Main content blocks
Section outline
-
-
Maamkizi na Utambulisho
Somo la Kwanza
Maana ya Maamkizi
A. Vifungu mbalimbali vya maamkizi
Tazama michoro ifuatayo kwa makini kisha kwa ushirikiano na wenzako tathmini maana ya maamkizi kwa kutumia maswali yanayoambatana nayo.Babu na mjukuu:
Shikamoo babu! Marahaba Jeni.
Baba na mtoto:
Umeshindaje mwanangu? Vyema baba.Mwanafunzi na mwanafunzi mwenzake:
U hali gani Juma? Njema Aisha.Kaka na dada:
Hujambo dada? Sijambo kaka.Muuzaji na mnunuzi:
Habari za asubuhi mteja wangu! Nzuri.Tathmini
a) Michoro iliyo hapo juu inahusu nini?
b) Unaweza kuwaeleza wenzako kinachoendelea katika michoro hiyo?Baada ya kuwaeleza wenzako, jigawe katika vikundi vya wanafunzi wawili wawili kisha muigize mifano hiyo ya michoro.
Maelezo muhimu
• Maamkizi ni kujuliana hali. Pia huitwa salamu.
• Maamkizi huleta amani baina ya watu na pia huwaunganisha. Maamkizi pia huondoa uadui miongoni mwa watu.Mifano zaidi ya maamkizi
Linganisha mifano ifuatayo na mawazo yako kuhusu michoro iliyotangulia:
Maamkizi Jibu 1. Hujambo? Sijambo. 2. Habari za jioni? Nzuri/Njema. 3. Shikamoo! Marahaba. 4. Hamjambo? Hatujambo. 5. U hali gani? Njema/Nzuri. 6. Kwaheri! Ya kuonana. 7. Sabalheri! Akheri. 8. Masalheri! Akheri. 9. Pole! Nishapoa. 10. Umeamkaje? Vyema. Maigizo ya maamkizi mbalimbali
Katika vikundi vya wanafunzi wawili wawili, igizeni maamkizi mbalimbali kutokana na mifano mliyopewa kwa kuzingatia ufasaha wa kujieleza na matamshi bora. Jaribuni kutatua matatizo yoyote ya kimatamshi.Zoezi la 1
Waamkie wenzako kwa salamu zifuatazo kisha fanyeni igizo la kuamkiana.1. Habari za jioni? - Njema/Nzuri. 2. Umeshindaje? - Vyema/Salama/Vizuri 3. Hujambo? - Sijambo. 4. U hali gani? - Njema/Nzuri. 5. Shikamoo! - Marahaba. 6. Hamjambo? - Hatujambo. 7. Salama? - Salmini. 8. Habari za asubuhi? - Njema/Nzuri. 9. Sabalheri! - Akheri. 10. Kwaheri! - Ya kuonana. Zoezi la 2
Fanya utafiti kutoka kwa wenzako kupitia mahojiano kisha uwaeleze wanafunzi wenzako ugunduzi wako kuhusu sababu za kuamkia mtu na umuhimu wake.B. Msamiati wa maamkizi
Rejelea mifano ya maamkizi uliyosoma na kisha uorodheshe maneno yote mapya na yanayotatiza kuelewa. Jaribu kuyatolea maana kutokana na yalivyotumiwa. Fanya utafiti kwenye kamusi ya Kiswahili kwa maneno yanayotatanisha zaidi.Mifano:
Zoezi la 1
Jaza nafasi zilizo wazi katika daftari lako kwa kuteua jawabu sahihi kutoka kwa yafuatayo:
Marahaba Sijambo Njema Ya kuonana AsanteMfano:
Sabalheri - ____________
Jibu: Akheri
1. Hujambo? - ___________________
2. Shikamoo! - ___________________
3. Kwaheri! - ___________________
4. Habari za mchana? - ___________________
5. Karibu! - ___________________Zoezi la 2
Tunga maamkizi yako binafsi na majibu yake kisha ujadiliane na wenzako kuhusu usahihi wake.Mfano:
Habari za leo? - Njema/Nzuri.C. Mazungumzo yenye maamkizi mbalimbali
Soma kwa sauti na kwa zamu maamkizi yafuatayo baina ya wazazi na watoto wao.Baba: Hujambo mwanangu?
Aisha: Sijambo baba. Shikamoo?
Baba: Marahaba mwanangu. U hali gani?
Aisha: Njema baba.
Baba: Salama?
Aisha: Salmini.Mama: Umeamkaje Juma?
Juma: Salama mama. Shikamoo?
Mama: Marahaba mwanangu. Habari za kushinda?
Juma: Njema mama.
Mama: Je, umemaliza kazi niliyokupa?
Juma: Ndio mama.
Mama: Sawa. Naenda sokoni kununua mboga na matunda.
Juma: Sawa mama.
Mama: Kwaheri Juma.
Juma: Ya kuonana mama.Zoezi
Tunga mifano zaidi ya maamkizi kwa kufuata mifano uliyopewa.Tathmini
Baada ya kusoma mifano uliyopewa na kutunga maamkizi yako, kwa ushirikiano na wenzako, jaribu kueleza:
a) Maana ya kuamkiana
b) Lengo la kuamkianac) Uhusiano wa wanaoamkiana
Je, majibu yako yanalingana na haya?
a) Maana ya kuamkiana ni:
• Kujuliana hali
b) Lengo la kuamkiana ni:
1. Kuonyesha adabu.
2. Kuonyesha kuna amani na upendo.
3. Kufahamu hali za watu wengine.c) Uhusiano wa kimaamkizi ni:
D. Sarufi
Umoja na wingi wa maamkizi
Katika makundi ya wanafunzi watatu watatu, someni sentensi zifuatazo kwa zamu katika umoja na wingi.
Umoja Wingi 1. Kwaheri Maria! - Kwaherini kina Maria. 2. Hujambo mwalimu? - Hamjambo walimu? 3. Shikamoo mama! - Shikamoo kina mama! 4. Habari yako? - Habari zenu? 5. Sijambo. - Hatujambo. 6. U hali gani? - M hali gani? 7. Umelalaje? - Mmelalaje? 8. Pole! - Poleni! 9. Karibu. - Karibuni. 10. Sabalheri! - Sabalheri! Tathmini
Gundua tofauti inayobainika katika maamkizi katika umoja na wingi. Zingatia mifano iliyopo hapa chini katika nafsi mbalimbali.
Umoja Wingi 1. Habari? (yako) - Habari? (zenu) 2. Hujambo? (wewe) - Hamjambo? (nyinyi) 3. Sijambo. (mimi) - Hatujambo. (sisi) 4. Shikamoo! (baba) - Shikamoo! (kina baba) 5. Shikamoo! (mama) - Shikamoo! (kina mama) 6. U hali gani? (wewe) - M hali gani? (nyinyi) 7. Kwaheri! (wewe) - Kwaherini! (nyinyi) 8. Ameamkaje? (yeye) - Wameamkaje? (wao) 9. Pole. (wewe) - Poleni. (nyinyi) Zoezi la 1
Kwa ushirikiano na wenzako, waulize maamkizi kwa umoja kisha nao wajibu kwa wingi. Tumia mifano iliyopo hapo juu.Zoezi la 2
Jibu kwa usahihi kwa kuteua jawabu sahihi la wingi wa kila salamu na neno la adabu.
Mfano: Hujambo? - Sijambo. 1. Sijambo - (Hatujambo, Jambo) 2. Hajambo. - (Hawajambo, Habari zenu) 3. Kwaheri! - (Kwaherini, Nzuri) 4. U hali gani? - (Njema, M hali gani?) 5. Karibu. - (Karibuni, Asante)
E. Matamshi na tahajia bora
Matamshi ya konsonanti
i) Soma kwa sauti.a) Konsonanti za Kiswahili
b) Soma silabi zifuatazo kwa sauti:
ii) Soma konsonanti ambatano zifuatazo kwa sauti.
1. [mw]
Matumizi katika maneno:
Mwalimu, mwangaza, mweupe, mweusi, mwanafunzi, mwisho, mwokozi, mwezi, mwizi, mwikoMatumizi katika sentensi:
1. Ni muhimu kuzima mwangaza mchana.
2. Uwe mweusi, mnene au mwembamba, sote tuko sawa!2. [bw]
Bwana, bwalo, kubwa, bwaga, bwekaMatumizi katika sentensi:
1. Habari bwana!
2. Wanyarwanda wote wana jukumu kubwa la kulipa ushuru.3. [kw]
Kweza, kwenda, kwikwi, kwaheri, kwangu, kwako, kwoteMatumizi katika sentensi:
1. Karibu kwangu.
2. Kwaherini wageni.4. [vy]
Vyakula, vyangu, vyombo, vyemaMatumizi katika sentensi:
1. Karibuni tule vyakula vitamu.
2. Asante kwa kunipa vyombo safi.5. [tw]
Twiga, tweza, twangaMatumizi katika sentensi:
1. Tafadhali nitwike mzigo huu.
2. Twanga nafaka hizi.Zoezi la 1
Kwa ushirikiano na wenzako, tumia kamusi ya Kiswahili kutafiti na kuandika maneno ya sauti ambatano zifuatazo: (mifano mitatu kwa kila sauti)Zoezi la 2
Kwa msaada wa wenzako na kamusi ya Kiswahili, eleza mbele ya wanafunzi wenzako maana ya maneno uliyopata yenye sauti [nj], [pw], [nz], [sw] na [mb].Mifano:
Njoo: Tamko la kumwita mtu aliye mbali aje karibu na pale ulipo.
Pweta: Ona haya baada ya kutenda kitendo cha aibu.Zoezi la ziada
Chagua jibu moja sahihi kati ya majibu yaliyo katika mabano ili kuelezea maelezo uliyopewa.Mfano: Neno linaloonyesha adabu na kujali. (Hodi, Pole)
Jibu: Pole1. Hutumiwa na kila mtu asubuhi, mchana na usiku.
(Salamu, Chuki)
2. Neno ambalo hutumiwa na mtu anayeagana na mtu mwingine.
(Kwaheri, Karibu)
3. Hutumiwa na mdogo kwa mkubwa tu!
(Marahaba, Shikamoo)
4. Jibu langu ni ‘Sijambo’.
(Jambo, Hujambo)
5. Jibu la ‘Sabalheri’.
(Akheri, Habari)Somo la Pili
Aina Mbalimbali za MaamkiziTazama picha zifuatazo kwa makini pamoja na maandishi yaliyo chini yake kisha utathmini maana inayojitokeza
Mifano mingine ya maamkizi:
1. Waambaje? - Vyema/vizuri.
2. Makiwa! - Tunayo.
3. Masalkheri! - Akheri.Maswali ya kutathmini
a) Picha zilizo hapo juu zinazungumzia nini?
b) Waeleze wanafunzi wenzako maana ya maelezo yaliyomo.Maelezo muhimu
• Hizi ni aina za salamu/maamkizi. Maamkizi huenda na umri, wakati na hali.Tazama mchoro ufuatao kisha usome kwa sauti salamu zinazoambatana na mchoro huo.
a) Umri
Kijana na kijana mwenzake
Kijana wa kiume: Waambaje?
Kijana wa kike: Vyema.Mifano zaidi:
1. Mwalimu na mwanafunzi
Mwanafunzi: Shikamoo mwalimu!
Mwalimu: Marahaba!2. Nyanya na babu
Nyanya: Habari mwenzangu!
Babu: Njema sana mwenzangu.b) Hali
i) Huzuniii) Furaha
c) Nyakati mbalimbali
i) Wakati wa jioniii) Wakati wa asubuhi
iii) Wakati wowote
Tathmini
Je, umegundua kwamba salamu na maamkizi hutegemea umri, hali na wakati?
Kama hujagundua hivyo, hebu soma tena maamkizi hayo kwa makini huku ukizingatia michoro uliyopewa.Maigizo ya maamkizi mbalimbali
Soma tena kimyakimya aina mbalimbali za salamu zilizo hapo juu. Kisha kwa makundi ya wanafunzi wanne wanne someni kwa sauti kwa njia ya kubadilishana kwa kuzingatia matamshi bora.Tathmini
a) Ni maneno gani yalikutatanisha kutamka?
b) Je, wenzako pia wana matatizo kama yako?
c) Wewe na wenzako mliyatatua vipi matatizo hayo?Sasa jadiliana na wenzako jinsi ya kuyatatua matatizo hayo yote ya matamshi.
Kazi ya makundi
Igizeni aina mbalimbali za maamkizi yaliyo kwenye ukurasa uliotangulia.KUMBUKA: Salamu zinaweza kumfanya mtu apate kitu ama akikose, apendwe ama akataliwe.
A. Msamiati wa maamkizi mbalimbali
Rejelea tena maelezo na mifano ya aina mbalimbali za maamkizi. Orodhesha maneno yote mapya na kuyatolea maana. Fanya utafiti kwa kutumia kamusi ya Kiswahili. Kwa mfano:Nyanya - Mzazi wa kike wa baba au mama.
Matumizi katika sentensi: Shikamoo nyanya!Babu - Mzazi wa kiume wa baba au mama.
Matumizi katika sentensi: Kwaheri babu!Kijana - Mtu wa umri wa kubalehe, mvulana ama msichana.
Matumizi katika sentensi: Waambaje kijana mwenzangu?Buriani - Maagano ya kuachana kwa muda mrefu.
Matumizi katika sentensi: Buriani Juma. Tuonane mwaka ujao.Makiwa - Tamko la kumpa pole mtu aliyepata msiba wa kufiwa.
Matumizi katika sentensi: Makiwa jirani kwa kumpoteza mwanao.Alamsiki - Neno la kuagana wakati wa usiku.
Matumizi katika sentensi: Alamsiki Aisha.Hongera - Neno la kupongeza mtu.
Matumizi katika sentensi: Hongera kwa serikali yetu kwa uongozi bora.Zoezi la 1
Jibu maswali yafuatayo kwa kuchagua na kuandika katika daftari lako jibu sahihi.Mfano:
Tamko la kuagana wakati wa usiku.
(Alamsiki, Kwaheri)
Jibu: Alamsiki1. Jibu la: Makiwa. _____________________
(Tunayo, Salama)
2. Jibu langu ni: Nishapoa. _____________________
(Pole, Makiwa)
3. Neno la kupongeza. _____________________
(Kwaheri, Hongera)
4. Jibu la: Buriani. _____________________
(Tunayo, Buriani dawa)
5. Salamu ya mtoto kwa mtu mzima. _____________________
(Shikamoo, Karibu)Zoezi la 2
Kwa ushirikiano na mwenzako aliye karibu nawe, tafuta majibu ya maamkizi yafuatayo:1. Waambaje? - _____________________
2. Hodi! - _____________________
3. Pole! - _____________________
4. Salama? - _____________________
5. Kwaheri! - _____________________B. Mazungumzo yenye maamkizi
Soma kwa sauti salamu baina ya Daktari na Gasore.Gasore: Shikamoo daktari!
Daktari: Marahaba Gasore. Karibu.Gasore: Asante.
Daktari: Habari ya leo?
Gasore: Njema, lakini mimi naugua.
Daktari: Unaugua wapi Gasore?
Gasore: Midomo yangu imevimba. Nashindwa hata kula. Nahisi uchungu sana.
Daktari: Pole sana Gasore.
Gasore: Nishapoa.
Daktari: Nitakupima kisha nitakupa dawa ya kupunguza uchungu huo.
Gasore: Asante sana daktari.
Daktari: Karibu.Zoezi la makundi
1. Katika makundi ya wanafunzi wawili wawili, igizeni maamkizi baina ya Gasore na Daktari.
2. Kwa ushirikiano na wenzako darasani, eleza maamkizi wanayoyatumia kwa kuyataja.Zoezi la ufahamu
1. Gasore anazungumza na nani?
2. ‘Marahaba’ ni jawabu la salamu gani?
3. Ni kwa nini Gasore anazungumza na Daktari?
4. Ili kumpa Gasore moyo, Daktari alimwambia nini?
5. Gasore alitumia neno ‘Asante’. Unadhani ni kwa nini alitumia neno hilo?Zoezi la ziada
Igiza maamkizi mengine kati ya watu wawili kwa vikundi vya wanafunzi wawili wawili. Zingatia mazungumzo yaliyopo hapo juu.C. Sarufi
Nafsi za KiswahiliSimama mbele ya wanafunzi wenzako kisha uwaamkie na ujitambulishe.
Tathmini
a) Ulianzaje kujitambulisha?
b) Unajua lugha ya Kiswahili ina nafsi ngapi? Waambie wenzako.Maelezo muhimu
- Kila binadamu ana lugha, utamaduni na hulka yake lakini pia kila binadamu anawahitaji wenzake.
- Lugha ya Kiswahili ina nafsi tatu ambazo zinajitokeza katika umoja na wingi.
- MIMI, WEWE, YEYE, SISI, NYINYI, na WAO ndizo nafsi za Kiswahili.
Mifano ya kujitambulisha kwa kutumia nafsi za Kiswahili
Jitambulishe kisha uwatambulishe wenzako ukitumia nafsi zilizo hapo juu.
1. Mimi ninaitwa _________________.
2. Wewe unaitwa _________________.
3. Yeye anaitwa _________________.
4. Sisi tunaitwa _________________.
5. Nyinyi mnaitwa ________________.
6. Wao wanaitwa _________________.Waambie wenzako nao wajitambulishe kwa kufuata mfano uliopo hapo juu.
Maelezo muhimu
• Nafsi za Kiswahili hujitokeza katika umoja na wingi kama ifuatavyoMatumizi katika sentensi:
Umoja Wingi
1. Mimi ninapenda amani. - Sisi tunapenda amani.
2. Wewe unafunga mfereji. - Nyinyi mnafunga mifereji.
3. Yeye anaokota uchafu. - Wao wanaokota uchafu.Zoezi la 1
1. Katika makundi ya wanafunzi wawili wawili, linganisha nafsi za umoja (A) na zile za wingi (B) kwa usahihi.a) Mimi Wao
b) Wewe Sisi
c) Yeye Nyinyi2. Sasa kwa kujitegemea, tunga sentensi sahihi kwa kutumia nafsi zote tatu katika umoja na wingi.
Mfano:
Mimi ni mzalendo. - Sisi ni wazalendoD. Matamshi na tahajia bora
1. Kwa ushirikiano na mwenzako, soma kwa sauti na kwa zamu sauti ambatano za konsonanti za Kiswahili zifuatazo:[Gh]
Ghala, ghamidha, lugha, ghulamu[Nd]
Ndani, ndimu, ndoano, ndoa, ndimi[Ng]
Ngeli, kengele, ngeni, ngao, ngamia[Mb]
Mbuzi, mbilikimo, mbili, tumbili, mbu2. Andika kwa hati nzuri maneno yenye sauti ambatano ambayo utasomewa na mwenzako kutokana na mifano iliyotolewa hapo juu.
E. Mjadala/Mazungumzo
Kwa kutumia nafsi za Kiswahili kwa usahihi, zungumza na wenzako juu ya ‘Umuhimu wa kuamkiana’.Matumizi ya Nafsi na Viwakilishi vya Nafsi katika Maamkizi
A. Maamkizi yenye nafsi katika umoja na wingi
Soma maamkizi yafuatayo yenye viwakilishi vya nafsi.A B
1. Mimi: Sijambo. Sisi: Hatujambo.
2. Wewe: Hujambo? Nyinyi: Hamjambo?
3. Yeye: Hajambo. Wao: Hawajambo.
4. Mimi: Habari yangu ni njema. Sisi: Habari zetu ni njema.
5. Wewe: U hali gani? Nyinyi: M hali gani?
6. Yeye: Ameshindaje? Wao: Wameshindaje?Baada ya kusoma kwa makini maamkizi katika A na B, eleza wenzako unachogundua katika kila kikundi.
Maelezo muhimu
• Haya ni maamkizi.
• A ni maamkizi katika umoja na B ni wingi wa maamkizi katika A.
• Nafsi mbalimbali zimetumika.Sasa unaweza kukumbuka tulichosema kuhusu nafsi? Tumia maswali yafuatayo kukumbuka.
a) Kiswahili kina nafsi ngapi?
b) Unaweza kuzitaja nafsi hizo katika umoja na katika wingi? Shirikiana na wenzako kupata jawabu.Baada ya kutoa maoni yako, angalia mifano ifuatayo kisha uisome kimyakimya kwa makini.
1. Mimi naitwa Iragena. - Sisi tunaitwa Iragena.
2. Wewe unaitwa Gahigi. - Nyinyi mnaitwa Gahigi.
3. Yeye anaitwa Nirere. - Wao wanaitwa Nirere.Kusoma mifano ya salamu kwa matamshi sahihi
Soma kimyakimya mifano ya salamu iliyo katika utangulizi uliopo hapo juu. Kisha kwa ushirikiano na wenzako, soma tena kwa sauti na kwa kubadilishana kwa kuzingatia matamshi bora. Tatueni kila tatizo la matamshi linalotokea. Fanya utafiti katika kamusi ya Kiswahili.B. Msamiati wa viwakilishi vya nafsi
Soma tena maandishi yaliyo mwanzoni mwa somo hili. Andika maneno yote mapya kisha utambue maana yake kwa kuzingatia jinsi yalivyotumika.Zoezi la 1
Andika majibu katika daftari lako kwa kuchagua jibu sahihi kutoka kwa majibu yaliyo mabanoni.Mfano: ____________ ninaitwa Nshuti. (Wewe, Mimi)
Jibu: Mimi ninaitwa Nshuti.
1. Wewe ____________. (Unanikumbuka, ninakumbuka)
2. ____________ anaitwa Samantha. (Yeye, Wewe)
3. ____________ mnaitwa. (Nyinyi, Wao)
4. ____________ wanasoma. (Wao, Wewe)
5. ____________ tunalima. (Sisi, Nyinyi)Zoezi la 2
Kwa msaada wa wenzako, tunga sentensi sahihi kwa kutumia: mimi, wewe, yeye, sisi, nyinyi na wao.Mfano: Sisi ni wanafunzi.
Zoezi la ziada
Kwa ushirikiano na wenzako, jibu maswali yafuatayo kutokana na uliyosoma kuhusu nafsi:
1. Mfano wa nafsi ni ____________ na ______________.
2. Umoja wa ‘Hatujambo’ ni ____________.
3. Jibu kwa kuteua neno sahihi.
a) Habari, hujambo; ni maamkizi. (Ndio, La)
b) Mimi, nyinyi, yeye; ni nafsi (Ndio, La)
c) Mimi, wewe, yeye ni umoja wa (Sisi, Wao, Nyinyi) ama (Sisi, Nyinyi, Wao) ama (Wao, Nyinyi, Wao)?
4. Rwanda ni nchi ____________. (yetu, sisi)
5. Andika kwa umoja kwa kuteua jawabu sahihi kati ya yale yaliyo kwenye mabano.C. Sarufi
Nafsi za Kiswahili
Kwa kutumia maarifa uliyopata mwanzoni mwa somo hili, tambua wingi wa nafsi za Kiswahili zifuatazo:Tumia jedwali hili:
Tunga sentensi kwa kutumia nafsi hizi katika umoja na wingi.
Mfano: Mimi ni Mnyarwanda. - Sisi ni Wanyarwanda.
Kazi ya kikundi
Unakumbuka somo kuhusu kujitambulisha?
a) Ninaitwa Mugisha.
b) Unaitwa Munezero.
c) Anaitwa Mushikiwabo.Unaweza kuwaelezea wenzako kwa nini ulianza na ‘ni’, ‘u’ na ‘a’?
1. Ninaitwa (mimi) - Tunaitwa (sisi)
2. Unaitwa (wewe) - Mnaitwa (nyinyi)
3. Anaitwa (yeye) - Wanaitwa (wao)Kumbuka
• ‘ni’, ‘u’, ‘a’ ‘tu’, ‘m’ na ‘wa’ ni viambishi vya nafsi mimi, wewe, yeye, sisi, nyinyi na wao mtawalia.Zoezi la 1
Kwa ushirikiano na wenzako, onyesha nafsi zinazochukua viambishi vya nafsi vilivyotajwa.Mfano: Ni - __________
Jibu: Mimi
1. a - __________
2. tu - __________3. wa - __________
4. u - __________
5. m - __________Zoezi la 2
Kamilisha maamkizi yafuatayo kwa kutumia nafsi katika umoja ama wingi.Mfano: __________ sijambo.
Jibu: Mimi
1. __________ hatujambo.
2. __________ hawajambo.
3. __________ m hali gani?
4. __________ waambaje?
5. __________ ni mzima.Zoezi la mjadala
Katika makundi ya wanafunzi wanne wanne, jadili kauli hii:‘Nafsi inaweza kutugawanya ama kutuunganisha kijinsia na kama nchi.’
D. Matamshi ya konsonanti na tahajia bora
1. Soma maneno yafuatayo kwa sauti kwa kutamka konsonanti kulingana na utaratibu wa sauti husika. Sikiliza kwa makini namna wenzako wanavyoyatamka.[k]
Kaka, kalamu, keti, korti, kazi, bakiMatumizi katika sentensi:
a) Kalamu hii ni ya mwalimu.
b) Koti la baba limepigwa pasi.[b]
Baba, barua, babu, bodi, batiMatumizi katika sentensi:
a) Barua ile ilitumwa jana.
b) Baba amenunua gazeti.[p]
Pesa, peni, penseli, pasha, pishaMatumizi katika sentensi:
a) Pesa zake ni nyingi.
b) Hii ni penseli ya mtoto wangu.2. Zoezi la Imla:
Andika kwa hati nzuri na ukamilifu maneno ambayo utasomewa na mwalimu wako.E. Maswali ya Marudio
1. Katika daftari lako, andika katika umoja.
Mfano: Mwaambaje? – Waambaje?2. Kwa zamu, jitambulishe na uwatambulishe wenzako.
Mfano: Ninaitwa Maria.
a) Ninaitwa _____________.
b) Anaitwa _____________.
c) Unaitwa _____________.3. Jibu kwa maneno bora ya kuagana.
Mfano: Kwaheri – Ya kuonana
a) Tuonane kesho _____________.
b) Buriani _____________.
c) Lala salama _____________.
d) Alamsiki _____________.4. Shirikiana na wenzako darasani kugundua maneno yanayofaa zaidi kujazia nafasi zilizoachwa wazi.
_____________ mwalimu! Tafadhali _____________ kalamu yako._____________, nimechelewa. _____________ mwalimu. Mzazi pia_____________.5. Tunga sentensi sahihi kwa kutumia maneno haya:
Mfano: Mama ananiamkia.
a) Pole b) Asante c) Tafadhali
d) Naomba e) Habari6. Onyesha viambishi vya nafsi zilizotajwa.
Mfano: Mimi - ni
a) Sisi - __________
b) Wewe - __________
c) Nyinyi - __________
d) Yeye - __________
e) Wao - __________Faharasa
Maamkizi: Salamu; maneno ya kujuliana hali
Kiwakilishi: Neno linalochukua nafasi ya nomino ama kiwakilishi kingine
Baba: Mzazi wa kiume
Mama: Mzazi wa kike
Mwalimu: Mtu anayempa mtu mwingine elimu ama maarifa
Nafsi: Mtu mwenyewe, binafsi
Mwanafunzi: Mtu aliye chini ya mwalimu kwa lengo la kupata elimu na maarifa
Jirani: Mtu aliye karibu nawe; anayeishi karibu nawe
Muuzaji: Mtu anayeuza bidhaa kwa watu wengine kwa kubadilisha hasa kwa pesa
Mnunuzi: Mtu anayetoa pesa ama kitu kingine ili kupata bidhaa kutoka kwa muuzajiMsamiati: Maneno mapya ambayo yanapatikana katika taarifa/kifungu
Hujambo?: Huna jambo?
Sijambo: Sina jambo
Habari: Taarifa, ujumbe; salamu (kujuliana hali)
Shikamoo: Salamu ya heshima inayotolewa kwa mtu mwenye umri mkubwa kukuliko
Marahaba: Kiitikio cha salamu iliyotolewa kwa neno ‘shikamoo’
Makiwa: Salamu kwa mtu aliyepatwa na msiba hasa wa kifo
Tunayo: Kiitikio cha salamu iliyotolewa kwa mtu aliyepata msiba hasa wa kufiwa
Sabalheri: Salamu ya kujulia mtu hali wakati wa asubuhi
Masalheri: Salamu za jioniPole: -enye utulivu, taratibu. Salamu za kutakia mtu utulivu.
Waambaje: Wasemaje? Unasema nini?
Twika: Wekea kichwani, begani; bebesha; twisha
Buriani: Salamu za kumuaga mtu ambaye hamtaonana kwa muda mrefu
Msichana: Mtoto wa kike
Mvulana: Mtoto wa kiume
Alamsiki: Salamu za kuagana usiku
Shirikiana: Fanya pamoja na wenzako. Kuwa katika kikundi -
Mada Ndogo:
Msamiati Katika Mazingira ya ShuleSomo la Kwanza: Mazungumzo shuleni
Somo la Pili: i) Mazungumzo kati ya wanafunzi
ii) Ratiba ya mwanafunzi ya wiki
Somo la Tatu: Viongozi wetu shuleni
Somo la Nne: Shule yangu
Somo la Tano: Usafi shuleniSomo la Kwanza
Mazungumzo Shuleni
A. Mazingira ya darasani
Tazama picha hizi:
Katika makundi ya wanafunzi watatu watatu, tazama picha hizi halafu tunga sentensi kwa kueleza kile kinachoendelea. Tanguliza sentensi yako kwa:
Mimi ninaona…
Mfano: Mimi ninaona wanafunzi.Soma mazungumzo yafuatayo baina ya wanafunzi na mwalimu wao.
Mutoni: Habari za asubuhi Musafi ri?
Musafiri: Nzuri.
Mutoni: Umefanya zoezi la Kiswahili ?
Musafiri: Ndiyo.
Mutoni: Na mimi pia nimefanya zoezi hilo.
Musafiri: Lakini, swali la kwanza ni gumu.
Mutoni: Hapana. Swali la kwanza ni rahisi sana.
Musafiri: Kila siku, mwalimu wetu hutupatia mazoezi ya kufanyia nyumbani.
Mutoni: Ndiyo. Ni mwalimu mzuri sana. Yeye anatufundisha vizuri na anatupenda.
Musafiri: Ndiyo. Eh! Kengele inalia.
Mutoni: Twende…twende haraka tusichelewe. Mwalimu anaweza kutupa adhabu.
Musafiri: Ndiyo. Twende haraka. Wenzetu wanajipanga mbele ya darasa letu. (Mutoni na Musafiri wanajiunga na wanafunzi wenzao. Wanafunzi wote na mwalimu wao wanaingia darasani.)
Mwalimu: Hamjambo wanafunzi?
Wanafunzi: Hatujambo. Shikamoo mwalimu.
Mwalimu: Marahaba. Ketini. Mutoni, umefanya zoezi la Kiswahili?
Mutoni: Ndiyo Mwalimu.
Mwalimu: Leta daftari lako hapa. Hum! Mbona umeharibu daftari lako? Hujui kuwa unapaswa kutunza vizuri daftari lako?
Mutoni: Samahani mwalimu! Mvua ilininyeshea.
Mwalimu: Sawa. Kumbukeni…ni muhimu sana kutunza vizuri madaftari na vitabu vyenu.
Wanafunzi: Sawa mwalimu.
Mwalimu: Sasa ni wakati wa kufanya jaribio. Wekeni vitabu na madaftari katika madawati yenu.
Wanafunzi: Ndiyo mwalimu.
Mutoni: Samahani mwalimu! Mimi sielewi swali la kwanza.
Mwalimu: Swali la kwanza… Kila mwanafunzi anachagua jibu sahihi kati ya A, B na C.
Mutoni: Sawa mwalimuZoezi la ufahamu
Soma mazungumzo hapo juu kati ya wanafunzi na mwalimu, kisha ujibu maswali yanayofuata kwa kuchagua jibu sahihi kati ya yale yaliyopendekezwa mabanoni.1. Musafiri amefanya _____________ (zoezi/daftari) la Kiswahili.
2. Swali la kwanza ni_____________ (gumu/rahisi) kwa Musafiri.
3. Swali la kwanza ni _____________ (gumu/rahisi) kwa Mutoni.
4. Mwalimu huwapa wanafunzi _____________ (daftari/kazi ya nyumbani) kila siku.
5. Mutoni na Musafiri wanaenda haraka kwa sababu _____________ (mwanafunzi/kengele) inalia.
6. Wanafunzi _____________ (wajambo/hawajambo).
7. Daftari la Mutoni _______ ______ (limeharibika/linanyesha).
8. Mutoni _____________ (amenyeshewa/ameharibiwa) na mvua.
9. Wanafunzi wanaweka vitabu na madaftari katika madawati yao. Sasa ni wakati wa kufanya ____________ (kazi ya nyumbani/jaribio).
10. Kila mwanafunzi anachagua _______ ______ (jibu/kiti) sahihi.B. Msamiati wa mazingira ya shuleni
Zoezi la 1
Jipange katika makundi ya wanafunzi watatu watatu ili msome sentensi zifuatazo na kujadiliana. Husisha sentensi hizi na shughuli mbalimbali katika darasa lako.Mfano:
a) Wanafunzi wamo darasani na mwalimu wao amesimama mbele ya darasa.
b) Kalisa ananyosha mkono ili ajibu swali la mwalimu.c) Mwanafunzi anampatia mwenzake kalamu ili aandike zoezi la Kiswahili.
d) Kengele inalia. Sasa ni wakati wa kuingia darasani.
e) Wanafunzi wote wanajipanga mbele ya darasa lao.
f) Mvua inawanyeshea wanafunzi.
g) Vitabu na madaftari yanaharibika.
h) Ni muhimu kutunza madaftari yetu. Sasa ninafunika daftari langu ili lisiharibike.
i) Mwalimu anaandika zoezi ubaoni.
j) Jibu sahihi la moja kuongeza mbili ni tatu.
k) Mutoni anaweka madaftari yake juu ya meza.Zoezi la 2
Katika makundi ya wanafunzi wawili wawili, kamilisha sentensi zinazofuata kwa kutumia msamiati unaofaa kati ya huu uliopewa:
Kiti, ninatunza, adhabu, madawati, gumu, ubaoni, jaribio, Samahani, anatupenda,muhimu1. Kiswahili ni somo _______ ______ kwa wanafunzi.
2. Mwalimu anauliza swali _______ ______ kwa wanafunzi.
3. Mwalimu anaandika _______ ______.
4. _______ ______ cha mwalimu kiko mbele ya darasa.
5. Wanafunzi wanaweka vitabu katika _______ ______ yao.
6. Mimi _______ ______ vifaa vya shule; vitabu, madaftari na kalamu.
7. Mutesi ameharibu daftari lake. Mwalimu atampatia _______ ______.
8. Sisi tumeshinda _______ ______la Kiswahili.
9. _______ ______ ! Mwalimu. Ninaomba ruhusa ya kuenda haja.
10. Mwalimu _______ ______ sana kwa sababu tunasoma vizuri.Zoezi la 3
Kwa kutumia mshale, husisha vifaa katika sehemu A na matumizi yake katika sehemu B.C. Shughuli za siku za mwanafunzi
Katika makundi ya wanafunzi watatu watatu, tazameni picha zilizochorwa hapa chini, kisha mueleze kile kinachoendelea kwa kuhusisha sentensi zilizotolewa chini yake:Ratiba ya siku ya Kalisa
Saa Shughuli12:00 alfajiri: Kalisa anaamka.
12:10 alfajiri: Kalisa anaenda bafuni kuoga.
12:30 asubuhi: Baada ya kuvaa sare, kuchana nywele na kupiga mswaki, Kalisa anapata kifungua kinywa kwa kunywa chai kwa kiazi kitamu na ndizi iliyoiva.
12:35 asubuhi: Kalisa anaenda shuleni. Mama yake anamuaga.
12:40 asubuhi: Kalisa anakutana na Gatete na Akaliza njiani.
1:00 asubuhi: Kalisa, Gatete na Akaliza wanaenda shuleni pamoja.
1:35 asubuhi: Kalisa, Gatete na Akaliza wanafika shuleni na kukutana na wanafunzi wenzao.
1:45 asubuhi: Kengele inalia. Ni wakati wa kuingia darasani.
1:50 asubuhi: Wanafunzi wote wanajipanga kwa msururu mbele ya darasa lao.
2:00 asubuhi: Wanafunzi wanaingia madarasani.
2:00 - 2:40 asubuhi: Somo la Hisabati linaanza.Shughuli zinazofuata:
2:50 - 3:30 asubuhi: Somo la Hisabati linaendelea.
3:40 - 4:20 asubuhi: Somo la Kiswahili linaanza.
4:20 - 4:40 asubuhi: Pumziko fupi. Wanafunzi wengine wanakimbia msalani, wengine wanacheza nje ya madarasa yao.
4:40 -5:20 asubuhi: Somo la Historia linaanza.
5:30 -6:10 adhuhuri: Somo la Historia linaendelea.
6:20 -7:00 adhuhuri: Somo la Bayolojia linaanza.
7:00 - 8:00 adhuhuri: Wanafunzi wanaenda bwaloni ili kupata chamcha.
8:00 - 8:40 alasiri: Somo la Jiografia linaanza.
8:50 -9:30 alasiri: Somo la Fizikia linaanza.
9:40 - 10:20 jioni: Somo la Kiingereza linaanza.
10:30 - 11:20 jioni: Wanafunzi wanaenda uwanjani kushirki katika michezo mbalimbali kama vile kandanda, mpira wa vikapu, riadha na voliboli. Ifikapo saa kumi na moja u nusu wanafunzi wote huruhusiwa kwenda nyumbani.Zoezi
Kwa ushirikiano na wenzako, zungumzieni shughuli zenu kuanzia kuamka, kufika darasani hadi kurudi nyumbani jioni.Maigizo ya shughuli za mwanafunzi
Katika makundi ya wanafunzi watano, jaribu kuigiza mazungumzo hapo juu kati ya wanafunzi na mwalimu.Ratiba ya mwanafunzi ya wiki
Katika makundi ya wanafunzi wawili wawili, someni ratiba ifuatayo.
Gasimba ni mwanafunzi wa kidato cha kwanza katika shule ya Bwiza. Yeye ni mwanafunzi mwenye bidii na huwa hachelewi shuleni.Jumatatu, Gasimba huamka saa kumi na moja na nusu alfajiri na kuanza kujiandaa kwenda shuleni. Yeye husali kwa dakika ishirini kisha huenda bafuni kukoga. Baadaye, yeye hupiga meno yake mswaki, huchana nywele zake na kuvaa sare yake.Mamake Gasimba huamka mapema zaidi ili kumwandalia mwanawe kiamsha kinywa. Gasimba hunywa chai kwa mkate kisha hubeba mkoba wake wenye madaftari na vitabu vyake kuelekea shuleni. Gasimba humuaga mamake na kuondoka. Gasimba hufika shuleni saa kumi na mbili u nusu na kuingia darasani na kuanza kusoma.
Yeye huwatangulia wanafunzi wengine. Saa mbili kasorobo kengele hulia na wanafunzi wote huenda kwenye gwaride ambapo wao husali kisha huimba nyimbo za kumsifu Mungu, na baadaye
hupandisha bendera huku wakiimba wimbo wa taifa la Rwanda. Mwalimu mkuu huwahutubia wanafunzi kisha kumpisha mwalimu wa zamu kuwapa wanafunzi matangazo yoyote muhimu.Saa mbili kamili kwa somo la kwanza. Baada ya masomo mawili wanafunzi hupewa dakika ishirini za mapumziko. Chakula cha mchana huliwa saa saba kamili. Masomo huendelea kuanzia saa nane alasiri.Saa kumi na dakika ishirini masomo ya siku huwa yamekamilika. Wanafunzi wote huenda uwanjani kwa michezo mbalimbali kama kandanda, voliboli na kuruka kamba. Ifikapo saa kumi na moja u nusu wanafunzi wote kuelekea nyumbani.
Gasimba afikapo nyumbani, yeye humsaidia mamake kufanya kazi za nyumbani kisha hapo baadaye yeye hufanya kazi zake za ziada za shuleni kabla ya kulala ifikapo saa tatu u nusu usiku.
Kila siku ya wiki huhusisha matukio haya ila siku ya Alhamisi jioni ambapo kina Gasimba hufanya mazoezi ya kuogelea katika dimbwi lao. Ijumaa jioni wanafunzi hushiriki katika mjadala kuhusu mada ambazo walimu wao huwa wamewachagulia. Jumamosi, Gasimba humsaidia mamake kufanya kazi za nyumbani. Jumapili wao huenda kanisani. Baadaye, Gasimba hupumzika. Kisha hujitayarisha kwa ajili ya kwenda shuleni Jumatatu.
Zoezi la ufahamu
Soma tena kifungu kilicho hapo juu kisha ujibu maswali yafuatayo.1. Gasimba anasoma katika shule gani?
2. Je, Gasimba yuko katika kidato cha tatu?
3. Gasimba hufanya nini anapoamka kabla ya kustaftahi?
4. Baina ya Gasimba na mamake, nani huamka mapema zaidi?
5. Gasimba hufanya nini afikapo shuleni kabla wanafunzi wengine wafike?
6. Nani huwahutubia wanafunzi kwenye gwaride?
7. Gasimba na wanafunzi wenzake hufanya nini Alhamisi na Ijumaa jioni baada ya masomo yao?
8. Gasimba hufanya nini Jumamosi?
9. Taja shughuli za Gasimba za siku ya Jumapili?
10. Eleza maana ya msamiati ufuatao:
a) Kiamsha kinywa
b) Sare
c) Mjadala
d) KandandaSomo la Pili
Mazungumzo Kati ya WanafunziA. Mazungumzo ya wanafunzi
Tazama picha hii:
Katika makundi ya wanafunzi watatu watatu, tazameni picha hii halafu tungeni sentensi kwa kueleza kile kinachoendelea.
Mfano: Wanafunzi wanacheza kandanda.
Soma kifungu cha mazungumzo kinachofuata kati ya Kalisa, Mutoni na Birasa.
Kalisa: Mimi ninapenda mchezo wa kandanda. Je, wewe unapenda mchezo gani?
Mutoni: Mimi ninapenda mchezo wa voliboli. Je, Birasa pia anapenda mchezo wa voliboli?
Kalisa: Ndio. Yeye pia anapenda mchezo wa voliboli.
Mutoni: Ooh! Wewe na Birasa mnapenda mchezo wa voliboli.
Kalisa: Kweli! Mimi na Birasa tunafurahia mchezo huo sana.
Mutoni: Na Muhire hufurahia mchezo upi?
Kalisa: Muhire hupenda kucheza mchezo wa vikapu. Urefu wake unamfaa sana katika mchezo huo.
Mutoni: Lakini, Muhire ni mwanafunzi mbaya. Yeye hupiga kelele darasani.
Kalisa: Ndiyo. Yeye ni mwanafunzi mtukutu na kila siku, yeye huchelewa kufika shuleni. (Birasa anajitokeza na Kalisa anamwita.)
Kalisa: Birasa! Njoo hapa. (Birasa anawakaribia) Wewe unatoka wapi?
Birasa: Mimi ninatoka zahanatini.
Kalisa: Kwani wewe unaumwa?
Birasa: Ndiyo. Mimi ninaumwa…niliumia nilipokuwa nikicheza mchezo wa voliboli. . . ninataka kuomba ruhusa ya kuenda bwenini.
Kalisa: Pole sana! (Akimuonyesha kwa kidole) Mwalimu wa zamu amesimama karibu na uwanja wa kuchezea kandanda.
Birasa: Asante! Naenda kumuomba ruhusa ya kupumzika. (Birasa anaelekea upande aliko mwalimu wa zamu).
Mutoni: Sasa twende tujiunge na wenzetu katika mchezo wa kandanda.
Kalisa: Ndiyo. Twende. Twende haraka.Zoezi la ufahamu
Soma tena mazungumzo yaliyo hapo juu, kisha ujibu maswali yafuatayo.1. Kalisa anapenda mchezo gani?
2. Mutoni anapenda mchezo gani?
3. Birasa anapenda mchezo gani?
4. Je, Birasa anapenda mchezo wa vikapu?
5. Tambua majina ya wanafunzi wanaopenda mchezo wa voliboli.
6. Ni mwanafunzi gani hupenda kupiga kelele darasani?
7. Mwalimu wa zamu yuko wapi?
8. Kwa nini Birasa anataka kumwona mwalimu wa zamu?
9. Birasa anatoka wapi?
10. Kwa nini Birasa anataka kuomba ruhusa?B. Msamiati wa shuleni
Jipange katika makundi ya wanafunzi watatu watatu kisha mtafute msamiati mpya katika kifungu cha mazungumzo hapo juu. Tafuta maana za msamiati huo kulingana na matumizi yake katika kifungu hicho. Tumia kamusi ya Kiswahili pale panapohitajika.Zoezi
Tunga sentensi zako mwenyewe kwa kutumia maneno yafuatayo yaliyokolezwa rangi.1. Issa ni mwanafunzi mtukutu. Yeye anachelewa kila siku na anapenda kudanganya mwalimu.
2. Mimi ninatoka shuleni, ninaenda nyumbani.
3. Mwanafunzi huyu ni mgonjwa. Yeye anaumwa kichwa.
4. Mwanafunzi huyu ni mgonjwa. Yeye anaenda zahanatini kutibiwa.
5. Wanafunzi wanalala katika mabweni.
6. Mutesi anaanguka chini. Amina anampa pole.Msamiati wa ziada:
• Mchezo wa vikapu
• Kandanda/Kabumbu
• Mchezo wa voliboli
• RiadhaC. Sarufi
Umoja na wingi wa vitenzi, viambishi na viwakilishi nafsiKatika makundi ya wanafunzi wawili wawili, someni sentensi zinazofuata katika umoja na wingi kisha mfanye zoezi linalofuata.
Zoezi la 1
a) Katika makundi ya wanafunzi wawili wawili, tungeni sentensi moja moja kwa kutumia kitenzi cheza katika nafsi zifuatazo: mimi, wewe, yeye, sisi, nyinyi na wao.
b) Linganisha sentensi zako na zile ulizotolewa hapo juu kuhusu kitenzi soma.Tafakari:
• Sehemu zinazorudiwa ni soma na cheza. Hivi ni vitenzi. Som’ katika kitenzi ‘soma’ na chez’ katika kitenzi ‘cheza’ ndiyo mizizi ya vitenzi hivyo. ‘-a-’ ni kiambishi tamati.
• Katika umoja, ni inatumiwa kuwakilisha nafsi mimi, u inatumiwa kuwakilisha nafsi wewe na a inawakilisha nafsi yeye.
• Katika wingi, tu inatumiwa kuwakilisha nafsi sisi, m inatumiwa kuwakilisha nafsi nyinyi na wa inawakilisha nafsi wao.Zoezi la 2
Katika daftari lako, jaza nafasi zilizoachwa wazi kwa kutumia nafsi inayofaa.Mfano: ____________ anatembea haraka.
Jibu: Yeye anatembea haraka.
1. ____________ ninakimbia.
2. ____________ wanafundisha.
3. ____________ unatunza mazingira yako.
4. ____________ anaenda shuleni.
5. ____________ mnatumia pesa zenu vizuri.
6. ____________ tunafurahia usawa wa kijinsia.
7. ____________ wanalala mabwenini.
8. ____________ ninaingia darasani.
9. ____________ anachunguza nidhamu.
10. ____________ tunajali maslahi ya wanafunzi walemavu.Zoezi la 3
Katika makundi ya wanafunzi wawili wawili, andikeni sentensi zifuatazo katika umoja au wingi.Mfano: Yeye analipa kodi.
Jibu: Wao wanalipa kodi.
1. Wewe unacheza kandanda.
2. Yeye anakuja darasani.
3. Sisi tunaandika barua.
4. Mimi ninaketi kwenye kiti.
5. Nyinyi mnachoma majani.
6. Wao wanatembea njiani.
7. Wewe unaandika kwenye ubao.
8. Wao wanazungumza Kiswahili.
9. Mimi ninasimama mbele ya darasa.
10. Yeye anaimba wimbo wa taifa la Rwanda.D. Kusikiliza na Kuzungumza
Zoezi la kuigiza
Katika makundi ya wanafunzi watatu watatu, igizeni mazungumzo kati ya wanafunzi yaliyotolewa hapo awali.Zoezi la imla
Funga kitabu chako, kisha katika daftari lako, andika kwa usahihi maneno na vifungu vya maneno utakavyosomewa na mwalimu wakoSomo la Tatu
Viongozi Wetu Shuleni
A. Mahusiano ya watu wanaopatikana shuleniKatika makundi ya wanafunzi watatu watatu, tazameni picha zilizopo hapo juu, kisha mueleze kile kinachoendelea: Tangulizeni sentensi zenu kwa kutumia: Mimi ninaona…
Mfano: Mimi ninaona ofi si ya mwalimu mkuu.
Soma kifungu cha habari kinachofuata kuhusu viongozi wetu shuleni.
(Kwizera ni mwanafunzi katika Shule ya Sekondari ya Gikondo. Yeye ni mwanafunzi mzuri na anapenda viongozi wa shule yake.)Mimi ninaitwa Kwizera. Mimi ninasoma katika kidato cha kwanza. Shule yetu inaitwa shule ya Sekondari ya Gikondo. Kayitare ni kiranja wa darasa letu. Yeye hutuwakilisha katika mikutano mingi ya shule. Katika mikutano na mkuu wa shule, yeye huuliza maswali mazuri kwa sababu yeye ni mwanafunzi hodari sana. Mimi ninaelewa vizuri masomo yote; Kiswahili, Kinyarwanda, Kiingereza, Hisabati, Jiografia, Historia na mengine.
Shule yetu ina viongozi wazuri. Baadhi ya viongozi wa shule yetu ni mkuu wa shule, naibu wa mkuu wa shule, mwalimu wa mitaala ambaye ni mwalimu wa taaluma, mwalimu wa nidhamu, mhasibu na mkutubi anayesimamia maktaba ambapo vitabu vyetu huhifadhiwa. Shule yetu ina vitabu vingi.
Kila asubuhi, mkuu wa shule hutukagua ikiwa tumevaa sare. Yeye pia hutushauri kupenda masomo yetu, kusaidiana na kufanya kazi kwa bidii. Mwalimu wa mitaala hupanga masomo ya kila muhula. Mwishoni mwa kila muhula sisi hufanya mitihani. Mhasibu wa shule hupokea karo za wanafunzi. Mwalimu wa nidhamu huwaadhibu wanafunzi wanaofanya makosa: wanafunzi watukutu, wanafunzi wanaotoroka shuleni na wale wanaopiga kelele darasani.
Mwalimu mshauri wa wasichana, huchunguza nidhamu ya wasichana. Yeye hutatua shida zao shuleni, hutushauri kuwa na mienendo mizuri, huchunguza wakati wa kuingia mabwenini na kadhalika. Mwalimu mshauri wa wavulana huchunguza nidhamu ya wavulana na kupanga michezo shuleni kwa kushirikiana na mwalimu mshauri wa wasichana. Wakati wa chakula cha mchana na chakula cha jioni, walimu wa zamu huingia bwaloni kuchunguza chakula chetu na kutushauri kuheshimiana wakati wa kula. Mimi ninapenda sana viongozi wetu shuleni.
Zoezi la ufahamu
Soma tena kifungu cha habari kilicho hapo juu kisha ujibu maswali yanayofuata.1. Kwizera anasomea wapi?
2. Yeye anasoma katika kidato gani?
3. Kiranja wao ni nani?
4. Kwizera anaelewa vizuri masomo gani?
5. Viongozi wao ni nani?
6. Mwishoni mwa kila muhula wanafunzi hufanya nini?
7. Katika mikutano na mkurugenzi, kiranja wao hufanya nini?
8. Mkuu wa shule anaitwa nani?
9. Mkuu wa nidhamu huwaadhibu wanafunzi gani?
10. Walimu washauri huingia bwaloni kufanya nini?B. Msamiati kuhusu viongozi wa shuleni
Soma tena kifungu cha habari kilicho hapo juu na katika makundi ya wanafunzi wanne wanne, tafuta maana za maneno mapya yaliyojitokeza. Tumia kamusi ya Kiswahili pale panapohitajika.Zoezi la 1
Jipange katika makundi ya wanafunzi watatu watatu ili msome kwa sauti na matamshi sahihi sentensi zifuatazo. Maana za maneno yaliyokolezwa rangi zielezwe kwa kutumia kamusi panapohitajika.Mfano:
a) Sisi tunavaa sare. Kila asubuhi tunafanya mkutano na mkuu wa shule. Yeye anatushauri kupenda masomo yetu.
b) Mukamwiza ni hodari katika michezo ya riadha. Yeye huwa wa kwanza katika mbio za mita mia moja.
c) Mimi ninalipa karo ya shule yangu kupitia Benki ya SACCO na kuletea mhasibu wa shule hati ya malipo yangu.
d) Kiranja wa darasa na wanafunzi wenzake wanazungumza kuhusu masomo yao.Zoezi la 2
Katika daftari lako, jaza nafasi zilizoachwa wazi kwa kutumia moja kati ya maneno haya: muhula, Kiranja, mtihani, Mkuu, sare, wanatushauri, wavulana, mabwenini, bwaloni, mchana, anachunguza.Mfano: Walimu washauri ___________ kuheshimiana na wenzetu.
Jibu: Walimu washauri wanatushauri kuheshimiana na wenzetu.
1. Huu ni ___________ wa kwanza wa mwaka wa shule.
2. Tunafanya ___________ wa Kiswahili. Mwalimu wetu ametupa maswali rahisi.
3. Wanafunzi wote wa shule yangu wanavaa ___________.
4. ___________ wa darasa letu anaitwa Kagabo. Yeye anasimamia wanafunzi wenzake.
5. ___________ wa shule yetu ni mzuri sana. Yeye anaongoza shule vizuri.
6. Mwalimu mshauri wa wasichana ___________ nidhamu ya wasichana.
7. Mwalimu mshauri wa ___________ anapanga michezo shuleni.
8. Wanafunzi wanalala ___________.
9. Walimu washauri wanaingia ___________ kuchunguza chakula chetu.
10. Wakati wa chakula cha ___________ tunaenda bwaloni.Zoezi la 3
Kwa kutumia mshale, husisha majina katika sehemu A na maelezo yaliyopo katika sehemu B.C. Majina ya watu mbalimbali na kazi zao
Soma majina yafuatayo ya watu mbalimbali pamoja na maelezo ya kazi zao.
Kiranja: Kiongozi wa wanafunzi shuleni. Aghalabu huwa mwanafunzi.
Mwalimu: Mtu anayewapa wanafunzi elimu au maarifa.
Daktari: Mtu anayewatibu wagonjwa kwa kuwachunguza na kuwapa dawa.
Dereva: Mtu anayeendesha vyombo vinavyosafiri kwenye nchi kavu kama vile gari, baiskeli na pikipiki.
Kandawala: Mtu anayeendesha garimoshi.
Nahodha: Mtu anayeendesha vyombo vya majini kama vile meli.
Seremala: Mtu anayetengeneza vifaa vya mbao.
Mwashi: Mtu anayejenga nyumba za mawe.
Dobi: Mtu anayefua nguo na kuzipiga pasi kwa malipo.
Rubani: Mtu anayeendesha ndege.
Mkunga: Mtu anayesaidia kina mama kujifungua.
Rais: Kiongozi wa nchi iliyo Jamhuri.
Hakimu: Mtu anayeamua kesi mahakamani.
Mfinyanzi: Mtu anayefinyanga vyombo vya udongo.
Msusi: Mtu anayefanya kazi ya kusuka nywele, mikeka n.k.Zoezi
1. Jigawe katika makundi ya wanafunzi wawili wawili kisha mjadiliane kuhusu majina ya watu mbalimbali yaliyo hapo juu pamoja na kazi zao.
2. Tafiti kuhusu kazi za watu wafuatao:
a) Mhariri
b) Malenga
c) Msasi
d) Sogora
e) MhandisiZoezi la kutamka
Tamka maneno katika sentensi zifuatazo kwa usahihi.Somo la Nne
Shule YanguA. Ufahamu
Soma kwa makini kifungu cha habari kinachofuata kuhusu ‘Shule Yangu.’(Kamali ni mwanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Mugano. Shule yake ni nzuri sana. Watu waliosomea kwenye shule yake sasa hivi ni watu wakubwa. Shule yake ina wanafunzi wazuri na walimu wazuri. Yeye anajivunia shule yake.)
Mimi ninaitwa Kamali. Mimi ni mwanafunzi. Mimi ninasoma katika Shule ya Sekondari ya Mugano. Shule yangu ina madarasa mazuri sana. Madarasa ya shule yangu ni sawa na madarasa ya Shule ya Sekondari ya Kimya. Lakini shule yangu ina viongozi wazuri kuliko viongozi wa shule ya Kimya.
Mimi ninasoma katika kidato cha kwanza. Darasa letu ni kubwa sana na lina wanafunzi wazuri. Ndugu zangu Kagabo na Mutesi wanasoma katika kidato cha tatu lakini darasa letu ni kubwa kuliko darasa lao. Wao wana darasa dogo. Mimi ninapenda shule yangu.
Kayitare, Mulisa na Munyana walisomea katika shule yangu. Sasa Mulisa ni daktari katika hospitali kuu ya Kigali. Kayitare anajenga maghorofa marefu mjini Musanze na Munyana ni mwimbaji maarufu sana. Yeye ana wafuasi wengi mjini Kigali.
Kayitare, Mulisa na Munyana wanapenda kuja hapa mara nyingi kutembelea wanafunzi. Wao wanapenda sana wanafunzi wa shule yangu. Kwa kweli, shule yangu ina wanafunzi wazuri, werevu na wenye nidhamu. Sisi sote tunaelewa masomo yetu na tunasoma kwa bidii sana. Wasichana wanavaa marinda marefu na wavulana wanavaa suruali na mashati mazuri. Walimu wetu nao ni wazuri. Wao wanatufundisha masomo muhimu. Mimi ninajivunia shule yangu.
Zoezi la ufahamu
Soma tena kifungu cha habari kilicho hapo juu kisha ujibu maswali yanayofuata:1. Mimi ninaitwa nani?
2. Mimi ninasoma wapi?
3. Ndugu zangu ni nani?
4. Wao wanasoma wapi?
5. Mimi ninasoma katika kidato gani?
6. Je, darasa la kagabo na Mutesi ni kubwa?
7. Munyana anafanya nini?
8. Kayitare anajenga nyumba wapi?
9. Je, Kalisa, Kayitare na Munyana walisomea wapi?
10. Wasichana na wavulana wanavaa nini?Msamiati kuhusu ‘Shule yangu’
Soma tena kifungu cha habari kilichotangulia kisha katika makundi ya wanafunzi wanne wanne, tafuta maana za maneno mapya yaliyojitokeza. Tumia kamusi ya Kiswahili pale panapohitajika.Kwa mfano:
Shule - mahali ambapo wanafunzi hupata elimu au maarifa kutoka kwa walimuZoezi la 1
Jipange katika makundi ya wanafunzi watatu watatu kisha msome sentensi zifuatazo.a) Nyumba ya Kagabo ni kubwa kuliko nyumba ya Bugingo. Bugingo ana nyumba ndogo.
b) Shati langu ni zuri kuliko shati lako.
c) Kanziga ni mwimbaji maarufu sana. Yeye ana wafuasi wengi; watoto na watu wakubwa wanampenda.
d) Mwizere anajenga ghorofa mjini Nyamata.
e) Mugabo ni fundi mkubwa katika uchoraji. Yeye anaweza kuchora picha za wanyama, watu na hata ndege.Zoezi la 2
Kwa kutumia mshale, husisha maneno katika sehemu A na maelezo yaliyopo katika sehemu B.Zoezi la 3
Kamilisha sentensi zinazofuata kwa kutumia maneno haya: mwerevu, maarufu, ndefu, nzuri, wabaya, mwimbaji, fundi, mdogo, kuliko, sawasawa, bidii.
Mfano: Wanafunzi wa shule yangu wanasoma kwa ____________. Wao wamejibu mazoezi yote ya Kiswahili.
Jibu: Wanafunzi wa shule yangu wanasoma kwa bidii. Wao wamejibu mazoezi yote ya Kiswahili.
a) Nyumba hii ni ____________. Nyumba hii ni safi sana.
b) Bagabo ni____________ wa uchoraji. Yeye anaweza kuchora picha za vitu vingi sana.
c) Mtoto huyu ni ____________ sana. Ana miaka mitatu.
d) Yeye alijenga nyumba ____________ sana. Nyumba yake inapendeza.e) Kalisa ni mchoraji ____________ sana. Picha zake zinapendwa na watu wengi.
f) Mwanafunzi huyu ni ____________ kabisa. Yeye anafaulu masomo yote.
g) Yeye ni ____________ mzuri sana. Anaimba nyimbo za Mungu.
h) Mtoto huyu ni mdogo ____________ Amina. Yeye hatembei vizuri.
i) Kitabu hiki ni ____________ na kitabu changu. Vitabu vyote vinazungumzia somo la Kiswahili.
j) Watoto ____________ hawapendi kufanya mazoezi yao. Wao wanapiga kelele darasani.B. Kifungu cha ratiba ya masomo shuleni
Katika makundi ya wanafunzi watatu watatu, tazameni picha zifuatazo na kueleza kinachoendelea:Soma kifungu kinachofuata kuhusu ratiba ya masomo ya wanafunzi.
Mimi ninafurahia masomo yangu. Katika darasa letu, sisi tuna vipindi viwili vya somo la Kiswahili kwa wiki. Leo ni Jumatatu. Leo tunasoma Kiswahili, Hisabati na Bayolojia. Kesho ni siku ya Jumanne. Jumanne tunasoma Fizikia, Kemia na Historia. Jumatano tunasoma tena Kiswahili, Kiingereza na Kemia pia. Alhamisi tunasoma Kifaransa na Sanaa. Ijumaa tunasoma Kiingereza, Historia na Kifaransa pia.Jumamosi na Jumapili ni siku za kupumzika; lakini mimi hurudia masomo yangu na kufanya mazoezi ya ziada. Mimi ninapenda sana somo la Kiswahili. Mwishoni mwa kila muhula tunafanya mtihani na mimi hufaulu.
Baada ya kusoma kifungu hiki, orodhesha majina ya siku za wiki. Anzia Jumatatu hadi siku ya mwisho ya wiki. Bainisha shughuli za kila siku katika sentensi fupifupi kama zinavyozungumziwa hapo juu.
Mfano: Jumatatu tunasoma Kiswahili, Hisabati na Bayolojia.
C. Kusikiliza na kuzungumza
1. Tamka maneno yafuatayo kwa usahihi.
1. Jumatatu 10. ninaitwa
2. Jumanne 11. mimi ninajivunia
3. Jumatano 12. maarufu
4. Alhamisi 13. daktari
5. Ijumaa 14. wafuasi
6. Jumamosi 15. hospitali
7. Jumapili 16. kuliko
8. bidii 17. mwimbaji
9. sawasawa2. Zungumzia shughuli unazozifanya nje ya darasa kuanzia Jumatatu hadi Jumapili.
D. Sarufi
Vivumishi vya sifa
Katika makundi ya wanafunzi watatu watatu, someni tungo zifuatazo. Baada ya kusoma, andikeni katika madftari yenu vifungu vya maneno vilivyokolezwa rangi katika kila sentensi.1. Mwalimu wetu ana kiti kizuri.
2. Huyu ni mtoto mzuri sana. Yeye anaheshimu wazazi wake.
3. Kagabo ana nyumba mbaya lakini Muhire ana nyumba nzuri.
4. Huyu ni mtu mzima. Mimi ni mtoto mchanga.
5. Mtu huyu ana mkono mchafu. Mwambie aende kunawa.
6. Mwanafunzi huyu ana viatu vizuri.
7. Wanafunzi wa darasa langu wanavaa mashati mazuri.
8. Darasa langu lina madirisha makubwa.
9. Darasa la Kayitesi lina mlango mrefu.
10. Mwanafunzi anasoma kitabu kizuri.Zoezi la 1
Linganisha maneno yaliyopigiwa mstari katika kila kifungu cha sentensi hapo juu.Mfano: Mwalimu wetu ana kiti kizuri.
Jibu: kiti kizuri: ki katika neno kiti ni sawa na ki katika neno kizuri.Tafakari:
Kila kifungu kilichopigiwa mstari katika mifano hapo juu kina maneno mawili yenye viambishi mwanzoni vinavyofanana. Neno la pili linaeleza zaidi au linaongeza sifa na maana kwa neno la kwanza. Neno hili la pili ndilo kivumishi cha sifa.Mifano:
a) kiti kizuri (kiti kina sifa ya kuwa kizuri; kizuri ni kivumishi cha sifa)
b) mtoto mzuri (mtoto ana sifa ya kuwa mzuri; mzuri ni kivumishi cha sifa)
c) mkono mchafu (mkono una sifa ya kuwa mchafu; mchafu ni kivumishi cha sifa)
d) mlango mrefu (mlango una sifa ya kuwa mrefu; mrefu ni kivumishi cha sifa)Zoezi la 2
a) Kwa kujitegemea, soma tena kifungu cha habari kilichotangulia, kisha uandike vifungu vyote vya maneno vyenye kuhusisha jina na kivumishi cha sifa.
Mfano: madarasa mazuri
b) Katika makundi ya wanafunzi watatu watatu, linganisheni shule mbili mnazozifahamu kwa kutumia vivumishi vya sifa.Mfano: Shule ya Sekondari ya Mtakatifu Yohana ina walimu wazuri kuliko shule ya Sekondari ya Kimisagara.
Kivumishi ni neno linalotoa maelezo zaidi kuhusu nomino
Somo la Tano
Usafi ShuleniA. Kifungu kuhusu usafi shuleni
Katika makundi ya wanafunzi wanne wanne, tazameni picha zinazofuata na mweleze mnachokiona.Soma kifungu cha habari kifuatacho kuhusu usafi shuleni.
(Mutoni ni mwanafunzi katika Shule ya Sekondari ya Bwiza. Shule yake ina wanafunzi wanaojali umuhimu wa usafi kushinda wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Kimira. Shule ya Sekondari ya Kimira ni chafu sana.)Mimi ni Mutoni. Shule yangu inaitwa Bwiza. Sasa ni wakati wa kufanya usafi shuleni. Wanafunzi wa darasa la kwanza wanachukua majembe na kutengeneza bustani iliyo karibu na shule. Mimi na Kayitare tunasafi sha vyoo. Aisha, Kabera na Marita wanafagia darasani. Mutesi na Muhire wanasaidia wengine kusafi sha darasa letu. Shule yangu ina wanafunzi wavulana na wasichana. Wote husaidiana katika shughuli zote za usafi . Wakati wa mvua tunapanda miti na maua karibu na shule.
Mugabe na Musa wanasoma katika shule ya Kimira. Shule yao ni chafu sana. Shule hii ina wanafunzi wavivu sana. Wao hutupa takataka popote. Wao hawasafishi madarasa yao na hawafui sare zao za shule. Wao hawachunguzwi vizuri na walimu wao na hawajali umuhimu wa usafi. Kweli, magonjwa huwashika mara kwa mara.
Zoezi la ufahamu
Soma tena kifungu cha habari kilicho hapo juu kuhusu ‘Usafi Shuleni’ kisha ujibu maswali yanayofuata.1. Mutoni anasomea wapi?
2. Ni nani wanaofagia darasani?
3. Mutoni na Kayitare wanafanya nini?
4. Ni nani wanaosafisha vyoo?
5. Mugabe anasomea wapi?
6. Je, shule ya Kimira ni safi?
7. Shule ya Kimira inazungukwa na nini?
8. Je, wanafunzi wa shule ya sekondari ya Kimira wanajua umuhimu wa usafi?
9. Wanafunzi wa Kimira wanatupa wapi takataka?
10. Ni wanafunzi gani wanaofaulu katika masomo yao?B. Msamiati kuhusu usafi shuleni
Soma tena kifungu cha habari kuhusu usafi shuleni na katika makundi ya wanafunzi wanne wanne, tafuteni maana za maneno mapya yanayojitokeza. Tumia kamusi ya Kiswahili panapohitajika.Kwa mfano:
Bustani: Sehemu ya kupandia miti, maua, matunda au mbogaZoezi
Kwa kuzingatia mifano ya sentensi iliyobainishwa hapa chini, tunga sentensi nyingine kwa kutumia maneno yaliyopigiwa mstari na kutiwa rangi.1. Nyumba yangu ni safi. Nyumba yangu ina rangi nzuri na huisafisha kila asubuhi.
2. Si vizuri kutupa takataka karibu na nyumba yako. Takataka huharibu mazingira.
3. Kalisa ni mchafu. Yeye haogi kila siku.
4. Mama yangu ana bustani nzuri nyumbani. Bustani yake ina maua mazuri sana.
5. Mimi ninatoka chooni. Mimi ninanawa mikono yangu.
6. Kalisa anafagia darasani, yeye anapenda sana usafi.
7. Kila mwisho wa wiki, mimi hufua nguo zangu na kusafisha nyumba yetu.
8. Kamana na ndugu yake wanasaidiana kufanya kazi zote za nyumbani.
9. Lugha ya Kiswahili ni muhimu sana. Kiswahili kinazungumzwa Afrika Mashariki.
10. Wanafunzi wavivu hawafaulu katika masomo yao. Wao hawapendi kufanya kazi.C. Sarufi
Tungo yakinishi na tungo kanushi
Soma sentensi zifuatazo, kisha ujibu maswali yanayofuata.
1. a) Mimi ninasoma kitabu cha Kiswahili.
b) Mimi sisomi kitabu cha Kiingereza.
2. a) Wewe unaandika ubaoni. Wewe huandiki daftarini.
b) Kayitesi anaingia darasani. Yeye haingii kanisani.
3. a) Mimi na Kayitare tunacheza kabumbu.
b) Sisi hatuchezi karata.
4. a) Wewe na Mutesi mnapenda kuimba.
b) Nyinyi hampendi kucheza.5. a) Kalisa na Mugabe wanafagia darasani.
b) Wao hawafuti ubao.Zoezi la sarufi
1. Je, mimi ninasoma kitabu cha Kiingereza? Hapana, mimi _____________.
2. Je, mimi ninasoma kitabu cha Kiswahili? Ndiyo, mimi _____________.
3. Je, wewe unaandika daftarini? Hapana, wewe _____________. Wewe_____________.
4. Je, Kayitesi anaingia kanisani? Hapana, yeye _____________. Yeye_____________.
5. Je, mimi na Kayitare tunacheza kandanda? Ndiyo, sisi _____________.
6. Je, mimi na Kayitare tunacheza karata? Hapana, sisi _____________.
7. Je, wewe na Mutesi mnapenda kuimba? Ndiyo, nyinyi _____________.
8. Je, wewe na Mutesi mnapenda kucheza? Hapana, nyinyi _____________.
9. Je, Kalisa na Mugabe wanafuta ubao? Hapana, wao _____________.
10. Je, Kalisa na Mugabe wanafagia darasani? Ndiyo, wao _____________.Tafakari:
Katika majibu hapo juu, unaweza kukubaliana na tendo linaloelezwa katika kitenzi kwa kutumia tungo yakinishi (angalia sentensi zenye kutumia neno ndiyo). Unaweza pia kukana (kukanusha) tendo hilo kwa kutumia tungo kanushi (angalia sentensi zenye kutumia neno hapana).Kazi ya makundi
Katika makundi ya wanafunzi wawili wawili, andika sentensi sita (tumia nafsi zote tatu katika umoja na wingi) katika tungo yakinishi, halafu ziandike pia katika tungo kanushi.Mfano:
Umoja:Zoezi la 1
Andika sentensi hizi katika tungo yakinishi au kanushi.
1. Yeye anaimba vizuri.
2. Yeye hazungumzi Kiswahili sanifu.
3. Mimi ninapenda somo la Kiingereza.
4. Sisi tunapuuza masomo haya.
5. Mimi situngi sentensi.
6. Wao wanashika madaftari.
7. Nyinyi hamjitambulishi mbele ya wanafunzi wengine.
8. Wewe unaazima kitabu.
9. Wao hawachoti maji.
10. Nyinyi mtaenda mjini Kigali.Zoezi la 2
Andika sentensi zifuatazo kwa kutumia kitenzi sahihi katika wakati uliopo, tungo yakinishi na tungo kanushi.Mfano: Wewe (kupanga) michezo ya wanafunzi (Tungo yakinishi)
Jibu: Wewe unapanga michezo ya wanafunzi.
1. Kalisa (kucheza) mpira. (Tungo kanushi)
2. Mimi na wewe (kuimba) vizuri. (Tungo yakinishi)
3. Sisi (kuingia) darasani. (Tungo kanushi)
4. Mama na baba (kulima) shamba. (Tungo kanushi)
5. Mimi (kufanya) mtihani. (Tungo yakinishi)
6. Wewe (kusikiliza) redio. (Tungo kanushi)
7. Kayitesi na wewe (kuigiza) mazungumzo mbele ya wanafunzi. (Tungo yakinishi)
8. Wewe na Aisha (kukimbia) haraka sana. (Tungo kanushi)
9. Wao (kuweza) kushinda vizuri. (Tungo kanushi)
10. Mutoni na Bwiza (kupenda) somo la Kiswahili. (Tungo yakinishi)D. Kusikiliza na kuzungumza
Zoezi la imla
Funga kitabu chako, kisha katika daftari lako, andika kwa usahihi maneno na vifungu vya maneno utakayosomewa na mwalimu wako.Zoezi la makundi
Katika makundi ya wanafunzi watatu watatu, zungumzieni vitu vinavyosafishwa shuleni.Faharasa
Adhabu: jambo analofanya mtu au kufanyiwa kutokana na kuvunja sheria au kanuni iliyowekwa, mateso anayopata mtu kutokana na makosa yake
Adhibu: tesa mtu kutokana na makosa yake, kumfanyia mtu jambo linalomuudhi kwa makosa aliyoyafanya
Alama: maksi za mwanafunzi baada ya kufanya zoezi au mtihani
Bustani: sehemu ya kupandia miti ya maua, matunda au mboga
Bwalo: chumba kikubwa kinachotumiwa kulia chakula hasa shuleni
Bweni: chumba kikubwa kinachotumiwa na wanafunzi kulalia
Choo kidogo: mkojo
Choo kikubwa: kinyesi; maviChoo: mahali pa kuenda haja, msala
Elewa: fahamu, kuwa na ufahamu wa jambo
Fua: safisha nguo kwa maji
Fuata: kuwa makini na kuelewa kile unachofundishwa, kuiga, kuja nyuma au baadaye, kuandama
Fundi: mtu mwenye ujuzi fulani, mtu anayefanya kazi za maarifa fulani kama vile seremala, mwashi, na kadhalika.
Gorofa: nyumba ndefu
Gumu: kitu kisicho rahisi, kitu kisichoeleweka
Haribu: fanya kitu kiwe katika hali mbaya, kuchafua, kuangamiza kitu
Hodari: mtu anayeweza kufanya kitu kinachowashinda watu wengine
Jaribio: tendo linalofanywa ili kuona kama jambo limefanywa vizuri au kama jambo linafaaJenga: simamisha nyumba kwa kutumia miti, udongo,matofali, saruji na kadhalika
Jibu: itikia kwa maneno, maandishi au kwa ishara
Jivunia: furahia kuwa kitu chako ni bora
Karo: ada ya shule inayotolewa na mwanafunzi, pesa zinazolipwa shuleni
Kelele: sauti kubwa hasa isiyokuwa na maana yoyote, ghasia, fujo, ugomvi
Kiranja: kiongozi wa darasa
Kumbuka: kuwa tena na fikira ya jambo lililofanywa, lililopita au lililotokea
Maktaba: nyumba yenye mkusanyiko wa vitabu vingi
Mbaya: kitu kisichopendeza, kitu chenye hitilafu, kinyume cha ‘nzuri’Mchafu: kitu chenye uchafu, kinyume cha ‘safi’
Mfuasi: mtu mwenye kupenda sana jambo fulani
Mkubwa: kitu chenye umbo linalopita kiasi au linalopita umbo la kawaida, kilichokwisha kua, kinyume cha ‘mdogo’
Mkuu wa shule: kiongozi mkuu wa shule
Mkutano: mkusanyiko wa watu wengi kwa ajili ya kuzungumzia jambo maalumu, kusikilizana au kujadiliana
Mlango: nafasi au uwazi wa kuingilia na kutokea nyumbani
Mtihani: mpango unaowezesha kufahamu uwezo au ujuzi wa mtu
Muhimu: kitu chenye maana, kitu chenye matumizi makubwa, kitu kinachohitajika sana
Mvivu: mtu asiyependa kazi, mwenye tabia ya ulegevu wa kutenda jamboMchafu: kitu chenye uchafu, kinyume cha ‘safi’
Mfuasi: mtu mwenye kupenda sana jambo fulani
Mkubwa: kitu chenye umbo linalopita kiasi au linalopita umbo la kawaida, kilichokwisha kua, kinyume cha ‘mdogo’
Mkuu wa shule: kiongozi mkuu wa shule
Mkutano: mkusanyiko wa watu wengi kwa ajili ya kuzungumzia jambo maalumu, kusikilizana au kujadiliana
Mlango: nafasi au uwazi wa kuingilia na kutokea nyumbani
Mtihani: mpango unaowezesha kufahamu uwezo au ujuzi wa mtu
Muhimu: kitu chenye maana, kitu chenye matumizi makubwa, kitu kinachohitajika sana
Mvivu: mtu asiyependa kazi, mwenye tabia ya ulegevu wa kutenda jamboShauri: kuambia mtu afanye jambo lililo zuri, kutoa maoni au nasaha ili mtu aweze kuwa na adabu, kuelekeza mtu ili afanye vizuri, kunasihi, kuonya
Shinda: kuwa wa kwanza, kupata alama ya kutosha
Takataka: vitu vibovu, vitu vilivyotupwa, vitu visivyohitajika, vitu vinavyokaa bila mpango na ambavyo havifai kwa matumizi
Tunza: weka kitu mahali penye usalama, kuhifadhi, kuweka kitu chini ya uangalizi ili kisiharibiwe
Ubao: kitu kilichotengenezwa na kuwekwa kwenye ukuta ili kitumike kuandikiwa kwa chaki
Usafi: tabia ya kutokuwa na uchafuVaa sare: vaa kwa namna moja inayofanana, vaa sawasawa
Zoezi: tendo la kupima ujuzi wa mtu
Zuri: kitu chenye kupendeza, kitu kisicho na hitilafu -
Mada Ndogo:
Msamiati Katika Mazingira ya NyumbaniSomo la Kwanza: Aina za nyumba, watu wanaoishi humo na ujenzi wake
Somo la Pili: Vifaa mbalimbali vinavyopatikana nyumbani
Somo la Tatu: Mifugo wanaofugwa nyumbani na vivumishi vya ngeli ya A – WA.
Somo la Nne: Majina yanayohusishwa na watu na uhusiano wao kijamii pamoja na vivumishi vya ngeli ya A-WA
Somo la Tano: Uhusiano wa kifamilia pamoja na vivumishi vya ngeli ya A-WASomo la Kwanza:
Aina za Nyumba, Watu Wanaoishi Humo na Ujenzi WakeA. Michoro na mazungumzo kuhusu aina za nyumba na watu wanaoishi humo
Tazama michoro ifuatayo kwa makini kisha utoe maelezo yako kwa wenzako kuhusu unachokiona.
Tathmini
Makao ni mahali wanakoishi watu. Makao ni muhimu kwa mwanadamu. Hueleza utamaduni wa watu, shughuli zao za kiuchumi na mazingira yao.Kwa kutumia sentensi fupifupi, eleza unachokiona.
Mifano: 1. Mimi ninaona nyumba ya…
2. Mimi ninaona baba, …Soma mazungumzo yafuatayo baina ya baba na mama nyumbani.
Baba: Habari ya kuamka mke wangu?
Mama: Njema mume wangu.
Baba: Naona nyasi zimepungua kwenye nyumba yetu.
Mama: Kweli. Tunafaa tutoke kwenye huu msonge tujenge nyumba ya mabati au mawe.
Baba: Kweli. Kama tutapata pesa tutajenga nyumba ya matofali na vigae.
Mama: Watoto wetu watafurahi sana.
Baba: Ndiyo. Hata nyanya na babu yao watafurahia.
Mama: Nitawaalika watoto wa shangazi yao. Pia binamu wao nitawaalika.Mama: Nitawaalika watoto wa shangazi yao. Pia binamu wao nitawaalika.
Baba: Nampenda jirani yetu. Amejenga kasri kubwa.
Mama: Tunampongeza kwa bidii. Kasri lake lina vyumba vingi.
Baba: Umemkama ng’ombe?
Mama: La hasha! Nimeanza na mbuzi.
Baba: Basi acha niwafungulie kuku, paka, kondoo na bata.
Mama: Na pia ukumbuke kumfungia mbwa.(Wanaendelea na shughuli zao mbalimbali)
Tathmini
Je, nyumba zilizotajwa katika mazungumzo yaliyo hapo juu hujengwa kwa vifaa gani?Zoezi la ufahamu
Kwa kujitegemea, soma tena mazungumzo baina ya baba na mama kimyakimya. Kisha kwa ushirikiano na wenzako, jibu kwa usahihi maswali yanayofuata.1. ___________ za kuamka mke wangu?
2. Baba pia angemwamkia mama vipi? ___________.
3. Mama aliitikia salamu za baba kwa kusema ___________.
4. Mama alitaka watoke kwa ___________ na kujenga nyumba ya ___________ na ___________.
5. ___________ wetu watafurahi sana.
6. Wazazi wa baba na mama tunawaitaje? ___________ na ___________.
7. Ninampenda ___________ yetu.
8. Acha niwafungulie _________, __________, _________ na __________.
9. Na umfungie ___________.
10. Kichwa mwafaka kwa mazungumzo haya ni: ___________.
a) Mazungumzo baina ya baba na mama
b) Mazungumzo baina ya mama na watotoB. Msamiati wa nyumbani
Kwa ushirikiano na wenzako, taja msamiati wote wa nyumbani uliosoma katika mazungumzo baina ya baba na mama. Tumia tathmini ifuatayo.
1. Aina ngapi za nyumba zimetajwa?
2. Nyumba hizo zimejengwa kwa kutumia nini?
3. Je, ni watu wangapi wanaopatikana nyumbani?
4. Ni mifugo gani wa nyumbani wametajwa?
-