Topic outline
MADA YA 1: UANDISHI WA BARUA ZA KIRAFIKI, MWALIKO NA MATANGAZO
Uwezo mahususi
Kuandika barua za kirafiki, mwaliko na matangazo kwa watu mbalimbali
Malengo ya ujifunzaji
- Kutaja sehemu kuu za barua za kirafiki, mwaliko na matangazo
- Kuchunguza muundo wa barua za kirafiki, mwaliko na matangazo
- Kutofautisha aina za barua za kirafiki, mwaliko na matangazo
- Kuelezea lugha inayofaa kutumiwa katika uandishi wa barua za kirafiki,
mwaliko na matangazo
- Kutunga barua za kirafiki kwa watu mbalimbali, barua za mwaliko na
matangazo ya aina tofauti
- Kuonyesha adabu na hehima kwa watu anaowaandikia- Kueleza matumizi ya aina za maneno
KIDOKEZO
Tazama kwa makini mchoro ufuatao kisha ujibu maswali
yaliyotolewa hapo chini:
Jibu maswali yafuatayo
-- Ni nini unachoona kwenye mchoro?
-- Ni mambo gani tunayotumia kwa kuwasiliana kimaandishi?
SOMO LA 1: BARUA YA KIRAFIKI
1.1. Kusoma na ufahamu: Wema HauoziSoma barua ifuatayo kisha ujibu maswali ya ufahamu.
Mpendwa Amina,Chuo cha Ualimu cha AmahoroS.L.P. 100,NGORORERO16/11/2019
Salamu!
Ninakuandikia waraka huu nikiwa nimejaa furaha ghaya kama mzazi aliyejifungua
pacha salama salimini. Wewe u mzima? Wazazi wako hawajambo ? Nasi hapa
nyumbani kwetu Ngororero mambo ni shwari.
Nia yangu ya kukuandikia barua hii ni kukushukuru kwa dhati ya moyo wangu.
Zaidi ya hayo ni kule kunialika kuja katika harusi ya dada yako huko kwenu. Harusi
ile ilikuwa ya kukata na shoka kabisa. Ilinivutia sana, hasa nilivyoona kwamba
harusi yenyewe ilionyesha utamaduni wetu wa Wanyarwanda bila kuchanganya
mambo ya kizungu. Hilo ni jambo nadra sana siku hizi wakati ambapo watu wengi
wamebobea uzunguni. Harusi ilionyesha mitindo ya asili na jadi. Bibi na bwana
arusi walikuwa wakipendeza mno na wakachagua kufanana sana kama mboni za
macho. Ninawaombea baraka za Bwana.
Zaidi ya hayo, usafi uliokuwa nyumbani kwenu ulikuwa wa kuvutia. Ugani
kulikuwa kunametameta na kupendeza kutokana na maua yaliyokuwa yakitoa
harufu nzuri. Vyakula na vinywaji vilivyoandaliwa mezani vilikuwa safi kwenye
kiwango kinachohitajiwa.
Isitoshe, ninakushukuru tena kwa msaada ulionipatia ukanisaidia masomoni
wakati tulipokuwa shuleni. Msaada wako ulinifaa zaidi kwa sababu niliweza
kushinda vizuri. Jambo hili lilinionyesha kwamba u rafiki wa kweli. Unajua?
Nilipofika nyumbani wazazi wangu walinichinjia jogoo! Nami wakati wowote ule
utakapohitaji msaada kutoka kwangu niko tayari kukupatia kwa kuwa « wema
hauozi ».
Kisha nisalimie wazazi wako na ndugu zako, maana walinishughulikia kupita
kiasi. Kwa hakika, ninashindwa niandike yapi hata waweze kuelewa upeo wa
furaha yangu.
Wako,gahamanjosGAHAMANYI Jonasi
KAZI 1
Maswali ya ufahamu :
a) Ni nani aliyeandika barua hii?
b) Taja jina la aliyeandikiwa barua.
c) Mwandikaji wa barua anasomea katika shule gani?
d) Mwandikajibarua anaishi wapi?e) Madhumuni ya barua hii ni yapi?
1.2. Msamiati kuhusu barua
KAZI 2
Baada ya kusoma barua ya hapo juu eleza maneno yafuatayo
-- Ghaya
-- Shwari
-- Nadra
-- Wamebobea
-- Dhati1.3. Sarufi : Aina za maneno ya Kiswahili
KAZI 3
Chunguza sentensi zifuatazo kisha utaje aina za maneno
yaliyopigiwa mistari.
-- Gahamanyi ni mwalimu wa chuo cha ualimu.
-- Darasa linasafishwa na wanafunzi wale.-- Yeye atakuja kesho.
• Gahamanyi, ualimu : ni nomino/majina
• Ni, linasafishwa ni vitenzi
• Cha, wale ni vivumishi• Yeye ni kiwakilishi
Maelezo muhimu kuhusu aina za maneno
Katika lugha ya Kiswahili kuna aina nane za maneno. Aina hizo ni kama vile
nomino, kitenzi, kivumishi, kiwakilishi, kihusishi, kielezi, kiunganishi na kihisishi.
Katika somo letu tutagusia kwenye aina nne yaani nomino, kivumushi, kiwakilishi
na kitenzi.
• Nomino (N)/ jina
a) Maana ya nomino
Nomino au jina ni neno linaloita kitu chenye uhai au kisicho hai kwa kukitoautisha
na vingine.
b) Aina za nonino
-- Nomino za pekee : Butare, Nyanza, Ngororero , Gahamanyi, Ibilisi,
Rukarara, Yesu, Akanyaru, …
-- Nomino za kawaida : ndege, gari, nyumba, kiongozi, tarafa, gunia, kobe,
miti …
-- Nomino za dhana au za dhahania : unyama, uzalendo, ualimu, utu,
ujinga, uroho…
-- Nomino za jamii/ za makundi : umma, familia, jamii, bodi, baraza,
genge, kikosi, jeshi, …
-- Nomino za wingi : mate, maji, mafuta, amani, madaraka, …
-- Nomino za kitenzi-jina : Kuishi kwingi kuona mengi. Kuimba kwakeni kuzuri.
KAZI 4
Baada ya kusoma maelezo ya hapo juu toa mifano mingine yaaina za nomino.
KAZI 5
Weka majina yafuatayo katika wingi
Vivumishi(V)
a) Maan ya kivumishi
Vivumishi au visifa ni maneno yanayotuelezea zaidi kuhusu nomino. Aghalabu
vivumishi hutanguliwa na nomino.
b) Aina za vivumishi
• Vivumishi vya sifa
Mifano:
-- Mke mfupi yule ni mpole.
-- Sauti nzuri humtoa nyoka mkali pangoni.
• Vivumishi vimilikishi
Vivumishi hivi hutumika kuonyesha nomino inayomiliki nyingine. Mizizi ya vivumishi
hivi huundwa kulingana na nafsi mbalimbali. Mizizi hiyo ni: -angu, -ako, -ake,
-etu, -enu, -ao.
Mifano :
-- Gari langu halina usukani.
-- jamii yao inaishi vizuri.
• Vivumishi vya idadi
Hutueleza zaidi kuhusu kiasi, au idadi ya nomino. Kuna aina mbili za vivumishi
vya idadi.a) Idadi kamili - hutumia nambari kuelezea idadi ya nomino.
Mifano:
-- Mmomonyoko wa ardhi ulibomoa nyumba tatu katika kijiji kimoja.
-- Alipotaka kuoa wake wawili wanakijiji walimzuia.
b) Idadi Isiyodhihirika - huelezea kiasi cha nomino kwa ujumla, bila kutaja
idadi kamili.
Mifano: Chache, nyingi, kadhaa, kidogo, wastani.
Mifano:
-- Watoto wengi waligeuka mayatima wakati wa mauaji ya kimbaridhidi ya
Watusi yaliyotokea mnamo mwaka wa 1994.
-- Mvua nyingi ilinyesha na kusababisha mmomonyoko wa ardhi.
• Vivumishi viulizi
Vivumishi viulizi hutumika kuuliza swali.
-ngapi?, -pi? wapi?, gani?
Mifano:
-- Mtu yule ana miguu mingapi?
-- Ni mbuga ipi inayohifadhi simba nchini Rwanda?
• Vivumishi viashiria / vionyeshi
Vivumishi viashiria hutumika kuonyesha au kuashiria nomino kulingana na mahali.
Karibu: hapa, huyu, hiki, hili, huku, haya.
Mbali kidogo: hapo, huyo, hiyo, hicho.
Mbali zaidi: pale, lile, kile. ule, wale, pale.
Mifano :
-- Kaeni mahali hapa.
-- Kijana yule ni mchezaji.
• Vivumishi visisitizi
Husisitiza nomino fulani kwa kurudia rudia kivumishi kiashiria.
Mifano:
-- Amekuja pahali papa hapa.-- Kiongozi yuyu huyu anatutawala vizuri.
• Vivumishi virejeshi
Hivi ni vivumishi ambavyo hurejelea nomino. Vivumishi hivi vinaweza kuwa
vivumishi vya O-/-ye rejeshi au vivumishi viashiria vinapotumika kurejelea nomino.
Mifano:
-- Raia ambaye atakamatwa akiuza au akinunua magendo ataadhibiwa.
-- Wanyama ambao ni wakali sana ni simba na chui.
• Vivumishi vya A-unganifu
Vivumishi hivi hutuelezea zaidi kuhusu nomino kwa kuonyesha kitu kinachomiliki
nomino hiyo. Huundwa kwa kuambatanisha kiambishi cha nafsi/ngeli pamoja na
kiambishi -a cha a-unganifu, kisha nomino.
Mfano: cha, la, kwa, za, ya, wa, …-- Uchungu wa mwana aujuaye mzazi.
KAZI 6
Pigia mstari vivumishi katika sentensi zifuatazo:
a) Jua kali hili husababishwa na uharibifu wa mazingira yetu.
b) Maneno matamu yalimtoa nyoka yule pangoni mle.
c) Koti hilo refu limekugeuza mzee.
d) Usafi utafanywa na sisi sote wenyewe.e) Ni walimu gani watakaofundisha somo la Kiswahili?
a) Maana ya viwakilishi
Viwakilishi (w)
Viwakilishi vya nomino ni maneno yanayotumika badala ya nomino. Kiwakilishihakiwezi kuambatanishwa na nomino inayorejelewa.
b) Aina za viwakilishi
• Viwakilishi vya nafsi
-- Viwakilishi nafsi huru: Mimi, wewe, yeye, sisi, nyinyi, wao.
-- Viwakilishi nafsi viambata : Ni-, u-, a-, tu-, m-, wa-, mi-, li-, ya-, ki-, vi-,i-, zi-, ku-, pa-
• Viwakilishi viashiria
Viwakilishi viashiria (vionyeshi) hutumika badala ya nomino kwa kutumia
kuonyesha nomino inayorejelewa bila kuitaja.
-- Haya ni madhara ya uharibifu wa mazingira.-- Wale wanahitaji amani.
• Viwakilishi visisitizi
Hutumika kwa niaba ya nomino kwa kutumia kiashiria chake mara mbili mfululizo.
Kwa mfano: yuyu huyu, wawa hawa, kiki hiki, papo hapo, mumu humu, zizi hizi,
→ Yuyu huyu ndiye rafiki yangu.
• Viwakilishi vya sifa
Husimama badala ya nomino kwa kurejelea sifa yake.
Kwa mfano: -chungu, -eupe, -dogo, -zuri, -tamu, -embamba, -rembo, -gumu,
-kali, ekundu.
→ Cheupe Kinapendeza.
• Viwakilishi vya idadi
Hutumika kusimama badala ya nomino kwa kurejelea idadi yake.
a) Idadi Kamili - hutumia nambari kuelezea idadi ya nomino
-- Ukikata mmoja panda miwili.
-- Anafuga watatu tu.
b) Idadi isiyodhihirika - huelezea kiasi cha nomino kwa ujumla, bila kutaja
idadi kamili.
Mifano:
-- Tutasikiliza maoni ya wengi baada ya kuuratibu mpango huu.
-- Mengi yalisemwa kuhusu maradhi ya UKIMWI.
• Viwakilishi viulizi
Viwakilishi viulizi hutumika kwa niaba ya nomino katika kuulizia swali.
Baadhi ya viwakilishi viulizi huchukua viambishi vya ngeli.
Mifano:
-- Uko wapi?
-- Unahitaji vingapi?
• Viwakilishi vimilikishi
Viwakilishi hivi hurejelea nomino kwa kutumia vimilikishi.
-- Kwetu kuna maji safi.
-- Zao zilibomolewa na mvua kali.
• Viwakilishi virejeshi
Hutumia O-/-ye-rejeshi kurejelea na kusimamia nomino.
Kwa mfano: ambaye, ambao, ambalo, ambacho, huyo, yule.
-- Ambao walizaliwa mwaka huu watapimwa.
-- Ambaye anahitaji fedha za shule
• Viwakilishi vya A-unganifu
Huwakilishi nomino kwa kutaja kinachomilikiwa na nomino hiyo. Huundwa
kwa kuambatanisha kiambishi cha nafsi/ngeli pamoja na kiambishi -a cha
a-unganifu.
Kwa mfano: cha, la, kwa, za, ya
-- Cha mlevi huliwa na mgema.-- La kuvunda halina ubani.
KAZI 7
Taja aina za viwakilishi vinavyopatikana katika sentensi zifuatazo:
-- Wao hawajafika kwangu.
-- Yule mweusi aende nyumbani.
-- La kuvunja halina rubani.-- Wengi walipanda miti kupambana na jangwa.
1.4. Matumizi ya lugha
KAZI 8
Soma upya barua uliyopewa hapo awali kisha utoe maana yabarua ya kirafiki na uonyeshe sehemu zake kuu.
Maelezo muhimu kuhusu barua ya kirafiki
a) Maana ya barua
Barua au waraka ni maandishi yaliyopangwa kwa utaratibu na mtiririko maalum
kwa minajili ya kuwasilisha ujumbe fulani. Barua ni risala au mmjumbe mwepesi
anayemwakilisha mtungaji wake kwa mtu mwingine na kuwasilisha taarifa yakekwa mtu huyo.
Barua huandikwa kwa madhumuni mbalimbali kama kuarifu, kuomba kitu kama
vile kazi, ruhusa; kuagiza bidhaa, n.k.
Kuna aina nyingi za barua lakini katika kitabu hiki tutashuhulikia barua tatu tu
ambazo ni:
-- Barua za kikazi zenye madhumuni ya kazi.
-- Barua za mwaliko zenye lengo la kualika mtu katika sherehe au sikukuu
fulani
-- Barua za kirafiki : ni zile ambazo huandikiwa na mtu au watu mbalimbali
walio na uhusiano wa karibu na anayeandika; k.v rafiki, ndugu, n.k. Barua
hizi zina uhuru mkubwa katika kuziandika. Hazidai utaratibu wa kipekee
sana. Mtu huwa huru kuandika apendalo ilimradi halimvunjii mtu heshima
yake.b) Sehemu za barua ya kirafiki
-- Anwani ya mwandikaji na tarehe: huandikwa kwenye pembe ya juu
upande wa kulia wa karatasi. Mwandikaji anaandika mahali anapoandikia
barua (au anapoishi). Anaweza kuongeza nambari za sanduku la posta
(S.L.P.) na mji, nambari ya simu na akaunti ya barua pepe. Tarehe huandikwa
chini ya anwani kwa kuacha nafasi ya mstari mmoja.
-- Jina la mwandikiwa: huja chini ya tarehe lakini kwenye upande wa
kushoto.
-- Salamu: sehemu hii hutoa maamkizi kwa mwandikiwa na huandikwa
chini ya jina la mwandikiwa.
-- Utangulizi: hujitokeza katika aya ya kwanza. Mwandikaji humjulisha hali
yake ilivyo,na kuuliza hali ya mwandikiwa na hata wenzake kwa jumla.
-- Barua yeynyewe: huu ni ujumbe kamili wa barua. Mwandikaji anaweza
kutumia aya moja au zaidi kulingana na urefu wa barua yake.
-- Hitimisho la barua: ni sehemu ya mwisho ya barua. Sehemu hii
huandikwa kwa aya moja na hujumlisha mambo ya kumuaga mwandikiwa.
Kwenye sehemu hii unaongeza maneno ya kuvutia (Wako, Wako mpendwa,
Mwanako, Wako mwaminifu, n.k.). Maneno haya huandikwa kwenye
upande wa kulia kabla ya kutia sahihi.
-- Sahihi ya mwandishi: huja chini ya hitimisho kwa upande wa kushoto.
-- Jina la mwandikaji: huja chini ya sahihi ya mwandikaji.
c) Aina za barua za kirafiki
Barua za kirafiki zinaweza kuwa mwana kwa mzazi au mzazi kwa mwana, za
mapenzi, za kindugu (kati ya ndugu), za kijamaa, n.k.
1.5. Kusikiliza na kuzungumza
KAZI 9
Tunga barua kisha uisomee wenzako hadharani kwa kuonyesha vitabia
1.6. Kuandika
KAZI 10
Mwandikie rafiki yako barua ukimwomba muende pamojakutembelea Mbuga ya Wanyama ya Akagera.
SOMO LA 2: BARUA YA MWALIKO
2.1. Kusoma na ufahamu: Ndoa ya dadangu
Soma kifungu cha habari kifuatacho kisha ujibu maswali ya ufahamu.NDOA YA DADANGU
Ilikuwa Jumamosi tarehe 15 mwezi wa Novemba wakati nilipohudhuria harusi ya
dada yangu Mukashema Maria aliyefungana pingu za maisha na Mutabazi Joni.
Harusi yenyewe ilikuwa ya kukata na shoka.
Kabla ya wiki mbili za arusi kufanyika familia mbili zilikuwa katika pilikapilika za
hapa na pale ili kuandaa sherehe hii ya harusi. Kwa upande wa familia yangu sisi
watoto tulikuwa tukitumwa huku na kule kwa kuwaalika watu watakaohudhulia
harusi hii. Wazazi wangu waliwaalika wazee majirani na dada yangu akawaalika
wenzake hasa wa rika lake. Wote walikuwa wakipelekewa barua za mialiko.
Siku moja kabla, nyumbani kwetu tulifanya usafi na majirani walikuwa wakimsaidia
baba kutayarisha pombe ya mtama, ya ndizi na juisi. Wengine walikuwa
wakipamba uga na kujenga nyumba za mahema.
Siku hiyo ilipowadia watu walimiminika kuelekea nyumbani kwetu. Asubuhi
majira ya saa nne hivi, familia ya bwana harusi ilifika kwetu na kukaribishwa kwa
taadhima. Walikuwa wamekuja kuposa na kutoa mahari. Waliandaliwa vyakula
na vinywaji mezani wakafurahi sana. Furaha yao ilipandishwa na nyimbo pamojana ngoma za wachezaji waliokuwa hapo.
Baada ya hapo bi harusi alivishwa veli. Bwana harusi alirudi kumchukua akiwa
na gari la kifahari wakaenda kanisani ili kuvishana pete mbele ya Bwana. Nasi
tuliandamana nao tukiwa katika magari kadhaa. Watu walipoona mlolongo wa
magari hayo waliduwaa wakidhani kuwa kulikuwa na kongamano la kimataifa
katika kijiji chetu.
Tulipotoka kanisani, tulifurika bustanini kama ilivyoelezwa kwenye barua za
mwaliko walizopewa watu. Watu walikuwa wengi sana na sherehe ilifana sana.
Tuliandaliwa vinywaji na vyakula tele tele. Watu wote walifurahi sana na kuchezangoma na nyimbo za utanaduni
KAZI 1
Maswali ya ufahamu
a) Harusi inayosimuliwa ilifanyika lini ?
b) Harusi hiyo ilikuwa ya kina nani ?
c) Ni vinywaji gani vilivyotayarishwa siku moja kabla ya sherehe?
d) Watu waliokuja harusini walipataje habari hizo?e) Kwa sababu gani watu walioona magari walishangaa?
2.2. Msamiati
KAZI 2
Eleza maneno yafuatayo
a) Aliyefungana pingu za maisha
b) Pilikapilika
c) Kifahari
d) Mahemae) Veli
2.3. Sarufi: Aina za maneno
KAZI 3
Tazama sentensi zifuatazo kisha ueleze maneno yaliyopigiwa
mistari
a) Nyumbani humu mna usafi.
b) Tia taka nje.c) Simba anaishi ndani ya msitu ule.
Maelezo muhimu kuhusu aina za maneno
Katika lugha ya Kiswahili kuna aina nane za maneno. Aina hizo ni kama vile
nomino, kitenzi, kivumishi, kiwakilishi, kihusishi, kielezi, kiunganishi na kihisishi.
Katika somo letu tutagusia kwenye aina tatu yaani kitenzi, kielezi na kihusishi.
• Kitenzi
a) Maana ya kitenzi
Kitenzi ni neno linaloeleza jambo linalotendwa au kufanywa na nomino au
kiwakilishi chake.
b) Aina za vitenzi
-- Kitenzi halisi: Ni kitenzi kimoja kinachotumiwa katika sentensi.
Mifano :
-- Raia walifanya msaragambo.
-- Meya amekuja hapa.
-- Vitenzi vikuu na vitenzi visaidizi: Wakati vitenzi viwili hutumika pamoja
kueleza kitendo kimoja, kitenzi cha kwanza huitwa kisaidizi na cha pili
ndicho kitenzi kikuu.
Mifano :
-- Yeye alikuwa akicheza.
-- Wao wanahitaji kula vizuri.
• Vitenzi vishirikishi: Vitenzi vishirikishi vina dhana ya kitenzi kuwa au
kuwa na.
Vitenzi vishirikishi huwa vya aina mbili kuu :
• Vitenzi vishirikishi vikamilifu: Hivi huchukua viambishi vya wakati
na viambishi nafsi.
Mifano :
-- Wanafunzi wangali usingizini
-- Yeye atakuwa mzembe.
• Vitenzi vishirikishi vipungufu : Hivi huchukua viambishi nafsi lakini
havichukui viambishi wakati.
-- Walozi si wazuri.
-- Yeye yu mkweli.-- Nyinyi ni walimu wa kesho.
KAZI 4
Tunga sentensi ukitumia vitenzi vifuatavyo :
• - yu
• - kimuona
• - u
• - kaa• - ni
• Vielezi
Vielezi ni maneno yanayotoa habari zaidi kuhusu kitendo kilivyofanyika. Pia vielezi
hutoa habari zaidi kuhusu hali, vivumishi na vielezi vingine.
Kuna vielezi vya namna, vielezi vya wakati, vielezi vya mahali na vielezi vya kiasi.
Mifano :
-- Mwanafunzi-mwalimu yule ameshinda mtihani vizuri (Kielezi cha
namna).
-- Mvua ilinyesha jana (kielezi cha wakati).
-- Samaki huishi baharini (kielezi cha mahali).-- Anamtembelea mara kwa mara (kielezi cha kiasi).
KAZI 5
Onyesha na utaje aina za vielezi vinavyopatikana katika sentensi
zifuatazo:
-- Simba huenda kimya anapowinda.
-- Vijana wa siku hizi huvaa kizungu, kichina na kihindi mara chache.
-- Wewe uliitwa mara kadhaa na hujaitika leo.
-- Gunia hili limejaa sana inafaa lipakuliwe.-- Imenyesha mchana kutwa
• Vihusishi (H)
Vihusishi ni maneno yanayoonyesha uhusiano baina ya watu au vitu viwili auzaidi. Kuna vihusishi vya mahali na vya wakati.
Mifano:
-- Tutaonana baada ya wiki moja .
-- Si vizuri kuishi kando ya mto.
-- Ng’ombe hulala ndani ya zizi.
-- Ameondoka hapa kabla ya mvua kunyesha.-- Wao wanaishi pamoja kwa amani.
KAZI 6
Tumia vihusishi vifuatavyo kwa kujaza mapengo: katika, kabla ya,
mbele ya, baada ya, pembeni mwa.
a) Miti ilipandwa................nyumba.
b) .................mvua kunyesha unaona dalili zake.
c) Watu wengi waliangamia ..............ajali ya ndege iliyotokea nchini
Kongo.
d) ...............kuondoka tulimfuata huko.e) Hakuna mtu anayeishi...............shimo siku hizi nchini Rwanda.
2.4. Matumizi ya lugha
KAZI 7
Jibu maswali yafuatayo
a) Mtu anapowakaribisha wengine karamuni anatumia nini?
b) Mtu anaweza kuwaalika wengine kwa madhumuni gani?
KAZI 7
Maelezo muhimu kuhusu barua za mwaliko
Maana ya barua za mwaliko
Barua ya mwaliko ni ujumbe unaotolewa kwa kumkaribisha mtu kuhudhuria
shughuli au hafla fulani. Barua za mwaliko zinaweza kuwa na madhumuni
yafuatayo:
Sherehe
Karamu
HarusiUbatizo
Sikukuu ya kufunga mwaka
Sikukuu ya kupata cheti au digrii
Kuadhimisha miaka fulani, n.k
Mambo ya kuzingatiwa katika uandishi wa barua ya mwaliko
Jina la mwalikwa
Sababu ya mwaliko
Mahali ukaribisho utakapofanyika, terehe na saa
Jina na anwani ya mkaribishaji
a) Mifano ya barua za mwaliko• Barua ya mwaliko kwenye harusi
Karibu sana!RWEMA Eric
2.5. Kusikiliza na Kuzungumza
KAZI 8
Shirikiana na wenzako mzungumzie kuhusu uandishi wa barua za mwaliko.2.6. Kuandika
KAZI 9Mkaribishe mwenzako kwenye sikukuu yako ya kuzaliwa
SOMO LA 3: MATANGAZO
KAZI 1
Tazama kwa makini mchoro ufuatao kisha ujibu maswaliyaliyotolewa hapo chini:
Jibu maswali yafuatayo:
–– Ni nini unachoona kwenye mchoro huu?–– Unafikiri kuwa mtu huyo mwenye kipazasauti anafanya nini?
3.1. Kusoma na ufahamu: Tangazo la ajira
Soma tangazo lifuatalo kisha ujibu maswali ya ufahamu.
TANGAZO LA AJIRA
Wilaya ya CHAPAKAZI inayo furaha ghaya ya kuwatangazia watu wote wenye
uwezo kwamba ina nafasi za ajira za ufundishaji katika shule za chekechea na
msingi. Nafasi hizo ni kama zifuatazo:
1. Walimu wa Kiswahili katika shule za msingi (nafasi kumi)
2. Walimu wa Kinyarwanda katika shule za msingi (nafasi tatu)
3. Walimu wa Hisabati katika shule za msingi (nafasi tano)
4. Walimu wa Kifaransa katika shule za msingi (nafasi tano)
5. Walimu wa Kiingereza katika shule za msingi (nafasi tano)
6. Walimu wa Mafunzo ya kijamii katika shule za msingi (nafasi tano)
7. Walimu wa Sayansi katika shule za msingi (nafasi mbili)
8. Walimu katika shule za chekechea (nafasi ishirini)
Anayehitaji kazi hizo anapaswa kuwa na sifa zifuatazo:
1. Kuwa Mnyarwanda,
2. Kuwa na astashahada ya ukufunzi (A2),
3. Kuwa na uwezo wa kutumia tarakilishi na vifaa vingine vya TEHAMA,
4. Kuwa na uwezo wa kutumia Kinyarwanda na Kiingereza kwa ujumla.
Kwa wakufunzi wa Kiswahili wanapaswa kuwa na uwezo wa kutumia
kinyarwanda, Kiingereza na Kiswahili. Wakufunzi wa Kifaransa wanapaswa
kuwa na uwezo wa kutumia Kinyarwanda, Kiingereza na Kifaransa.
5. Kuwa na afya bora,
6. Kuwa na umri usiozidi miaka thelathini,
7. Kuwa na uwezo wa kufanyia kazi katika eneo na mazingira yoyote.
Barua zenye maombi ya kazi pamoja na viambatisho vingine kama vile wasifu kazi,
kitambulisho cha uraia na astashahada, vitapokelewa hadi tarehe 20/12/2019katika ofisi ya katibu wa wilaya. Tarehe ya kusailiwa mtaijuzwa baadaye.
Tangazo limetolewa tarehe 1/12/2019.
Meya wa Wilaya ya Chapakazi
(Saini + mhuri)GAHIZI Musa
KAZI 2
Jibu maswali yafuatayo
Tangazo hili ni la aina gani?
Tangazo hili linalenga nani ?
Tangazo hili linatangaza nini ?
Neno TEKNOHAMA ni ufupisho wa nini ?Kwa sababu gani Meya wa wilaya alitia saini yake kwenye tangazo?
KAZI 3
3.2. Msamiati kuhusu tangazo
Eleza maneno yafuatayo :
-- Ajira
-- Shule za chekechea
-- Viambatisho
-- Astashahada-- Mhuri
3.3. Sarufi: Aina za maneno ya kiswahili
KAZI 4
Chunguza sentensi zifuatazo kisha utaje aina za maneno
yaliyopigiwa mistari.
-- Kobe na Kijumbamshale walikaa chini ya mti ili kuzungumza.
-- Lo! Umemwona mshamba yule!-- Fisi wala Simba hawakucheza mchezo wa riadha.
Maelezo muhimu kuhusu aina za maneno
KAZI 5
Soma maelezo yafuatayo kisha ujadili kuhusu matumizi ya maneno
yanayounganisha sentensi:
Katika lugha ya Kiswahili kuna aina nane za maneno. Aina hizo ni kama
vile nomino, kitenzi, kivumishi, kiwakilishi, kihusishi, kielezi, kiunganishi nakihisishi. Katika somo letu tutaona aina mbili yaani kiunganishi na kihisishi.
• Viunganishi (U)
Viunganishi ni maneno yanayofanya kazi ya kuunganisha. Huonyesha uhusiano
baina ya neno na neno, fungu moja la maneno na fungu jingine au sentensi na
sentensi.
Mifano:
a) Unataka maji au juisi?
b) Anasoma kitabu badala ya kupiga ubwana.
c) Kufanikiwa maishani si bahati bali ni kujishughulisha na kujitolea.
d) Alishinda mtihani ijapokuwa alipatwa na ugonjwa mkali.
e) Alienda shuleni bila kupata chakula.
KAZI 6
Tunga sentensi sahihi kwa kutumia viunganishi vifuatavyo:
a) Halafu
b) Kisha
c) Ili
d) Ingawae) Kama
• Vihisishi (I)
Vihisishi ni maneno ambayo yanaonyesha hisia za mtu za ndani kwa mujibu wa
hali na muktadha. Yanaonyesha hangaiko la moyo ama kudokeza mguso wamoyo ama hata wa akili.
Mifano:
Mtume! Umefika asubuhi hii!
Lo! Mvua imenyesha!Salaa! Inawezekana mtu kunywa chupa ishirini za juisi!
KAZI 7
Tunga sentensi sahihi kwa kutumia vihishi vifuatavyo:
a) Mungu wangu!
b) Mama wee!
c) Ng’o!
d) Barabara!e) Masalale
3.4. Matumizi ya lugha
KAZI 8
Soma upya tangazo la hapo juu kisha ujadiliane na wenzako kuhusu muundowa matanganzo.
Maelezo muhimu kuhusu matangazo
Maana ya tangazo
Tangazo au ilani ni mpangilio wa maandishi kwa mtindo maalumu kwa lengo la
kupasha habari ama kupokeza ujumbe fulani wa kidhalura au muhimu. Taarifa
inayosambazwa kwa tangazo inaweza kuwa kifo, mkutano, taratibu za kutumia
barabara vizuri, kazi na mengineyo.
Aina za matangazo
Zipo aina nyingi za matangazo
Matangazo ya kibiashara
Matangazo ya kifo
Matangazo ya serikali, n.k.
Mambo ya kuzingatiwa katika uandishi wa matangazo
Kwa kuandika tangazo ni lazima kuzingatia mambo yafuatayo :
Kichwa cha tangazo
Kutaja anayetoa tangazo
Kutaja walengwa wa tangazo
Ujumbe wa tangazo
Sahihi na jina la anayetoa tangazo (tangazo lisilokuwa na sehemu hii huitwa
tetesi, fununu au uvumi)Mfano wa tangazo
3.5. Kusikiliza na Kuzungumza
KAZI 9
Sikiliza matangazo redioni kisha ujadiliane na wenzako kwakuzingatia maudhui, aina ya matangazo na lugha iliyotumiwa.
3.6. Kuandika
KAZI 10Tunga tangazo la kibiashara
Tathmini ya mada
1. Eleza maana ya barua.
2. Taja aina za barua tulizoona.
3. Zitaje sehemu kuu za barua ya kirafiki.
4. Ni mambo gani muhimu yanayopaswa kuonekana kwenye barua ya
mwaliko?
5. Tunga tangazo la kazi.
6. Taja aina za meneno yanayojenga sentensi zifuatzo.
-- Eeh! Unataka kitu gani?
-- Wao walikufa hapa na kuondoka haraka.
-- Mama alikuwa akipalilia maharagwe yake katika bonde lile.
-- Ingawa mvua ilinyesha vizuri, mavuno yanaendelea kudidimia.-- Chukua hicho kizuri ila hakitoshi.
MADA YA 2: UTUNGAJI WA BARUA RASMI
Uwezo mahususi
Kuandika barua rasmi kwa ufasaha
Malengo ya Ujifunzaji
-- Kubainisha sehemu kuu za barua rasmi;
-- Kutunga barua rasmi kwa ufasaha;
-- Kutunga sentensi sahihi kwa kutumia kirejeshi – po - .
SOMO LA 4: TARATIBU ZA KUTUNGA BARUA RASMI
KIDOKEZO
4.1. Kusoma na ufahamu: Barua ya kuomba kazi
Maswali ya ufahamu
KAZI 1
Soma kifungu cha habari hapo juu na ujibu maswali ya ufahamu
yafuatayo:
1. Mwandishi wa barua hii ni nani?
2. Mwandishi huyu anaishi wapi?
3. Amemwandikia nani?
4. Nini lengo la barua yake?
5. Mwandishi amemshawishije mwandikiwa?
KAZI 2
Chagua jibu lililo sahihi kuliko mengine
1. Mwandishi ana tajiriba ya:
a) Miaka miwili
b) Cheti cha ualimu
c) Kuomba kazi
d) Miaka miwili ya kufundisha katika shule za msingi.
2. Baadhi ya vitambulisho vilivyoambatishwa kuna:
a) Ombi la kazi
b) Cheti cha ualimu pamoja na nakala ya kitambulisho cha uraia
c) Kitambulisho cha mwajiri wa mwisho
d) b na c ni sahihi
3. Mwombaji kazi anaamini kuajiriwa kwa sababu:
a) alijifunza ualimu.
b) ana tajiriba ya kutosha katika ualimu na uwezo wa kutumia kompyuta.
c) ana tajiriba katika ualimu katika shule za msingi pamoja na uwezo wa
kutumia kompyuta.
d) ana mbinu nzuri za kutimiza kazi yoyote.
4. Kweli au uongo/sikweli
a) Bila shaka Ndizeye ataajiriwa kwenye Shule ya Msingi Mukingi.
b) Ndizeye ni mwalimu mwerevu sana na mwenye uwezo sana.
c) Atakapoajiriwa kwenye alipoomba kazi wanafunzi wote watafaulu
mitahani yao.
d) Cheti cha ualimu ni kitambulisho pekee kinachofaa kupata ajira ya ualimu.
e) Kufaulu mitihani kwa wanafunzi hutegemea jinsi mwalimu anavyotumia
vizuri mbinu shirikishi za ujifunzaji na ufundishaji.
4.2. Matumizi ya msamiati
KAZI 3
Jaza sentensi zifuatazo kwa kutumia msamiati huu: kuhitimu,
uthibitisho, tarakilishi, kutimiza, feli, nakala
1. Wanafunzi wanaombwa kufanya bidii ili wasi.............................majaribio
na mitihani yao.
2. ...............................ni kifaa cha kiteknolojia kinachorahisisha leo kazi ya
mawasiliano kwa kupitia njia ya maandishi.
3. Unapoomba kazi ni lazima kutoa ...................za vyeti na vitambulisho
vingine muhimu vya..............................
4. Katika barua yake ya kuomba kazi, Ndizeye aliahidi...........................
wajibu wake ipasavyo.
5. Baada ya .......................masomo yake ya ualimu, Ndizeye alipata kazi
kwenye Shule ya Msingi Mukingi.
4.3. Sarufi: Matumizi ya kirejeshi – po -
KAZI 4
Eleza matumizi ya mofimu yenye wino uliokolea
i) Mahali tunapoishi ni pasafi.
ii) Mahali ambapo panapatikana mbu ndipo panapoweza kuhatarisha
maisha ya binadamu.
iii) Mahali walipokaa palikuwa na utulivu.
iv) Mahali wezi hujifichapo hapajulikani.
MAELEZO MUHIMU
- Po – ni kiambishi rejeshi cha mahali. Kwa kawaida hujihusisha na majina ya
ngeli ya PA-M-KU na kutumiwa kama ifuatavyo:
-- Katikati ya kiambishi nafsi cha kitenzi na mzizi wa kitenzi.
-- Kwenye mzizi wa amba- na ndi-.
-- Mwishoni mwa kitenzi.
Tanbihi: Katika wakati ujao, kirejeshi –po- husababisha kiambishi –ka-.
Mfano: Utakapofika utanipigia simu.
Wakati wowote mtakapokata tamaa mtafeli mitihani yenu.
Mifano mingine:
i) Mahali nitakapoajiriwa nitafanya bidii.
ii) Mahali ambapo panapatikana mbu panaweza kuhatarisha maisha ya
binadamu.
iii) Nipo tayari kuwasili wakati wowote nitakapohitajika.
iv) Hapa ndipo patakapopandwa miti kwa ajili ya kuhifadhi mazingira.
v) Mahali nitakapoajiriwa nitafanya bidii.
vi) Mahali ambapo panapatikana mbu panaweza kuhatarisha maisha ya
binadamu.
vii) Nipo tayari kuwasili wakati wowote nitakapohitajika.
viii) Hapa ndipo patakapopandwa miti kwa ajili ya kuhifadhi mazingira..,
KAZI 5
Unganisaha sentensi zifuatazo kwa kutumia kirejeshi –poi)
Tunakaaa mahali pengi. Mahali papo ni penye raha.
ii) Mahali pale panajulikana kama Eldorado. Ni pazuri sana.
iii) Tulitembelea mahali penye mbugaza wanyama.
iv) Walijenga nyumba mahali penye harufu nzuri.
4.4. Matumizi ya lugha: Mwongozo wa kutunga barua
rasmi
Maelezo muhimu
a) Maana ya barua rasmi:
Barua rasmi au barua za kiofisi ni barua ambazo zinahusu mambo ya kiofisi kama
vile taarifa za mikutano, kuomba kazi, kuagiza vifaa vya shughuli nyingine rasmi.
b) Aina za barua rasmi
Barua rasmi zipo za aina nyingi lakini zinaweza kugawanyika katika makundi au
mafungu matatu makubwa yafuatayo:
1. Barua za taarifa
2. Barua za maombi mbalimbali
3. Barua za upokeaji vifaa.
c) Mtindo wa barua rasmi:
Barua rasmi huandikwa kuelezea ujumbe maalumu, kwa hiyo huhitaji kuandikwa
kwa uangalifu na umakini wa kutosha. Ni muhimu kuandika jambo husika waziwazi
na kuepuka maelezo yasiyo muhimu, kama vile salamu na kadhalika. Mwandishi
analazimika kuandika kwa ufupi na lugha nyepesi. Barua rasmi huwa na sentensi
chache tena fupi, na ni lazima kufuata taratibu za uandishi, sentensi ziwe kamili.
d) Lugha ya barua rasmi:
Tofauti na lugha ya barua ya kirafiki, barua rasmi hutumia lugha fupi
na mwandishi hulenga mada mara moja bila kuzungukazunguka. Kwa mfano,
kama minajili yako ni kuomba hela za kulipa karo ya shule kama barua hii ya
EssayVikings, hutazungukazunguka. Utayataja madhumuni ya barua mara moja.
Lugha yenyewe huwa nyepesi kuelewa na haina misimu. Unapoandika barua
ya kirafiki, waweza kutumia misimu ambayo mwandikiwa ataelewa kwa sababu
ni rafiki yako. Katika barua rasmi, hili halifanyiwi. Mwandikiwa si rafiki yako na
huenda ikawa humjui. Pia yafaa usome barua yako vizuri kabla ya kuituma ili
isiwe na makosa ya tahajia au lugha.
e) Mtindo wa barua rasmi:
Barua rasmi huandikwa kueleza ujumbe maalumu, kwa hiyo huhitaji kuandikwa
kwa uangalifu wa umakini wa kutosha. Ni muhimu kuandika jambo husika
waziwazi na kuepuka maelezo yasiyo muhimu, kama vile salamu na kadhalika.
Mwandishi analazimika kuandika kwa ufupi na lugha nyepesi. Barua rasmi huwa
na sentensi chache tena fupi, na lazima kufuata taratibu za uandishi, sentensi
ziwe kamili.
f) Lugha ya barua rasmi: Tofauti na lugha ya barua ya kirafiki, barua
rasmi hutumia lugha fupi na mwandishi hulenga mada mara moja bila
kuzungukazunguka. Kwa mfano, kama minajili yako ni kuomba hela za
kulipa karo ya shule kama barua hii ya Essay Vikings, hutazungukazunguka.
Utayataja madhumuni ya barua mara moja. Lugha yenyewe huwa nyepesi
kuelewa na haina misimu.
Unapoandika barua ya kirafiki, unaweza kutumia misimu ambayo mwandikiwa
ataelewa kwa sababu ni rafiki yako. Katika barua rasmi, hili halifanyiki. Mwandishi
si rafiki yako na huenda ikawa humjui. Pia, yafaa usome barua yako vizuri kabla
ya kuituma ili isiwe na makosa ya tahajia au lugha.
KAZI 6
Jadili muundo wa barua rasmi
Muundo wabarua rasmi
Anwani ya mwandishi huandikwa katika barua yake juu, kwenye pembe ya
upande wa kulia wa karatasi.
Tarehe: hii huandikwa upande wa kulia wa karatasi katika mstari uleule
wa kumbukumbu namba ya barua kama ipo; tarehe iwe chini ya anwani ya
mwandishi
Kumbukumbu namba: hii ni namba ambayo huwa kama kitambulisho cha
barua; mara nyingi huwa na tarakimu pamoja na herufi, kwa mfano: SRB MD 05.
Anwani ya mwandikiwa: hii hutangulia na cheo cha mwandikiwa na huandikwa
katika mkono wa kushoto, chini ya namba ya kumbukumbu.
Mwanzo wa barua: huandikwa chini ya anwani ya mwandikiwa; mara
nyingi neno ndugu hutumika kama salamu au mwanzo wa barua.
Kichwa cha barua: Hutangulizwa na maneno kama vile KUHkuhusu),
MINTmintarafu). Ni sharti kiachwe kiandikwe kwa herufi kubwa na kipigiwe
mstari. Kichwa kinapaswa kuwa kifupi na kinachoelezea mada ya barua
kiukamilifu.
Barua yenyewe: hii huandikwa mambo yote muhimu kuhusu barua yenyewe,
barua iwe fupi na taarifa muhimu tu.
Mwisho wa barua huwa ni kimalizio cha barua: ni tamko la heshima la kumalizia
barua; mara nyingi miisho ambayo hutamkwa ni kama vile, “wako mtiifu”, “wako
katika kazi”, “wako katika kujenga taifa”, “wako mwanachama”.
Saini au jina la mwandishi: baada ya kimalizio cha barua mwandishi atie
saini yake, kisha jina lake kwa ukamilifu.
Cheo cha mwandishi: mwisho wa barua, chini ya jina la mwandishi huandikwa
cheo cha aliyeandika barua; cheo chaweza kuwa ni mwombaji, mwalimu wa
darasa, mwanafunzi, kiranja mkuu, waziri wa elimu, mjumbe wa tawi, n.k.
4.5. Kusikiliza na Kuzungumza
KAZI 7
Fikiria barua moja rasmi uliyowahi kuisoma na kuizungumzia
hadharani.
4.6. Kuandika
KAZI 8
Rejelea hapa chini mfano wa barua rasmi. Bainisha makosa ya
kimuundo na kuyasahihisha.
12/12/2019.
GATETE, S.L.P. 2345, PAUL
SIMU +2507345621876, KIGALI.
Kumb.Nb 003
KWA MKURUGENZI MKUU,
SHAMBA LA MIKAHAWA LA USANASE, S.L.P. 3000,
RUHANGO.
Kwa Bi. Ituze,
MINT: Kuomba Nafasi ya kuwa meneja wa uzalishaji kahawa
Narejelea tangazo kutoka Gazeti la Mkulima Bora, toleo la siku ya Ijumaa
tarehe 6, Desemba, 2019, kuhusu kuwepo kwa nafasi niliyotaja hapo juu
nikiomba nizingatiwe. Mimi ni Mnyarwanda na ninapenda sana kilimo hasa
cha mikahawa. Kwa miaka zaidi ya kumi, nimekuwa nikijihusisha katika
kuwahamasisha wanakijiji kuhusu mbinu bora za kuimarisha kilimo cha
mikahawa. Kwa sasa, kijiji chetu kinaongoza katika uzalishaji wa mikahawa
mingi yenye thamani ya juu zaidi.
Nimefanya utafiti kuhusu mbinu za kisasa za kuimarisha uzalishaji wa
mikahawa na ninatumai kuwa maarifa niliyonayo yatakufaidi katika kukuza
uzalishaji wa kahawa.
Natazamia mawasiliano kutoka kwako wakati wowote.
wako mwaminifu,
Paul Gatete.
Saini
KAZI 9
Rejelea mfano wa barua rasmi kuhusu ombi la kazi ya hapo juu. Tunga barua
yako kwa Waziri wa Elimu kwa ajili ya kuomba kuendendelea na masomo
katika Chuo Kikuu cha Ualimu.
Tathmini ya mada
7. Nini maana ya barua rasmi?
8. Jadili muundo wa barua rasmi.
9. Zungumzia aina za barua rasmi.
10. Andika barua rasmi kwa mkuu wa shule kuhusu ombi la maandalizi
ya mazoezi ya ufundishaji.
11. Tunga sentensi angalau mbili mbili kwa kila nafasi ya matumizi ya
kirejeshi –po-, yaani katikati ya kiambishi nafsi cha kitenzi na mzizi
wa kitenzi, kwenye mzizi wa amba- na ndi – pamoja na mwishoni
mwa kitenzi.MADA YA 3 :MIDAHALO
Uwezo mahususi
Kushiriki vilivyo katika midahalo, kuongoza na kutoa hoja kwa kutetea aukupinga mawazo yaliyotolewa.
• Malengo ya ujifunzaji
-- Kutoa maana ya mdahalo
-- Kubainisha sifa za mdahalo mzuri
-- Kuonesha mbinu au taratibu za mdahalo
-- Kueleza umuhimu wa mdahalo
-- Kutaja masuala mtambuka mbalimbali yaliyozungumziwa katika midahalo.
-- Kueleza maana ya viambishi rejeshi-- Kuorodhesha viambishi rejeshi
KIDOKEZO
Tazama mchoro ufuatao kisha ujibu maswali yaliyo hapo chini yake
Maswali
1. Elezea yale unayoyaona kwenye mchoro2. Watu hawa wanafanya nini?
SOMO LA 5. MAANA YA MDAHALO
5.1. Kusoma na ufahamu: Utekelezaji wa elimu ya
kujitegemea kwa vijana
Soma mdahalo ufuatao wenye mada “ Utekelezaji wa elimu ya
kujitegemea kwa vijana wa leo ni dhaifu zaidi kuliko ule wa vijana wa
miaka iliyopita ”, kisha ujibu maswali yaliyotolewa hapo chini.
Mwenyekiti (anasimama): Waheshimiwa mabibi na mabwana mliokusanyika
hapa hivi leo, hamjambo? Mada ya mdahalo wetu wa leo ni kama mnavyoiona
ubaoni ni“Utekelezaji wa elimu ya kujitegemea kwa vijana wa leo ni dhaifu zaidi
kuliko ile ya vijana wa miaka iliyopita.”
Mimi jina langu ni Kabatesi, mwenyekiti wa mdahalo. Niko pamoja na Gahizi
kama katibu wa mdahalo wetu pamoja na Uwase atakayechunga muda. Vilevile
tuna pande mbili hapa. Timu moja inatetea mada na nyingine inapinga mada.
Bila ya kuchelewa Napenda kumkaribisha bwana (anataja jina lake) ambaye ni
msemaji mkuu wa kwanza upande wa utetezi ili atoe hoja zake kuhusu mada
yetu ( anakaa).
Msemaji wa 1 (Utetezi): Mheshimiwa mwenyekiti na washiriki wote, ni wazi
kabisa kwamba hali ya elimu ya kujitegemea si dhaifu kwa vijana wa leo kama
mada isemavyo vijana wa leo wameenda shule, wameanza wakiwa wadogo,
wameendelea na masomo hadi chuo kikuu na kuhitimu itakiwavyo kiasi kwamba
wanaweza kufanya kazi katika nyanja mbalimbali zinazohitajika katika harakati za
kulijenga taifa. Vijana wa leo wana mishahara minono. Mheshimiwa Mwenyekiti,
waheshimiwa wote mnaoshiriki katika mdahalo huu; haya ni baadhi ya mambo
mengi yanayoweza kututhibitishia kwamba vijana wa leo hushiriki vizuri katika
kutekeleza elimu ya kujitegemea.
Mwenyekiti: Naam, wasikilizaji washiriki. Nafikiri baada ya kusikiliza hoja za
msemaji mkuu
wa kwanza upande wa utetezi, sasa ningependa kumkaribisha msemaji mkuuwa kwanza upande wa upinzani naye atowe hoja zake. Karibu!
Msemaji wa 1 (Upinzani): Asanteni sana mwenyekiti na wasikilizaji washiriki.
kwa kunipa fursa hii. Sikubaliani na hoja za mtetezi wa mada hii. Msemaji
aliyetangulia alisema kwamba vijana wa leo wanaanza kusoma wangali wadogo
na kufikia viwango vikubwa na kupewa shahada za hali ya juu pamoja na
mishahara minono kuliko wa miaka iliyopita. Vijana wa miaka iliyopita walikuwa
na namna yao ya kufanya kazi walikuwa wanajituma na walifanya kazi bila
usimamizi au unyampala, walikuwa si wavivu, vijana wa leo baadhi yao ni wavivu
kazi haiwezi kufanyika bila kuwa na mtumishi nyumbani kwao, ambapo vijana wa
miaka iliyopita walijituma kwa shughuli yoyote ile iliyohitaji ujenzi wa taifa, kama
kuwinda, kwenda vitani, pia kuliwasidia wale wasiojiweza, n.k Nashukuru sana
kwa kunisikiliza.
Mwenyekiti: Naam! Mambo yameanza kupamba moto. Baada ya kusikiliza
hoja za wasemaji wakuu wa kwanza kutoka pande zote mbili ningependa
kumkaribisha msemaji mkuu wa pili kwa upande wa utetezi ili naye atoe hoja
zake.
Msemaji wa 2 (Utetezi): Asante sana mwenyekiti, wenzangu watetezi na
mahasimu wangu wapinzani pamoja nanyi wasikilizaji-washiriki. Ni wazi kwamba
utekelezaji wa elimu ya kujitegemea kwa vijana wa leo ni dhaifu zaidi kuliko ile
ya vijana wa miaka iliyopita. Hili ni kwa sababu vijana wa leo hawawezi kufanya
kazi bila kulazimishwa. Lakini vijana wa zamani walikuwa wakijituma katika
kutekelza kazi zote ili kuendeleza nchi. Kazi hizo hasa zilikuwa za kilimo, ujenzi
na kazi nyingine za mikono. Vijana wa leo wao huogopa kutumia mikono yao. Je
tutaendeaje? Haviwezekani. Asante sana.
Mwenyekiti: Naam! Wapinzani mmekubali? Au mtashikilia shindano? Msemaji
wa pili, fursa kwako!
Msemaji wa 2 (upinzani): Asante sana mwenyekiti na nyinyi nyote ambao
mmekusanyika hapa leo hii. Sisi wapinzani hatukubaliani na maoni ya watetezi
hata kamwe! Je? Mnasema kuwa vijana wa leo hawafanyi kazi lakini siku hizi
ndipo unaona kuwa kazi mpya zinabuniwa ilhali hapo zamani mtoto alikuwa
akifuata kazi ya wazazi wake. Kama wahenga walivyosema “Mtoto wa mhunzi
asiposana huvukuta”. Vilevile hapo zamani vijana waliokuwa wakitoka shuleni
walikuwa wakisuburi kazi kutoka kwa serikali. Lakini leo mambo ni kinyume.
Hatusubiri kazi za ofisini tunabuni nyingine mpya na kuajiri vijana wenzetu. Je
huo si utekelezaji thabiti wa elimu ya kujitegemea? Asante sana.
Mwenyekiti: Mambo yamekuwa shamrashamra kweli! Lakini ninaona kwamba
muda hauturuhusu kusonga mbele. Hoja nzuri zimetolewa kwa kila upande
lakini tunahitaji mshindi wa leo. Kwa hiyo ningependa kumkaribisha katibu
aje atupigishe kura ili tujuwe mshindi wa leo. (Katibu anasimama na kuomba
wanaotetea wanyoshe mikono na wanaopinga wafanye hivyo baadaye na
kuhesabu kura).
Katibu: Upande wa utetezi umepata kura kumi na tano. Upande wa upinzani
umepata kura ishirini na moja. Kwa hiyo washindi wa mdahalo wa leo ni upande
wa upinzani. (Wasikilizaji washiriki wanawapigia makofi.)
Mwenyekiti: Mabibi na mabwana, baada ya matokeo haya sina budi kuwaambia
kuwa huu ni mwisho wa mdahalo wa leo. Tukutane wakati ujao panapokuwamajaliwa ya Mungu.
KAZI 1
Maswali ya ufahamu
1. Andika kichwa cha mada ya hapo juu.
2. Ni pande gani zinazoonekana katika mdahalo huu?
3. Eleza hoja za mtetezi wa kwanza katika mdahalo huu.
4. Eleza jinsi vijana wa miaka iliyopita walivyoweza kujituma.5. Kwa sababu gani wapinzani walishinda ?
5.2. Msamiati kuhusu mdahalo
KAZI 2
Unganisha maneno ya safu A na maana yake katika safu Bkutokana na jinsi yalivyotumika katika kifungu cha habari .
KAZI 3
Tunga sentensi zenye maana kamili kwa kutumia maneno
yafuatayo yaliyotumika katika kifungu cha ufahamu:
1. Kutetea
2. Kujituma
3. Katibu
4. Mwenyekiti5. Kusikiliza
5.3. Sarufi: Matumizi ya viambishi rejeshi kulingana nangeli za majina
KAZI 4
Angalia mifano ya sentensi zifuatazo kisha ueleze viambishi
vilivyopigiwa mistari.
1. Mwenyekiti aliyeongoza mdahalo wa jana alikuwa msomi.
2. Wanafunzi- walimu watakaoshinda vizuri watazawadiwa.
3. Vijana waliokuwa wakitoka shuleni walikuwa wakisubiri kazi kutoka
kwa serikali.
4. Kazi nyingi zilizobuniwa ni za vijana.
• Viambishi vilivyopigiwa mistari ni virejeshi au viambata.
Maelezo muhimu kuhusu virejeshi/viambata
Kirejeshi ni kiambishi kinachotiwa katika kitenzi ili kurejerea tendo kwa
mtendaji. Ni kusema kuwa kirejeshi hujulisha kwamba jina/kiwakilisha
kilichotajwa ndicho kilichofanya/kinachofanya/hufanya/kitakachofanya au
kilichofanyiwa’kinachofanyiwa/hufanyiwa/kitakachofanyiwa jambo fulani. Jina/
kiwakilishi kinachorejelewa hutangulia kitenzi.
Isipokuwa kwenye ngeli ya A-WA katika umoja mahali ambapo kirejeshi huwa –
ye mahali pengine kirejesshi ni –o kikabadilika kulingana na ngeli za majina kamajedwali lifuatalo linavyoeleza :
KAZI 5
Jaza kwa kutumia kirejeshi kilicho mwafaka
1. Kitabu uli…nipa kimenifurahisha.
2. Mwendo una…kwenda utakuponza.
3. Jino daktari ataka…ng’oa ni hili bovu.
4. Saa ili------tundikwa ukutani imeanguka.5. Mwenyekiti ataka…ongoza mdahalo amefika.
5.4. Matumizi ya Lugha: Maana ya MdahaloKAZI 6
Soma maelezo muhimu yafuatayo kisha ujibu maswali ya hapo
chini
Mdahalo ni majadiliano baina ya watu wengi juu ya jambo moja maalumu.
Kuna mada inayozungumziwa, wazungumzaji wakuu wanaotetea mada
(upande wa utetezi) na wazungumzaji wakuu wengine wanaopinga mada
(upande wa upinzani). Aghalabu huwa wazungumzaji wakuu wawili kwa kila
upande.
Mwenyekiti wa mdahalo ana wajibu wa kufungua na kuendesha mdahalo,
kuwapa wasemaji nafasi ya kuzungumza, kupigisha kura na kufunga mdahalo.
Katibu wa mdahalo ndiye huandika hoja zinazotolewa na wazungumzaji
mbalimbali, kufanya na kusoma muhtasari wa hoja zilizotolewa na pande
mbili mwishoni mwa mdahalo na kutangaza matokeo ya kura zilizopigwa.
Mdahalo ukifanyiwa darasani, mwalimu atatoa maoni yake juu ya mdahalo.
Mdahalo mzuri unaonesha namna ya kuchagua mada inayoleta hoja nyingi
tofauti (mada hii inapaswa kuwa ile inayoleta mchango fulani katika maisha
ya jamii, uongozi mzuri wa mwenyekiti na umahiri wa wanaozungumza katika
utafutaji na utoaji wa hoja ndivyo baadhi ya vipengele vinavyochangia katika
kuboresha mdahalo.
Jibu maswali yafuatayo:
1. Ni lipi jukumu la mwenyekiti wa mdahalo?
2. Katibu ana jukumu lipi katika mdahalo?
3. Kuna aina ngapi za wazungumzaji katika mdahalo? Zitaje4. Ni zipi sifa za mdahalo mzuri?
5.5. Kusikiliza na Kuzungumza
KAZI 7
Andaa mdahalo kisha uwasomee wenzako msimamo wako kuhusumada isemayo:
«Kazi za ofisini ndizo zinazoendeleza uchumi wa nchi yetu. »
5.6. Kuandika
KAZI 8Tunga mdahalo kuhusu mada ifuatayo :
“Usawa wa jinsia ndiyo njia sahihi ya kuendeleza nchi yetu”
SOMO LA 6: MWONGOZO WA MDAHALO
KAZI 1
Tazama mchoro hapo juu kisha ujadili unayoyaona yakitendeka kwenye
mchoro husika.
6.1. Kusoma na ufahamu: Tutokomeze dawa za kulevya
Soma mdahalo ufuatao kisha ujibu maswali ya ufahamu.
“Wazazi wana wajibu mkubwa katika kutokomeza dawa za kulevya
zinazoharibu vijana.”
Mwenyekiti: Waheshimiwa wote mabibi na mabwana mliokusanyika hapa,
kwanza ninataka niwakaribisheni kwenye mdahalo usemao kuwa “Wazazi wana
wajibu mkubwa katika kutokomeza dawa ya za kulevya zinazoharibu
vijana.” Karibuni sana nyote na bila kupoteza muda, ninamkaribisha mshirikiupande wa utetezi kutoa mchango wake.
Msemaji wa 1 (Upande wa utetezi): Ninawashukuru sana viongozi,
wasikilizaji na washiriki wenzangu. kuniruhusu kuzungumzia mada isemayo
“Wazazi wana wajibu mkubwa katika kutokomeza dawa za kulevya
zinazoharibu vijana.” Kama inavyojulikana elimu ya kwanza ya mtoto huanzia
nyumbani. Nyumbani ndipo mtoto anapopata malezi ya msingi ambayo huanzia
uimarishaji wa msingi wa malezi. Malezi haya ya kwanza ambayo hupatikana
nyumbani humsaidia na kumuimarisha mtoto katika kufanikiwa katika maisha
yake. Kwa hiyo wazazi wakitoa malezi bora vijana wataepukana na utumiaji wa
madawa ya kulevya.
Mwenyekiti: Asante sana kwa mazungumzo mazuri. Kama mlivyosikia, msemaji
huyu ameeleza kwamba wazazi ndio wenye jukumu la kuwapatia watoto wao
uimalishaji imara wa elimu ya mtoto kutokana na haya ndio wenye wajibu mkubwa
katika kutokomeza madawa ya kulevya. Sasa ebu nitoe fursa kwa mshiriki wa
upande wa upinzani.
Msemaji wa 1 (Upande wa upinzani): Asante sana kiongozi kwa fursa hii ya
kuniruhusu kutoa mchango wangu. Kwa maoni yangu, ni kweli kwamba wazazi
wana nafasi kubwa kwa watoto wao na hasa wale walio wadogo kuanzia
chekechea . Lakini, kwa wale walio wakubwa kuna matatizo makuu ambayo
wazazi hawawezi kutilia mkazo kwani watoto hao hawashindi na wazazi wao,
wengine wako shule za sekondari wengine wanajipangia nyumba zao za kuishi
wakati wa kusoma shule; kwa hiyo naona jukumu kubwa ni la walimu katika
kutokomeza madawa ya kulevya yanayoharibu vijana. Hili ni kwa sababu walimu
ndio wanaoshinda na watoto hao muda mrefu. Kwa hiyo walimu wakiwafuatilia
karibu wanaweza kuepukana na madawa hayo nao wakatoa mchango wao
katika kuendeleza nchi.
Mwenyekiti: Ninamshukuru sana mshiriki upande wa upinzani. Ameelezea
kwamba jukumu
kubwa katika kutokomeza madawa ya kulevya yanayoharibu vijana ni kazi ya
walimu ambao huwa na vijana hawa muda wote wa masomo. Hebu, tumsikilize
pia mshiriki aliyenyosha mkono pale upande wa utetezi .
Msemaji wa 2 (Upande wa utetezi): Ninawashukuru Mheshimiwa
kiongozi,wasikilizaji na washiriki wenzangu. Watu ambao wako karibu sana
na watoto ni wazazi wao ambao wana mchango wa kwanza katika malezi ya
watoto hao. Wazazi huwatunza watoto wao, tangu wanapozaliwa na wakati
wa kwenda shule unapofika, wao ndio wanapiga hatua ya kwanza kuwapeleka
shuleni. Wajibu wa kila mzazi ni kupeleka mtoto wake shuleni kwani anapata
mwenendo mwema utakaomsaidia maishani mwake. Watoto wanapofika
shuleni, ni vyema wazazi wao wawajibike kufuatilia malezi, nidhamu na matendo
ya watoto wao kwa kuwashauri, kuwafundisha kuwa na mienendo mizuri.
Waheshimiwa wasikilizaji, kama mnavyoelewa, bila mchango wa wazazi, vita hivi
dhihi ya dawa za kulevya vitatushinda. Je mtoto anapokuwa likizoni, atampata
wapi mwalimu wa kumkanya? Au anapotoka shule jioni na kuelekea nyumbani
mwalimu atamsindikiza? Tunaposema mzazi hatusemi yule aliyemzaa mtoto tu!
Hapa tunataka kusema kila mtu mzima anayekutana na mtoto huyu. Akimwona
katika matendo maovu vizuri amkanye. Wazazi wakifanya haya visa vile vya
wizi, madawa ya kulevya, utovu wa nidhamu hautakuwepo kwa sababu wazazi
watakuwa wakiwafuatilia karibu watoto wao. Asante sana kwa kunitega sikio,
hayo ndiyo maoni yangu.
Mwenyekiti: Baada ya kusikiliza hoja za msemaji mkuu wa pili kwa upande
wa utetezi, ningependa kumpa fursa msemaji wa pili upande wa upinzani. Karibu
ndugu!
Msemaji wa 2 (Upande wa upinzani): Asante sana mwenyekiti kwa kunipa
fursa hii. Mimi sina mengi ya kusema kwa kuwa msemaji wa kwanza mwenzangu
amesema mengi. Na ninafikiri kuwa yanatosha. Asante sana.
Mwenyekiti: Naam! Baada ya kusikiliza hoja za wasemaji wakuu wa pande
zote mbili yaani upande wa utetezi na upande wa upinzani, tutafanya uchaguzi ili
tuone ni upande upi ambao umeshinda safari hii. Tutapiga kura kwa kunyoosha
mikono kisha katibu atahesabu kura.
Katibu: Upande wa utetezi umepata kura kumi na tano (aandike 15 ubaoni).
Upande wa upinzani umepata kura kumi (anaandika 10 ubaoni).
Mwenyekiti: Mabibi na mabwana, baada ya matokeo haya kura zinaonyesha
kuwa ushindi katika mdahalo huu umeangukia upande wa utetezi (ukumbi
uliwapigia makofi washindi na mwalimu wa somo akatoa maoni yake juu ya
mdahalo huo. na ukawa mwisho wa mdahalo)
KAZI 2
Maswali ya ufahamu
1. Taja mada inayozungumziwa katika mdahalo.
2. Kuna makundi ya aina ngapi katika mdahalo huu ?
3. Mtetezi wa pili alieleza kuwa mzazi ni nani ?
4. Ni upande gani ulioshinda? Kwa sababu gani?
5. Mdahalo ulimalizika kivipi?
6.2. Msamiati Kuhusu mdahalo
KAZI 3
Tunga sentensi sahihi kwa kutumia maneno yafuatayo:
-- Wajibu
-- Kutokomeza
-- Jukumu
-- Mienendo
-- Ukumbi
6.3. Sarufi: Matumizi ya viambishi rejeshi kulingana na
ngeli za majina.
KAZI 4
Chunguza sentensi zifuatazo kisha ueleze mabadiliko
yanayojitokeza
1. Mwenyekiti ambaye aliongoza mdahalo wa jana alikuwa msomi.
2. Mwenyekiti aliyeongoza mdahalo wa jana alikuwa msomi.
3. Binadamu ambao huishi kwa amani na wenzao pamoja na mazingira
yao husifika.
4. Binadamu waishio kwa amani na wenzao pamoja na mazinira yao
husifika.
Maelezo muhimu
Kirejeshi ni kiambishi kinachotiwa katika kitenzi ili kurejerea tendo kwa mtendaji.
Ni kusema kuwa kirejeshi hujulisha kwamba jina lililotajwa ndilo lililofanya au
lililofanyiwa jambo fulani.
Tunapotumia amba- haturuhusiwi kutumia kirejeshi hii ni kwa sababu ambainasimama
sawasawa na kirejeshi. Kwenye vishirikishi vipungufu na kwenye
kitenzi katika wakati wa mazoea, kirejeshi huja mwishoni.
Mifano
1. Mkufunzi ambaye alitufundisha Kiswahili mwaka jana amehama.
2. Mkufunzi aliyetufundisha Kiswahili mwaka jana amehama.
3. Mvua ambayo hunyesha kila siku si nzuri.
4. Mvua inyeshayo kila siku si nzuri.
5. Ni huku ambako tulikuwa tukizungumzia.
6. Huku ndiko tulikokuwa tukizungumzia
KAZI 5
Ondoa amba- katika sentensi zifuatazo:
1. Gari ambalo tulisafiria lilikuwa na hitilafu.
2. Mchuzi ambao tulikunywa ulipikwa kwa ustadi.
3. Amani ambayo sisi Wanyarwanda tunayo tuyatunze vyema.
4. Nyumba ambazo tutazijenga ziwe na viwango vya kujengea nyumba.
5. Mazingira ambayo tunastahili kuishi ndani ni yale yenye hewa safi.
6.4. Matumizi ya lugha: Mwongozo na utekelezaji wa
mdahalo
KAZI 6
Soma maelezo muhimu hapo chini kisha ujibu maswali yanayofuata:
Maandalizi ya mdahalo
a) Kuchagua mada ya kuzungumzia katika mdahalo: uchaguzi huu
hufanyika kwa kupiga kura.
b) Kumchagua mwenyekiti wa mdahalo: mwenyekiti huchaguliwa kwa
kupiga kura na atakayechaguliwa ni yule mwenye uwezo wa kuongoza
na kuendesha mdahalo.
c) Kumchagua katibu wa mdahalo: mhusika huyu pia huchaguliwa, yeye
ana wajibu wa kuandika na kuwasomea hadhira muhtasari na matokeo
ya mdahalo.
d) Kumchagua mtunzawakati: huyu ana jukumu la kuchunguza kwamba
kila mhusika anatumia muda aliopewa katika kutoa hoja zake.
e) Kupanga wahusika kwa upande wa utetezi na upande wa upinzani
kama wasemaji wakuu wa pande hizo.
f) Kupanga namna ya kukaa kwa wahusika wa mdahalo upande wa
utetezi na upande wa upinzani na wasikilizaji pia. Kitendo hiki huweza
kufanywa kwa kupanga watetezi na wapinzani kwenye pande mbili
(upande wa kulia na upande wa kushoto) ambapo watabadilishana
mawazo kwa urahisi.
g) Kupanga muda utakaotumiwa na wahusika wa pande hizo mbili.
• Mambo ya kuzingatia katika utekelezaji wa mdahalo :
a) Kutumia vizuri muda uliopangwa.
b) Kuepuka fujo, kelele na usumbufu wowote.
c) Kutoa sauti inayosikika unaporuhusiwa kutoa hoja yako.
d) Kutoa maoni kuendana na mada inayozungumziwa.
e) Kutumia lugha rahisi na yenye adabu au heshima.
f) Kuheshimu mawazo ya watu wengine wanapoongea
g) Kuwa na mpangilio mzuri wa mawazo wakati wa kuzungumza
h) Kukumbuka kuwa mdahalo ni mchezo si pambano.
Jibu masali yafuatayo:
1. Mtunzawakati ana jukumu gani?
2. Mwenyekiti anapaswa kuwa na sifa gani?
3. Jadili mambo mawili ya kuzingatia katika uandalizi wa mdahalo.4. Kwa sababu gani tunasema kuwa mdahalo si pambano?
6.5. Kusikiliza na Kuzungumza
KAZI 7
Chunguza mada ifuatayo kisha utafute hoja za kuitetea na za
kuipinga hatimaye uwasilishe darasani:
“Nidhamu ya vijana wa leo ni bora kuliko nidhamu ya vijana wa zamani.”
6.6. Kuandika
KAZI 8
Tunga mdahalo juu ya mada ifuatayo:
“Madawa za kulevya hazina umuhimu katika maisha ya binadamu.”
Tathmini ya mada
1. Toa maana ya mdahalo.
2. Eleza baadhi ya mambo ya kuzingatia katika utekelezaji wa mdahalo.
3. Taja sifa za mdahalo mzuri.
4. Eleza mambo ya kujiepusha katika mdahalo.
5. Mdahalo huongozwa na nani? Anafanya kazi gani?
6. Kwa sababu gani tunasema kuwa mdahalo si pambano?
7. Taja masuala mtambuka yanayopatikana katika midahalo tuliyoona hapo juu.
8. Jaza nafasi kwa kutumia kirejeshi kilicho mwafaka:
i) vyakula viandaliwa-----vitafurahisha kila mtu.
ii) Nguo wazishona ------ ni za bei nafuu.
iii) Aisifu------ imemnyea.
iv) Zimwi likujua------- halikuli likakwisha.
v) Hamna hamna ndi----- mliwamo.
9. Ondoa amba- katika sentensi zifuatazo:
i) Mbunge ambaye hutuwakilisha bungeni atatutembelea kesho.
ii) Kazi ambazo serikali inatuhamasisha kuunda ni zile zinazojenga nchi.
iii) Vyakula na vinywaji ambavyo sisi hutumia huwa na viwango vya ubora.
iv) Dawa za kupunguza ukali wa UKIMWI ambazo atapewa zitamsaidia sana.v) Umoja ambao sisi Wanyarwanda tunao tuulinde usije ukavunjika tena.
MADA YA 4: KISWAHILI NA TEKNOLOJIA
Uwezo mahususi
Kutumia kwa ufasaha msamiati maalum katika uwanja wa teknolojia
Malengo ya Ujifunzaji
-- Kubainisha vyombo vitumiwavyo katika mawasiliano ya kiteknolojia;
-- Kujadili faida na hasara za mawasiiliano ya kiteknolojia;
-- Kutunga barua mbalimbali za mawasiliano ya kiteknolojia kwa kutumia
msamiati maalum
-- Kutunga sentensi sahihi kwa kutumia viambishi vya masharti: -nge- -ngelina-ngali-
KIDOKEZO
Toa maoni yako kuhusu maswali yafuatayo:
1. Ni vyombo vipi vya kiteknolojia vinavyoweza kutumiwa
katika mawasiliano?2. Je, vyombo hivyo vina faida au hasara gani?
SOMO LA 7: MAWASILIANO YA KITEKNOLOJIA
KAZI 1
Tazama kwa makini picha hapa juu. Jadili moja kwa moja matumizi yake.7.1. Kusoma na ufahamu: Tahadhali vijana!
Amina na Simeon ni wanafunzi wa Shule ya Ualimu wilayani Gatsibo.
Wanazungumzia jinsi teknolojia ya habari na mawasiliano (TEHAMA) huweza
kurahisisha mawasiliano na kupotosha akili ya watumiaji wake.
KAZI 2
Maswali ya ufahamu
Chagua jibu sahihi
1. Wahusika wanaozungumziwa ni:
a) Amina na Simeon.
b) Watumiaji wa vyombo vya mawasiliano ya kiteknolojia.
c) Amina, Simeon pamoja na mpenzi wake Amina.d) Hakuna jibu sahihi
2. Amina ameleta simu ya mkononi shuleni kwa sababu ya:
a) kuwasiliana na mpenzi wake aliyeko ugenini.
b) kutupia jicho wakati wa jaribio na mtihani.
c) kupakua maelezo ya somo la Biolojia na Jiografi.
d) burudani kwa mawasiliano na mpenzi wake pamoja na kuitupia jichowakati wa jaribio na mtihani.
3. Amina alipata anwani ya mpenzi wake kupitia:
a) Watisapu.
b) Fesibuku.
c) Tovuti.
d) barua pepe.
4. Mpenzi wake Amina alimpelekea Amina simu ya mkononi kwa ajili ya:
a) kurahisisha mawasiliano kati yao.
b) kuendeleza hali ya teknolojia ya habari na mawasiliano barani Afrika.
c) kumwondolea mpenzi wake aibu.
d) Majibu mengine ni sahihi isipokuwa b.
5. Simu ya mkononi hairuhusiwi shuleni kwani:
a) inaweza kutumiwa katika vitendo tofauti vya upotovu.
b) ni chombo cha bei ghali.
c) inaweza kuleta fujo darasani.
d) husababisha gharama nyingi.
6. Wakati una mabawa maana yake ni:
a) Ningekuwa na mabawa nigeruka mpaka Marekani.
b) Wakati wa jambo kutendeka ni huu.
c) Utakuwa na mabawa lini?d) Majibu yote ni sahihi.
7.2. Matumizi ya msamiati
KAZI 3
Jaza sentensi zifuatazo kwa kutumia msamiati huu: kupekua,
tovuti, kupiga marufuku, kutia aibu, ana kwa ana, kubakwa,
uasherati, barua pepe.
1. Kufeli mtihani wa taifa ni jambo la..........................kwa mwanafunzi
binafsi na kwa wazazi wake.
2. ...............huanzwa na https://www.
3. Watu wengi hu.................picha kwa kutumia Youtube.
4. ......................ni vitendo vya uzinifu, yaani kufanya mapenzi nje ya
ndoa. Vitendo hivyo ni vya........................kwa ajili ya kupigana dhidi ya
ugonjwa wa UKIMWI.
5. .......................ni njia ya kuwasilisha ujumbe kwa mtu aliye mbali au
karibu bila kuangaliana..............................
6. Wakati wa mauaji ya kimbari dhidi ya Watutsi nchini Rwanda
wanawake pamoja na wasichana wengi waliumizwa na vitendo vya.......................
7.3. Sarufi: Matumizi ya kiambishi cha masharti –nge-
KAZI 4
Eleza dhana ya kiambishi –nge- katika sentensi zifuatazo:
i) Ungejua athari ya mienendo mibaya hiyo kwa maisha yako,
usingeendelea kupotoshwa na uongo wa mawasiliano kutoka
mitandao ya intaneti au tovuti mbalimbali.ii) Nisingekuwa na simu ya mkononi, nisingekuwa kama nilivyo leo.
MAELEZO YA KUZINGATIA
Nge hutumika kuonesha uwezekano au majuto, yaani hutumika kuonyesha
kwamba kitendo fulani hakijafanyika na kwa hiyo jambo fulani halijatokea lakini
kuna uwezekano wa kufanya kitendo hicho na jambo hilo litokee.
Mfano:
1. Ningejua umuhimu wa elimu, ningewafundisha watoto wangu.
→ Sentensi hii inaonesha majuto: Sikujua umuhimu wa elimu, kwa hiyo
sikuwafundisha watoto wangu.
2. Ningekuwa na mchumba, angeninunulia simu ya mkononi aina ya Nokia.
→ Sentensi hii inaonyesha uwezekano: Bado sina mchumba wala simu ya
mkononi aina ya Nokia, lakini nikimpata mchumba ataweza kuininunulia.
Tanbihi: Katika hali kanushi nge hutanguliwa na kikanushi –si-
Mfano:
Nisingekuwa na simu ya mkononi, nisingekuwa kama nilivyo leo.
KAZI 5
Eleza ikiwa kiambishi -nge- kinaonyesha uwezekano au majuto.
a) Angefanya bidii, asingeshindwa mtihani wa taifa.
b) Wangewapatia watoto wao maadili, wangefaidika na matokeo mazuri.
c) Tungejua kuwa mvua itanyesha leo, tungeleta miavuli.
d) Mngetimiza wajibu wenu kazini, msingefukuzwa.
7.4. Matumizi ya lugha: Vyombo na njia mbalimbali katika
teknolojia ya habari na mawasiliano
KAZI 6
Zungumzia kuhusu vyombo vinavyotumiwa pamoja na njia za
kuwasilisha ujumbe
MAELEZO YA KUZINGATIA
A. Vyombo vya uwasilishaji wa habari na mawasiliano.
Kuna aina mbalimbali za vyombo ambavyo hutumiwa katika teknolojia ya habari
na mawasiliano kama vile:
• Redio.
• Runinga au televisheni.
• Simu.
• Tarakilishi au kompyuta.
• Posta.
• Satalaiti, n.k.
B. Njia za uwasilishaji wa habari na mawasiliano
• Fesibuku
• Watisapu
• Twita
• Skaipu
• Faksi
• Barua pepe
• Tovuti
• Telegramu• Instagramu
KAZI 7
Husisha ishara zifuatazo na maana yake
7.5. Kusikiliza na Kuzungumza
KAZI 8Igiza mazungumzo kati ya Amina na Simeon.
7.6. Kuandika
KAZI 9Tunga kifungu cha habari chenye aya tatu kuhusu faida za TEHAMA.
SOMO LA 8: MAWASILIANO KWA NJIA YA SIMUYA MKONONI
KAZI 1
Tazama kwa makini mchoro hapo juu. Unadhani watu hawawanashughulikia nini? .
Maswali ya ufahamu
KAZI 2
Chagua jibu sahihi
1. Wahusika wanaozungumza ni:
a) Mkuu wa shule na Mkuu wa masomo.
b) Viongozi wa shule.
c) Fisto, Mkuu wa shule na Angela, Mkuu wa masomo.
d) Majibu yote ni sahihi.
2. Kifungu cha habari kinazungumzia:
a) Mkuu wa shule na Mkuu wa masomo.
b) Kupata hati kutoka tarakilishi kwa ajili ya mkutano.
c) Matumizi ya simu ya mkononi.
d) Kubonyeza vidude kwenye tarakilishi.
3. Angela amepata matatizo ya:
a) Kutomudu matumizi ya kompyuta.
b) Kukatika kwa simu.
c) Kufiuka kwa simu.
d) Mtandao wa simu, kusanidi kicharazio na kielekezi pamoja na kusabidikichapishi.
4. Kabla ya kuzima tarakilishi inatubidi:
a) Kuchapisha nakala.
b) Kuhifadhi mabadiliko.
c) Kusasaisha.d) Kubonyeza vidude.
8.2. Matumizi ya msamiati
KAZI 3
Jaza sentensi zifuatazo kwa kutumia msamiati huu: kubonyeza
vidude, kusasaisha, nakala bayana, kumemeka, kicharazo,
kusanidua, kuamilisha, nakala laini.
1. Hati iliyohifadhiwa katika kompyuta bila kuchapishwa huitwa...................
wakati ambapo nakala iliyochapishwa huitwa...................
2. Zoezi la kwanza kwenye kompyuta ni ...................................
3. Unaweza .............programu matumizi za simu ya mkononi au tarakilishi
wakati ambapo zinaonekana kama siyo muhimu.
4. Ili uweze kuandika kwenye kompyuta ni lazima utumie .........................
....................
5. Baada ya muda mrefu .hati kuhifadhiwa katika kompyuta inatubidi ....
..........................................
6. Simu ya mkononi haiwezi ..................................bila kuchajiwa.
7. Inatubidi ......................kingavirusi katika kompyuta zetu ili kulinda hatizetu dhidi ya virusi.
8.3. Sarufi: Matumizi ya kiambishi cha masharti –ngeli- au–ngali-
KAZI 4
Eleza dhana ya kiambishi –ngeli- au –ngali- katika sentensi
zifuatazo:
-- Ningelikuwa na kingavirusi, ningeliiamilisha katika tarakilishi yako ili
kuepuka uharibifu wa hati.-- Ningalifuata maonyo ya wazazi wangu, nisingalipata cha mtemakuni.
MAELEZO YA KUZINGATIA
Ngeli au ngali mara nyingi hutumiwa katika wakati uliopita kuonesha uwezekano
au majuto, yaani hutumika kuonesha kwamba kitendo fulani hakijafanyika na kwa
hivyo jambo fulani halijatokea lakini kuna uwezekano wa kufanya kitendo hicho
na jambo hilo litokee.
Mfano:
Ningelikuwa na kingavirusi, ningeliiamilisha katika tarakilishi yako ili kuepuka
uharibifu wa hati.
Ningalifuata maonyo ya wazazi wangu, nisingalipata cha mtemakuni.
Tanbihi:
1. Ni kosa la kisarufi kuchanganya ngeli na ngali katika sentensi moja. Ikiwa
kipande cha kwanza kimetumia ngeli, ni lazima ngeli itumiwe pia katika
kipande cha pili n.k
2. Katika hali kanushi ngeli au ngali hutanguliwa na kikanushi –si-Mfano: Ningalifuata maonyo ya wazazi wangu, nisingalipata cha mtemakuni.
KAZI 5
Weka sentensi hizi katika hali yakinishi au kanushi.
a) Nisingelisoma, nisingeliwafundisha watoto wangu.
b) Wangalihifadhi mazingira yao, wangaliishi kwa usalama.
c) Mngeliepuka tabia ya uzinifu, msingeliambukizwa ugonjwa wa ukimwi.d) Ungalishughulikia kazi za ujasiliamali, ungalijiendeleza kiuchumi.
8.4. Matumizi ya lugha: Vyombo na njia mbalimbali katikateknolojia ya habari na mawasiliano.
KAZI 6
Kwa kutegemea mchoro, onyesha vipengele muhimu vyakompyuta au tarakilishi
8.5. Kusikiliza na Kuzungumza
KAZI 7Igiza mazungumzo kati ya Fisto na Angela.
8.6. Kuandika
KAZI 8
Tunga kifungu cha habari chenye aya angalau tatu kuhusu hasaraza TEHAMA.
Tathmini ya mada
I) Taja vyombo angalau vitano vya TEHAMA na kueleza matumizi yake.
II) Chagua jibu sahihi:
1. Ili ujumbe kutoka Fesibuku uwasilishwe ni lazima kuwe na vifaa
vifuatavyo isipokuwa:
a) tarakilishi au simu ya mkononi.
b) mtandao wa intaneti.
c) anwani ya mtumaji na mpokezi wa ujumbe.
d) meza ya kuwekea tarakilishi pamoja na kiti cha kukalia.
2. Mawasiliano kwa njia ya Watisapu huwezekana iwapo kuna:
a) simu ya mkononi iliyounganishwa kwenye mtandao wa intaneti.
b) simu kadi pamoja na chaji.
c) simu ya mkononi pamoja na mtumiaji.
d) simu ya mkononi iliyounganishwa kwenye mtandao wa intaneti pamoja
na mtumiaji.
3. Google ni aina ya:
a) mtandao.
b) tovuti.
c) barua pepe.
d) tarakilishi.
4. Youtube hutumiwa:
a) kupelekea mtu barua pepe.
b) kubonyeza vidude.
c) kupakua picha.
d) kutangaza habari.
5. Kielekezi kazi yake ni:
a) kuonesha nafasi ya kuandikia kwenye tarakilishi.
b) kufuta maandishi.
c) kuchapisha nakala.
d) kusanidua nakala laini.
6. Badilisha sentensi zifuatazo kwa kutumia kiambishi –nge-, -ngeli- au–ngali-.
a) Sikununua chai kwa sababu nilikosa pesa.
b) Nikifanya kwa bidii sitafeli mtihani wa taifa.
c) kama hukujua umuhimu wa kuhifadhi mazingira hukupanda miti karibuna nyumba yako.
MAREJEO
Waititu, F. na Wenzake (2008): Kiswahili Fasaha. Kitabu cha Mwanafunzi.
Kidato cha Tatu. Oxford University Press, East Africa Ltd, Nairobi, Kenya.
TUKI (2004): Kamusi ya Kiswahili Sanifu. Toleo la Pili. Oxford University Press.
Bakhressa, S.K. na Wenzake (2008): Kiswahili Sanifu. Kitabu cha Mwanafunzi.
Darasa la Saba. Oxford University Press, East Africa Ltd, Elgon Road, Upper
Hill, Nairobi, Kenya.
Nkwera F.M.V. (1978): Sarufi na Fasihi Sekondari na Vyuo. Tanzania Publishing
House, Dar Es Salaam.
HARERIMANA, F. (2017): Tujivunie Lugha Yetu. Kitabu cha Mwanafunzi, Kidato
cha 5. MK Publishers (R) Ltd. Kigali, Rwanda.
Ndalu, A. E. (2016): Masomo ya Kiswahili Sanifu. Kitabu cha Mwanafunzi.
Kidato cha 2. Moran (E.A) Publishers Limited.
Bakhressa, S.K. na Wenzake (2008): Kiswahili Sanifu. Kitabu cha Mwanafunzi.
Darasa la 8. Oxford University Press, East Africa Ltd, Elgon Road, Upper Hill,
Nairobi, Kenya.
Ntawiyanga, S. na Wenzake (2017): Kiswahili kwa Shule za Rwanda. Mchepuo
wa Lugha, Kidato cha 5. Longhorn Publishers (Rwanda) Limited. Kigali, Rwanda.
Kenya Literature Bureau (2006): Kiswahili kwa Darasa la Nane. Kitabu cha
Wanafunzi. Kenya Literature Bureau, Nairobi, Kenya.
Ntawiyanga, S. na Wenzake (2017). Kiswahili kwa Shule za Rwanda. Mchepuo
wa Lugha, Kidato cha 6. Longhorn Publishers (Rwanda) Limited. Kigali, Rwanda.
Niyirora, E. na Ndayambaje, L. (2012): Kiswahili Sanifu kwa Shule za Sekondari.
Kitabu cha Mwanafunzi Kidato cha Tano. Tan Prints (India) Pvt. Ltd.
Massamba, D.P.B. na Wenzake (2009): Sarufi Miundo ya Kiswahili Sanifu,
Sekondari na Vyuo. Taasisi ya Uchunguzi wa Kiswahili. Chuo Kikuu cha Dar es
Salaam, Tanzania.
Massamba, D.P.B. na Wenzake (2012): Sarufi Maumbo ya Kiswahili Sanifu,
Sekondari na Vyuo. Taasisi ya Uchunguzi wa Kiswahili. Chuo Kikuu cha Dar es
Salaam, Tanzania.
Nkwera, F.M.V. (1979): Sarufi na Fasihi, Sekondari na Vyuo.Tanzania PublishingHouse, Dar es Salaam,Tanzania.