA SABUNI BAADA YA KUTOKA CHOONI.iii) HAKIKISHA UNAKULA KATIKA MAHALI SAFIiv) WATU WASILE KWENYE MIKAHAWA.v) ALIYE NA DALILI ZA KUENDESHA NA KUTAPIKA AKIMBIZWE MARAMOJA HOSPITALINI KWA UCHUNGUZI NA MATIBABU.vi) ALIYEAMBUKIZWA APEWE MAJI MENGI YA KUNYWA WAKATIANAPOPELEKWA HOSPITALINI.vii) KILA MTU ACHEMSHE MAJI YA KUNYWA.viii)MTU YEYOTE ALIYEAMBUKIZWA ATENGWE NA WATU WENGINE.ONYO:MTU YEYOTE ATAKAYEPATIKANA AKIUZA CHAKULA KATIKAMAENEO WAZI ATASHTAKIWA.ii) Ilani kuhusu unywaji wa pombe
Mfano
POMBE HATARISerikali, kupitia wizara ya afya, inawatahadharisha wananchi kuhusu kuzuka kwapombe hatari ya SUMEDA inayonywewa sana katika sehemu mbalimbali nchini.SUMEDA ni pombe hatari kwa afya yako kwa kuwa inatengenezwa kwa kutumiadawa ya kuhifadhi maiti na kemikali nyingine hatari.Pombe hii hatari imesababisha vifo vya watu zaidi ya 50, kuwapofushawengine wengi pamoja na kutoa mimba.Atakayepatikana akiuza ama kunywa aina hii ya pombe atakamatwa.Ofisi ya mkuu wa wilaya.iii) Ilani ya kutokanyaga nyasi
Mfano
ILANIHAPANA RUHUSA KUKANYAGA NYASINA MENEJIMENTIZoezi
i) Tazama mifano ya ilani zilizotolewa hapo juu. Je, ilani hizo zina sifa gani?ii) Andika ilani kuhusu mada yoyote upendayo.Kazi ya wanafunzi wawili wawili
Jiunge na mwanafunzi mwenzako. Andikeni ilani kuhusu mada hizi na mziwekekwenye maeneo husika shuleni.i) Kutokanyagwa kwa sehemu fulani zenye nyasi.ii) Kuwepo kwa mjadala kuhusu: mbinu za kisasa za kilimo ni bora kuliko mbinuza jadi za kilimo.iii) Kuwafahamisha wanafunzi kunawa mikono watokapo msalani.iv) Kuzingatia usafi jikoniD. Mialiko
Mwaliko ni mwito wa kumtaka mtu au watu kuhudhuria shughuli au hafla fulani.Wito wa namna hii huweza kufanywa kwa njia ya barua ya kirafiki au barua rasmina hata kwa matangazo.Kazi ya kikundi
Jiunge na mwanafunzi mwenzako na mchunguze mchoro huo uliopo hapo chini.Jadilianeni kuhusu mambo yaliyomo ubaoni.Mifano ya mialiko
i) Mwaliko wa harusi
Je, umewahi kualikwa katika harusi au kuona kadi ya mwaliko wa harusi? Je,mwaliko huo ulikuwa na mambo gani?Mwaliko wa harusi huwaomba jamaa na marafiki kuhudhuria sherehe ya harusi.Kadi za mialiko ya harusi huchukua miundo na sura tofautitofauti. Miundo yakadi hizo hutegemea ubunifu wa anayeziunda au mapendekezo ya maarusi auwaandalizi wa harusi.Kazi ya kikundi
Jiunge na wanafunzi wenzako. Tazameni mialiko ya harusi iliyotolewa hapa chini.Jadilianeni kuhusu mambo yaliyomo katika mialiko hiyo.Mfano
A .
B.
Kanuni za kuzingatiwa katika uandishi wa mwaliko wa harusi
Unapoandika mwaliko wa harusi, ni sharti utaje majina ya watu wanaofunga ndoa,tarehe ya harusi, mahali pa harusi na wakati sherehe itakapoanza.Watu mbalimbali huandika mialiko ya harusi kwa njia tofauti tofauti. Maranyingi, kadi hutumika. Wao hurembesha kadi za harusi ili kuwavutia wasomajina kuonyesha mapenzi yaliyopo kati ya maharusi. Wengine hunukuu maandikotakatifu yanayotaja mapenzi na ndoa. Almuradi, kila mwaliko wa harusi huwa naumbo lake maalumu.Kazi ya kikundi
Jiunge na wanafunzi wenzako na mchukulie kuwa nyinyi ni wanachama wa kamatiinayoandaa harusi. Mna nia ya kutengeneza kadi nzuri ya mwaliko wa harusi. Kilammoja achore kadi ya mwaliko na aweke ujumbe wake. Linganisheni mialiko yenuna mchague mwaliko bora zaidi kisha muufanye urembeke zaidi. Onyesheni namlisomee darasa zima kadi yenu.ii) Mwaliko wa kutembelea mbuga ya wanyama
Mwaliko kama huu huchukua umbo la barua rasmi.ii) Mwaliko wa maonyesho ya vitabu
Zoezi
i) Soma tena barua za mialiko hapo juu. Taja mambo muhimu yaliyozingatiwakatika uandikaji wazo.ii) Mwandikie aliyekuwa mwalimu wako barua ya kumwalika kwenu kwasherehe ya kukuaga kwa safari ya kwenda ng’ambo kusoma.Zoezi la ziada
Andika barua za mialiko kuhusu mada yoyote.E . Aina za alama za uandishi na matumizi yake
Wenzetu wanapozungumza, tunaweza kutambua wanapomaliza usemi wao kwakusikia sauti zao. Lakini katika uandishi, hakuna sauti. Badala ya sauti, zipo alamaza uandishi ambazo hutumiwa kuwakilisha sauti katika uandishi. Kutokana naalama hizo, tunatambua kama usemi umekwisha, kuulizwa swali, kushangaa nakadhalika. Pia, tunaposoma, tunajua wapi tunafaa kupumua kidogo, kushusha aukupandisha sauti na kadhalika.Alama hizi huitwa viakifishi. Hivyo basi, viakifishi ni alama zinazotumiwa katikamaandishi ili kuleta maana ikusudiwayo katika matini mbalimbali kama vilesentensi, aya, mtungo, barua, mialiko, matangazo, ilani na kadhalika.Aina za viakifishi
Nukta (.)
a) Huwekwa mwishoni mwa sentensi. Kwa mfano:i) Nimechoka.ii) Waziri mkuu wa Uchina amewasili mjini Kigali.b) Hutumiwa kuonyesha ufupisho wa maneno. Kwa mfano:i) S.L.P. – Sanduku la Postaii) Bi. – Bibic) Hutumika kubainisha saa na dakika au tarehe. Kwa mfano:i) 3.20 – saa tisa na dakika ishiriniii) 14.5.2016- tarehe kumi na nne, mwezi wa tano, mwaka wa elfu mbili na kumi na sitad) Hutumiwa kuonyesha vipashio vya pesa. Kwa mfano:Sh. 10.50 – shilingi kumi na thumuni hamsinie) Zikitumiwa mara tatu mfululizo (...), huonyesha kutokamilika kwa sehemuhusika. Kwa mfano:Nitakupa lakini ni sharti...Mkato/koma ( , )
a) Hutumiwa kuonyesha pa kutua kwa muda mfupi katika sentensi. Kwa mfano:i) Nilipowasili nyumbani, nilienda kuteka maji kisimani.ii) Kwa kuwa tulijiandaa vilivyo kwa mtihani wa kitaifa, tulipita.b) Hutumiwa kutenga maneno yaliyo katika orodha:i) Kwenda sokoni ununue mboga, nyama, mafuta, na unga.ii) Mwanafunzi huyu ni mtiifu, mwerevu, mtanashati, na mwenye bidii.c) Hutumiwa kubainisha sehemu mbili za sentensi zilizo kinyume:i) Umoja ni nguvu, utengano ni udhaifu.ii) Aliniambia atakuja, hakuja.d) Hutumiwa kabla ya alama za mtajo. Kwa mfano:Mama akasema, “Niletee chumvi.”e) Hutumiwa wakati sentensi inapoanza kwa kiunganishi. Kwa mfano:Kweli, alikuwa mtu mwovu.f ) Hutumiwa unapoita mtu ili kupata usikivu wake kabla hujamwambiachochote. Kwa mfano:Nkusi, niletee kalamu.g) Hutumiwa unapokubali au unapokataa kitu. Mfano:i) Ndio, nitakuja.ii) Hapana, sitakulipa.Nukta mbili/koloni (
a) Hutumiwa kutanguliza maneno yaliyo katika orodha.Kwa mfano:i) Nenda kaniletee: kalamu, karatasi na kifutio.ii) Amenunua: machungwa, sukari, na ndizi.b) Hutumiwa kuashiria maneno ya msemaji badala ya alama za mtajo hasa katikauandishi wa mazungumzo au tamthilia.i) Mama: Lazima uniambie ulikokuwa tangu jana.ii) Mwalimu alisema: Ingieni darasani.c) Hutenganisha numerali za saa.Kwa mfano:4:10 – saa kumi na dakika kumiNukta na kituo (;)
a) Hutumiwa kuunganisha vishazi vikuu bila kutumia kiunganishi. Kwa mfano:Sikwenda Kayonza; nilienda Kirehe.b) Hutumiwa kumpumzisha msomaji katika sentensi iliyo ndefu ili apumzikezaidi kuliko pale inapotumiwa koma. Kwa mfano:Alipofikiri sana, alitanabahi kuwa hakikuwepo cha kutorokwa; yeye angewezakuondoka nyumbani au kumwacha mumewe, aende popote kufanya lolote.Kistari kifupi (-)
a) Hutumiwa kuonyesha kuwa neno linakatwa kwa vile limefika ukingoni mwamstari husika na bado linaendelea katika mstari unaofuatia.Tanbihi: Neno la silabi moja halikatwi.b) Hutumiwa kuunga maneno yanayojenga neno moja. Mtindohuu aghalabu hujitokeza katika maneno yenye asili ya kigeni. Kwa mfano:i) Idd-el-Fitriii) Dar-es-Salaamc) Huweza kutumiwa badala ya koma. Kwa mfano:Nyimbo za asili-hasa rumba-zinapendwa na wengi.Alama ya mshangao (!)
Hutumiwa kuashiria mahangaiko ya moyo kama vile hasira, hofu, mshangao nakadhalika.i) Lo! Mwanafunzi ameangusha kitabu cha mwalimu matopeni.ii) Wamefungwa mabao kumi kwa nunge!Alama ya kuulizia/kiulizi (?)
a) Hutumiwa mwishoni mwa sentensi kuonyesha kuwa sentensi hiyo ni swali.Mwa mfano:
Unaitwa nani?
b) Hutumiwa kuonyesha ukosefu wa uhakika kuhusu jambo kama vile mwaka.Kwa mfano:Shule hii ya Tumaini ilianzishwa 1992 (?)Mabano/parandesi
a) Hutumiwa kufunga maneno ya ziada katika sentensi. Kwa mfano:Nyamata (makao makuu ya Bugesera) inakua kwa kasi.b) Hutumiwa mwandishi anapotaka kutoa ufafanuzi kwa lugha nyingine tofautina ile anayoitumia.Kwa mfano: Walowezi (settlers) walifukuzwac) Hutumiwa kufungia herufi za kuorodhesha. Kwa mfano:(a) huelimisha, (b) huburudisha, (c) huonyaMkato (/)
Hutumiwa kuonyesha kuwa mojawapo ya vitu vilivyotajwa chaweza kutumiwabadala ya hivyo vingine.Tazama: Abera alishangaa/aliduwaaMtajo: (“ ” au ‘ ’)
Hutumiwa kuonyesha maneno halisi ya mzungumzaji. Kwa mfano:“Nitafika kesho jioni,” alisema mdogo wake.Herufi kubwa (H)
Hizi ndizo alama za uandishi zinazotumiwa sana kuliko nyingine zote. Hutumiwakila baadaya herufi kubwa.Mama anapika.Zoezi
Kiakifishe kifungu kifuatachoIlikuwa asubuhi na mapema bw butera alipotoka kwake kwenda kazini fikiranimwake alijikumbusha pindi nikifika ofisini nitaomba ruhusa niende nimlipie bintiyangu karoaliabiri gari linaloelekea ruhango baada ya mwendo mfupi tu lo gari hilo lilipataajali liligongana na lori japo ng'ombe waliokuwemo njiani walikufa takriban woteabiria walipata majeraha madogo madogo lakini ililazimu wapelekwe hospitalinihivyo butera hakutimiza azma yakeMazoezi ya ziada
Zoezi A
Andika kifungu cha habari kuhusu mada yoyote ukitumia alama za uandishi kwausahihi.Zoezi B
Jiunge na mwanafunzi mwenzako na msome vifungu mbalimbali vya habarivilivyomo katika kitabu hiki, magazeti, na vitabu vinginevyo. Bainisheni na kuainishaalama mbalimbali za kuakifisha zilizotumika na jinsi zilivyotumiwa.Maswali ya marudio
1. Eleza maana ya barua ya kirafiki.2. a) Taja watu watano wanaoweza kuandikiwa barua ya kirafiki.b) Mwandikie mmoja wa hao uliowatajia barua ya kirafiki.3. Zitaje sehemu zote kuu za barua ya kirafiki huku ukizieleza.4. Eleza maana ya barua rasmi.5. Taja aina tano za barua rasmi.6. Mwandikie Mwalimu Mkuu wa shule ya msingi ulikosomea ukiomba nafasi yakufunza katika shule hiyo.7. Zitaje sehemu kuu za barua rasmi.8. Eleza kanuni za kuzingatiwa wakati wa kuandika barua rasmi.9. Eleza tofauti zilizopo kati ya barua rasmi na barua ya kirafiki.10. Kwa maneno yako mwenyewe, eleza tangazo ni nini.11. Ipo tofauti gani kati ya matangazo na barua rasmi?12. Eleza tofauti kati ya tangazo la tanzia na tangazo la mkutano.13. a) Ilani ni nini?b) Andika ilani utakayoweka msalani ili kuwatahadharisha wanafunziwenzako kuhusu madhara ya kutonawa mikono baada ya kutoka msalani.14. a) Eleza sifa za matangazo ya biashara.b) Andika tangazo la biashara kuhusu bidhaa upendayo.15. Eleza umuhimu wa mwaliko.16. Je, kuakifisha ni kufanya nini?17. Eleza umuhimu wa uakifishaji.18. Yataje kwa mifano matumizi matano ya nukta.19. a) Eleza maana ya mtajo.b) Andika mifano miwili ya matumizi ya mtajo.20. Eleza kwa ufupi mambo muhimu uliyojifunza katika sura hii. Taja jinsi mambohayo yatakavyokusaidia na kuisaidia jamii yako.Sura 3: Matumizi ya lugha katika mazingira mbalimbali
Mada ndogo: Rejesta za mpira na burudani
A Rejesta mbalimbali nchini Rwanda
Rejesta au sajili ni lugha inayotumiwa mahali ama katika hali fulani na wala haiwezikuhamishwa kutoka mazingira yale na kutumiwa katika mahali pengine. Lugha hizihutofautiana kwa misingi ya msamiati, muundo wa sentensi na kadhalika. Kutokanana tofauti hizi, tunapata rejesta za aina mbalimbali. Baadhi ya rejesta hizo ni kamahizi zifuatazo.i) Rejesta ya mpira wa miguu
Mpira wa miguu pia huitwa kandanda, soka au kambumbu. Huu ni mchezomaarufu sana hapa nchini Rwanda na duniani kote. Kwa mfano, mashindano yakombe la dunia hutazamwa na watu wengi sana kote duniani. Mashindano hayohuandaliwa kila baada ya miaka minne. Pia, yapo mashindano ya Bara la Afrika,Kombe la Kagame, ligi mbalimbali na kadhalika.Baadhi ya watu hufuatilia mechi mbalimbali kupitia redio au televisheni. Wapowanahabari ambao hutangaza mpira kupitia vyombo hivyo. Rejesta ya mchezohujitokeza kupitia matangazo hayo.Kazi ya wanafunzi wawili wawili
Jiunge na mwanafunzi mwenzako. Tazameni mchoro huu. Jadilianeni kuhusuyaliyomo michoroni na myahusishe na mazingira yenu.Soma kifungu hiki na ujibu maswali chini yake.
Matangazo ya kandanda sehemu I
Hujambo msikilizaji. Karibu katika matangazo haya ya moja kwa moja ya kabumbu.Ni mimi mtangazaji wako, Teta. Huu ni mchuano wa fainali ya kuwania kombe laFahari ya Rwanda kati ya shule ya wasichana ya Elimu Bora na Tusonge Mbele.Timu hizi mbili ni wapinzani sugu tangu jadi. Elimu Bora inajivunia historia nzurikwa kushinda kombe hili mara kumi. Wao ndio bingwa tetezi. Tusonge Mbeleimeshinda kombe hili mara tatu. Mwaka jana walitimuliwa katika nusu fainali.Katika awamu hii, wana rekodi ya kutoshindwa katika mechi zote hadi kufikiafainali. Je, rekodi hiyo itavunjwa na Elimu Bora?Naona timu zote mbili zikiingia uwanjani tayari kwa pambano. Kwa sababu ya mudasitataja majina ya wachezaji wote. Nitayataja kadri wanavyozidi kucheza. Kwa ufupi,kila timu ina golikipa mmoja. Elimu Bora wameweka wachezaji watatu katika safuya ulinzi nao Tusonge wanawachezesha wachezaji wanne katika safu hiyo hiyo.Timu ya Elimu Bora wametia wachezaji watano katika kiungo cha kati nao Tusongewanawachezesha wachezaji watatu. Elimu Bora wana washambulizi wawili naoTusonge wana washambulizi watatu katika safu ya mashambulizi. Timu zote mbilizina wachezaji wa akiba watano. Refa mkuu anapuliza kipenga nao wasaidizi wakewawili wanakimbia pembeni mwa uwanja kuinua kijibendera. Mmoja anakimbiakushoto naye mwingine anakimbia kulia.Manahodha wa timu zote mbili wapo pale katikati ya uwanja kurusha sarafu ilikuamua timu inayoanzisha mpira. Mashabiki wa timu zote mbili wanaimba nyimboza kushangilia timu zao. Nao makocha wao wamekaa pembeni mwa uwanjakushuhudia wasichana wao wakimenyana.Naam, refa anapuliza kipenga. Mpira unaanzishwa pale na Ikirezi na Uwamwizawa timu ya Elimu Bora. Ikirezi anapiga pasi kwake Gwiza. Gwiza anapiga chenga.Anaangalia aupige wapi. Anapiga pasi safi kwake Umuliza. Umuliza na mpira.Umuliza anakwenda. Anapiga shoti ndefu kuelekea lango la Tusonge. Munyanaanajibu kombora kwa kichwa. Mpira unakuwa mwingi na kutoka nje.Hee! Hee! Elimu Bora wameanza mchuano huu kwa kasi mno. Wanatafuta baola mapema. Kamaliza anarusha ngoma ile kwake Muteteri. Muteteri anatelezana kuanguka. Refa anasema twendelee. Mutoni anachukua mpira. Tusongewanafanya shambulizi la kujibu. Kamiza kwake Umuhire. Umuhire...Umuhire nampira. Umuhire anakwenda. Umuhire anavuka mstari wa katikati. Anatoa pasi safi..go..go..ah! Kijibendera kipo juu. Tona amejenga kibanda katika ardhi ya wenyewepasi ruhusa. Lo! Leo kuna kazi hapa.Msamiati
kabumbu – mchezo wa mpira wa mguu/kandandamchuano – mashindano baina ya timu mbilifainali – shindano la mwisho kabisa la kutafuta mshindikuwania kombe – kushindania kombe/tuzo katika mchezowapinzani – kikundi cha watu wanaoshindana na wenginebingwa tetezi – timu ambayo iliibuka mshindi/kuchukua kombe katika awamuiliyopita ya shindano fulani.nusu fainali – mchezo unaotangulia fainali ambapo washindi hucheza katika fainalisafu ya ulinzi – wachezaji ambao huzuia wapinzani kufunga baokiungo cha kati – wacheza ambao hucheza sana katikati ya uwanjawashambulizi – wachezaji ambao hucheza karibu na lango la wapinzani ili wafunge baowachezaji wa akiba – wachezaji ambao hukaa nje ya uwanja na ambao huingizwandani kuchukua nafasiza wenzao waliopata jeraha au kuchokakuinua kijibendera – kuonyesha kuwa mchezaji amekiuka kanuni za mchezokurusha sarufi – kuamua timu gani inaanzisha mchezo kwa kurusha sarafu juu.anapiga pasi – mchezaji mmoja kumpigia mwenzake mpiraanapiga chenga – kumhepa au kumpita mpinzani kwa mpiraanapiga shoti – kupiga mpira kuelekea lango la mpinzanianajibu kombora – kuzuia mpira kwa kuupiga kuelekea upande wa pilimpira unakuwa mwingi – mpira kukosa kuthibitiwa na wachezajimpira umetoka nje – mpira kuenda nje ya mstari wa nje uwanjanibao – mpira kuingia ndani ya langoshambulizi la kujibu – wachezaji kuelekeza mpira kwa kasi kuelekea lango lawapinzani punde tu baada ya mpira kuelekezwalangoni mwaokujenga kibanda/kuotea – kuvunja kanuni za ushambulizi kwa kushambuliaghafla nyuma ya mchezaji wa mwisho wa timu pinzaniZoezi
1. Tunga sentensi sahihi ukitumia msamiati uliotolewa maelezo hapo juu.2. a) Orodhesha na utoe maana ya maneno yote katika rejesta ya kandandakifunguni humu lakini ambayo hayakuelezwa hapo juu.b) Tunga sentensi ukitumia msamiati uliotaja hapo juu.Kazi ya kikundi
Wewe ni mtangazaji wa mpira wa miguu. Andika matangazo ya mchezo kati yatimu zozote mbili upendazo. Baada ya kuandika, jiunge na mwanafunzi mwenzako.Kila mmoja amsomee mwenzake matangazo yake.Sifa za rejesta ya mpira wa miguu
Tazama matangazo ya mpira katika kifungu ulichosoma. Je, pana sifa gani katikarejesta hiyo?Zifuatazo ni orodha ya sifa za rejesta ya mpira wa miguu.i) Hujaa jadhba hasa baada ya mchezo kuanza,ii) Hujaa mazungumzo ya kuhamisha ndimi ambapo baadhi ya maneno yaKiingereza na hata kienyeji hutumiwa,iii) Huwa na lugha ya kuchekesha na kuburudisha wanaoisikiliza,iv) Hujaa maoni mbalimbali kuhusu nani atashinda, nani mchezaji bora zaidi,na kadhalika,v) Huwepo kurudiarudia maneno kama vile majina ya wachezaji, dakika zilizopita,mabao yaliyofungwa na kadhalika,vi) Huwa na lugha ya kuibua hisia na kumfanya mtu kuingiwa na mahangaiko ya moyo,vii) Sentensi fupi fupi huweza kutumika pamoja na taswira ya kuchora picha kamili yayanayotendeka.Kazi ya wanafunzi wawili wawili
Jiunge na mwenzako mmoja. Someni kifungu hiki ili mbainishe rejesta ya mpira wamiguu na sifa zao.Matangazo ya kandanda sehemu II
Mlinda lango wa Elimu Bora anaenda kupiga mpira wa madhambi. Anapiga komborandeeeefu na kutoka nje. Munyana anarusha ngozi iliyowambwa na kutengenezwa mpira.Kamiza anapiga chenga. Anatoa pasi kwake Usanase. Usanase anakwenda.Anaingia ndani ya kijisanduku. Hatari katika lango la Tusonge. Hatariiiii! Lo! Kayitesiananawa mpira. Refa anasemaje. Naam, kipenga kinapulizwa. Refa anawapa ElimuBora penalti. Shangwe na vifijo kutoka kwa mashabiki wa Elimu Bora. Kayitesianaonyeshwa kadi ya manjano. Kayitesi amecheza rafu. Achunge asionyeshwe kadinyingine ya manjano kwani atatolewa uwanjani.Haya! Tuone jinsi mambo yatakavyokuwa hapa. Refa anahesabu miguu kumi namiwili kutoka lango la Tusonge. Anaweka mpira chini. Ikirezi amesimama nyumaya mpira ule tayari kupiga mkwaju wa penalti. Mlinda lango wa Tusonge, Kabatesi,amesimama mbele ya wavu. Refa anapuliza kipenga. Ikirezi anapiga hatua mbilitatu nyuma. Anapiga...go...goo... Nje! Heeee! Heee! Ikirezi ameshindwa kutikisawavu. Alipiga kombora zito. Kabatesi akaruka na kuupiga mpira ule ukapitia juu yamtambaa panya wa goli hadi nje. Kona! Kona ile inapigwa kutoka kushoto wa golila Tusonge.Dakika zilizokatika hapa ni dakika kumi na tano. Bado dakika thelathini kipindicha kwanza kikamilike. Tutakupa nafasi ya kuwasiliana nasi wakati wa mapumzikoambao utachukua dakika kumi na tano. Baadaye tutarudi hapa kwa kipindi chapili ambacho kitachukua dakika nyingine arubaini na tano pamoja na dakika zanyongeza kutoka kwa refa mkuu. Ikiwa timu hizi zitatoka sare baada ya kipindicha lala salama, dakika thelathini za ziada zitaongezwa. Ikiwa bado mshindihatapatikana, watapiga penalti ya kuamua mshindi. Mshindi na mshinde shartiwapatikane leo kwa sababu hii ni fainali.Umuliza anapiga kona safi pale. Uwamwiza anakimbilia mpira ule. Anapiga kichwa..go..goo...goooooool! Mpenzi msikilizaji, hayawi hayawi huwa! Hatimaye ElimuBora wamepata goli la kwanza. Uwamiza amecheka na wavu. Yeye ndiye mfungajibora kufikia sasa. Mashabiki wote wa Elimu Bora na makochi wao wameacha vitivyao. Mashabiki wa Tusonge wameinamisha vichwa vyao. Wachezaji wa Tusongewamepandwa na mori. Wamemzingira refa mkuu. Wanadai kuwa Uwamwizaalikuwa ameotea. Nahodha wao, Mutoni, ambaye ni beki wa kupanda na kushukaanammiminia refa maneno makali. Refa anatia mkono katika mfuko wa nyumaya kaptura na kuchomoa kadi nyekundu. Salaale! Mutoni ameonyeshwa kadinyekundu kwa kukosa adabu. Anasindikizwa nje ya uwanja. Timu ya Tusongewamebaki na wachezaji kumi pekee. Je, itakuaje?i) Rejesta ya burudani
Kama ujuavyo, burudani ni shughuli ifanywayo kwa ajili ya kuchangamsha nakufurahisha watu. Nayo mazingira ya namna hii yana msamiati wake ambao ndiolengo la sehemu hii.Tazama mchoro huu na ueleze mambo yanayojiri katika mchoro wenyewe.
Soma kifungu hiki cha habari na ujibu maswali chini yake.
MFAWIDHI:Leo ni leo! Asemaye kesho....?WATU: Ni mwongo!MFAWIDHI:Hapana! Asemaye kesho hayuko hapa. (Watu wanacheka) Leo showhii itakuwa ya kukata na shoka.Kama huna shoka sijui utakata na nini.MTU I: Tutakata na wembe.MFAWIDHI: Wembe utavunjika. (Watu wanacheka) Tuna wasanii wanaotajika ambao wamefika hapa kututumbuiza.Mko tayari kuvunjika mbavu?WATU: Ndiyooooo!MFAWIDHI: Shauri yenu. Mimi sitagharamia matibabu ya mbavu zitakazovunjika.(Watu wanacheka) Mabibi na mabwana, sote tumkaribishe mwimbajikatika jukwaa kwa makofi na vigelegeleeeeee!(Watu wanapiga makofi. Mwimbaji anaingia.)MFAWIDHI: Kwenu mnanunua sindano kweli?MWIMBAJI: Hapana.MFAWIDHI: Ningeshangaa. Wewe ni sindano tayari. (Watu wanacheka)MWIMBAJI: Kwetu tuko wengi sana.MFAWIDHI: Mko wengi hadi mnapika chapati moja kisha mnapiga chapa.(Kicheko). Kabla hatujaanza, ebu tupe historia fupi kuhusu safariyako katika muziki.MWIMBAJI: Nilianza kwa kucheza kayamba kanisani.Hapo ndipo bendi yaUmoja Jazz wakatambua kipawa changu. Wakanichukua kuwachezeatarumbeta. Baada ya muda mfupi, nikaanza kujisimamia. Nikatungana kurekodi nyimbo zangu kama na kujichezea gitaa.Hivi karibuni nitaunda bendi yangu.MFAWIDHI: Usikose kunijumuisha katika kwaya yako. Nitakuimbia soprano.(Watu wanacheka) Leo umetuandalia nini?MWIMBAJI: Leo nitawatumbuiza kwa taarabu.MFAWIDHI: Haya haya! Wakati wa burudani umewadia. Kila mtu atafute nafasina mwandani wake. Muwe wawili wawili. Kama huna wako, elekajiwe. Kuna mawe mengi hapa. (Kicheko) Hakuna kukanyagana mguu.(Watu wanacheka). Kama hujui kucheza miondoko ya taarabu,kuja hapa mbele nikufunze. (Watu wanacheka). Haya twende kazi.(Mwimbaji anaimba. Watu wanacheza.)Maelezo ya msamiati
kukata na shoka – kufanakuvunjika mbavu – kuchekakayamba – ala ya muziki yenye umbo la kisanduku ambayohutengenezwa kwa matete na kutiwa punje kavu auchangarawe na hutikiswatikiswa wakati wa kuimbabendi – kikundi cha waimbaji wanaoimba pamojatarumbeta – ala ya muziki ya kupuliza ambayo hutengenezwa kwa shaba nahutoa sauti mbalimbaligitaa – ala ya muziki ambayo kwa kawaida huwa na nyuzi sitakwaya – uimbaji wa pamoja katika kikundi maalamu cha kuimbataarabu – muziki wenye mahadhi ya mwambao wa Afrika Masharikiunaotumia mchanganyiko wa ala za Kiarabu, Kihindi na KizunguZoezi
1. Tunga sentensi sahihi ukitumia msamiati uliotolewa maelezo hapo juu.2. Toa mifano zaidi ya rejesta ya burudani. Andika msamiati wa kimsingiunaotumika katika rejesta hizo.3. Eleza sifa ya lugha iliyotumika kifunguni.Sifa za rejesta ya burudani
Rejesta ya burudani huwa na sifa mbalimbali. Tazama baadhi ya sifa hizo katika orodha ifuatayo:i) Kuwa na maneno ya raha,ii) Huibua hali za kutuliza na kupumbaza mshiriki,iii) Kuwepo na uwezekano wa washirika wake kukesha hadi che hukuwakijifurahisha kwa namna wapendavyo,iv) Kuwepo bendi ya muziki na wanasarakasi,v) Hali ya kusahau shida na mahangaiko aliyonayo mshiriki angalau kwa wakati mfupi tu.Kazi ya wanafunzi wawili wawili
Jiunge na mwanafunzi mwenzako. Fanyeni mazoezi haya:1. Toeni mifano zaidi ya rejesta za burudani.2. Jadilianeni sifa za lugha inayotumika katika rejesta mlizotaja.3. Linganisheni na mtofautishe msamiati uliotumika katika rejesta hizo mbalimbali za burudani.Umuhimu wa michezo na burudani
a) Umuhimu wa michezoMichezo ni shughuli za kushindana kati ya timu au watu tofauti tofauti ili kutafuta ushindi.Je,wewe unapenda kucheza mchezo gani?Kazi ya wanafunzi wawili wawili
Jiunge na mwanafunzi mwenzako. Tazameni michoro iliyopo hapo chini na mtaje yanayotendeka.Soma kifungu na ujibu maswali yaliyoulizwa chini yake.
Michezo ina umuhimu mkubwa kwetu kutokana na sababu mbalimbali. Kwanza,mchezo huimarisha afya yetu. Wachezaji hufanya mazoezi ya viungo. Mazoezihayo ya viungo husaidia miili yetu kuyeyusha mafuta ya ziada, kunyosha misuli,kuimarisha mapigo ya moyo na kadhalika.Pili, michezo huleta umoja miongoni mwa jamii. Watu wanapoenda kutazamamchezo kama vile kandanda, hujumuika pamoja kushabikia timu fulani. Pale,wao hujenga urafiki. Mathalan, timu yetu ya taifa inapocheza, Wanyarwandawote huja pamoja kuishabikia. Tunapofanya hivyo, tunajenga umoja wetu kamaWanyarwanda. Baadhi ya mashabiki pia husafiri pamoja na timu yetu ya taifawanapocheza nje ya Rwanda. Safari kama hizo huchangia kujenga umoja naurafiki miongoni mwa mashabiki hao.Tatu, michezo huleta fahari. Mchezaji mashuhuri, timu bora na taifa bingwa katikamichezo fulani hujulikana kwingi na kusifiwa. Sifa hizi huinua hadhi ya mtu binafsi,timu na taifa kwa jumla. Nchi inayosifika kwa mchezo au michezo fulani huwakatika hali nzuri ya kuvutia watalii.Michezo huleta pato la kuridhisha. Pato hili huwa kwa mchezaji binafsi, kwakilabu na hata kwa taifa. Wachezaji wa vilabu mbalimbali na timu ya taifa hulipwamshahara na marupurupu mengi. Baadhi ya wachezaji hawa hasa wanaochezeavilabu vya kimataifa ni matajiri wa kutajika kutokana na michezo.Vilabu mbalimbali pia hunufaika pakubwa. Wao hukusanya pesa nyingi kutokana namauzo ya tikiti, matangazo ya biashara katika viwanja vyao, kuuzwa kwa wachezajiwao kwa vilabu vinginevyo na kadhalika. Taifa zima pia hunufaika kutokana naushuru mbalimbali unaolipwa na wachezaji pamoja na vilabu husika.Michezo huburudisha na kutuliza roho. Baada ya shughuli nyingi za siku au wiki,mashabiki hujipumzisha akili kwa kutazama michezo wanayopenda. Pia, kushabikiatimu na kusherehekea ushindi huleta uchangamfu.Maswali
1. Taja umuhimu wa michezo kulingana na kifungu hiki.2. Michezo ni njia bora kuu ya kuimarisha afya yetu. Tetea kauli hii.3. Eleza jinsi michezo huleta ushirikiano kati yetu.4. Jadilianeni kuhusu jinsi mnavyoweza kutumia michezo kukuza ushirikiano,kuboresha afya na kutatua matatizo yanayokumba jamii yenu.b) Umuhimu wa burudaniTazama michoro iliyopo hapa chini. Je, mambo gani yanafanyika?Soma kifungu kifuatacho na ujibu maswali chini yake.Kama ilivyo michezo, burudani ina umuhimu mkubwa kwa jamii. Kwanza, burudanihukuza umoja na utangamano miongoni mwa wanajamii. Watu wanapokuja pamojakucheza densi, kutazama sarakasi, sinema na kadhalika, wao hujenga urafiki nauhusiano mwema miongoni mwao.Vilevile, burudani hukuza ushirikiano. Watu wanaoshiriki katika kuwaburudishawanajamii huja pamoja ili kuafikia malengo hayo. Mfano, bendi au kwayahushirikisha watu mbalimbali. Ushirikiano huu hukuza umoja miongoni mwa wahusika wote.Burudani pia hukuza afya yetu. Tunaposhiriki katika densi, viungo vya miiliyetu hupata mazoezi muhimu ambayo huboresha afya yetu. Vilevile, akili zetuhuchangamka kupitia burudani hasa baada ya kazi nyingi za siku au msiba.Uchangamfu huu huleta utulivu na liwazo katika akili zetu. Pia, hutuepushiahuzuni ambayo ni hatari kwa afya yetu.Burudani hudumisha utamaduni. Hapa, chukua mfano wa ngoma zetu maarufu.Unapata kuwa ngoma hizo zilichezwa enzi za kale. Kupitia nyimbo hizo, tunafahamuhali ya maisha katika enzi hizo za kale. Kwa hivyo, hii ni njia moja yakuhakikisha kuwa utamaduni wetu haupotelei mbali.Burudani pia ni chanzo cha ajira na pato. Watu wengi wameajiriwa kupitia burudanikama vile bendi, sarakasi, mchezo wa kuigiza na kadhalika. Burudani pia huwezakumletea mtu sifa nzuri. Kwa mfano, wapo waimbaji, waigizaji, wanasarakasina kadhalika ambao wanajulikana kote ulimwenguni na kupendwa na wengi.Maswali
1. Kwa maneno yako mwenyewe, eleza maana ya burudani.2. Je, ni jambo lipi unaloliona kuwa ni la muhimu zaidi kuhusu burudani? Kwa nini?3. Andika sifa ambazo zinafanya michezo na burudani kuwa sawa.4. Taja umuhimu wa burudani ambao haukutajwa kifunguni humu.Kazi ya wanafunzi wawili wawili
Jiunge na mwanafunzi mwenzako. Jadilianeni kuhusu umuhimu wa burudani kiafya na kiushirikianoiii) Rejesta ya hotelini
Hoteli ni nyumba ambamo vyakula na vinywaji huuzwa. Vyumba vya kulalia piahupatikana hotelini. Rejesta ya hoteli hutumika katika mazingira haya.Jiunge na mwenzako na msome kifungu kifuatacho.
NDOLI: Karibuni katika hoteli yetu! Jina langu ni Ndoli na mimi ndiye mhudumu.ITUZE: Asante sana kwa makaribisho yenu.GANZA: Tunashukuru. Mna nini leo?NDOLI: Tuna vyakula vingi kwenye ankra. Tuna tilapia, matoke, ugali, kisamvu na mizuzu.Pia tuna vinywaji vingi. Tuna uji, chai na kahawa.GANZA: Niletee matoke sahani moja.ITUZE: Mimi juisi ya baridi. Nitaitisha vingine baadaye.(Ndoli anaondoka na kurudi na vyakula vilivyoagizwa)NDOLI: Karibuni. Mjihisi nyumbani.GANZA: Asante. Nina swali kabla hujaenda. Sisi ni wageni hapa Kigali. Jioni tutahitaji mahali pa kulala.Je, tunaweza kupata vyumba vya kukaa?NDOLI: Bila shaka vyumba mtapata. Vyumba vyetu vyote ni vya hali ya juu kwa wageni kama nyinyi.Vyumba hivyo vina maji moto, televisheni nahuduma za bure za mtandao.Pia, tunawapa wageni wetu kiamsha kinywa, chamcha na chajio.GANZA: Mna huduma gani zaidi?NDOLI: Tuna mabwawa ambapo wageni wetu huogelea. Pia, tuna ukumbi wa mazoezi ya viungo.Mtakaa kwa muda gani?GANZA: Tutakaa kwa siku tatu. Tunahudhuria kongamano kuhusumbinu mpya za kilimo. Baadaye tutazuru mbuga ya wanyama ya Akagera.NDOLI: Karibuni tena.GANZA na ITUZE: Asante sana.Maswali
1. Eleza maana ya msamiati mbalimbali wa hoteli jinsi ulivyotumika kifunguni.2. Tunga sentensi sahihi ukitumia msamiati uliotaja hapo juu.3. Je, pana umuhimu gani kwa mhudumu kuonyesha adabu na heshimaanapozungumza na wateja katika hoteli?Kazi ya wanafunzi wawili wawili
Jiunge na mwanafunzi mwenzako. Fanyeni utafiti kuhusu lugha gani inayotumikakatika mazingira ya hoteli nchini Rwanda. Wasilisheni matokeo yenu mbele ya darasa.Sifa za rejesta ya hotelini
Rejesta ya hotelini huwa na sifa zifuatazo:i) Kuwepo kwa lugha ya vyakula mbalimbali,ii) Kupatikana kwa msamiati wa vinywaji vingi,iii) Wahudumu kuzungumza na wateja kwa unyenyekevu,iv) Kupatikana maneno ya huduma mbalimbali,v) Lugha ya mkato hutumika.Kazi ya kikundi
Jiunge na wanafunzi wenzako katika kikundi. Fanyeni maigizo ya mazungumzo yahotelini kati ya mhudumu na wateja. Zingatieni sifa mbalimbali za rejesta ya hoteli.iv) Rejesta ya mahakamani
Mahakamani au kortini ni mahali pa kusikilizwa na kuamuliwa mashtaka na kesi mbalimbali.Yeyote anayefanyiwa mabaya ana ruhusa ya kumshtaki mahakamani aliyemfanyia ubaya huo.Je, umewahi kuhudhuria vikao vya mahakama?Jiunge na mwanafunzi mwenzako. Tazameni mchoro uliopo hapa chini.Jadilianeni kuhusu watu waliopo kwenye mchoro na shughuli zinazoendelea.Linganisheni yaliyomo humo na yale mnayofahamu kuhusu mahakama.Soma kifungu kifuatacho na ujibu maswali chini yake.
Mahakamani sehemu I
KARANI: Shughuli za korti hii zimeanza. Hakimu Ganza ndiye mwamuzikatika kesi hii. Ketini tafadhali. (watu wanakaa)HAKIMU: Ninatangaza rasmi kusikilizwa kwa kesi ya Thierry Ngabo dhidi yaJane Usanase. Je, pande zote mko tayari?KIONGOZI WA MASHTAKA: Tayari kwa niaba ya upande wa mashtaka,Mheshimiwa.WAKILI: Tayari kwa niaba ya mshtakiwa, Mheshimiwa.HAKIMU: Thierry Ngabo?MSHTAKIWA: Naam, mheshimiwa. HAKIMU: Natumai unajua haki zako.Una haki ya kuwakilishwa na wakili mbele ya mahakama hii.Una haki ya kunyamaza kimya au kujibu mashtaka. Pia,una haki ya kukata rufaa ikiwa hutaridhika na uamuzi wa mahakama.Je, ni kweli kuwa unajua haki hizi?MSHTAKIWA: Naam.HAKIMU: Unashtakiwa kwa mashtaka mawili. Katika shtaka la kwanza,unashtakiwa kuwa mnamo usiku wa tarehe ishirini na tisa, mweziwa kumi na moja mwaka wa elfu mbili kumi na sita ulipatikanaukiendesha gari la kibinafsi lenye nambari ya usajili ASA000Rkatika barabara kuu ya kutoka Ngoma kuelekea Kirehe bila idhiniya mmiliki wa gari hilo. Gari hilo liliripotiwa kupotea mnamotarehe ishirini na nane, mwezi wa kumi na moja mwaka wa elfumbili kumi na sita. Katika shtaka la pili, unashtakiwa kwa kukwepavizuizi vya polisi na kutumia njia mbadala polisi walipojaribukukusimamisha. Unakubali au unakataa shtaka la kwanza?MSHTAKIWA: Ninakataa.HAKIMU: Unakubali au unakataa shtaka la pili?MSHTAKIWA: Ninakataa.HAKIMU: Upande wa mashtaka.KIONGOZI WA MASHTAKA: Asante Mheshimiwa. Nina ushahidi wa kutosha kuthibitishakuwa mshukiwa ana hatia kwa mashtaka mawili yaliyopo mbeleya mahakama. Mheshimiwa, ushahidi utaonyesha kuwa gariASA 000 R liliibwa mnano tarehe ishirini na nane, mweziwa kumi na moja mwaka wa elfu mbili kumi na sita, usiku. Sikumoja baadaye, mshukiwa alipatikana akiendesha gari hilo.Mheshimiwa, mshukiwa alishindwa kutoa idhini ya mwenyegari na stakabadhi za kumilikigari hili. Alama za vidole vya mshukiwa pia vilipatikana katika funguo bandia zilizotumikakatika wizi wa gari husika. Mheshimiwa, kwa mshukiwa kujaribukukwepavizuizi vya polisi ni ithibati tosha kuwa aliiba gari hili.(Wakili anaomba nafasi ya kuchangia. Hakimu anampa nafasi.)WAKILI: Mheshimiwa, ni haki kwa Kiongozi wa mashtaka kudai kuwamshukiwa ana hatia bila kuthibitisha?Mheshimiwa, kwa mujibu wa sheria kuhusu haki za mshtakiwa, mteja wangu hana hatihadi mahakama hii itakapoamua kesi yake hii. Wakati wa kesi hii, utajua ukweli wa mambo.Ngabo alikuwa akiendesha gari ambalo liliibwa na mtu mwingine. Ngabo alipogundua kuwagari limeibwa, alikuwa mbioni kurejesha gari hilo. Alikuwa amempigia polisi simu katika kituocha polisi mjini Kerehe kuwa gari analoendesha limeibwa. Hakuwa na nia ya kukwepa vizuizi vya polisi.Alikuwa na nia ya kukwepa mlolongo mrefu wa magari ili afike mjini Kerehe mapema iwezekanavyo.Mheshimiwa, mteja wangu ni mtu asiyekuwa na rekodi yoyoteya wizi.Ndio maana alipewa dhamana bila kuhitajika mdhamini.Kwa hivyo mteja wangu hana hatia.Msamiati
korti – mahali ambapo kesi na mashtaka mbalimbali husikilizwa na kuamuliwa.Pia huitwa mahakama.hakimu – mtaalamu wa sheria anayeajiriwa kusikiliza mashtaka kortini na kutoa maamuzikesi – mashtaka yanayosikilizwa mahakamanimshtakiwa – mtu anayefikishwa kortini kwa kudaiwa kufanya kosamheshimiwa – jina la heshima ambalo watu hutumia kortini kumrejelea hakimukukata rufaa – mshtakiwa kukataa hukumu aliyopewa kwa kuomba mahakamaya juu isikilize tena kesi yake au ipunguze adhabu aliyopewaunashtakiwa kwa mashtaka mawili – makosa mawili yameletwa mbele ya mahakama dhidi yako.ushahidi – thibitisho kuwa jambo fulani lilifanyika au halikufanyikaMaswali
1. Bainisha msamiati zaidi wa kimsingi katika rejesta ya mahakama katika kifungu ulichosoma.2. Eleza maana ya kila msamiati na utungie sentensi sahihi.Sifa za sajili ya mahakamani
Baadhi ya sifa zinazoweza kubainisha rejesta ya mahakamani ni:i) Matumizi ya lugha ya adabu,ii) Kuwepo tafsiri na fasiri ya yanayosemwa hasa ambapo mshtaki amamshtakiwa haijui lugha rasmi ya mahakamani,iii) Mawakili hutumia lugha iliyojaa msamiati wa sheria,iv) Kunukuliwa kwa vifungu mbalimbali vya katiba au sheria,v) Kukosekana kupinga uamuzi wa korti papo kwa papo bali kupinga huja baadaye,vi) Kuwepo msamiati wa Kilatini.Soma mazungumzo haya ya mahakamani na ujibu maswali.Mahakamani sehemu IIHAKIMU: Upande wa mashtaka, mna mashahidi?KIONGOZI WA MASHTAKA: Naam, Mheshimiwa.HAKIMU: Walete kizimbani.(Askari analeta shahidi wa kwanzaAnasimama kwenye kizimba.Karani wa korti anaelekea alipo shahidi akiwa na Biblia na Kurani.)KARANI: Unaitwa nani?SHAHIDI I: Jane Usanase.KARANI: Uko mbele ya mahakama. Mahakama inataka kujua ukweli.Usimwogope mshukiwa wala mtu yeyote. Ujikaze ili korti ijueukweli wa mambo. Utakula kiapo kwa Biblia au Kurani?SHAHIDI I: Biblia. (Jane anainua Biblia kwa mkono kwa kulia)KARANI: Uyarudie maneno haya kwa sauti. Mimi Jane Usanase.SHAHIDI I: Mimi Jane Usanase.KARANI: Ninaapa kwamba yale ambayo nitasema mbele ya korti hii ni ukweli.SHAHIDI I: Ninaapa kwamba yale ambayo nitasema mbele ya korti hii ni ukweli.KARANI: Ewe Mungu nisaidie.SHAHIDI I: Ewe Mungu nisaidie. (Karani anakaa. Kiongozi wa Mashtaka anaamkana kuelekea alipo shahidi.)KIONGOZI WA MASHTAKA: Unafanya kazi wapi?SHAHIDI I: Katika Halmashauri ya Wilaya ya Kerehe.KIONGOZI WA MASHTAKA: Unatumia mbinu gani za usafiri ukienda kazini?SHAHIDI I: Gari langu la kibinafsi.KIONGOZI WA MASHTAKA: Gari hilo lilikuwa wapi mnamo usiku wa tarehe 29/11/2016?SHAHIDI: Nilikuwa nimeliegesha mbele ya hoteli ya Starehe mjini Kirehe.KIONGOZI WA MASHTAKA: Nambari ya usajili wa gari hilo ni A...WAKILI: (Baada ya kumwomba Hakimu nafasi ya kuongea) Mheshimiwa,nihaki kwa kiongozi wa mashtaka kumwelekeza shahidi katika kutoaushahidi wake? Gari likiwa lake, mbona asiseme nambari yakeya usajili bila kuambiwa?HAKIMU: Kiongozi wa mashtaka, shahidi anajua nambari ya usajili wa gari lake.Mwache aitaje.Kazi ya kikundi
Jiunge na wanafunzi wenzako na mfanye mazoezi haya:i) Jadilianeni kuhusu sifa za rejesta ya mahakamani.Rejeleeni vifungu mlivyopewa na ikiwezekana msikilize rekodiza matukio mahakamani au kuhudhuria vikao vya mahakama.ii) Kamilisheni kesi iliyopo mahakamani kuanzia ilipofikia katika kifungu cha pili kwa kuigiza.v) Rejesta ya bungeni
Bunge ni baraza la taifa linalotunga sheria na lenye wajumbe waliochaguliwa nawananchi kwa kupigiwa kura ama kwa kuteuliwa na rais.Soma kifungu kifuatacho na ujibu maswali chini yake.KARERA: Jina langu ni Karera.RUSARO: Na mimi ninaitwa Rusaro.RURANGIRWA: Nami ninaitwa Rurangirwa.KARERA: Tupo hapa mbele yenu, wanadarasa wenzetu, kukuelezenimengi kuhusu bunge letu ama baraza letu la taifa. Mambo hayatumeyapata kupitia kwa utafiti wa kina ambao tumekuwa tukiufanya.RUSARO: Wabunge wetu huwawakilisha watu waliowachagua amavikundi fulanifulani vya raia wa jamhuri yetu.RURANGIRWA: Namo bungeni, yamo mambo mengi unayostahili kuyajua.Mathalan, mwenye mamlaka ya kuongoza, kuamuru au kuzuiashughuli bungeni ni spika ambaye husaidiwa na naibu wa spika.RUSARO: Spika ana mamlaka ya kuamua ni mbunge gani atazungumza,atazungumzaje na kwa muda gani na kadhalika. Hapana lolotelinaloweza kuendelea bungeni bila yeye kuliruhusu.KARERA: Hali kadhalika, yamo mambo mengi mengineyo yanayopatikana bungeni.Mambo hayo ni kama vile rais, makamuwa rais, sheria, kutunga sheria,hoja, upinzani, kura, uchaguzi, wakala, eneo la ubunge, piga kura,mjumbe mteule, mjumbe wakilishi na kadhalikaRUSARO: Tukianza na rais tunapata kuwa hakuna bunge bila kuwepo rais.Yeye huhitaji kutawala serikali na nchi nzima kwa mujibu wa sheria.RURANGIRWA: Nazo sheria hizo ni lazima zitungwe na bunge. Kwa hivyo,kila nchi huhitajika kutawaliwa na rais kwa sheria zilizotungwana bunge.Naye makamu wa rais ni yule anayemsaidia rais kutawala nchi.Lakini, je, sheria nazo ni nini?RUSARO: Sheria ni kanuni za kutawalia nchi na ambazo, kama ilivyotajwa awali,hutungwa na bunge. Wabunge huwasilisha hoja bungeni na zikajadiliwa.Baadhi yazo hupitishwa kuwa sheria baada ya kuidhinishwa na rais.Lakini zile hoja zinazopingwa na upinzani na kukataliwa haziwi sheria.Nazo zile anazozikataa rais hurudishwa bungeni ama kurekebishwaama kutupiliwa mbali.KARERA: Nao takriban wabunge wote hupigiwa kura ili kuingia bungeni.Wafikapo huko huwa ni mawakala wa wale waliowachagua kutokamaeneo yao ya bunge na huhitajika kufanya juu chini ili kuwainuliahali yao ya kimaisha.RURANGIRWA: Hata hivyo, huwepo wajumbe wateule ambao huteuliwa na raisili kuwakilisha sehemu fulani fulani. Kwa mfano, panaweza kuwepombuge mteule anayewawakilisha masilahi ya wanawake ama vijana.KARERA: Isitoshe, ipo kura ya kutokuwa na imani na mtu ama tume fulani.Inaweza kutokea kwamba kiongozi fulani anatuhumiwa kukosea.Basi, bunge linaweza kupitisha kura ya kutokuwa na imani naye na akafutwa kazi.Katika hali kama hii, mara nyingine huteuliwa tume ya kuchunguza ukweli wa tuhumakabla ya uamuzi kama huu kutolewa.Zoezi
Bainisha msamiati maalumu wa bungeni kutoka katika kifungu huku ukiutungia sentensi sahihi.Sifa za rejesta ya bungeni
Rejesta ya bungeni kama rejesta yoyote ile huwa na sifa zake. Ifuatayo ni orodha yabaadhi ya sifa hizo:i) Kumrejelea spika kila wakati kwa heshima,ii) Matumizi ya maneno yenye adabu,iii) Kutokuwepo ruhusa ya kumshtaki mzungumzaji kwa maneno aliyotamka,iv) Kuwepo kwa lugha ya kupiga kura kwa hoja fulani,v) Kuwepo kwa mtindo fulani wa kuandika ama kuwasilisha hoja,vi) Kuwepo kwa utaratibu wa kuzungumza,vii) Kurejelewa kwa vifungu vya sheria mbalimbali za bunge na katiba kila wakati,viii)Kutumika kwa lugha ya utafiti.Kazi ya wanafunzi wawili wawili
Sokoni ni mahali penye mkusanyiko wa watu wanaouza na kununua bidhaa mbalimbali.Wauzaji wengi huuza bidhaa zao kwa rejareja, kwenye kibanda au katika maduka.Baadhi ya masoko hutenga siku moja au mbili kama siku maalumu za soko kila wiki.Siku kama hiyo ya soko huitwa chete. Masoko mengine huendesha shughuli zake kilasiku. Bidhaa nyingi huuzwa sokoni.Soma kifungu hiki ili kujifunza mengi kuhusu rejesta ya sokoni.(Umuhire anaingia sokoni. Sauti za wauzaji mbalimbali zinasikika.)SAUTI: Mia bei! Mia bei...Karibu mteja..Ni za leo...ni za leo...bei rahisi...bei yajioni...bei ya hasara...karibu, chagua...chagua...beba nguo na hamsini...MWUZAJI: (Umuhire anaingia katika kioski kimoja.) Karibu mteja wangu! Beirahisi kwa bidhaa nzuri! Karibu katika kibanda changu! Karibuuchague bidhaa utakazo. Leo nina mboga safi safi, matundamatamu matamu na nyanya kubwa kubwa.UMUHIRE: Ahaa! Leo sina pesa ya matunda. Nitanunua siku nyingine.Una kitunguu?MWUZAJI: Siwezi kukosavitunguu, bi mdogo.Ndivyo hivi hapa.UMUHIRE: Je, kifungu kimoja nipesa ngapi?MWUZAJI: Hicho ni bei rahisi sana.Kila kifungu ni faranga kumi tu.Nikufungie ngapi?UMUHIRE: Aa! Hiyo ni bei ghali mno.Tafadhali, niuzie vifunguvitano kwa faranga arubaini.MWUZAJI: Hapo umenizamisha, bi mdogo.Sitapata faida yoyote. Bei ni hiyo tu.UMUHIRE: Wewe nawe!Faida utapata kwabidhaa nyingine.Hutaki nirudi tena?MWUZAJI: Ninataka urudi kila mara. Basi ongeza faranga tano nikufungie.UMUHIRE: Jamani! Unataka tule mboga bila chumvi?Hiyo faranga tano ni ya chumvi.MWUZAJI: (Anacheka) Nami hutaki nile chamcha?Hiyo faranga tano ni ya kujinunulia chakula.Unataka babu yako afe kwa njaa?UMUHIRE: Haya! Chukua faranga zako arubaini na tano.MWUZAJI: Asante bi mdogo. Chukua bidhaa zako.UMUHIRE: Asante.MWUZAJI: Karibu tena. Mbona hununui mboga pia?UMUHIRE: Mboga ninazo katika shamba langu nyumbani.MWUZAJI: Pongezi sana. Una aina gani ya mboga?UMUHIRE: Nina sukumawiki.MWUZAJI: Unaweza kuniuzia gunia moja la sukumawiki?UMUHIRE: Sawa. Nitakuletea siku ya Jumamosi. Nyama inauzwa wapi?MWUZAJI: Nyama inauzwa kwenye buchari. Buchari ipo nyuma ya kibanda hiki.UMUHIRE: Nimeshukuru.: Jamani! Unataka tule mboga bila chumvi? Hiyofaranga tano ni ya chumvi.MWUZAJI: (Anacheka) Nami hutaki nile chamcha? Hiyo faranga tano ni yakujinunulia chakula. Unataka babu yako afe kwa njaa?UMUHIRE: Haya! Chukua faranga zako arubaini na tano.MWUZAJI: Asante bi mdogo. Chukua bidhaa zako.UMUHIRE: Asante.MWUZAJI: Karibu tena. Mbona hununui mboga pia?UMUHIRE: Mboga ninazo katika shamba langu nyumbani.MWUZAJI: Pongezi sana. Una aina gani ya mboga?UMUHIRE: Nina sukumawiki.MWUZAJI: Unaweza kuniuzia gunia moja la sukumawiki?UMUHIRE: Sawa. Nitakuletea siku ya Jumamosi. Nyama inauzwa wapi?MWUZAJI: Nyama inauzwa kwenye buchari. Buchari ipo nyuma ya kibanda hiki.UMUHIRE: Nimeshukuru.Zoezi
1. Eleza maana ya maneno yaliyokolezewa wino katika kifungu.2. Tunga sentensi ukitumia msamiati ulioorodhesha hapo juu.Sifa za rejesta ya sokoni
Sifa zinazobainisha rejesta ya sokoni ni:i) Lugha ya kurudiarudia maneno hutumika huku bidhaa zikinadiwa,ii) Lugha ya kuwavutia wateja huweza kutumiwa,iii) Hutumika lugha isiyo rasmi na sarufi hukosa kufuatwa,iv) Kiimbo cha wauza bidhaa hutumika kama vile kuzungumza kwa upole kwawazee na kutumia lugha ya kusifu kwa wateja wanaonekana tajiri,v) Lugha ya kununua na kuuza hutumiwa kama vile: panda bei, shuka beiKazi ya wanafunzi wawili wawili
Jiunge na mwanafunzi mwenzako. Igizeni mazungumzo kati ya mwuzaji na mnunuzi.Zingatieni sifa za rejesta ya sokoni.vii) Rejesta ya kanisani
Kanisa ni jengo ama mahali panapotumiwa na Wakristo kufanyia ibada.Ama pia neno hili lina maana ya Jumuiya ya Wakristo.Kazi ya kikundi
Jiunge na wenzako watano na mjadili mambo mnayoyaona katika mchoro ufuatao.Sasa someni kifungu kifuatacho na halafu mjibu maswali yaliyoulizwa.Mambo yote yanayohusu kanisa na imani ya mtu ni mambo magumu sana maishani mwetu.Amri Kumi za Mungu pamoja na amri nyingine zozote zinazohusu dini ya kweli,huhitaji mwanadamu kukaa katika mema na haki mbele ya Mwenyezi Mungu.Hayo ndiyo masharti ya Neno ama Biblia. Mitume na malaika wa Munguwaliwajia mara kwa mara waumini walioamini katika dini kuwakumbusha haya.Nayo misahafu dini mbalimbali za haki huyasisitiza yaya haya.Sasa ugumu huja katika kuyatekeleza.Hata hivyo, kupo kutubu. Huku kutubu ni njia ya pekee ya kuondoa ugumu huo.Kila atendaye dhambi mbele ya Mola ana ruhusa ya kutubu. Makasisi, mapadri,wachungaji, maaskofu, maaskofu wakuu pamoja na viongozi wengine makanisaniwana jukumu la kuhakikisha kuwa waumini wao hutubu na kumrudia Manani.Nako kutubu huko kunaweza kufanywa wakati wa ibada wanapokuwa wanamwabuduMuumba ama wakati mwingine wowote. Kunaweza pia kufanywa kupitia kwa sala.katika haya yote, ni sharti ikumbukwe kwamba mwovu shetani hapumziki mpakaaone kuwa binadamu wengi ama wote wamo katika dhambi. Binadamu huyo akitubu,malaika mbinguni wanafurahi sana. Lakini shetani anatafuta njia nzurinzuri za kumfanya mwanadamu yuyo huyo arudi dhambini tena.Mbinu zake nyingi huwa za msingi wa raha. Anajua kuwa binadamu ni mpenda raha.Hata hivyo, lipo Neno linalovunjavunja juhudi kama hizo.Kanisa huhubiri habari za jahanamu, kuangamia motoni, kuingia mbinguni, njiapana, njia nyembambana, msalaba wa Yesu, Mwokozi Yesu, Utatu wa Uungu, nahata siku ya kiama. Jahanamu ama ahera ni pahali ambapo inaaminika roho za walewaliokufa huenda kungoja siku ya kiama ambayo itakuwa siku ya kutolewahukumu na Mungu Muumba. Swali kuu siku hiyo litakuwa, Umefanya nini na Neno langu?Wale ambao hawatajibu vilivyo watatupwa motoni na wale ambao watajibu vilivyo wataingia mbinguni.Jambo jingine kanisani ni msalaba. Yesu Kristo alisulubishwa kwenye msalabaili amfie mwanadamu apate kuokolewa na damu yake. Kwa hiyo, msalaba niukumbusho kwamba tayari mwanadamu ameokolewa na analohitaji kufanya ni kuungama dhambi zake.Jambo jingine ni kwamba maeneo mbalimbali ya kuabudia huwa na manenowanayochukulia kuwa yanawawezesha kuwasiliana vilivyo na Mungu.Maeneo hayo ni kama vile kanisani, msikitini, hekaluni na kwingineko kukiwa pamoja na barabarani.Zoezi
Jiunge na mwenzako. Jadilianeni maana ya maneno yaliyokolezewa wino namsamiati zaidi unaotumiwa kanisani na msikitini.Sifa za rejesta ya kanisani
Baadhi ya sifa za rejesta ya kanisani ni kama vile:i) Huwepo na pahali pa kumwabudia Mungu,ii) Katika baadhi ya dini, hutumika msamiati wa wale walioileta dini k.v. Kiingereza,iii) Huwezekana kuwepo mkalimani wa kutafsiri na kufasiri,iv) Baadhi ya wahubiri huanza kuzungumza kwa kasi wanapopandwa na jadhba,v) Sadaka hupewa majina mbalimbali na huwa ni sharti zitolewe,vi) Waumini hawana ruhusa ya kuulizia wasilolielewa wakati mhubiri anapokuwa anahubiri,vii) Ni sharti msamiati wa kidini utumiwe badala ya ule wa lugha ya kawaida,viii)Huwepo kwaya ama mwimbaji, ix) Vifungu mbalimbali vya Biblia hunukuliwa.viii) Rejesta ya sarufi ya Kiswahili
Sarufi ni kanuni za lugha zitumiwazo ili kupata ufasaha katika lugha. Kila lughahuwa na sarufi yake. Hivyo basi, ipo sarufi ya Kiswahili ambayo ina rejesta yake.Someni kifungu kifuatacho ili kujifunza maneno zaidi ya sajili hii ya lugha.Fikiria ingekuwaje kama hatungekuwa na lugha? Hata ishara mbalimbali zina msingi wa lugha.Ama kwa kweli, mambo mengi yangalikwama kama hapangekuwa na lugha.Rejesta ya lugha ni muhimu kama lugha ilivyo kwa kuwa mambo hayo mawilini jambo moja tu. Katika rejesta ya sarufi mna maneno kama vile sajili, sarufi,Kiswahili, sentensi, lafudhi, alfabeti, vitenzi, mnyambuliko, maandishi, majina,namna za majina, vivumishi, vielezi, viwakilishi, viunganishi, vihusishi, vihisishi,aya, kuakifisha na kadhalika.Ukija kuangalia maana ya maneno haya, unapata kuwa sajili ni rejesta kamailivyoelezwa hapo awali lakini sarufi ni sheria ziongozazo lugha fulani. NachoKiswahili ni lugha izungumzwayo na Waswahili lakini sentensi ni tungoijitoshelezayo na ambayo huhusisha mtendaji na kitendo. Nayo lafudhi au lafidhini namna maneno yanavyotamkwa ilhali alfabeti ni herufi za lugha ambazozimepangwa kwa utaratibu maalumu.Navyo vitenzi ni maneno yakuambiayo cha kufanya na mnyambuliko ni namnavitenzi hivyo hujigeuzageuza ili kuleta maana ihitajikanayo. Maandishi nayo nikuwakilisha sauti kwenye karatasi kwa kutumia kalamu ilhali majina ni neno lakumtaja mtu, kitu au jambo.Namna za majina ni vikundi vya majina yanayochukua sifa fulani inayoyasawazisha.Vivumishi ni maneno yaongezeayo majina maana na pia kujiongezea maana.Vielezi navyoni maneno yaongezeayo vitenzi maana ilhali viwakilishi ni maneno ama viungo vya maneno vinavyosimamia majina.itoshe, kuna viunganishi, vihusishi, vihisishi, aya, na kuakifisha. Viunganishi nimaneno yanayounganisha maneno mengine lakini vihusishi huhusisha watu amavitu na mahali. Navyo vihisishi ni maneno yanayoonyesha mahangaiko ya moyoilhali aya ni fungu la sentensi lililo na maana kamilifu, yaani paragrafu. Nakokuakifisha ni kuwakilisha sauti kimaandishi. Ufahamu ni pale ambapo mtu husomakifungu na halafu akapima ama akapimwa ufahamu wake kuhusu hayo aliyoyasoma.Imla nayo ni pale ambapo unasomewa maneno ama kifungu huku ukiandika.Zoezi
Jiunge na wenzako watatu na mjadili maana na matumizi ya maneno haya yafuatayo:1. mtungo au insha 2. msamiati 3. rejesta4. vitendawili 5. methali 6. misemo7. nahau 8. mafumbo 9. barua10. masimulizi 11. dhahania 12. istilahi13. kiimboSifa za rejesta ya sarufi ya Kiswahil
Nazo sifa za rejesta ya sarufi ya Kiswahili zinaweza kuwa hivi:i) Imejaa maneno ya kitaalamu,ii) Hufundisha jinsi ya kutunga tungo sahihi,iii) Huwa na semi za kutia hekima,iv) Huwa ndio msingi wa maongezi yote katika lugha husika,viii)Huwezesha kuhifadhi mila za kabila husika,ix) Huwa na tamathali za usemi za kuungia usemiZoezi la ziada
Kazi ya wanafunzi wawili wawili
Jiunge na mwanafunzi mwenzako na mjibu maswali yaliyopo hapa chini.Jazeni jedwali hili. Sehemu ya kwanza imejazwa kama mfanoB . Matumizi ya majina ya ngeli ya KI-VI katika umoja na wingi
Ngeli ya KI-VI hujumuisha majina mbalimbali. Majina yote katika ngeli hii huchukuaupatanisho wa sarufi, ki- katika umoja na vi- katika wingi. Hii ndiyo sababu ya ngelihii kuitwa ngeli ya KI-VI. Maumbo ya majina katika ngeli ya KI-VI hubadilika kutoka umoja hadi wingi.Je, unakumbuka majina yanayopatikana katika ngeli hii? Yataje matano katikaumoja pamoja na wingi wayo.Tazama jedwali hili. Je, ni mabadiliko gani yanayotokea katika majina yanapotoka umoja hadi wingi?Yapo makundi mbalimbali ya majina yanayopatikana katika ngeli ya KI-VI.i) Majina yanayoanza kwa ki- katika umoja na kuchukua vi- katika wingiKundi hili la majina ndilo huwa na majina mengi ya ngeli hii ya KI-VI.Kumbuka
Majina ya viumbe wenye uhai ambayo huanza kwa kiambishi ki- katika umoja na vi- katikawingi hayawekwi hapa bali huchukua viambishi ngeli vya ngeli ya A-WAZoezi
Andika majina kumi zaidi ya ngeli ya Ki-Vi pamoja na wingi wayo.ii) Majina yanayoanza kwa ch- katika umoja na kuchukua vy- katika wingiKumbuka
Majina ya viumbe wenye uhai ambayo huanza kwa kiambishi ch- katika umoja navy- katika wingi hayawekwi hapa bali huchukua viambishi ngeli vya ngeli ya A-WA.Zoezi
Andika majina kumi zaidi yanayopatikana chini ya orodha hii ya majina katika ngeli ya KI-VI.iii) Majina kutokana na vitenzi
Yapo baadhi ya majina ambayo huundwa kutokana na vitenzi. Majina hayo pia hupatikana katika ngeli ya KI-VI.MfanoZoezi
Andika majina kumi zaidi yaliyomo katika kundi hili.iv) Majina yanayoanza kwa ki- lakini hayachukui wingi
Yapo majina katika Kiswahili ambayo huanza kwa kiambishi ki- lakini hayana wingi.Majina haya huwa ya viumbe wasiokuwa na uhai.Zoezi
Andika majina matano zaidi yanayopatikana katika kikundi hiki.v) Majina ya vitu katika hali ya udogo
Katika Kiswahili, majina yanaweza kuwa katika hali ya wastani, udogo au ukubwa.Majina yote yanapoandikwa katika hali ya udogo, huwekwa katika ngeli ya KI-VIiwe majina ya viumbe wenye uhai au vitu visivyokuwa na uhai.Katika mfano uliotolewa hapo juu, mtu na mtoto ni viumbe wenye uhai.Majina haya hupatikana katika ngeli ya A-WA. Unaposema kijitu au kitoto,unarejelea mtu mdogo zaidi ya kawaida. Kwa hivyo, majina kitoto na kijitu yanawekwa katikangeli ya KI-VI. Katika wingi huwa tunasema vitoto au vijitu. Vilevile, nyumba ipo katika ngeli ya I-ZI.Hata hivyo, kijumba (nyumba ndogo kupita kiasi) hupatikana katika ngeli ya KI-VI.Tazama mifano zaidi katika jedwali hapa chini.Zoezi
Andika majina matano zaidi yanayopatikana katika orodha hii ya majina katika ngeli ya KI-VI.Matumizi ya majina ya ngeli ya KI-VI
Kama ilivyoelezwa hapo mwanzoni, vitenzi vinavyoambatana na majina katikangeli hii ya KI-VI huchukua kiambishi ki- katika umoja na vi- katika wingi.Tazama mifano iliyotolewa katika jedwali lifuatalo:Zoezi
1. Eleza maana ya ngeli ya KI-VI.2. Eleza mabadiliko yanayotokea katika wingi ukirejelea majina haya ya ngeli ya KI-VI.i) chombo ii) kioo iii) kiti iii) cheo3. Kamilisha sentensi zifuatazo:i) ___akula ___livyonunuliwa ___meliwa.ii) ___dege ___mekamatwa.iii) ___beti ___mejaa faranga.iv) ___sima vya maji ___nachimbwa hivi sasa.v) Niliwaambia waniletee ___uma ___livyokunjwa.vi) Nitasoma kwa bidii ili niingie katika __uo _kuu.4. Bainisha sentensi sahihi kutoka kwa zile zisizokuwa sahihi na uzisahihishe.Nambari za kwanza mbili zimetolewa kama mfano.i) Kiti hiki kinapendeza. SAHIHIii) Choo vimebomolewa. SI SAHIHI. Vyoo vimebomolewa. SAHIHIiii) Viswahili kinazungumzwa Afrika Mashariki.iv) Kioo kinanipendeza.v) Kitoto anaruka.vi) Kijiti limevunjika.vii) Vyuo vikuu vinatoa elimu ya juu.viii)Vyuma kinachomwa.ix) Kigelegele kinasikika.Kazi ya wanafunzi wawili wawili
Jiunge na mwanafunzi mwenzako. Tungeni sentensi sahihi katika umoja na wingimkitumia majina ya ngeli hii ya KI-VI.Matumizi ya majina ya ngeli ya KI-VI pamoja na vivumishi
Je, unakumbuka vivumishi ulivyosoma katika sura ya kwanza? Rejelea vivumishi hivyo.a) Majina ya ngeli ya KI-VI pamoja na vivumishi vya sifa
Vivumishi vya sifa ni maneno yatajayo tabia au sifa za mtu, kitu au jambo.Mifano katika sentensi:Zoezi
Tunga sentensi zozote kumi ukitumia majina ya ngeli ya KI-VI na vivumishi mbalimbali vya sifa.b) Majina ya ngeli ya KI-VI pamoja na vivumishi vya pekee
Vivumishi vya pekee hutoa habari kuhusu nomino au kiwakilishi chake kwa njia ya kipekee.Huwa vitano.i) -enye ii) -enyewe iii) -ote iv) -o-ote v) -ingineMajina katika ngeli ya KI-VI huchukua kiambishi ch- katika umoja na vy- katika wingi yanapotumika pamoja navivumishi vya pekee vyote isipokuwa -ingine au -ingineo.Hata hivyo, kivumishi cha pekee -ingine na -ingineo huchukua viambishi ki- katika umoja na vi- katika wingi kinapotumika na majina ya ngeli ya KI-VI.Zoezi
Tunga sentensi zozote kumi ukitumia majina ya ngeli ya Ki-Vi pamoja na vivumishi mbalimbali vya pekee.c) Majina ya ngeli ya KI-VI pamoja na vivumishi vionyeshi
Vivumishi vionyeshi au viashiria ni maneno ya kuonyesha alipo mtu au kitu, yaani ujirani.Kuonyesha huko kunaweza kuwa kwa ujirani wa karibu – hapa,ujirani wa mbali kidogo – hapo, na ujirani wa mbali – pale.Katika ngeli ya KI-VI, kivumishi kionyeshi cha karibu huwa: hiki (umoja) na hivi (wingi),kionyeshi cha mbali kidogo huwa hicho (umoja) na hivyo (wingi) na kionyeshi cha mbali huwakile (umoja) na vile (wingi).Mfano katika sentensi:
Zoezi
Tunga sentensi zozote sita ukitumia majina ya Ki-Vi pamoja na vivumishi vionyeshi mbalimbali.d) Majina ya ngeli ya KI-VI pamoja na vivumishi vya idadi
Vivumishi vya idadi ni maneno yanayoonyesha idadi ya watu ama vitu. Vipo vivumishi vya idadi kamili,vivumishi vya idadi ya jumla na vivumishi vya idadi ya matokeo.Majina ya ngeli ya KI-VI huchukua viambishi ki- katika umoja na vi- katika wingiyanapotumika pamoja na vivumishi vya idadi vinavyochukua viambishi.Kumbuka
Idadi sita, saba, tisa na kumi hazichukui kiambishi chochote cha ngeli.Zoezi
Tunga sentensi zozote kumi ukitumia majina katika ngeli ya KI-VI na vivumishi mbalimbali vya idadi.e) Majina ya ngeli ya KI-VI pamoja na vivumishi viulizi
Hili ni kundi la vivumishi ambalo lina maneno yatumiwayo kuulizia maswali.Baadhi ya mifano ya vivumishi viulizi ni: -pi?, na -ngapi?Majina katika ngeli ya KI-VI huchukua kiambishi ki- katika umoja na vi- katika wingi yanapotumiwa pamoja na viulizi.Kumbuka
Kiulizi -ngapi hutumika katika wingi pekee.Kiulizi gani? hakichukui kiambishi.Tunasema: Kijiko gani? au vijiko gani?Zoezi
Tunga sentensi zozote tano ukitumia majina ya ngeli ya KI-VI na vivumishi viulizi mbalimbali.f) Majina ya ngeli ya KI-VI pamoja na vivumishi vimilikishi
Maneno katika kundi hili la vivumishi hujibu swali mtu, kitu au jambo ni la nani?Maneno haya huwa sita pekee katika Kiswahili.-angu -etu-ako -enu-ake -aoKatika ngeli ya KI-VI, kiambishi ch- hutumika katika umoja na vy- katika wingi.Zoezi
Tunga sentensi zozote sita ukitumia majina katika ngeli ya KI-VI na vivumishi mbalimbali vya kumiliki.Maswali ya marudio
1. Kwa maneno yako mwenyewe, eleza maana ya rejesta za lugha.2. Jaza jedwali hii kwa kuandika mifano kumi ya msamiati unaotumika katika kila rejesta iliyotajwa.3. Eleza sifa za rejesta zifuatazo:a) Michezob) Burudanic) Hotelinid) Sokoni4. Pana tofauti gani kati ya rejesta ya burudani na ile ya michezo?5. Rejesta ya hotelini ni sawa kabisa na ile ya sokoni. Je, haya ni kweli? Kwa nini?6. a) Bainisha aina mbalimbali za michezo katika jamii.b) Eleza umuhimu wa michezo katika afya ya binadamu.7. a) Taja namna mbalimbali za burudani katika jamii.b) Eleza umuhimu wa burudani kiafya na kiushirikiano.8. Eleza umuhimu wa kuonyesha adabu na heshima kwa watu katika mazingira mbalimbali.9. Bainisha rejesta zifuatazo na utaje sifa zao za kimsingi:a) Mheshimiwa spika, sheria hii imekiuka katiba ya nchi yetu. Mheshimiwa spika,ikiwa sheria hii itapitishwa jinsi ilivyo, patatokea migogoro.b) Bei rahisi...bei imeshuka...njoo mteja..karibu..usitembee kwa miguumitupu....nunua viatu kabla bei kupanda...c) Maandiko yanasema kuwa wenye dhambi watachomwa motoni.10. Linganisha na utofautishe rejesta ya bungeni na mahakamani.11. Rejesta ya hospitalini inaweza kufaa sana katika mazingira ya jikoni.Hili ni sawa? Kwa nini?12. Taja maneno sita ya rejesta ya utamaduni.13. Huku ukitoa mifano, eleza rejesta ya sarufi.14. Tunga sentensi sahihi ukitumia msamiati ufuatao:a) mwana mpotevub) barakac) mpira umekuwa mwingid) densie) bei ghalif ) ankrag) kukata rufaa15. Andika maneno haya katika wingi:a) chombob) kitic) kiood) choo16. Eleza muundo wa nomino za ngeli ya Ki-Vi katika umoja na wingi.17. Tunga sentensi tano tano ukitumia majina ya ngeli ya Ki-Vi na vivumishivilivyotolewa hapa chini katika umoja na wingi.a) vivumishi vya sifab) vivumishi vionyeshic) vivumishi viulizid) vivumishi vimilikishi18. Sahihisha makosa katika sentensi hizi:a) Kijiko vyangu kimenunuliwa.b) Vioo vikumi vitaletwa kesho.c) Niletee kitabu hivyo.d) Vyumba chote vimefagiliwa.19. Tunga sentensi sahihi ukitumia vivumishi vilivyotolewa.a) vyetub) vinanec) kiled) kipie) vyenyewe20. Eleza jinsi utakavyotumia ujuzi uliopata katika sura hii.Sura 4: Mazungumzo na mawasiliano katika shughuli mbalimbali za kijamii
Mada ndogo: Msamiati katika kazi za jumuiya
A . Shughuli mbalimbali za jumuiya
i) Mkutano wa kijiji chetu
Kijiji ni mgao wa chini zaidi katika migao ya utawala. Kijiji aghalabu hujumuishawatu wanaotoka koo mbalimbali na ambao wanajuana. Watu hawa huja pamojakufanya shughuli mbalimbali. Mikutano mbalimbali ya vijijini huweza kutumiwakuinua hali ya maisha ya jamii ya vijiji hivyo.Kazi ya wanafunzi wawili wawili
Je, kijiji chenu kinaitwaje? Je, umewahi kuhudhuria mkutano wa kijiji chenu? Jiungena mwanafunzi mwenzako na mjadilianeni shughuli mbalimbali ambazo hufanyikakatika mikutano vijijini mwenu.Sasa tazameni michoro iliyopo hapa chini na msome kifungu cha habari.Mimi ni Munyana. Leo ni siku ya mkutano wa kijiji hiki chetu. Mwenyekiti wakijiji chetu anamwomba Nziza kufunguamkutano kwa maombi. Wanakijiji wotewanasimama na kuomba kisha wanakaa.“Asanteni sana kwa kuitikia mwaliko wamkutano wetu. Shughuli yetu kuu sikuya leo ni kujadiliana kuhusu ugonjwawa UKIMWI. Patakuwepo upimajiwa UKIMWI ndani ya hema. Upimajiutakuwa kwa hiari yako. Kwa sasa,ninamwalika mgeni wa heshima katikamkutano wetu huu wa leo atuhutubie.Mgeni huyo ni afisa wa afya kutokaWizara ya Afya, Bi. Abigael Uwera.Tumkaribishe kwa makofi na vigelegele.”Watu wote wanasimama na kupigamakofi.“Mabibi na mabwana, UKIMWI ni ugonjwa usiojua umri, utajiri wala umaskini. Uwetajiri au maskini unaweza kuupata. Unamshika yeyote anayeshiriki ngono hasabila kutumia kinga. Pia, unaweza kuambukizwa ikiwa damu yenye maradhi hayaimechanganyika na damu yako. Damu hizi zinaweza kuchanganyika kwa kutumiasindano au wembe mmoja au kugusa damu ya mtu aliyeambukizwa. Tukumbukekuwa huwezi kupata UKIMWI kwa kumsalimia au kumkumbatia au kula pamoja namtu aliyeambukizwa.”Watu wanatazamana na kunong’onezana. Ninainua mkono na kumwuliza mgeniwa heshima ikiwa ugonjwa huu una tiba.“La hasha! Ugonjwa huu hauna tiba. Hata hivyo, zipo dawa nzuri za kupunguzamakali yake. Unapougua UKIMWI, ni sharti utumie dawa hizi tena kwa wakatiuliopendekezwa bila kukosa. Ni vizuri sote tujue kuwa miili yetu ina chembechembekatika damu zetu ambazo hutukinga dhidi ya magonjwa. UKIMWI hudhoofishachembechembe hizi. Miili yetu hukosa uwezo wa kupiga vita dhidi ya magonjwa.Hivyo, waathiriwa huweza kuuliwa na magonjwa kama vile malaria, kifua kikuu namagonjwa mengineyo.”Bi. Mutesi anainua mkono. Anapewa nafasi ya kuongea.“Mimi ni mwathiriwa wa ugonjwa huu wa UKIMWI. Bwanangu aliaga dunia kutokanana ugonjwa huu. Wanangu wawili pia wanaugua ugonjwa huu. Sote tumekubalihali zetu. Tunatumia dawa za kupunguzia makali. Tunakula vizuri na kuendelea nashughuli zetu za kila siku. Ningependa kuwaambia wenzangu ambao wanauguaugonjwa huu wasiogope. Ninawashukuru sana wanakijiji hiki kwa kunionyeshamapenzi na kunisaidia kukubali hali yangu. Kwa wale ambao hawana UKIMWI,nawasihi mwepuke ngono nje ya ndoa. Wasichana kwa wavulana, jiepusheni nangono hadi mfunge ndoa. Asanteni.”Tunampigia Bi. Mutesi makofi. Wengine wanasimama na kumkumbatia. Anaonekanamwenye afya nzuri. Kumbe mtu anayeugua UKIMWI huwa na afya nzuri! Huwezikujua anayeugua ugonjwa huu kwa kumtazama. Njia ya kipekee ni kupitia upimaji.Ninasimama na kuwahutubia wanakijiji.“Mimi nipo tayari kupimwa. Baada ya kupimwa, nitakubali hali yangu. Ikiwasina, nitajilinda. Baada ya kumaliza masomo na kuanza kufanya kazi, nitakubalikuchumbiwa. Nitamwambia mpenzi wangu tujipime ili tuwe na uhakika wa halizetu. Nitakuwa mwaminifu kwake. Nipo tayari kushirikiana na wanakijiji wenzanguili tuwapende na kuwasaidia waathiriwa wa UKIMWI. Pia, nipo tayari kujiunga nawanakiji kufanya kampeni ya kuwahamasisha wenzetu wajue kuhusu UKIMWI nawaepuke kuambukizwa ugonjwa huu. Asanteni.”Wanakijiji wote wanasimama. Wanasema kwa pamoja kuwa wako tayari kujua nakukubali hali zao za UKIMWI.“Haya, twende tukajipime wenzangu,” anasema Kiongozi wa kijiji. Watu wotewanapiga foleni nyuma yake.Maswali
1. Bainisha msamiati wa kimsingi kifunguni kuhusu shughuli katika mkutano nauutolee maana.Mfano: kufungua mkutano: kutangaza rasmi kuwa mkutano umeanza.2. Ni nini kilichokuwa kiini cha mkutano uliopo kifunguni?3. Nani alikuwa mgeni rasmi katika mkutano wa kijiji?4. Eleza mambo muhimu yanayojitokeza katika kifungu hiki.5. Toa muhtasari wa kifungu cha habari ulichosoma hapo juu katika aya moja.Kazi ya kikundi
Jiunge na wenzako katika kikundi. Nyinyi ni wanachama wa kijiji kimoja. Mmeandaamkutano. Jadilianeni kuhusu mambo mbalimbali mtakayofanya ili kuangamizaumaskini katika kijiji chenu.ii) Sherehe ya harusi ya rafiki yangu
Kazi ya wanafunzi wawili wawili
Jiunge na mwanafunzi mwenzako. Jadilianeni kuhusu mambo muhimu ambayo
hufanyika katika sherehe ya harusi. Kwa mfano:
1. Watu huja pamoja kutengeneza hema la wageni.
2. Maarusi huimbiwa na kuchezewa.
Baada ya kujadiliana mambo muhimu katika harusi, simulianeni kuhusu sherehe ya harusi mliyohudhuria.
Tazama michoro hii. Je, mambo gani yanafanyika?
Someni mazungumzo haya na mjibu maswali chini yake.
SHEMA: Hujambo mwenzangu?
TONA: Sijambo, ulikuwa wapi wiki nzima?
SHEMA: Nilihudhuria harusi ya rafiki yangu.
TONA: Kumbe! Ndiyo sababu una furaha tele.
SHEMA: Mbona nisiwe na furaha? Ndoa ni jambo linalowafurahisha watu wengi. Kutajwa tu kwa neno hili hufanya roho za kila mtu kusisimka kwa furaha.
TONA: Haya! Hata mimi ipo siku nilikuwa mpambe nilipokuwa mdogo. Bibi. harusi alivaa mavazi yake maalumu ya kupendeza kweli. Sisi wapambepia tulinunuliwa viatu na nguo za kupendeza. Sisi na bibi harusitulipambwa tukapambika. Nieleze kuhusu harusi hiyo uliyohudhuria.
SHEMA: Sikujua kuwa Ganza angeweza kumchumbia msichana mrembo kamayule. Aliponiambia eti posa yake imekubalika nilidhani ananitania.Aliniandikia barua kunieleza eti amepeleka mahari. Bado sikuamini hadi aliponitumia kadi ya kunialika harusini.
TONA: Ehe...
SHEMA: Mimi nilifika mapema na wenzangu kumsaidia rafiki yangu.Tulitengeneza mahema na kupanga viti hemani. Wengine walirembeshamahema kwa maua, baluni, na mapambo yenye rangi mbalimbali. Mahema yale yalivutia kwelikweli. Wengine walikuwa jikoni wakiandaa vyakula nao wengine walipokea wageni ambao walianza kuwasilimapema. Tukakodisha magari ambayo yangemsafirisha bwana na bibiharusi. Tukahakikisha kuwa vyombo vya burudani vipo katika hali sawatayari kuwatumbuiza wageni.
TONA: Ahaa! Bibi harusi alikuwa wapi wakati huu wote?
SHEMA: Ah! Kwani hujui? Bibi harusi alikuwa mahali kusikojulikana. Huko alikuwa na wapambe ambao walikuwa wakimrembesha.
TONA: Ehe...
SHEMA: Baada ya maandalizi, nikajiunga na wanaume ambao huandamana nabwana harusi. Pale, tulipewa mafunzo ya jinsi ya kutembea nakumsindikiza bwana harusi. Tukapima suti zetu nyeusi na kujaribu kutembea kwa viatu vyetu vipya. Bwana harusi naye akajaribu kuvaa pete ili ahakikishe kuwa inamtosha. Kila kitu kikawa shwari.
TONA: Nieleze mambo yaliyojiri siku ya harusi.
SHEMA: Harusi hiyo ilianza kwa watu kukaa kanisani kwa matarajio makubwahuku wakinong’onezana. Mara mfawidhi akatangaza kuwa tusimamekwa kuwa bibi harusi sasa anaingizwa kanisani. Bibi harusi akasindikizwa kanisani na babake na kupelekwa pale mbele alipokuwa akisubiriwa na mchumba wake pamoja na mchungaji. Hapo, waliapishwa na halafu kuvishana pete na mwishowe kutangazwa bibi na bwana. Wacha sasasherehe kamili zianze. Waliokula walikula na waliokunywa walikunywa.Nao waliocheza walicheza na waliofanya urafiki kwa matarajio yakufanya ndoa kama hiyo walifanya.
TONA: Ama kwa kweli harusi hiyo ilifana kweli! Asante.
SHEMA: Karibu.
Maswali
1. Kwa nini ndoa ni jambo la kufurahisha?
2. Eleza maana ya msamiati uliowekewa wino nzito.
3. Tunga sentensi sahihi ukitumia msamiati ulioeleza hapo juu.
4. Eleza mambo muhimu yanayofanyika harusini kwa mujibu wa kifungu hiki.
5. Eleza umuhimu wa ushirikiano katika jamii kwa kurejelea matukio kifunguni.
6. Toa muhtasari wa kifungu hiki cha habari katika aya moja.
iii) Mazishi
Mazishi ama maziko ni shughuli za kuzika mfu au wafu. Mfu ni mtu aliyeaga dunia. Shughuli hizi huendeshwa kutegemea utamaduni na imani za kidini za wahusika au waathiriwa.
Kazi ya wanafunzi wawili wawili
Jiunge na mwanafunzi mwenzako. Tazameni mchoro ulio kwenye ukurasa ufuatao. Je, ni shughuli gani inayofanywa? Jadilianeni kuhusu shughuli ambazo hufanywa wakati wa mazishi katika jamii yenu.Soma kifungu kilichopo hapa chini na ujibu maswali chini yake.
Sikujua kuwa sigara huua hadi nilipompoteza mjomba wangu mwaka jana. Mjomba aliaga dunia kutokana na ugonjwa wa saratani ya mapafu. Alipenda sana kuvuta sigara. Aliaga dunia katika hospitali moja jijini Kigali. Punde tu alipofariki, mwili wa mjomba ulipelekwa katika mochari. Huko, mwili wake ulisafishwa na wahudumu wa mochari na kuwekwa katika jokofu.
Jamaa na marafiki walikuja pamoja kumpa mjomba heshima zake za mwisho. Wanakijiji na watu kutoka mbali walishiriki katika shughuli mbalimbali kufanikisha mazishi ya mjomba.
Wanakijiji walichanga pesa za kulipia gharama za mochari na shughuli nyinginezo. Wengine walijitolea kutengeneza jeneza zuri la kumzikia mjomba. Wengine walinunua sanda. Wengine walichimba kaburi. Kila mtu alishiriki katika shughuli hizi kadiri ya uwezo wake.
Mwili wa mjomba uliondolewa kwenye mochari baada ya wiki moja. Mwili huo ulisafirishwa hadi kanisani. Alifanyiwa ibada ya wafu. Jamaa na marafiki walifika kanisani kushiriki katika ibada hiyo.
Baada ya maombi, watu walipewa ruhusa ya kutazama mwili wa mjomba. Hali ya huzuni ilitanda kanisani.Baada ya ibada, mwili huo ulisafirishwa nyumbani kwake. Mimi na jamaa za mjomba tulihuzunika. Wanakijiji na marafiki zetu walitufariji.
Siku ya mazishi ilipofika, ibada ya wafu iliandaliwa. Mchungaji aliendesha shughuli akishirikiana na familia ya marehemu mjomba. Mchango wa kusaidia familia ya marehemu mjomba pia ulifanywa. Wanakijiji na wageni walitoa michango yao. Hatimaye wakati wa kuteremshwa kwa jeneza kaburini ulifika. Baada ya maombi mafupi kando ya kaburi, jeneza lilitiwa ndani ya kaburi. Mchungaji alituhutubia.
“Tunasikitika kuwa marehemu aliaga dunia kutokana na uvutaji wa sigara. Nawasihi vijana kwa wazee mwepuke uraibu wa sigara na dawa za kulevya. Tumempoteza mwenzetu aliyekuwa na bidii ya mchwa. Tuige tabia zake nzuri na kuepuka zile mbaya. Ikiwa pana mtu ambaye mfu huyu alikuwa na deni lake, aseme sasa.”
Hakuna aliyeinua mkono. Mhubiri alifanya ombi la mwisho kisha shughuli za kufunika kaburi zikaanza. Familia ya mjomba ilikuwa ya kwanza kuweka mchanga kwenye kaburi. Baadaye, wanakijiji walisaidia katika kufunika kaburi.
“Asanteni kwa kushiriki katika mazishi haya. Tunamwomba Mungu amlaze mahali pema peponi,” mhubiri alisema kisha watu wakaondoka.
Wageni kutoka mbali walipewa vyakula na vinywaji. Baadaye waliondoka kwenda zao.
Maswali
1. Kwa maneno yako mwenyewe, eleza maana ya mazishi.
2. Bainisha na utoe maana ya msamiati mbalimbali kuhusu mazishi kifunguni.
3. Tunga sentensi ukitumia msamiati uliotajwa hapo juu.
4. Eleza shughuli muhimu za mazishi zilizotajwa kifunguni.
5. Kwa maneno yako mwenyewe, eleza mambo muhimu kifunguni katika aya moja.
Kazi ya kikundi
Jiunge na wanafunzi wenzako. Jadilianeni kuhusu utaratibu wa mazishi ya kienyeji katika sehemu mtokako.iv) Kazi ya umuganda
Umuganda ni mkusanyiko wa watu kutoka vijiji mbalimbali kwa ajili ya ujenzi wa taifa. Mnamo siku ya Jumamosi ya mwisho kila mwezi, Wanyarwanda wote walio na miaka kati ya kumi na minane na sitini na mitano hukusanyika katika makundi mbalimbali kushiriki katika kazi za umuganda.Kazi ya wanafunzi wawili wawili
Jiunge na wanafunzi wenzako. Jadilianeni kuhusu shughuli mbalimbali ambazo hufanywa siku ya kazi ya umuganda.Tazama michoro hii kuhusu shughuli mbalimbali za umuganda na usome kifungu cha habari.
Wanyarwanda hushiriki katika shughuli mbalimbali siku ya kazi ya umuganda. Umuganda huandaliwa kila Jumamosi ya mwisho ya mwezi. Kila kijiji huamua shughuli muhimu wanazostahili kufanya. Wao huchagua shughuli ambayo ina umuhimu kwao.Baadhi ya wanakijiji huweka vizuizi vya mmomonyoko wa udongo kwa kuchimba mitaro. Wengine wanajaza mitaro hiyo kwa magunia yaliyojaa mchanga. Wengine wanafunika magunia hayo kwa mchanga. Mvua inaponyesha, maji tu ndiyo hupita lakini udongo hubakia kwenye mitaro na magunia yaliyowekwa. Hivyo, rutuba hubakia kwenye udongo nayo ardhi huweza kutumiwa tena katika shughuli za kilimo.Wanyarwanda pia huja pamoja kusafisha maeneo wanamoishi. Watu hupewa majukumu mbalimbali wakati wa usafishaji. Baadhi ya watu huondoa taka kwenye mitaro ya maji machafu. Wengine hupewa jukumu la kuokota taka zilizotapakaa. Wengine huchoma taka hizo. Nao baadhi ya watu kufyeka nyasi zilizomea kando ya mitaro na maeneo mengineyo. Shughuli hizi hulenga kudumisha usafi katika miji na vijiji vyetu.Wanyarwanda pia hupanda miti siku ya kazi ya umuganda. Wao hupanda miti hasa kwenye ardhi tambarare. Wengine hunyunyizia miche maji. Miti mingi hupandwa na wanakijiji mbalimbali kwa kuwa miti ni muhimu katika mazingira yetu.Mbali na hayo, baadhi ya Wanyarwanda hulima na kupalilia mashamba yao. Wao huja pamoja kwa ajili ya kuwasaidia wenzao hasa wazee katika mashamba yao.Maswali
1. Eleza umuhimu wa kazi ya umuganda katika jamii zetu.2. Jiunge na mwanafunzi mwenzako. Kila mwanafunzi asimulie mambo muhimu yanayojitokeza katika shughuli ya kijamii aliyoshiriki zaidi.Kazi ya kikundi
Jiunge na wanafunzi wenzako. Jadilianeni kuhusu shughuli za kijamii mlizoshiriki kisha mziwasilishe mbele ya darasa.B. Namna sahihi ya kuuliza maswali
Kufikia sasa, umejifunza mengi kuhusu shughuli mbalimbali za kijamii. Unaposhiriki katika mazungumzo kuhusu shughuli hizi za kijamii au mambo mengineyo, unaweza kuuliza maswali mbalimbali.Katika Kiswahili, zipo namna mbalimbali za kuuliza swali. Maneno ambayo hutumiwa kuulizia maswali huitwa viulizi. Zipo aina mbalimbali za viulizi. Je, unakumbuka viulizi hivyo?Viulizi huuliza maswali kuhusu jinsi kitendo kilivyotendeka (vipi), wakati kitendo kilipofanyika (lini), mahali kitendo kilipofanyika (wapi), aliyetenda kitendo (nani), kitendo chenyewe (nini), idadi (-ngapi) na namna ya kitendo au kifaa (gani).Hapa, maneno yaliyowekwa kwenye mabano ndiyo viulizi vinavyotumiwa kuulizia maswali.Soma kifungu hiki ili ujifunze mengi kuhusu namna sahihi ya kuuliza maswali.
INEZA: Wenzangu, kwa nini hamkuhudhuria mkutano wa kijiji uliokuwepoJumamosi iliyopita?
TONA: Shoga yangu, wewe unafahamu kuwa mamangu mzazi hajisikii vizuri.Sasa, siku hiyo ilibidi niondoke niende kumtazama.
NDOLI: Nami wenzangu sina sababu ya kutohudhuria bali nilisahau tu na kutanabahi mkutano umekwisha. Mambo gani yalijiri mkutanoni humo?
INEZA: Lo! Tulifanya shughuli mbalimbali...
TONA: Samahani kwa kukutatiza usemi. Shughuli hizo mlizifanya wapi?
INEZA: Tulikusanyika katika uwanja wa mkutano wa kijiji kisha tukajigawa katikavikundi mbalimbali. Kila kikundi kilishiriki kufanya kazi katika maeneo mbalimbali.
NDOLI: Kwa jumla, vikundi vilikuwa vingapi?
INEZA: Vikundi vyote vilikuwa tisa.
TONA: Nani aliongoza kikundi chenu?
INEZA: Kikundi chetu kiliongozwa na Bi. Kabatesi.
NDOLI: Nini alichowapa kabla ya kazi?
INEZA: Alitupa vifaa mbalimbali.
TONA: Mlipewa vifaa gani?
INEZA: Tulipewa mapanga na majembe.
NDOLI: Mlifanya kazi ipi katika kikundi chenu?
INEZA: Tulifyeka na kulima shamba la nyanyake Teta.
TONA: Mkutano ujao utakuwa lini?
INEZA: Mkutano ujao utakuwepo Jumamosi ya mwisho, mwezi ujao. Msikosekuhudhuria kikao.
NDOLI: Ni vifaa gani vitahitajika katika kazi hiyo ya umuganda?
INEZA: Vifaa vitakavyohitajika vitakuwa fagio, ndoo, majembe, mapanga namafyekeo. Msikose kushiriki.
TONA na NDOLI: Tukijaaliwa tutakuwepo. Asante.
Kazi ya wanafunzi wawili wawili
Jiunge na mwanafunzi mwenzako. Tungeni maswali sahihi kuhusu shughuli mbalimbali za kijamii mkitumia viulizi vifuatavyo. Sahihishianeni majibu yenu.
a) vipi
b) lini
c) wapi
d) nani
e) nini
f ) -ngapi
g) gani
Kazi ya kikundi
Jiunge na wanafunzi wenzako katika kikundi. Rejeleeni vifungu vya habari mlivyosoma kuhusu shughuli mbalimbali za kijamii katika vipindi vilivyopita. Tumieni viulizi mbalimbali kuulizana maswali kwa zamu kutokana na yaliyomo kwenye vifungu hivyo. Anayeulizwa ajibu kila swali kwa usahihi. Anapopata jibu, naye amwulize mwenzake swali.Mifano
1. Afisa wa afya kutoka wizara ya kilimo alisema nini kuhusu UKIMWI?2. Nani alifanya harusi?C. Aina saba za maneno
Lugha ya Kiswahili huwa na aina saba kuu za maneno. Maneno haya hutambuliwa kulingana na muundo na matumizi yake katika sentensi. Maneno hayo saba huwa nomino, vitenzi, vielezi, vivumishi, viwakilishi, viunganishi na vihisishi.Nomino
Kufikia sasa, umejifunza mengi kuhusu aina mbalimbali za nomino. Je, unazikumbuka?Tunaweza kutumia nomino mbalimbali kutaja mtu au watu walioshiriki katika shughuli mbalimbali za kijamii. Pia, tunaweza kutumia nomino kutaja vifaa mbalimbali vilivyotumika kutendea shughuli fulani za kijamii, mahali shughuli hizo zilipofanyika na kadhalika. Tazama aina mbalimbali za nomino katika jedwali na usome mifano kando yake.
Zoezi A
Soma kifungu kifuatacho cha habari. Bainisha na uainishe nomino mbalimbali katika kifungu.Ama kwa kweli, ndoa ni jambo linalowafurahisha watu wengi. Kutajwa tu kwa neno hili hufanya roho za watu wengi kusisimka. Takriban watu wote husikia neno hili kwa upendo. Kwa nini upendo? Unapotajiwa neno hili, fikira ya kwanza kukujia ni raha. Watu husikia raha kwa sababu huwepo maakuli na vyakula vingi vya bwerere. Pia, harusi huleta heshima na umaarufu.
Kabla ya kufanya harusi, yapo mambo mengi ambayo hufanyika. Kwanza kabisa, ni sharti mchumba apatikane. Halafu ni sharti ujumbe wa posa upelekwe na mshenga kwa kina mchumba. Ukikubalika, mahari huzungumziwa na kulipwa. Ni baada ya haya yote tu ambapo siku ya harusi huwekwa.
Nayo matayarisho ya harusi huwa mengi. Bi harusi pamoja na wapambe wake sharti wanunuliwe mavazi mbalimbali ya harusi. Mavazi haya huwa pamoja na nguo maalumu za Bi harusi na wapambe wake. Pia ni sharti pawepo jozi mpya za viatu, pete ya harusi, mashada ya maua na kadhalika. Matayarisho mengine ni usafiri, waendesha harusi, kwaya, na matayarisho mengine mbalimbali.
Hatimaye huja siku yenyewe ya harusi. Mfano mzuri wa siku hii ni harusi ya rafiki yangu Iliza iliyofanyika Ijumaa jijini Kigali. Umati wa watu ulihudhuria harusi hiyo. Baada ya ibada, tulienda katika Hoteli ya Serena ambapo sherehe kamili iliandaliwa.
Zoezi B
Jiunge na mwanafunzi mwenzako. Tungeni sentensi zinazohusu shughuli mbalimbali za kijamii kwa kutumia nomino mbalimbali mlizobainisha kifunguni.Vitenzi
Kitenzi ni neno lielezalo jambo la kutendwa au kufanywa.
Je, unakumbuka mifano mbalimbali ya vitenzi ulivyosoma?
Tunaposhiriki katika mazungumzo kuhusu shughuli mbalimbali za kijamii, ni sharti tutumie vitenzi mbalimbali.
Tazama aina mbalimbali za vitenzi katika jedwali na usome matumizi yake.
Zoezi A
Soma kifungu kifuatacho cha habari. Bainisha na uainishe vitenzi mbalimbali vilivyomo kifunguni.“Tuharakishe. Ujenzi wa choo umeanza,” Ikirezi aliniambia. Alikuwa akihema. “Mimi ni mgonjwa. Ningali ninaumwa na tumbo lakini nitajikaza,” nilimjibu. Hatimaye tuliwasili penye mkutano. Watu walikuwa wamejigawa katika vikundi tayari kwa kazi mbalimbali.“Tazama. Kila mtu ameanza kujenga choo isipokuwa sisi,” nilimwambia Ikirezi. Kiongozi wa kijiji alinisikia.“Msiwe na shaka. Nyinyi mtaokota taka zote zilizopo pale uwanjani. Baada ya hapo, mtafagia kando ya barabara. Kazi hiyo si ngumu,” kiongozi wa kijiji alisema.Mimi na Abatoni tulitafuta fagio. Tuliongezewa vijana watatu ili watusaidie kufanya kazi hiyo. Tulifurahia sana kushirikiana na wanakijiji.Zoezi B
Jiunge na mwanafunzi mwenzako. Tungeni sentensi zinazohusu shughuli mbalimbali za kijamii kwa kutumia vitenzi mbalimbali mlivyobainisha kifunguni.Vielezi
Vielezi pia huitwa viarifa nayo ni maneno yafafanuayo vitenzi, vivumishi au vielezi. Tunaweza kutumia vielezi kueleza jinsi shughuli mbalimbali za kijamii zilivyofanywa. Mathalan, ukisema: Anafanya kazi haraka neno haraka linaeleza jinsi kazi inavyofanywa.Je, unakumbuka vielezi ulivyosoma?Tazama aina mbalimbali za vielezi katika jedwali na matumizi yavyo.
Zoezi A
Soma kifungu kifuatacho cha habari. Bainisha na uainishe vielezi mbalimbali kifunguni.Ilikuwa siku ya Jumamosi. Ilikuwa siku ya kuwasaidia wazee kuandaa mashamba yao na kupanda mbegu. Wanakiji wote waliamka alfajiri. Mimi pia nilijiunga nao kwa hiari. Wa kwanza kusaidiwa aliitwa Abera. Tulitembea upesi kuelekea shambani mwake ili tufike mapema. Tulipofika ndani ya shamba, kila mtu alipewa jukumu. Wengine walifyeka majani marefu yaliyomea pembeni mwa shamba.Waliyafyeka majani kwa panga. Wengine walilima kwa jembe la mkono. Wengine waliondoa magugu hatari kutoka shambani na kuyachoma kwa moto. Sisi tulipanda mbegu. Kila mtu alipewa kazi ya kufanya mara kwa mara. Hakuna aliyekaa bure. Sote tulifanya kazi kijeshi.Zoezi B
Jiunge na mwanafunzi mwenzako. Tungeni sentensi zinazohusu shughuli mbalimbali za kijamii kwa kutumia vielezi mbalimbali mlivyobainisha kifunguni.Vivumishi
Kwa kawaida, kivumishi ni neno linaloongezea nomino maana. Vivumishi vinaweza kutumiwa kuelezea sifa za mtu au watu walioshiriki katika shughuli mbalimbali za kijamii. Pia, tunaweza kutumia vivumishi kueleza sifa za vifaa vilivyotumika katika shughuli za kijamii na kadhalika.Kumbuka kuwa vivumishi ni sharti vitumiwe pamoja na nomino. Je, unakumbuka vivumishi gani ulivyosoma?Tazama aina mbalimbali zifuatazo za vivumishi huku ukisoma matumizi yaliyotolewa.
Zoezi A
Soma kifungu kifuatacho cha habari. Bainisha na uainishe vivumishi mbalimbali katika kifungu.
Ni taifa gani ambalo halipendi maendeleo? Ama ni watu wepi ambao hawapendi kuendelea? Sisi Wanyarwanda tunapenda maendeleo ili taifa letu likue hata zaidi. Nchi yenye watu wanaopenda maendeleo hukua haraka. Ili jambo hili liwezekane, ni sharti tufanye mambo kadhaa.
Kwanza kabisa, nchi yetu haiwezi kukua bila masomo. Lazima watoto wote waliofika umri wa kuenda shule waende shuleni. Nasi wanafunzi wenyewe tulenge kufikia elimu ya chuo kikuu. Ili kufaulu masomoni, ni sharti tushirikiane na jamii. Ujuzi huu tunaopata shuleni ni sharti tuutumie kusaidia jamii. Tusingoje hadi tumalize chuo kikuu ndipo tuanze kujenga taifa hili letu.
Pili, usafi ni jambo muhimu sana. Jamii haiwezi kujenga taifa lake kama haina afya nzuri. Je, kina nani wanafaa kudumisha usafi huu? Watu hao si watu wengine bali ni mimi na wewe. Kila mmoja wetu ahakikishe kuwa anaishi katika mazingira safi kila siku.
Tatu, kuna shughuli ya mikutano tofauti tofauti ya kutangaza na kuhimiza maendeleo. Jamii inapokutana na kuelezwa maendeleo yaliyopatikana, hupata motisha ya kufanya mengi zaidi. Hali hii basi huwa ni msukumo muhimu katika kazi zao. Vilevile, vijiji hushindana katika maendeleo. Mashindano ya dhati kati ya vijiji huwa ni motisha nzuri ya ujenzi wa taifa. Kumbuka kuwa vijiji vikipiga hatua mbele nalo taifa hufanya vivyo hivyo.
Jambo jingine linalohitajika katika huu ujenzi wa taifa ni kuwa na mikakati kabambe ya kushughulikia mikasa. Mathalan, tumejitayarisha vipi kukabiliana na mkurupuko wa magonjwa hatari na njaa? Ni sharti tushirikiane ili kuibuka na mikakati kabambe ya kukabiliana na mikasa kama hii.
Ili haya yote na mengine mengi yafaulu, umoja na ushirikiano wetu lazima uwepo. Kumbuka kuwa kidole kimoja hakivunji chawa nalo jiwe moja haliinjiki chungu.
Zoezi B
Jiunge na mwanafunzi mwenzako. Tungeni sentensi zinazohusu shughuli mbalimbali za kijamii kwa kutumia vivumishi mbalimbali mlivyobainisha kifunguni.Viwakilishi
Viwakilishi ama vibadala ni maneno kamili ama viambata (sehemu za maneno) vinavyosimama badala ya majina. Je, unakumbuka viwakilishi ulivyosoma?Tazama aina mbalimbali hizi za viwakilishi katika jedwali lifuatalo huku ukisoma matumizi yake.
Zoezi
Soma kifungu kifuatacho cha habari. Bainisha na uainishe viwakilishi mbalimbali katika kifungu.Waliosema kuwa umoja ni nguvu hawakukosea bali waligonga ndipo. Mimi ninaamini sana katika msemo huu. Ninaamini kwa sababu ya mambo niliyoshuhudia nilipompoteza mama mzazi. Mama alikuwa mtu wa watu. Aliwapenda wanakijiji nao wanakijiji wa mbali na wa karibu wakampenda. Kifo chake kiliwashtua wengi. Kilifanya kijiji kizima kiomboleze. Watu walifurika nyumbani kwetu kutupa pole. Kuwepo kwao kulituliwaza. Licha ya machungu, tulihisi kuwa hatupo peke yetu. Nani angekosa kupata nguvu katika hali kama hii? Msiba huleta unyonge. Wetu ulileta nguvu kutokana na ushirikiano huo.Mbali na kutupa moyo, wanakijiji waligharamia mazishi. Wao walisimamia kila kitu. Sisi tulishuhudia tu mambo yakitendeka. Hawakutaka tushiriki katika shughuli zozote kutokana na huzuni. Waliopika walipika. Waliotengeneza jeneza walifanya hivyo tena kwa ustadi. Waliochimba kaburi hawakusita kumaliza mapema. Kila kitu kilifanywa kwa haraka na ustadi. Mama akalazwa na kupewa heshima zake za mwisho kwa ushirikiano wa wanakijiji. Wao hao wakatuchangia pesa za matumizi ya baadaye. Tulikosa maneno ya kuelezea furaha na shukrani zetu kwao. Kweli, umoja ni nguvu.Viunganishi
Haya ni maneno yanayotumika kuunganisha maneno, vikundi vya maneno au sentensi ili kupitisha ujumbe fulani.
Tazama mifano hii ya viunganishi.
1. Tulikuja pamoja ili kuwafariji waliofiwa.
2. Mkutano uliahirishwa kwa sababu mvua kubwa ilinyesha.
3. Mbali na kufagia, wanakijiji hupanda miti na kujenga vizuizi vya kukinga mmomonyoko wa udongo.
4. Tulisameheana maadamu tulishiriki kazi pamoja.
Zoezi
Soma kifungu kifuatacho. Bainisha aina mbalimbali ya viunganishi vilivyotumika.
Kila jamii huwa na ngoma yao waipendayo. Aghalabu wao huipenda kwa sababu wameirithi kutoka kwa mababu zao. Mathalan, Waswahili hupenda sana msondo. Je, nyinyi mnapenda ngoma gani katika jamii yenu?Kwa kawaida, ngoma kama hiyo huchezwa na wale waliopo sasa. Baadaye hupitishwa kwa vizazi vijavyo. Kwa namna hiyo, ngoma husika huja ikawa sehemu kuu ya utamaduni wao japo baadhi ya mambo ya kisasa huongezwa. Mambo hayo ya kisasa huongezwa pasipo kubadilisha asilia ya ngoma hizo.
Sisi Wanyarwanda pia tunapenda ngoma zetu za kiasili. Itokeapo shughuli muhimu, sisi hushiriki katika kuimba na kucheza ngoma zetu za kitamaduni. Hivyo basi, ngoma huchezwa kama njia mojawapo ya kujiburudisha. Shughuli hii huambatana sana sana na sherehe fulani kama vile siku za kitaifa, harusi, kusherehekea mavuno, siku ya kutoka jandoni au kuvunja ungo na kadhalika. Mbali na hayo, ngoma ni njia moja kuu ya kutuleta pamoja ili kufanya shughuli mbalimbali za kimaendeleo.
Aidha, tunapocheza ngoma fulani siku ya taifa, tunapata kumbukumbu muhimu katika historia yetu. Kwa mfano, tunakumbuka jinsi tulivyokuja pamoja kujikomboa kutoka kwa minyororo ya wakoloni. Ikiwa umoja wetu ulifukuza wakoloni sembuse umaskini?
Ngoma vilevile hutukumbusha umuhimu wa kuwepo kwa amani. Pia, ngoma hutuonya dhidi ya kuchukiana. Hutukumbusha kuwa amani, upendo na umoja ni mambo muhimu katika ujenzi wa nchi yetu.
Iwapo tutapenda ngoma zetu za kienyeji na kutunga nyimbo za kisasa zenye kukuza ushirikiano, basi tutapiga hatua kubwa katika maendeleo yetu.
Kazi ya kikundi
Jiunge na wanafunzi wenzako. Jadilianeni kuhusu aina na mifano mbalimbali ya viunganishi katika Kiswahili. Tungeni sentensi sahihi mkitumia viunganishi hivyo.
Vihisishi
Vihisishi ni maneno ambayo huonyesha hisia mbalimbali za mzungumzaji. Unaweza kuelezea hisia zako kuhusu shughuli mbalimbali za kijamii kwa kutumia vihisishi. Vihisishi hutumika pamoja na alama ya hisi (!).
Tazama mifano iliyotolewa hapa chini.
a) Huree! Tumemaliza kujenga nyumba.
b) Alaa! Mbona harusi haijaanza?
c) Ole wangu! Kumbe nilikosa mengi katika mkutano wenu!
d) Inshallah! Tukutane kesho twendelee na kazi yetu.
Zoezi
Soma kifungu kifuatacho. Bainisha aina mbalimbali za vihisishi vilivyotumika.Sote tulifunga safari ya kumtembelea Gatete kijijini mwao. Lo! Hatukuamini macho yetu tulipofika huko. Kumbe kijiji hicho kilikuwa safi na tulivu mno!Gatete alipokuja kutulaki, tulimpa pongezi. “Hongera! Mnafanya kazi nzuri kweli,” Ndoli alisema.Gatete alimtazama Ndoli kwa mshangao. Hakuelewa sababu za hongera zake.“Jamani! Mbona kijiji hiki chenu ni safi namna hii?” nilimwuliza Gatete.“Ahaa! Sisi hutupa taka zote katika majaa. Pia, tunachimba mitaro ili tusiwe na vidimbwi vya maji. Yeyote, awe mdogo au mkubwa, huokota majani makavu au taka zozote popote,” Gatete alisema akitabasamu.“Maskini sisi! Hatufanyi hivyo hata!” Ndoli alisema.“Alaa! Mnafaa mwanze kufanya hivyo moja kwa moja. Usafi ni jambo muhimu sana katika maisha yetu.”“Naam! Kuanzia leo, nitahimiza wanakijiji wenzangu ili kwa pamoja tudumishe usafi.”Kazi ya kikundi
Jiunge na wanafunzi wenzako. Fanyeni utafiti kuhusu aina mbalimbali za vihisishi katika Kiswahili. Tungeni sentensi sahihi mkitumia vihisishi hivyo.Zoezi la ziada
Soma kifungu hiki. Bainisha na uanishe aina saba za maneno ya Kiswahili (nomino, vitenzi, vivumishi, vielezi, viwakilishi, viunganishi na vihisishi)Kukoga mwaka
Hapo zamani, watu tofauti walikuwa na itikadi mbalimbali kuhusu kuanza kwa mwaka. Baadhi yao walisherehekea siku hiyo kwa kuchinja na kuandaa karamu murua! Nao wengine waliwatambikia wazee wao waliofuata njia ya marahaba. Zaidi ya haya, baadhi ya watu waliamini kuwa ni lazima mwaka mpya uanze kwa usafi. Hii ndiyo ilikuwa sababu ya kukoga mwaka.Kukoga mwaka kulikuwa na utaratibu wake. Kazi hizo zote zilitegemea mwanzo wa mwaka wa kiasili bali si ule wa kizungu. Mwaka huo wa kiasili ulikuwa ukianza saa thenashara hivi za asubuhi. Hivyo basi, kabla ya wakati huo, wenyeji walirauka saa kumi. Madhumuni ya kuamka wakati huo yalikuwa kusafisha kila kitu kabla ya mapambazuko. Basi wanawake waliamka na kukusanya vitu vyote ambavyo viliweza kuoshwa na kuvipeleka mtoni. Wengine walibaki nyumbani kusafisha vile vitu ambavyo havikuweza kuchukuliwa mtoni lakini ambavyo vilihitaji kuoshwa au kusafishwa.Baadhi ya vitu vilivyooshwa mtoni vilikuwa nguo zilizomea koga, vyungu, sahani, sufuria na vyombo vinginevyo. Baadhi ya watu walisafisha vyombo hivyo kwa sabuni lakini wengine walivisafisha kwa majani maalum. Jambo lililokuwa la mwisho kufanywa huko mtoni ni kuwaosha watoto. Baadaye watu wazima wangeoga wao wenyewe. Wakati mwingine, watu wangeosheana miguu kama ishara ya upendo.Nao wanawake wale waliobaki nyumbani walikuwa na kazi kubwa ya kusafisha nyumba mbalimbali za msonge. Baadhi yao walipaka sakafu kwa samadi mbichi iliyochanganywa na udongo na maji. Nao wanawake wengine waliondoa masizi yaliyokuwa yakining’inia kwenye mapaa.Vijana nao walisomba maji kutoka mtoni. Maji hayo yangetumiwa na wanaume kuogea. Wao pia wangeoga baadaye.Wanaume nao hawakukaa bure. Ilikuwa kazi yao kufyeka na kusafisha uani, mbele na pande zote za nyumba. Pia ilikuwa kazi yao kufyeka nyasi zo zote zilizokuwepo pale kiamboni pamoja na kukata matagaa yasiyohitajika ili kwamba jua la mwaka mpya lichomozapo liangaze boma zima.Je, ni kwa nini kazi hizo zote zilifanyika? Hata wakati huo, wenyeji waliamini kuwa Mungu hakupenda uchafu. Isitoshe, waliamini kuwa mtu akianza jambo fulani kwa nuksi basi hatafanikiwa katika mambo mengi. Hivyo basi, imani yao ilikuwa kwamba mwaka ukianza kwa uchafu basi shughuli zao zote mnamo mwaka huo zingekumbwa na nuksi. Hapana hata mmoja aliyetaka kutofanikiwa. Naam! Mwaka mpya ungeanza kwa usafi kweli.Kazi ya kikundi
Jiunge na wanafunzi mwenzako. Someni vifungu mbalimbali vya habari vilivyopo katika sura hii ya nne. Bainisheni na kuainisha aina saba za maneno ya Kiswahili katika vifungu hivyo.D. Matumizi ya wakati uliopita -li- hali yakinishi na hali kanushi
Tunaweza kuzungumzia shughuli mbalimbali za kijamii tulizoshiriki muda au wakati uliopita. Wakati huu huwasilishwa na -li-. Vitendo katika wakati uliopita vinaweza kuwa katika hali yakinishi au katika hali kanushi. Hali yakinishi ni ya kukubali na hali kanushi ni kukataa.Tazama mifano ya matumizi ya wakati huu iliyotolewa kwenye jedwali lifuatalo.
Je, unaona mabadiliko gani katika hali kanushi ya vitenzi hivyo? Katika jedwali lililopo hapo juu, vitenzi walihudhuria, nilienda na ilianza vipo katika hali yakinishi au kukubali kwa wakati uliopita.Vitenzi hawakuhudhuria, sikuenda na haikuanza vimo katika hali ya kukataa yaani hali kanushi kwa wakati uliopita. Kiambishi ‘li-‘ hakitumiki katika hali kanushi. Huondolewa.Kazi ya wanafunzi wawili wawili
Jiunge na mwenzako. Tungeni sentensi sahihi kuhusu shughuli za kijamii mkitumia wakati uliopita katika hali yakinishi na kanushi.E. Matumizi ya wakati ujao -ta- katika hali yakinishi na hali kanushi
Wakati ujao hutumiwa kuelezea mawazo au vitendo vitakavyofanyika baadaye. Kiambishi -ta- hutumika pamoja na kitenzi husika kuonyesha kuwa kitendo kitafanyika baadaye.Tunaweza kuzungumzia shughuli mbalimbali za kijamii ambazo zitafanyika baadaye. Mfano: unapoandika ratiba ya shughuli au kutoa maelekezo ya mambo yanayofaa au ambayo hayafai kufanywa, unatumia wakati ujao.Vitendo katika wakati ujao vinaweza kuwa katika hali yakinishi au kanushi. Hali yakinishi ni ya kukubali na hali kanushi ni kukataa.Tazama mifano iliyotolewa kwenye jedwali lifuatalo.
Vitenzi vilivyopo katika jedwali viko katika wakati ujao.Je, unaona mabadiliko gani katika hali kanushi ya vitenzi hivyo?Katika jedwali lililopo hapo juu, vitenzi utaandaliwa, litatufaa na mtafyeka vipo katika hali yakinishi au kukubali kwa wakati ujao.Vitenzi hautaandaliwa, halitatufaa na hamtafyeka vimo katika hali ya kukataa yaani hali kanushi kwa wakati ujao.Kazi ya wanafunzi wawili wawili
Jiunge na mwenzako. Tungeni sentensi sahihi kuhusu shughuli za kijamii mkitumia wakati ujao. Mzingatie hali yakinishi na kanushi.Mifano
ABATONI: Vijana watafyeka barabara.NDOLI: Vijana hawatafyeka barabara. Watasomba maji ya kujengea nyumba.ABATONI: Wazee hawatasomba maji ya kujengea nyumba. Watatoa maelekezo.Maswali ya marudio
1. Eleza mambo muhimu ambayo hutendeka katika shughuli za ubudehe.
2. Linganisha na utofautishe shughuli za mazishi na harusi katika jamii.
3. a) Bainisha wahusika wakuu katika shughuli hizi za kijamii:
i) Mazishi
ii) Harusi
iii) Ibada msikitini au kanisani
b) Eleza tofauti za kimawasiliano katika shughuli zilizotajwa hapo juu.
4. Tunga sentensi ukitumia msamiati ufuatao:
a) kuchimba mitaro
b) kusomba maji
c) kula kiapo
d) peleka mahari
5. Taja sherehe nne muhimu za jamii katika eneo utokako huku ukiielezea kila moja umuhimu wayo.
6. Wewe ni kiongozi wa kikundi kinachoshiriki katika shughuli fulani ya kijamii. Chagua shughuli upendayo kisha utoe maelekezo kwa wanachama wa kikundi chako.
7. Eleza manufaa ya kazi ya umuganda kwa jamii ya Wanyarwanda.
8. Taja mambo mawili yanayoweza kukuonyesha kuwa tungo ni swali.
9. Tunga maswali matano ukitumia viulizi mwafaka.
10. Zipo aina ngapi za maneno ya Kiswahili? Zitaje.
11. Yataje maneno kumi ya Kinyarwanda ambayo ni sawa na yale ya vihisishi vya Kiswahili.
12. a) Nomino ni nini na huweza kuitwaje pia?
b) Tunga sentensi tano sahihi ukitumia aina mbalimbali za nomino.
13. Tambulisha vitenzi katika maneno yafuatayo:msamaha samehe hisi kihisishi rehema kurehemu rehemu fikira fikiri kilio lia
14. Zieleze aina zote za vivumishi ambazo umejifunza hadi sasa. Tunga sentensi ukitumia kila mojawapo.
15. Eleza tofauti iliyopo kati ya viunganishi na vihisishi.
16. Andika aya moja kuhusu shughuli fulani ya kijamii. Tumia maneno yote saba ya Kiswahili katika aya hiyo kwa usahihi.
17. Pigia kistari sentensi zilizopo katika wakati ujao na useme ikiwa ni hali yakinishi au kanushi.
i) Siendi Kigali.
ii) Wanaenda harusini.
iii) Nitashiriki katika kazi zote kijijini.
iv) Aliniita sikusikia.v) Hawatachelewa leo.
18. Eleza umuhimu wa ushirikiano katika jamii.
19. Taja mambo yote muhimu uliyojifunza katika sura hii.
Faharasa
adimika – kosa kupatikana kwa urahisiambukiza – enezea ugonjwaandaa - tayarishaankra – orodha ya vitu vilivyouzwa pamoja na bei ya kila bidhaaanuani – maelezo ya mahali mtu anapoishi ambayo huandikwa katika baruaasali – namna ya kitu kioevu na kitamu sana kitengenezwacho na nyukiazma – lengo au shabahabainisha – tambua jambobao – mpira kuingia katika lango katika mchezo wa kandanda (goli)baridi kali – hali isiyokuwa na joto na isisimuayo sana mwilibei – kiasi cha pesa kinachotumiwa kununulia ama kuuzia bidhaa fulaniburudani - stareheburudisha – sababishia rahachai – zao la mchaidumisha – endelezafaranga – pesa, fedha, dirhamu, senti, fulusifilisika – ishiwa na malifyeka – kata nyasigharamia – lipia gharamaharage/haragwe– nafaka ya jamii ya kundeharamu – -siyoruhusiwa, -siyokuwa halaliHisabati – sayansi ya tarakimu ijumuishayo aljebrahitaji – kuwa na haja ya kituhuzuni – hisia za majonziibuka – tokezaidadi – hesabu au jumla ya vituilani – tangazo la kuonya watu wasifanye jambo fulani hasa lenyekuleta madharaingawa – hata ikiwajadhba/jazba – hisia isababishayo kujisahaujamii – watu wanaoishi pamojajangili – mwindaji haramujedwali – orodha ya maelezo kuhusu mambo fulani kwa namnayatakavyofuatanajibini – chakula kinachotengezwa kwa kuyagandisha maziwa na kuyatoamajijukumu – wajibujumuiya– mkusanyiko wa watukabuti – koti zito la kuzuia baridikagua – chunguza kwa makinikahawa – zao la mkahawa ama mbunikandanda – mchezo wa miguukauli – usemikiasili – kienyejikifaa – chombokikao – mkutanokipindi – mudakipusa – pembe ndogo ya kifalukivuna nafaka – mashine kama trekta ambayo huvuna ngano hukuikiitoa wishwakiwanda – mahali panapotengenezwa bidhaakodi ya mapato – fedha zinazolipwa serikali kama ushuru wa mapato ya mtukupanda– tia mbegu mchangani ili ziotelimbikiza – weka vitu kidogo kidogo ili viwe vingilishe bora – chakula kinachohitajika kwa afya nzuri ya mwilimaabara – mahali mnamofanyiwa majaribio ya kisayansimaalumu – -enye sifa ya kipekeemada– kiini cha jambo linalozungumziwamajira– wakati au kipindimajira ya kiangazi – kipindi cha kiangazimajira ya kipupwe – kipindi cha baridimajira ya mvua– kipindi cha mvuamajira ya vuli– kipindi cha mvua chachemajivuno – hali ya kujionamanufaa – faidamapato – kitu kinachopatikana kama vile baada ya kufanya kilimo amakufanya biashara.masuala mtambuka – mambo muhimu yanayoiathiri jamii katika kipindi chasasamatini – kifungu cha habari iliyoandikwamazingira – mambo yanayotuzunguka mahali tunapoishimaziwa – kitu kioevu kitokacho ndani ya titi la mnyamambatata – namna ya viazi vilivyo mviringo na visivyo na ladhambinu – njia au namna ya kufanyia jambombuga – eneo lililotengewa wanyama wa porinimchele – mpunga uliokobolewa,yaani kuondolewa mashukemfawidhi – mtu aliyepewa wajibu wa kuendesha shughuli fulani, kama vilemkutano au sherehe fulanimfugaji tajiri – mfugaji ambaye ana mali nyingimifugo – wanyama wanaotunzwa nyumbanimikahawa – mimea izaayo kahawamkulima tajiri – mkulima ambaye ana mali nyingimmomonyoko – kuchukuliwa kwa udongo wenye rutubamori – hasira kalimshinde – aliyeshindwamshindi – aliyeshindamsimu – majiramtama – zao la mtamamuhogo – mzizi wa muhogo unapokuwa umekomaa tayari kwa kuliwandama – mtoto wa ng’ombendizi – tunda la mgomba linalomea kwenye mkungu.ngeli – kikundi cha majina au nomino zinazofuata kanuni sawa za kisarufinjugu – mbegu zitengenezewazo mafuta ya karanganyama – sehemu laini ya mwili ambayo ikikatwa hutoka damupandwa – ingiwa napekee – pweke; bila ya -inginepesa – noti na sarafu zinazotolewa na kuidhinishwa na serikali kuwa nifedha rasmi za kubadilishana na bidhaa.pori – mahali palipo na miti mingi, nyasi na vichakaratiba – mpango wa mfululizo wa shughuli fulanirefa – mwamuzi katika mchezo wa mpirarejesta – lugha inayotumiwa katika mahali maalum, kama vile hospitalini, hotelini, msikitini na kwinginekorutuba – mbolea ya kukuzia mimea ardhinisajili – rejestashabiki – apendaye sana timusheria – kanuni za kuongoza watushime – neno la kuhimizia mtushiriki – husika au kuungana na watu katika kufanya shughuli fulanisoseji – namna ya chakula kinachotengenezwa kutoka kwa nyama yanguruwe au ya ng’ombesuala – jambo au hojasufu – manyoya ya kondootakwimu – nambari zinazoeleza ukweli kuhusu matukio ya mambo, kwamfano idadi ya watu katika eneo fulanitambua – fahamu au maizitanbihi – maelezo yanayotoa habari muhimutathmini – pimategemea– weka matumaini kupata kitutia mdomoni– kumsema ama kumsengenya mtuulinzi – ulindaji, hali ya kulindaupanzi – upandaji (uwekaji mbegu ardhini)utafiti – uchunguzi wa kisayansivanila – kiungo kiyafanyayo maziwa yaliyoganda kuwa na ladha yakupendezaviazi vitamu– namna ya viazi vikubwa na vilivyo vitamuwadau – mtu mwenye maslahi katika shughuli fulaniwadhifa – madaraka au cheo fulaniwaligonga ndipo – walisema ukweliwasifukazi – maandishi yanayoeleza kuhitimu kwa mtu katikakutekeleza kazi fulani, aghalabu, kimasomo, tajiriba ya kazina ujuzi wakewishwa – takataka za nafaka kama vile mtama au nganoyakinishi – hali ya kukubalizao – kile kinachozaliwa na mmeazaraa – kilimoVitabu vya rejea
Kagwa, F.M. na Waihiga, G. (2007) Kamusi Changanuzi ya Methali. Nairobi:Moran (E.A.) Publishers.Kipande, M. (2013) Sarufi. Nairobi: Moran (E.A.) Publishers.Massamba D.P.B. (2004) Kamusi ya Isimu na Falsafa ya Lugha. Dar es Salaam.TUKI.Mogambi Hezron (2007) Premier Golden Tips; Kiswahili kwa Shule za Upili.Nairobi: Moran (E.A.) Publishers.Mutali Chesebe (2010) Premier Golden Tips; Stadi za Uandishi wa Insha. Nairobi:Moran (E.A.) Publishers.Oxford University Press (2013). Kamusi ya Kiswahili Sanifu. Toleo la tatu.Oxford University Press.Rwanda Education Board. (2015) Kiswahili Sylabus for Ordinary Level. S1-S3.Kigali: Rwanda Education Board.TUKI (1990) Kamusi Sanifu ya Isimu na Lugha. Dar es Salaam. TUKI.